UHALISIAlABU
KATIKA RIWAVA VA BABU ALIPOFUFUKA
(2001)
VA S.A MOHAMED NA BINA-ADAMU! (2002)
VA K.W
WAMITILA
NA:
JACINTA KAGENDO
~GAJU
IDARA VA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA
CHUO KIKUU CHA KENVATTA
Tasnifu hii imetolewa iIi kutosheleza baadhi ya mahitaji ya Shahada
ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta
AGOSn
2004
Magaju, Jacinta, Uhalisiajabu katika riwaya ya 'Babu1111111111111111111111111111111111111111111111111111111 OS/277415
IKIRARI
Tasnifu hii ni kazi yangu binafsi na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika Chuo Kikuu
kingine.
JACINTA KAGENDO MAGAJU
Tasnifu hii imetolewa kutahiniwa kwa idhini yetu kama wasimamizi wa kazi hii katika Chuo
hiki.
&
-
(
DKT. R.M. WAFULA
Na
,
G-O---TABARUKU
Naitabaruku kazi hii kwa mume wangu mpenzi Franklin Magaju. Mbali na kunihimiza kila nilipohisi kulemewa na kuwa nami kwa kila hatua, ulinifaa kwa hali na mali. Binti zangu wapendwa Doreen Kinya na Emily Mukami hawawezi kusahaulika kwa uvumilivu wao si
haba nilipokuwa nikisoma. Mwisho ni kwa kitindamimba changu David Mwenda. Asante
IV YAlIYOMO Mada Ikirari Tabaruku Yaliyomo ...•...•..••....•...
Shukrani
••••••••••••••••••••
"'
r •••••••••••••••••••••••••••••••••
c •••••••••••••••••••••••••••Ikisiri ...
1.II' 11.1 ••II ••••••• II•••• II. I" II. II ••••• 1.11.11. II. II•••••••••••••••• 11.11 ••1 ••1 ••SURA YA KWANZA
1.0
Utangulizi ...II. II. II. II •••• II. II. II ••••••• 11.11. II. II •••• I••••• II •••• II' II1.1
Usasa, Usasaleo, Uhalisiajabu ...•..1.2
Mada ya Ut:afiti II. II••••••• I •• 11 ••1 •••••••••••••• 1 ••1.11 ••1.1 ••1
.
3
Yaliyoandikwa kuhusu Mada ...•... II. II. II •••• II •••• II. II •••••1.4
Maswala la U'tafiti ..II •••• II' II. II. II' II •••• II. 11.11. II. II ••••••• II' II' II1.5
Malengo Ya Utafiti1.6
Sababu ya kuchagua Mada ...••...••.••...•1
.
7
Upeo wa Utafiti1.8
Misingi ya Nadharia ...•...•••.•...•.••1.9
Mbinuza
Utafiti .1.1
0
Kiishilio .,...•...SURA YA PILI
2.0
Utangulizi ...•....••••...•.•••...••...••...2.1
Vipindi vya uandishi wa S.A. Mohamed .2.
1
.
1
Kipindi cha Uhalisia hakiki .2.1.2
2.1.3
2.1.4
2.2
2.2.1
2.2.2
2.3
Kipindi cha Uhalisia wa Kijamaa .
Hatua za mwanzo za Uhalisiajabu .
Kipindi cha Uhalisiajabu ...••...
Vipindi vya uandishi wa K.W Wamitila .
Hatua za mwanzo za Uhalisiajabu .
Kipindi cha Uhalisiajabu .
Kiishilio I •••••••••••••• 11 •••••••• 1 ••••••• I" II••••••••••••••••••••
SURA YATATU
3.0
3.1
3.1.1
3.1.2
3.1.3
3
.
2
3.3
3
.
4
3.5
3
.
6
3.7
3
.
8
Utangulizi
Muhtasari wa Riwaya ya 8abu Alipofufuka .
Sehemu ya Kwanza ..
II. 11.11 ••••••• II. II. II •••• II' II. II ••••• I. II' II. IISehemu ya Pili II. II. II. II' •••••••••••• II •••• II. 11.11. II •••• II. II.
Sehemu ya Tatu ..II •••• II. I•••••••• II' II' II. II •••••••••• II. 1 ••• 1. II' II ••
Matukio ya Kiajabuajabu .
Ndoto na Uhalisia ..II. II. II. II •••• II. 11.11. II. II. I•• II. II ••••••• II' II. II
Uduara wa Wakati
Uvunjaji wa Mipaka ya Mahali
Mtindo wa Riwaya
·Visaasili ••••••••••••••••••••••••••..•••• ,» •••••••••••••••••••••....•••..•••••
vt
SURAVA NNE
4.0
Utangulizi 11 •••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••4.1
Muhtasari wa Riwaya ya Bina-Adamu! .4.1.1
Sehemu ya Kwanza ..II' II' II. II •••• 11.11. II. II. II. II. II ••••••• II ••••4.1.2
Sehemu ya Pili ..11.11. II' II. II. 11.11. II. 11.11.11.11. II. II. II•••••••••••4.1.3
Sehemu ya TatuMatukio ya Kiajabuajabu
4.2
4.3
Ndoto na Uhalisia ..II. II. II. II. II. II' •••••• II •••• II' 11.11 ••••• 1 •••• II ••4.4
Uduara wa Wakati4.5
Uvunjaji wa Mipaka ..II. II. II. II. II •••• II. II. II •••• II. II ••••••• II. II ••••4.6
Visaasili .~ •••••••••••••••••••••••••••••••••••••••• a •••• a •••••••••••••••••••••4.7
Kiishilio ..II•••••••••• II••••••••••••••• 10:1.II. II. 11••1.II. 11.11 •••• I ••I" II••SURAVA TANO
5.0
Hitimisho ...11 ••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••5.1
Matokeo ya Utafiti .5.2
Matatizo ...t.I•••••••••••••••5.3
Mchango ...•...5.4
Mapendekezo .(
MAREJElEO •••••••••••••••••••••••••••••••••••••••• ,.••••••••••••••••• 1 •••••••••••••••• I ••••
SHUKRANI
Kwanza natoa shukrani kwa Mungu Muumba kwa kunijalia afya na uwezo wa kuifanya kazi
hii. Namshukuru Dkt. Richard Wafula ambaye mbali na kuwa msimamizi wangu, alinishauri
na kunitia moyo katika kila hatua ya utafiti huu. Natoa shukrani kwa Dkt. catherine Ndungo
kama msimamizi wangu kwa kunishauri na kuniongoza katika kazi hii.
Nawashukuru wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika wa Chuo Kikuu
cha Kenyatta kwa motisha walionitia wakati nilipokuwa nikitafiti.
Shukrani zangu zimwendee Profesa Kimani Njogu aliyenitia mshawasha wa kushughulikia
swala la utafiti huu. Dkt. Kyalo Wamitila hawezi kusahaulika. Namshukuru kwa kunifaa kwa
vitabu namajalada yaliyoshadidia pakubwa usomaji wangu wakati nikitafiti.
Nawashukuru wengine wote waliochangia kwa njia moja au nyingine katika ufanisi wa
\111
IKISIRI
Utafiti huu umeshughulikia swala la uhalisiajabu katika riwaya teule za fasihi ya Kiswahili.
Riwaya zilizohakikiwa ni Babu Alipofufuka (2001) ya S.A. Mohamed na Bina-Adamu!
(2002) yaK.W. Wamitila. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mwelekeo
wa usasaleo. Hii ni nadharia ya uhalisiajabu. Katika nadharia ya uhalisiajabu, matukio
yanasawiriwa kiajabuajabu, ni ya kuogofya na kutisha. Matukio haya huashiria hali halisi ya
maisha katika jamii. Uhalisiajabu ni mtindo wa riwaya wa hivi majuzi unaopiku njia za
kimapokeo za uandishi wa fasihi ya Kiswahili na usawiri wa jamii. Kimapokeo, riwaya
inapaswa kujengeka katika misingi ya uhalisia.
Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo
tumeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada na
yaliyoandikwa kuhusu hii mada. Aidha, tumejadili upeo wa utafiti huu na misingi ya
nadharia iliyouongoza. Mwisho, mbinu za utafiti zimeelezwa.
Sura ya pili imejadili maisha ya waandishi S.A. Mohamed na K.W.Wamitila. Tumeonyesha
vipindi mbalimbali vya uandishi wao. Uchunguzi huu umedhamiria kuonyesha mitindo
waliyoitumia tangu waanze kuandika na pia kuonyesha ni kwenye kipindi gani cha uandishi
waliingilia uandishi wa kihalisiajabu na kwa nini walifanya hivyo.
Sura ya tatu na nne zinachunguza jinsi riwaya za Babu Alipofufuka na Bina-Adamu!
zimetumia uhalisiajabu katika kuwasilisha ujumbe. Tumeonyesha mihimili ya nadharia ya
uhalisiajabu waliyoitumia. Mihimili hii ni pamoja na matukio ya kiajabuajabu, ndoto na
uhalisia, uduara wa wakati, visaasili, uvunjwaji wa mipaka ya mahali na upekee wa mtindo
wa riwaya ya kihalisiajabu. ,;~
Sura ya tano imehusika na kulinganisha na kulinganua riwaya zote mbili kwa mujibu wa
mada husika. Aidha, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyokabiliwa katika utafiti na
Kutokana na utafiti huu, imebainika wazi kwamba Mohamed na Wamitila wanatumia
uhalisiajabu kimakusudi.Mihimili mikuu ya uhalisiajabu imo katika kazi zao. La maana zaidi
ni kwamba wanatumia uhalisiajabu kama mkakati unaowawezesha kujadili maswala
yanayousibu ujirani wetu. S.A. Mohamed anatumia mkakati huu kumulika rnatatizo ya
kiuchumina ya kijamii yanayowakabili Waafrika kutokana na utawala finyu wa viongozi
wao. K.W.Wamitila anatumia mtindo huo huo kuupiga vita utandaradhi na ubepari wa
kimataifa. Pamoja na kuonyesha matatizo yanayoyakabiliwa na Waafrika, Mohamed na
Wamitilawana imani kwamba matatizo ya Waafrika yanaweza kutatuliwa si kwa kutafuta
tiba hukonje katika mataifa ya Kimagharibi, bali kwa kuyatafuta humuhumu barani Afrika
SURAVA KWANZA
1.0 Utangulizi
Katika sura hii tumeshughulikia mada ya utafiti. Tumetambulisha mada yetu ambayo ni
kuchunguza jinsi uhalisiajabu unavyojitokeza katika riwaya za S.A Mohamed Babu
Alipofufuka(2001) na K.W Wamitila Bina-Adamu! (2002). Maswala na malengo ya utafiti
yameshughulikiwa pia. Tumejadili yale yaliyoandikwa kuhusu mada yetu. Hizi ni kazi
mbalimbali za kihakiki kuhusu uhalisiajabu katika uandishi wa sehemu mbalimbali
ulimwenguni kwa jumla, barani Afrika, kwenye fasihi ya Kiswahili na hatimaye na muhimu
zaidi katika riwaya zetu mbili. Aidha, yaliyoandikwa kuhusu nadharia ya uhalisiajabu
tunayoitumia katika uhakiki wetu yamepitiwa.
Tumefafanua sababu za kuchagua mada tunayoishughulikia na pia kuelezea upeo wa
utafiti wetu. Nadharia tunayoitumia imeelezewa na hatimaye mbinu za kukusanya,
kuchanganua na kuwasilisha data zimefafanuliwa.
1.1 Uhalisia, Usasaleo na Uhalisiajabu
Uhalisia ni mojawapo wa matapo maarufu katika ulimwengu wa fasihi na lenye athari
kubwasana. Kwanza uhalisia huashiria tapa la kipindi maalum cha kihistoria katika fasihi
ya Ulaya na pili huelezea aina ya mtazamo au tapa la kifasihi ambapo kazi za kifasihi
zinachukuliwa kama zinazohifadhi au kuakisi sifa za kimsingi zinazohusishwa na uhalisi.
Kazi zinazoangaliwa kama za kihalisia zinatarajiwa kuwa akisio la hali halisi ya maisha
katika jamiii inayohusika (Wamitila 2002: 114).
Uandishi huu ndio uliopokelewa katika baadhi ya nchi za Kiafrika ukawa uhalisia na uhalisia
wa kijarnaa. Uliingia katika riwaya ya Kiswahili katika kazi za waandishi kama vile
Shaft kwenye Kasri va Mwinvi Fuad (1978) na Kuli (1979) na Mohamed S. Mohamed
kwenye Kiu (1972) na Nvota va Rehema (1976) miongoni mwa nyingine.
Usasaleo ni dhana inayotumiwa kuelezea mielekeo ya kitamaduni na kisanaa
mavonusishwa
kwa kiasi kikubwa na karne ya ishirini. Kimsingi, dhana hii hutumiwa../
kuelezea au kuzitambulisha sifa mpya za dhamira, tanzu, dhana na mitindo ya kifasihi
inayohusishwa zaidi na miongo ya kwanza ya karne ya ishirini. Wakati unaohusishwa zaidi
na mkabala huu ni Vita Vikuu vya Pili vya Ulimwengu. Ni muhimu ikumbukwe kwamba
Vita Vikuu hivi vilisababisha uvunjifu mkubwa wa maendeleo na utamaduni wa kimagharibi.
Katika hali hii palihitajika njia, mbinu na hata miundo tofauti ya kuangazia na kuelezea
uvunjifu huo (Wamitila 2002: 123-124).
Harrow (2002:3) anasema kwamba fasihi ya Kiafrika katika karne ya ishirini imekua na
kutoka katika ushairi wa asili wa hapo awali wa kinegritudi (swala la ujitambuzi wa
Mwafrika) hadi kufikia riwaya za kisasa za hivi majuzi za uhalisiajabu. Waandishi wa riwaya
na mashairi walipoendelea kushuhudia mambo ya kipekee katika maisha yao na jamii zao,
mikakati mipya ya uandishi ilianza kujitokeza. Swala hili la mabadiliko liIijitokeza katika
shughuli za waandishi waliokabiliwa na migogoro ya jamii zao na wanaokusudia kuanzisha
utaratibu rnova wa kijamii na kitamaduni. Hapo awali waandishi wengi wa Kiafrika
wa uhalisia katika uandishi wao kwani ndio uliokuwa
ume oelewa na kukita mizizi.
Uhalisia huu ulitokana na mapokeo ya Kimagharjbi. Kizazi cha kwanza cha waandishi wa
Kiafrika kilisomea katika vyuo vya kimagharibi au vyuo vilivyoazima mitaala kutoka kwa vyuo vikuu vya kimagharibi. Hivi ndivyo waandishi kama Chinua Achebe, Ngugi wa
Thiong'o, Wole Soyinka na Ayi Kwei Armah waliandika kazi zao kama vile A Grain of Wheat,
3
Uhalisiauna misingi yake katika maendeleo na ustaarabu wa jamii za Kimagharibi. Uhalisia
ulifika kilele chake katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda na maendeleo mengine ya
kisayansi.Hivyo basi, uhalisia kama ulivyopokelewa hapo awali barani Afrika ni kielelezo
cha mitazamo na mielekeo liliyothaminiwa na jamii za Kimagharibi. Uhalisia ndio uliowapa
wazungu mantiki na motisha wa kutawala wananchi wa maeneo mengineyo. Waafrika
"waliazima" uhalisia kam~ ambavyo walivyoazima mambo mengine ya Kimagharibi.
Inaelekea kwamba uhalisia wa kifasihi kama amali zingine zilizoazimwa kutoka kwa jamii za
kimagharibi haujaleta maendeleo bora katika mitazamo ya Waafrika. Hii ndiyo sababu
ambayo imewafanya baadhi ya waandishi wa Kiafrika kuanza kuandika kwa kutumia mbinu
zingine za usanii. Waandishi wa Kiswahili hawajaachwa nyuma katika shughuli hii. Katika
karne ya ishirini na miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini na rnoja, kumeibuka baadhi ya
riwaya za Kiswahili ambazo zinadhihirisha vipengele vya uandishi wa usasaleo. Usasaleo
haukuibuka katika ombwe tupu. Kwa hakika usasaleo ni njia ya kuufinyanga ukweli wa
maisha kwa njia tofauti na vile ilivyozoeleka. Wasanii wanaoutumia hawautumii tu kwa ajili
ya kuutumia bali kwa lengo la kuangazia hali zao katika jamii wanamoishi
(Gromov 2002:3-4).
Uhalisiajabu ni mojawapo wa mikondo tofa utitofa uti ya usasaleo kama vile udenguzi wa
lugha, nadharia baada ukoloni na baadhi ya nadharia za kifeministi. Kutokana na kusoma
kwangu kwa riwaya ya Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002), nimegundua
kwamba riwaya hizi zina mwelekeo wa uandishi wa kihalisiajabu.
Katika mojawapo ya makala kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya riwaya ya Kiswahili Said
A.Mohamed katika Gromov (2002: 12) anasema:
Miongo ya mwisho ya karne ya ishirini ni kipindi mwafaka cha maendeleo ya
mbawa zao zimekatwa huku mashetani wakitembea wapendavyo na kuingia popote bila kikwazo chochote. Tunaishi katika ulimwengu ambao binadamu
amepokwa kwa kila njia kwa maslahi ya kiuchumi. Ni ulimwengu ambao hakuna aliye na uhakika kuhusu sio kesho tu bali hata leo, ambao watu hawakumbuki jana ... Ni ulimwengu ambao mambo ambayo hayangefikirika katika mwongo uliopita yanadhaniwa kuwa ya kawaida ... Ndio maana waandishi wengi wa Kiswahili wanashughulikia maswala ya kilimwengu kwenye kazi zao.
Wanafanya hivyo kwa mtazamo wa kisasa slo kwa kutoa maelezo ya matatizo ya ulimwengu wa leo, bali kwa kwanza kujaribu kuchunguza ukosefu wa mantiki wa matukio ya ulimwengu wa leo. IIi kuweza kutekeleza jukumu hili,waandishi wanatumia uhalisiajabu, uhalisiafifi na usasaleo - mitindo iliyoanzishwa katika fasihi ya Kiswahili katika miaka ya sabini.(Tafsiri yetu)
Riwaya za Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002) ni mifano ya uandishi huu.
Kwa kuzikabili riwaya hizi kama za kiuhalisiajabu, tumeweza kuzielewa vizuri zaidi na
kujua ni misingi gani au vichocheo vipi viliwasukuma waandishi hawa hata wakaanza
kutumia mbinu hii. Pamoja na haya, tumeweza kutambua sababu zilizowafanya kuasi
mbinu za awali kama vile uhalisia na uhalisia wa kijamaa.
1.2 Mada ya utafiti
Utafiti huu unakusudia kuchunguza jinsi vipengele vya uhalisiajabu vinavyodhihirika katika
riwaya ya Said Ahmed Mohamed Babu Alipofufuka (2001) na ya K.W. Wamitila
Bina-Adamu! (2002). Aidha, utafiti huu utabainisha jinsi uhalisiajabu unavyoshughulikia kadhia
zinazohusu maisha halisi ya watu wanaozungumziwa katika riwaya za Kiswahili teule.
Kutokana na jambo hili, tutaonyesha ni kwa nini uhalisiajabu ni njia mwafaka zaidi ya
5
1.3 Yaliyoandikwa kuhusu mada
Alexander (1990: 127) anasema kwamba uhalisiajabu ni kielelezo cha jinsi nadharia ya
usasaleo inavyotulazimu kufikiria upya juu ya dhana za kimapokeo kuhusu riwaya ya
uhalisia ya karne za kumi na nane na kumi na tisa. Aidha, uhalisiajabu umetulazimu
kuwazia ufaafu wa baadhi ya mitindo ya uandishi kwa mada tofauti tofauti. Baadhi ya
maendeleoya kuslsirnua katika mwisho wa karne ya ishirini ni kuwa kumeibuka waandishi
wanaotalii uhusiano kati ya historia na masimulizi ya ubunifu. Waandishi wa riwaya wa
Marekani Kusini Gabriel Garcia Marquez, Isabel Allende na Vargas Llosa kati ya wengineo
wameibusha na kutumia visaasili vya kitaifa katika kazi zao. Visaasili vya kitaifa ni visa
vinavyojaribu kuelezea mustakabali wa taifa lote kwa ujumla.
Drouart (1993) anasema kwamba tangu miaka ya 1950 na 1960, dhana ya uhalisiajabu
imehusishwa sana na uandishi wa kibunifu katika Marekani Kusini. Katika miaka ya 1940
huko Marekani Kusini, uhalisia wa kimaajabu ulikuwa njia ya kudhihirisha fikra za kikweli za
Wamarekani kusini na kuunda mtindo mpya wa kipekee na huru wa fasihi. Hata hivyo, ni
muhimu sana kujua kuna to fauti kati ya uhalisiajabu katika sanaa ya uchoraji na
uhalisiajabu katika sanaa ya uandishi hususan fasihi.
Roh (1925) alitumia neno uhalisiajabu katika mukhtadha wa ulimwengu wa sanaa
kuelezea aina fulani maalum ya kudhihirisha usiri ulioko kwenye maisha ya kila siku bila
kuupigia maswali yoyote uhalisia huo. Pamoja na hayo, uhalisiajabu katika kazi ya sanaa
hushughulika na kazi zinazoambatana na zisizoambatana na ujumi wa uhalisia.
Kulingana na Ousbv (2002) riwaya mashuhuri zaidi ya kiuhalisiajabu ni ile ya Gabriel Garcia
Marquez One Hundred Years of Solitude (1980). Riwaya hii ilichangia kutuzwa kwa
Riwaya zingine za Marquez zingine zinazoafiki utanzu huu ni pamoja na Chronicle of
Death Foretold (1983) na Love in the Time of Cholera (1985). Marquez aliathiriwa sana
katika uandishi wake na mitazamo na hali ya maisha ya umma uliokuwa mchanganyiko wa
Waafrika,Wahindi katika sehemu aliyozaliwa huko Colombia ya Marekani Kusini.
Chanady(1985) katika Rio (1999) anasema kwamba uhalisiajabu unahusu matukio yasiyo
ya kawaida, ya kiujiza au chochote kile kilicho kinyume cha uhalisia wa kawaida. La
muhimu zaidi ni kwamba matukio yanayotendeka katika uhalisiajabu hayawezi kujitenga na
uhalisia.
Floyd·Merrel anaelezea kwamba uhalisiajabu unatokana na hali mbili za ulimwengu
zinazopingana. Uhalisiajabu una misingi yake katika uhalisia au ulimwengu ambao
mwandishi anaujua, na pia humwezesha mwandishi kuuona uhalisia ambao kwa kawaida
hatuufahamu.
Okah (2002:94) akizihakiki kazi za Okri (1991) anatuelezea kwamba katika uhalisiajabu
uhalisia na ndoto havitofautishwi. Anaeleza kwamba:
Kwa kuingilia uwanja wa uhalisiajabu, Okri anatoa maelezo ya maisha nchini Nigeria. Maisha ya uhalisi na ya ndoto hayatofautishwi katika nchi hii ya Abiku. Maisha nchini Nigeria ni kama ya ndoto na yasio na mantiki. Kipengele hiki cha kifantasia kinafaa sana kufafanulia hall mbaya ya mambo katika taifa hili.
(Tafsiri yetu)
Gromov (2002:3-4) anaelezea usasa leo kuwa njia ya kuufinyanga ukweli wa maisha kwa
njia tofauti na vile ilivyozowewa. Yaani, wasanii wanaoutumia hawautumii tu kwa ajili ya kuutumia bali kwa lengo la kuangazia hali za jamii wanamoishi. Kulingana na Gromov
(2002), uhalisiajabu ni kitengo cha usasaleo ambacho kimefanikiwa kuzungumzia maswala
7
Mbatiah (2002:60) anaeleza kwamba uhalisiajabu ni istilahi inayotumiwa kuelezea mkondo
wa uandishi ambapo mazingira, matendo na matukio ya kifantasia husawiriwa kwa kuiga
mtindo wa uhalisia. Uhalisiajabu hufanya hivyo kwa kuyaeleza matukio kwa njia ya moja
kwa moja kana kwamba ni mambo ya kawaida. Wasanii wanaoutumia mtindo huu
hudhamiria kuonyesha kuwa ingawa mambo yanayoshughulikiwa ni ya kiajabuajabu,
hutokea katika maisha ya kawaida ya jamii inayohusika. Uhalisia wa kimaajabu huusishwa
zaidi na nchi zinazoendelea kutoka bara la Afrika, Marekani ya Kusini na Bara Hindi.
Wamitila (2003:274) naye anasema dhana ya uhalisiajabu huhusishwa na waandishi wa
Marekani ya Kusini au hata nchi zinazoitwa ulimwengu wa tatu. Sifa yake kuu ni
kuyaelezeamatukio ya kifantansia au ya kiajabu au kichawi kwa namna ya moja kwa moja
na kwa namna inayoyafanya yaonekane ya kawaida tu. Sababu hasa ya matumizi ya
mtindo huu ni kuonyesha kuwa matukio ya aina hii hupatikana katika maisha ya kawaida
katika jamii zinazohusika. Waandishi wanaoandika katika misingi hii hushikilia kuwa
mtazamo wao wa uhalisia unawakilisha msimamo wa jamii zao. Mpaka uliopo kati ya
mambo yanayoweza kupatikana katika ulimwengu halisi na yasiyowezekana kuwepo katika
ulimwengu huo huwa mdogo sana.
Hadi kufikia miaka ya 1960, fasihi ya Marekani kusini ilikuwa haitiliwi maanani na wasomi.
Kuibuka kwa riwaya ya kisasa katika miaka ya 1950 na 1960 kulibadillisha hali hii pakubwa.
Aidha, kuibuka kwa riwaya za kubuni
za
usasaleo kuliibadili hali iliyokuwepo hata zaidi(Williams 1995: 1). Gabriel Marquez kama mwanzilishi wa uandishi wa kisasaleo anafikiriwa
na wasomaji wengi wa kimagharibi kuwa mwandishi wa kifantasia. Kinyume na madai
haya, yeye mwenyewe amedai mara nyingi kuwa ni mhalisia ambaye anajaribu kuelezea
Kwa mfano, kwa mujibu wa Williams (1995), katika riwaya ya One Hundred Years of
Solitude (1980), Marquez anaelezea kuhusu wafanya kazi wa Macondo ambao wanaandaa
mgomo. Baadaye uvumi unaenezwa kwamba serikali imewaua mamia ya wafanyakazi.
Kisa hiki kimetajwa kuwa cha kifantasia kuliko vingine kwa sababu tukio la kihistoria
linapuuziliwa mbali na kuwasilishwa kama uvumi tu.
Wanahistoria na wasomi
warnekubaliana
kwamba hadithi hiyo ina ukweli wa kihistoria nayenye ukweli kuliko zingine. Hii ni kwa sababu inarejelea mauaji ya wafanyakazi wa
mashamba ya ndizi katika sehemu iliyojulikana kama Cienaga nchini Colombia mnamo
mwaka wa 1928. Ni wazi basi kwamba riwaya hii ya Marquez ni yenye ukweli
unaoshahabiana na matukio halisi ya kihistoria (Williams 1995:6).
Williams (1995:5) akimnukuu Fuentes ambaye ni mwandishi wa kihalisiajabu, anasema
kwamba wanahistoria wa Marekani Kusini wamebadili vile ukweli umekuwa ukitazamwa.
Ukweli ulikuwa ukipuuzwa. Kwa sababu hiyo, riwaya za usasa na usasaleo za Marekani
Kusini zimetoa hali tofauti ya ukweli. Fuentes anadai kwamba ni jukumu la waandishi wa
C
riwaya wa Marekani Kusini kuuelezea 'ukweli (kivyao) wanavyouelewa'.
Katika miaka ya 1960, Julio Cortazar na carlos Fuentes walipigia swali jitihada za falsafa za
kimagharibi katika kutafuta ukweli uliofanana, lakini ulioko katika mazingira tofauti. Yaani
kulingana na wamagharibi, ukweli ni bia. Fuentes na Cortazar wanasema kwamba jitihada
ya utafutaji wa 'ukweli' kila wakati ni ya Kimagharibi na yenye kupendelea mitazamo ya
Kimagharibi.
Nchini Chile, Allende ndiye mwandishi aliyeandika kazi zake za kwanza kwa kuiga mtindo
wa uhalisiajabu
ulioturniwa
hapo awali na Marquez. Alitumia mtindo huu kuandika riwaya9
kisiasa. Kama mtangulizi wake, anatumia uhalisiajabu kuyaangazia maswali ya nchi yake
yakiwemo siasa (Encarta Encyclopedia 2002).
Nchini Cuba kazi za Alejo Carpentier zina mchango mkubwa kwa uandishi wa kisasa.
Katika kazi zake The Kingdom of this World (1949) na The Lost Steps (1979), Carpentier
anatumia mtindo wa usasa kuelezea historia na utamaduni wa Cuba kibunifu. Waandishi
wengine kutoka Cuba waliotumia uhalisiajabu ni kama vile Miguel Angel Astrurias na Juan
Rulfo.
Mwandishi mwingine anayetumia uhalisiajabu katika kazi yake ni Mario Llosa Vargos
kutoka Peru. Riwaya moja aliyoandika kwa mtindo wa uhalisiajabu ni The Time of The Hero
(1963) inayozungumzia maisha yalivyokuwa katika chuo kimoja alichohudhuria nchi yake
ilipokuwa ikiongozwa na makadeti ikilinganishwa na uhuru uliokuwa nje ya chuo hicho.
Riwaya nyingine maarufu aliyoiandika Llosa ni Green House (1969) inayolinganisha maisha
ya jangwa la Peru na maisha katika mazingira ya kimji ya Piura (Wamitila 2002).
Salman Rushdie ni mwandishi wa riwaya wa Kiingereza, mzaliwa wa India ambaye
ametumia mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya zake. Riwaya ya Midnight's Children
inahusu rnaendeteo.va kisiasa nchini mwake India katika miongo iliyofuata kupata uhuru
kwa nchi hiyo kutoka kwa Waingereza (Alexander 1990: 127, 138-139).
Riwaya nyingine aliyoiandika katika mtindo huu ni ile iliyojaa ubishi mwingi ya SataniC
Verses (1988). Alexander (1990) akinukuu maneno y"aRushdie alipokuwa akihojiwa kuhusu
riwaya hii Rushdie alisema:
Kwa hivyo tunaona kuwa Rushdie anapendekeza kwamba watu katika nchi yake
wasijifunge kwa kila waambiwalo kuwa ndilo kila siku bali watazame na kuona linalowafaa
wao wenyewe.
Katika bara la Afrika, wengi wa waandishi waliotumia uhalisiajabu ni wa kutoka Afrika
Magharibi. Waandishi hawa nji kama Cheney-Coker wa Sierra Leone, Okri wa Nigeria na
Kojo Laing wa Ghana (Cooper, 1998: 1).
Oka (2002:90) akiielezea riwaya ya Okri ya The Famished Road (1991) iliyomwezesha
kutuzwa tuzo ya "Booker" (1991), anasema kwamba Okri anakagua kwa upekuzi maisha
ya wananchi wa Nigeria. Anatueleza kwa undani historia ya nchi ya Nigeria kuanzia wakati
wa ukoloni hadi wakati wa uhuru na maajilio ya utawala wa kijeshi. Kuzaliwa na kufa kwa
mhusika Azaro mara tano kunasimamia miongo mitano ya utawala nchini Nigeria. Miongo
hiyo mitano ni: utawala wa kikoloni, jamhuri ya kwanza, utawala wa kijeshi, jamhuri ya pili
na hatimaye utawala wa kijeshi tena. Oka (2002:90) anasema kuwa hadithi ya uhalisiajabu
ya Azaro ni kielelezo cha hali ya umaskini na siasa za nchi ya Nigeria.
Okri anasema kwamba:
Uandishi wangu ulikuwa zao la hasira, umaskini ulionizunguka na mwelekeo mbaya wa serikali kwa mateso ya wananchi. Ulikuwa wakati wa ufisadi mwingi nchini Nigeria. Kuwa mamlakani na uongozini na kuwa na nguvu kisiasa kulimaanisha kujinyakulia pesa kwako na jamii (kabila) lako (Okri 1990:viii).
Katika fasihi ya Kiswahili, kuna waandishi watangulizi wa uwanja huu wa uandishi.
Miongoni mwao ni Topan katika tamthilia ya Aliyeonja Pepo (1973) na Hussein katika
tamthilia ya Mashetani (1971). Hawa watunzi wanakaribia kutumia mbinu ya uhalisiajabu.
Hata hivyo, ingawa waliweza kubuni hali za kiajabuajabu, walifanya hivyo kwa kuchota
11
dhanaza miungu, mashetani pepo na mengineo zimekuwepo. Hata kama hadithi zao ni
zenye uajabu, walijua kwamba kuna ujumbe fiche humo ndani.
Aliyeonja Pepo ni hadithi kuhusu jinsi maisha yanavyoendelea baada tu ya mtu kufa.
(Topan 1970:3). Hata hivyo, kiini ni kuhusu mhusika mmoja aitwaye Juma Hamisi
anayeuawa na malaika wa kifo (Ziraili) kimakosa kupitia ajali ambapo Juma anapigwa
dafrau na punda badala y~tmtu anayestahili kufa anayeitwa John Houghton. Mushkili
unatokea kwa sababu Juma Hamisi anayetoka Bagamoyo ashazikwa na ameingia peponi
mahalikuliko na furaha nyingi. Basi inamlazimu Ziraili kumrudisha duniani tena kwa kipindi
cha mwaka mmoja ndipo atakapokufa.
Hii ni kwa sababu kila mtu ana wakati wake wa kufa na huo ulikuwa wakati wa John
Houghton wa kufa. John alikuwa afe kama matokeo ya gari lake kupambana na farasi saa
nne ya usiku. (Topan 1970:6) Hatimaye inambidi Juma Hamisi hata baada ya kuonja
utamuwa peponi kurudi duniani na kungoja wakati wake. Tatizo ni kwamba kwa sababu
huko duniani watu wake washamzika, Juma hawezi kurudi katika nafsi yake tena bali
atarudi katika nafsi ya paka wa rangi ya kijivujivu na madoa ya chui (Topan 1970:20).
Kwa mujibu wa maelezo ya Kruisheer (1997), tamthilia hii inaweza kusimamia hali
ilivyokuwa nchini Tanzania katika miaka ya sabini wakati ambapo mfumo wa ujamaa
ulikuwa ukitekelezwa. Topan anaelezea hali ya nchi ya Tanzania katika miaka ya baada ya
uhuru kwa kutumia mtindo fiche.
Anwani ya Aliyeonja Pepo ni falsafa ya Ujamaa. Bamkubwa ni Nyerere (kwa sababu ndiye
rnkubwa/rnkuu) wa wafanya kazi na aliyeanzisha falsafa ya ujamaa), sera ya miaka saba
inalinganishwa na sera ya miaka tano inayoongoza nchi, malaika - Ziraili, Jiburili, Munkari
na Sirafili ni wawakilishi na watumishi wa serikali, (Kruisheer katika Kiswhaili 59, 1997, uk.
10). Peponi ni afisi za serikali, duniani ni vijiji vya ujamaa.
JumaHamisi anapojulishwa kwamba arudi duniani kwa mwili wa John Houghton anasema
kwamba yeye ana roho ya kiujamaa na maisha ya kibepari ya Uropa, yeye hawezi
kuyafikiria. Kwa mfano analalamika kwamba yeye hawezi kamwe kuishi maisha ya
kuwanyonya binadamu wenzake. (Topan 1971: 19) Anasema yeye ni Muislamu na hawezi
kufanya kazi ya kuuza bia na kukaa na mbwa kama John Houghton. Hapa tunamwona
Topan akilinganisha mfumo wa Ujamaa wa Ubepari kama inavyojidhihirisha katika sura
mbalimbali.
Katika tahakiki yao ya tamthilia ya Mashetani, Kimani na Chimerah (1999:200-201)
wanatujulisha kwamba Juma na Kitaru wameamua kucheza mchezo wa Shetani na
Binadamu ili waielewe barabara hali yao ya sasa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa jumla.
Mchezo huu unachezwa katika jukwaa karibu na mbuyu (maskani ya mashetani
inavyoaminiwa na Waswahili).
Ni uigizaji unaomfunulia msomaji, mtazamaji na msikilizaji mahusiano yaliyopo baina ya
viongozi na waongozwa, uhuru na ukoloni mamboleo, ukoloni mkongwe,
unyanyaswajijugandamiswaji wa Waafrika na mabwana wazungu na vilevile mabwana
Waafrika wenye madaraka sasa na hata wale waliokuwa na madaraka hapo mbeleni kabla
ya kupokonywa.
Shetani amesawiriwa kama kiumbe mwenye nguvu na uwezo wa kufanya mambo yasiyo ya
kawaida kama vile kujibadilisha nafsi. Shetani anasema anaweza kujigeuza ndege, kuwa
upepo na pia kuweza kurukia tawi (Hussein 1971:2).
Vilevile tamthilia za Mashetani inaashiria uhalisiajabu pale ambapo sehemu ya pili ya
13
Aidha, Kitaru anatuelezea kuhusu sifa nyingine ya uhalisiajabu anapomwambia Juma kuwa
hajui kama alikuwa amelala au alikuwa anaota na kwa kweli mtu huona ukweli zaidi
kwenyendoto kuliko katika maisha ya kweli. Hiki ni kipengele muhimu sana cha nadharia
hii.Anasema:
Juma: Ndoto gani ulikuwa unaota? Unaikumbuka?
Kitaru: (kimya) Hata sijui kama ilikuwa ndoto au ni fikira tu.
Juma: Juu ya?
Kitaru: Wewe, mimi. (Anacheka) Ajabu katika maisha ya ndoto, mtu anaona ukweli
zaidi kuliko katika maisha ya ukweli.Tena siyo ndoto tu, na katika mchezo vilevile.
Kitaru: Kwa mfano, nimekujua wewe, nimejua mimi zaidi katika ... mchezo...
C
hapana, katika ndoto? Ajabu siwezi kusema ile ilikuwa ndoto, mchezo au ukweli
(Hussein 1971:47).
Kezilahabi ni mwandishi na mwanafasihi mwingine mashuhuri anayetumia mtindo wa
usasaleo katika kazi zake.Riwaya zake maarufu Nagona (1990) na Mzingile 1991) zimezua
mijadala mirefu kati ya wasomi mbalimbali.
Mbatiah (1997) anasema kwamba kimsingi riwaya za Kezilahabi zinahusu maisha ya
Tanzania na mandhari yake ni kisiwa cha Ukerewe. Anaendelea kusema kwamba katika
Nagona na Mzingile, mwandishi anamgurisha msomaji kutoka mazingira ya kilimwengu
aliyoyazoea na kumpeleka kwenye ulimwengu wa kindoto baina ya kifo na uhai, kuwa
macho na kuwa ndotoni.
Kwa kufanya hivyo, anamshirikisha msomaji katika safari ya kifikra ya kutalii ulimwengu ili
kuujua ukweli wake. Safari hii inapindua kabisa mtazamo wa kawaida wa ulimwengu na
Wamitila (1991) anasema kwamba riwaya za Kezilahabi za awali zilihisu ulimwengu wa
kimaumbile au jinsi ulivyo, kama tuujuavyo na kama tuionavyo. Hata hivyo, Wamitila
anazionariwaya za Nagona na Mzingile kuwa za kimetafizikia - yaani zilizopita ufahamu
wetu wa ulimwengu kama ulivyo. Mwandishi anaendelea kueleza kwamba ingawa haina
haja kujichosha kwa kujiuliza kwa nini Kezilahabi akajiingiza katika udhanifu au utopia,
yeye (Wamitila) anaona kwamba picha yoyote ya kimaumbile inayopuuza utopia si picha
kamilifu. Kwa mujibu wa Wamitila (1991), tunahitaji udhanifu iIi kuwa na uhalisia. Uhalisia
wenyewe huhusisha udhanifu. Anapendekeza kwamba riwaya hizi zichunguzwe upya labda
kwa mtazamo wa kifalsafa (1991:66).
Mbali na mshabaha wa waandishi Topan (1970) na Hussein (1971) katika misingi ya
uhalisiajabu, ni muhimu kutaja kwamba uandishi wao una tofauti kubwa na ule wa
Mohamed (2001) na Wamitlla (2002). Sababu hii ni ya kifalsafa. Ingawa watangulizi wa
uhalisiajabu waliweza kubuni hali za kiajabuajabu, walifanya vile kwa kuchota kutoka kwa
malighafi ya utamaduni wa Kiafrika ambapo tunajua tangu kale dhana za miungu,
mashetani, pepo na zinginezo zimekuwepo.
Waandishi Mohamed (2001) na Wamitila (2002) wanatumia uhalisiajabu kuandika
kimakusudi kwa sababu ya kutaka kuyaangalia maswala ya kijamii kiajabu na kwa njia ya
kipekee. Topan, Hussein na Kezilahabi wanaweza kufahamika vizuri kwa kutumia nadharia
nyinginezo.Mohamed na Wamitila katika kazizao za hivi karib,uni wanafahamika vizuri zaidi
kwa kuzingatia uhalisiajabu Tunachunguza ni kwa kiasi gani Mohamed na Waamitila
wamefaulu au kutofaulu kutumia mtindo huu. katika katika Babu Alipofufuka (2001) na
15
Fani na miundo ya mengi ya mashairi haya imeathiriwa sana na yale ambayo yamekuwa yakijiri katika jamii zetu tokea wakati huo (yaani 1987 alipoanza
kukiandika kitabu hicho) na hasa hiihali ninayoiita mimi
'uhalisiamazingaombwe', hali ya ndoto si ndoto, ukweli si ukweli.
Kutokana na maneno haya, inabainika kuwa huyu mwandishi mwenyewe anajua kuwa
amebadili mtindo wake wa kuandika kazi za sanaa za hivi karibuni. Babu Alioofufuka (2001)
inapatikana katika mkabala huu ambapo mtindo mpya umetumiwa kuzungumzia maudhui
mapya.
Waandishi wa fasihi ya Kiswahili wametumia uhalisiajabu kama vile wenzao katika maeneo
mengine ya ulimwengu kama vile Marekani kusini, Afrika ya Magharibi na kwingineko ili
kuyapigia mbizi maswala muhimu yanayowakabili wao na jamii zao. Hii ni njia mpya na ya
kipekee ambayo waandishi Mohamed na Wamitila wanaamini kuwa tofauti na zile zingine
zinazoonekena kugonga mwamba katika kuyaangazia na kuyasuluhisha matatizo ya mataifa
ya Kiafrika.Hii ni kwa sababu
uhahslajabu
una mkuruba zaidi na jamii zinazoshughulikiwa.1.4 Maswala ya utafiti
Katika kuzihakiki riwaya za Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002), tunazikabidhi
muktadha wake ambao ni kuzichunguza kwa mtazamo wa kiuhalisiajabu. Kwa hivyo ili
kuweza kushughulikia mada yetu ifaavyo, utafiti huu umeongozwa na maswali yafuatayo:
1. Je, uhalisiajabu unajitokeza vipi katika riwaya za Babu Alipofufuka na
Bina-Adamu!?
2. Ni kwa namna gani uhalisiajabu unaashiria na kuzungumzia uhalisia wa kimapokeo
katika katika riwaya hizi?
1.5 Malengo ya utafiti
Utafiti huu unalenga:
1. Kuchunguza ni vipi uhalisiajabu unajitokeza katika riwaya za Babu Alipofufuka na
Bina-Adamu!
?
2. Kubainisha ni vipi uhalisiajabu unavyoashiria uhalisia wa kimapokeo katika riwaya ya
Kiswahili. 'I
3. Kuonyesha ni vipi muktadha wa uhalisiajabu unatuwezesha kuzieleza zaidi riwaya za
Babu Alipofufuka (2000) na Bina-Adamu!
4. Kuchangia nadharia ya uhakiki wa fasihi ya Kiswahili.
1.6 Sababu za kuchagua Mada
Sababu kuu ya kuchagua mada hii ni kwamba kuna uandishi mpya katika fasihi ya Kiswahili
ambayo yanahitaji usomaji mpya. Uandishi huu umejitokeza katika riwaya za Babu
Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002). Pengine kutungwa kwa riwaya hizi kunaashiria
kuzuka kwa mikakati ya kipekee ya kushughulikia matatizo yanayoukabili ujirani wetu.
Jambo hili linapaswa kukaguliwa.
Utafiti huu pia umechangia uhakiki wa fasihi ya Kiswahili kwa kumzingatia mwandishi
Mohamed ambaye ni mwanariwaya mkongwe na Wamitila ambaye ni mwandishi riwaya
chipukizi kwa kuchunguza kazi zao zinazofanana. Uandishi wa Mohamed na Wamitila
katika Babu Alipofufuka na Bina-Adamu! ni uasi dhidi ya jinsi ambavyo waandishi wengi
wamekuwa wakiandika kwa miongo mingi. Utafiti huu unachunguza ni kwa nini waandishi
hawa wawili wameamua kutumia mtindo huu katika kazi zao. Aidha, riwaya hizi mbili
17
Kwa hivyo, tutakuwa tukiziba pengo katika uhakiki wa fasihi ya Kiswahili. Hatimaye,
uhalisiajabu ni uandishi wenye changamoto kubwa ambapo utunzi na uhakiki hukutanika.
Yaani, ni mtindo wa kuandika na vilevile mtindo wa kuhakiki. Hii ni kwa sababu wale
waandishi wanaoandika ni hao hao wanaozungumzia kazi zao au nyinginezo
zinazoshabihiana na zao. Tumetalii na kuona ni kwa kiasi gani mambo haya yanaingiliana
na ni kwa nini Mohamed na Wamitila wameamua kutumia mtindo wa uandishi wa namna
hii.
1.7 Upeo/Mipaka ya utafiti
Uchunguzi huu umejikita katika riwaya za Kiswahili tu ambapo tumechunguza riwaya ya
Mohamed Babu Alipofufuka (2001) na ya Wamitila Bina-Adamu! (2002). Waandishi hawa
wameandika riwaya zingine lakini hizi mbili zinatosheleza mahitaji ya utafiti huu kwa
sababu kutokana na mapitio tuliyoyafanya, riwaya hizi mbili zimeonyesha mwelekeo wa
uhalisiajabu. Inawezekana kuwa na riwaya zingine, tamthilia au mashairi yanayoweza
kuhakikiwa kwa kutumia mihimili ya uhalisiajabu. Hata hivyo hatujajihusisha na hayo kwa
sababu riwaya hizi mbili zina ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai yetu.
1.8 Misingi ya Nadharia
Nadharia tunayoamini inaafiki utafiti huu ni ya uhalisiajabu. Zamora (1995) anatueleza
kwambanadharia hii iliasisiwa mwaka wa 1925
na-
Mjerumani aliyejulikana kama Franz Rohaliyekuwa mhakiki wa sanaa.
Franz Roh alitumia istilahi uhalisiajabu katika muktadha wa sanaa kuelezea na kuonyesha
jinsi ya kusawiri aina fulani ya uujiza uliomo kwenye uhalisi uliozoelewa na unaotokana na
Akielezeauhalisiajabu Mbatiah (2002:60) anasema kwamba:
Istilahi hii inatumiwa kuelezea mkondo wa uandishi ambapo mazingira, matendo na matukio ya kifantasia husawiriwa kwa kuiga mtindo wa uhalisia. Yaani, kwa kuyaeleza kwa njia ya moja kwa moja kana kwamba ni mambo ya kawaida. Wasanii wanaoutumia mtindo huu hudhamiria kuonyesha kuwa ingawa mambo yanayoshughulikiwa ni ya kiajabuajabu, hutokea katika maisha ya kawaida ya jamii
inayohusika. Uhalisia wa kimaajabu huusishwa zaidi na nchi zinazoendelea kutoka bara la Afrika, Marekani ya Kusini na Asia.
Wamitila (2003:274) naye anaeleza kuwa:
Dhana hii ya uhalisiajabu huhusishwa na waandishi wa Marekani ya Kusini au hata nchi inazoitwa ulimwengu wa tatu. Sifa yake kuu ni kuyaelezea matukio ya kifantansia au ya kiajabu au kichawi kwa namna ya moja kwa moja kwa namna
inayoyafanya yaonekane ya kawaida tu. Sababu hasa ya matumizi ya mtindo huu ni kuonyesha kuwa matukio ya aina hii hupatikana katika maisha ya kawaida katika jamii zinazohusika. Waandishi wanaoandika katika misingi hii hushikilia kuwa mtazamo wao wa uhalisia unawakilisha msimamo wa jamii zao. Mpaka uliopo kati ya mambo yanayoweza kupatikana katika ulimwengu halisi na yasiyowezekana
huwa mdogo sana.
Kutokana na maelezo ya Mbatiah (2002) na Wamitila (2003), uhalisiajabu ni namna fulani
ya kueleza uhalisia uliotuzunguka. Waandishi wametumia mtindo huu makusudi kwa kujua
kwamba ni njia mwafaka ya kuyapigia mbizi maswala muhimu katika jamii. Tukiichunguza
mihimili ya nadharia ya uhalisiajabu inatosheleza uhakiki wa kazi yetu. Kwa kuzingatia
mihimili muhimu ya nadharia hii tutaweza kuzielewa riwaya tunazozihakiki na hatimaye
kufanikisha malengo yetu.
Amaryll katika Michelle (1993) anatueleza kuwa uhalrslajabu una sifa na mitazamo miwili
inayokinzana lakini pia inayokubaliana. Mtazamo mmoja ni ule wenye msingi wa uhalisi
ilhali wa pili una msingi wake katika imani kuwa uajabu ni kiungo muhimu cha ulimwengu
wa kila siku. Kwa hivyo kiini cha uhalisiajabu katika fasihi huwa ni msisitizo wa ushirikiano
19
Ingawa kuna matukio ya kiajabu katika kazi zinazozingatia uhalisiajabu, yanaunganishwa
na ulimwengu 'halisi' na matukio haya yana misingi yake katika uhalisi wa kijamii, uhalisi
wa kihistoria na kisiasa.
Cooper(1998: 16) ameshughulika kwa kina na uandishi wa kiuhalisiajabu hasa kwa kutilia
maananiwaandishi wa kutoka Afrika Magharibi. Anaelezea kuwa sababu za kiuchumi,
kijamii na kisiasa ndizo zinazowachochea waandishi kutumia mtindo huu katika kazi zao.
Akiwarejelea Jameson na Anderson, Cooper (1998) anasema kwamba kuna uhusiano kati
yamaendeleo ya kibepari na kuibuka kwa uhalisiajabu.
Jambo linalodhihirika kutokana na maelezo ya wasomi tuliowarejelea ni kwamba
uhalisiajabu haujajitenga na hali halisi ya jamii zetu, bali kwa kweli umeibuka kutokana na
hali mbalimbali za hizo jamii.
Kwamuhtasari, ifuatayo ndiyo mihimili ya nadharia ya uhalisiajabu:
(i) Matokeo ya kiajabuajabu yanayoonekana ya kawaida. Pia huwa na hali za
kushangaza, kuduwaza na kuogofya.
(ii) Uhalisi na ndoto vinachanganyika. Hakuna mipaka ya uhalisi na utohalisi katika
uhalisiajabu. Labda wakati mtu anapoota ndipo yupo uhalisini na wakati yupo
uhalisini ndipo tumo ndotoni.
(iii) Mipaka ya kijamii, kitaifa na kimataifa huvunjwa. Maanake ni kuwa
wanauhalisiajabu wanajadili mambo yanayohusu ulimwengu kwa jumla bila
kujiweka katika mazingira finyu kama vile.jamii, nchi au bara moja.
(iv) Wakati na mahali vina uhusiano wa kiduara badala ya kistari. Inamaanisha
kwamba jambo linaloweza kufanyika wakati mmoja (ambalo linaweza kuwa si la
(v) Uhahalisiajabu umefungamana na sanaajadi kama vile visaasili na hadithi. Kisaasili ni hadithi zinazoeleza asili ya watu na matukio fulani.
(vi) Matukio hayafuatani kimantiki kama ilivyo kawaida. Mtindo wa baadhi ya tanzu za fasihi simulizi hutumika. Jambo hili hufanywa kwa kumpeleka msomaji kwenye safari ya hali na matukio ya kikweli na yanayowezekana. Aidha, wasanii hutumia mbinu ya ukumbukaji, mbinu rejeshi, mtiririko wa urazini na ujenzi wa wahusika wenye nafsi mbili.
(vii) Mazingira' ni sehemu muhimu sana katika aina hii ya fasihi. Wanyama, majitu, misitu mikubwa yenye giza totoro, wanyama hatari na mazimwi hurejelewa.
Vilevile mimea, mito, maziwa na bahari huchukua nafasi muhimu katika uandishi wa uhalisiajabu.
(viii) Uhalisiajabu unapinga uhusiano wa kadhia zinazotendeka katika maisha ya mtu kiutengano. Hali mbalimbali kama vile uhalisi na ndoto, kifo na uhai, usasa na
uzamani, shamba na mjini, ugeni na wenyeji tamaduni huonekana zikiingiliana (Danow
1995:74,
Cooper1998,
Zamora1995,
Drouart1993
& Encarta Encyclopedia 2002).21
1.9 Mbinu za utafiti
Utafiti wetu umejikita maktabani. Sababu ya kwanza ya kufanya hivi ni kuwa huko ndipo
tumepata vitabu vinavyohusiana na riwaya za Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu!
(2002).
Vilevile, katika maktaba tumepata vitabu vya kusoma kuhusiana na nadharia ya
uhalisiajabu tunayoitumia katika uhakiki wa kazi yetu. Aidha tumepata vitabu, majarida na
makala mengine yaliyochangia kazi hii.Tumesoma vitabu vingine vya waandishi Mohamed
na Wamitila ili kuweza kuelewa falsafa zao kuhusu uandishi wa kazi zao. Aghalabu
mazingiraanamoishi mwandishi, uhusiano wake na jamii, juhudi na mafanikio yake huathiri
mtazamo wake kuhusu maisha. Jambo hili linaweza kujulikana kwa kusoma kazi nyingine
za mwandishi. Hatimaye, tumeshawahoji waandishi wa riwaya hizi mbili. Jambo hili
limetusaidia pale inapowezekana na kuhitajika.
IIi kupata data ya kutumia katika utafiti huu, tumesoma riwaya mbili tunazozihakiki kwa
lengo la kuchunguza jinsi uhalisiajabu unavyosawiriwa.
Pili,tumesoma vitabu vinavyohusu nadharia tunayoitumia ili kuielewa na vilevile kuifaharnu
mihimili yake mahsusi. Hii ni muhimu kwa sababu vipengele hivyo ndivyo tunavyotumia
kutuongoza katika uchunguzi wetu na kutuwezesha kuelewa msingi wa kuudhibiti utafiti
huu. Kazizilizohakikiwa kwa kutumia nadharia hii pia zimesomwa ili kutupa mwanga zaidi
kwenye uhakiki wetu.
Mambo haya yote yamefanywa ili tupate data ya kutuwezesha kujibu maswali yetu na
hatimaye kufanikisha lengo letu. Baada ya kusoma riwaya zetu mbili tumepata data
ambayo imejenga uchunguzi wetu. Data ambayo tumekusanya baada ya kusoma nadharia
nayo piaimetumiwa katika ufafanuzi wa uhakiki wetu.
Hivi ni vipengele vile tunavyohisi vitafaa zaidi katika uhakiki wa kazi hii. Baada ya kusoma
riwaya zetu tunazihakiki kwa mujibu wa nadharia ya uhalisiajabu na kwa kufuata mihimili
ya uhalisiajabu tutaweza kuchunguza ikiwa vigezo hivyo vinabainika katika riwaya za Babu
Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002). Zaidi ya hayo, tumeshirikisha maoni ya
wataalamu katika taaluma hii hasa kuhusiana na mada na nadharia ya utafiti.
1.10 Kiishilio
Katika sura ya kwanza tumetambulisha utafiti wetu unahusu nini. Mada ya utafiti
imeelezwa. Tumeelezea yale yaliyoandikwa kuhusu mada yetu ya utafiti. Maswala na
malengo ya utafiti yamegusiwa na tumetoa sababu za kuchagua mada husika. Hatimaye,
upeo wa utafiti, nadharia ya iliyotumiwa katika utafiti imefafanuliwa na pia mbinu za utafiti
zimeelezewa. Katika sura ya pili, tutashughulikia maisha ya Mohamed na Wamitila na kazi
ambazo wameziandika. Tutachunguza maendeleo ya mawazo yao katika uandishi wao
tangu waanze kuandika hadi wanapofikia kiwango cha kuandika kwa kutumia mbinu ya
uhalisiajabu. Sababu hasa ya kufanya hivi ni kuweza kupata mwanga zaidi wa kutuwezesha
kuelewa riwaya zao tunazozihakiki za Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002).
23
SURAVA PILI
2.0 Utangulizi
Katika sura ya kwanza tuliitambulisha mada ya utafiti huu ambayo ni kuchunguza jinsi
uhalisiajabu unavyojitokeza katika riwaya za Mohamed Babu Alipofufuka (2001) na
Wamitila Bina-Adamu! (2002). Maswala na malengo ya utafiti pia yalishughulikiwa.
Tumejadili yale yaliyoandikwa kuhusu mada yetu. Sababu za kuchagua mada
tunayoishughulikia zimefafanuliwa na upeo wa utafiti wetu kuelezewa. Nadharia
tunayoitumia imeelezewa na hatimaye mbinu za utafiti zimefafanuliwa.
Kama ilivyotajwa katika kiishilio cha sura ya kwanza, katika sura hii tutashughulikia historia
ya uandishi ya waandishi Mohamed na Wamitila. Katika kufanya hivyo tutaweza kuelewa
wamekuwa wakiandika kwa kutumia mitindo gani hapo awali na ni kwa nini
wameshughulikia kazi zao mahsusi tunazohakiki kwa kutumia mtindo wa uhalisiajabu.
2.1 Vipindi vya Uandishi wa Said Ahmed Mohamed
5.A.Mohamed alizaliwa Unguja (Zanzibar) mwaka wa 1947. Alipata elimu yake ya msingi na
shule ya sekondari visiwani Zanzibar.Baadaye mwaka wa 1974 alijiunga na Chuo Kikuucha
Dar-es-Salaam kusomea shahada ya B.A (Elimu) na kisha kusomea Isimu katika kiwango
cha M.A katika chuo hicho hichb. Baadaye alisomea shahada yake ya Ph.D nchini
Ujerumani. Ni mhadhiri aliyefundisha visiwani Zanzibar, Vyuo Vikuu vya Nairobi na Moi
nchini Kenya na Chuo Kikuu cha Osaka nchini Japani. Kwa sasa, ni mhadhiri katika Chuo
Kikuu cha Bayreuth nchini Ujerumani anakofundisha fasihi ya Kiafrika.
5.A. Mohamed alianza kuandika alipokuwa katika shule ya msingi mnamo miaka ya 1960.
Alitunga mashairi yaliyosomwa siku za wazee na mengine kutangazwa katika idhaa
Katika miaka hiyo hiyo ya 1960, idhaa ya Kiswahili ya BBC ilianzisha mashindano ya
uandishiwa hadithi fupi za Kiswahili.Alishiriki katika mashindano hayo. Moja kati ya hadithi
alizoandika ni 'Msiba wa Pamoja' katika Hekaya za Kuburudisha. Katika miaka ya 1970
alianza kuandika vitabu vya misemo. Vitabu hivi ni kama vile Vito vya Hekima, Methali na
Misemoya Mshangao na Milio na Tashbihi. Baadaye alianza kuandika riwaya. Riwaya yake
ya kwanza ilikuwa Asali Chungu (1978). Riwaya nyingine alizoandika ni Utengano (1980),
Dunia Mti Mkavu (1980), Kiza katika Nuru (1988), Tata za Asumini (1990), na Babu
Alipofufuka (2001).
S.A.Mohamed ni mwandishi wa mashairi
~a
tamthilia pia. Diwani za mashairi alizotunga ni Sikate Tamaa (1980), Kina cha Maisha (1984) na Jicho La Ndani (2001). Nazo tamthiliaalizotunga ni Pungwa (1988) Kivuli Kinaishi (1990), Amezidi (1995) na Kitumbua Kimeingia
Mchanga (2001).
Uandishi wa S.A. Mohamed unaweza kugawanywa katika vikundi vinne.
2.1.1 Kipindi cha uhalisia hakiki
Huu,ni uhalisia ambao huhusisha uchunguzi wa kihakiki wa hali ya kijamii, matatizo
yanayoikabili jamii hiyo na madhara yake. Uhakiki huu hata hivyo hautoi suluhisho ya
matatizo hayo mbalimbali. Uhalisia ya kihakiki unaelekea kuchukua msimamo wa ubaki
fulani wa kuendelezwa kwa hali kama ilivyo. Kwa mujibu Wamitila (2003:274), huu ndio
mojawapo ya upungufu wa uhakiki huu.
Katika kipindi hiki cha uandishi wa S.A.Mohamed kaziambazo zinaweza kuratibiwa hapa ni
kama vile Asali Chungu (1978) na Utengano (1980).
Kipindi hiki cha uandishi kinahusisha uandishi unaoshambulia maovu ya kijamii bila
25
nzuri.Hata hivyo katika hii hii jamii hutokea watu ambao huharibu utaratibu ama kwa
kukiuka maadili ya kidini na kutatiza hali nzuri inayotarajiwa katika jamii husika. S.A.
Mohamed alipokuwa akiandika kwa mtindo wa uhalisia hakiki, alikuwa akiihurumia jamii
yake. Anaihakiki jamii kwa kuzingatia jinsi jamii ya Kiislamu inavyopaswa kuongozwa kwa
sababu kuna sheria ambazo waumini hupaswa kutii na matarajio wanayopaswa kutimiza.
Hata hivyo baadhi ya wahusika ni wanafiki na hawafuati utaratibu wa jamii uliozoewa.
Uandishi wa aina hii unaweza kuchukuliwa kama mahubiri ili kuirudisha jamii kwenye
mwelekeo unaofaa. Kwa mfano katika riwaya ya Asali Chungu (1980), Zuberi anasawiriwa
kama mzee aliye na tabia ya kupenda kushiriki kimapenzi na wasichana wa umri wa binti
zake inwenyewe. Ni watu kama hawa ambao Mohamed anaodhamiria kuasa.
Upungufu wa mtindo huu wa uandishi ni kwamba utatuzi wa matatizo yaliyowakabili
wanyonge hutegemea huruma ya wenye nguvu. Ina maana kwamba anayenyanyaswa
asipohurumiwa na mnyanyasaji hali yake ya maisha haitabadilika. Wanajamii wanategemea
majaaliwa. Mtindo huu wa uandishi hauleti mapinduzi ya msingi. Jambo hili linafafanuliwa
zaidi na mwandishi wa Kirusi Maxim Gorky.
Maxim Gorky ni mmoja wa wale waliopinga mtazamo wa uhalisia hakiki na kuunga mkono
nadharia ya uhalisia wa kijamaa. Alielezea upungufu wa nadharia ya uhalisi wa kihakiki kwa
kusema:
Uhalisia hakiki ni muhimu tu kwa kadri unavyoangazia kujimudu kwa zamani na harakati za rnwanajarnu kuparnbana dhidi ya hali dhalili ...Uhalisia wa kijamaa kwa upande mwingine hupambanua kwamba maisha ni vitendo na uzalishaji ambao lengo lake ni maendeleo bila kizuizi cha uwezo wa binadamu dhidi ya nguvu za mazingira (Khaemba 1990: 14).
Mwandishi anasisitiza kwamba ingawa uhalisia hakiki,ulionyesha matatizo na uozo wa jamii
na kumulika maisha na matatizo ya mtu binafsi pamoja na mafunzo ya imani za kidini na
. .'
sheria dhalimu za nchi, haukuonyesha jinsi ya kujinasua na hali hii. Pengine hapo ndipo
-S.A.Mohamed alionakwamba wahusika wake walibaki pale pale wakiwa wamekubali nafasi
yao. Labda haya ndiyo yaliyomfanya mwandishi kubadilisha mtazamo wake na njia yake ya
uandishi.Lengo la Mohamed la kufanya hivyo likawa la kuwaumba wahusika wachochole
lakini waliokuwa na nia na ari ya kuzibadilisha hali zao kwa kupigana na utabaka na
unyanyasaji. Wahusika walio na uwezo wa kuiangalia hali yao ya maisha kama
iliyosababishwa na historia wala sio majaliwa.
2.1.2 Kioindi cha uhalisia wa kijamaa
Kwa mujibu wa Suchkov katika Khaemba (1999), nadharia ya uhalisia wa kijamaa ilizuka
pale wanajamii walipong'amua kwamba rnahttaji ya jamii yanatawaliwa na mahitaji ya
kiuchumi na wala si fikra za watu ama majaaliwa. Uhalisia wa kijamaa uliiona jamii jinsi
ilivyo na ukaonyesha mikinzano iliyomo na chanzo chake. Nadharia hii inapendekeza
namna ya kutatua matatizo ya kijamii ili kuunda jamii mpya iliyokuwa bora zaidi na ikawa
sharti kanuni za nadharia hii zizingatiwe na waandishi na wahakiki.
Baada ya kongamano la waandishi uliofanyika mnamo 1934 nchini Sovieti ya za~ani,
uhalisia wa kijamaa ulipendekezwa kuwa msingi wa fasihi ya Kisovieti. Ilipendekezwa kuwa
mwandishi wa fasihi katika Usovieti anapaswa kusema ukweli juu ya jamii bila kuficha
chochote. Katika kazi za fasihi, pia kulihitajika kuonyesha kipindi mahsusi cha kihistoria.
Lukacs (1963:91) anasisitiza umuhimu wa jambo hili kwa kuliona katika misingi ya uhalisia:
Tofauti ya uhalisia hakiki na ule wa kijarnaa umo katika mitaala iliyobobea kiitikadi.
Muhimu ni pendekezo kuwa sanaa ya kijamaa ni sanaa ya kitaifa kwa kuwa
huangazia mazingira mahsusi ya kihistoria ambamo jamii fulani imepitia (Khaemba
1999:16).
Tunaweza kusema kwamba hiki ndicho kipindi cha pili katika uandishi wa S.A.Mohamed.
Mtazamo huu hujaribu kusisitiza uwasilishi wa uhalisia unaotilia mkazo mkubwa maendeleo
27
Kaziambazo S.A.Mohamed aliandika wakati huu ni kama vile Dunia Mti Mkavu (1980),
Utengano(1980), Kiza katika Nuru (1988) na Tata za Asumini (1990).
Katikakipindi hikimwandishi anachagua kimakusudi itikadi ya kijamaa kuuelekeza uandishi
wake. Katika kufanya hivyo anadhamiria kuwa itikadi ya kijamaa inaweza kumsaidia
,
kutatua matatizo ya kijamii
"
ha
kiuchumi. Mwandishi anonyesha katika uandishi wake kuwamatatizo yajamii yanatokana na mitafaruku ya kiuchumi, kitabaka na unyonyaji. Suluhu ya
matatizohaya ni mapinduzi yatakayoleta usawa kati ya wanajamii.
Kamunde (1983) katika tasnifu yake anashughulikia unyonge wa kiuchumi uliomo katika
tabaka la chini katika jamii. Aidha anajadili kiburi cha watukufu katika riwaya za Asali
Chungu (1978), Utengano (1980) na Dunia Mti Mkavu (1980). Kamunde anakusudia
kuwajadili wahusika mbalimbali na jinsi wanavyodhihirisha unyonge wa kiuchumi, kisiasa
na kijamii.Kutokana na uhakiki huu, uhalisia wa kijamaa unadhihirika zaidi katika riwaya ya
Dunia Mti Mkavu (1980). Katika riwaya hii, wahusika wanajaribu kuboresha hali yao ya
maishakwa kufuata mwelekeo wa uhalisia wa kijamaa.
Jambo hili linashadidiwa katika uhakiki wa Alamin Mazrui (1984) anapojadili n~mna
maudhui ya mapinduzi yanavyojitokeza katika riwaya ya Dunia Mti Mkavu kwa kutumia
nadharia ya Kimarx. Kimani Njogu (1997) anatumia nadharia ya uhalisia wa kijamaa
kujadili maudhui katika riwaya za visiwani hususan zilizotungwa na Shafi A. Shafi,
Mohamed S. Mohamed na S.A. Mohamed. Uhakiki wa Njogu unajadili utabaka, migogoro
inayotokea katika haya matabaka, chanzo cha migogoro, na kulipuka kwa mapinduzi
2.1.3 Hatua za mwanzo za uhalisiajabu
Kazi zilizoshughulikiwa na S.A. Mohamed katika kipindi hiki cha uhalisiajabu ni kama vile
Pungwa (198 ), Kivuli Kinaishi (1990 ) na Amezidi (1995).
Pungwa ni tamthilia inayohusu migogoro iliyopo baina ya ubepari na ufanyikazi.
\
Tamthilia ya Kivuli Kinaishlt(1990) inaonyesha misingi ya imla na jinsi inavyoendelezwa.
Mwandishi anasema kwamba mashiko ya uongozi wa kiimla ni ufisadi, uwongo,
ukandamizaji na upungufu wa nafsi ya mtu (Wafula 1999: 148).
Dalili za uhalisiajabu zinaonekana katika tabia ya Kirembe hasa anapofuma uongozi wake
katika miujiza, uajabu na sihiri. Tunaambiwa kwamba Bi. Kirembwe anajilinganisha na
mmoja kati ya miungu wa Rorna. Kwa kufanya hivi, anajipa uwezo na sifa za kuishi daima
dawamu. Hiki ni kielelezo cha jinsi baadhi ya viongozi wanavyohusudu nguvu za kisiasa na
kiuchumi hivi kwamba wanatamani hata kuwa miungu ili wasife na kuacha uongozi.
Wafula (1999) anasema kwamba kuzaliwa\wa Kirembwe kumefumwa katika miujiza.
Kirembwe anadai kwamba alizaliwa na tete za utawala. Miviga yote inayofanywa baada ya
kuzaliwa kwake ni dhihirisho la wajibu huu wa kirnalkia:
Nikafikishwa mafusho ... uvumba ... ubani ... mvuje; kitunguu saumu na ma]am mlangamia. Wakanifundisha mizungu. Mimi malikia wa wachawi Kirembwe niliyerembekezwa. Kirembe mnywa kinywaji cha uzima kilichoremwekewa wengu la mamba na mafuvu yawafu... Kinywaji chenye sumu isiyotupata wazee. Nani atakaye ubishi? Nani? (Mohamed 1990:42).
Maelezo haya yanapaswa kuwasadikisha Wanaginingi kwamba Bi.Kirembwe ni malkia wao
kutokana na majaliwa wasiyokuwa na uwezo juu yake. Uwezo wake unafanana na uwezo
wa kiungu tuuonao katika mhusika shetani katika tamthilia ya Mashetani (1971).
Wafula (1999: 162) anasema kwamba 'kivuli' ni tamathali inayoashiria upinzani dhidi ya
29
Madai haya yanatukumbusha jinsi S.A.Mohamed anavyomtumia mhusika Babu katika
riwaya ya Babu Alipofufuka ili kumjulisha K kwamba amefufuka na pia kumkumbusha
wajibu wake katika jamii yake ambao alikuwa ameusahau. Babu anamwambia K kwamba
ni lazima aamini kwamba wafu huweza kufufuka. Bi Kirembwe anaweza kumithilishwa na K
wa Babu Alipofufuka kama tunavyoona kwenye dondoo hii:
Bi Kirembwe: Sauti:
Bi. Kirembwe: Sauti:
Bi. Kirembwe: Sauti
Bi. Kirembwe Sauti:
Nini ni nini hicho? (kaemewa zaidi) Sauti .
Haya sa ... sau ... sauti ya nini tena? Sauti ya Kivuli
Kivuli gani? Kivuli kinachoishi!
Kivuli gani hicho, kivuli kisichokufa/
Kivuli kinachoishi, kivuli kisichoweza kufa ... kivuli cha ukweli na haki ... (Mohamed 1990:127).
S.A.Mohamed ametumia ngano, visakale na maono ambavyo ni vipengele vya uhalisiajabu.
Kwa mfano katika onyesho la kwanza tunasawiriwa Bi. Kizee akiwatambia watoto hekaya.
Kipengele cha kufungamanisha vipengee vya kijadi vya sanaa za maonyesha na mbinu za
kileo za kuigizia tarntluua .. Mohamed anaithamini ngano ya Wanaginingi kwa vile
anatufundisha sisi wa kizazi hiki kuhusu hali yetu ya maisha na jinsi ya kuirekebisha ikiwa
imeenda kombo au jinsi ya kuyaboresha maisha kwa kuyarahisisha na kuyafurahia.
Tamthilia ya Amezidi (1995) ni kazi nyingine ya S.A. Mohamed inayodhihirisha hatua za
mwanzo za uandishi wa kihalisiajabu. Huu ni mchezo wa mawazoni unaotazama matatizo
ya kijamii na ya kiuchumi katika nchi nyingi za Kiafrika za hivi leo. Hii ni sifa mojawapo ya
uhalisiajabu. Katika tamthilia hii, pia tunaona matukio ya kiajabu kama vile wahusika
wanaokufa kwa kipindupindu kwa sababu ya kula nyama ya msaada iliyooza. Ame na Zidi
walinayokuwa nayo. Wanaishi katika kasri la mawazoni, kupiga simu zisizokuwepo na
kulaliavitanda vipana visivyokuwepo.
Kimani na Chimerah (1999:75) wanasema kwamba wahusika wa kibwege si wa kihalisia
wanaoweza kutambulika na kuonekana katika mazingira yetu, bali wamebuniwa akilini
mwa mwandishi ili kuendeleza mawazo yake. Udhahania wao unatufanya tuwacheke, na
katika kuwacheka tunajicheka sisi wenyewe.
Vipengele vingine vinavyoonyesha dalili za uhalisiajabu katika tamthilia ya Amezidi ni kule
kuwa na mhusika mmoja anayechukua sura za watu mbalimbali, vicheko vinavyotumiwa
na mwandishi kuonyesha ukengeushi na vicheko visivyojulikana mahali vinatoka.
Kwa mujibu wa Wafula (1999:83), mtindo wa uandishi wa Amezidi unasawiri tarehe mpya
katika utunzi wa tamthilia ya Kiswahili. Nakubaliana naye kuhusu kauli yake na kuongeza
kwamba tarehe hii mpya haiko katika tamthiia ya Kiswahili tu bali pia kwenye riwaya ya
Kiswahili. Mohamed amethibitisha haya katika utunzi wa Pungwa, Kivuli kinaishi, Amezidi
na kwa kinaganaga zaidi katika Babu Alipofufuka.
Wamitila (2002:273) anaelezea kwamba katika miaka ya hivi karibuni mtazamo wa uhalisia
umeelekea kushambuliwa kwa sababu ya ubunifu wake. Ubunifu huu unahusiana na
majaribio ya kifasihi, kupinga kwake kwa sifa kama za kifantansia, bulinizi za kisayansi
ambazo kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya uhalisi wa siku hizi na ugumu uliopo wa kuielezea
dhana yenyewe. Inaelekea kwamba waandishi kama S.A. Mohamed na K.W. Wamitila ni
31
2.1.4 Kipindi cha uhalisiajabu
Hikindicho kimekuwa kipindi cha hivi karibuni na pia kilele cha uandishi wa S.A. Mohamed.
Katikadibaji ya Jicho la Ndani (2001) S.A. Mohamed mwenyewe anasema:
Fani na miundo ya mengi ya mashairi haya imeathiriwa sana na yale ambayo
yamekuwa yakijiri katika jamii zetu tokea wakati huo (yaani 1987 alipoanza
kukiandika kitabu hicho) na hasahii hali ninayoiita mimi
'uhalisiamazingaombwe' hali ya ndoto si ndoto, ukweli si ukweli.
Madaihaya ya mwandishi huyu yanadhihirisha kwamba anajua yeye mwenyewe amebadili
mtindo wake wa utunzi. Anasema hali ni ile anayoiita "uhalisiamazingaombwe" yaani hali
ambayo ndoto si ndoto ukweli si ukweli. Hiki ni kigezo cha uhalisiajabu kwa sababu katika
mtindo huu ukweli na ndoto ni kama kitu kimoja. katika Mohamed katika Gromov
(2003:12) anasema kwamba, miongo ya mwisho ya karne ya ishirini ni kipindi mwafaka
cha maendeleo ya riwaya. Hii ni kwa sababu katika kipindi cha mwanzo wa utandaradhi
tumeshuhudia uporomokaji wa maadili ya kibinadamu. Mwandishi anasema kwamba
tunaishi katika ulimwengu ambao binadamu amepokwa kwa kila njia kwa maslahi ya
kiuchumi.Ni ulimwengu ambapo hakuna aliye na uhakika kuhusu sio kesho tu balihata leo.
ulimwengu ambao watu hawakumbuki jana na ulimwengu ambao mambo ambayo
hayangefikirika mwongo uliopita yanachukuliwa kama ya kawaida.
Hii ndio sababu inayowafanya waandishi wengi wa Kiswahili kushughulikia maswala ya
kilimwengu katika kazi zao wakitumia mtazamo wa kihalisiajabu kuelezea matatizo ya
ulimwengu wa leo na pia kujaribu kuchunquza ukosefu wa mantiki wa matukio ya
ulimwengu wa leo. IIi kuweza kutekeleza jukumu hili, waandishi wanatumia uhalisiajabu,
uhalisiafifi na usasaleo.
Riwaya ya Babu Alipofufuka (2001) ni kielelezo mwafaka cha uandishi wa uhalisiajabu.
Kwenye kazi hii mwandishi ametumia mtindo ambao huhusisha matukio ya ajabuajabu
ambayo hufikiriwa kama ya kawaida tu. Katika uadishi huu pia, mpangilio tuliouzoea katika
mitindo mingine ya kuwa na mwanzo, kiini cha kazi ya fasihi na hitimisho, haufuatwi bali
hadithi inaweza kuanzia mwisho ikafuatia sehemu ya katikati na kuishia na sehemu
inayopaswakuwa ya kwanza. Mipaka ya kitaifa na kimataifa huondolewa na mwandishi na
mhusikaanaweza kutoka nchi au hata bara moja na kuzuru lingine. Aidha, dhana ya wakati
katikauhalisiajabu ni ya duara wala si kistari kama ilivyozoeleka.
Kwa kutumia mtindo huu kama tulivyoeleza hapo juu, waandishi wanaoutumia wanaamini
kwamba wataweza kufanikiwa zaidi kuwasilisha ujumbe wao kuliko vile ingekuwa
wangalitumia mitindo ya kimapokeo.
2.2 Vipindi vya Uandishi wa K.W. Wamitila
Wamitila ni mwandishi, mwalimu, msomi na mhakiki wa fasihi ya Kiswahili. Katika maisha
yake ya awali alikulia Arusha nchini Tanzania. Alisomea shahada ya B.A na M.A katika Chuo
Kikuu cha Nairobi. Baadaye alisomea shahada yake ya Ph.D katika Chuo Kikuu cha
Bayreuth nchini Ujerumani. Wamitila amechapisha makala na tahakiki za fasihi ya Kiswahili
katika majarida mengi ya kitaaluma barani Afrika, Ulaya, Asia na Marekani. Ameandika
tamthilia, riwaya fupi, riwaya na mashairi. Baadhi ya vitabu vyake vilivyochapishwa ni
Wingu la Kupita (1999), Nguvu ya Sala (1999), Bina-Adamu! (2002), Pango (2003) na
Musaleo (2004). Baadhi ya kazi za Wamitila ambazo hazijachapishwa ni tamthilia ya Sumu
33
Kwa mujibu wa mazungumzo niliyokuwa nayo na mwandishi mnamo tarehe 25/6/2004,
imani yake ni kwamba maisha ya binadamu huthibitiwa na hali ya urazini na kutokuwa na
urazini ya binadamu. Jambo ambalo mwandishi ana vita nalo ni jinsi nchi za Kimagharibi
zinadhibiti na kujinufaisha na dhana kama vile utandaradhi. Hii ni kwa sababu Waafrika
ndio wanaoumia wakati ulimwengu mzima unajulikana kama 'kijiji'. Dhana kama vile
,
utandaradhi na ullrnwenqukuwa kijiji kimoja ni kwa manufaa ya Wamagharibi tu. Riwaya
yake ya Bina-Adamu inadhihirisha hayo waziwazi.
2.2.1 Hatua ya mwanzo ya uhalisiajabu
Wamitila (2002: 118) anasema kwamba kazi za kihalisiajabu zinavunja muundo wa ~
u;
a::
~ kikawaida wa utanzu kama njia ya kuzuka na istiara ya miundo ya mifumo ya kisiasa,
z
~ ~
~ kiuchumi na kitamaduni ya ulimwengu. Sababu ya kufanya hivi ni ili kufanikiwa katika
7-~
kuchunguza kile ambacho kinaitwa "ung'amuzi wa kisiasa". Kwa mfano, msomaji wa riwaya
ya Babu Alioofufuka anapaswa kuigundua siasa ya ulimwengu inayozihusu nchi za Kiafrika
na hasa nchi ya Tanzania.
Riwaya ya Wamitila Zimwi wa Leo (2002) inaonyesha kwamba, tangu mwanzo, uandishi
wake umekuwa na dalili za uhalisiajabu. Hii ni hadithi kuhusu zimwi moja ambalo linatoka
mahali kusikojulikana na kuwatokea watu waliokuwa wakiishi kwa amani na upendo.
Watu hawa ni wenye safi na wanapoona kuwa zimwi linakitamani chakula wanachokila
wanalikaribisha kwa mikono miwili.Tatizo ni kwamba zimwi hili halionekani kushiba. Inabidi
watu hawa wafanye kazi kwa bidii sana ili kuweza kutosheleza mahitaji ya zimwi hili. Kwa
upande wake zimwi, linawaona watu wanaoweza kulisaidia kujifaidi. Liliwaza:
Zimwi hili linawaza sana jinsi linavyoweza kuwashawishi hawa watu kulifanyia kazi.
Hatimaye linajiwa na wazo kwamba likiwapa Wantu nguo nyingi na zawadi watashirikiana
nala.
Zimwi hili linaendelea kutumia kutojua na wema wa watu wa jamii hii na kuanzisha mambo
mengi ambayo Wantu (kama walivyoitwa) waliyakubali bila kung'amua hatari iliyokuwepo.
Kwa kifupi, Wamitila (2002) anaeleza kifumbo jinsi wazungu walivyoingia Afrika. Waafrika
kwa moyo safi na bila kuwa na tuhuma yoyote, walivyowakaribisha. Wazungu walitumia
werna huo kuchukua mashamba ya Waafrika na hatimaye kuwatumikisha katika nchi yao
wenyewe. Mwandishi anatupitisha kwenye vipindi mbalimbali kuanzia pale zimwi linapofika
Afrika. Kwa sababu ya ile tabia yake ya 'kukaba' chakula tu bila kujali kilitoka wapi pamoja
na hila zake, Wantu walianza kuliita 'Kabaila' (Wamitila 2002: 15).
Baadaye yule Kabaila (halikuitwa zimwi tena) anabadilishiwa jina na Wantu. Hii ni kwa
sababu baada ya kuanzisha viwanda, anajipatia pesa zaidi kutokana na kodi anayowatoza
Wantu huku wao wakiendelea kuteseka tu. Aidha, kabaila anawafunza mchezo wa kamari
ili Wantu 'wajipatie pesa nyingi' lakini Kabaila ndiye anashinda karibu mara zote. Wantu
wanapoona tabia hii ya 'kubeba' na 'kuparia' Wantu wanaanza kumwita kabaila 'Bepari'.
Jambo moja linalostaajabisha kuhusu mchezo wa kamari ni kwamba kila anayeucheza na
kushinda, anabadilika kwa sura na tabia. Kiumbo, anaanza kuota mikono na vinywa vingi
kama Bepari. Kitabia anaanza kuwachukia wenzake polepole. Hawa ni wale waitwao
35
Wamitilaanasema:
Wantu waliopata pesa hawakuwa watu tena bali vizimwi vilivyokuwa na mikono
kama Bepari.Vizimwi hivyo vilikuwa tayari kuvitumia vikono vyao kuua kama Bepari
ili vipate pesa (Wamitila 2002:29).
Bepari linakuwa halifanyi kazi ila kukaa tu na kula. Hali hii inalifanya linoneane na
linashindwa na kazi yake ya awali ya kupitapita ili kuona kama Wantu wanafanya kazi.
Linawatumia vizimwi na vibepari vinavyofanana nave riale kwa ya pili kufanya hivyo. Hawa
ni vibaraka wazungu-weusi waliotumia na wazungu kufanikisha lengo lao.
Kwa sababu ya kule kutooga na kunoneana kwa Bepari, linaanza kutokwa na harufu mbaya
sana kama ya beberu. Harufu hii inatanda kila mahali kama upepo wa msimu wa rnvua.
Tangu siku hiyo Bepari linapewa jina jingine. Wantu wanaliita Beberu. Mwandishi anasema:
Hata baada ya kuondoka, mnuko ulibakia ukienea. Waliokwenda viwandani
walikumbana na mnuko wa Beberu. Hata pesa zenyewe zilikuwa na mnuko huo. Kila kitu kilikuwa kinanuka beberu (Wamitila 2002:33).
Mwandishi anataka kutujulisha kwarnba hata baada ya wakoloni kuondoka, alama zake
bado zipo. Hii ni kwa njia ya wazungu weusi/wakoloni mamboleo waliobaki. Aidha, athari
ya ukoloni bado ipo kupitia jinsi nchi nyingi za Kiafrika zimeendelea kutegemea nchi za
Kimagharibi kwa misaada ya pesa, mikopo, madawa na hata vyakula.
2.2.2 Kioindi cha uhalisiajabu
Wamitila (2002) katika Bertoncini (2004:1) anasema:
Nimeamua kuandika riwaya hii (Bina-Adamu!) hivi ili kuweza kuzungumzia suala
ambalo nahisi nisingeweza kulizungumzia kwa njia ya kawaida (kwa riwaya za