~·300'"D
IATHARJ YA MBINU REJESHI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISW AIDLI.
NA
LUCIA MULl MUSILI
TASNIFU HII lMETOLEWA ILl KUTOSHELEZA BAADHI YA MARITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATlKA CHUO KIKUU CRA KENYATTA.
NOVEMBA 2015
---~-IKIRARI
Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika chuo kikuu chochote.
LUCIA MULl MUSILl NAMBARl YA USAJlU: C50/CE22593111
Sahihi ~... Tarehe
yJ.u.l~.\..~
.
Tasnifu hii imetolewa kwa idhini yetu kama wasimamizi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta.
DKT. JOSEPH N MAITARIA.
Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafirika
Tareheu¥i~E~
DKT. EDWIN W. MASINDE.=-_-...::Lugha za Kiafirika
Tarehe
·
+/tj/~t£.
u
Sahihi .
TABARUKU
Naitabaruki kazi hii kwa Bwana yangu mpendwa Francis Musili Maithya, watoto wangu Ann, Margaret, Grace, Elizabeth, Everlyn, Mary, Kelvin na Victor. Mwisho naitabaruki kazi hii kwa marehemu mama yangu Josphine King'elu Nzumbu ambaye alikuwa akinipa moyo wa kuendelea na masomo. Mungu ailaze roho yake mahali perna peponi.
SHUKRANI
Natoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu ambaye amenipa uhai mpaka nikafika kiwango cha kumalizia kazi hii. Shukrani zangu pia ziwaendee wasimamizi wangu Daktari J.M Maitaria na Daktari Edwin Masinde kwa kuniongoza katika kila sura ya tasnifu hii. Waliweza kunisaidia kwa nakala nilizohitaji aidha kunip~ mwongozo wa uandishi. Sitasahau kuwashukuru wahadhiri wote katika idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika. Waliweza kunipa msingi wa elimu ndio nikaweza kufika kiwango hiki. Natoa shukrani za dhati kwa Bwana yangu mpendwa Francis Musili Maithya kwa kugharamia masomo yangu. Baba yangu Daniel Nzumbu apokee shukrani kwa kuwa msingi imara wa elimu yangu kuanzia masomo ya kiwango cha msingi hadi cha upili. Watoto wangu wote nawashukuru kwa kunivumilia wakati nilikuwa katika chuo nikiendelea na masomo yangu. Kuna mambo ambayo sikuyatimiza kama mzazi wao . Mwisho natoa shurkrani zangu kwa wandani wangu katika chuo ambao bila wao kazihii haingekamilika .Tuliweza kusaidiana bega kwa bega. Baadhi ya marafiki hawa ni Sarah, Sophie, Charity, Munyao, Florence, Gecere miongoni mwa wengine.
iv
IKISIRI
Utafiti huu ulishughulikia athari ya mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili. Diwani zilizoshughulikiwa ni za miaka ya elfu mbili nazo ni Mwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) na Kunani Merikani na Hadithi Nyingine (2011). Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya eilmumtindo. Nadharia hii ilimfaa mtafiti katika utafiti huu maana diwani hizi ambazo zimeteuliwa zimesheheni matumizi ya mtindo wa mbinu rejeshi. Utafiti huu umegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ilitupa mwelekeo wa utafiti wetu. Katika sura hii tumejadili swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchangua mada. Pia katika sura hii tumejadili misingi ya nadharia, upeo wa mipaka na yalioandikwa kuhusu mada. Mwisho mbinu za utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa data zimeangaziwa, Sura ya pili nayo imejadili matumizi ya mbinu rejeshi katika diwani ya Mwendawazimu na hadithi Nyingine. Katika sura hii mtafiti amebainisha matumizi ya mbinu rejeshi katika diwani hii na athari ya mtindo huu. Sura ya tatu imezingatia matumizi ya mbinu rejeshi na athari yake katika diwani ya Kunani Merikani na Hadithi Nyingine. Sura ya nne ambayo ni hitimisho imekuwa muhtasari, matatizo na mapendekezo ya mtafiti. Utafiti huu unanuia kuwafaidi wahakiki wengine, wasomi na waandishi wa kazi za fasihi. Pia utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuhakiki kazi zao.
ABSTRACT
The study was to investigate effects of flashback in Kiswahili short stories. The study aimed at aspects of flashback in Kiswahili short stories. The researcher dealt with two selected Kiswahili short story books of different editors. Selected books were Mwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) edited by Mwenda Mbatiah and Kunani Merikani na Hadithi Nyingine(2011) edited Iribemwangi. The researcher employed stylistic theory. The theory explained the study well since the short story books selected were rich in flashbacks. This thesis comprises of four chapters. Chapter one discussed the introduction and background to the study, statement of the problem, objectives, research questions, the theories used, the scope of the study and literature review. Lastly it discussed about the methods of the research. Chapter two dealt with the history of short stories and development up to date. Chapter three discussed about the effects of flashback in Mwendawazimu na Hadithi Nyingine and Kunani Merikani na Hadithi Nyingine. The researcher tried to show flashbacks used in these books and how they bring effect to characters. Chapter three discussed about flashback in Mwendawazimu na Hadithi Nyingine and Kunani Merekani na Hadithi Nyingine and how they affect settings. Different flashbacks were also analysed.Chapter four gave the summary of the research, the findings of the research, the problem encountered and the proposals for the future study. This research intends to benefit other researchers, learners and literature writers. It will also go a long way in assisting lecturers
MAELEZO YAISTILAHI MUHIMU
Dhamira: Kiini chajambo au habari iliyosimuliwa ama kuandikwa.
Hadithi Fupi: Hii ni hadithi ambayo inashughulikia suala fulani kwa muhtasari na huwa aghalabu na mhusika mmoja anayejitokeza ingawa hakuzwi kama ilivyo katika novela au riwaya.
Matini: Kifungu cha maandishi au taarifa inayojisimamia katika kueleza dhana
Mbinu rejeshi: Ni mbinu anayoitumia mwandishi kuyaeleza matukio yaliyotokea wakati wa nyuma ya wakati wa hadithi
Msuko: Ni mpangilio wa matukio yanayopatikana katika hadithi na huhusisha matendo ya nguli najinsi yanavyoathiri wahusika wengine.
Nadharia: Ni maelezo au mwongozo uliopagwa ili kusaidia kueleza, kutatua au kutekeleza jambo.
YALIYOMO IKIRARI ii TABARUKU iii SHUKRANI iv IKISIRI v ABSTRACT vi
MAELEZO Y A ISTILAHI MUHIMU vii
Y ALIYOMO viii
SURA YA KWANZA : 1
1.0UTANGULIZI 1
1.4 Sababu Za Kuchangua Mada 4
1.6 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 15
1.7.1 Muundo Wa Utafiti 22
1.7.2 Mahali Pa Utafiti 22
1.7.3 Uteuzi Wa Sampuli 22
1.7.4 Ukusanyaji Wa Data 24
1.7.5 Uchanganuzi Wa Data 24
1.7.6 Uwasiiishaji WaMatokeo 25
1.8 HITIMISHO 25
ATHARI YA MBINU REJESHI KATlKA UWASILSHAJl WA MAUDHUI 26
2.0 UTANGULIZI 26
2.1 Mchango Wa Mbinu Rejeshi Katika Usawiri Wa Wahusika Na Uwasilishaji Wa
Maudhui 26
2.1.1 Mwendawazirnu-Rose Shake 28
2.1.2 Kunani Merikani - Iribemwangi 30
2.k1 Korti Ya Kishenzi - David Maillu 35
2.1.4 Siri- Stephen Munyasi 39
2.1.5 Walicheka Kicheko - John Habwe 42
2.1.6 Mbio Za Sakafuni - O. Ong'utu 44
2.1.7 Mboni La Jicho -Kyallo Wamitilla 47
2.1.8 Kwa Nini - Hassan Ali 51
2.2 Hitimisho 55
SURA YA TATU 56
ATHARI YA MANDHARI NA UWASILlSHAJl WA MAUDHU 56
3.1.1 Kunani Merkani -Iribemwangi 57
3.1. 2 Mwendawazimu - Rose Shake 60
3.1.3 Mja Mja- Rabbecca Nandwa 62
3.1.4 Mtego Wa Panya - Hamisi Babusa 66
3.1.5 Mboni Ya Jicho - Kyalo Wamitila 69
3.1.6 Mapenzi Chungu - Betty Kiruja 71
3.1.7 Jitu La Kisasa-R. M Wafula 74
3.1.9 Maji Aliyavulia Nguo!- Assumpta Mulila-Matei 80
3.2Hitimisho 83
SURA YA NNE 85
HITIMISHO 85
4.0 Utangulizi 85~
4.1 Muhtasari , 85~
4.2 Matokeo Ya Utafiti 871
Umuhimu Wa Matokeo Ya Utafiti 90
Changamoto Zilizoathiri Utafiti 90
Mapendekezo
21
Marejeleo 92
ix
SURA YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Hadithi ni mfululizo wa matukio kwa kuzingatia mfuatano au mpangilio
wa kiwakati. Hadithi ni kipengele muhimu sana katika utanzu wa fasihi.
Katika kufafanua hadithi fupi tuliyoisoma inatulazimu kuyachukua matukio
yaliyomo na kuyapanga kiwakati. (Wamitila, 2002). Katika hadithi fupi za
Kiswahili, hoja kuu ni kuwasilisha ujumbe kwa kutumia vipengele
mbalimbali vya kimtindo. Kipengele kilichoshughulikwa ni mbinu rejeshi
na athari yake katika hadithi fupi za Kiswahili. Mbinu rejeshi ni kipengele
cha mtindo kinachotumiwa na mtunzi wa kazi ya kisanaa kwa kurejerea
mambo yaliyokwisha kusimuliwa awali kupitia mpangilio wa matukio ya
kazi au uzungumzi nafsia wa wahusika.
Katika utafiti huu kazi za wahariri wawili tofauti zimeangaziwa. Mwenda
Mbatiah amehariri diwani yaMwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) naye Iribemwangi amehariri diwani ya Kunani Merikani na Hadithi Nyingine (2011). Hata hivyo Kuna kazi zingine za fasihi ambazo waandishi
hawa wamehariri. Kwa mfano Iribemwangi amehariri diwani ya Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine (2007). Naye Mwenda Mbatiah, amehariri kitabu
cha Kurudi Nyumbani na Hadithi Nyingine (2007) miongoni mwa kazi zingine.
Diwani za Mwendawazimu na Hadithi Nyingine na Kunani Merikani na
Hadithi Nyingine ni kazi za fasihi ambazo hazijafanyiwa utafiti
tukiangazia kipengele cha mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili. Hivyo kulikuwa na haja ya kushughulikia kazi hizi kwa upana.
Hata hivyo, uhakiki umefanywa kuhusu hadithi fupi za kiswahili kwa jumla. Uhakiki ambao umefanywa unalenga wahusika, ,mtindo, mandhari
na usimulizi. Utafiti wetu umekuwa tofauti kwa sababu umejikita katika kuchunguza athari ya mbinu rejeshi katika kazi mbili teule za wahariri tofauti ambao ni Mwenda Mbatiah na Iribemwangi.
1.1Swala la utafiti
Mbinu rejeshi ni kipengele muhimu sana cha mtindo katika kazi ya fasihi. Fasihi ni sanaa ambayo huitaji lugha ili kuyasimulia maisha ya wanajamii kwa jumla. Hivyo matumizi ya lugha katika kazi ya fasihi huwa moja kwa moja na wakati mwingine matumizi haya huwa fiche. Kuna mitindo mbalimbali ambayo mtunzi wa kazi ya fasihi anaweza kutumia ili kuwasilisha ujumbe. Mtindo wa mbinu rejeshi ni mojawapo wa mbinu zinazotumiwa na watunzi wa kazi ya fasihi. Hivyo basi utafiti
huu umeshughulikia athari ya mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili.
Utafiti huu umechunguza athari ya mtindo wa mbinu rejeshi katika kazi
mbili za fasihi ambazo zimehaririwa na wahariri wawili tofauti. Diwani
ya Mwendawazimu na Hadithi Nyingine na Diwani ya Kunani Merikani
na Hadithi Nyingine. Mtindo wa mbinu rejeshi ambao umetumiwa na
wahariri hawa wawili ulichunguzwa. Ujumbe ambao uliweza kuwasilishwa na
mtindo huu uliangaziwa pia. Aidha, utafiti huu umebainisha na kuchanganua
mbinu rejeshi kwa lengo la kuonyesha iwapo imefanikisha malengo ya
mtunzi kisanaa. Vilevile mtindo huu umeonyesha kama malengo ya mtafiti
yamefanikishwa.
Kwa vile kuna pengo katika mtindo wa mbinu rejeshi ambao unatumiwa
na watunzi wa kazi ya fasihi, katika utafiti huu tuliweza kuangazia huu
mtindo na kujua athari yake katika hadithi fupi za kiswahili hivyo basi
kujaza pengo hila kupitia utafiti wetu.
1.2 Maswali ya utafiti
Utafiti huu umeongozwa na maswali yafuatayo:
1. Ni aina zipi za mbinu rejeshi zinazopatikana katika diwani teule za
Kiswahili?
2. Mbinu rejeshi imeathiri vipi msuko wa maudhui katika diwani teule
za Kiswahili?
3. Mbinu rejeshi imetumiwa vipi kuwasawiri wahusika katika diwani teule
za Kiswahili?
1.3 Malengo ya utafiti
Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo.
1. Kubainisha aina mbalimbali za mbinu rejeshi zinazopatikana katika
diwani teule za Kiswahili.
2. Kuonyesha vile mbinu rejeshi imeathiri msuko wa maudhui katika diwani za teule za kiswahili.
3. Kuonyesha vile mbinu rejeshi imewasawiri wahusika katika diwani teule
za Kiswahili.
1.4 Sababu za kuchangua mada
Sababu ya mtafiti kushughulikia mada hii ilitokana na hoja nne kuu.
Kwanza swala hili halijashughulikiwa kwa upana na watafiti wengine hivyo
kuna pengo ambalo linahitaji kujazwa. Ingawa mtafiti alihusika na mtindo
mmoja tu wa mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili, mtindo huu
umeonyesha vile una uwezo wa kuendeleza kazi ya fasihi kwa wasomi na
wasanii mbalimbali tukiangazia hadithi fupi za Kiswahili. Pili utafiti huu
umechunguza kazi za wahariri wawili na kuangalia kama wametumia mtindo
wa mbinu rejeshi katika vitabu vya hadithi fupi za Kiswahili. Diwani hizi
ni Mwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) na Kunani Merikani na
Hadithi Nyingine (2011). Tatu ni maoni yetu kuwa utafiti huu utawasaidia
wahakiki wa kazi za fasihi kwa kuchunguza mitindo inayotumiwa na
waandishi wa hadithi fupi za kiswahili. Nne utafiti huu utakuwa na
manufaa kwa wasomi na wapenzi wa lugha ya Kiswahili kwa jumla.
1.5Upeowa Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu umeshughulikia diwani mbili za hadithi fupi ambazo ni
Mwendawazimu na Hadithi Nyingine ya Mwenda Mbatiah na Kunani
Merikani na Hadithi Nyingine ya Iribemwangi. Kazi hizi mbili zimeteuliwa
kwa sababu data inayopatikana katika diwani hizi ilitarajiwa kutosheleza
mahitaji ya utafiti huu. Kuna kazi nyingi za kisanii ambazo zimeandikwa
na watunzi wengi kama vile riwaya, tamthilia, ushairi na hadithi fupi.
Diwani hizi mbili zimeteuliwa kwa sababu ya ufaranguzi wa kimtindo
uliotumika humu wa kutumia mtindo wa mbinu rejeshi.
1.5.1 Nadharia ya Elimumtindo
Nadharia ni maelezo ya jambo kufungamana na vigezo vilivyowekwa au
vinavyozalika kutokana na majarimbio ya jambo hilo. Swala la utafiti ndilo
linalomwongoza mtafiti kutumia nadharia ifaayo.
Nadharia hii iliweza kutekeleza swala la mtafiti vyema. Mtafiti alichunguza
athari ya mbinu rejeshi katika diwani mbili za hadithi fupi za Kiswahili.
Matumizi ya mbinu rejeshi yamechanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya
nadharia ya elimumtindo.
Mwasisi wa nadharia hii rn Buffon (1930) ambaye kwa mawazo yake alidai
kuwa mtindo ni mtu mwenyewe kumaanisha jinsi mtu anavyotumia lugha
kupitisha ujumbe wake. Mawazo yake ni kuwa kazi ya fasihi hudumu kupitia
mtindo wake na mtindo huo ni mtu mwenyewe. Hivyo mtindo huweza
kumtambulisha mtunzi wa kazi yoyote ya fasihi. Aidha mtindo ndio kifaa cha
pekee ambacho mtunzi ana uwezo wa kukimiliki hivyo akasema kuwa
tunaweza kusema huu ni mtindo wa mtunzi fulani. Kwa mfano tunaposema mtindo wa M.S Mohamed, inamaanisha kuwa ametumia lugha yake. M.S
Mohamed ametumia jazada na sitiari katika utunzi wake kwa upana naye
Shafi Adam Shafi ameengemea kwa upande wa wepesi wa lugha na
tamadhali katika kazi zake (Wamitila, 2003). Watunzi hawa wametumia vipengele tofauti vya mtindo ili kuwasilisha ujumbe wao.
Crystal na Davy (1969) wametoa maoni kuhusu mtindo. Wanaeleza mtindo
kwa kutumia njia nne kuu. Kwanza wanasema mtindo ni tabia ya mtu kupitia
matumizi yake ya lugha. Hapa wana maana kuwa namna mtu anavyotumia
lugha kuwasilisha ujumbe wake. Crystal na Davy wanaendelea kudai kuwa
mtindo ni tabia ya mtu binafsi kuhusu matumizi yake ya lugha. Matumizi haya
ya lugha huweza kudhihirisha hulka ya mtunzi. Mfano mzuri ni mtindo wa watunzi mbalimbali kama vile Shakespheare na Jacob Joyce. Tunaposema
mtindo wa Shakespheare tunamaanisha jinsi mtunzi ametumia lugha yake.
Vilevile tunaposema mtindo wa Jacob Joyce tuna maana kuwa mtunzi huyu
ametumia lugha yake. Pili wahakiki hawa wanaeleza mtindo kama namna
6
kikundi cha watu wanavyotumia lugha katika kipindi fulani, yaani tabia za
matumizi ya lugha ambazo zinashughulikiwa na jamii fulani. Kwa mfano
mtindo wa mashairi ya kina Augustan au mtindo wa mashairi ya kishujaa ya
kingereza. Aidha wanasema kuwa mtindo ni tabia ya kueleza mambo kama
vile matumizi mwafaka ya lugha katika mazingira. Mwisho wanasema kuwa
mtindo umekuwa ukihusishwa na fasihi kama sifa bora na yenye maandishi
yenye mapambo.
Naye Leech (1969) anatilia mkazo kuwa nadharia ya mtindo inalenga
matumizi ya lugha ambayo ndio huibua dhamira za mwandishi. Kipengele muhimu alichokizungumzia ni lugha ambayo inamsadia mwandishi kutoa
dhamira yake kwa wasomaji au wasikilizaji.
Naye Epstein (1978) anasema mtindo ni mapambo yanayojitokeza katika kazi
nzuri. Epstein anadai kuwa mtindo ni elementi ya lazima katika mawasiliano
ya binadamu. Tabia ya binadamu huonekana kupitia mtindo wake kwa njia
tofauti hivyo basi mtindo wa mtu ndio unaweza kumtofautisha binadamu
na wengine. Mhakiki huyu anayaunga maoni ya Buffon kwa kudai kuwa
mtindo ni mtu.
Naye Diyann (1976:81) anasema kuwa mtindo ni jinsi mwandishi anavyopanga
maneno na sentensi katika kazi yake. Aidha, anasema mtindo ndicho
kitambulisho ambacho kina uwezo wa kumtambulisha mtunzi kupitia
maandishi yake ya kipekee.
Scot (1925) ametoa mawazo yake kuhusu mbinu rejeshi. Hiki ni kipengele
cha mtindo ambacho hutumiwa na waandishi wa kazi ya fasihi. Maoni yake ni
kuwa mwandishi hutumia mbinu rjeshi kwa sababu kadhaa. Kwanza huwa
anataka kuwasilisha kina cha ujumbe katika kazi ya fasihi. Vilevile mtunzi
huonyesha kazi zilizopendwa ambazo zimetiliwa chuku au zinazosisimua.
Aidha anasema kuwa mbinu rejeshi huibua taharuki kwa kuzingatia vipengele
vya hadithi fupi kama vile wahusika. Amesisitiza kuwa mbinu rejeshi huweza
kumsawiri mhusika kwa kuangalia tabia yake.
Kimani Njogu na Dorothy (1996) wanasema mtindo ni namna mwandishi
au msimulizi anavyounda kazi yake. Wahakiki hawa wamedai kuwa
mtindo ni mazoea ya msanii vile yanajitokeza katika kazi yake. Maoni
yao ni kuwa mtindo waweza kujitokeza katika kazi kadhaa za mwandishi
mmoja au kazi za wasanii wa kipindi kimoja cha historia. Hivyo basi
wakasema mtindo hujitokeza katika fani na maudhui. Haya yanapatikana
katika tamathali za usemi, taswira, ujengaji wa wahusika, mandhari au
uteuzi wa msanii. Mwisho wanasisitiza kwamba mtindo si mali ya msanii
fulani peke yake. Mtindo anaoutumia msanii mmoja waweza kutumiwa na
msanii mwingine.
Kimani na Chimera (1999) wanasema kuwa mtindo ni ufundi wa kupanga
kupangua. Vilevile wanaeleza kuwa mtindo ni ujuzi wa kujieleza. Maoni
yao ni kuwa mtindo huwa na vipengele vyake kama vile jazada, taashira,
tashbihi, tasfida, taswira, taharuki, mbinu rejeshi na viangaza mbele.
Wahakiki hawa wamesisitiza kuwa mtindo hutumiwa kupeleka mbele
maudhui na dhamira pamoja na kusanifu kazi nzima ili ufasaha ujitokee.
Kwa mujibu wao mtindo ndio unaomtofautisha fanani na mwingine hivyo
basi wakasema ni mseto wa fani na maudhui. Maoni yao kuwa, mbinu
rejeshi ni mtindo wa kisanaa ambao unatumiwa na rntunzi kwa kurudia
mambo yaliyokwisha simuliwa awali kupitia mpangilio wa matukio ya
kazi au uzungumzi nafsia wa wahusika. Wanasema kwamba mbinu hii ni
kinyume cha mbinu ya kiangaza mbele ambayo badala ya kubashiria
yaliyotokea baadaye, hurejelea mambo yaliyopita.
Naye Wamitila (2002) anasema kwamba mbinu rejeshi hutokea pale
ambapo matukio hutokea kabla ya sasa hadithi inapowasilishwa.
Saundra na Richard (2004) wanasema mtindo ni matokeo ya vile mtunzi
huchangua na kupanga maneno na sentensi. Mawazo yake ni kuwa watu huchangua maneno mbalimbali ili kuwasilisha ujumbe wao na kila mtu ana
mtindo wake mwenyewe. Hivyo kila mtu hutumia mtindo wake kuwasilisha
ujumbe wake kulingana na hali. Mtindo wa mbinu rejeshi ni kipengele cha
lugha ambacho kinaaminika kuwa kinaibua mawasiliano katika hadithi. Hata
hivyo maoni ya wahakiki hawa ni kuwa ikiwa mtu ana ujumbe unaofaa wakati
fulani, na msikilizaji awe amefutwa na ujumbe huo yale atakayewasilisha
huenda yakapotea ikiwa mtindo wake haufai.
Leech (2008) anadai kuwa mtindo ni matumizi ya lugha kulingana na
mabandiliko ya hali. Kwa mfano, hali ya sehemu za isimu zinazohusiana na maandishi ambayo yana vigezo vyenye utaratibu. Leech amesisitiza kuwa
kuna uwezekano wa kutofautisha elimu mtindo ya jumla na elimu mtindo ya
fasihi. Tofauti iliopo mitindo hii ni kupitia maandishi. Maoni ya Leech ni
kuwa mtindo unaweza kujulikana kupitia mwandishi na vile alinuia kueleza
wazo lake kupitia maandishi yake. Hivyo, mtindo ni jinsi lugha inavyotumiwa
tukiangazia vigezo vya lugha. Anaeleza umuhimu wa mtindo katika kazi ya
fasihi. Kwanza mtindo husaidia wasomi na wasanii kuwa na uwezo wa kukumbali kazi ya fasihi. Pili husaidia kufunza vikundi vidogo na kuwa na
uwezo wa kufikia kiwango cha elimu vizuri. Tatu mtindo husaidia kupata ujuzi
wa isimu unaojitajika katikajamii. Mwisho husaidiajamii kuwa na uwezo wa
kupata ujumbe wowote katika maeneo mengine.
Wamitila (2003:191-192) anasema kwamba mtindo nijumla ya mbinu au sifa
zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe wake. Anasema kuwa
mtindo huelezajinsi mwandishi anavyounda kazi yake. Mawazo ya Wamitila
ni kuwa mwandishi anapotumia mtindo fulani anajitambulisha kwa wasomi
na wanaweza kutambua kazi ya mtunzi fulani kupitia kuisoma tu. Anaendelea
kusema kwamba mtindo unaweza kujitokeza kwenye kazi kadhaa za
mwandishi mmoja au pia kwa waandishi wa sehemu fulani au kipindi cha
kihistoria. Wamitila anasisitiza ya kwamba fani peke yake haitoshi
kumtambulisha msanii hivyo basi akasema kuwa mtindo huweza kujitokeza
kwenye fani na maudhui ya mwandishi fulani. IIi tuweze kuangalia mtindo
ambao ameutmia mtunzi, alisema ya kwamba ni vyema kuzingatia vielekezi
mbalimbali. Vielekezi hivi ni kama; matumizi ya lugha, mpangilio wa matukio,
taswira, tamathali za usemi, ujezi au usawiri wa wahusika, mandhari mpangilio
wa matukio, uteuzi wa msamiati miongoni mwa vielekezi vingine. Wamitila
amezungumzia muundowa kazi ya asihi ambapo tunatoa kauli ya mwandishi
kutumia wahusika changamano, kutmia lugha nyepesi, ana tamathali nzito na
usimulizi wa kuvutia.
Leech (2008) anadai kuwa mtindo ni matumizi ya lugha kulingana na
mabandiliko ya hali. Kwa mfano hali ya sehemu za isimu zinazohusiana
na maandishi ambayo yana vigezo vyenye utaratibu.
Wafula na Njogu (2007:97) wametoa mawazo yao kuhusu nadharia ya mtindo.
Maoni yao ni kuwa mtindo huelezwa kwa kuainishwa na madhumuni ya
msanii. Madhumuni wanayaeleza kama dhamira hivyo basi wakasema
mtindo ni jinsi dhamira zinavyowasilishwa. Kauli hii inachukuliwa kuwa
wazo huota katika fikra za mwanasanaa au msemaji yeyote wa kifasihi.
Wadhifa wa mwanasanaa ni kuainisha na kutumia lugha inayofaa kulieleza
wazo hilo. Wanamtindo huchukua lugha kama vazi la fikra. Maoni ya
wahakiki hawa ni kwamba fikra hizi zilielea angani bila umbo au muundo
wowote. Ilibidi fikra hizi zivishwe nguo yaani zielezwe kimaneno ili zipate
sura maalum. Imani hii ilichukuliwa kwamba kuna maudhui na mtindo na
kwamba maudhui yanapasa kuwasilishwa katika mtindo unaofikiana nayo.
Senkoro (2011) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo
msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na maudhui huainisha
kanuni au kaida zilizofuatwa kama ni za mapokeo au za kipekee.
Charles na Mary, (2005) wametoa mchango wao kuhusu mbinu rejeshi na
kusema kuwa ni sehemu ya kazi ya fasihi ambayo inaleta mfuatano wa
matukio. Iii kuwe na uhusiano wa hayo matukio kutoka mwanzo wa kazi ya
fasihi, waandishi hutumia mbinu rejeshi kuonyesha kile kilimpa motisha
mhusika au kurudia tukio fulani lililopita kuhusu mhusika.
Wamitila, (2008:153-157) anazungumzia mtindo wa anakroni au urejeshi
ambapo mkondo asilia wa matukio umekiukwa. Anaeleza aina mbili za
anakroni yaani mbinu rejeshi na mbinu elekezi. Wamitila anasema kwamba
mbinu hizi mbili zinaweza kupimwa kwa kuangalia mfiko wa upana wake.
Mhakiki huyu wa fasihi anasema kuwa mbinu rejeshi hutokea pale ambapo
matukio yaliyotokea kabla sasa ya hadithi yanapowasilsihwa. Wamitla
anasema kuwa kuna aina mbalimbali za mbinu rejeshi.
Nazo ni;
1. Mbinu rejeshi ya ukamilishaji: Hapa ni pale mtunzi hutumia mbinu
rejeshi kurejelea. maelezo au tukio ili kukamilisha au kulijaza pengo
fulani katika usimulizi na ambalo msomaji wa kazi inayohusika anahisi
anaposoma maelezo au tukio linalorejelewa.
2. Mbinu rejeshi ya nje: Hii ni mbinu ambapo urejeshi unaotokea
unapatikana nje ya pale matini au hadithi kiwakati inayohusika
inapoanzia.
3. Mbinu rejeshi ya urudiaji: Hapa tukio linalorejelewa huweza kuwa nt
tukio lililosimuliwa kabla na kwa hivyo linarudiwa.
4. Mbinu rejeshi ya kibinafsi: Hii ni mbinu ambayo inamhusu mhusika
kibinafsi. Mbinu rejeshi ya aina hii hutokea pale ambapo maelezo ya
ndoto au kumbukumbu zinazomhusu mhusika binafsi zinarejelewa.
Hapa kazi za fasihi zenye mielekeo ya kisaikolojia uangaziwa.
5. Mbinu rejeshi ya ndani: Hapa urejeshi unaohusika haupo nje ya wakati
unaondokezwa na mwanzo wa matini au kazi ya fasihi inayohusika.
6. Mbinu rejeshi mseto: Hii ni aina ya mbinu rejeshi ambapo wakati
unaohusika unaanza kabla ya hadithi yenyewe lakini unaelekea kwenye
wakati wa hadithi kuingia kwenye hadithi kuu yenyewe.
7. Mbinu rejeshi ya muktadha wa karibu: Mbinu rejeshi hii urejelea
mhusika, au unaozunguka mhusika au tukio fulani.
8. Mbinu rejeshi muktadha mpana: Mbinu hii inatokea wakati kile
kinarejelewa kiko nje ya ulimwengu wa mhusika au tukio fulani.
9. Mbinu rejeshi ndani ya mbinu rejeshi: Urejeshi wa aina hii unafuata
misingi sawa na mchezo ndani ya mchezo. Katika mbinu rejeshi
iliyopo kuu, panakuwako na rnbinu nyingine ndani yake, inaweza
ikawa mbinu rejeshi moja au zikawa mbinu rejeshi kadha na kwa
njia hii kuunda aina ya ngazi katika kiwango cha usimulizi.
10. Mbinu rejeshi za kikufu: Dhana hii hutumika kuelezea hali katika
matini au kazi ya kifasihi. Huwa kuna matumizi ya mbinu rejeshi
kadha ambazo zinaunganishwa kwa namna ya kuunda mkufu fulani. Hali hii hutokea pale ambapo hadithi inarejelea tukio fulani kisha tukio
hilo nalo likarejelea matukio mengine kadha.
Wanamtindo wanasisitiza umuhimu wa lugha kama chombo kinachosaidia
katika kuelewa ujumbe au maudhui kwa hivyo kama hakuna lugha hakuna
fasihi. Wanaeleza kuwa vipengele vya isimu hutumika katika kueleza namna
ambavyo lugha hutumika katika kazi ya fasihi. Mbinu rejeshi kipengele cha
mtindo kinachutumiwa na watunzi wa kazi ya fasihi. Kipengele hiki ndicho
muhimu sana katika utafiti huu maana ndicho kitakachotumika kuongoza
utafiti wetu.
Nadharia ya elimumtindo ilitusaidia kuchuguza athari ya mbinu rejeshi katika
hadithi fupi za Kiswahili. Kwa mujibu wa nadharia hii, tuliangazia mtindo wa
mbinu rejeshi na vile mwandishi anaweza kujenga ufanisi wa kazi yake
akitumia lugha tukiangazia kipengele cha mbinu rejeshi.
Kutokana na maoni ya wataalamu hawa, tumeweza kubainisha mihimili ya
kimtindo tukirejelea kipengele cha mbinu rejeshi. Mihimili minne iliweza
kubainishwa kama ifuatayo:
1. Matumizi ya mbinu rejeshi huonyesha kile kilimpa mhusika motisha katika hadithi. Muhimili huu ulitusaidia kuangalia kilichomsukuma
mhandishi kutunga kazi yake namna alivyoitunga.
2. Mbinu rejeshi hurudia tukio fulani lililopita kuhusu mhusika. Muhimili
huu ulitusaidia kuchunguza matukio yaliyorudiwa pamoja na athari
yake katika kuendeleza hadithi fupi.
3. Mbinu rejeshi huibua taharuki kwa kuzingatia vipengele vya hadithi
fupi. Muhimili huu ulitusaindia kuangalia athari ya taharuki katika
uwasilishaji ujumbe katika hadithi fupi
4. Matumizi ya mbinu rejeshi uwasilisha dhamira ya mtunzi katika
hadithi. Muhimili huu ulitusaindia kuangalia dhamira ya mtunzi
ilivyowasilishwa pamoja na athari yake.
1.6 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada
Baadhi ya wahakiki ambao wameshughulikia tafiti za hadithi fupi na
kuonyesha maswala mbalimbali yanayojitokeza katika hadithi fupi za kiswahili
ni wafuatao.
King'ala, (1985) anadai kuwa mwandishi huwezeshwa na matumizi ya lugha
kuwasilisha mawazo yake kwa msomaji wake. Anasema kuwa matumizi ya
lugha ya mwandishi yaweza kuwa yanavutia au yakawa dufu, ambayo
hayawatii moyo wasomaji. Rata yote hutengemea ufundi wa mwandishi katika
kutumia lugha. Hivyo ni matumizi ya lugha ambayo hufanya ujumbe wa
mwandishi ueleweke vyema au usieleweke na msomaji. Utafiti wa King'ala ni tofauti na wetu. Ameangazia matumizi ya lugha kwa jumla na vile yanaweza
kuwavutia wsomaji au yakawa hayawavuti wasomaji. Utafiti wetu umeangazia
kipengele cha mbinu rejeshi na vile kimeweza kuibua athari kwa msomaji,
mhusika na mandhari katika hadithi fupi za Kiswahili.
Mwachofi (1987:57) katika tamthilia ya Mama Ee ametumia mbinu rejeshi
ndani ya mbinu rejeshi. Mwachofi anatoa sifa za wahusika akizingatia mandhari yao. Mtunzi ameshugulikia mbinu rejeshi kwa kuwahusisha
wahusika katika kazi yake. Utafiti wetu uliangalia kwa kina jinsi wahusika
wanaathiriwa na mtindo wa mbinu rejeshi.
Naye Burhani (1987) katika riwaya ya Mwisho wa Kosa amezingatia matumizi
ya mbinu rejeshi katika sura ya kwanza. Hapa mtunzi anarejelea kuwasili kwa
Monica na tabia yake. Msilimulizi ametumia mbinu rejeshi ya ukamilishaji
kwa kuonyesha kuwasili kwa Monica na kueleza tabia yake kama mhusika
aliyedhoofika kitabia. Monica ameathiriwa na mandhari ya nchi za ughaibuni.
Aidha utafiti wetu uliangalia vile mandhari yanamuathiri muhusika katika
hadithi fupi.
Kwa mujibu wa Walibora na Wange'ndo, (2004:50-60) hadithi sharti ijenge
taharuki. Aidha wamesema kuwa taharuki hii huzua udadidisi wa wasomaji.
Maoni yao ni kuwa hadithi ambayo ni ya kweli itakuwa na sifa hii ya
kitaharuki. Kwa mantiki hiyo kasoro kubwa ambayo hadithi inaweza kuwa
nayo ni kukosa kuibua taharuki miongoni mwa wasomaji. Utafiti huu ni tofauti
na wetu. Mtindo wa taharuki umeangaziwa hata hivyo si kwa upana. Utafiti
wetu uliweza kuchunguza kwa kina jinsi mtindo wa mbinu rejeshi unaibua
taharuki kwa msomaji.
Walibora (1996) katika riwaya ya siku Njema amehakiki kazi hii na kutumia
mbinu rejeshi katika sura ya kwanza. Hapa mwandishi anaeleza maisha ya
mama yake vile alikuwa mwimbaji wa nyimbo za taarabu na jinsi alimpa
malezi bora hata hivyo mamake mtunzi alikuwa marehemu. Walibora
ameangalia sifa za mhusika katika riwaya. Utafiti wetu umekuwa tofauti na
huu. Tumeshughulikia vile wahusika wanaathiriwa na mtindo wa mbinu rejeshi
katika hadithi fupi za Kiswahili.
Mkangi (1997) ametumia mbinu rejeshi ya kibinafsi katika riwaya ya Walenisi.
Mhusika mkuu Dzombo anakumbuka jinsi alivyoasishwa kazi kutokana na
harakati zake za kuwazindua wafanyikazi wenzake. Mtunzi amewasilisha
mandhari ya ukoloni. Utafiti wetu uliweza kuchunguza jinsi mandhari
yanayoibuka kupitia matumizi ya mbinu rejeshi yanavyomuathiri mhusika.
Mbinu hii pia imetumiwa katika diwani ya Hekaya za Abunuwas na
Hadithi Nyingine katika hadithi ya kisa cha majuha wawili na wanawake.
Mtunzi wa hadithi hii arneonyesha ile athari iliyowapata wahusika na kuwa na
17
hisia za huzuni. Utafiti wetu pia uliweza kuchunguza kwa kina hisia
mbalimbali zinazowapata wahusika mtunzi anapotumia mbinu rejeshi katika
hadithi fupi za Kiswahili.
Wamitila, (2002) alisema kwamba kazi yoyote ya fasihi huwa na mwanzo, kati
na mwisho. Alitoa maoni kuwa kazi ya hadithi fupi inatarajiwa kuwa na
mtindo wa lugha ambao una uwezo wa kuwanasa wasomaji wa kazi ya fasihi.
Maoni yake ni kwamba mbinu za mtindo wa lugha ndizo zinamwongoza
mwandishi kufikia Lengo Lake. Hata hivyo Wamitila alisema kuwa mtindo wa
mbinu rejeshi hautakiwi kutumiwa kwa upana kama tanzu zingine mathalani
riwaya.
Aidha anasisitiza kuwa msomaji anapatwa mvuto ambao unamletea hisia alizo
nazo kumhusu mhusika fulani. Zinaweza kuwa ni hisia za kuchukia, kupenda,
kuhurumia, kusikitikia, kujitsmbulisha, kusinya, kukerwa na kadhalika. Ikiwa
msomaji amevutwa na mhusika huwa ana hamu ya yatakayompata. Wamitila
amesema mvuto hasi ni ule wa kinyume yaani kuchukia, kukerwa, kusnywa na
kadhalika. Mvuto hasi katika hadithi fupi hupatikana katika wahusika wawi au
asidi. Mvuto hasi katika hadithi fupi hupatikana katika wahusika nguli
kinyume na riwaya.
Utafiti wetu ulikuwa na tofauti na Wamitila kwa vilie alishughulikia matumizi
ya mbinu rejeshi katika riwaya. Utafiti wetu uilijikita katika athari ya mbinu
rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili. Aidha utafiti wetu utaangazia jinsi
mbinu rejeshi imekuwa na uwezo wa kumvuta msomaji ili aendelee kusoma
hadithi husika.
Wafula (1999) anasema kuwa mtindo wa mbinu rejeshi umetumiwa katika
tamthilia ya Marejeo. Wafula anadai kuwa mtunzi wa kazi hii ametumia
mbinu rejeshi kwa kuangazia vitendo viwili ili kuwasilisha ujumbe wake.
Mtunzi ameshughulikia ujumbe na mandhari. Utafiti wetu umeweza
kuchunguza kwa kina jinsi mbinu rejeshi huathiri ujumbe na mandhari ya
mtunzi katika hadithi husika.
Wamitila (2002:13) katika kitabu chake cha Uhakiki wa Fasihi anasema kuwa
mtindo wa mbinu rejeshi hutumiwa na mwandishi wa fasihi pale ambapo
anayarudia maswala au mambo ya nyuma. Wamitila anaeleza vile mwandishi
anaweza kutumia mtindo huu akiangazia sababu kadhaa. Kwanza
alizungumzia swala la kuwapa wasomi msingi au usuli wa hali ya mhusika au
wahusika mbalimbali. Aidha Wamitila anasema kwamba mtindo huu
unatumiwa ili kuweka misingi imara ya kuendeleza dhamira ya maudhui ya
kazi inayohusika. Utafiti wake unaeleza vile mbinu rejeshi katika riwaya ya
Kiu ya M.S Mohamed inajitokeza. Hapa mhusika ambaye ni Bahati
anayasimulia maisha yake na kabla ya kufikia hali ya sasa ya kupuuzwa na
kutengwa. Bahati ameathiriwa na matukio ya nyuma. Hii ndio sababu
anayasimulia maisha yake ya hapo awali. Aidha utafiti wetu utaangazia athari
ya mbinu rejeshi kwa wahusika.
Wamitila anasisitiza kuwa msomaji anapatwa na mvuto ambao unamletea
hisia. Mvuto ni hisia alizo nazo kumhusu mhusika fulani. Zinaweza kuwa ni za kuchukia, kupenda, kuhurumia, kusikitikia, kuj itambulisha, kusinya,
kukerwa na kadhalika. lkiwa msomaji amevutwa na mhusika fulani huwa ana
hamu ya kujua yatakayompata. Msomaji anaweza kuwa na mvuto chanya au
mvuto hasi. Mvuto hasi ni ule wa kinyume yaani kuchukia, kukerwa,
kusinywa na kadhalika. Mvuto wa aina hii unapatikana katika wahusika wawi
au asidi. Mvuto hasi katika hadithi fupi hupatikana katika wahusika nguli
kinyume na riwaya. Utafiti wetu unajikita katika kipengele cha mtindo cha
mbinu rejeshi najinsi inaibua mvuto kwa msomaji.
Walibora na Wang'endo (2004:59-60) wamesema kuwa ni sharti hadithi ijenge
taharuki. Aidha wamesema kuwa taharuki hii huzua udadisi wa wasomaji.
Taharuki ni mbinu inayotumiwa ili kuwafanya wasomaji au hadhira kutaka
kujua ni nini kitakachofuata. Maoni yao ni kuwa hadithi ambayo ni ya kweli
itakuwa na sifa hii ya taharuki. Kwa mantiki hiyo kasoro kubwa ambayo
hadithi inaweza kuwa nayo ni kukosa kuibua taharuki miongoni mwa
wasomaji. Maoni ya wataalamu hawa ni kuwa hadithi ambayo haina taharuki
itakuwa imepwaya na kuwa ovyo.
Kwa mujibu wa Wafula na Njogu (2007:69-70) katika Nadharia za uhakiki wa
Fasihi, mtindo wa mbinu rejeshi umetumiwa na Mazrui katika tamthilia ya
Kilio cha Haki kuthimbitisha namna matendo yaliyopita yanavyoathiri matukio
na maamuzi ya wahusika Musa na Dewe. Utafiti wetu ulichunguza kwa kina
jinsi mbinu rejeshi huathiri mtukio ya wahusika yaliyopita.
Babu (2010) amesema kuwa hadithi huwa zimekolezwa taharuki inayotarijiwa
kumvuta msomaji ili aendelee kuisoma na pia zina mwisho wa kushtukiza.
Anasisitiza kuwa mbinu hii hutumiwa kama ya kupitisha muda na kukuza
ploti. Utafiti wetu aidha uliangazia jinsi mbinu rejeshi uibua taharuki kwa
msomaji wa hadithi fupi.
Naye Mwanzi (1997) katika tasnifu yake ya uzamivu ameshughulikia mtindo
wa hadithi fupi za ngugi Wathiong'o , Leonard Kibera na Grace Ogoti.
Amezingatia matumizi ya lugha kama vile taharuki, mazungumzo na ishara.
Utafiti wetu ulikwa tofauti na wa Mwanzi. Tuliweza kuchunguza kwa kina
athari ya mtindo wa mbinu rejeshi katika hadithi fupi za wahariri Mwenda
Mbatia na Tribemwangi.
Muusya (2012) ametoa maoni kuhusu matumizi ya lugha katika hadithi fupi.
Amesema kuwa mwandishi mzuri wa hadithi fupi ni yule ambaye matumizi
yake ya lugha yatakuwa na athari wkwa msomaji wa hadithi fupi. Aidha
alitafiti mandhari katika hadithi za kiswahili. Matokeo yaliweza kugudua
kuwa waandishi wa hadithi fupi husawiri madhari iliyojikita katika en eo moja.
Anaeleza kwamba mandhari haya hayabadiliki na ikiwa yanabadilika uwa ni
kwa kiwango kidogo. Hivyo akasema kwamba mandhari yanayosawiriwa
hutengemea mwandishi mwenyewe na tajriba yake katika mazingira
anayoishi. Utafiti wa Muusya ulikuwa tofauti na wetu kwa kimsingi kwamba
utafiti huu ulijikita katika kuchunguza athari ya mbinu rejeshi katika hadithi
fupi za kiswahili.
1.7 Mbinu za utafiti
1.7.1 Muundo wa Utafiti
Utafiti huu ni wa kimaelezo. Maelezo yametolewa kuhusu namna mbinu
rejeshi inavyotumiwa katika hadithi teule. Aidha maelezo kuhusu athari ya
mbinu rejeshi katika kuwasilisha ujumbe yametolewa.
1.7.2 Mahali paUtafiti
Utafiti huu umejikita katika maktaba. Usomaji mpana wa maktabani
ulifanywa. Usomaji huu ulilenga kwa kina diwani mbili za hadithi fupi na yale
yaliandikwa kuhusu mbinu rejeshi na nadharia ya elimumtindo. Mtafiti
alisoma makala mbalimbali yalioandikwa kuhusu mada ya utafiti kama vile;
vitabu, tasnifu, magazeti na majarida. Kutokana na makala haya mtafiti alipata
mwongozo juu ya yaliyoandikwa kuhusu mada napia kujua yale yaliyofanyiwa
utafiti na wataalamu wengine. Mtafiti aliyanakili mambo muhimu aliyoyasoma
kuhusu mada ya utafiti. Miongoni mwa yale aliyoyatengwa ni matumizi ya
mbinu rejeshi na athari ya mtindo huu katika diwani mbili teule za hadithi fupi.
1.7.3 Uteuzi wa Sampuli
Mtafiti alizingatia mbinu kusudio kwa sababu alilenga diwani mbili za
hadithi fupi ambazo zimehaririwa na watunzi wawili wa kazi ya fasihi. Kazi
hizi ni Mwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) na Kunani Merikani na
Hadithi Nyingine (2011). Pamoja na hayo mbinu kusudio ilitumiwa
kuchanganua athari ya mbinu rejeshi katika diwani hizi mbili. Diwani za
Mwendawazimu na Hadithi Nyingine na Kunani Merikani na Hadithi
Nyingine ziliteuliwa. Kazi hizi mbili ziliteuliwa kwa sababu ziliweza kumfaa
mtafiti katika utafiti wake wa kuchunguza athari ya mbinu rejeshi katika
hadithi fupi za kiswahili. Kazi hizi zimehaririwa na waandishi tofauti. Bali
na tofauti ya waandishi, ni kazi ambazo zimeangazia matumizi ya mbinu
rejeshi ambalo ndilo wazo kuu la mtafiti katika mada yake. Mtindo wa
mbinu rejeshi umeteuliwa ili uweze kuchunguzwa kwa kina. Sababu ni
kwamba utafiti huu ulinuia kuchunguza athari ya mbinu rejeshi katika hadithi
fupi za kiswahili. Mbinu kusudio ilitumiwa kuteua hadithi kumi na nne
ambazo ni asilimia hamsini na sita kati ya hadithi ishirini na tano.
Mwendawazimu na Hadithi Nyingine
Hadhithi: Ukurasa:
1. Mwendawazimu l-10
2. Korti ya kishenzi. 28-44
3. Walicheka Kicheko .45-49
4. Mbio za sakafuni 50-54
5. Mboni ya Jicho 55-60
6. Jitu la kisasa : 66-72
23
7. Hachukuliki.. 73-90
Kunani Merikani na Hadithi Nyingine
Hadithi Ukurasa
I. Kunani Merikani 1-15
2. Mja ni mja 16-33
3. Kwa nini'r.. 56-70
4. Siri 71-77
5. Mapenzi chungu 78-84
6. Mtengo wa panya I13-119
7. Maji aliyavulia nguo!. 144-164
1.7.4 Ukusanyaji waData
Katika utafiti huu njia kuu ya kukusanya data ilikuwa ni usomaji wa kina.
Katika kusoma mtafiti alinukuu sehemu ambapo mbinu rejeshi imetumika.
Data iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywa kutoka kazi mbili za fasihi
andishi. Kazi hizi ni Mwendawazimu na Hadithi Nyingine na Kunani Merikani
na Hadithi Nyingine. Mtafiti alisoma vitabu hivi kwa kina na kuyaandika
mambo yale muhimu yanayohusu utafiti huu. Miongoni mwa yale
yaliyotengwa ni matumizi ya mtindo wa mbinu rejeshi na kuandikwa kando
kama mojawapo ya data ya utafiti.
1.7.5 Uchanganuzi wa Data
Data iliyokusanywa baadaye ilidondolewa na kunukuliwa. Mwishowe
ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na vilevile kuzingatia
nadharia ya mtindo. Katika uchanganuzi huu aina mbalimbali za mbinu
rejeshi zilichuguzwa. Vilevile athari ya msuko wa maudhui na usawari wa
wahusika ziliangaziwa kulingana na malengo yetu.
1.7.6 Uwasilishaji wa Matokeo
Data iliyokusanywa i1iwasilishwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia sura
mbalimbali. Uwasilishaji wa data ulifanywa kwa kuongozwa na malengo ya
utafiti pamoja na mihimili ya nadharia teule ambayo ni nadharia ya
elimumtindo.
1.8 HITIMISHO
Sura hii imejadili mambo ya kimsingi ambayo yanahusiana na utafiti huu.
Haya ni pamoja na swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchangua
mada. Aidha misingi ya nadharia imeshughulikiwa. Upeo wa mipaka na
yaliyoandikwa kuhusu mada yameangaziwa. Mwishowe mbinu za utafiti
zimeshughulikiwa pamoja na uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data,
uwasilishaji wa data na uwasilishaji wa matokeo.
SURA YAPILI
ATHARI YA MBINU REJESHI KA TIKA UWASILSHAJI WA
MAUDHUI
2.0 UTANGULIZI
Sura hii imezingatia athari ya mbinu rejeshi katika diwani ya Mwendawazimu
na Hadithi Nyingine (2000) ambayo imehaririwa na Mwenda Mbatiah na
Kunani Merikani na Hadithi Nyingine (2011) ya Iribemwangi. Sura hii
ilishughulikia mchango wa mbinu rejeshi katika uwasilishaji wa maudhui na
usawiri wa wahusika katika hadithi fupi. Mihimili ya mbinu rejeshi
imezingatiwa. Nayo ni; matumizi ya mbinu rejeshi huonyesha kile kilimpa
mhusika motisha katika hadithi, mbinu rejeshi hurudia tukio fulani kuhusu
mhusika, mbinu rejeshi huibua taharuki kwa kuzingatia vipengele vya hadithi
fupi na matumizi ya mbinu rejeshi uwasilisha dhamira ya mtunzi katika
hadithi.
2.1 Mchango wa mbinu rejeshi katika usawiri wa wahusika na
uwasilishaji wa maudhui.
Fasihi yoyote, iwe andishi au simulizi huwa na wahusika. Kwa kuwa
wahusika wanatokana na kubuniwa na msanii, hatuwezi tukawaona, bali
tuanawasihi tu. Ingawa tunaweza kuwaona wahusika katika maigizo ya
tamthilia, huwa wanawakilisha wahusika jinsi wanavyoumbwa na msanii.
Hivyo msanii huwatumia kama vyombo vya kuwasilisha ujumbe ( KLB
1989:1).
Kwa mujibu wa Maitaria (2012:5) wahusika ni viumbe wanaotenda mambo
katika hadithi. Wanaweza kuwa binadamu au hata viumbe wasiokuwa na uhai
kama vile wanyama, shetani, mizuka au vizuu.
Wamitila (2008:33) anasema kuwa wahusika wanadhibitiwa kwa kiasi
kikubwa na majukumu yao ya kiujumi katika kazi za kifasihi zinazohusika.
Maelezo ya Wamitila ni kuwa wahusika wa fasihi wanaweza kutazamwa kwa
jira za kidrama. Amemnukuu mwanatolorojia maarufu Mieke ambaye alitaja
sifa kadha za kumtambua mhusika. Kwanza, ni kuuchunguza urudiaji wa sifa
zitakazotajwa na mhusika huyo. Pili, ukusanyaji wa ujalishaji wa sifa ambazo
zinasaidia kuelezea wasifu fulani. Tatu, uhusiano wa mhusika mmoja na
wahusika wengine. Nne, kuchunguza mageuko ya mhusika - ni kwa kiasi gani
mhusika fulani anabadilika au kugeuka kitabia katika kazi inayohusika?
Matumizi ya mtindo wa mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili
yameweza kuwasawiri wahusika kwa kuleza tabia zao za hapo awali.
Vipengele kama vile mandhari, dhamira na maudhui huwa na mchango
mkubwa katika athari hii. Katika kiwango kikubwa mandhari yanawaathiri
wahusika kama wahusika wanaweza kuathiriana wao kwa wao. Wahusika
wanaweza kuathiriwa na mazingira, hali ya kimaumbile, mikasa na hata
tabianchi.
Mbinu rejeshi ni mtindo wa lugha unaotumiwa na waandishi wengi wa hadithi
fupi ili kupanua mawanda yake. Kwa kufanya hivyo sehemu kubwa ya
mhusika huweza kumulikwa.
2.1.1 Mwendawazimu-Rose Shake.
Mwandishi ameirudisha hadithi nyuma kwa kuelezea matukio yaliyopita.
Mzee Katona anasoma gazeti kuhusu mwanadada mmoja aliyevamiwa na
majambazi watatu katika barabara kuu ya mjini Nairobi na kupokonywa
shilingi elfu hamsini alipokuwa akitoka benki. Hapa mhusika Katona ana
mawazo kuhusu visa vya unyang'anyi wa pesa ambavyo vinatokea mjini
Nairobi. Hii ni mbinu rejeshi ya kibinafsi. Kwa mfano katika nukuu ifuatayo
kuna maelezo kuhusu visa vya vinavyotokea mjini Nairobi
Ni juzi tu kulikuwa na kisa cha jamaa mmoja aliyeghibiliwa
kwamba atazidishiwa pesa zake maradufu akisali pamoja na
"makasisi" wawili waliokuwa na kipawa cha kuwaombea watu.
Katika maombi yaliyofanyika katika kichocheo kimoja karibu
na kituo kimoja cha magharibi cha "Tea Room, jamaa huyu
alifumbua macho baada ya"Amen na kujikuta peke yake.
Shilingi zake elfu kumi na moja na viatu alivyambiwa avivue
katika kusali vikawa vimeporwa (uk. 2-3).
Aidha Mzee Katona anaonekana akiwa na mawazo zaidi kuhusu vile mkewe
alimshawishi ili waambatane pamoja akienda kuchukua kiinua mgongo. Hata
hivyo mzee Katona hakuyakubali maoni ya mkewe kwa sababu ameishi
Nairobi kwa miaka kadhaa na haoni sababu ya kuandamana na bibi yake
Ndunge.
Mtunzi ametumia mbinu rejeshi ya kibinafsi na kuweza kuwasawiri wahusika.
Maelezo haya yote ya mwanadada, jamaa na Mzee Katona yameweza
kuwasawiri wahusika na tabia zao. Makasisi wanaotajwa na mwandishi si
makasisi wa kweli bali ni wezi ambao wamejibandika jina la dini. Hawa si
waumini wa Mungu maana wanaiba mali ya wenyewe.
Mzee Katona ni mtu mwenye tamaa kwa sababu hataki kuandamana na bibi
yake kwenda kuchukua kiinua mgongo. Shida anazozipata mzee Katona
zinasababishwa na kukosa kutilia maanani maoni ya mkewe Ndunge. Kama
angemsikiliza mkewe, yanayompata kwa sasa hayangempata. Hii ndio sababu
ana mawazo mengi kuhusu wizi wa ulaghai unaoendeleajijini Nairobi.
Mwandishi ameweza kuwasilisha masuala ya wizi na tamaa. Haya yanajitokeza
kupitia wahusika kama Mzee Katona, wezi wanaojifanya kuwa makasisi na
kisa cha mwanadada aliyeibiwa na majambazi.
Ndunge ni mhusika ambaye ana maono na anampenda mume wake Katona. Ni
mnyenyekevu na anatumia lugha yenye heshima. Mwandishi anatumia mbinu
rejeshi ya ndani na kuonyesha vile Ndunge aliweza kumpa mumewe nasaha
kuhusu safari yake. Haya yanawasilishwa na nukuu ifuatayo:
"Mume wangu si vyema kwenda peke yako. Unaweza kuporwa mali
hiyo na majambazi. Tafadhali tuandamane ili tuweze kusaindiana kuzilinda pesa hizo majambazi watasita kutuvamia tukiwa pamoja
kuliko ukiwa peke yako ... "(uk. 3)
Ndunge anatumia lugha yenye unyenyekevu. Hii ni dhibitisho kuwa huyu ni mhusika mwenye heshima kwa mumewe.
2.1.2 Kunani Merikani--Iribemwangi
Hadithi hii imeanza na mbinu rejeshi ya muktadha mpana. Mwandishi ambaye
ni msimulizi anayasimulia maisha yake ya tangu utotoni. Ameeleza ile tamaa
aliyekuwa nayo ya kwenda Merikani katika enzi zake za utotoni. Kule
kumulika maisha ya mhusika ya hapo awali kumeweza kuibua maudhui ya tamaa na kumsawiri msimulizi kama mhusika mwenye tamaa kupitia maelezo
yafuatayo;
Nilipokuwa mtoto mdogo nilitamani sana kwenda Merikani, kwa
hakika nilitamani sana kupanda ndege. Wakati huo, uzuri au ubaya wa ndege ulikuwa wa kufikirika tu; kwa hakika sikumbuki kufikiri ubaya wowote ... (ukl). Merikani. Ni tamaa iliyoniandama sana wakati wa miaka yangu ya awali (uk.l)
Mtunzi anadhamiria kuonya jamii dhidi ya tamaa katika maisha. Mwandishi ana tamaa ambayo iliweza kumpa motisha, akasoma hadi Merikani na kuweza
kutimiza ndoto zake. Rata hivyo kuna baadhi ya wahusika ambao wameweza kuwa na tamaa yenye mwelekeo hasi na kupotoka katika maisha yao.
Kulingana na mwandishi wahusika hawa ni kama mkurugenzi, kasisi na Liz.
Ni tamaa ambayo i1iweza kumfanya mkurungezi kwenda Merikani na kuacha
kazi yenye hadhi nchini. Mwandishi ametumia mbinu rejeshi ya muktadha mpana na kueleza maisha ya mkurugenzi na vile aliathiriwa na tamaa na
mwishowe akaanza kuishi maisha ya dhiki. Anaeleza jinsi Mkurugenzi
alikuwa akifanya kazi ya kifahari akiwa nchini Kenya. Mwishowe mwandishi
anaonyesha vile Mkurugenzi anasosoneka akiwa nchini Merikani (3-4).
Mkurgenzi na familia yake wameathiriwa na maisha wanayoishi kwa sasa kwa
sababu ya tamaa. Alikuwa anaishi maisha ya ubwanyenyenye akiwa nchini
Kenya lakini kwa sasa yeye na familia yake wanaishi maisha ya ufukara.
Mkurugenzi anafanya kazi ya shokoa huku Merikani kisa na maana
hakutosheka na mapato aliyekuwa akiyapata katika nchi yake.
Mwandishi amemsawiri mhusika kasisi kama mhusika mwenye tamaa kwa
matumizi ya mbinu rejeshi. Kasisi alipatwa na tamaa ambayo ilimpeleka
Merikani na kuacha kuendeleza injili ya Bwana. Mwandishi anaeleza kuwa si
Mkurugenzi ambaye alikuwa na tamaa ya kwenda Merikani bali kulikuwa na
wengine kama kasisi ambaye mwishowe aliweza kuathiriwa na tamaa
aliyekuwa nayo. Mtunzi ametoa maelezo yafuatayo kuhusu tamaa iliyompata
kasisi.
I1ifika wakati kasisi akapatwa na wazimu wa kwenda Merikani. Mwanzo akitafuta visa ya kwenda kule kama mwanafunzi lakini
31
hatimaye "akafanikiwa" kapata mwaliko kuhudhuria mkutano mkubwa wa dini. I1ivyo ni kwamba bahati, kama vile msiba, haiji pekee; huja na mwezake ...(uk 6-7).
Hii ni mbinu rejeshi ya muktadha mpana. Sifa za kasisi zinajitokeza. Yeye
ni mhusika mwenye tamaa kwa sababu hatosheki na mapato anayoyapata
kutokana na kuendeleza inj ili.
Kasisi aliishi maisha ya wastani na familia yake akiwa nchini. Kwa sasa
anaishi maisha ya dhiki na shida. Ameshindwa na kuendelea na elimu na
kuanza kutafuta kazi hapa na pale. Mwishowe hakufanikiwa kuipeleka familia
yake Merikani kama alivyotarajia. Kwa sababu ya tamaa alianza kuogopa
kushikwa na mkono wa sheri a na hii ndio sababu alikosa kukutana na jamaa
yake katika uwanja wa ndege huko Merikani.
Liz naye kwa kukosa kufanikiwa kwenda Merikani na kuishi huko kama ahadi
ya baba yake, aliamua mwishowe atasafiri hadi Merikani liwalo liwe. Tamaa
ndio ilimfanya kumtafutia mtoto wake bibi yaani Natasha bila hata kujali hali
yake na kumfanya kupatwa na ugonjwa wa Ukimwi. Natasha anamwandikia
Liz barua na kumpasha juu ya siha yake na kumueleza vile aliweza kumkosea
mtoto wake. Haya yanaelezwa kwa matumizi ya mbinu rejeshi ya muktadha
mpana. Barua ifuatayo imetoa maelezo zaidi.
13-03-200
Kwa Liza
Salamu zangu bibie. Natumai kuwa hali yako ni nzuri tangu
nilipokuletea mwanao miaka ipatao miwili sasa. Mimi nipo ingawa bado sijampata Mwafrika mwingine WA kutaka niolewe Na mwanaye
japo Kwa muda, labda nikushukuru kwa sababu ya fadhila hiyo
uliyonitendea. Hata ssuliyoyatenda, yaani kumkosea mwanao heshima ulivyomkosea, na mengine nitakayokupasulia hivi punde?.
Lakini samahani kwa hayo, kusudi la kukuandikia barua hii haikuwa
kuzungumza mambo ya dawa. Nilitaka kumjulia h"alialiyekuwa mume wangu. Nimekuuliza ni lipi la mno Merikani hata ukamletea mwanao maafa uliyomletea. Uliponilipa nikaolewe naye, hata
hukusaili kujua haliyangu. Haliyangu si nzuri kiafya, lakini nilihitaji
fedha, fedha! Tangu miaka minne iliyopita niliguduliwa kuwa nimeambukizwa virusi vya ukimwi, na kwa sababu hiyo, nimekuwa
mhitaji wa fedha ili kuweza kujikimu kwa chakula kifaacho na
dawa. Hii ndio ilikuwa sababu nilikubali ombi lako jambo shingo
upande na kwa moyo mzito. Nilibaini kwamba kama singefanya hivyo, ningekufa mapema, labda hata sasa ningekuwa marehemu, na sikuwa tayari kufa kijana ...
Kila la kheri,
Natasha carrier (uk14).
Barua hii inatoa maelezo kuhusujinsi Liz alimuoza Natasha kwa
mwanaye Sisika bila hata kujali hali ya Tasha ambaye alikuwa na maradhi ya
Ukimwi. Hii ni thiibitisho kuwa Liz alikuwa na tamaa. Mwandishi
ameyamulika maisha ya Liz yenye tamaa na kumsawiri kama mhusika mwenye
tamaa. Shida zinazompata mtoto wake zinasababishwa na yale maisha ya
kwenda Merikani. Mwanawe kwa sasa ni mlaguzi wa dawa za kulevya kama
yeye na isitoshe, ameabukizwa maradhi ya Ukimwi.
Kama tulivyosema hapo awali wahusika wa hadithi fupi huwa wachache.
Ukweli ni kuwa kuna wahusika wengine ambao wamesadia kuendeleza hadithi
ingawa sio wahusika wakuu. Matumizi ya mbinu rejeshi huwasawiri wahusika
wasaidizi. Mfano wa wahusika hawa ni kama Natasha, watoto wa kasisi
kama Liz, Sisika ambaye alikuwa mtoto wa Liz na Natasha bibiye Sisika.
Mwandishi ameyasawiri maudhui mbalimbali kama tamaa, matumizi ya dawa
za kulevya, maradhi ya Ukimwi, elimu na kazi. Suala la tamaa lajitokez kwa wahusika kama msimulizi. Alitamani sana kwenda nchini Merikani na
mwishowe akafanikiwa na akarudi nchin na shahada yaphD. Hapa mwandishi
amejaribu kuonyesha jamii kuwa kuna tamaa ambayo inaweza kuwa na
mwelekeo chanya na kuweza kumfanya binadamu kuishi maisha yenye
mafanikio. Msimulizi kwa sasa anaishi maisha ya furaha akiyalinganisha
na yale ya Mkurugenzi, kasisi, mke wa kasisi na watoto wa kasisi kama
Liz.
Kwa wahusika hawa matarajio yao yaligonga mwamba na mwishowe
wanapata dhiki badala ya mafanikio. Mkurugenzi anaishi maisha ya
kuhurumiwa maana anafanya kazi usiku na mchana huku akidhulumiwa.
Kasisi naye hana lingine isipokuwa kutafuta kazi hapa na pale ndio
aweze kupata mkate wa siku. Liz amekuwa mlaguzi wa dawa za kulevya
pamoja na mwanaye. Wahusika hawa wameathiriwa na matukio ya
nyuma ambayo ni majuto kwa sasa.
Maudhui ya dini na elimu aidha yamesisitizwa. Kasisi alikuwa anaeneza injili
ya Mungu. Suala la elimu linajitokeza wakati msimulizi anayaeleza maisha
yao ya shuleni na mkurugenzi. Msimulizi naye anaenda Merikani na kumaliza
masomo yake. Kazi ni muhimu sana katika jamii. Mkurugenzi alikuwa
akifanya kazi ambayo ilimfanya kuishi maisha ya mlalaheri. Kasisi alifanya
kazi ya kuendeleza ya Mungu na iliyowakimu maishani.
2.1.1 Korti ya Kishenzi - David Maillu
David Maillu anadhamiria kulenga dhana ya elimu na utamaduni katika
jamii. Mwandishi anaeleza vile elimu na utamaduni katika jamii
zimekizana na kuleta mgogoro baina ya waliosoma hasa wale wenye
elimu ya juu na wale ambao hawajasoma. Aidha vijana wanaonywa
kuhusu uhusiano wa kimapenzi katika ujana wao ambao kwa upande
mmoja unaathiri hasa jinsia ya kike.
Mtunzi ametumia mbinu rejeshi ya ndani ambayo inaibua mbinu rejeshi
ya kibinafsi. Mhusika Kanu anaathiriwa na habari alizoletewa juzi
kuhusu uhusiano wa kimapenzi baina ya mume wake na mhazili. Kanu
alipoteza uwezo wa kupanga na kuendesha shughuli zake. Anapatwa na
fikra kuhusu maisha yake, mapenzi, ndoa na watoto. Hii ni mbinu rejeshi
ya kibinafsi.
Jana alipoletewa habari kuwa mumewe anatembea na mhazili
wake, uwezo wa kupanga na kuendeleza shughuli zake ulimwishia
(uk29).
Kanu anapatwa na fikra za maisha yao na Ngoloso wakiwa shuleni.
Mtunzi ameweza kueleza vile vijana hawa waliweza kuongelelea katika
bahari ya mapenzi bila kuwa na mbinu tosha kwa matumizi ya mbinu
rejeshi. Anaeleza vile maisha ya Kanu yaliweza kuathiriwa na matukio
yaliyopita kupitia mbinu rejeshi ifuatayo.
Kabla ya kuoana, Agnes Kanu na Onesmas Ngoloso walijikuta
katika bahari ya mapenzi bila ya kuwa mbinu tosha za
kuongelea. Walipatana humo kwa muda. Ngoloso alikuwa
chuo kikuu akisomea uanasheria, naye Kanu alikuwa
mwanafunzi wa shule ya upili. Wote walikuwa vijana wabichi. Katika bahari ya mapenzi wanagenzi wasio na
uzoefu wa kuongelea hukumbwa na ajali nyingi. .. (uk 29).
Hapa mbinu rejeshi kadhaa zimefuatana na kuweza kuibua mbinu rejeshi
ya kikufu. Mbinu rejeshi hizi zimeweza kuwasawiri wahusika kwa kutoa
siri zao kama vile; mhazili, Kanu na Ngoloso. Maisha ya Agnes Kanu
na Onesmas Ngoloso .yanaelezwa na sababu zinazomfanya Kanu kuwa na
mateso anayoyapata kwa sasa. Kanu hakuweza kumaliza masomo ya
shule ya upili kwa sababu alipata mimba akiwa katika kidato cha pili
naye Ngoloso akiwa katika chuo kikuu akisomea uanasheria. Jambo ili
lilimlazimisha Kanu kuacha shule na kuolewa na Ngoloso.
Uhusiano wa kimapenzi wa Ngoloso baina ya mhazili wake ni jambo la
siri hivyo Iikafichuliwa na matumizi ya mbinu rejeshi.
Sifa za Ngoloso na Faith zinajulikana kupitia mapenzi yao. Mwandishi
anaeleza uhusiano wa Ngoloso na Faith vile ulianza na vile Ngoloso alikuwa
na mbinu za kuwatongoza wan awake kwa kuirudisha hadithi nyuma.
Tangu mapenzi ya Faith na Ngoloso yaanze, mwanamke
huyu alijihisi kwamba, aliyokuwa akifanya siyo sawa lakini
angefanyaje na Ngoloso alikuwa bosi wake na bali na
hayo Ngoloso alikuwa na sifa chungu nzima zilizowafanya
wan awake wengi kuvutiwa naye ...(uk32).
Ngoloso ni mhusika ambaye amekosa uwajibikaji. Si kielelezo chema katika
jamii. Anamnyanyasa Faith ambaye ni mhazili wake kupitia mapenzi nje
ya ndoa. Ingawa hisia za Faith zinamuarifu kuwa yale anayoyafanya
hayafai, hana suluhisho kwa sa sa maana Ngoloso ni bosi wake.
Kanu ni mlezi wa watoto wao: Ana fikra kuhusu vile ataendelea na
kuwalea watoto wao peke yake alipopata habari ya uhusiano
37
wakimapenzi wa mumewe na mhazili wake.
Ngoloso hana utu maana anafanya mapenzi na mhazili wake na
kumnyima mkewe mapenzi.
Ngoloso m mhusika asiyewajibika kwa sababu anatafuta mbinu za
kumuacha Kanu kupitia fikra alizokuwa nazo ili aweze kumuoa Faith
ingawa alijua ukoo ulimpenda Kanu sana. Nukuu ifutayo inatoa maelezo
zaidi.
Bwana Ngoloso alifikiria njia kadha wa kadha za kumfukuzia
Kanu ili aweze kupata njia ya ndoa baina yake na Faith.
Lakini hakuweza kupata njia mwafaka. Alifahamu kwamba
wazazi wake walimpenda Kanu na hawangesikiliza sababu
zake za kutaka kumfukuza (uk 35).
Mwandishi ameweza kuyasawiri maudhui mbalimbali. Suala la mapenzi na
ndoa limeangaziwa. Ngoloso anafanya mapenzi nje ya ndoa. Aidha maudhui
ya elimu yanajitokeza wakati mwandishi anaeleza maisha ya Ngoloso na
Kanu wakiwa shuleni. Ngoloso aliweza kumaliza masomo yake na
kupata kazi ya uanasheria. Kanu naye hakuweza kumaliza masomo yake.
Alipata mimba na kuolewa na Ngoloso.
2.1.4 Siri- Stephen Munyasi.
Hadithi hii imeanza na mbinu rejeshi ya muktadha wa karibu. Mwandishi
anadhamiria kueleza jamii kuhusu athari ya vyombo vya teknolojia ya
kisasa kwa vijana. Kwa mujibu wa mada ya hadithi hii, mwandishi
ameweza kuficha siri za wahusika Siri na mama yake akizingatia mbinu
rejeshi.
Siri ana mawazo kuhusu rafiki yake aliyempata katika mtandao. Mawazo
haya yamemsababisha kuumwa na kichwa huku maneno ya mpenzi wake
yakimpitikia akilini mwake huku akimwita kirukanjia (uk 71-72).
Siri ameathiriwa na mapenzi kiasi cha kuwa na fikra kuhusu mpenzi
aliyempata katika Facebook. Hata hivyo haya ameyaweka kama siri.
Anaathiriwa na mapenzi ya mpenzi wake na kuanza kuumwa na kichwa.
Iwapo hangekuwa na uhusiano huu tena wa mpenzi aliye mbali
hangekuwa na mawazo ambayo yanamtatiza.
Mamake mzazi anaathiriwa na tabia ya Siri mpaka anawaza na kuwazua
ni nini cha mno kinachosababisha binti yake Siri kuwa na tabia ya kutojieleza
ni jambo gani linalomuathiri. Hapa ndipo mama mzazi anapatwa na fikra
kuhusu tatizo la bintiye. Mamake Siri hakuweza kueleza mwanawe kile
kilisababisha kifo cha mumewe. Jambo hili aliliweka kama siri na ndio maana
anaona kama Siri ameligudua (uk73).
Bi Mkata pamoja na Siri ni wasiri. Kati yao wawili hakuna anayetaka
kueleza shida zake. Mamake Siri ameweka siri kuhusu kilichosababisha kifo
cha mumewe naye Siri ameficha shida inayamkabidhi kwa mamake ingawa
anasononeka.
Kuna matumizi ya mbinu rejeshi ndani ya mbinu rejeshi wakati mhusika
Siri anakumbuka kuhusu riwaya aliyoisoma ya wahusika wawili. Mtunzi
ameanza na mbinu rejeshi ya kibinafsi mwishowe anasimulia hadithi ya
wahusika wawili waliopendana katika nukuu ifuatayo:
Alikumbuka riwaya aliyokuwa amesoma kuhusu wahusika wawili waliopendana kama chanda na pete. Wahusika hawa walifunga ndoa ya kukata na shoka lakini wakatalikiana miezi mwili tu baada ya arusi yao (uk 74).
Maudhui ya ndoa na talaka yamewasilishwa. Aidha Siri ni msomi kwa
sababu anakumbuka yale aliyeyasoma kuhusu wapenzi wawili wailopendana.
Jambo hili linamuathiri Siri hadi sasa ndio sababu analikumbuka.
Mhusika Siri alibakwa akiwa na miaka minane na kuamua kutosonga
karibu na mwanamume. Haya yanajitokeza wakati anapokumbuka tukio la
ubakaji ambalo linamuathri kwa sasa (uk76).
Iwapo Siri angetilia maanani ahadi yake ya kutojihusisha na mapenzi
kiholelaholela, shida alizo nazo kwa sasa hazingempata. Rafiki wa
facebook ameweza kumuabukiza maradhi ya Ukimwi. Sijali ameanza
urafiki na mabinti wengine wakati Siri hakuwa karibu.
Wakati uhusiano huu ulivunjika na kuelewa fika kuwa ana maradhi ya
Ukimwi, Siri anajiua na kuweza kuipa dunia mkono wa buriani. Kabla
ya kifo chake alimwandikia mamake barua na kumharifu kuhusu rafiki
yake aliyempata kutoka kwa facebook Sijali na ni yapi yaliyotokea baada
ya urafiki wao.
Kwa mama mpendwa, Bi Mkata,
Nasikitika kukufahamisha kwamba nina ugonjwa wa ukimwi.
Niliambukizwa na kijana mmoja aliyekuwa rafiki yangu niliyempata kwenye mtandao wa facebook. Niliamini ahadi zake, kisha yakawa na kutimia yalivyo sasa hivi licha ya kuahidiwa maisha ya uaminifu na raha mustarehe. Nilivutiwa na pasipo kujua kuwa anasambaza gonjwa hili kwa yeyote anayenaswa mtengoni.
Usinichukie kwa sababu nishajichukia. Ongea na Bw. Mroho akuonyeshe miradi niliyokuwa nimeandika kwa jina lako ili usiteseke. Rafiki yangu, Roka, atakupatia kadi ya kutoa pesa mtamboni katika benki ya Wanyonge niliyompa jana. Mama, amini kuwa Roka, hakujua masaibu wala mipango yangu ya kulitekeleza hili.
Mwanao, Siri Mkata (uk77).
Mwandishi ametumia mbinu rejeshi ya muktadha mpana aidha ya
muktadha wa karibu. Barua hii imefichua siri zote za mhusika Siri
alizokuwa amemficha mamake Bi Mkata. Uhusiano wake wa kimpenzi na
mpenzi wake Sijali na mali ambayo mamake atakayeimiliki baada ya
kifo chake. Mhusika siri ni msiri. Ameweza kumficha mamake uhusiano
wake na rafiki yake Sijali hadi dakika ya mwisho.
Mtunzi ameonyesha i1e athari inayoweza kuwapata wahusika ambao
wanajihusisha na uhusiano wa marafiki kutoka vyombo vya tekinolojia
bila hata kujali hali yao ya kiafya.
Suala la mapenzi nje ya ndoa hasa kwa vijana wa sasa Iimesisitizwa.
Vijana wengi katika jamii wameweza kuathiriwa na mapenzi wanaofanya
kiholelaholela bila hata kujali athari ya hayo mapenzi.
2.1.5 Walicheka Kicheko - John Habwe.
Mwandishi ameyarejerea maisha ya Zainabu na Mogambi wakati ndoa
yao ilikuwa bichi kwa kutumia mbinu rejeshi ya muktadha mpana.
Maelezo haya yamepichua siri za wahusika hivyo kuweza kuwasawiri.
Walipooana Mogambi alikuwa hatoki. Yuko pale
kama paka na JIVU lake. Hata si fungate Hata
baadaye alikuwa siku zote yuko ... (uk. 45).
Mogambi kwa wakati huu alikuwa bwana aliyewajibika katika ndoa yao
na Zainabu. Mtunzi ameonyesha vile matukio ya mhusika yalikuwa ya
furaha na yenye starehe. Hii ni dhihirisho kuwa tabia zake zilikuwa za
kupendeza hasa kwa mke wake.
Mbinu rejeshi inayofuata ni ya kibinafsi. Starehe walizokuwa nazo Mogambi na Zainabu hazipo kwa sasa. Zainabu anakumbuka ile siku ya Jumamosi
Mogambi alikunywa hadi akajitapikia. Mwandishi ametumia mbinu rejeshi
ya kibinafsi ambayo imeweza kuibua mgogoro baina ya Zainabu na nafsi
yake na pia Mogambi. Aidha tabia za Mogambi na Zainabu zinajitokeza.
Haya yanajitokeza kupitia nukuu lifuatalo.
Hii tabia ya Mogambi ya kuchelewa imekuwa ya muda. Anakumbuka siku ile ya Jumamosi alipofika nyumbani amekunywa hadi kujitapikia,
Zainabu hakuwa na budi i1a kumpiga kofi tatu (uk.46-47).
Zainabu anaathiriwa kiasi cha kumchapa mumewe kofi tatu. Mbinu rejeshi hii
imeleta mgogoro wa kisaikolojia kwa mhusika. Mhusika anakubwa na
mvutano wa ndani kwa ndani. Mwandishi amewaathiri wahusika Mogambi
na Zainabu kwa kuibua mgogoro ambao unamsaidia kuwasawiri. Zainabu
amechangia kusaidia katika kujaribu kukomesha tabia ya mumewe ya
ulevi kwa kumchapa kofi tatu na kuweza kupingania haki yake.
Sifa za Mogambi na Zainabu zinajitokeza. Ulevi wa Mogambi ni tukio
ambalo limekuwa la mazoea ambalo linamfanya kulewa kiasi cha kujitapikia
na kudondokwa na mkojo kama mtoto mchanga. Mwandishi amenuia
kutengua kitendawili cha ndoa ambazo zimetiliwa mbolea na ulevi na
kuwazidua wahusika- kama Zainabu ili waweze kujitetea. Tabia za
Mogambi na Zainabu zimefichuliwa na mtunzi kwa matumizi ya visegere nyuma hivyo basi kuweza kuwaathiri. Mogambi ni mlevi ambaye hajali utu wake. Kule kulewa kiasi cha kujikojolea kumempotezea utu. Naye Zainabu ni mtetezi wa haki za wanawake katika jamii.
Maudhui ambayo yanayoibuka katika hadithi hii ni ya ndoa, ulevi na haki za wanawake. Zainabu anatetea haki za wan awake kwa kukataa dhuluma ya mumewe anayomfanyia kupitia ulevi wa kupindukia.
2.1.6 Mbio za Sakafuni -0. Ong'utu
O. Onguti katika "Mbio za Sakafuni" amewasawiri wahusika Mosoti, Okiomo na Gladys kwa matumizi ya mbinu rejeshi. Mbinu rejeshi mbalimbali zimewasilishwa kama vile; mbinu rejeshi ya muktadha mpana, mbinu rejeshi
ya ndani na mbinu rejeshi ya kibinafsi.
Mapenzi ya Gladys baina ya Okiomo na Mosoti yalianza wakiwa katika shule za upili. Wanafunzi hawa walipokuwa wakisoma katika shule ya upili ndio walianza kumpenda Gladys wakiwa katika kidato cha kwanza. Mtunzi anaeleza vile Okiomo na Mosoti hawangeweza kujua kama wana urafiki na msichana mmoja Gladys maana hawakuambiana siri zao kupitia urejeshi ufuatao.
Gladys alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya wasichana ya Nyahururu. Okiomo alikuwa katika shule ya upili ya wavulana ya Sameta na Mosoti
alikuwa akisomea shule ya wavulana ya
Mosocho .... Mosoti na Okiomo walikuwa wamemtaka
mapenzi Gladys walipoingia kidato cha kwanza.
Mosoti na Okiomo hakuambiana siri zao (uk 52).
Mwandishi ametumia mbinu rejeshi ya ndani kwa kuonyesha vile hali
ilivyokuwa au mandhari yanayojitokeza wakati Okiomo na Mosoti
wanaenda kumtembelea mpenzi wao Gladys bila kujuliana hali. Anaeleza
vile Okiomo alianza kusinzia baada ya muda wasaa moja na mwishowe
alipatwa na hofu (uk 53).
Aidha kuna maeleza kuhusu Okiomo na vile alikuwa akifanya wakati
Mosoti aliona mbalamwenzi na kukimbilia usalama wake.
Wakati huu Okiomo alikuwa ameanza kusinzia kwani
saa moja ilikuwa imeshapita. Aliposikia sauti fulani
alianza kushikwa na hofu ... (uk 53).
Mwishowe matumizi ya mbinu rejeshi ya kibinafsi yanajitokeza. Okiomo na
Mosoti waliweza kukimbilia usalama wao kwa kuogopa wasionekane na
babake Gladys ambaye walifikira amekuja kuwaadhibu. Okiomo aliposikia
kwamba nyasi aliyokuwa amejifunika nayo imeondolewa alifikiria ni
babake Gladys amekuja kumshambulia. Wakati huu naye Mosoti alitoka
ndani ya nyasi alifikria kwamba ni babake Gladys amekuja kumwadhibu.
Mbinu rejeshi kadhaa zimeweza kuwasawiri wahusika ambao
wamemsaidia mwandishi kuwasilisha dhamira yake. Aidha mandhari