Mwingilianomatini Katika Cheche za Moto na Kidagaa Kimemwozea

112  116 

Loading.... (view fulltext now)

Loading....

Loading....

Loading....

Loading....

Full text

(1)

MWINGILIANOMATINI

KATlKA CHECHE ZA

MOTO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA

KULOBA PATRICK WAFULA

TASNIFU

nn

IMEW ASILISHW A KW A AJILI YA KUTIMIZA

BAADHI YA MAHITAJI

YA DIGRII

YA UZAMILI

(M.A)

KATlKA KISW AHILI YA CHUO KIKUU CHA KENY ATTA

(2)

UNGAMO

Tas

ni

f

u hii ni kazi

y

angu mwenyewe

na haija

w

ahi kuchapi

s

h

wa

popo

t

e

wala k

u

was

ilish

w

a

katika Chuo Kikuu kin

gi

n

e

ili

k

u

t

im

iza

m

ah

i

taj

i

ya

digri

i

y

o

y

ot

e

ile .

...~

.

~

.

KULOBA PATRICK WAFULA

C50/CE/2232 9 12010

TAREHE

T

as

ni

f

u hii im

e

wasilishwa

kwa idhini

y

etu kama

w

a

s

imam

iz

i

wa C

hu

o

K

iku

u

.

~

...

~

.

DR. PAMELA M. Y. NGUGI CHUO KIKUU CHA KENYATTA

TAREHE

~

-

s1r)1?:?(;-TAREHE PETE

(3)

TABARUKU

K wa mamangu mpendwa, Marehemu Getrude Namalwa Kuloba.

Na babangu mpendwa, Mzee Kuloba Nabumbayi.

Mlinipeleka shuJeni kupata elimu yenye tija. Kwa binti zangu; Valarie na Vanessa.

Mlikuwa mhimili muhimu kwangu; Kueni muwe watu wa kutegemewa maishani.

K wa Marehemu Dkt. Abel Gregory Gibbe, Ulinitoa 'jaani' na kunifanya 'mtu'.

(4)

SHUKRANI

Kwanza, natoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kunijalia neema na afya mpaka nilipoikamilisha hii kazi. Pili, natoa shukrani zangu za dhati kwa Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa kunikuza na kunipa fursa ya kutangamana najumuia ya wasomi adhimu tangu nilipoanza shahada ya kwanza hadi sasa. Isitoshe, naishukuru sana Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika kwa kunilea na pia kuniweka mikononi mwa Dkt. Pamela M. Y. Ngugi na Mwl. Peter J. M. Mugambi walionishika mkono na kunielekeza katika ulimwengu huu wa kitaaluma. Wasomi hawa walinionyesha vikwazo njiani na namna ya kuvikwepa. Nilipokunguwaa na kuanguka, walinishika mkono, wakaninyanyua na kunishajiisha. Asanteni sana.

Sitawasahau Dkt. Richard M. Wafula naDkt. Edwin W. Masinde kwa kuniangazia njia ili niweze kuona macho yalipoingia kiwi. Pia, walinipa moyo wa kujitosa katika bahari hii kuu na kunifunza kupiga makambi hadi ufuoni. Nawashukuru walimu wangu hapo idarani walionipa misingi na nadharia katika taaluma hii. Hawa ni pamoja na Prof. G. K. King'ei, Prof. C. Ndungo, Dkt. L. M. Chacha, Dkt. A.N. Mwihaki, Dkt.

- -

-C. W. Ryanga;-Dkt. J.-N. Maitaria, Dkt. M. K. Osore na Mwl. E. S. Mudhune. Dkt. Peter Karanja, alinifaa sana katika kikao cha utetezi wa mada ya utafiti. Naye Dkt. Sim Kilosho Kabale kutoka Idara ya Lugha za Kigeni alinifunza mbinu za utafiti. Aidha, Dkt. Eunice Nyamasyo wa Idara ya Kiingereza na Isimu alinichechemua sana wakati wa kikao cha utetezi wa-pendekezo la utafiti. Naye Dkt. J. K. Gakuo alinihimiza kila mara nikaze nyonga na kuchukua hatua hii kubwa na ndefu.

(5)

Kwa watunzi, Prof. Ken Walibora na Prof. John Hamu Habwe, utunzi wenu uliniwezesha kuandika haya yote. Vinginevyo, ningeandika nini kweli? Kwa Bi. Margaret Wekesa, ufadhili wako unifaa sana. Bw. John M. Mukongolo, Mwalimu Mkuu wa St. Paul's High School-Sinoko; asante sana kwa msaada wako ulioninyanyua na kunifikisha hapa. Nawashukuru wazamili wenzangu tulioingia hii suna pamoja. Hawa ni pamoja na Marehemu Wycliffe Anyasi, John Ojuma Karani, Erick Mogeni, Joy Gatwiri Njue, Margaret Wanjiru Titi, Victor Onsarigo, Simon Ngige, Ezekiel Kinoti Magaju, Erick Nyandoro, Sr. Celestine Katuka, Samwel Kazungu Lewa, Kalume Katsoma Nzai, Benson Ngige, Waithaka Mburu na Kiange Ngui miongoni mwa wengine. Asanteni nyote kwa vikao na mijadala tuliyofanya pamoja. Na kwa wote walionitilia pondo katika kazi hii, nasema asanteni sana na Mungu awajalie neema maishani mwenu. Amina.

(6)

IKISIRI

(7)

ABSTRACT

This study on Intertextuality in Cheche za Moto and Kidagaa Kimemwozea is anchored on the premise that; since the novel is a product oforal literature, it is greatly influenced by this genre. Also, poetry being the oldest literary genre, continues to influence the novel. Again, many other genres and texts continue to manifest themselves in the novel making it a corpus of several genres and texts. This interdependence and influence among genres and texts is refered to as intertextuality. Intertextuality as a concept emanated from two theories: Semiotics by Ferdinand Mongin de Saussure and Dialogism by Mikhail Bakhtin. This study set out to investigate the application of intertextuality, especially the use of genres such as poems and songs, proverbs and speeches; plus texts like letters, media reports and references in writing a Kiswahili novel. This study demonstrates the genric and textual influence and interdependence in developing the novel,and explains the functions of such genres and texts in the novel. In addition, the study shows the role played by such genres and texts in advancing themes and style in the novel. The two novels which were used in this study are: Kidagaa Kimemwozea (Walibora) and Cheche za Moto (Habwe). This study was guided by the Intertextuality Theory. This topic was chosen because the Kiswahili novel is continuously developing and absorbing other genres and texts in its form, hence becoming more complex. This complexity inhibits the reception and appreciation of themes, given that such novels are used in the school curriculum in the country. Therefore, it was imperative to carry out this study with the aim of enabling _the reception and appreciation of these novels, especially-for teachers and students. In order to realize this objective, the study identifies and analyses genres'and texts used, showing the role of such genres and texts in developing themes and form in the novel. Also, the study illustrates the role of genric and textual influence and interdependence in advancing themes and style in the Kiswahili novel. It also shows how genres and texts relate and depend on each other in communicating the author's message. This thesis is divided into five chapters. Chapter One is the introduction to the study and gives the background of the study and its methodology. Chapter Two shows the environmental influence on the authors' intertextual works. Chapter Three shows the role of intertextuality in developing themes in the relevant novels. Chapter Four shows the role of intertextuality in developing the form of the Kiswahili novel. Lastly, Chapter Five summarises the findings, gives the conclusion and recommendations of the study.

(8)

MAELEZO YA ISTILAHI MAALUMU

Matini

Aina zamaandishi au taarifa ambazo si lazima ziwe za kifasihi. Mfano ni barua na taarifa zavyombo vya habari.

Mwingilianomatini

Dhana inayoelezea kuwapo kwa sifa mbalimbali za matini moja au zaidi katika kaziya fasihi.Dhana hii inachukulia kuwa kila kazi ya fasihi inahusiana na kazi iliyoandikwa kabla kwa namna moja au nyingine.

Usemezano

Dhana inayohusishwa na Mikhail Bakhtin na inayotumiwa kueleza uhusiano kati ya matamko (matini) mbalimbali ya sasa na ya awali.

-Utanzu

Mgawanyiko watungo mbalimbali za kifasihi kama vile riwaya, ushairi, tamthilia na hadithi fupi. Ni tawi la fasihi.

Utanzu wa kimonolojia

Ni utanzu usioweza kuhusisha sifa za tanzu nyingine katika umbo lake. Kwa mfano, ushairi hauwezi kuhusisha nathari katika umbo lake.

Utanzu wa kiheteroglosia/kipolifoni

(9)

YALIYOMO

Ungamo i

Tabaruku ii

Shukrani iii

Ikisiri v

Abstract vi

Maelezo ya Istilahi Maalumu vii

Yaliyomo viii

Sura

ya Kwanza

Utangulizi

1.0 Usuli wa Mada ya Utafiti 1

1.1 Suala la Utafiti : 3

1.2 Malengo ya Utafiti 3

1.3 Maswali ya Utafiti. · 4

1.4 Sababu za Kuchagua Mada 4

1.5 Upeo na Mipaka ya Utafiti.: 5

-1.6 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 5

1.7 Nadharia ya Utafiti 11

1.8 Mbinu za Utafiti .14

1.8.1 Ukusanyaji wa Data - .15

1.8.2 Uteuzi wa Sampuli. .16

1.8.3 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Data 16

Sura

ya Pili

Athari ya Mazingira

ya Watunzi kwa Riwaya Zao za

Kimwingilianomatini

2.0 Utangulizi. 17

2.1 Watunzi na Mazingira Yao 17

2.1.1 Walibora: Mwanariwaya 17

2.1.2 Habwe: Mwanariwaya 21

2.2 Muhtasari wa Riwaya Husika 22

(10)

2.2.1 Kidagaa Kimemwozea 22

2.2.2 Cheche za Moto 23

2.3 Hitimisho 24

Sura ya Tatu

Mchango wa Mwingilianomatini

Katika Kukuza Maudhui

3.0

Utangulizi 25

3.1 Matumizi ya Tanzu Kuendeleza Maudhui Katika Riwaya 25

3.1.1 Matumizi ya Ushairi na Nyimbo 26

3.1.1.1 Ushairi Kama Nyenzo ya Kuleta Mageuzi na Haki.. 27 3.1.1.2 Ushairi Kama Chombo cha Kuapishia Wanajamii 32

3.1.1.3 Ushairi Kama Chombo cha Kupitishia Hisia 33

3.1.1.4 Ushairi Kama Nyenzo ya Kukemea Maovu , 36

3.1.1.5 Ushairi Kama Chombo cha Kukuzia Uzalendo 36

3.1.2 Matumizi ya Methali 38

3.1.3 Matumizi ya Hotuba 40

3.1.3.1 Hotuba Kama Chombo cha Kudhihiririshia Ubarakala ~ .41 3.1.3.2 Hotuba Kama Chombo cha Kubaini Ukoloni Mamboleo na Utegemezi .43 3.1.3.3 Hotuba Kama Chombo cha Kubaini Urazini na Uzinduzi .45 3.1.3.4 Hotuba Kama Nyenzo ya Ujenzi wa Jamii Mpya .46 3.2 Matumizi ya Matini Kukuza Maudhui Katika Riwaya .48

3.2.1 Matumizi ya Barna 48

3.2.1.1 Barna Kama Chombo cha Kufichua Maovu .49

3.2.1.2 Barna Kama Chachu ya Uasi Katika Jamii 50

3.2.1.3 Barna Kama Chombo cha Kuleta Ukombozi 52

3.2.1.4 Barna Kama Chombo cha Kutolea Msamaha 53

3.2.1.5 Barua Kama Chombo cha Kuendelezea Dhuluma 54

3.2.1.6 Barna Kama Chombo cha Kuonyesha Utamaushi 56

3.2.2 Matumizi ya Taarifa za vyombo vya Habari 56

3.2.2.1 Vyombo vya Habari Kueneza Propaganda 56

3.2.2.2 Redio Kukuza Uzalendo 59

(11)

3.2.3 Matumizi ya Marejeleo Kukuza Maudhui Katika Riwaya 62 3.2.3.1 Marejeleo Kama Njia ya Kutolea Kemeo na Uzinduzi 63

3.2.3.2 Marejeleo Kama Njia ya Kufichua Unafiki 68

3.2.3.3 Marejeleo Kama Njia ya Kujitukuza 72

3.3 Hitimisho 74

Sura ya Nne

Mchango

wa Mwingilianomatini

Katika Kukuza Fani ya Riwaya

4.0 Utangulizi 75

4.1 Dhana ya Fani Katika Fasihi 75

4.1.1 Dhana ya Mtindo Katika Fasihi 76

4.1.1.1 Matumizi ya Ushairi Katika Riwaya 78

4.1.1.2 Matumizi ya Methali Katika Riwaya 80

4.1.1.3 Matumizi ya Hotuba Katika Riwaya 89

4.1.1.4 Matumizi ya Barua Katika Riwaya 90

4.1.1.5 Matumizi ya Matini za Vyombo vya Habari Katika_~iwaya 90

----

-4.1.1.6 Matumizi ya Marejeleo Katika Riwaya 91

4.2 Hitimisho 92

Sura ya Tano

Muhtasari,

Hitimisho na Mapendekezo

5.0 Utangulizi : 93

5.1 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti 93

5.1.1 Usuli wa Mada na Mbinu za Utafiti. 93

5.1.2 Watunzi na Mazingira Yao 94

5.1.3 Tanzu, Matini na Maudhui Katika Riwaya 94

5.1.4 Tanzu, Matini na Fani Katika Riwaya 95

5.2 Hitimisho - 96

5.3 Mapendekezo 96

Marejeleo 98

(12)

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

1.0

Usuli wa Mada ya Utafiti

Uchambuzi kuhusu historia ya riwaya ya Kiswahili uliofanywa na Senkoro (1983), Syambo na Mazrui (1992), Njogu na Chimerah (1999), King'ei (1999), na Wamitila (2003b) unaonyesha kuwa utanzu wa riwaya ulichipuka kutokana na tanzu za fasihi simulizi na umeendelea kukua kwa haraka sana na kudhihirisha mabadiliko makubwa kimtindo. Kadhalika, kwa kuwa ushairi ulikuwa umeshika sana hapo awali, riwaya ya Kiswahili imeendelea kuathiriwa na utanzu huu kwa kuhusisha vipande vya mashairi na nyimbo katika umbo lake. Kezilahabi (1983) anakubaliana na maoni haya anaposema:

Mtindo huu wa kuandika hadithi na kutumbukiza shairi hapa na pale unakubaliana na mtindo wa kusirnulia hadithi zetu za fasihi simulizi. Wapo waandishi wanaoamini kuwa mtindo huu ukiwekewa mkazo unaweza kuleta umbo jipya la riwaya yaKiswahili (Kezilahabi

1983:226).

Nao Syambo na Mazrui (1992) wanashadidia maoni haya kwa kusema kuwa: Na maandishi haya (ya riwaya) ni lazima yawe ya nathari, yaani ya lugha ya usimulizi wa moja kwa rnoja, ingawa hapa na pale katika riwaya tunaweza kupata vipande vya ushairi, wimbo au lugha ya mazungumzo (Syambo na Mazrui 1992:63).

(13)

nyingine. Hii ina maana kuwa hakuna matini iliyo huru. Kila matini inahusiana

na kutegemea mseto wa matini nyingine (Kristeva 1980).

Kutokana na maoni ya Alfaro (1996) na Heberer (2007), mwingilianomatini ni

dhana inayohusishwa na Usasaleo uliojitokeza katika miongo miwili ya

mwanzoni mwa kame ya ishirini. Ingawa istilahi yenyewe ilikuwa bado

kubuniwa, kazi za kimwingilianomatini zilikuwa zimeanza kushughuliwa na

wana-usasa kama T.S Eliot na David Jones. Wanaendelea kueleza kuwa istilahi hii ilibuniwa na Julia Kristeva mnamo mwaka wa 1966. Kristeva hakuibuni

kutoka katika ombwe tupu, bali ndiye aliyekuwa wa kwanza kuitumia katika

makala yake kuhusu Mikhail Mikhailovich Bakhtin, baada ya kusoma kazi zake katika Kirusi alipokuwa mwanafunzi huko Bulgaria kabla ya kuhamia

Ufaransa. Makala hizo zililenga kuziingiza kazi za Bakhtin nchini Ufaransa.

K wa msingi huu, istilahi ya mwingilianomatini ilitumika kwa mara ya kwanza kurejelea kile ambacho Bakhtin alikiita usemezano katika lugha (Holquist

1990). Kwa maoni ya Bakhtin, utanzu wa kifasihi wa pekee ulio na sifa za

kisemezano ni riwaya huku ushairi ukiwa na sifa za kimonolojia. Ni wazi kuwa

Kristeva ni mwathiriwa wa nadharia ya Bakhtin ya Usemezano. Kwa mujibu

wa Bakhtin (Angalia Alfaro 1996 na Heberer 2007), kazi za kisemezano zinaendelea kusemezana na kazi nyingine za fasihi na hata watunzi wengine.

Hivyo basi, fasihi ya kisemezano daima inawasiliana na kuathiriana na mseto

wa kazi nyingine za awali na za sasa.

Kadhalika, Kristeva (1980) aliathiriwa na nadharia ya Ferdinand Mongin de Saussure ya Semiotiki (1916) iliyojishughulisha na jinsi ishara

(14)

zinavyowasilisha maana katika matini. Nadharia hii inaangazia uashiriaji na

jinsi kazi za kifasihi zinavyowasiliana na wasomaji wake. Kutokana na msingi

huu, Kristeva alisisitiza kuwa matini daima zimo katika hali ya kuzalishwa na

wala hazijakamilika kwa matumizi. Kwa maoni yake, mawazo hayawasilishwi

kama bidhaa kamilifu, bali huwasilishwa kwa namna inayompa msomaji fursa

ya kufasiri maana kivyake. Anaonyesha j insi matini zinavyoweza kusukwa

kutokana na matini za awali. Pia anahoji kuwa watunzi hawatungi matini zao

kutoka katika mawazo yao. Badala yake, wanazitunga kutokana na matini za

awali. Anaendelea kushikilia kuwa matini si umbo moja huru, bali ni mseto wa

maumbo mbalimbali.

1.1 Suala la Utafiti

Utafiti huu ulichunguza matumizi ya mwingilianomatini katika riwaya ya

Kiswahili. Kimsingi, ulijikita katika matumizi ya tanzu za ushairi na nyimbo,

methali na hotuba; pamoja na matini ya barua, taarifa za vyombo vya habari na

marejeleo katika kuumba riwaya ya Kiswahili kimaudhui na kifani. Utafiti

ulilenga kudhihirisha mchango wa mwingilianornatini katika kuikuza riwaya

kimaudhui; na kisha kuonyesha mchango wa mwingilianomatini katika kukuza

fani ya riwaya. Katika kutekeleza haya, utafiti ulitumia riwaya mbili: Kidagaa

Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Moto (Habwe).

1.2 Malengo ya Utafiti Utafiti huu ulilenga;

(a) Kubainisha athari ya mazingira ya watunzi kwa riwaya zao za

(15)

katika kuendeleza riwaya kimaudhui.

(c) Kuonyesha jinsi tanzu na matini zilivyotumika katika kuikuza nwaya kifani.

1.3 Maswali ya Utafiti

Utafiti huu uliongozwa na maswali yafuatayo:

(a) Mazingira ya watunzi yana mchango gani katika nwaya zao za kimwingilianomatini?

(b) Tanzu na matini zilizotumika katika riwaya zinasaidia vipi katika kuendeleza maudhui?

(c) Tanzu na matini hizo zilitumika vipi kifani?

1

.

4

Sababu za Kuchagua Mada

Riwaya ya Kiswahili --.imeen~lea kukua na kudhihirisha matumizi y~ mwingilianomatini katika umbo lake na hivyo kuzidi kuwa changamano zaidi. Uchangamano huu unatatiza upokeaji na uelewekaji wa maudhui yanayowasilishwa katika riwaya, hasa ikizingatiwa kuwa riwaya hizi zinatumiwa katika mtaala wa elimu nchini. Kwa hivyo, ilibidi kufanya utafiti huu ili kurahisisha upokeaji na uelewekaji wa riwaya hizi, hasa kwa walimu na wanafunzi. Katika kutimiza hili,utafiti ulibainisha na kisha kuchanganua tanzu pamoja na matini zilizotumika katika kuiandika riwaya na pia kuonyesha nafasi ya tanzu na matini hizo katika kukuza maudhui na fani katika riwaya ya Kiswahili. Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Moto (Habwe) zilichaguliwa kwa sababu ni miongoni mwa kazi za hivi karibuni zinazodhihirisha matumizi ya mwingilianomatini. Kadhalika, riwaya hizi zimebeba matumizi ya tanzu za ushairi na nyimbo, methali na hotuba pamoja

(16)

na matini ya barua, taarifa za vyombo vya habari na marejeleo. Isitoshe, riwaya

hizi zinaonyesha namna riwaya ya Kiswahili ilivyokua na kupata umbo jipya.

Aidha, utafiti huu umeonyesha namna tanzu na matini zinavyoweza kuhusiana

na kutegemeana katika kuwasilisha ujumbe wa mwandishi.

1.5 Upeo na Mipaka ya Utafiti

Mwingilianomatini umetokea kuwa muhimu sana katika utunzi wa riwaya ya

Kiswahili. Kwa msingi huu, utafiti huu ulijikita katika kuchunguza matumizi

yake, hasa matumizi ya tanzu za ushairi na nyimbo, methali, hotuba na matini

ya barua, taarifa za vyombo vya habari pamoja na marejeleo katika riwaya

mbili: Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Mota (Habwe). Utafiti

huu umebainisha na kuchanganua kwa tafsili matumizi ya tanzu na matini hizo

katika kuumba riwaya na kisha kuchunguza nafasi ya tanzu na matini hizo

katika kukuza maudhui na fani katika riwaya. Utafiti huu haukujishughulisha

na vipengele vinginevyo katika riwaya hizi.

1.6 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada

Tafiti kadha zimefanywa kuhusu mwingilianomatini katika fasihi andishi.

Baadhi ya tafiti hizo ni zile zilizofanywa na Marete (1994), Kehinde (2003),

Wamitila (2003a), Babusa (2005), Wanyela (2007) na Habwe (2010). Katika

sehemu hii utafiti huu umeshughulikia tafiti zilizoelekea kulenga matumizi ya

mwingilianomatini katika fasihi.

Kwanza, utafiti ulioelekea kulenga matumizi ya mwingilianomatini katika

tamthilia ni ule wa Marete (1994) ambaye alishughulikia uchambuzi wa ujadi

(17)

katika tamthilia ya Kiswahili. Alijikita katika tamthilia mbili za Emmanuel Mbogo: Ngoma ya Ng'wanamalundi na Morani. Katika uchunguzi wake, alichanganua na kuainisha uamilifu wa ujadi katika tamthilia ya Kiswahili. Vipengele vya kijadi alivyoshughulikia ni matumizi ya nyimbo na ngoma, utongoaji wa majigambo, urithi wa tamathali za lugha za kijadi, uchawi na imani za kishirikina pamoja na asasi za jando. Mtafiti huyu alionyesha kuwa matumizi ya ujadi katika tamthilia hizi yametokana na athari ya mazingira ya kitamaduni yaliyomlea mtunzi. Amedhihirisha kuwa vipengele vya kijadi vimetumika kutekeleza dhima mbalimbali. Hizi ni pamoja na kukuza na kuendeleza utamaduni wa Kiafrika, kushajiisha, kutumainisha, kuzindua na kuhamasisha umma; kuleta mageuzi katika jamii na pia kuzipa tamthilia husika uasili. Kadhalika, mtunzi alitumia ujadi ili kufumba ujumbe uliowakosoa viongozi vikali na hivyo kuweza kukwepa rungu la dola. Katika uchunguzi huu, Marete (1994), "akiongozwa na Nadharia ya Kimarx ya Sanaa na Fasihi kama ilivyoendelezwa na Lenin, alijikita katika matumizi ya ujadi katika tamthilia. Hivyo basi iliafiki kuegemeza utafiti huu kwenye matumizi ya mwingilianomatini katika riwaya ya Kiswahili ili kuendeleza utafiti zaidi katika utanzu huu, hasa kwa kutumia Nadharia ya Mwingilianomatini.

Mtafiti mwingine aliyeshughulikia mwingilianomatini katika tamthilia m Wanyela (2007) aliyechunguza matumizi ya ushairi katika tamthilia na kubainisha namna ushairi unavyosaidia kusawiri maudhui yaliyonuiwa na mwandishi wa tamthilia. Alionyesha kuwa matumizi ya lugha ya kishairi yanajitokeza sana katika fasihi za kiulimwengu na ni msingi mkubwa wa ufanisi wa ulumbi wa kazi nyingi. Alidhihirisha kuwa utumiaji wa ushairi

(18)

huchangia ufanisi wa utanzu wa tamthilia kwa kusaidia usawiri wa ujumbe kwa mujibu wa lengo la msanii. Alihoji kuwa, watunzi wengi wa tamthilia hutumia ushairi ili kufanikisha uwasilishaji wa maudhui na ujumbe. Kadhalika, alieleza kuwa ushairi hutumiwa ili kuendeleza mtindo na kuwakuza wahusika katika tamthilia yaKiswahili. Katika uchunguzi huu, Wanyela (2007)

alizingatia tamthilia tatu za Kiswahili: Kilio Cha Haki (Mazrui), Mama Ee (Mwachofi) na Amezidi (Mohamed). Kadhalika, alidhihirisha kuwa ushairi hutekeleza majukumu mbalimbali katika jamii. Haya ni pamoja na

kuirekebisha, kuiongoza, kuielimisha na kuizindua jamii kisiasa na kidini.

Mwisho, alipendekeza kuwa utafiti ufanywe juu ya matumizi ya mbinu za lugha katika ushairi na jinsi zinavyotumika kuendeleza riwaya ya Kiswahili.

Hivyo basi, utafiti huu uliitikia wito huu, na kisha kuipanua mada hiyo kwa

kuchunguza matumizi ya tanzu za ushairi na nyimbo, methali na hotuba pamoja na matini ya barua, taarifa za vyombo vya habari na marejeleo katika

kuikuza riwaya ya Kiswahili. Pia, uchunguzi huu ulitumia Nadharia ya Mwingilianomatini katika kuonyesha matumizi ya tanzu hizi katika riwaya,

-tofauti na Nadharia ya Utanzu iliyotumiwa na Wanyela (2007) katika

uchunguzi wake.

Nao utafiti kuhusu mwigilianomatini katika riwaya ulifanywa na Wamitila

(2003a) aliyelinganisha riwaya mbili za Nagona na Mzingile (Kezilahabi), na Pedro Paroma (Juan Rulfo). Hapa Wamitila (2003a) alihoji kuwa

(19)

kuziandika hizi riwaya zake. Kwa hivyo, taathira ya Juan Rulfo inadhihirika

katika riwaya za Kezilahabi. Katika riwaya zote tatu kuna taswira na mbinu

nyingine ambazo zimetumika ili kuunganisha vipengele anuai katika mseto

mmoja imara. Baadhi ya taswira zilizotumika ni pamoja na uharibifu wa

kimazingira, magofu na mahame ya nyumba, mabonde yenye giza, mwanga

hafifu, ndege na wanyama wenye mikosi na motifu ya safari. Kadhalika,

riwaya hizi zinavunja mipaka ya wakati na ya kihistoria katika usimulizi wake

na kumsawiri binadamu kama kiumbe mlaanifu na anayeteseka. Pia alionyesha

mfanano wa kimaudhui na kifani baina ya riwaya za hawa watunzi wawili.

Utafiti huu, tofauti na ule wa Wamitila (2003a), ulionyesha namna tanzu na

matini mbalimbali zilivyochangia katika kurutubisha riwaya za Kiswahili

kimaudhui na kimtindo. Kwa hivyo, utafiti huu haukulinganisha na kulinganua

riwaya teule kwa misingi ya matumizi ya mwingilianomatini.

Kadhalika, Kehinde (2003) alishughulikia matumizi ya mwingilianomatini

katika riwaya. Katika kutathmini matumizi ya mwingilianomatini katika riwaya

za Kiafrika, yeye alimwona Chinua Achebe kama mwanariwaya aliyeongozwa

na Nadharia ya Mwingilianomatini katika riwaya zake mbili: Things Fall

Apart na Arrow of God. Aliendelea kuhoj i kuwa Achebe alitumia misingi ya

tamaduni za Kiafrika kusahihisha imani na mielekeo potovu ya Wazungu

kuhusu Afrika na Waafrika. Alifanya hivi baada ya kusoma riwaya zifuatazo:

Heart of Darkness (Joseph Conrad), Mister Johnson (Joyce Cary) na King

Solomon's Mines (fL- Rider Haggard) zilizomdunisha na kumuumbua mtu

mweusi. Hapa, ni wazi kuwa Achebe anatukuza utu na utamaduni wa Mwafrika

katika Things Fall Apart kwa kuchota maudhui na fani kutoka katika fasihi

(20)

simulizi ya Mwafrika. Hapa, mwingilianomatini ulitumiwa kama nyenzo ya

kumkornboa Mwafrika kutokana na maonevu na mielekeo hasi ya Wazungu.

Kadhalika, riwaya hii ya Achebe inadhihirisha mwingilianomatini kwa kuwa

ilipata kichwa chake Things Fall Apart kutokana na shairi la William Butler

Yeats (1865-1939) liitwalo The Second Coming. Kehinde (2003) aliendelea kudhihirisha mwingilianomatini katika A Grain of Wheat (Ngugi wa

Thiong'o), The Famished Road (Ben Okri) na So Long a Letter (Mariama Ba)

miongoni mwa riwaya nyingine za Kiafrika. Mwingilianomatini katika riwaya

hizi unadhihirika katika maudhui na fani. Hata hivyo, tathmini hii

haikushughulikia riwaya za Kiswahili. Kwa hivyo, utafiti huu ulijikita katika

kuchunguza matumizi ya mwingilianomatini katika kuikuza riwaya ya

Kiswahili kimaudhui na kimtindo. Ulizingatia riwaya za Kiswahili pekee na

kuchunguza matumizi ya tanzu za ushairi na nyimbo, methali na hotuba pamoja

na matini ya barua, taarifa za vyombo vya habari na marejeleo katika

kuziandika riwaya hizo.

Babusa (2005) alishughulikia uainishaji wa mashairi ya Kiswahili kiwakati.

Alieleza mabadiliko ya tanzu za ushairi ambayo yamesababisha kubadilika kwa

uainishaji wa ushairi wa Kiswahili. Alidai kuwa yalikuwepo matapo mawili ya

mashairi kabla ya kuja kwa maandishi. Haya ni yale yaliyofuata arudhi na

yasiyo na arudhi. Mashairi katika muhula huu yaliainishwa kwa kutumia

kigezo cha maudhui. Kuja kwa hati za Kiarabu kuliambatana na kuzuka na

kisha kukita mizizi kwa mashairi ya-arudhi yaliyoainishwa kwa kutumia kigezo cha muundo. Kuja kwa hati za Kirumi nako kuliambatana na mashairi

(21)

Kiswahili liwe na urari wa vina na mizani. Ushairi huu pia uliainishwa kwa

kutumia kigezo cha muundo. Kuzuka kwa mashairi huru kulileta mgogoro na

hivyo kuleta mwainisho mpya wa mashairi haya. Mtafiti huyu alijikita katika

kuzuka kwa vitanzu zaidi katika utanzu wa ushairi pekee. Hakujishughulisha na

uenevu wa vitanzu vya ushairi katika tanzu nyingine kama riwaya na tamthilia.

Utafiti huu ulilenga kuchunguza matumizi ya tanzu nyingine hasa ushairi na

nyimbo, methali na hotuba pamoja na matini ya barua, taarifa za vyombo vya

habari na marejeleo katika kusuka riwaya ya Kiswahili.

Mwisho, kwa kutumia data iliyokusanywa kutoka miji ya Nairobi na Mombasa,

Habwe (2010) alichanganua matumizi ya dayalojia katika hotuba za kisiasa

nchini Kenya. Alihoji kuwa mbinu hii ni muhimu katika kuishirikisha hadhira

katika uwasilishaji wa hotuba. Aliendelea kuhoji kuwa mbinu hii hutumika

kupima umaarufu wa msemaj i na pia kuishinikiza hadhira kuafikiana na

msemaji. Vilevile, alisema kuwa, hadhira nayo hutumia mbinu hii ili kuelekeza

mkondo wa mada ya hotuba. Katika hali kama hii, maswali ya kawaida na yale

ya balagha hutumika kukuza na kuendeleza dayalojia katika mchakato wa

mawasiliano ambapo msemaji na hadhira yake wana majukumu sawa ambayo

ni kusikiliza na kusema. Mtafiti huyu alijishughulisha na kitanzu cha dayalojia

pekee katika hotuba za kisiasa. Hakushughulikia vitanzu vingine

vinavyodhihirika katika hotuba za kisiasa. Vitanzu hivi ni pamoja na

vitendawili, nyimbo na kejeli miongoni mwa vingine. Kwa msingi huu, ilibidi

kuendeleza utafiti huu kwa kushughulikia matumizi ya tanzu na matini

mbalimbali katika riwaya ya Kiswahili.

(22)

1.7 Nadharia ya Utafiti

Utafiti huu uliongozwa naNadharia ya Mwingilianomatini ambayo ina misingi yake katika Nadharia ya Usemezano iIiyoasisiwa na Mikhail Mikhailovich Bakhtin (1895-1975) aliyedai kuwa matini ya kisemezano inaendeleza usemezano na matini nyingine za fasihi na hata watunzi. Matini hiyo inajibu,

inasahihisha, inanyamazisha na kuendeleza matini za awali. Kadhalika, inaarifu

na daima inaarifiwa na matini zilizotangulia. Fasihi ya kisemezano

inawasiliana na fasihi nyinginezo. Hivyo basi matini za mwanzo na za sasa

zinaendelea kuathiriana.

Mishra (2012) anashadidia haya kwa kusema kuwa waasisi wa Nadharia ya

Mwingilianomatini ni Ferdinand de Saussure, C. S.Pierce, T. S. Eliot naM. M.

Bakhtin. Baadaye iliendelezwa na Julia Kristeva, Roland Barthes, Harold - ~--Bloom na Gerald Genette. Istilahi yamwingilianomatini ilitumiwa kwa mara ya

kwanza na Julia Kristeva mnamo mwaka wa 1966 katika makala zake mbili:

TheBounded Textna Word, Dialogue and Novel ambazo baadaye zilikusanywa

katika Kristeva (1980) ambapo anahoji kuwa waandishi hawatungi matini zao

kutoka katika mawazo yao, bali kutokana na matini za awali. Anaendelea

kusema kuwa matini yoyote ile imefumwa kama mseto wa unukuzi, na matini

yoyote ile inahusisha na kugeuza matini nyingine. Katika matini husika, kauli kadha kutoka matini nyingine, zinahusiana na kuathiriana (Clayton na

Rothstein 1991). Kwahivyo, Kristeva aliamini kuwa mwingilianomatini ni hali:

ambapo matini inadhihirisha usomaji wa mseto wa matini za awali, hivyo basi

(23)

Kristeva (1980) pamoja na wanamwingilianomatini wengine kama Bloom

(1994) na Barthes (2002) wanaamini kuwa msomaji wa pekee ni mwandishi

asomaye matini nyingine, hali inayopelekea matini kujisoma yenyewe huku

ikijiandika yenyewe. Hivyo basi, mwingilianomatini ni usukaji wa maana ya

matini kutokana na matini nyingine. Unaweza kuhusisha mtunzi kuazima na

kugeuza matini ya awali au kwa msomaji kurejelea matini mojawapo katika

kusoma nyingine. Nadharia hii inakumbusha kuwa kila matini inahusiana na

matini nyinginezo. Matini zinafumwa na matini nyingine kwa namna nyingi.

Wamitila (2003b) anaelekea kukubaliana na maelezo haya anaposema kuwa

mwingilianomatini ni dhana inayotumiwa kuelezea kuwepo kwa sifa

mbalimbali za matini moja au zaidi katika kazi fulani ya kifasihi. Nadharia hii

huchukulia kuwa kila kazi ya kifasihi inahusiana na kazi iliyoandikwa kabla

-kwa namna moja au nyingine. Abram (1981) anaongeza kwa kusema kuwa

mwingilianomatini unadhihirisha njia mbalimbali ambamo matini ya kifasihi

inaweza kujidhihirisha, au kujihusisha na matini nyingine kiwaziwazi, kwa kunukuu, kudoridoa, kutaja, kurejelea au kusilimisha sifa za matini za awali; au

kuwa katika mkumbo mmoja wa kifasihi na kikaida.

Eagleton (1983) anasema kuwa kazi zote za fasihi huandikwa upya kwa

kiwango fulani, ingawa bila ya jamii husika kufahamu. Kwa hivyo anasisitiza

kuwa hakuna usomaji wa matini ambao si utunzi mpya. Hivyo basi,

mwingilianomatini unaweza kuelezwa kama upanuzi wa mawazo

yanayofahamika au kama dhana mpya kabisa badala ya dhana chakavu ya

uathirifu. Mwingilianomatini ni mpana zaidi kuliko dhana ya uathirifu

iliyomzingatia mtunzi pekee. Ni mpana zaidi kuliko uathirifu wa mtunzi

(24)

mmoja kwa mwingine. Maisha ya mtunzi pekee hayawezi kumpa msomaji au hadhira msingi imara wa maana ya matini aliyo nayo msomaji. Nadharia hii ya mwingilianomatini inachukulia kuwa maana ya matini haipatikani katika matini yenyewe, bali inajengwa na msomaji katika matini husika na mseto wa matini nyingine zinazotajwa na kurejelewa katika huo usomaj i.Basi, riwaya ni mseto wa matini nyingi. Hii ni kwa kuwa zinarejelea, ndani mwazo, tanzu nyingine. Zinanukuu tanzu nyinginezo katika hali moja au nyingine (Coyle na wengine 1990). Kwa mujibu wa Wamitila (2002: 153), Bakhtin anaamini kuwa utanzu wa riwaya una uwezo wa kujumulisha wasifu wa tanzu nyingine lakini ukabakia na sifa zake kama utanzu. Kwa mfano, riwaya inaweza kuhusisha mazungumzo na ushairi na bado ikabakia kuwa riwaya.

Mihimili mikuu ifuatayo ya nadharia hii ilitumika katika utafiti huu:

(a) Waandishi hutunga rnatini-zao kutokana na matini za awali na wala++ ----hawaziandiki kutoka katika mawazo yao. Kutokana na hili, matini

zinahusisha kauli na tanzu kutokana na matini nyingine za awali na za sasa. Hivyo basi, matini zinaingiliana na kuathiriana pakubwa.

(b) Maana ya matini haipatikani katika matini yenyewe, bali inajengwa na msomaji katika matini husika na mseto wa matini nyingine zinazotajwa na kurejelewa katika huo usomaji.

(c) Mawasiliano baina ya mtunzi na msomaji huambatana na mwingiliano uliopo baina ya maneno na namna yalivyokuwa katika matini za awali.

(25)

Matini yoyote ile hufumwa kama mseto wa unukuzi; na hivyo, kila matini inahusisha na kugeuza matini nyingine.

(d) Matini ya kifasihi inaweza kujidhihirisha, au kujihusisha na matini

nyingine kiwaziwazi, kwa kunukuu, kudondoa, kutaja, kurejelea au

kusilimisha sifa za matini za awali; au kuwa katika mkumbo mmoja

wa kifasihi.

(e) Matini yoyote ile inahusiana na muktadha wa kitamaduni au kijamii

ulioizalisha na haiwezi kutenganishwa nao. Kwa hivyo, matini zote

zimesheheni imani na mawazo yanayotokana na miktadha hii.

Katika utafiti huu, mihimili yote mitano ilitumiwa. Mhimili wa kwanza (a)

ulitumiwa kuonyeshanamna tanzu au matini zinavyoingiliana na kuathiriana. - - -Nayo mihimili mingine mitatu: (b), (c), na (d) ilitumiwa kupata maana ya

matini kutokana na matini zilizotajwa, rejelewa, nukuliwa, dondolewa na kusilimishwa 'katika riwaya zilizoteuliwa. Mhimili wa tano (e) ulitumiwa

kuonyesha mahusiano ya matini na muktadha wa kitamaduni au kijamii

ulioizalisha matini husika.

1.8 Mbinu za Utafiti

Katika kuelezea viwango vya mwingilianomatini, Bazerman (2011) na Mishra

(2012) wanasema kuwa mwingilianomatini unaweza kudhihirika kupitia njia

mbalimbali. Hizi ni pamoja na unukuzi wa moja kwa moja wa matini au tanzu

nyingine; unukuzi usio wa moja kwa moja ambapo mtunzi anaiwasilisha upya

maana kutoka matini ya awali; na kwa kutaja na kurejelea vyanzo vya habari

(26)

anazowasilisha mtunzi katika matini yake. Kadhalika, wanaendelea kueleza

kuwa mwingilianomatini unaweza kudhihirika kupitia matumizi ya lugha,

kauli, semi na maneno yanayohusishwa na watunzi au tanzu maalumu.

Viwango hivi vyote vinadhihirika katika riwaya ya Kiswahili ambayo inabeba

tanzu za fasihi simulizi, unukuzi, marejeleo, hotuba, barua na taarifa za

vyombo vya habari miongoni mwa tanzu na matini nyingine katika umbo lake.

Utafiti huu ulijikita maktabani na kuchunguza matumizi ya mwingilianomatini

katika riwaya teule. Vitabu, majarida, makala na tasnifu kuhusu mada ya utafiti

zilisomwa na kuchanganuliwa kwa tafsili. Hili liliwezesha kupatikana kwa

data mwafaka kwa ajili ya utafiti huu na pia kubainisha pengo katika utafiti wa

awali. Utafiti ulifanyika katika maktaba za vyuo vikuu vya Kenyatta, Nairobi

na MoL Pia tovuti mbalimbali zilitumika katika utafiti huu. Mbinu hii ilikuwa

mwafaka katika kupata data zilizoendana na malengo ya utafiti na mihimili ya

nadharia ya utafiti. Kadhalika, vitabu vya fasihi vilivyotumika katika utafiti

huu: Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Moto (Habwe) vilisomwa

na kuchanganuliwa ili kupata data za utafiti. Makala katika mtandao kuhusu

Nadharia ya Mwingilianomatini pia zilisomwa ili kujenga msingi imara wa

kinadharia kwa utafiti wetu. Mihimili ya nadharia hii ilibainishwa na kutumiwa

katika kutafuta na kuchanganua data zilizokusanywa.

1.8.1 Ukusanyaji wa Data

Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua riwaya mbili

zilizoteuliwa: Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Moto

(Habwe). Vitabu hivi vilisomwa kwa kina na kudondoa vipande vya mashairi

(27)

ili kupata data zinazotosheleza mahitaj i ya utafiti huu. Kadhalika, vitabu,

majarida, makala na tasnifu zilizolenga mada ya utafiti zilisomwa ili kupata

data kwa ajili ya utafiti huu.

1.8.2 Uteuzi wa Sampuli

Uteuzi wa sampuli ulifanywa kimakusudi. Riwaya mahsusi za Kiswahili

ziliteuliwa kwa kuwa ni miongoni mwa kazi za hivi karibuni zinazodhihirisha

matumizi ya mwingilianomatini. Pia, kutokana na upekuzi wa awali

zimesheheni matumizi ya tanzu za ushairi na nyimbo, methali na hotuba

pamoja na matini ya barua, taarifa za vyombo vya habari na marejeleo. Riwaya

hizo ni Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Mota (Habwe) .

.Malengo ya utafiti na mihimili ya Nadharia ya Mwingilianomatini iliongoza

katika kuchunguza matumizi ya mwingilianomatini katika riwaya hizi. Uteuzi

huu ulisaidia katika kuonyesha jinsi watunzi walivyotumia mwingilianomatini

katika kukuza maudhui na fani katika riwaya zao.

1.8.3 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Data

Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti.

Tanzu na matini zilizotumiwa katika riwaya zilichanganuliwa na kubainishwa.

Kadhalika, utafiti ulidhihirisha namna tanzu na matini hizo zilivyotumiwa kuendeleza maudhui, kisha ukaonyesha upekee wa kimtindo unaotokana na

matumizi ya tanzu na matini hizo. Uchanganuzi huu uliongozwa na mihimili ya

nadharia ya mwingilianomatini. Data zilizokusanywa na kuchanganuliwa

ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo katika tasnifu,

(28)

SURA YA

PILI

ATHARI YA MAZINGIRA YA WATUNZI KWA

RIWAYA ZAO ZA KIMWINGILIANOMATINI

2.0 Utanguiizi

Katika sura hii, utafiti umebainisha kuwa mazingira ya mtunzi yana mchango

mkubwa katika kutunga kazi za kimwingilianomatini. Pia umetoa muhtasari wa

historia ya Ken Walibora na John Habwe ambao ni watunzi wa riwaya

zinazounda msingi wa utafiti huu na pia kuonyesha mchango wao katika fasihi

kwa jumla, pamoja na kubainisha athari ya mazingira yaliyowalea kwa utunzi

wao. Aidha, umetoa muhtasari wa riwaya za Kidagaa Kimemwozea (Walibora)

na Cheche za Moto (Habwe) ambazo zimeshughulikiwa katika utafiti huu.

2.1 Watunzi na Mazingira Yao

Waandishi wa riwaya za Cheq]zf!.-.!J2Mota (Habwe) na Kidagaa Kimemwozea

(Walibora) hawakutunga katika ombwe tupu, ila walizitunga kutokana na

mazingira yaliyowalea. Walichota rnalighafi yao kutoka katika matini

rnbalirnbali za kitarnaduni, kijarnii na kisiasa katika rnazingira hayo. Kwa

hivyo, kazi zao zinaingiliana na kuathiriana na mazingira walimokulia na

kuishi. Athari hii inadhihirika katika riwaya hizi rnbili.

2.1.1 Walibora: Mwanariwaya

Ken Walibora ni miongoni mwa waandishi rnaarufu sana wa riwaya kutoka

Kenya. Yeye ni mzaliwa ~a rnagharibi rnwa Kenya. Jina lake halisi ni Kennedy

Waliaula. Walibora ni lakabu yake aliyoiunda baada ya kuligawa jina lake

(29)

maana ya bora. Hivyo, alichukua kiungo cha kwanza chajina lake,ambacho ni

Wali na kukiunganisha na bora, kisawe cha aula na hivyo kuliunda jina

Walibora (Kuloba 1999 na Bertoncini 2007).

Walibora alizaliwa tare he 6/1/1965, maeneo ya Trans Nzoia (Kitale) na kukulia

huko. Alisoma katika Shule ya Msingi ya St. Joseph's (Kitale) alikofanyia

mtihani wa Darasa la Saba (C.P.E) mwaka wa 1978. Kadhalika, alisoma katika

Shule ya Upili ya Teremi (Bungoma), Suwerwa (Trans Nzoia) na kisha

Olkejuado (Kajiado) alikofanyia mtihani wa Kidato cha Nne (K.C.E) mwaka

wa 1982. Kisha, alijiunga na Shule ya Upili ya Koelel (Gilgil) na kuufanya

mtihani wa Kidato cha Sita (K.A.C.E) mwaka wa 1984.

Baadaye alifunza Kiswahili na Kiingereza katika Shule ya Upili ya Sitatunga

(Trans Nzoia) baina-ya -1985 na-1986. Kati ya 1986 na 1988 alikuwa katika"

Taasisi ya Utawala ya Kenya (Kenya Institute of Adminstration) alikosomea

Masuala ya Maendeleo ya Jamii. Alianza kuchangia makala kama mwandishi

huria kwenye magazeti na pia kutuma habari za michezo katika Sauti ya Kenya

wakati huo akiwa katika taasisi hii. Baada ya mafunzo yake alikuwa Afisa

Probesheni (Probation Officer)katika Idara ya Magereza, Wizaraya Mamboya

Ndani na Turathi za Kitaifa baina ya 1988 na 1996. Alifanya kazi hii katika

sehemu mbalimbali nchini zikiwemo Nairobi, Nakuru na Kitale. Ni wakati huu

alipoitunga riwaya yake ya kwanza yaSiku Njema. Hata hivyo, matamanio yake

yalikuwa katika taaluma ya uanahabari.

(30)

Mnamo mwaka 1996 alijiunga na Shirika la Utangazaji la Kenya (K.B.C) alikofanya kazi kama msomaji wa habari redioni, mhariri na mtafsiri wa habari hadi mwaka wa 1999. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi akiwa K.B.C na kuhitimu na Shahada ya Kwanza (B.A) katika Fasihi na Kiswahili. Baadaye alihamia Nation Media Group (NMG) kama msomaji wa habari katika NTV na Nation FM kati ya 1999 na 2004. Kufikia wakati huu, Walibora alikuwa ametokea kuwa mwanahabari maarufu sana wa redio na runinga nchini. Alipohitimu na Shahada ya Kwanza kwa Sifa Zilizotukuka (First Class Honours) mnamo 2004, alielekea katika Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani alikopata shahada mbili za Uzamili na pia ile ya Uzamifu mwaka wa 2009. Kisha alihamia katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madson (Marekani), alikofunza hadi Mei, 2013 aliporejea nchini na kisha kujiunga tena na NMG kama Meneja wa Ubora wa Kiswahili (Group Quality Manager, Kiswahili Media), ambapo baadhi ya vyombo anavyosimamia ni QTV, QFM, Taifa Leo, Mwananchi, Mwanaspoti na Tovuti ya Swahilihub.

Kama mwanariwaya, Walibora ametunga riwaya ya Siku Njema (1996), Kufa Kuzikana (2003), Ndoto ya Almasi (2007) na Kidagaa Kimemwozea (2012). Kadhalika, ametunga novella ya Innocence Long Lost (2005) na Upande Mwingine (2010). Mbali na riwaya, pia ameandika vitabu vya wasomaji chipukizi ambavyo ni pamoja na Ndoto ya Amerika (2001) na Mtu wa Mvua

(2004 miongoni mwa vingine vingi.

(31)

Baadhi yadiwani hizo niDamu Nyeusi na Hadithi Nyingine (2007) naKiti cha

Moyoni na Hadithi Nyingine (2008). Aidha, Walibora ametunga tamthilia ya Ahsante ya Punda (2009) na Mbaya Wetu (2014). Tawasifu yake inayoitwa Nasikia Sauti ya Mama imetoka mitamboni hivi punde. Katika ushairi vitabu vyake nipamoja naDiwani ya Kame (2005) na Waja Leo: Diwani ya Mashairi (2012).

Inavyodhihirika hapa ni kuwa, mwanariwaya huyu ametanda katika tanzu zote

za fasihi andishi (riwaya, hadithi fupi, tamthilia na ushairi). Pia ameandika makala nyingi katika majarida ya kitaaluma pamoja na vitabu vya kiada. Vitabu vyake vinatumika katika mtaala wa elimu ndani na nje ya nchi. Yeye mwenyewe amekiri kuwa kariha ya utunzi na ubunifu wake ilichochewa na kuhimizwa na mamake mzazi Ruth Nasambu Makali, nyanyake Sara Kusimba, babake pamoja na walimu wake (Kuloba 1999, Walibora 2013 na 2014).

Masuala ambayo Walibora (2012) ameyashughulikia yametokana na matini mbalimbali zinazopatikana katika mazingira yake. Kwa mfano, baadhi ya majina ya wahusika wake yametokana na matini alizopata kusoma. Hususan, katika Kidagaa Kimemwozea (2012), kuna wahusika kama Mtemi Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu ambao wametokana na wahusika katika Kusadikika (S. Robert). Vilevile, kuna Dora naZuhura ambao wanahusiana sana wahusika wa S.A.Mohamed katika Utengano.

Aidha, Walibora (2012) amekitohoa kisa cha Lord Egerton, anayehusishwa na Chuo Kikuu cha Egerton na kukisimulia kama kisa cha Major Noon

(32)

(Majununi). Rata masuala ya unyakuzi wa mashamba ya umma anayoshughulikia yamekithiri katika mazingira alimokulia. Kadhalika, athari ya maisha yake ya awali kama mwanafunzi na pia mwalimu inadhihirika kupitia kisa cha Fao kumringa mwanafunzi wake pamoja na wizi wa mitihani anaohusishwa nao. Isitoshe, athari ya kazi yake kama afisa probesheni na mwanahabari inabainika kupitia kisa cha Amani, Imani na Matuko Weye

kutiwa kizuizini na wakati huo matangazo ya mpira baina ya timu ya Songoa FC na Meza Wembe yakitokea kwa njia ya redio. Haya yanathibitisha kuwa utunzi wake umetokana na matini anuai katika mazingira yake.

2.1.2 Habwe: Mwanariwaya

John Hamu Habwe ni mmoja wa watunzi ambao wamechangia sana ukuaji wa utanzu wa riwaya ya Kiswahili nchini Kenya. Mtunzi huyu, mbali na kufundisha katika shule za upili, amefunza katika vyuo vikuu hapa nchini na pia nje ya nchi kwa muda mrefu sana. Alipata shahada yake ya kwanza (B.A) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mnamo 1987. Baadaye alipata shahada ya Uzamili (M.A) katika Kiswahili mwaka wa 1989 na kisha shahada ya Uzamifu (Ph.D) katika Isimu kutoka chuo hicho hicho cha Nairobi mnamo 1999. Baadhi ya riwaya alizotunga ni pamoja na Maumbile si Huja (1995), Maisha Kitendawili (2000), Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008) na Fumbo la Maisha (2009). Mbali na kutunga riwaya hizi, Habwe pia ametunga hadithi fupi mbalimbali zikiwemo Pendo la Heba katika Pendo la Heba na Hadithi

-Nyingine (1995), Walicheka-Kicheko katika Mwenda Wazimu na Hadithi

Nyingine (2000) na Mkimbizi katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi

(33)

lsitoshe, Habwe ameandika vitabu vya wasomaji chipukizi vikiwemo Sofia

Mzimuni (2006), Ayubu Mashakani (2007), na Safina na Kima wa Ajabu

(2007). Mbali na Habwe kuchangia sana ukuaji wa riwaya ya Kiswahili,

ameandika vitabu vya kitaaluma pamoja na makala nyingi katika majarida ya

kitaaluma.

Kadhalika, Habwe (2008) ametunga riwaya yake kutokana na tajiriba ya

maisha yake. Yeye alisoma katika Chuo Kikuu cha Nairobi wakati ambapo

wahadhiri wengi walikuwa wakihangaishwa na kudhulumiwa na vyombo vya

dola kutokana mihadhara waliyotoa. Hawa walikuwa pamoja na Prof. Ngugi

wa Thiong'o, Prof. Micere Mugo na Prof. Alamin Mazrui miongoni mwa

wengine. Dhuluma hizi zilisababisha wahadhiri wengi kutiwa kizuizini na

wengine kuwalazimika kuenda uhamishoni. Pia alishuhudia mauaji ya viongozi wa kisiasa pamoja na udikteta na dhuluma za serikali ya chama kimoja nchini.

Kwa hivyo, amechota mambo haya yote na kuyatumia kama malighafi ya

riwaya yake.

2.2 Muhtasari wa Riwaya Husika

2.2.1 Kidagaa Kimemwozea

Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea (Walibora) inamhusu Mtemi Nasaba Bora

aliyetawala eneo laSokomoko katika nchi ya Tomoko kwa udhalimu mkubwa.

Mtemi huyu alijiona kuwa bora zaidi kuliko wananchi aliowatawala kwa

mabavu kwa sababu alitoka katika nasaba bora kuwaliko. Alijilimbikizia mali

kwa kunyakua mashamba ya watu na hata kuwaiba mabinti na wake zao.

(34)

Aliwatia watu jela bila sababu na hata kuwaua wengine ili achukue mali yao.

Aliwatendea watu maonevu ya kila aina. Hata hivyo, wakati wake ulifika

mambo yalipomharibikia na akaondolewa madarakani na wananchi

waliongozwa na Amani na Madhubuti (mwanawe). Maasi dhidi ya utawala

wake yalianzia katika aila yake yakiongozwa na Madhubuti. Mali yote

aliyonyakua ilirejeshewa wenyewe. Alijutia makosa yake na kisha kujiua.

Uongozi mpya ulianzishwa chini ya Mtemi mpya na wananchi nao walijiwekea

msimamo wa kutokubali dhuluma tena. Riwaya hii imesheheni maudhui mengi

yakiwemo udhalimu, ufisadi, usaliti, ubinafsi, ukoloni na ukoloni mamboleo,

mapinduzi na ujenzi wa jamii mpya.

2.2.2 Cheche za Moto

Riwaya ya Cheche za Moto (Habwe) inafichua maovu yaliyokithiri katika nchi za Kiafrika. Inaonyesha uongozi mbaya uliozidi barani Afrika pamoja na

maonevu wanayofanyiwa wasomi. Wasomi wanahangaishwa na kudhulimiwa

katika vyuo vikuu. Uhuru wa kiusomi haupo katika vyuo vya Kiafrika. Prof.

Mule ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu ananyanyaswa kwa kutuhumiwa

kufundisha vijana mambo yanayosemekana ni ya kuharibu vichwa (fasihi).

Askari walivamia makazi yake na kumpiga vibaya sana. Pia walimnajisi

mkewe na kisha kumuua kwa kumpiga risasi. Isitoshe, alifukuzwa kazi chuoni

kwa kuonekana kuwa hasidi wa maendeleo kwa namna alivyohakiki serikaliya

usosholisti. Wasomi vyuoni walihangaishwa na kunaswa na polisi kutokana na

mihadhara waliyotoa na kupelekwa Dhiki House kuteswa. Wengine walitiwa

kizuizini na hata kuuawa kinyama. Kuna wale waliotoroka nchi zao ili

(35)

Kadhalika, viongozi wanawamaliza walewanaowaona kuwa tisho kwautawala

wao. Mauaji ya kisiasa yanatokea kila mara hivi kwamba yeyote anayeshukiwa

kwa lolote hupotea na baadaye mwili wake kupatikana mtoni, au hata

usionekane kabisa. Udikteta unaoendeshwa na chama kimoja unaendeleza

dhuluma na kuzidishia wananchi umaskini na utumwa. Isitoshe, ufisadi na

uporaj i wa mali ya umma, utabaka, ufuska na utovu wa maadili, ukabila na

ubaguzi, pamoja na utegemezi na ukoloni mamboleo vimekithiri katika nchi za

Kiafrika. Hata hivyo, wananchi walichoka na kufanya mapinduzi yaliyolenga

kuleta nafuu maishani mwao.

2.3 Hitimisho

Sura hii imetoa mchango wa mazingira ya watunzi kwa kazi zao za

kimwingilianomatini na kuonyesha kuwa watunzi hawatungi katika ombwe

- ~fiipii bali kutokana na mazingira yao. Pia, imetoa muhtasari wa historia ya

watunzi wawili ambao riwaya zao zimeshughulikiwa na hivyo kuunda msingi

wa utafiti huu. Hawa ni K. Walibora na J. Habwe. Utafiti umeonyesha

mchango wao katika kukua kwa riwaya ya Kiswahili na fasihi kwa jumla.

Imedhihirika kuwa watunzi hawa, mbali na kuchangia maendeleo ya riwaya,

wametanda katika tanzu nyingine za fasihi hasa hadithi fupi, tamthilia na

ushairi. Mwisho, sura hii imetoa muhtasari wa riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea (Walibora) na Checheza Mota (Habwe) na kudokeza kwa kifupi maudhui yanayojitokeza katika riwaya hizi. Sura inayofuata inashughulikia

mchango wa mwingilianomatini katika kukuza maudhui katika riwaya.

(36)

SURA

YA TATU

MCHAN

GO WA MWINGIIIANOM

A

T

INI

KATIKA

KUKUZA MAUDHUI

3.0 Utangulizi

Sura hii inalenga kuonyesha namna matumizi ya tanzu na matini mbalimbali

yalivyochangia katika kuendeleza riwaya yaKidagaa Kimemwozea (Walibora)

na Cheche za Mota (Habwe) kimaudhui. Utafiti umejikita katika kubainisha na

kuchanganua maudhui yanayowasilishwa na tanzu pamoja na matini

zilizotumika kwa kuzingatia Nadharia yaMwingilianomatini inayohusishwa na

Bakhtin (1982), Kristeva (1980), Barthes (2002) na (2007), Bloom (1994) na

Foucault (1974) walioeleza kuwa kila kazi ya fasihi inahusiana na kazi

nyingine iliyoandikwa kabla kwa namna moja au nyingine. Nwagbara (2011:

84) anakubaliana nao kwa kusema kuwa nadharia hii inajishughulisha na

---mahusiano baina ya matini na kuwa hakuna matini iliyojitenga na nyingine.

Utafiti umebainisha matumizi ya tanzu za kifasihi kama ushairi, methali na

hotuba; na pia matini ya barua, taarifa za vyombo vya habari na marejeleo

katika kuzijenga riwaya hizi kimaudhui. Matumizi ya tanzu na matini hizi

yanaendeleza mwingilianomatini na usemezano baina ya tanzu na matini.

3.1 Matumizi ya Tanzu Kukuza Maudhui Katika Riwaya

Utafiti huu ulichukulia tanzu kuwa mgawanyiko wa tungo mbalimbali za fasihi. Kwa hivyo, utanzu ni tawi la fasihi au aina ya kazi mbalimbali za kifasihi.

Utanzu mkuu unaweza kuwa na vitanzu vingine_vidogo vidogo. Tanzu kuu za

fasihi andishi ni riwaya, novela, ushairi, tamthilia na hadithi fupi. Pia kuna

(37)

mazungumzo. Kila mojawapo ya tanzu hizi ina vitanzu kadhaa. Kwa mfano, utanzu wa mazungumzo una vitanzu kadha vikiwemo hotuba, mawaidha na soga. Kutokana na msingi huu, utafiti umezingatia matumizi ya tanzu za kifasihi ambazo ni ushairi na nyimbo, methali na hotuba katika kuendeleza maudhui katika riwaya.

3.1.1 Matumizi ya Ushairi na Nyimbo

Mashairi na nyimbo ni baadhi ya tanzu zilizotumika katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Moto (Habwe). Utafiti huu umechukulia mashairi na nyimbo kuwa pande mbili za sarafu moja kwa kuwa tanzu hizi zinahusiana na kukaribiana sana. Uamuzi huu ulifanywa baada ya kuzingatia maoni ya Shaaban Robert aliyesema kuwa:

, ... wimbo ni shairi dogo. Shairi ni wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa shairi'. (Harries 1962: 272).

Kadhalikar Wamitila (2003b) anaongeza kwa kufafanua kuwa shairi ni'ufiiirgo ambao una mistari iliyogawika katika mafungu kadhaa na unaweza kuwa na mpangilio unaoonyesha mfuatano maalumu wa silabi au ukawa hata na idadi maalumu ya silabi hizo. Kadhalika, inawezekana mpangiiio wake ukawa huru pia. Anaendelea kudai kuwa wimbo ni bahari mojawapo ya ushairi. Kwa hivyo utafiti huu hautaziwekea tanzu hizi mpaka ila utazishughukulikia kwa pamoja kama utanzu mmoja.

Katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea (Walibora) na Cheche za Moto (Habwe), ushairi umetokea kuwa nyenzo muhimu ya kukuzia maudhui. Katika riwaya hizi, ushairi ni chombo cha kudhihirishia na kuendeleza mageuzi na ukombozi katika jamii. Aidha, umeonyesha misimamo ya jamii kuhusu

(38)

masuala mbalimbali pamoja na kutolea hisia na kukemea maovu katika jamii.

Kadhalika, ushairi hapa ni chombo muhimu katika kuibua na kuendeleza

uzalendo. Hali hii inadhihirisha kuwa ushairi una uwezo na nguvu za ajabu

kama anavyosema Shaaban Robert kuwa, 'Kwa nguvuye ushairi, natema mota

na radi' (Gibbe 1999a: 2). Ni kutokana na haya ndipo ushairi umeweza

kupenya na kisha kusambaa katika riwaya hizi ili kutekeleza jukumu muhimu

la kuendeleza maudhui.

3.1.1.1 Ushairi Kama Nyenzo ya Kuleta Mageuzi na Haki

Ushairi ni nyenzo muhimu katika kuleta na kuendeleza mageuzi na haki katika

jamii. Hili linadhihirika katika Kidagaa Kimemwozea (Waliborajambapo shairi

lifuatalo la utangulizi limetumiwa kama chombo cha kuleta na kutangazia

mageuzi katika jamii.

Ajabu hino-ajabu,-ya nyangumi kufa maji Alokuwa ni hatibu, ameshauhama mji Naye alokuwa bubu, keshakuwa mnenaji

N'naona shani kubwa

Mitamba wanasifika, wakokotavyo piau Mafahali wameuka, toka ulimwengu huu Wakati umeshafika, nyekundu kuwa bluu

N'naona shani kubwa

Vikwara waliowika, tizama wanatamia Nyundu zimeshakatika, vitwani kutokomea Kukujike wanawika, mawio yakitimia

N'naona shani kubwa

Wasiokuwa na macho, ndiwo sasa marubani Wasompa Mola kicho, waongoza ibadani Aliyekuwa hanacho,hana anachotamani

N'naona shani kubwa

(Walibora2012: iii)

Shairi hili limetumiwa kuiwekea riwaya hii msingi na kudokeza japo kwa ufupi

mageuzi yanayotokea katika riwaya nzima. Haya ni mageuzi ya kiajabu

(39)

ambapo mambo ambayo watu walikuwa wameyazoea na kuyaona kuwa ya kawaida, yamebadilika na kuwa kinyume kabisa. Ni sawa na kuubadili ulimwengu juu chini. Inabainika kuwa waliokuwa wanyonge warnejikomboa na kuondoa udhalimu waliotendewa na wenye nguvu. Kadhalika, nafasi ya wan awake iliyokuwa duni sasa imeimarika na kuwapa fursa ya kutekeleza majukumu muhimu katika maendeleo ya jamii. Imani na mielekeo hasi

iliyokuwa imekita mizizi katikajamii imeng'olewa na jamii kujenga mtazamo mpya wa maisha katikajamii.

Kinachodhihirika katika shairi hili ni kuwa binadamu ana uwezo wa kugeuza maisha yake, hali yake, mtazamo wake, imani yake na mielekeo yake mradi awe na nia, ari na sababu ya kufanya hivyo. Akijihami na haya yote, hakuna lisilowezekana kwake. Kwa hivyo,_~~~h~_ y~ mageuzi ni binadamu mwenyewe. Katika kuleta hayo mageuzi, tahadhari sharti ichukuliwe ili udhalimu usiendelezwe dhidi ya mtu yeyote au kikundi chochote kile. Hii ni kwa sababu watu wanaweza kugubikwa na hamu ya kutaka mabadiliko na kusahau kuwa mabadiliko hayo huenda yakaendeleza maonevu dhidi ya kundi fulani la watu katika jamii. Mageuzi yenye manufaa ni yale yanayoleta nafuu kwa wote na wala si kuendeleza dhuluma na uonevu kwa yeyote. Kwa mfano, mageuzi yanayowaondolea dhuluma wanawake yasilenge kuwadhulumu wanaume au kulipiza kisasi dhidi ya yeyote.

Isitoshe, ushairi umetumiwa katika Cheche za Moto (Habwe) kama nyenzo ya kudai demokrasia, haki na amani. Haya ni kwa mujibu wa mayowe ya kishairi yal iyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha BarnaInternational na wale

(40)

wa Chuo Kikuu eha Hekima waliokuwa wakifanya fujo katika uga wa kanisa

wakati wa ibada ya wafu kwa heshima ya Thuo. Walitaka mauaji ya wasomi

yakome mara moja. Walisema kuwa:

Tunataka demokrasia! Tunataka ukweli!

Ni nani aliyemwua Thuo?

Gari lililomkanyaga lilikuwa la nani? Tupeni haki!

Tupeni amani! Wasomi tunamalizwa!

(Habwe 2008: 60)

Kadhalika, hawa waandamanaji walitaka kujua ukweli kuhusu kifo eha Thuo.

Pia, walisema kuwa wasomi walimalizwa kwa kuuliwa. Ikumbukwe kuwa

Thuo alikuwa mtetezi maarufu wa haki za binadamu na alifunza katika Chuo

Kikuu eha Hekima. Yeye pamoja na Prof. Mule walikuwa wanaharakati

waliopinga kuwepo kwa serikali ya chama kimoja, kutia watu kizuizini, na

__ kunyimwa uhuru wa kusema na kuandika. Wao waliandaa mkutano katika

uwanja wa Uhuru Stadium kueleza umma kuhusu masuala ya demokrasia na

kuufundisha kuhusu haki yao na kuwataka kukamia uhuru mpya. Serikali

iliupinga mkutano huo na kuonya umma kutohudhuria. Rata hivyo, wananchi

walipuuza onyo hili na kuhudhuria. Polisi walitumia nguvu kuuvunja huo

mkutano na kisha kuwatawanya raia. Thuo alikufa katika ehamkano lililofuatia

kwa kugongwa na basi la Boma Bus Co. alipokuwa akivuka barabara mbio.

Kifo hiki kiliwahamakisha sana wanafunzi vyuoni na wakazua fujo na kupiga

mayowe haya ya kishairi.

Aidha, mayowe ya wabunge yalizidisha malalamishi dhidi ya mauaj i

(41)

wengine kupotea kabisa. Mayowe haya yaliyochukua mtindo wa kishairi,

yalilaani mauaji hayo na kudai maonevu yakomeshwe mara moja:

Tunamalizwa! Soote tutakufa!

Uhuru tuiiopata ni wakuibiana! Uhuru tuiiopigania niwa kuhadaana! Mungu tuokoe!

Usipotuokoa Mungu tutakufa sote! Tupeni Okgibo!

Tupeni Mheshimiwa Karume! TupeniAskofu Kanuri! Tupeni Masinde wetu! Tupeni Nyeiele,

Tupeni Loiioi wetu, mweusi na mrefu! Tupeni Ssemogerere!

Tupeni Ngoia wetu! (Habwe 2008: 146)

Wabunge hawa walisema kuwa uhuru waliopata ni wa kuibiana na kuhadaana.

Walimwomba Mungu awaokoe la sivyo wangekufa wote. Walidai wapewe

viongozi maarufu nchini waliouawa kiholela. Hawa ni viongozi walioazimia

kuleta uhuru wa kweli nchini na hivyo kupinga dhuluma na maonevu

yaliyokithiri. Serikali nayo iliwaona kuwa waharibifu na kuwaangamiza.

Viongozi hawa walikuwa pamoja na Okgibo, Karume, Askofu Kanuri,

Masinde, Nyelele, Loiloi, Ssemogerere na Ngola. Mayowe haya yalichochewa

na kifo cha Muga aliyekuwa Waziri wa Mali ya Asili serikalini. Alipotea na

kutafutwa kila mahali bila mafanikio yoyote. Wengine walidai alionekana

madukani Botswana akinunua viatu. Serikali nayo ilidai kuwa alikimbilia nchi

ya Botswana kama mkimbizi wa kisiasa. Baadaye mwili wake ulipatikana

katika Mto Sese na watoto chokoraa ukiwa umechubuka ngozi na ilikuwa

vigumu kuutambua.

(42)

Aidha, ushairi unazidi kujitokeza katika Cheche za Moto (Habwe) wakati

wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtanda State University walifuata msafara wa

kuupeleka mwili wa Nandi katika uwanja wa ndege kwa mabango na matawi

huku wakipiga mayowe, wakiimba na kulaani kifo cha Nandi; na kudai

demokrasia:

Tunalaani mauaji! Tunalaani mauaj i! Tunalaani mauaji! Wapi demokrasia?

(Habwe 2008: 201)

Mheshimiwa Nandi alikuwa waziri katika serikali ya Rais Mtanda. Kadhalika,

alikuwa mshauri wa karibu wa Rais. Lakini baadaye alitengwa na kisha

kufutwa kazi. Alfajiri moja Nandi aliamua kuenda kwao nyumbani. Alienda

kwa gari lake bila dereva. Njiani, aliandamwa na Land Rover rnoja kwa muda.

Watu waliokuwa katika Land Rover hii ndio waliompiga na kumuua.

Waliutupa mwili wake barabarani ili uganyagwe na magari. Baadaye

ilitangazwa kuwa alikufa katika ajali ya barabarani akiwa safarini kuenda

nyumbani. Mwili wake ulipokuwa ukisafirishwa hadi uwanja wa ndege ili

kuzikwa kwao nyumbani ndipo wanafunzi hao wa chuoni walipopiga mayowe

na kuimba wimbo huo.

Rata hivyo, mbali na ushairi kutumiwa kudai mageuzi, haki na demokrasia; pia

ulitumiwa kuendeleza ubarakala na hata kuwatukuza madhalimu na

kuwaombea watawale milele. Wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya

Mtanda Day katika uwanja wa Mtanda Revolution Square, Rais Mtanda alitoa

-hotuba iliyoshangiliwa na wananchi. Aliahidi kutoa elimu ya bure hadi shule za

(43)

waliterema na kuimba wakimtukuza Mtanda pamoja na Chama Cha Mapinduzi

cha Zanze (CCMZ). Walimshukuru Mungu kwa kuwapa Rais Mtanda na

kumwombea atawale milele kupitia shairi hili:

Mtanda! Mtanda! Mtanda! CCMZ! CCMZ! Woyee! Uhuru, Uhuru,Uhuru! Asante Mungu, Asante Mungu, Asante Mtanda, Asante baba yetu. Atawale milele!

(Habwe 2008: 208)

3.1.1.2 Ushairi Kama Chombo cha Kuapishia Wanajamii

Ushairi umetumiwa katika Kidagaa Kimemwozea (Walibora) kama njia ya

kulishia watu kiapo katika jamii. 'Wimbo wa Mwiko' umetumika kutekeleza

hili. Wanajamii waliapa kuwa:

Nijapolewa tembo

-Nikalewa chakari Nipepesuke

Nijapovuta kasumba na kuyumba Niyumbeyumbe

Nikapayuke

Sinywi maji ya Kiberenge Siyanywi katu siyanywi

(Walibora 2012: 4)

Kwa watu wa Sokomoko, ilikuwa ni mwiko kuyanywa maj i ya Mto Kiberenge.

Hii ni kwa sababu mtu mmoja mwenye kifafa alizama katika mto huo na mwili

wake ukapotea kabisa. Mwiko huu ulishadidiwa na kutupwa kwa maiti za

Waafrika waliouawa na Wazungu wakati wa harakati za ukombozi dhidi ya

wakoloni; na damu yao kugeuza rangi ya maji ya mto huo kuwa nyekundu,

Kwa hivyo watu wa Sokomoko waliapa na kuweka msimamo wa kutoyanywa

maji ya mto huu kwa vyovyote vile kutokana na imaniwaliyoshikilia kuuhusu.

Msimamo huu uliwekwa na kutangazwa kishairi ili kushadidia imani yao.

(44)

Walishikilia imani hii hadi Imani na Amani waJipovunja mwiko huu kwa

kuyanywa maji hayo. Hii ni ithibati ya imani nyingi ambazo bado watu

wanazing'ang'ania na ambazo kwa kweli hazina mashiko. Watu wengi

wamekuwa watumwa wa imani hizi kwa kufuata mkumbo tu bila ya kuzidadisi

na kuzichunguza ili kupata ukweli kabla ya kuzipapia na kuzibwia kiholela. La

muhimu ni kufanya juhudi za kujikomboa kutokana na imani za aina hii

zinazokwamisha maendeleo katikajamii. Juhudi za mtu mmoja au kundi dogo

la watu zinaweza kuleta mageuzi katikajamii nzima.

Hapa, Imani pamoja na Amani wanapanda mbegu inayobadilisha mielekeo na

mitazamo ya watu kuhusu Mto Kiberenge na kuubatilisha wimbo uliotungwa

kutangaza mwiko wa watu wa Sokomoko kuyanywa maji ya mto huo. Haya

yanaendana na maoni ya Kehinde (2003) kuwa matini yoyote ile inahusiana na

muktadha wa kitamaduni au kijamii ulioizalisha na haiwezi kutenganishwa - -

---nao. Kwa hivyo, matini zote zimesheheni imani na mawazo yanayotokana na

miktadha hii.

3.1.1.3 Ushairi Kama Chombo cha Kupitishia Hisia

Katika kurejelea shairi kwa 'Heshima ya Mamake' katika Kidagaa

Kimemwozea (Walibora), Amani ametumia shairi hilo kuonyesha machungu

yaliyompata baada ya kufiwa na mamake:

Mkono umeniacha, mwanao kindakindaki Jitimai imechacha,Amani sifarijiki Nahisi lau machicha, thamani sithaminiki Maskini kutwa kucha,natamani kufariki

Tukutane kuko huko

(45)

Machozi kikombe tele

(Walibora 2012: 33-34)

Kupitia shairi hili, Arnani anadhihirisha majonzi yaliyomkumba baada ya

kifo hicho kiasi cha kumkatisha tamaa ya kuishi. Anaonyesha pengo

lililoachwa na mamake maishani mwake. Pia anadhihirisha udhalirnu

aliotendewa na wenye nguvu, hasa kwa kumtia jela kwa kosa lakusingiziwa.

Kadhalika, anaonyesha namna mamake alivyojihimu kumlea peke yake

baada ya kifo cha babake. Babu yake (Chichiri Hamadi) pia aliuawa na kisha

amu yake Yusufu kusingiziwa uhalifu huo na kufungwa jela. Mtu aliyefanya

haya yote alimpokonya mzee huyo shamba lake huko Sokomoko.

Kupitia shairi hili, mtunzi anaonyesha madhila yanayowakumba wanyonge

wanaonyanyaswa na wenye uwezo ili kukidhi kiu yao ya mali. Pia,

anaonyesha namna akina mama wanavyojitahidi kuwalea watoto pekee yao

baada ya kuondokewa na waume zao. Kinachomchoma Amani ni kuwa

hakupata fursa ya kumzika mamake mpendwa kutokana na kusingiziwa kosa

na kutiwa jela. Aliyetenda hayo yote alipania kuhakikisha kuwa hakuna mtu

yeyote kutoka katika aila ya Mzee Chichiri Hamadi aliyeweza kumzuia

kumiliki shamba alilonyakua. Huyu alikuwa Mtemi Nasaba Bora aliyetumia

mamlaka yake kuwadhulumu wanyonge na hata kuvuruga ushahidi wote.

Shairi hili linadhihirisha jitimai iliyornkumba Amani kutokana na dhuluma

hizo. Ushairi hapa umetumika kutolea kilio cha wanyonge katika jamii na

kudhihirisha dhuluma wanazotendewa na walio mamlakani.

Vilevile, katika 'Shairi la Shakawa', Amani anadhihirisha uchungu wa

kuondokewa na kitoto Uhuru alichokilea na kukipenda licha ya hali yake

(46)

ngumu kimaisha. Alikitafutia matibabu kilipougua lakini hakuweza

kukiokoa. Wale walio na uwezo katika jamii walihakikisha kuwa

hakufanikiwa. Kwa hivyo, ushairi unakuwa njia mwafaka ya kuombolezea

kama inavyodhihirika hapa:

Uhuru mwanangu, mkembe ukiwa, umekatika

Hukuwa ni wangu, mwanzo kuzaliwa, ukatupika

Ni pakavu pangu,ulikolelewa, ukapendeka

Nami 'na uchungu,kwa kuondokewa, nawe hakika

(Walibora 2012: 110)

Amani alitunga shairi hili baada ya kuachiliwa huru kutoka kizuizini pamoja

na Imani walikotiwa na Mtemi Nasaba Bora kwa tuhuma za kukiua kitoto

hicho kichanga alichokipenda na kukilea licha ya kuwa alitupiwa mlangoni

pake na mtu asiyemjua. Alihangaika nacho ili kukitafutia matibabu lakini

hakufanikiwa. Sasa yeye ndiye mtuhumiwa kwa kifo hicho.

Isitoshe, mbali na kutumiwa kutolea machungu, ushairi pia umetumiwa

kutolea hisia za mapenzi. Amani anatekeleza hili kupitia shairi lake kwa

Imani ambapo anadhihirisha mapenzi ya dhati hasa baada ya kushiriki

kikamilifu katika harakati za kuondoa maonevu na udhalimu uliokuwa

umekithiri katika jamii hapo awali. Vijana hawa walikuwa wamependana

vilivyo na Amani akaamua kumwoa. Haya mapenzi anayodhihirisha hapa

yanaweka msingi imara wa kuijenga jamii mpya isiyo na dhuluma wala

maonevu yoyote. Katika hila shairi, Amani anasema kuwa:

Ewe wangu wa ubani, nikuenziye moyoni Amani nakutamani, kwa huba ziso kifani Nipe kibali lmani, niwewako maishani

(47)

3.1.1.4 Ushairi Kama Nyenzo ya Kukernea Maovu

Katika Kidagaa Kimemwozea (Walibora), baada ya Amani kugundua

kwamba Mwalimu Majisifu ndiye mwizi wa riwaya yake, alimtungia shairi la

kumkemea kwa kosa hilo. Mbali na kumkemea, alimsamehe kwa kosa hilo,

maadamu mkono wake ungeendelea kutunga. Hapa, ushairi umetumiwa

kukemea maovu, kutolea msamaha na kusafiana nia miongoni mwa

wanajamii kama inavyodhihirika hapa:

Ewe msema urango, ili sifa upaliwe Sikuwekei kinyongo, bilashi nijisumbuwe Japo umeiba tungo, mbona usisamehewe? Usidhani umekoma,mkono wangu kutunga

(Walibora 2012: 143)

Mwalimu Majisifu ndiye aliyeuiba mswada wa riwaya ya Amani iitwayo

Kidagaa Kimemwozea. Ameogelea katika sifa asizostahili kutokana na wizi

huu wa miswada ya watu wengine~!lata hivyo, Amani hana kisasi naye.

Alimsamehe kwa sababu mkono wake bado ungeendelea kutunga.

3.1.1.5 Ushairi Kama Chombo cha Kukuzia Uzalendo

Mwisho, katika Cheche za Moto (Habwe), Fatuma akiwa amepakata Checheza

Moto kama talasimu (Habwe 2008: 245-246), aliliona bandiko ukutani na kulisoma mara ya kumi kwa sauti ya kishairi. Sauti hiyo imetumiwa kama

chombo cha kuibulia na kukuzia uzalendo barani Afrika. Kupitia sauti hiyo,

mshairi anasema kuwa amekuja kulifuta machozi bara la Afrika na analiomba

lisiendelee kulia. Anaendelea kusema kuwa anataka kulitibu kutokana na

sononeko na madhila yanayolisonga. Anaahidi kulifunga bendeji kwenye

vidonda vyake na kulipa dawa mwafaka itakayopenya hadi kwenye mifupa na

mishipa na kuliponya. Tiba hii italiwezesha bara hili kusimama, kutembea,

(48)

kusema na kupigana ten a ili kupata uhuru kamili, kujiletea fahari na hata

kupata haki yake duniani. Juhudi hizi zitaliondolea vifo, aibu, njaa, na maradhi

yaliyoenea kote. Hivyo basi, bara la Afrika litakuwa na nguvu na halitachezewa

na mtu yeyote ulimwenguni. Litaheshimika na watu wake hawatakuwa

wakimbizi ama mayatima barani mwao na kwingineko duniani. Kadhalika,

rasilmali zake zitatumiwa kwa manufaa ya wenyeji na wala hazitaporwa na

wageni wanaendelea kujinufaisha kutokana nazo. Bara hili linahimizwa

kusimama imara na kisha kupinga na kukataa maovu yanayolikumba.

Kupitia shairi hili, matumaini mapya barani Afrika yanayotokana na

kupatikana kwa suluhu kwa madhila yaliyolikumba yanadhihirika. Ujenzi wa

Afrika yenye heshima, haki na fahari unahimizwa. Afrika isiyodhulumu wala

kudhulumiwa. Waafrika wanahimizwa kuliondolea bara hili sononeko na

madhila mengi yanayolikumba na hivyo kulirejeshea heshima na fahari yake.

Haya yataliwezesha bara hili kuchukua nafasi yake ulimwenguni na kuondoa

dhuluma zote. Hivyo basi, haki itadumishwa huku maradhi, njaa na ukimbizi

vikimalizwa barani.

Matumizi haya ya ushairi katika riwaya yanathibitisha madai ya Gibbe (1999a:

2) kwamba ushairi una adhama kubwa katika jamii. Adhama hiyo inatokana na

historia yake ndefu, kuenea kwake na kusambaa katika tanzu nyingine za

fasihi, kutumika kwake katika maandiko matakatifu kama vile Biblia na

Kurani, sifa yake ya kuweza kuimbika, na pia kuweza kutayarishwa kwa muda -.

mfupi na kisha kutumika mara moja. Kadhalika, ushairi umetukuka sana kwa

Figure

Updating...

References

Updating...