• No results found

Lugha ya kimafumbo katika riwaya za katama mkangi

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Lugha ya kimafumbo katika riwaya za katama mkangi"

Copied!
154
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

CHUO KIKUU CHA KENYATTA

LUGHA YA KIMAFUMBO KATlKA RIWAYA ZA KATAMA MKANGI

NA

MERCY WARUGURU KAMACHU

TASNIFU

HII

IMETOLEWA

ILl

KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA

SHAHADA YA UZAMILI KATlKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA

(2)

UNGAMO

Tasnifu hii ni kazi yangu na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika chuo kikuu kingine

Sahihi ----~~~~~~---~j' Tarehe

~~~~-=--~---Jina: MERCY WARUGURU KAMACHU

C50/CE/23170/20

10

Tasnifu hii imetolewa kwa idhini yetu kama wasimamizi wa kazi hii ya Chuo Kikuu cha

1. Sahihi ----~--~~---~---Kenyatta

Tarehe

~~~~~~----~~~+--Jina: PROF: KITULA KING'EI

Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika

Chuo Kikuu cha Kenyatta

2.sahihi~

/'

Jina: DKT. JOSEPH N. MAITARIA

Tarehe

If-~

Idara ya Lugha

(3)

TABARUKU

(4)

SHUKRANI

Namshukuru Mungu kwa kunipa nguvu, uwezo na mwongozo katika kila hatua ya maisha yangu na kunipa uwezo wa kumaliza kazi hii.

Nawashukuru wasimamizi wangu Prof. Kitula King'ei na Dkt. Joseph N. Maitaria kwa kunipa

mwongozo na kutumia wakati wao mwingi ili kuhakikisha kuwa kazi hii imekamilika.

Siwezi kuwasahau wahadhiri wote katika idara ya Kiswahili, has a wale waliongoza masomo

yangu ya shahada ya uzamili hadi lengo Iikatimia, Mchango walioutoa Dkt. Richard M. Wafula, Dkt. Edwin W. Masinde na Dkt. Alice N. Mwihaki ulinifaa sana. Ninawapongeza kwa vile walikuwa tayari kila nilipowaendea kunishauri na kunielekeza hasa mwanzoni mwa kazi hii.

Vile vile, nakishukuru Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa kunipa nafasi ya kuendeleza masomo yangu ya uzamili. Aidha, natoa shukurani kwa wanafunzi wenzangu Charity Kibaru na Triza Mwangi ambao kila wakati walinitia moyo kuendelea na kazi hii. Pia, namshukuru mwalimu

mwenzangu Bw. Kamau kwa kunihimiza nijitahidi kumaliza kazi hii.

Nawashukuru wazazi wangu Bw. Peter Kamachu na Bi. Alice Kamachu walionizaa, wakanilea,

na kunipa elimu. Mungu aendelee kuwalinda na kuwapa maisha marefu. Namshukuru mume wangu mpendwa Michael Kimani pamoja na wanangu Samuel Mwangi na Natasha Wangui kwa kuvumilia na kunihimiza kufikisha ukingoni, Mungu aendelee kuwaongoza na kuwabariki.

Mwisho, shukurani zangu ziwaendee ndugu zangu wote hasa dada zangu Keziah Wanjiru na Pauline Wangari ambao walinifaa sana wakati nilipokuwa naendelea na kazi hii, Mungu

(5)

IKISIRI

Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya lugha ya kimafumbo katika riwaya za Mkangi Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Kutokana na udurusu wa maandishi ya wahakiki na watafiti mbalimbali wa riwaya za Mafuta (1984) na Walenisi (1995) ilibainika kwamba, kuna pengo linalohitaji utafiti zaidi. Matumizi ya lugha ya kimafumbo inayojumuisha istiari, tashbihi, jazanda, majazi, methali na ishara ambapo haikuwa imeshughulikiwa kama mada mahususi ya

utafiti katika riwaya hizi mbili. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha mifano ya matumizi ya lugha ya kimafumbo, kutathmini mchango wa lugha ya kimafumbo katika kuibua na kuendeleza maudhui, mwisho ni kutathmini jinsi lugha ya kimafumbo ilivyotumiwa katika usawiri wa wahusika katika riwaya hizo teule.

(6)

ABSTRACT

The topic of this study is "metaphorical language in Katama Mkangis novels." The novels are: Mafuta (1984) and Walenisi (1995). After reading various literary works and research works it is evident that there are various works related to this work but the topic of this study has not been researched on before, that is the usage of metaphor, simile, proverbs, allegory, imagery and other metaphorical sayings in Katama Mkangi' s novels. The objectives of this study were: to show the different types of metaphorical language used by the writer, to find out how the usage of metaphorical language has influenced the themes and finally to investigate how the usage of metaphorical language has influenced the characters. The topic of study is important because of various reasons. First, metaphorical language is among the major styles used in literary works, also Katama Mkangi's novels are widely read and taught in education institutions thereby will assist the learners in understanding the usage of metaphorical language in his novels. Finally, as the area of novel continues to grow it is important to evaluate the styles used by the writers. The researcher used contemporary metaphor theory. This theory suited the topic of study since the novels are rich in the usage of metaphorical language. The data was collected from various books and journals which have information related to the topic of the study. Finally, the data was .analysed using the tenets of the theory being used and thereby assisted the researcher to achieve

(7)

Lugha ya kimafumbo:

Maana ya kitamathali:

Isitiari:

Jazanda:

MAANA YA ISTILAHI MUHIMU

Lugha ya kimafumbo ni lugha ambayo huwasilisha ujumbe kwa njia

fiche na vilevile kwa kulinganisha dhana.

Maana ya kitamathali ni maana zalishi kutoka kwa maana halisi.

Maana hii inatokana na matumizi ya vipengele vya lugha ya

mafumbo.

Isitiari ni usemi ambao huelezea sifa za kitu fulani kwa kusema ni

kingine.

Jazanda ni picha ambayo hujirudia katika kazi ya fasihi na ambayo

(8)

YALIYOMO

UNGAMO ii

TABARUKU iii

SHUKRANI. .iv

IKISIRI v

ABSTRACT vi

MAANA YA ISTILAHI MUHIMU vii

yALIYOMO viii

SURA YA KWANZA 1

1.1 Utangulizi 1·

1.2 Suala la Utafiti 3

1.3 Malengo ya Utafiti 4

1.4 Maswali ya Utafiti 5

1.5 Upeo na Mipaka 5

1.6 Sababu za Kuchagua Mada 5

1.7 Misingi ya Nadharia 7

1.8 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 12

1.9 Mbinu za Utafiti 17

1.9.1 Muundo wa Utafiti 17

(9)

1.9.3 Uteuzi wa Sampuli 18

1.9.4 Ukusanyaji wa Data 19

1.9.5 Uchanganuzi wa Data 19

1.9.6 Uwasilishaji wa Data 19

1.9.7 Changamoto 19

1.10 Muhtasari 20

SURA YA PILI 22

LUGHA YA MAFUMBO NA UHAMISHAJI MAANA KA TIKA RIW AYA ZAMAFUTA NA

WALENfSf 22

2.1 Utangulizi 22

2.2 Taswira Katika Ujenzi wa Mafumbo 23

2.2.1 Taswira katika Riwaya ya Walenisi 25

-,

2.2.2 Taswira katika Riwaya yaMafuta 28

2.3 Majazi kama Mbinu ya Kujengea Mafumbo 30

2.3.1 Majazi katika Riwaya ya Walenisi 32

2.3.2 Majazi katika Riwaya ya Mafuta 34

2.4 Mafumbo Kupitia kwa Jazanda 39

,

2.4.1 Jazanda katika Riwaya ya Walenisi 40

2.4.2 Jazanda katika Riwaya yaMafuta .41

(10)

2.5.1 Taashira katika Riwaya ya Walenisi .46

2.5.2 Taashira katika Riwaya ya Mafuta 47

2.6 Muhtasari 49

SURA YA TATU 50

UBUNIFU WA MAFUMBO KA TIKA RIW AYA ZA MAFUTA NA WALENISI.. 50

3.1 Utangulizi 50

3.2 Mafumbo kupitia kwa methali 51

3.2.1 Methali katika Riwaya ya Walenisi 52

3.2.2 Methali katika Riwaya ya Mafuta 58

3.3 Misemo kama Mbinu ya Kujengea Mafumbo 63

3.3.1 Misemo katika Riwaya ya Walenisi 64

3.3.2 Misemo katika Riwaya yaMafuta 67

3.4 Tashihisi kama Mbinu ya Mafumbo 71

3.4.1 Tashihisi katika Riwaya ya Walenisi 72

3.4.2 Tashihisi katika Riwaya ya Mafuta 73

3.5Sitiari kama Mbinu ya Kujengea Mafumbo 75

3.5.1 Sitiari katika Riwaya ya Walenisi 76

3.5.2 Sitiari katika Riwaya ya Mafuta 77

3.6 Tashibihi katika Ujenzi wa Mafumbo 80

(11)

3.6.2 Tashibihi katika Riwaya ya

Mafuta

86

3.7 Tasifida katika Kujengea Mafumbo 88

3.7.1 Tasifida katika Riwaya ya

Mafuta

88

3.8 Muhtasari 89

SURA YANNE 90

LUGHA YA KIMAFUMBO NA USA WIRI WA WAHUSlKA KA TIKA RIW AYA ZA

MAFUTA

NA

WALENISI

90

4.1 Utangulizi 90

4.2 Lugha ya Mafumbo na Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya

Mafuta

91

4.2.1 Wahusika wa Kimajazi 91

4.2.1.1 Kazamoyo 91

4.2.1.2 Zuka ~ 93

4.2.1.3 Jali ; 94

4,2.1.4l\1tue 95

4.2.1.5 Mama Shibe 96

4,2.1.6 Sifa 98

4.2.1.7 Matope 99

4.2.1.8 Dubwana 101

4.2.1.9 Gweni : 104

(12)

4.2.2

Wahusika Waliosawiriwa Kijazanda

106

4.2.2.1 Ti

106

4.2.2.3

Msati

110

4.3

Lugha ya Mafumbo na Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Walenisi 111

4.3.1

Wahusika wa Kimajazi

111

4.3.1.1

Mama Mtu Maanani

111

4.3.1.2

Mtu Binti Fikirini

114

4.3.1.3

Mzee Mtu Mwenzio

118

4.3

.1.4

Maskini .Jeuri

120

4.3.1.5

Mtu Nasi

121

4.3.2

Wahusika Waliosawiriwa Kijazanda

122

4.3.2.1

Mtu Dzombo

122

4.3.2.2

Mabavu, Moto na Mchawi

123

4.4

Muhtasari ;

126

SURA YA TANO ::

127

Hitimisho

127

5.1

Utangulizi

127

5.2

Muhtasari

127

5.3

Matokeo ya Utafiti

129

(13)

5.5 Mapendekezo 134

5.7 Hitimisho 135

(14)

SURA YAKWANZA

1.1 Utangulizi

Lugha ni kipengele muhimu katika uwasilishaji wa kazi yoyote ya fasihi. Fasihi hupewa umbo kupitia lugha, vilevile kazi ya fasihi

haiwezi

kueleweka bila lugha. Kwa hivyo, lugha ni kigezo muhimu cha kupima ufariisi wa kazi ya fasihi. Lugha ya kimafumbo ni lugha fiche ambayo huhitaji kufasiriwa ili maana inayokusudiwa iweze kueleweka. Lugha hii, ni mojawapo ya kipengele muhimu katika kazi ya fasihi na hujumuisha matumizi ya methali, tashbihi, sitiari, jazanda, majazi, ishara na nahau. Vipengele hivi vya lugha huwasilisha ujumbe kwa njia isiyo ya moja kwa moja na huhitaji msomaji kufasiri maana kusudiwa. Aidha, vipengele hivi vya lugha ya kimafumbo huipa mvuto kazi ya fasihi na vilevile humsaidia mtunzi kuibulia na kuendeleza maudhui ambayo husheheni ujumbe mzito.

Kazi za fasihi huwasilishwa kwa kutumia lugha ya mafumbo. Aina hii ya lugha huwa na maana fiche, yaani huwa na maana isiyo wazi. Aidha, husheheni uwili wa maana unaotokana na matumizi ya tamathali za usemi. Pia, lugha hii huhuisha ujumbe na wakati mwingine husaidia kuweka wazi ujumbe hivyo kueleweka zaidi. Lugha ya kimafumbo hujibainisha katika maana ya kitamathali. Maana ya kitamathali ni maana ya ndani ya kazi za kifasihi inayopatikana kutokana na ufasiri wa mbinu za kitamathali ambazo zimetumiwa katika kazi hiyo.

(15)

kupendeza, kama inavyodhihirika katika riwaya hizi za Katama Mkangi Mafuta (1984) na Walenisi (1995).

Goerge Katama Mkangi ni mwanaelimu jamii aliyeandika riwaya za Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Kazi hizi za Mafuta (1984) na Walenisi (1995), zinahusu jinsi mfumo wa kisiasa, unaodhibitiwa na tabaka la watu wachache, unavyoweza kuathiri maisha ya watawaliwa kijamii, kiuchumi na hata kisaikolojia. Katama Mkangi ni mtunzi aliyetumia lugha kwa njia ya kipekee hasa katika matumizi ya lugha ya mafumbo. Riwaya hizi zake zimesheheni kwa kiwango

kikubwa vipengele vingi vya lugha ya mafumbo.

Uhakiki mchache umefanywa kuhusiana na riwaya hizi mbili na umelenga matumizi ya hadithi, ukinzano na majazi kama mbinu za kuleta uzinduko. Rata hivyo, hakuna uhakiki wa kina uliolenga matumizi ya lugha ya kimafumbo ambayo inahusu matumizi ya jazanda, istiari, tashbihi ,methali na semi mbalimbali. Lugha ya kimafumbo ndiyo ilichunguzwa katika utafiti huu. Vonyoli (2004) amehakiki riwaya hizi mbili Mafuta na Walenisi. Amezingatia suala la hadithi kama chombo cha maudhui. Utafiti wake umechanganua hadithi tofauti katika riwaya hizi na kubainisha maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayowasilishwa katika hadithi

hizo. Utafiti wake umeonyesha jinsi hadithi za jadi zilivyotumiwa na Mkangi kama nyenzo ya kutoa maudhui.

-Matumizi ya majazi kama mbinu ya kuepuka upigaji marufuku ni suala alilotafiti Musee (2007),

(16)

matumizi ya lugha ya mafumbo katika riwaya teule. Namna lugha hii inavyoathiri uwasilishaji

wa maudhui na usawiri wa wahusika.

Umuhimu wa kutumia lugha ya kimafumbo katika kazi ya fasihi ni kusawiri mawazo yamtunzi

kwa kina kwani matumizi ya lugha ya kimafumbo humpa msomaji viwango vingi vya ufasiri na

ufahamu. Aidha, lugha ya kimafumbo ni dhana ya kimsingi katika kuzungumza na kufikiri lakini

pia isiyo rahisi kueleweka. Mafumbo huchochea tafakari miongoni mwa wanajami kwa

kuwazindua kimawazo. Wakati ambapo mtunzi alikuwa akiandika riwaya hizi, uhuru wa

kuikosoa serikali haukuwepo. Kazi zilizoikashifu serikali hazikukubaliwa, hivyo kulikuwa na

umuhimu wa kutumia lugha ya mafumbo katika kuwasilisha ujumbe wa mwandishi. Lugha ya

mafumbo humsaidia mwandishi kuwasilisha masuala mazito yanayohusu jamii kwa njia isiyo ya

moja kwa moja.

1.2 Suala la Utafiti

Kazi ya fasihi huwasilishwa kupitia lugha, mtunzi huteua lugha yenye mvuto itakayomsaidia

kuipa kazi yake umbo mahususi. Aidha, kazi ya fasihi haiwezi kueleweka bila lugha kwani lugha

ndicho kifaa muhimu cha kupima ufanisi wake. Lugha ya kimafumbo ni lugha fiche, ni

mojawapo ya kipengele muhimu katika kazi ya fasihi na hujumuisha matumizi ya methali,

tashbihi, sitiari, jazanda, majazi, lakabu na nahau ..Vipengele hivi vya lugha ya hii huipa mvuto

kazi ya fasihi na vilevile humsaidia mtunzi kukuza na kuendeleza maudhui ambayo husheheni

ujumbe mzito.

Vipengele vya lugha ya mafumbo vinavyotumiwa katika uwasilishaji wa kazi ya fasihi

hutekeleza dhima mbalimbali kama vile, kuipa mvuto kazi ya fasihi na kuchochea tafakari

(17)

kuleta utata katika maana, kwani hutegemea ufasiri na ufahamu wa msomaji. Lugha ya mafumbo huwa ni dhana ya kimsingi katika kazi ya fasihi na ambayo huchochea na kuibua hisia fulani

..

...

rmongom mwa wanajamu,

Kwa kuzingatia maandishi ya wahakiki na watafiti mbalimbali wa riwaya za Mafuta na Walenisi imebainika kwamba kuna pengo linalohitaji kufanyiwa utafiti zaidi, kwani matumizi ya lugha ya kimafumbo inayojumuisha istiari, tashbihi, jazanda, majazi, methali na semi nyingine haijashughulikiwa kama mada mahususi ya utafiti katika riwaya hizi mbili. Vipengele hivyo ni muhimu kwa kuwa husaidia mtunzi katika kuwasilisha ujumbe wake kwa njia ya kipekee.

Utafiti huu ni muhimu kwani, umetathmini na kuchanganua mifano ya matumizi ya lugha ya kimafumbo katika Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Uchanganuzi wa lugha ya kimafumbo aliyotumia mtunzi umetusaidia kubaini iwapo kuna mabadiliko katika matumizi ya vipengele vya lugha ya kimafumbo na iwapo matumizi ya lugha hii ya kimafumbo yamemefanikisha kazi za mtunzi.

1.3 Malengo ya Utafiti

Utafiti huu ulichunguza jinsi lugha ya kimafumbo ilivyotumiwa na mwandishi katika riwaya zake kwa;

1, Kubainisha vipengele vya lugha ya kimafumbo katika uwasilishaji wa fasihi andishi kama inavyodhihirika katika Mafuta (1984) na Walenisi (1995).

11, Kutathmini mchango wa lugha ya kimafumbo katika uwasilishaji na uendelezaji wa maudhui.

111, Kutathmini jinsi lugha ya kimafumbo inavyotumiwa katika usawiri wa wahusika katika riwaya teule.

(18)

1.4 Maswali ya Utafiti

Utafiti huu ulishughulikia maswali yafuatayo ya utafiti.

1. Je, ni vipengele vipi vya lugha ya kimafumbo vinayojitokeza zaidi katika riwaya za

Mafuta (1984) na Walenisi (1995)7

11. Je, lugha ya kimafumbo imechangia katika uwasilishaji na uendelezaji wa maudhui7

111. Lugha ya kimafumbo inaweza kutumiwa vipi kama kipengele cha usawiri wa wahusika7

1.5 Upeo

na Mipaka

Utafiti huu umeshughulikia riwaya mbili za Katama Mkangi Mafuta (1984) na Walenisi (1995).

. Kazi hizi ni miongoni mwa riwaya ambazo zinabainisha matumizi tofauti tofauti ya lugha ya

kimafumbo. Utafiti huu umebainisha jinsi mwandishi alivyoendeleza matumizi ya lugha hii ya

mafumbo kwa kuteua vipengele muhimu vya lugha hii na jinsi vipengele hivi vilivyomsaidia

kuimarisha uwasilishaji.

Riwaya hizi, ingawa mtunzi ill mmoja zilichapishwa katika vipindi tofauti lakini zote

zinasheheni masuala muhimu katika jamii. Kwa hivyo, ni kazi ambazo zimebainisha mabadiliko

ya kiutunzi ya msanii huyu kuhusu uhusishaji wa lugha ya mafumbo katika vipindi tofauti.

Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya lugha ya kimafumbo katika riwaya teule.

1.6 Sababu za Kuchagua Mada

.Lugha ya kimafumbo ni miongoni mwa vipengele muhimu vya lugha katika kazi za fasihi.

Mafumbo hujumuisha matumizi ya jazanda, tashbihi, sitiari, methali, majazi ishara, taswira na

semi nyingine. Matumizi yanayofaa ya vipengele hivi hudhihirisha umahiri wa mtunzi. Lugha ya

kimafumbo inapotumiwa ipasavyo katika kazi ya fasihi, huipa mvuto rnkubwa kazi hiyo na

(19)

mtunzi kwa kuendeleza maudhui na kujenga wahusika. Vile vile, matumizi chapwa ya lugha ya

kimafumbo huweza kukwamiza uwasilishaji wa ujumbe wa mtunzi. Lugha ya kimafumbo

hufasiriwa kwa njia mbalimbali na wasomaji has a kutegemea tajriba zao.

Kazi za kifasihi za Katama Mkangi zina upekee katika matumizi ya lugha ya mafumbo. Hivyo,

matumizi yake ya lugha hudhihirisha umahiri rnkubwa, ambayo ni mojawapo ya sababu za

kuteuliwa kwa riwaya zake. Katika kuzipa riwaya zake vichwa

'Mafuta'

na

'Walenisi',

ni dhahiri

kuwa ametumia lugha ya kimafumbo kwani vichwa hivi havieleweki moja kwa moja. Matumizi

ya lugha ya kimafumbo huwasilisha tajriba ya mwandishi, mawazo yake na hisia zake kuhusu

asasi zote za kijamii katika jamii yake. Ufanisi wa kazi ya fasihi hutokana na matumizi mwafaka

ya lugha.

Baadhi ya riwaya zake hutahiniwa nchini Kenya katika ngazi za vyuo na shule za upili. Lugha ya

kimafumbo ni mojawapo ya mbinu za lugha anazoweza kutumia mwandishi katika kazi yake ya

fasihi. Lugha ya kimafumbo ni kipengele muhimu cha lugha ya fasihi, hivyo matumizi mwafaka

yatadhihirisha umahiri wa mtunzi. Katika kuwasaidia wasomaji wa riwaya hizi kuelewa zaidi na

kuwa na ufasiri na ufahamu unaofaa basi haina budi kutathmini na kubainisha lugha ya

kimafumbo iliyotumiwa na mwandishi katika riwaya hizi mbili.

Utanzu wa riwaya ni muhimu katika fasihi na unaendelea kukua. Hivyo, utafiti unafaa kufanywa

ili kutathmini matumizi ya lugha katika utanzu huu. Utafiti umebainisha iwapo mtunzi ametumia

mitindo mipya au ametumia mitindo ya hapo awali. Mtunzi anapotumia lugha ya kimafumbo

ifaavyo, kazi yake huwa bora zaidi na ya kuvutia ..Aidha, lugha ya kimafumbo huwasilisha mawazo ya mwandishi kwa njia fiche. Mtindo wa Mkangi ni wa kipekee, msomaji yeyote lazima

(20)

1.7

Misingi ya

Nadharia

Katika kuhakiki kazi za Mkangi, utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kimafumbo ya kisasa hasa, kwa kuzingatia kitengo cha lugha ya mafumbo. Nadharia hii iliasisiwa na Lakoff na Johnson, katika mwaka wa (1992). Nadharia hii inaeleza kuwa lugha ya kimafumbo hutumika kurejelea dhana fulani bila ya dhana rejelewa kutajwa. Kulingana na Lakoff (1993) lugha ya mafumbo hutumika katika maisha ya kila siku ya binadamu na vilevile katika kazi za kifasihi. Anaeleza kuwa, lugha ya kimafumbo inapotumiwa katika utunzi wa kazi ya fasihi, matumizi

yake hutegemea tajriba aliyonayo mwandishi. Anafafanua kuwa, maneno yanayotumiwa katika lugha ya kimafumbo huwa na maana msingi ambapo kuna uhamisho wa maana kutoka kitu

kimoja hadi kingine, yaani kutoka matumizi halisi hadi maana ya kitamathali.

Kulingana na nadharia ya kimafumbo ya kisasa, lugha hutumiwa kwa njia tofauti na ile ya matumizi ya kila siku. Lugha hii ya mafumbo imetumiwa katika utunzi wa riwaya kwa kame nyingi. Wasomaji wanapopatana na dhana ya mafumbo katika riwaya, hutafsiri dhana zile kutegemea ujuzi na tajriba zao na vilevile mazingira waliyolelewa Sadock (1993). Lugha ya kimafumbo huelekeza wasomaji katika kutafsiri yale mwandishi anayokusudia ingawa kwa njia isiyo ya moja kwa rrioja.

(21)

Lugha ya kimafumbo hutumiwa kama nyenzo ya kufikirisha na kusaidia kujenga taswira au

maswali ya balagha kwenye akili ya msomaji, lugha ya kawaida haiwezi kufanya hivyo. Lugha

ya kimafumbo si elezi tu bali ni dhanishi. Lakoff na Johnson (1994: 43) wanasema kwamba,

waandishi wa kazi za fasihi hutumia lugha ya kimafumbo kwani inafuata utaratibu fulani katika

kuwasilisha ujumbe, jambo hili hutokea kwa sababu mafumbo husaidia katika kuficha ujumbe na

vilevile ufasiri na ufahamu wa ujumbe uliowasilishwa kwa mafumbo hutegemea tajriba ya

msomaji.

Aidha, Lakoff na Johnson wanatoa mfano katika kutumia fumbo mapenzi ni safari, ina maana

kuwa wapendanao ni kama wasafiri, uhusiano wao ni chombo au gari na lengo lao ni kufika na

kukamilisha safari yao wakiwa pamoja kama ilivyo katika safari ya kawaida. Mafumbo

yanayoweza kujitokeza kutokana na fumbo hili ni kama: uhusiano hauelekei popote, uhusiano

haupo kwa njia inayofaa tena na uhusiano umegonga mwamba. Vile vile, wanafafanua fumbo

'maisha ni safari' ambapo maisha ya binadamu yanalinganishwa na safari, wanasema kuwa

mambo mengi katika maisha ya binadamu huenda yakafanana na yale msafiri anapitia katika

safari.

Katika kutumia mbinu za kimafumbo lazima mwandishi ajiulize maswali kama: fumbo

analolitumia lina misingi gani, fumbo hilo limeenea vipi katika jamii na je, hutumiwa na

wanajamii wa kawaida. Hivyo, huweza kuamua narnna litakavyoeleweka katika utunzi wake.

Aidha, lugha ya kimafumbo hutumiwa katika kazi za fasihi has a riwaya na ushairi ambapo

maneno fulani hutumiwa kusimamia dhana tofauti. Kwa mfano, maneno 'mama' na 'usiku'

yanatumiwa kwa maana tofauti na ile ya kawaida kwani dhana nyingine tofauti huweza kuwa na

sifa sawa na za maneno haya. Wanaeleza kuwa lugha hii huhusishwa sana na kazi ya sanaa

(22)

Berggen (1962) anaeleza kuwa, lugha ya kimafumbo huhusisha virejelewa vingi ambavyo

hutenganishwa na mipaka fulani inayofahamika na kanuni za uhamisho wa maana ambazo

zinavuka mipaka lakini ambazo haziondoi au kuharibu mipaka hiyo. Kanuni hizi huibua uwezo

wa kuelewa uhusiano wa mafumbo na hali halisi ya kijamii. Berggen anatambua kuwa mafumbo

huhusisha uwili wa maana. Aidha, kuna aina mbalimbali za mafumbo.

Lugha ya kimafumbo inaleta taswira ambayo hutusaidia kuona jambo zaidi ya maana yake

dhahiri au ya juujuu na kuona ile maana ya ndani au maana batini. Lugha hii ina upekee ambayo

ndiyo sababu inaifanya kupewa msisitizo. Katika lugha ya kimafumbo mtunzi husema kuhusu

jambo X kana kwamba ni Y. Yaani anatumia Y katika kurejelea X has a katika matumizi ya

jazanda na sitiari.

Naye Hester (1967), akimnukuu Aristotle anasema kwamba katika lugha ya kimafumbo kitu

hupewa jina la kitu kingine, yaani uhamisho wa sifa za kitu kimoja hadi kingine. Lugha ya

kimafumbo hutumiwa badala ya lugha

ya

kawaida ili kuibua taswira fulani inayokusudiwa na

mwandishi, taswira hii hujitokeza kupitia uhuishi, majazi, jazanda, methali na semi ambapo zote

huhusisha mafumbo kwa kurejelea kitu kwa kutumia kingine au kwa njia isiyo ya moja kwa

moja. Kwa mfano, kifo hurejelewa au hulinganishwa na vitendo vya kuvuna au kuharibu.

Hakilinganishwi na vitendo vya kujenga kama useremala au ualimu kwani kazi hizi ni za

kujenga na si kubomoa.

Lakoff (1993), akifafanua mihimili ya nadharia hii anamnukuu Leech (1969) anayeelezea

kwamba, lugha ya kimafumbo inahusishwa na kanuni mahsusi ya uhamisho ambayo inajulikana

kama kanuni fumbo na ambayo tunaweza kueleza kwa utaratibu huu; "T" ni sawa na "H". Hii

(23)

fumbo lina sehemu mbili; dhana asilia au suala kuu na chombo kifanani. Hii inamaanisha kuwa

dhana asilia na chombo kifanani zinakaribiana sana katika sifa zao. Kutokana na mtazamo wa

kiisimu maana halisi ndiyo ya kimsingi na maana ya kitamathali ndiyo maana zalishi.

K

wa kawaida uhamisho wa kimafumbo huwezekana iwapo mshabaha utaonekana kati ya swala

kuu na chombo kifanani. Hata hivyo, Leech anadai kuwa kutenganisha dhana asilia na chombo

kifanani sio dhahiri katika baadhi ya mafumbo. Tajriba ya msomaji huathiri ufasiri wake wa

maana na hutegemea muktadha na maelezo halisi. Fumbo linalohusika huweza kuwa na

mshabaha mkubwa na chombo kifanani.

Mtazamo wa Hester (1967) una mshabaha na wa nadharia hii ya kimafumbo ya kisasa.

Akimnukuu Aristotle anasema kwamba, lugha ya kimafumbo huhusisha kuwasilisha ujumbe

kwa njia fiche. Lugha hii hupatia lugha uangavu, ucheshi, mvuto, ubora na utofauti wa kipekee.

Lugha ya kimafumbo ni pambo katika matumizi ya lugha.

Aidha, matumizi ya lugha ya kimafumbo hujumuisha matumizi ya methali. Kulingana na Lakoff

(1993) baadhi ya kauli teule huwa na maana fiche. Kutegemea ufasiri na ufahamu wa wasomaji

maana ya methali moja huweza kuwa tofauti kwa wasomaji tofauti. Lakoff anaendelea kusema

kwamba, methali hutumia lugha ya kimafumbo na huweza kuchota amali zake kutoka kwa lugha

na tamaduni za jamii husika. Lugha ya kimafumbo huweza kusheheni mfumo mzima wa jamii

husika. Hivyo, kupitia lugha ya kimafumbo inayotumiwa na jamii fulani msomaji anaweza

kuielewa jamii hiyo, kuelewa tamaduni zake na vilevile kuelewa imani na itikadi za zake.

Waandishi wengi hutumia lugha ya kimafumbo kimaksuudi kwa nia ya kuwasilisha maudhui yao

(24)

kutumia lugha ya kimafumbo kwa njia mahususi. Hivyo basi wasomaji huweza kufasiri na

kuelewa maana halisi aliyokusudia mwandishi. Lakoff (1993)

Matumizi

ya lugha ya kimafumbo vilevile huhusisha matumizi ya majazi. Majazi ni hali ya

kuwapa watu au mahali majina yanayoafiki au yanayofanana na sifa zao. Hivyo basi, mwandishi

huweza kuteua majina hivi kwamba majina hayo ya kimajazi huweza kuwasilisha ujumbe

maalumu aliokusudia mwandishi. Aidha, mwandishi hujenga wahusika wake hivi kwamba

wanakuwa wawakilishi wa wahusika katikajamii halisi.

Aidha, lugha ya kimafumbo hujumuisha matumizi ya tashibihi. Katika kutumia tashbihi

.mwandishi hulinganisha vitu kwa kutumia maneno linganishi. Lakoff anasema kuwa, mtu

anapolinganishwa na kitu fulani ina maana kuwa sifa za mtu yule zinafanana na kile

anacholinganishwa nacho. Anafafanua kuwa, katika matumizi ya sitiari mwandishi hutumia

dhana fulani kusimamia dhana nyingine kutokana na mfanano mkubwa wa dhana hizo mbili.

Nadharia ya kimafumbo ya kisasa ni kama kigezo cha kusaidia katika kuelewa maana ya ndani

ya kazi za fasihi, yaani maana aliyokusudia mwandishi. Kwa kupitia nadharia hii msornaji

anaelewa vipengele vya lugha ya kimafumbo na vilevile dhima yake katika fasihi.

Kutokana na nadharia ya kimafumbo ya kisasa, mihimili yake ni:

1. Aina mbalimbali za lugha ya kimafumbo hujitokeza katika kazi ya sanaa .

. 11. Matumizi ya lugha huhitaji ufasiri wa maana kusudiwa. Kwa hivyo, lugha ya kimafumbo

hujitokeza katika kiwango dhanishi na kile cha lugha ambapo kuna uhamisho wa

kimaana kutoka kitu kimoja hadi kingine.

111. Lugha ya kimafumbo hutumiwa katika jamii kwa lengo la kuficha ujumbe au pia kuweka

(25)

IV. Lugha ya kimafumbo huichochea akili ya hadhira kujenga taswira fulani.

1.8 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada

Lugha ya kimafumbo ni lugha ambayo hupitisha ujumbe kwa njia fiche, yaani maana yake siya

moja kwa moja na huhitaji kufasiriwa ili ieleweke. Katika kazi mbalimbali dhana ya lugha ya

kimafumbo imeshughulikiwa lakini haijashughulikiwa kwa kina kwani ni wasomi wachache tu

wameishughulikia. Katika matumizi yake, dhana moja hutumiwa kusimamia dhana nyingine na

huibua maana tofauti na ile yake ya kawaida, maelezo haya ni kwa mujibu wa Lakoff (1994).

Aidha, Cuddon (1999) anaeleza kuwa, kutumia lugha ya kimafumbo ni kule kutumia dhana

fulani ili kuwasilisha maana fiche, hivyo hujitokeza kama dhana mbili, dhana iliyotumiwa na

dhana kusudiwa. Dhana hizi mbili katika hali ya kawaida huwa na maana tofauti. Hivyo, katika

kuangalia uamilifu wa lugha ya kimafumbo inabainika kuwa hutekeleza majukumu mbalimbali,

hivyo huhusisha vipengele vingi na vingine huonekana kama vinapingana. Ufasiri wa msomaji

hutegemea tajriba yake na hali ya jamii yake. Hivyo, wanajamii tofauti huweza kuwa na ufasiri

unaopingana au unaofanana kutegemea tamaduni zao.

Vile vile, lugha ya kimafumbo hutumika katika tanzu zote za fasihi na huweza kuangaliwa kwa

njia mbalimbali kwanza, huonekana kama njia ya upole ya kuwasilisha ujumbe ambao

ungewasilishwa kwa lugha ya kawaida ungeudhi au uibue hisia kali. Msemaji au mwandishi

aliyetumia lugha ya kimafumbo anaweza kufafanua alimaanisha nini hasa, tofauti na maoni ya

wengine, Sheikh (1994). Lugha ya kimafumbo inapotumika ili kuwasilisha ujumbe kwa njia ya

upole hata kama ni ujumbe mzito hauibui hisia kali kwani huweka wazi utangamano wa kila siku

wa wanajamii kama vile migogoro, kutoridhika na pia mambo yanayohusu mtu kuwa mume au

(26)

Aidha,

lugha ya kimafumbo huonekana kama mbinu ya kipekee ya kutumia lugha ili kuipa

mvuto au kuirembesha kazi ya fasihi. Abdalla (1979) anasema kuwa, kazi yoyote ile ya fasihi

huonekana bora zaidi mwandishi anapotumia mbinu hii ya lugha ya kimafumbo. Abdulaziz

(1979) anasisitiza kuwa, tanzu za fasihi andishi lazima zizingatie matumizi ya lugha ya

kimafumbo kwani ndio njia kuu ya kuwasilisha ujumbe kupitia kwa tanzu hizi.

Lugha ya kimafumbo

vilevile

huwa kama dhana za kiakili zinazojitokeza katika maisha ya

binadamu ya kila siku hivyo, hutumika kama nyenzo ya kubainisha fikra za binadamu, yaani

hutumika kama njia ya kurahisisha mambo anayopitia binadamu kila siku. Katika utafiti wake

Jilala (2008) anaeleza kuwa utanzu wa nyimbo na hasa nyimbo za bongo flava hutumia lugha ya

kimafumbo ili kupitisha ujumbe kwa hadhira. Nyimbo hizi husheheni matumizi ya methali

tashbihi na sitiari, mbinu hizi huwasilisha ujumbe kwa mafumbo. Lugha hii ni nyenzo kuu ya

kupitisha ujumbe kwa wanajamii. Lugha hii hubainika katika kiwango dhanishi na hivyo

hutumiwa na binadamu katika shughuli zake za kila siku kwani zote huhusisha fikra.

Matumizi ya lugha ya kimafumbo hujikita katika mipaka ya tamaduni ya jamii husika, Jilala

anafafanua kuwa, maneno tunayotumia katika jamii yetu maana zake zinajulikana kulingana na

mila na desturi zetu. Hivyo, matumizi ya lugha ya kimafumbo hutegemea jamii husika. Lakoff

anaeleza kuwa, lugha ya mafumbo hujengwa kwa kauli za kurudiwa katika jamii, kauli hizi

huficha ujumbe. Naye Maitaria (2012) anaeleza kuwa, kauli za mafumbo hufanyiwa

marekebisho na wanajamii na huwasaidia katika kuficha ujumbe.

Murry (1931) anaeleza lugha ya kimafumbo kama dhana ya kimsingi katika kuzungumza na

kufikiri lakini pia isiyo rahisi kueleweka. Huchochea au huibua hisia fulani miongoni mwa

(27)

Richards (1965) vitu hivi viwili vinavyolinganishwa ndivyo vya kimsingi zaidi katika lugha hii

ya kimafumbo. Yaani kuna kiashiria kinacholinganishwa na kiashiriwa.

Lugha ya kimafumbo hutumika katika kiwango cha mawasiliano ya kawaida na pia katika

uandishi wa kisanaa. Leech (1974) anaeleza kuwa, lugha ya kimafumbo hufanikisha

mawasiliano katika kiwango cha juu zaidi ikilinganishwa na lugha ya kawaida. Hivyo basi, lugha

ya kimafumbo huipa mvuto mkubwa kazi yoyote ya fasihi na kuifanya ya kupendeza.

Wanafasihi

katika matumizi ya lugha ya mafumbo huwasilisha ujumbe wao kwa namna ya

kipekee yenye kuficha makali ya ujumbe huo.

Lugha ya kimafumbo hutumika katika jamii mbalimbali. Shariff (1983) anaelezaa kuwa,

matumizi ya lugha ya kimafumbo ni kama sehemu ya utamaduni wa jamii ya Waswahili. Kwa

hivyo, tafsiri lazima ifanywe kutegemea mipaka ya utamaduni unaohusika. Tafsiri za jamii

tofauti hutegemea tamaduni, tajriba na mazingira yao, kwa mfano methali hueleweka vizuri zaidi

katika mazingira iliyoibuliwa.

Aidha, tafiti chache zimefanywa kuhusu riwaya hizi za Katama Mkangi, Mafuta (1984) na

Walenisi (1995). Hata hivyo, baada ya Walenisi kuidhinishwa kama kitabu cha kutahini

wanafunzi wa kidato cha nne, waandishi kadhaa waliandika miongozo, mfano ni Mogambi

(2003). Miongozo hii imetoa tahakiki za jumla kuhusu ploti, muhtasari wa kila onyesho,

wahusika maudhui na mtindo. Hawajashughulikia lugha ya kimafumbo kwa kina ambalo ndilo

suala letu.

Baadhi ya wahakiki wamehakiki masuala mbalimbali katika riwaya hizi. Vonyoli (2004)

amehakiki riwaya hizi mbili Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Amezingatia suala la hadithi

(28)

kubainisha maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayowasilishwa katika hadithi hizo. Utafiti wake umeonyesha jinsi hadithi za jadi zilivyotumiwa na Mkangi kama nyenzo ya kutoa maudhui.

Matumizi ya majazi kama mbinu ya kuepuka upigaji marufuku ni suala alilotafiti Musee (2007), katika riwaya hizi mbili za Mkangi. Amechunguza jinsi lugha ya majazi ilivyotumiwa ili kuepuka upigaji marufuku wa kazi hizi za Mkangi nchini Kenya, wakati ambao serikali iliyokuwa mamlakani haikutaka kukosolewa au kukashifiwa. Katika utafiti wake, Musee amebainisha jinsi Katama Mkangi alivyoweza kuepuka kupigwa marufuku kwa kazi zake kwa kutumia mbinu ya majazi. Utafiti wetu ni tofauti na huu kwani umeshughulikia matumizi ya lugha ya kimafumbo inayojumuisha matumizi ya istiari, tashbihi, methali, jazanda, majazi na

.

. .

serm nymgme.

Aidha, baadhi ya wahakiki wa kifasihi wameshughulikia lugha ya mafumbo katika kazi zao, kwa mfano Jilala (2012) ameshughulikia dhima ya mafumbo katika nyimbo za bongo, anafafanua kuwa mafumbo ni kigezo muhimu katika kupitisha ujumbe. Abdilatif Abdala katika mashairi yake 'Telezi', 'Mnazi', 'Vuta N' Kuvute', 'Jibu', na 'Mamba', ametumia lugha ya kimafumbo kwa kina has a istiari, methali na jazanda. Kazi hizi zimeshughulikiwa na tafiti nyingi hapo awali lakini suala letu ni tofauti na masuala yaliyoshughulikiwa.

Kadhalika, wahakiki wengine wamehakiki riwaya mbalimbali za Kiswahili. Muindi (1990), alihakiki riwaya za Said Ahmed Mohamed, ambapo alishughulikia usawiri wa wahusika

(29)

jinsi mwandishi anawaondosha katika maisha hayo ya ukahaba. Utafiti wa Muindi umejikita

katika kipengele cha wahusika.

Aidha, suala la ukengeushi wa wasomi katika riwaya za Euphrase Kezilahabi, lilishughulikiwa

na Mayaka (1991). Riwaya zenyewe ni: Rosa Mistika (1971), Kichwa Maji (1974), Dunia

Uwanja wa Fujo (1975), na Gamba la Nyoka (1979). Amechambua usawiri wa wahusika kwa

lengo la kuainisha hali zinazosababisha ukengeushi huo. Mayaka ametumia nadharia ya uhalisia

wa kijamaa katika kuhakiki vitabu hivyo. Utafiti wetu ni tofauti kwani umeshughulikia matumizi

ya lugha ya kimafumbo katika riwaya za Katama Mkangi na vilevile utatumia nadharia tofauti.

Osore (1994), amehakiki riwaya za Suleiman Mohamed kiisimu. Amechunguza jinsi maudhui ya

Suleiman yanavyobainika kupitia viwango vya sintaksia, semantiki na isimu amali. Anaonyesha

kwamba kupitia viwango maalum vya kiisimu tunafahamu maudhui kwa njia nzuri. Aidha

amebainisha uhusiano uliopo kati ya isimu na fasihi. Riwaya alizohakiki ni: Kiu (1972) na Nyota

ya Rehema (1976). Utafiti wake ni tofauti na huu kwa sababu huu umejikita katika matumizi ya

lugha ya mafumbo.

Maganju (2004) ameshughulikia uhalisiajabu katika riwaya mbili: Babu Alipofufuka ya Said

Ahmed Mohamed (2001) na Bina-Adamu (2002) ya Wamitila. Amesema kwamba waandishi

hawa wametumia uhalisiajabu kwa maksudi ili kufanikisha maudhui yao. Aidha, ametumia

nadharia ya uhalisiajabu ambapo matukio yanasawiriwa kiajabuajabu, ni ya kuogofya na kutisha.

Utafiti wake ni tofauti na huu kwani umejikita katika kutathmini matumizi ya lugha ya

kimafumbo. Katika riwaya za Mafuta (1984) na Walenisi (1995).

Aidha, Mavisi (2007), amehakiki usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za Zainabu Burhani.

(30)

Mizani(2004). Mavisi amebainisha jinsi Burhani katika kusawiri wanawake anapiga vita mfumo

wa kuumeni, ijapokuwa haepuki athari zake kabisa. Mavisi ameshughulikia kitengo chauhusika.

Mtafiti mwingine aliyehakiki riwaya ni Kamau (1992) ameshughulikia ufundi katika riwaya za

Mohamed Said Abdula. Amefafanua ufundi aliotumia mwandishi katika kuwasilisha ujumbe

wake. Riwaya alizoshughulikia ni: Mzimu wa Watu wa Kale (1960), Kisima cha Giningi (1968),

Duniani Kuna Watu (1973) na Siri ya Sifuri (1974).

Rajab (2008) ameshughulikia maigizo kama mbinu ya maudhui katika riwaya za Ken Walibora.

Riwaya alizoshughulikia ni: Ndoto ya Amerika (2001) na Kufa Kuzikana (2003). Amebainisha

jinsi riwaya hizi zimesheheni sifa za kitamthilia kwa sababu mwandishi amewashirikisha

wahusika wake zaidi katika kutenda na kusema kuliko kusema pekee. Utafiti wake ni tofauti na

huu kwa sababu sisi tumejikita katika matumizi ya lugha ya kimafumbo.

Utafiti huu utahakiki lugha ya kimafumbo katika riwaya za Katama Mkangi, Mafuta (1984) na

Walenisi (1995), kwa sababu kipengele hiki cha matumizi ya lugha ya kimafumbo

hakijashughulikiwa kwa kina. Aidha, kuna viwango mbalimbali vya mafumbo vinavyotumika

katikauwasilishaji wa kazi za fasihi.

1.9 Mbinu za Utafiti

Mbinu za utafiti humsaidia mtafiti katika kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data ya utafiti

. wake. Mbinu hizi ni kama zifuatazo.

1.9.1 Muundo wa Utafiti

Utafiti huu ulitegemea muundo wa maelezo. Matokeo ya utafiti yalitolewa kwa maelezo kwa

kuangazia matokeo ya utafiti yaliyopatikana kutokana na kusoma makala muhimu ambazo

(31)

namna mtunzi alivyotumia vipengele vya lugha teule vinavyohusishwa katika kusawiri na kutoa ujumbe wake.

1.9.2

Mahali Pa Kufanyia .Utafiti

Utafiti huu ulifanyiwa maktabani. Utafiti wa maktabani ulinuia kupata data kutokana na usomaji mpana wa riwaya teule. Ulijikita katika kusoma kwa kina riwaya mbili za Katama Mkangi, Mafuta (1984) na Walenisi (1995), na yale yaliyoandikwa kuhusu lugha ya kimafumbo na vilevile riwaya za Kiswahili. Mtafiti alisoma makala na machapisho yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti kama vile: tasnifu, majuzuu, vitabu, magazeti na majarida. Aidha, makala na vitabu

vinavyoeleza kuhusu nadharia ya kimafumbo ya kisasa vilisomwa. Machapisho mengine muhimu yalisomwa ili kuimarisha suala la utafiti na mbinu za utafiti. Usomaji wa maktabani ulimwezesha mtafiti kusoma kwa kina na kuchambua mbinu za lugha ya mafumbo alizotumia mtunzi katika riwaya hizi mbili.

1.9.3

Uteuzi wa Sampuli

(32)

1.9.4 Ukusanyaji wa Data

Mbinu iliyotumiwa kukusanya data ya utafiti huu ni usomaji wa maktabani; kusoma kwa kina

riwaya zilizoteuliwa kisha kunukuu sehemu ambazo zina matumizi ya vipengele vya lugha ya

kimafumbo, aidha, data hii ilikusanywa kwa kuzingatia malengo ya utafiti. Mbinu hii ilitosheleza

data ya utafiti huu.

1.9.5 Uchanganuzi wa Data

Utafiti huu ulitumia data iliyokusanywa kutoka kwa maandishi ya wasomi tofauti tofauti,

majarida na majuzuu yanayohusiana na mada na kutoka kwa vitabu teule ili kutathmini lugha ya

kimafumbo. Data iliainishwa na kupangwa kulingana na matumizi ya vipengele vya lugha ya

kimafumbo. Aidha, utafiti umechanganua lugha ya kimafumbo ilivyotumiwa kwa kuzingatia

vipengele vya methali, majazi, jazanda, tashbihi, istiari, taswira na misemo, vilevile, namna

vipengele hivi vimeathiri usawiri wa wahusika. Aidha, utafiti huu umezingatia malengo ya

utafiti, maswali ya utafiti na mihimili ya nadharia ya kimafumbo ya kisasa.

1.9.6 Uwasilishaji wa Data

Data iliyokusanywa iliwasilishwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia malengo ya utafiti na

mihimili ya nadharia ya kimafumbo ya kisasa iliyoongoza utafiti huu. Matokeo yameonesha

namna mtafiti ametumia mifano yenye kurejelea jinsi vipengele vya lugha ya kimafumbo

vimettimiwa katika vitabu teule.

1.9.7 Changamoto

Katika utafiti huu tulikabiliana na tatizo la ukanganyifu wa dhana ya mafumbo. Katika utafiti

huu tuligundua kuwa dhana ya mafumbo inakanganya kwa jinsi wataalamu mbalimbali

(33)

kuwasilisha ujumbe. Wataalamu wengme wanafafanua mafumbo kama mbinu mbalimbali

ambazo hutumika kuwasilisha ujumbe kwa njia fiche. Utafiti huu ulishughulikia lugha ya

kimafumbo kamba vipashio mbalimbali ambavyo huwasilisha ujumbe kwa njia fiche.

Aidha tulikumbana na tatizo la tafsiri. Tatizo hili lilijitokeza sana has a katika kushughulikia

nadharia.Machapisho katika lugha ya kiswahili yanayozungumzia nadharia ya kimafumbo ya

kisasahayapo. Ililazimu kutegemea machapisho na vitabu vya kiingereza kupata data toshelevu.

Aidha, haikuwa rahisi kupata baadhi ya visawe ili kupata maana kamili kwa sababu baadhi ya

visawe vilipoteza maana wakati wa kutafsiri. Rata hivyo, mtafiti alitumua kamusi mbalimbali

pamojana kutafuta usaidizi kutoka kwa wataalamu wa lugha, ili kusuluhisha tatizo hili.

1.10 Muhtasari

Sura hii imeshughulikia utangulizi, swala la utafiti, malengo pamoja na maswali ya utafiti.

Vipengele vingine ambavyo vimeangaziwa hapa ni upeo na mipaka, sababu za kuchagua mada,

misingi ya nadharia ya kimafumbo ya kisasa pamoja na mihimili yake na yaliyoandokwa kuhusu

mada. Mwisho, mbinu za utafiti zimeangaziwa ambapo vipengele vifuatavyo vimeshughulikiwa:

muundo wa utafiti, mahali pa kufanyia utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data,

uchanganuzi wa data na hatimaye uwasilishaji wa data. Katika sura inayofuata vipengele vya

lugha ya mafumbo ambavyo ni jazanda, taswira, ishara na majazi vimeshughulikiwa.

idha, utafiti huu umezingatia sura tano kama ifuatavyo: Sura ya kwanza imejumuisha:

utangulizi wa utafiti, suala la utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua

mada, upeo na mipaka ya utafiti, yalioandikwa kuhusu mada, misingi ya nadharia na mbinu za

utafiti na changamoto za utafiti. Katika sura ya pili mtafiti amefafanua matumizi ya jazanda,

(34)

tashbihi, tashihisi na tasifida katika sura ya tatu. Katika sura ya nne mtafiti amechunguza namna

matumizi ya lugha ya kimafumbo yameathiri usawiri wa wahusika. Sura ya tano ni hitimisho na

mapendekezo kutokana na uchanganuzi wa matokeo kuhusu matumizi ya lugha ya kimafumbo

(35)

SURA YAPILI

LUGHA.YA MAFUMBO NA UHAMISHAJI MAANA KATIKA RIWAYA

ZAMAFUTA

NAWALENISI

2.1 Utangulizi

Sura ya kwanza ilizingatia mambo ya kimsingi kuhusiana na utafiti. Haya ni pamoja na ufafanuzi

wa istilahi muhimu, utangulizi wa utafiti, suala la utafiti, malengo ya utafiti pamoja na maswali

ya utafiti. Vipengele vingine vilivyoshughulikiwa ni sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka,

misingi ya nadharia na yaliyoandikwa kuhusu mada. Hatimaye, sura ilishughulikia mbinu za

utafiti, mbinu za ukusanyaji data, uchanganuzi wa data, uteuzi wa sampuli na uwasilishaji wa

matokeo.

Sura hii inafafanua namna mtunzi wa riwaya teule alivyotumia vipengele vya lugha ya mafumbo

ambavyo ni jazanda, taswira, majazi na taashira kwa njia ya kipekee katika uwasilishaji wa

ujumbe wake. Umuhimu wa kutumia vipengele hivi katika riwaya ni kusawiri mawazo ya mtunzi

kwa kina kirefu zaidi kwa sababu matumizi ya vipengele hivi: jazanda, taswira, majazi, na

taashira humpa msomaji viwango vingi vya ufasiri na ufahamu. Lugha ya mafumbo ni dhana

inayohusisha tamathali mahsusi na ulinganishi unaodokezwa katika mafumbo hayo ni wa lugha

ya kitamathali Chapman (1973).

Hivyo, mtunzi huteua kauli ambazo hutumika katika uwasilishaji wa ujumbe wake, mtunzi

huelewa ni kauli zipi zitakuwa na athari anazokusudia kwa wasomaji wa kazi yake. Katama

Mkangi aliandika vitabu teule wakati ambapo utunzi uliokashifu serikali haukukubaliwa, hivyo

(36)

Isitoshe, Hawkes (1972) anafafanua lugha ya mafumbo kama kauli zinazoweza kutumiwa kama ishara zinazoweza kupata maana kutokana na miktadha ya kijamii, tajriba ya watu, mazingira yao na utamaduni wao. Lugha ya mafumbo ni lugha ambayo haimaanishi kile inachosema. Lugha ya kimafumbo haitumii maana halisi ya maneno mbali huchukua maana ya kitamathali.

Kuna uhamisho wa maana katika lugha ya mafumbo.

Kwakufafanua zaidi, Lakoff (1993) amethibitisha kuwa lugha ya kimafumbo huweza kujitokeza kama jazanda, majazi, taashira, taswira na semi nyingine. Hii inatokana na kuwa lugha inayotumiwa katika mbinu hizi za lugha haieleweki moja kwa moja, yaani huwa na maana fiche. Aidha,huweza kuwa na uwili au vivuli vya maana ili kumpa msomaji jukumu la kufasiri. Lugha ya aina hii huongezea kazi ya kifasihi ladha. Vijenzi hivi vya lugha ya mafumbo vitaangaziwa katikasura hii, navyo ni:jazanda, majazi, taashira na taswira.

2.2 Taswira Katika Ujenzi wa Mafumbo

Taswira ni rnkusanyiko wa picha ambazo zinaundwa na maelezo ya msanii katika kazi ya fasihi. Msokile (1993). Taswira hizi huweza kuundwa kwa kirai au neno. Msokile anaeleza kuwa, taswira hujengwa kutokana na matumizi ya tamathali za usemi haswa sitiari, tashbihi na ishara mbalimbali ambazo zinahusu mawazo, dhana, vitu au maumbile. Ujenzi wa taswira humfanya msomaji apate aina mbalimbali za hisi zinazoshughulikiwa na kazi ya kifasihi.

(37)

mahali, hali, na vitu kwa kutumia ishara. Picha hizi za kimaelezo hutokana na matumizi ya tamathali za usemi haswa tashbihi na sitiari. Pia hujengwa kwa kutumia methali, vitendawili na misemo ya kawaida. Picha hizi zenye mnato hutumiwa na mtunzi kutoa taarifa fulani. Kwa mfano,kuna picha fulani inayoweza kutokea akilini mtu anaposoma aukusikia methali 'baada ya dhiki faraja' au tashbihi 'ni mfupi kama nyundo' hivyo, taswira hujengwa kupitia maelezo au tamathali mbalimbali.

Wataalamu wa fasihi wameibuka na njia mbalimbali za kuainisha taswira. Kwa mfano, Senkoro (1982) anatambua makundi matatu ya taswira: taswira zinazoonekana, taswira za mawazo na taswira za hisi. Taswira zionekanazo ni zile ambazo zinatumia ishara zinazoonekana ambazo pia ni taswira za kiishara. Aghalabu taswira hizi huambatana na matumizi ya tashbihi na sitiari. Taswira za mawazo ni za kidhahania ilhali taswira za hisi huibua hisi fulani mawazoni.

Wataalamu wengme wamependekeza uainishaji tofauti. Kwa mfano Kezilahabi (1992) amependekeza makundi matatu ya taswira lakini anatumia mtindo tofauti. Makundi haya ni: taswira za maumbile yaani hali ya hewa angani, hali ya nchi juu ya ardhi, taswira za viumbe yaani watu na wanyama wa mwituni na mwisho taswira za viumbe wasiokuwa na mwili kama

majini,mashetani na kadhalika.

Vilevile, Wamitila (2003) anatambua aina mbili kuu za taswira; taswira za kimaelezo na taswira za kiishara, za kimaelezo hujengwa kutokana na maelezo ya mwandishi. Hata hivyo, hazihitaji kutambuliwa kwani hakuna maana fiche au maana ya ziada. Nazo taswira za kiishara huunda picha iliyo na ujumbe uliofichika au ujumbe wa ziada, hivyo ishara hizi huhitaji kufumbuliwa kwani huwa na maana wasilishi iliyo tofauti na maana asili ya neno. Wazo hili limetokana

(38)

Kwa kuchangia, Wamitila amebainisha taswira nyingine: taswira kuu, taswira za kimsingi,

taswira za uoni, taswira za harufu au mnuso, taswira za joto, taswira za mguso, taswira za

mwonjo, taswira za mwendo na taswira za usikivu. Aidha, taswira za kiishara hujengwa katika

akili ya msomaji kutokana na uteuzi wa lugha ya mwandishi kama taswira za kimaelezo lakini

zina ujumbe uliofichika. Kimsingi taswira hizi hufanya kazi kama ishara. Hali kadhalika, taswira

zinazojengeka ndani ya tamathali za usemi ni zile zinazotumia tashbihi, sitiari, jazanda, misemo,

na vitendawili katika kuchora picha inayokusudiwa. Taswira hizi huambatana na ishara za

kufumba na kujificha ndani ya tamathali za usemi kama tashbihi, sitiari, jazanda, methali na

zmgme.

2.2.1 Taswira katika Riwaya ya

Walenisi

Kupitia kwa maelezo mbalimbali, mwandishi ameweza kuchora picha akilini mwa msomaji.

Kwanza,maelezo kuhusu namna hakimu alivyoingia mahakamani, " ... aliingia kama malaika wa

mauti ... alipoingia tu na watu kuamriwa kuketi, yule hakimu aliegemeza miwani yake ya nusu

glasi puani kwake. Huku akimtazama kwa ile sehemu iliyokuwa wazi ..." (uk. 1), maelezo haya

yanaibua picha akilini mwa msomaji ya namna hakimu alivyokuwa.

Taswira nymgme inadhihirika wakati ambapo mwandishi anatoa maelezo ya sayan

iliyokusudiwa kumwangamiza Dzombo. Kwa mfano, kulikuwa na giza, kulikuwa na mwanga wa

kitaa kidogo kiambazani. Tunaelezwa kuhusu mtambo mtu, na wakati Dzombo anapoelezwa

.kuhusu jinsi ya kuutumia mtambo mtu na wakati Dzombo anapoelezwa jinsi ya kuitumia sayari,

"Unazo dakika tano tu Angalia maelezo ya kuiendesha hapo mbele yako, ... na hii nuru ya

taa ikigeuka kuwa nili " (uk. 7). Taswira hii inamwezesha msomaji kuelewa hali halisi

(39)

Taswira nyingine inapatikana pale sayari iliyokusudiwa kumwangamiza Dzombo inapong'oa

nanga, "...sayari ilijing'oa baada ya ndimi nyeupe za moto kuonekana zikifyatuka kutoka

tumboni mwa ardhi na kuifunika ... Nao ulikikuwa moto mkali mno kuuwezesha kuonekana hata

kama mtu alikuwa amefunga macho yake." (uk. 8). Maelezo haya yanamfanya msomaji kupata

picha ya namna hali ilivyokuwa wakati sayari ilipaa angani.

Kupitia mawazo ya Mtu Dzombo mwandishi anatuchorea picha ya namna Mtu-Binti Fikirini

alivyokuwa, huenda kutokana na sura yake Mtu Dzombo alimtamani "...ngozi yake nyeusi

ilikuwa laini. Joho lake la hariri lilikuwa hafifu na lililomganda mithili ya ndizi na ganda lake.

Mwana mwenye meno meupe yaliyopangika. Macho ya kobe ya kurntwaza mtu ..." (uk. 49).

Msomaji anaweza kuona narnna msichana huyu alivyopendeza.

Mtu Dzombo alirnhurumia zaidi Mtu-Binti Fikirini kuliko Mtu Wazo, kutokana na kudhoofika

kwake alikumbuka namna alivyopendeza kabla ya safari ya utu, "Nywele laini za komvi. Uso wa

moyo na macho ya gololi meupe. Nyusi nyembamba za kubeta pamoja na kope za paka. Pua

ndogo nyepesi, midomo ya kuiva, meno yaliyokaa sambamba, meupe ... shingo la ninga, maziwa

ya wastani ... , kiuno cha kuviringika. Si mrefu wala si mfupi... alikuwa mrembo siyo mzaha."

(uk. 62) Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kuwa Mtu-Binti Fikirini alikuwa mrembo sana na

anaonekana akimvutia Mtu Dzombo.

Mwandishi pia anatuchorea taswira ya Mtu Dzombo na Mtu-Binti Fikirini baada ya safari ya utu.

Dzombo alijiona akiwa na sura ya kupendeza, ya kuvutia na kiwiliwili kilichonjengeka, uchovu

ulikuwa umemtoka. Hali hii ni tofauti na mwenzake Mtu Binti Fikirini. Mwandishi anatuchorea

sura ya binti Fikirini kama aliyekonda na kuwa kinyanya kikongwe. Hii ilitokana na kuwa

(40)

na blanketi tatu za kujisitiri baridi, tofauti na wenzake waliozongwa na kiu, njaa na baridi, na

kuchangia kubadilika kwao kiafya. " ... lakini sio wenzake. Wao walionekana wameparara na

kusinyaa..." (uk.54)

Mwandishi anatoa maelezo yafuatayo kumhusu Binti Fikirini, " ...marashi ya Mtu Binti Fikirini

yalimwingia mpaka mishipani. Harufu yake ilikuwa inanukia kivyake. Hakuwa amewahi kunusa

manukato sampuli hiyo maishani mwake ... Haya yalikuwa ya kipekee. Yalikuwa ya aina ya

"Jua-Tujuane" (uk. 63), maelezo haya yanamfamya msomaji kuona na vilevile kunusa uzuri wa

marashi hayo.

Taswira nyingine inayojitokeza, ni wakati Dzombo na maskini Jeuri wanapowakisha kibatari.

Mwandishi anaelezea kinagaubaga, yanayojiri wakati moto unapowashwa na kuripuka.

Mwandishi anatupa taswira ya alipokuwa karibu nao Dzombo. Maji yalikuwa meupe, kulikuwa

na nyasi, misitu, aina ya miti mikubwa kwa mbali.

Taswira zilizofafanuliwa zimechangia kwa upana, kukuza maudhui katika riwaya hii. Taswira ya

Mtu-Dzombo na Mtu Binti Fikirini baada ya safari ya utu, inadhihirika wazi kuwa Dzombo

hakuwana utu yaani alikuwa mbinafsi. Ubinafsi ni hali ya mtu kujipenda mwenyewe na

kutowajali wengine. Ubinafsi hujitokeza sana katika mifumo ya kiutawala ya umwinyi na

ubepari. Mwandishi anatuwasilishia taswira hii wakati Dzombo alipewa maji, blanketi na mkate,

alivitumia bila kujali wenzake ndio maana walikuwa wanyonge. Maudhui ya ubinafsi na utu

yanakuzwa kupitia taswira hii.

Aidha, taswira tunayopata kutokana na namna hakimu anavyoingia mahakamani, na namna

baada ya kusimama tu anatamka 'kifo'(uk. 1), inadhihirisha maudhui ya dhuluma. Dzombo

(41)

mahakama hazikuwa zikifuata sheria kwa mujibu wa kulinda, au kutetea, wala kudumisha haki

za kibinadamu. Kazi yake kubwa ni kumtia hatiani yeyote. Hakimu anapoingia tayari ameamua

hukumu yake. Dzombo alipigwa na butwaa kwani hakutarajia hukumu aliyopewa. Taswira hizi

zinafanya akili ya msomaji kutalii ulimwengu halisi kwani picha anayopata inamkumbusha

tajriba zake katika ulimwengu halisi.

2.2

.

2 Taswira katika Riwaya ya

Mafuta

Kupitia mbinu hii mwandishi ametuchorea picha ya akilini kuhusu matukio mbalimbali kutoka

kwenye riwaya. Kwa mfano, mwandishi ametuchorea picha ya jinsi Jali alivyojinasua kutoka

kwa umati uliokuwa ukitaka kumwangamiza. Mwandishi anatuelezea kuwa Jali alifyatua teke la

kipunda, umati ukarudi nyuma. Alivua koti lake haraka na kulitupa matawini, kisha akaruka juu

nakuwashtua watu, hali iliyosababisha wajigawe na kumpatia nafasi ya kuchopeka vya ajabu

kama swara, (uk. 5).

Taswira nyingine ni kumhusu mtu aliyelala matopeni. Mtue alipokuwa akisozana na kidimbwi

cha matope alikutana na mtu aliyekuwa amelala matopeni. Mwandishi anaibua hisia akilini

mwetu kwa kumsawiri mhusika huyu akiwa matopeni. Anatupiwa kila aina ya uchafu;

kukojolewa na kutupiwa kikohozi, (uk. 8). Mhusika huyu anaitwa Matope na sifa hii ya kimajazi

inampa msomaji taswira kamili ya alivyokuwa.

Mwandishi pia amewasilisha taswira ya makazi ya Ti, kupitia kwa mhusika Mtue. Mtue anasema

kuwa chumba kilikuwa cha kuvutia. Madirisha mawili mapana sana yenye urefu wa kuanzia

sakafuni mpaka darini. Mandhari ya nje ya kijani kibichi yalikuwa ya kupendeza. Hali hii

(42)

Mwandishi ametoa maelezo ya kimaumbile ya mtu aliyeamkuana na Ti kupitia kwa mhusika Mtue. Mwandishi amemsawiri kama pande la mtu lilokuwa likimeremeta kama jongoo. Mashavu

yake yalikuwa makubwa na ya kuvimba. Turnbo kubwa kana kwamba limebeba mimba nne,

utosiwake ulikuwa kama uwanja wa ndege, macho meupe na kiuno chembamba. Kwa kifupi maelezo haya yanatupa taswira ya jinsi mtu huyu alivyokuwa mnene na mfupi, (uk. IS).

Aidha, maelezo ya Mama Fofi kuhusu tofauti ya maisha yake na ya mumewe yanatupa taswira

ya matabaka mawili ya kimalezi. Mwandishi amewasilisha mazingira ya umaskini aliyozaliwa

Sifa. Sifa alizaliwa katika mazingira ya ukame na walikuwa watu hohehahe. Alizaliwa ngozini

ya mbuzi na nyumba ya nyasi isiyo madirisha. Alichunga mbuzi na kondoo na kufanya kazi ya

uwindaji. Naye Mama Fofi alizaliwa katika mazingira ambayo hayakuwa magumu. Wazazi wake

walimfundisha jinsi ya kumhudumia atakayekuwa mumewe, alielekezwa jinsi ya kuwa mtiifu,

mchekevu na mvumilivu kwa mume atakayemwoa.

Mwandishi amechora picha ya mandhari ya nyumba ya Msati kupitia kwa mhusika Ti. Ti

anapofika nyumbani kwa Msati anatueleza kuwa kibatari kilikuwa kiking'arisha ndani na moshi

wake wa mafuta taa ulikuwa umetapakaa kote ndani. Nyumba ilikuwa imeezekwa kwa

matambara ya plastiki. Mabati mabovu na mabaki ya makadibodi. Kulikuwa na meko na

matabarajuu ya ulingo. Kupitia maelezo haya mwandishi ametupa maisha au hali duni anayoishi

Msati.

Kupitia kwa taswira zilizobainishwa mwandishi amefaulu kuwasilisha maudhui kadhaa. Taswira

ya mtu aliyelala matopeni inaendeleza maudhui ya umaskini, Hawa ni watu ambao hawana

makaoyaani tabaka la chini. Mwandishi anasema kuwa mtu huyu anatupiwa kila aina ya uchafu;

(43)

alikuwa masikini hohehahe. Hakuwa na budi ila kulala matopeni kwa kuwa hakuwa na mafuta.

Aliishi matopeni ambapo ni mahali pa mabata, kuku na vifaranga vyao.

Watu kama Ti wanaishi katika mazingira ya kifahari. Taswira hii ya makazi ya Ti inaibua maudhui ya matabaka katika jamii. Tabaka la juu kama familia ya Ti inaishi raha mustarehe. Tabaka hili la wateule linaishi maisha ya anasa na raha bila kukosa chochote. Mkao yao ni ya kifahari na vilevile maisha yao. Watuwaliokuwa na mafuta kama Ti ni wa tabaka la matajiri

lakini waliokosa mafuta kama Matope ni masikini hohehahe wa tabaka la chini.

Mandhari ya nyumba ya Msati ni picha ya ufukara. Kupitia mhusika Ti mwandishi ametuchorea

.picha ya jinsi nyumba ya Msati ilivyo duni. Kwa mfano, nyumba hii ilikuwa imeezekwa kwa

matambara ya plastiki, mabati mabovu na mabaki ya makadibodi. Msati ni kielelezo cha watu ambao wanaishi katika ufukara katika jamii. Mwandishi ameibua taswira ya namna umaskini ulivyokithiri katika tabaka la chini la wahusika kama Msati. Hali kadhalika, taswira ya Matope alipokuwa amelala matopeni, hana makazi na anakosa mahitaji mengi ya kimsingi, inadhihirisha namna mwandishi alijaribu kuonyesha jinsi umaskini umekita mizizi katika jamii.

2.3

Majazi kama Mbinu ya Kujengea Mafumbo

Majazi ni utumiaji wa majina yanayobaini taarifa au hali ya maisha ya mhusika au miji au kati ya

kitu, maelezo haya ni kulingana na Mazrui (1981). Majazi ni mbinu anayotumia mwandishi kuwapa wahusika wa kazi yake majina yanayodokeza sifa na tabia zao. Vilevile majina ya mahali, miji au vitu hutumiwa kimajazi. Senkoro (1982) anatumia dhana ya majazi kuitafsiri

(44)

ambazo maana yake hufasiriwa katika kiwango kingine cha simulizi, hivyo basi, kulingana na

senkoro majazi ni sitiari ndogo ambayo ni kidokezo cha hali nyingine kubwa na nzima

iliojificha.

Kwa kuzingatia maana hii majazi ni ishara ya kile ambacho hakibainiki wazi kwa sababu

inatubainishia ya kwamba kuna kile kilicho dhahiri na kile kilichojificha. Hivyo, inasadifu kuwa

majazi hubainisha maana isiyo dhahiri bali ni fiche. Licha ya kuwa kuna maana ya juu ya hadithi

husika; ina maana kuwa matumizi ya mbinu ya majazi ni mfano wa uandishi ambao hukusudia

usomaji, ufahamu na ufasiri wa kazi ya fasihi katika viwango tofauti tofauti. Viwango hivi

vinaweza kuwa viwili au zaidi. Hivyo, huwa kwa maana ya kijumla na maana finyu.

Harris (1992) ameeleza ya kwamba majazi ni usemaji wa kitu kimoja huku ukimaanisha kitu

kingine ambapo maana ya ndani inahusishwa na maana ya juu kwa kiulinganifu. Maoni haya

yanakubaliana na ya Wafula ya kwamba majazi ni hadithi yenye fumbo fulani. Hadithi ya majazi

ni kinyume cha hadithi za ajabu na za kubuni ambazo zinakusudia kuchangamsha na

kumfurahisha mtu. Hivyo, kazi ya kimajazi huwa si njia ya kujifurahisha bali njia ya mwandishi

kuweza kuifunza jamii maana ya masuala mazito yanayoihusu jamii.

Wamitila (2003) anasema majazi ni mbinu ya kuwapa wahusika majina ambayo yanaakisi au

yanayotuelekeza kwenye wasifu wa tabia zao. Jina la mhusika linakuwa kielekezi cha tabia yake,

majazi,huhusisha sifa za majina ya mahali, mandhari na mengine. Pili, mwandishi anaweza

kutumia mbinu hii kuuchimuza mtazamo na mwono wake kuwahusu wahusika fulani na hata

(45)

Wataalamu wametumia dhana na maelezo mbalimbali kueleza dhana ya majazi. Imebainika kuwa dhana hii ina maana mbili bayana. Utafiti huu umezingatia maana ya kuwa majazi ni upatianaji majina katika kazi ya fasihi kwa kuzingatia sifa na tabia za wahusika.

2.3.1Majazi katika Riwaya ya

Walen

i

si

Majina mengi katika riwaya hii ni ya kimajazi, kwa mfano Mzee Mtu-Mwenzio ambaye ndiye

kiongozi wa familia inayompokea Dzombo baada ya sayari kutua. Mwenzi ina maana ya rafiki. Aghalabu tunamwona Mzee Mtu- Mwenzio akimjali sana na kumshughulikia Dzombo. Anampa Mtu- Binti Fikirini na Mtu-Wazo waandamane naye katika safari ya utu. Anamchukulia mtu Dzombo kama mwanawe kwa kumuuliza kuhusu mapokezi ya mtu wazo na wenzake walivyokuwa.

Mama Mtu-Maanani ni jina la kimajazi. Maana ni kutafsiri, jambo lisiloeleweka vizuri, heshima au busara. Katika riwaya hii, tunamwona Mama Mtu-Maanani akimkaribisha Dzombo katika familiayake kwa moyo mkunjufu. Maongezi yake kwa Dzombo ni ya heshima na pia anagundua kwa haraka dalili za mtu Dzombo kumpenda bintiye Mtu binti Fikirini.

Fikirini ni dhana ya kutumia ubongo ili kutatua jambo fulani. Mtu Binti Fikirini amejaliwa na akili tambuzi ambazo zinamsaidia kugundua mambo na pia kuyatatua kwa urahisi. Yeye ni mkurugenzi wa kiwanda cha trimi licha ya kuwa yeye ni mwanarnke. Anasisitiza kuwa wao wana akili tambuzi kuliko Wachuna hivyo basi wana uwezo wa kuendeleza maendeleo. Kivulana Mtu Tabia ana tabia njema kama lilivyo jina lake. Anapozungumza na Dzombo anatumia maneno ya he shima, "Tafadhali nakuomba ... "

(46)

maanaya tunda mbichi la mzabibu na kulingana na wawalenisi rika hili lilijumuisha watoto, watoto hawajakomaa kama lilivyo tunda hili.

Hani alikuwa mkewe Dzombo huko duniani, jina hili ni la kimajazi kwa namnambili. Kwanza, hani lina maana ya kumpa pole aliyefiwa. Tunapochunguza katika riwaya Dzombo ana wasiwasi kuwa baadhi ya marafiki zake, katika harakati za kumfariji wakachukua nafasi yake na kumdhulumu kimapenzi. Hani pia limetoholewa kutokana na neno la kiingereza 'honey' ambalo hutumiwa mno na watu wawili wenye mahusiano ya kimapenzi, kama ilivyokuwa baina ya Dzombo na mkewe hani.

Wachuna walikuwa watawala wa ualenisi, ambao waliwadhulumu na kula jasho la wawalenisi. Inadhihirika kwenye wimbo unaoimbwa na vijana wakiwa kazini au kupitia kwa maelezo ya Fikirini kwa Dzombo. Nomino Wachuna limetokana na kitenzi 'kuchuna' yaani kutoa ngozi ya

I

mnyama. jambo hili linaashiria kwamba, wachuna walikuwa wakiwanyanyasa wawalenisi. ~

~ Hawa Wachuna kama lilivyo jina lao ni wanyanyasaji wanaowanyanyasa wanyonge katikajamii.

Mhusika mwingine ambaye jina lake limetumika kimajazi ni Bwana Shibe. Shibe ina maana ya aliyeshiba au tajiri. Hili linadhihirika kupitia kwa msimamo wake mkali tofauti na Dzombo anayeamini kuwa kifo ni kimbilio la umaskini. Maskini Jeuri ni maskini sawa na Dzombo lakini

anatumia ujeuri na kumpa Dzombo changaa kama mafuta ambayo yanalipuka kusingizia kuwa au kumzindua kuwa taa yao ni chang'aa.

(47)

wengine, baada ya safari hii anaanza kutumia maneno ya he shima kama 'asante' na kukosa kuwa

na ubinafsi. Jina hili Mtu ambalo wawalenisi wanapewa linaashiria mtu aliye na utu.

Majazi kama mbinu ya kimafumbo imechangia katika kuendeleza maudhui mbalimbali, mfano

maudhui ya utu. Familia ya Uwalenisi ilikuwa imejawa na utu haswa tukichunguza uhusiano kati

ya Mtu- Dzombo na familia ya Mama Mtu-Maanani. Ndiyo maana majina yao huambatanishwa

na neno utu, kumaanisha kuwa wana utu kwa mfano, Dzombo alikaribishwa vizuri na Mtu Binti

Fikirini. Kupitia kwa wachuna mwandishi ameendeleza maudhui ya dhuluma au unyanyasaji.

Wachuna kama lilivyo jina lao wanawadhulumu na kuwanyanyasa wanyonge. Wachuna hawa ni

.viwakilishi vya vyongozi wabaya katikajamii halisi, hii ni kutokana na sifa zao za unyanyasaji.

2.3.2

Majazi katika Riwaya ya

Mafuta

Wahusika wengi katika riwaya ya Mafuta wamepewa majina kulingana na sifa zao. Mbinu hii

inajulikana kama majazi. Kwa mfano, mhusika Matope. Maana ya matope ni udongo wa

majimaji yanayonata. Aghalabu neno hili huashiria uchafu. Matope wanakutana na Mtue akiwa

kwenye kidimbwi cha matope. Mtu alikuwa akizunguka hapa na pale akisozana na kidimbwi cha

matope. Anavuta makohozi na alipokuwa tayari kuyatema ndipo anamwona Matope. Mtue

anaona kuwa mahali pale ni pa bata, kuku na vifaranga ambao ni viumbe duni lakini si pa

binadamu.

Matope anapoingia mahakamani kushtakiwa, Mtue anamkumbuka alipokutana naye akiwa na

matope yaleyale lakini wakati huu yalikuwa yamekauka na kuwa makavu. Nywele zake zilikuwa

na vilimalima vya udongo. Matope yalikuwa kila mahali si shingoni, ki fuani, kiunoni na

(48)

mfano,kuendesha, kwa sababu ya uchafu aliokuwa nao. Ndwele hizi zinaashiria matatizo yanayotokana na umaskini uliokithiri.

Matope anapata riziki yake kwa kuchakura masaza ya chakula kutoka kwa mapipajaa. Akiwa

mahakamanianasema kwamba, "tumezaliwa matopeni, tumezaana matopeni, tumekufa matopeni

na tukazikana matopeni." (uk. 39). Kama lilivyo jina lake Matope anajiingiza katika uchafu wa

kila aina ili kukithi mahitaji yake. Mfano mwingine wa majazi ni Dubwana. Dubwana

anapoingia mahakamani anafanya umati kusitiza kumpiga Matope mara moja. Kwa sababu umati

unamwogopa. Matope anaeleza kuingia kwa Dubwana namna hii, " ... wakati huu vicheko

viliishia midomoni kwani ni hapo lile njemba lilipoingia" (uk. 41). Dubwana alibatizwajina hili

na Matope kutokana na umbo lake nene. Dubwana ina maana ya mtu aliye na umbo kubwa lisilo

la kawaida. Alipewa jina hilo kulingana na ukubwa wake. Dubwana anaingia mahakamani na

kumnusuru Matope kutokana na kipigo cha umati, kwa kuogopwa tu Matope anasema, "..kutisha

kwajibaba hili hakukuweza kufichika ..Ikiwa walionyesha ishara yote ya kurnheshimu basi

ilikuwa ni kwa shauri ya uoga basi si kwa eti walikuwa wakimpenda."(uk. 41). Ukatili wa

Dubwana hili unadhihirika pale linapornhukumu Matope kunyongwa ili awe kielelezo kwa

wengme.

Sifa ni rnhusika mwingine ambaye amepewa jina la kimajazi, alikuwa mumewe Mama Fofi. Neno sifa lina maana mbili, maelezo yanayoonyesha utafutaji wa kiwango cha wastani cha hali

ya

mtu kama vile uzuri. Pia linaweza maanisha mafuta yanayotokana na samaki. Lakini rnhusika

Sifa ametumiwa kimajazi. Kwanza, yeye anasifika sana. Mkewe anasema, "kwenda kuwinda na

(49)

yake,Sifa anajikakamua na kufikia kilele cha hata kununu mafuta. Alikuwa amefikia kiwango chakuwa mwanakandarasi mkubwa wa kumbikumbi na hata kuwaajiri watu wengi.

MhusikaJali ana jina la kimajazi. Jali ambalo linamaanisha karata au kadi zinazotumika katika michezo hii. Mwandishi amemchora Jali kama mhusika mjanja na anayetumia akili kuchezea

wengine shere. Mfano, anachukua nazi moja kutoka kwa mwenye kunazi na kuwaambia kina Kazamoyo kuwa alikuwa akitaka kuonja nazi moja. Hapa tunamwona mhusika huyu akitumia ujanja kumwimbia mwenye kunazi licha ya kuwa hakuwa na pesa za kulipia, hakujua kuwa mwenye mali alikuwa akijifanya kuwa amelala na alikuwa akiona kilichokuwa kikiendelea, anaamkana kumnasa Jali mkono na kumwambia, "mwizi leo nimekushika." Jali anajisalimisha kutoka kwa umati uliokuwa ukitaka kumwangamiza kwa kutumia ujanja wake. Mwandishi anasema kuwa, alifyatua teke la kipunda, watu wakarudi nyuma, akavua koti na kulitupa matawini, umati ukarudi nyuma, akaruka juu, watu wakashtuka na kujigawa, akapata njia akachopoka. Jail anajali na kuchukua tahadhari kabla ya hatari, huyu ni mhusika mjanja.

(50)

turnbo.Njia hii ya Msokoteni imefananishwa na msokoto wa tumbo kwa sababu ni ya kutesa. Ti

anatesekasana anapoipitia.

Vilevile kuna mhusika anaitwa Chanzo. Chanzo ina maana ya sababu au kiini. Yeye ni kitinda

mimbakatika familia inayozungumziwa kwenye hadithi ya Mbeyu. Yeye aliasi mtindo wa

kusomamaombi ya chakula kama walivyofanya nduguze na kubuni maombi yake mwenyewe.

Mtindowa maombi ya nduguze uliwasifu wazazi wao na kazi zao licha ya kuwa hawakuwa

wakifanyakazi halali. Mtindo anaouasisi Chanzo, unawashukuru wafanyikazi waliohusika katika

uzalishaji wa chakula na kumsifu mama ardhi. Jambo hili linawakera wazazi wake. Hiki

kinakuwa chanzo cha masaibu ya Chanzo kwa sababu anafukuzwa na kutoka siku hi yo akaanza

kulamasaza pamoja na wafanyikazi wengine.

Aidha,mhusika mwingine anaitwa Gweni. Gweni ni jina ambalo limetokana na neno weni. Weni

niainayammea ambao majani yake huwasha na hufanyiza dawa ya kidonda. Tabia za mhusika

huyu zinaweza kufafananishwa na uwezo wa weni wa kutengeza dawa. Yeye anampa pole na

kumtuliza Ti kwa yaliyompata na kumpa matumaini. Anamwambia, "pole kwa yote." Pia

Gweni anawagawia chakula na kuwapa kopo kubwa la maji. Kwa kifupi mhusika huyu

amesawiriwa kama mtu mwenye kutuliza na kuposha. Bwagu na Bwaguzi ni majina ya kimajazi,

majina haya yametokana na pwagu na pwaguzi, ambao maana yake ni wezi. Kazi za wahusika

hawa ni kuhudumia miguu ya kitanda. Ingawa ni wawili , wanajidai kuwa wote ni wanne kwa

kubadilishana majina na kila mtu anahudumia miguu tofauti ya kitanda. Wanatumia ujanja

kuwafanya watu wateule. Kwa mfano, wanadai kuwa wana aina saba za mafuta lakini inabainika

wazi kuwa ni aina moja tu ya mafuta. Mafuta haya inabainika wazi kuwa ni mkojo wa paka na

(51)

Kadhalika,Kazamoyo lina maana ya kukaza moyo yaani kuendelea kufanya jambo fulani kwa matumaini. Kazamoyo na wenzake wanajikaza na kumaliza kusoma hadithi ya mafuta. Kazamoyoanawaambia akina Zuka wasife moyo, warudi ili watie juhudi zaidi kuyafahamu zaidi maanaya maandishi yale.

Mwandishi ameibulia na kuendeleza maudhui mbalimbali kupitia kwa mbinu hii ya majazi. Maudhui ya umaskini yanajitokeza kupitia kwa mhusika Matope, Matope kama lilivyo jina lake anaishimatopeni na kula masaza ya chakula kutoka kwenye mapipajaa. Hali hii inadhihirika pale anaposema kuwa wamezaliwa matopeni, wamezaana matopeni, wamefia matopeni na kuzikana matopeni. Kwa kutumia jina la kimajazi la mhusika huyu mwandishi amefaulu kupitisha maudhui ya dhuluma au unyanyasaji. Kwa kuwa yeye ni mtu duni katika jamii anadhulumiwa haswa pale mahakamani na Dubwana na pia hata umma. Hali yake ya matopetope inamnyima nafasi ya kuheshimika na hivyo basi anadharauliwa sana. Ndio maana umati uliokuwa mahakamani udai kupatwa na ndwele tofauti wakati Matope anapoingia.

Kupitia kwa mhusika Dubwana mwandishi amefaulu kuwasilisha maudhui mawili. Kwanza Dubwana kama lilivyo jina lake kimajazi ni mtu mnene. Inadhihirika wazi kwamba mhusika huyu amekula akashiba licha ya kuwa kazi anazofanya si halali. Maudhui ya haki na sheri a yanajitokeza hapa. Yeye anapata riziki kwa kuwanyanyasa wengine. Jitu hili pia ni katili. Maudhui ya udhalimu - yanajitokeza kupitia kwa jina la kimajazi la mhusika huyu. Anamnyanyasa sana Mtue mahakamani. Mtue hangeweza kufanya lolote kutokana na unene wa jitu hili.

References

Related documents

The fuzzy based expert system applied to the battery scheduling based on the measured real time data or forecasted data as follows: Time(T), The Battery State of

Figure 7 Highest posterior density (HPD) intervals for effects parameters fi tted to systolic blood pressure data collected on 188 mice from an incomplete diallel of Collaborative

Solanke, “ Protection and Monitoring Of Transformer Using Arduino” International Journal for Research in Applied Science & Engineering Technology (IJRASET), Volume 6 Issue

The goal of this paper is to present a general convergence and stability theory for approximation methods for the treatment of time dependent parameter identication problems

After 14 days, the inflammatory response to silk had increased whereas the tissue reactions to polyglyconate and polyglactin 910 had decreased slightly (Fig 2), although

As part of the defense-in-depth approach to information security (multiple layers of security controls), and a critical part of honeypot architecture, intrusion

simulations of present (2001-2005) and future (2026-2030) regional air quality are conducted with the newly released Community Multiscale Air Quality (CMAQ) model version 5.0 to

Android is the most popular OS in all over the world.The android OS has captured the 79.3 percent market share.But there are lots of security issues related to smart phones and