• No results found

Masuala ibuka katika riwaya za kisasa: kidagaa kimemwozea na mhanga nafsi yangu

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Masuala ibuka katika riwaya za kisasa: kidagaa kimemwozea na mhanga nafsi yangu"

Copied!
130
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

Ml,,·3

DOl)

I

MASUALA IBUKA KATlKA RIWAYA ZA KISASA:

KIDAGAA KIMEMWOZEA

NA

MHANGA NAFSI YANGU

NA

MAYIEKA NYANGARA MAUREEN

TASNIFU

HII

IMEWASILISHWA

KATlKA

IDARA

YA KISW AHILI

ILl

KUTOSHELEZA

BAADHI

YA MAHITAJI

YA SHAHADA

YA UZAMILI

KATlKA CHUO KIKUU CHA KENY ATT A.

(2)

U GAMO

Tasnifu hiini kazi yangu asilia na haijawahi kuwasilishwa katika Chuo Kikuu kingine.

Mayieka Nyangara Maureen

(C501CE/21212/20 12)

Sahihi ~ Tarehe. ~.\

.I.~\

?:-~.\~

.

Tasnifu hii imetolewa kwa idhini yetu kama wasimamizi walioteuliwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Prof. Kitula King'ei

Sahihi . . Tarehe

~({O~[)~

.

Idara ya Kiswahili

Dkt. Timothy Arege

Idara ya Kiswahili

Sahihi.

l~ ~

Tarehe ..::L.?~..'. ~.

~.'.-f.

(3)

TABARUKU

(4)

SHUKRANI

Ningependa kumshukuru jalali kwa kunijalia uhai, nehema na kibali chake. Amekuwa

mwaminifu na mwenye upendo. Utukufu na sifa ni kwake.

Pili, ni kwa wasimamizi wangu: Prof. Kitula King'ei na Dkt. Timothy Arege kwa msaada

wenu wa maoni, maarifa, mapendekezo na mwongozo wa kila aina ambao hausahuliki.

Asanteni

Tatu, ni kwa wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa

ushauri na maarifa yao yasiyopimika. Mungu awabariki.

Shukrani zingine ni kwa wazazi wangu. Babangu, Raphael Mayieka, kwa mapenzi yako

ya dhati na kunisaidia kifedha. Mamangu, Beriness Mayieka, kwa ushauri na kunitia

moyo kila uchao. Nawapenda sana.

Kwa marafiki zangu wa dhati walionitia moyo na kunipa ujasiri wa kukamilisha utafiti

huu: Violet Simiyu, Anna Githuthwa, Lisbeth Kaburu, Manani Tirimba na Jeff Gikonyo.

Mola awajalie merna. I'

Mwisho, ni kwa wanafunzi wenzangu walioniauni darasani: Sarah Moraa, Seth Gekuno,

Rael Babera, Onesimus Kioko, Ashioya Cosnet, Carolyne Wafumbwa, Georgina Makini,

Gladys Ombese, Murega Murithi, Judy Ong'uko, Naomi Waita, Elmelda Onsare,

Everlyne Atemo, Victor Ingosi, Patricia Muluko na Ephraim Gathogo. Nawatakia merna

maishani.

(5)

MAELEZO YA ISTILAHI

Masuala ibuka

Ni maudhui yanayorejelea mambo ambayo yamezuka katika jamii na yanaiathiri moja kwa moja.

Riwaya ya usasa

Ni riwaya iliyozuka miaka ya 1990 na huakisi matumizi ya mbinu za kiubunifu zinazoasi

kaida za kijadi za uandishi wa riwaya .

Uhalisia

Ni mkondo unaosisitiza usawiri wa matukio katika fasihi kama yalivyo katika maisha ya kila siku.

Ujarabati

i ufafanuzi wa ujuzi unaotokana na mambo halisi yanayoshikika, kuonekana na kuhisika katika fikra na mishipa ya binadamu

Mfumo

Ni mpangilio ambao una vipengele vinavyojengana na kukamilishana

Usasa

(6)

IKISIRI

MASUALA IBUKA KA TlKA RIWA Y A ZA KISASA

Utafiti huu unatathimini namna masuala ibuka yanavyosawiriwa katika riwaya za kisasa. Katika kuendeleza kazi hii, mtafiti anateua riwaya mbili za kisasa ambazo ni: Kidagaa Kimemwozea(2012) ya Walibora Kenna Mhanga Nafsi Yangu (2012) ya Mohamed S.A. Masuala ibuka ni mambo halisi yanayoikumba jamii ya kisasa ambayo inapitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya huwa ni ya kijamii, kisiasa, kiuchurni, kidini na kiteknolojia na huiathiri jamii katika mawanda yote. Waandishi wa riwaya wanateua masuala yenye mguso kwa jamii na kuyasimulia kwa kiwango cha juu cha ubunifu. Maudhui haya yanaangazia hali halisi, maingiliano, mivutano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira yao. Malengo ya utafiti huu ni kuangazia mbinu za kisasa zilizotumiwa kuwasilisha masuala ibuka katika riwaya ya kisasa na kubainisha jinsi riwaya ya kisasa inavyoyaangazia masuala ibuka katika jamii ya mwandishi na kufafanua. Utafiti unaongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inaeleza kuwa kazi ya msanii inapaswa kuwasilisha ukweli kama ulivyo katika mazingira, matukio yanayosimuliwa sharti yawe yanatokea katika ulimwengu halisi na msanii anayaangalia matatizo ya jamii na kuchunguza vyanzo vyake. Mihimili ya nadharia hii inaturnika kama dira katika kutafiti huu. Uteuzi wa sampuli ni Kidagaa Kimemwozea ya Walibora Ken naya Mhanga

Nafsi

Yangu yake Mohamed S.A. Riwaya hizi zinatupa data faafu katika utafiti huu. Data ya kimsingi inakusanywa maktabani kutokana na kazi teule, majarida, magazeti, tasnifu na kwa mtandao. Data inayopatikana inachanganuliwa kwa kuzingatia maswali ya utafiti, malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia teule. Matokeo yanawasilishwa kwa njia yamaelezo.

(7)

ABSTRACT

EMERGING ISSUES IN CONTEMPORARY KlSWAHILI NOVELS

(8)

YALIYOMO

U GAMO ii

TABARUKU iii

SHUKRANI iv

MAELEZO YA ISTILAHI v

IKISIRI vi

ABSTRACT vii

SURA YA KWANZA 1

MASUALA IBUKA KATlKA RIWAYA ZA KISASA: KIDAGAA

KIMEMWOZEA (2012) NA MHANGA NAFSI YANGU (2012) 1

1.0 UT ANGULIZI 1

1.1USULI WA MADA 1

1.2 SW ALA LA UT AFITI 4

1.3MASW ALl YA UTAFITI 4

I' 1.4MALENGO YA UTAFITI 4

1.5 SABABU ZA KUCHAGUA MADA 5

1.6UPEO NA MIPAKA 6

1.7 YALIYOANDIKWA KUHUSU MADA 6

1.8 MISINGI YA NADHARIA YA UTAFITI 11

1.9.0 MBINU ZA UTAFITI 13

1.9.1 MUUNDO WA UTAFITI 13

1.9.2 MAHALI PA UTAFITI 13

(9)

1.9.3 UTEUZI WA SAMPULI 14

1.9.4 UKUSANYAJI DATA 14

1.9.5 UCHANGANUZI DATA 14

1.9.5 UWASILISHAJI WA DATA 15

1.10 HITIMISHO 15

,

SURA YA PILI 16

2.0 UCHAMBUZI WA DHANA YA USASA NA RIWAYA ZA KISASA 16

2.1 UTANGULIZI 16

2.2 DHANA YA USASA WAF ASIHI 16

2.3 SIF A ZA RIW A YAY A KISASA 17

2.3.1 MCHANGANYIKO WA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI 18

2.3. 2 MTINDO W A UT ANZU NDANI YA UT ANZU 20

2.5.3 UKATIZAJI WA MKONDO WA MASIMULIZI 21

2.5.4 UPUUZAJI WA KAIDA ZA KIMSINGI ZA USA WIRI WA WAHUSlKA. 23

2.5.5 MSUKO CHANGAMANO , 27

2.5.6 MANDHARI YA UHALISIA NA UHALISIAJABU 30

2.5.7 MUUNDO WA LUGHA NA UWIANO WA LUGHA KIMASIMULIZI 31

2.6 HITIMISHO 35

SURA YA TATU 36

3.0 MASUALA IBUKA KATIKA RIW AYAY A KIDAGAA KIMEMWOZEA ... 36

3.1 UTANGULIZI , 36

3.2 ULEMAVU 36

3.3 MAPENZI A NDOA 39

(10)

3.4.1 HAKI ZA WAFUNGWA 45

3.4.2 HAKI ZA WATOTO 47

3.4.3 HAKI ZA WAFANYAKAZI 51

3.5 KUTOWAJIBIKA KATIKA KAZI.. 53

3.6 UFISADI 56

3.7 LUGHA YA KISWAHILI 59

3.8 ElIMU KATlKA JAMII 61

3.9 UONGOZI WA KIIMLA 63

3.10 HITIMISHO 65

SURA YA NNE 67

4.0 MASUALA IBUKA KATIKA RIWAYA YA MHANGA NAFSI YANGU 67

4.1 UT ANGULIZI 67

4.2 MIT AZAMO ISIYO NA UHALISIA YAW AMOTONI KUHUSU PEPONI. 68

4.3 UBAGUZI 71

4.3.1 UBAGUZI WA KITABAKA 76

4.3.2 UBAGUZI WA LUGHA 78

,.,4.4 UKENGEUSHI 79

4.4.1 UKENGEUSHI W A KIMAADILI r••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••• 80

4.4.2 UKENGEUSHI W A KIJAMII 84

4.5 HAKI NA SHERIA 85

4.5.1 HAKI ZA WATOTO 86

4.5.1.1 HAKI YA MALEZI 86

4.5.1.2 HAKI YA KULINDWA KUTOKANA NA MADHARA 88

4.5.2 SHERIA , 89

4.6 MAGONJW A SUGU 91

(11)

4.6.1 SARATANI 91

4.6.2 UKIMWI 92

4. 7NDOA ZA KISASA 94

4.7.1 UKOSEFU W A MAPENZI YA DHA TI 95

4.7.2 MAWASILIANO HAFIFU 97

4.8 HITIMISHO 97

SURA YA TANO 99

5.0 HITIMISHO 99

5.1 UTANGULIZI 99

5.2 MUHTASARI 99

5.3 MATOKEO YA UTAFITI 101

5.4 MCHANGO WA UTAFITI 107

5.5 MATATIZO YA UTAFITI.. 107

5.6 MAPENDEKEZO 107

(12)

SURA YA KWANZA

MASUALA IBUKA KATlKA RIWAYA ZA KISASA: KIDAGAA KIMEMWOZEA (2012) NA MHANGA NAFSI YANGU (2012)

1.0 UTANGULIZI

1.1 USULI WA MADA

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kiubunifu ili kueleza tajriba mbalimbali za maisha ya wanajamii. Njogu na Chimerah (1999) wanaeleza kuwa fasihi inawasilisha hali, maingiliano, mivutano na mikizano miongoni mwa binadamu na mazingira yake. Fasihi inawasilisha maudhui yenye mguso kwa wanajamii kupitia kwa lugha iliyojaaa mvuto. Njogu na Chimera (1999) wanafafanua kuwa msanii ni zao la jamii na inajaribu kuwasilisha matukio ya jamii katika uhalisia wake. Msanii anachota maudhui yake

r

kutokana na hali halisi zinazomzunguka za kitamaduni, kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kupitia kwa kazi za fasihi tunapata picha kamili ya jamii ya kisasa. Hakuna fasihi ipayoibuka katika ombwe. Kila fasihi ni zao halisi la jamii na inaonyesha kuwepo kwa jamii hiyo kijamii, kisiasa na hatakiuchumi. Masuala ambayo Mohamed na Walibora wanaibua ni tajriba yao kijamii. Ingawa ni kazi za kubuni, zinaeleza ukweli kuhusu maisha ya jamii.

Njogu na Chimera (1999) wanaendelea kusisitiza kuwa fasihi ni zao la wakati na jinsi jamii inavyobadilika ndivyo kazi ya fasihi inavyobadilika ikiwemo riwaya ya Kiswahili.

Utanzu wa riwaya unachipuka baada ya ukoloni wa Kimagharibi na unaendelea kukua ili

1

(13)

kukidhi mahitaji ya jamii inayopitia mabadiliko katika nyanja za kijamii, kisiasa, kielimu,

kiuchumi na kiteknolojia. Ngano za fasihi simulizi zinatafsiriwa na kuwa msingi wa riwaya za kisasa. Baadhi ya ngano hizo ni Swahili Tales as Told by the Natives of Zanzibar (1889) na Edward Steere, Mazungumzo ya Alfu Lela- Ulela (1928) kinachotafsiriwa na Edwin Brenn na kuharariwa na F. Johnson, Mashimo ya Mfalme Suleiman na Rider Haggard na Safari za Galiva na Jonathan Swift. Riwaya za awali zina wahusika wanyama kwa vile zinafuata rnkondo wa ngano.

Riwaya ya kisasa inazaliwa katika miaka ya 1950 na inauakisi uhalisia wa hali ya juu. Wavumbuzi wake ni kama Shabban Robert, J. Kiimbila, Naila Harusi na Leo Omollo. Waandishi hawa wanalenga kuwaadilisha wanajamii. Lengo lac linaingiliana na matakwa ya ujamaa nchini Tanzania, kukua kwa miji ya Afrika Mashariki, uhamiaji wa watu katika miji hiyo na kukuza utamaduni wa maisha rriapya ya mjini.

Miaka ya 1970 inazua mabadiliko makubwa katika utanzu wa riwaya. Hili linatokana na uhuru wa kisiasa unaowapa wasanii furs a ya kuangazia maudhui ya unafiki, ukoloni, ukoloni mambo leo, ufisadi, usaliti, ujamaa kama mfumo wa siasa na utawala wa kiimla. Baadhi ya riwaya zinazotungwa miaka hii niRosa Mistika (1971) .

(14)

Katika miaka ya 1990, kunazuka riwaya za usasa zinazoathiriwa na mbinu mpya za

uandishi. Baadhi ya mbinu hizo mpya ni uhalisia ndoto na ubunaji wa visasili. Khamis (2012) anaeleza kuwa aina ya lugha inayotumika katika kazi fulani ya fasihi inaathiriwa na kinachotokea katika jamii ya mwandishi. Mwandishi anachota fikra, maudhui, falsafa,

itikadi, mitindo, jazanda, maumbo na miundo ya lugha has a inapokuwa jamii yenyewe imo katika kasi ya mabadiliko makubwa kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia kuanzia miaka ya 1990. Anasisitiza kuwa riwaya ya kisasa inashughulikia matatizo yanayoikabili nchi na jamii husika na kwa kiasi kikubwa inakiuka mipaka ya kitaifa hadi kimataifa.

Anaendelea kufafanua kuwa fasihi ya Kiswahili inaendelea kuchukua dhima ya

uchunguzi wa jamii huku ikibeba silaha mpya za utunzi na inajishughulisha na matatizo mapya katika jamii ya kisasa.Baadhi ya riwaya zinazochapishwa katika wakati huo ni za Mohamed S.A kama vile Babu Alipofufuka (2001), Dunia yao (2005), Mhanga Nafsi Yangu (2012), Walenisi (1995) yake Katama, M na Bina-Adamu (2002) yake Wamitilla K.W.

Njogu na Chimerah (1999) wanatambua sifa mbalimbali za riwaya za kisasa. Kwanza, I'

zinaibua uhalisia; taratibu za maisha kama vile dini na siasa zinatazamwa kwa jicho la

ukali na udhaifu wake unafichuliwa bila uoga. Pili, wahusika wanahusishwa zaidi na hisia zao na masuala ya utu wao; wanaingiliana na jamii pana. Vilevile, wahusika halisi

wanatumiwa kinyume na wahusika wanyama waliotumiwa katika riwaya za awali. Hali yakisaikolojia ambayo inamsukuma mhusika kutendajambo fulani inatiliwa maanani.

(15)

1.2 SW ALA LA UT AFITI

Utafiti huu unashughulikia masuala ibuka katika riwaya za K. Walibora Kidagaa Kimemwozea (2012) na ya S.A Mohamed, Mhanga Nafsi Yangu (2012). Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imejikita katika uhalisia ilihali ile ya Mhanga Nafsi Yangu imechanganya uhalisia na fantasia. Masuala yanayoangaziwa ni ya kijamii, kisiasa, kielimu, kiteknolojia, kiuchumi na kitamaduni. Masuala haya yanaelezwa kupitia kwa matumizi ya mbinu mpya za kifasihi kama vile matumizi ya visasili, uhalisiamazingaombwe na urejeleo matini.

1.3 MASW ALl YA UT AFITI

Utafiti huu unaongozwa na maswali yafuatayo:

1. Riwaya zilizoteuliwa zinatumia mbinu za kisasa katika kuwasilisha masuala ibuka?

11. Ni kwa kiasi gani riwaya zilizoteuliwa zinayaangazia masuala ibuka katikajamii?

1.4 MALENGO YA UT AFITI I'

Madhumuni ya utafiti huu ni:

1. Kuangazia mbinu za kisasa zinazotumiwa kuwasilisha masuala ibuka katika riwaya zilizoteuliwa.

(16)

1.5 SABABU ZA KUCHAGUA MADA

Utafiti huu unachochewa na sababu mbalimbali:

Kwanza, masuala ibuka katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Mhanga Nafsi Yangu hayajashughulikiwa. Jamii inavyobadilika ndivyo riwaya zinavyobadilika. Mabadiliko

haya huiathiri jamii, kwa hivyo wasanii wa riwaya za kisasa wanabadilisha maudhui yao

kuiakisi hali halisi katika ulimwengu wa sasa. Masuala ambayo S.A Mohamed na K.

Walibora wanaibua ni tajriba yao ya kijamii. Ingawa ni kazi za kubuni, zinaeleza ukweli

kuhusu maisha.

Utafiti huu pia unachochewa na haja ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu masuala

ibuka katika riwaya za kisasa zinazoibuka katika mazingira ya utandawazi na mabadiliko

mengi ya kijamii. Katika miaka ya sabini kuendelea kunatokea mabadiliko ya kijamii,

kisiasa, kimaadili, kiteknolojia, kiuchumi na kiutamaduni ambayo yanaiathiri jamii kwa

jumla. Jamii inakumbwa na misukosuko kutokana na mabadiliko hayo. Utafiti huu

unawafaa wanajamii wote kwani wanaathiriwa kwa njia moja au nyingine.

Karanja (2008), katika tasnifu yake, anachunguza masuala ibuka katika fasihi ya watoto

na anapendekeza utafiti ufanywe katika utanzu wa riwaya kuhusu masuala ibuka. Mwito

unaotolewa unaashiria bado kuna pengo katika suala hili na utafiti zaidi unahitajika.

Katiba mpya nchini Kenya inaleta fasiri mpya katika asasi mbalimbali za kijamii. Asasi

hizi ni pamoja na za kijamii, kisiasa, kiuchumi, kidini, kiteknolojia na kitamaduni.

Masuala yanayoangaziwa ni kama: maz'ingira, afya, elimu, haki za walemavu, ajira ya

watoto, usawa wa kijinsia, utandawazi, uongozi nauwajibikaji. Masuala haya yalikuwepo

(17)

katika katiba ya awali ila hayakupewa kipaurnbele. Katika katiba mpya, masuala haya

yanaangaziwa kwa kina kama vipengele vinavyojisimamia. Mabadiliko haya

yanatuchochea kuyatafiti masuala haya katika riwaya za kisasa zinazoandikwa baada ya

kuidhinishwa kwa katiba mpya.

Vyombo vya habari vinaangazia masuala ibuka katika jamii. Makala mengi yanaeleza

kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu, ubaguzi, ufisadi, uongozi wa kimla, afya na

magonjwa, mapuuza na uzembe, elimu na maadili. Visa hivi vinatuchochea kufanya

utafiti wa masuala haya katika riwaya za kisasa. Hii ni kwa sababu msanii ni zao la jamii

na huathiriwa na yanayotokea katika jamii yake. Kwa hivyo, kazi yake inauwakilisha

ukweli kama ulivyo katikajamii.

1.6 UPEO A MIPAKA

Utafiti huu unayafafanua masuala ibuka katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea (2012)

na

Mhanga

Nafsi Yangu

(2012). Riwaya hizi zinateuliwa kimakusudi kwa vile ni za kisasa na zinaibua matukio ya jamii katika msingi wa uhalisia. Aidha, zimevuka mipaka

ya taifa hadi kimataifa. Masuala ibuka ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na

kielimu yanateuliwa na kuelezwa kwa kina.

1.7 YALIYOANDIKWA KUHUSU MADA

Kuna tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa kuhusu masuala ibuka katika riwaya za

kisasa kwa kiwango kimoja au kingine.

Riwaya za wakati wa ubepari ni ~a kipelelezi na hazijajishughulisha na masuala halisi ya

(18)

(1987) anasema kuwa riwaya hizo zinapumbaza na kusisumua. Utafiti huu ni tofauti na

wa Senkoro kwa sababu unatathimini riwaya zakisasa zinazoiakisi hali halisi katika jamii

ya sasa.

Wamitila (2003) anaeleza kuwa riwaya ya kisasa imezaliwa mwanzoni mwa miaka ya

1950. Riwaya hizi zinauakisi uhalisia kwa kiwango cha juu. Waandishi wa riwaya hizi

wanayaibua masuala yanayoiathiri jamii wanamoishi. Khamis (2012) anasema kuwa

lugha ya riwaya ya kisasa inahusiana na utandawazi. Lugha inayotumika katika kazi

fulani ya fasihi inaathiriwa na mambo yanayotokea katika jamii ya mwandishi.

Mwandishi anachota fikra, maudhui, falsafa, itikadi, maumbo na mitindo ya lugha.

Anasisitiza kuwa fasihi ya Kiswahili inaendelea kuchukua dhima ya uchunguzi wa jamii

huku ikibebea silaha mpya za njia ya utunzi na fikra za majadiliano na matatizo mapya

yanayoikumba jamii. Anabainisha mbinu mpya katika riwaya ya kisasa. Mbinu hizo ni

pamoja na uhalsiaajabu, ubunifu wa visasili na mighani, urejeleo matini, usasabaadaye na

utouzowefu. Maelezo haya yanataufaa kuyahakiki masuala ibuka katika riwaya teule.

Masuala ibuka yanaangaziwa na watafiti mbalimbali. Makala ya "Ufundishaji wa "

Masuala Ibuka kwa Kiswahili" ya Njogu (2007) yanafafanua masuala ibuka kama vile:

UKIMWI, katiba, haki za binadamu, afya,.mazingira, ajira ya watoto, usawa wa kijinsia

na utandawazi. Njogu anajadili mbinu mwafaka za kuyafundishia masuala haya katika

shule za msingi na upili. Makala haya yanatufaa kwa vile mojawapo ya nwaya

tunayoishughulikia yaKidagaa Kimemwozea inatahiniwa katika shule za upili.

(19)

Utafiti wa Karanja (2008) unaangazia masuala ibuka katika hadithi za watoto. Anateua vitabu sita vya watoto vikiwemo: Yalianza Kimchezomchezo,Ndoto ya Riziki, Mama wa Kambo, Ngano za Mfalme Tapwara Tapwar, Mnyama Mwenye Huruma na Mchuuzi wa

Matambara. Karanja anayaainisha masuala ibuka katika vi tabu hivyo, anabainisha

mitindo inayoturnika kuyawasilisha na anatathimini ufaafu wa vitabu hivyo kwa watoto.

Utafiti huu unatufaa kuyaeleza masuala ibuka yanayowaathiri watoto. Kinyurne naye,

tunatumia riwaya za kisasa.

Suala ibuka la dhulurna dhidi ya watoto linaangaziwa na watafiti mbalimbali. Tomison (1996) anatafiti kuhusu uhusiano kati ya dhuluma za watoto na madawa ya kulevya nchini Australia. Utafiti huu unaangazia maturnizi ya madawa ya kulevya kama mojawapo ya maovu ya jamii yanayofaa kuangamizwa. Anaonyesha kuwa vyanzo vya dhulurna za watoto ni maturnizi ya madawa ya kulevya katikajamii. Ingawa utafiti huu si wa kifasihi, unachangia pakubwa kuielewa mada hii. Masuala ibuka ya jamii

yanayoangaziwa katika utafiti huu yanashughulikiwa kisanii na waandishi wa riwaya za

kisasa zinazoteuliwa. Hata hivyo, utafiti huu ni tofauti kwa sababu unafanywa katika I"

mazingira, wakati na utamaduni tofauti.

(20)

vyautetezi wa haki za watoto, uhamasishaji wajamii dhidi ya dhuluma hizi na sheri akali

kuwekwa na serikali kwa wale wapatikanao wakizikiuka haki za watoto. Ingawa hili ni

suala ibuka katika riwaya za kisasa, utafiti huu ni tofauti na wa Kavuri kwa sababu

unaziangazia riwaya tofauti na unatumia nadharia ya uhalisia.

Suala la uongozi mbaya linaelezwa na watafiti wengi. Mugambi (1983) anaangazia kilio

cha wanyonge katika riwaya za Mohamed S. A. :Asali Chungu, Dunia Mti Mkavu na

Utengano. Utafiti wake unabainisha kuwa viongozi waliochaguliwa wanaendeleza

ukoloni mambo leo, ufisadi, ukatili, ubinafsi na unafiki. Wananchi waliowachagua

wanaishi katika uchochole ilihali viongozi wao wanaishi katika maisha ya ukwasi.

Njoroge (2014) anatafiti kuhusu suala la viongozi kama visababishi vya mabadiliko

katika riwaya za Mwenda Mbatiah: Vipanya vya Maabara na Majira ya Tufani. Anabainisha kuwa viongozi wengi hawawajibiki katika kuiendeleza jamii. Aidha,

anaeleza kuwa vijana wanaopaswa kuwa viongozi shupavu wanajiingiza katika ufisadi,

ukahaba na ujambazi. Hali hizi zinawasukuma wananchi kutafuta mbinu za kujikomboa.

Tafiti hizi zinatufaa katika kuyaangazia masuala ya uongozi wa kimla na ufisadi katika

katika riwaya teule.

Suala la ndoa ni msingi wa jamii ya kisasa na chochote kinachoiathiri, kinaiathiri jamii

nzima. Sanja (2012) analiangazia suala la ndoa katika riwaya za Kala Tufaha na Paradiso. Katika utafiti wake, anabainisha kuwa hatuwezi kuitenga kazi ya kubuni na

uhalisia. Anasema kuwa asasi ya ndoa inahitaji fasiri mpya kulingana na mabadiliko ya

kiwakati. Jamii inapaswa kuishi kulingana na hali ya maisha ili kuepuka migogoro ya

(21)

kisasa ya ndoa. Tafiti nyingi kuhusu nafasi ya mwanamke katika ndoa zinamwonyesha

kama kiumbe duni ambaye hajajikomboa kimawazo. Hata hivyo, wanawake wa kisasa

wanakengeuka na kutambua nafasi yao katika jamii. Suakei (2013) anaangazia usasa na mwanamke wa kisasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke. Anaongozwa na nadharia

ya ufeministi kuzieleza changamoto zinazomkabili mwanamke wa kisasa mikononi mwa wanaume wenye ubabedume. Changamoto hizo ni kama vile: kuozwa katika umri mdogo, kupigwa, kutukanwa, kubakwa na kunyimwa fursa ya kujiendeleza. Hata hivyo,

mhusika mkuu, Nana, anafaulu kupambana na dhuluma hizi kutokana na ukakamavu na maadili yake. Nana ni kiwakilishi cha mwanamke wa kisasa anayejua nafasi yake katika jamii yenye mabadiliko mengi ya kijamii, kielimu, kiteknolojia na kiuchumi. Hii ni kwa

sababu anajikomboa kimawazo na yuko tayari kuzipigania haki zake. Ukengeushi wa wanawake unachangia unyanyasaji wa wanaume katika jamii ya kisasa. Gitau (2005) anaeleza dhuluma wanazofanyiwa wanaume kama vile kupigwa, kutukanwa na kudhulumiwa kimapenzi. Wanaume huamua kutoroka au kuoa wake wengine kama njia

ya kujinasua. Tafiti hizi zinatusaidia kulielewa suala la ndoa katika jamii ya kisasa. Hata

hivyo, riwaya tunazozihakiki ni tofauti I'

Dini inatumiwa kama chombo cha kuwadhulumu waumini katika jamii ya kisasa. Ng'etich (2011) anajadili kuhusu aina mbalimbali za dhuluma, athari za dhuluma hizo na namna ambavyo waandishi wanatumia mbinu za kisanaa kuupinga udhalimu wa kidini.

(22)

dini ya kikristo, ila utafiti huu unagusia dini za kiisilamu na kikristo. Aidha, riwaya tunazozihakiki ni tofauti.

Suala ibuka la ugonjwa wa UKIMWI linaangaziwa na watafiti wengi. Baadhi yao ni Kinara (2012) anayetafiti kuhusu maudhui ya UKIMWI katika riwaya za Kiswahili. Anaongozwa na nadharia mbili; naratolojia na ya matendo na usemi kuangazia usemi unaotumiwa katika kuusawiri UKIMWI kama vile laana, kifo, janga na uchawi. Anafafanua athari za maradhi kwa wahusika. Baadhi ya athari hizo ni unyanyapaa, uyatima na vifo vya mapema. Aidha, anaonyesha namna wagonjwa wanavyoyapokea maradhi hayo. Baadhi wanatamauka na mwishowe kujitia kitanzi, wengine wanaamua kulipiza kisasi kwa kuusambaza kwa watu wengine na wengine wanaikabili hali hiyo kwa ukakamavu na kuamua kuendeleza maisha yao kama awali. Njia za kujikinga ni matumizi ya kondomu na kujiepusha na mapenzi ya kiholela. Utafiti huu unatufaa kwa sababuUKIMWI ni suala ibuka katika riwaya teule. Hata hivyo, kinyume naye, tunatumia nadharia ya uhalisia na riwaya tunazozishughulikia ni tofauti.

1.8 MISINGI YA NADHARIA YA UTAFITI

Utafiti huu unaongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia hii iliasisiwa katika kame ya 19na kufafanuliwa zaidi na E. Goffman (1952) anayeishi kati ya mwaka (1922- 1982). Baadhi ya wataalamu wengine wanaotoa mchango wao ni Gustav Flaubert (1850), George Lukacs (1979), Rene Wellek (1960), Macdowell Arthur (1918) na Hegel G.

(1971). Lukacs (1963) anaeleza kuwa mwandishi anasukumwa na njia ya kuusawiri

uhalisia katika ukamilifu na wakati wake maalumu. Mwandishi anapaswa kupenya chini

(23)

ya picha za kijuujuu na kudhihirisha mifanyiko ya mabadiliko yaliyopo. Uhalisia wa maisha katika jamii unapewa msingi mkubwa wa uandishi kuhusu uhalisia. Tukio,

mhusika au mandhari huelezwa kama vya kihalisia ikiwa vinafanana na sura fulani ya maisha. Naye Wamitila (2002) anaeleza kuwa uhalisia unasisitiza usawiri wa maisha ya jamii kwa uaminifu na usahihi rnkubwa. Waaandishi wa kazi ya teule wanatoa picha za wahusika, matukio na mandhari ambayo yanaoona kwa kiasi kikubwa na uhalisia wa jamii ya mwandishi anayehusika. Fasihi yoyote lazima ionekane kama kioo cha jamii.

Hivyo basi, lazima jamii iweze kujitazama na kujiona kupitia fasihi ambayo ni zao la

jamii. Msingi wa nadharia hii ni kuwa sanaa iwakilishe ukweli na kuwakilishwa kwa maneno halisi, iwe aminifu na ionyeshe hali halisi ya mazingira.

Utafiti huu unaongozwa na mihimili ya nadharia ya uhalisia ambayo ni:

(a) Kazi ya fasihi inajitosheleza. Riwaya ni kazi ya sanaa kwa vile ina msuko, mtindo,

wahusika na ujumbe.

Mhimili huu unatusaidia kuonyesha kuwa riwaya teule ni kazi ambazo zinajitosheleza

,-kama kazi ya fasihi. Hii ni kwa sababu zina sura, ploti, maudhui, wahusika na zinatumia mitindo ya kisanii.

(b) Kazi ya msanii inapaswa kuwasilisha ukweli kama ulivyo katika mazingira yake.

Uhalisia sharti ujihusishe na mambo halisi yanayotokea katika mazingira halisi kupitia

kwa wahusika. Mhimili huu unatusaidia katika uchanganuzi wa masuala ibuka katika

riwaya za kisasa yaliyo ya kikweli katikajamii ya sasa.

(24)

(c) Wahusika ni vielelezo yakini vya binadamu wa kawaida kwa vile wao hutumia lugha ya binadamu wa kawaida. Hali halisi ya ya wahusika na lugha wanayoitumia

humwezesha mwanadamu kujifafanulia uwezo wake wa kutenda mambo na mtazamo

wake kuhusu maisha.

Mhimili huu unatumiwa kuonyesha kuwa wahusika wa riwaya teule wanaathiriwa na

yale wanayoyapitia.

(d) Msanii anaangalia matatizo na kuchunguza chanzo chake. Anachunguza mabadiliko ambayo hutokea kwa kipindi fulani cha historia na kuyatumia kuwasawiri wahusika wake.

Mhimili huu unatumiwa kuonyesha kuwa matatizo wanayoyapitia wahusika wa riwaya teule yana chanzo chake.

1.9.0 MBINU ZA UTAFITI

1.9.1 MUUNDO WA UTAFITI

Utafiti huu ni wa kimaelezo. Muundo wa kimaelezo unatumiwa kueleza masuala ibuka I'

katika riwaya za kisasa zinazoteuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia teule.

1.9.2 MAHALI PA UTAFITI

Utafiti wa kina unafanywa maktabani. Mbinu hii inatumika ili kupata data kulingana na malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia teule. Maandishi mbalimbali yanapitiwa

(25)

maktabani ikiwa ni pamoja na majarida, makala, magazeti na mtandao ili kupata data

faafu ya mada ya utafiti.

Vitabu vya fasihi vinavyoteuliwa kwa minajili ya mada hii; Kidagaa Kimemwozea (2012)

na Mhanga Nafsi Yangu (2012) vinachanganuliwa kwa kina ili kupata data inayofaa

utafiti. Vitabu vinavyoendeleza nadharia ya uhalisia vinasomwa ili kubainisha mihili

inayoongoza kuchanganua data ya utafiti. Tafiti za awali zinazohusiana na mada hii

zinachunguzwa kwa lengo la kupata data faafu.

1.9.3 UTEUZI W A SAMPULI

Uteuzi wa sampuli ni wa kimakusudi. Kazi teule za fasihi andishi ya Kiswahili

zinateuliwa. Kazi hizi ni riwaya mbili za kisasa ambazo ni Kidagaa Kimemwozea (2012)

naMhanga Nafsi Yangu (2012). Masuala ibuka katika riwaya hizi ndiyo yanateuliwa ili

kuafikiana na malengo ya utafiti huu. Mihimili ya nadharia ya uhalisia inamwongoza

mtafiti kupata data inayohusiana na maswali na malengo ya utafiti.

1.9.4 UKUSANYAJI DATA

Data inakusanywa kutoka maktabani kupitia mbinu ya kusoma machapisho, magazeti,

vitabu, majarida na makala yanayohusu riwaya za kisasa, masuala ibuka na nadharia ya

uhalisia. Data faafu inadondolewa na kunakiliwa.

1.9.5 UCHANGANUZI DATA

Data inayokusanywa inachanganuliwa kwa kuzingatia maswali ya utafiti, malengo ya

(26)

Mhimili wa 1: Riwaya teule kama kazi ambazo zinazojitosheleza kwa vile zina sura,

ploti, maudhui, wahusika na mitindo ya kifashi

Mhimili wa 2: Uchanganuzi wa masuala ibuka ya kikweli katika jamii ya mwandishi

kutoka.

Mhimili wa 3: Wahusika wa riwaya teule wanaathiriwa na yale waliyoyapitia.

Mhimili wa 4: Matatizo wanayoyapitia wahusika wa riwaya teule yana chanzo chake.

1.9.5 UWASILISHAJI WA DATA

Data inayokusanywa inawasilishwa kwa njia ya maelezo. Maelezo haya yanazingatia

ufafanuzi wa masuala ibuka yanavyosawiriwa katika riwaya teule. Uwasilishaji wa data

unafanywa kwa kuzingatia maswali ya utafiti,.malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia

teule.

1.10 HITIMISHO

Sura hii imeangazia usuli wa mada, suala lautafiti, maswali ya utafiti, malengo yautafiti,

I'

sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, misingi ya

nadharia ya utafiti, muundo wa utafiti, mahali pa utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji

wa data, uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa data.

(27)

SURA YAPILI

2.0 UCHAMBUZI W A DHANA YA USASA NA RIWA YA ZA KISASA

2.1 UTANGULIZI

Sura hii inaeleza kuhusu dhana ya usasa na riwaya za kisasa. Madurnulla (2009) anaeleza kuwa riwaya ni sanaa ya kubuni ambayo huturnia lugha ya kinathari katika uwasilishaji wake na inazingatia vipengele vinavyotokana na utamaduni na tajriba ya maisha ya jamii. Katika riwaya, kuna nafasi ya kujadili kwa kina masuala yanayodhihirika katika jamii. Maudhui yanayoshughulikiwa hujitokeza kama ubunifu au uhalisia. Riwaya tunazozichanganua; Mhanga Nafsi Yangu na Kidagaa Kimemwozea ni za kinathari na zenye uchangamano kimtindo, kimandhari na zina urefu wa kuridhisha.

2.2 DHANA YA USASA KATlKA FASIHI

(28)

watu weusi ili kuupinga utamaduni wa Kimagharibi unaomfinyilia Mwafrika. Weusi

hawa wanatafuta mbinu na mtindo mpya wa kuuvunja utamaduni wa Kimagharibi. Hali

hii inachangia kuibuka kwa uandishi wa fasihi ya kisasa ili kutimiza lengo lao la

kujieleza. Wamitila (2003) anatambua sifa za kazi za fasihi ya kisasa: Kwanza, zinatia

mkazo katika fani kuliko maudhui. Pili, zinazua utata rnkubwa; kuficha au kuzua hisia

kinzani za mwandishi wa kazi husika. Tatu, mpaka uliopo baina ya uhalisia na ubunifu

unavunjwa.

2.3 SIFA ZA RIWAYAY A KISASA

Khamis (2012) anaeleza kuwa fasihi ya Kiswahili inaendelea kuchukua dhima ya

uchunguzi wa jamii kwa kutumia silaha mpya za njia ya utunzi na fikira za majadiliano

ya wanafalsafa. Kimaudhui, riwaya ya kisasa inajishughulisha na matatizo halisi

yanayoikabili jamii ya sasa katika viwango vya kitaifa na kimataifa. Matatizo

yanayoibuliwa na waandishi wa riwaya teule ni kama vile ufisadi, uongozi wa kimla,

ubaguzi, uchafuzi wa maadili, tamaa, magonjwa ya UKIMWI na Saratani, kutowajibika

kazini, migogoro katika mapenzi na ndoa na ukiukaji wa haki za makundi mbalimbali

kama vile walemavu, watoto, wafungwa na wafanyakazi ..Riwaya ya kisasa ina sifa

zifuatazo: Mchanganyiko wa vipera vya fasihi simulizi, mtindo wa utanzu ndani ya

utanzu, ukatizaji wa mkondo wa masimulizi, upuuzaji wa kaida na kanuni za kimsingi za

kuwasawiri wahusika, muundo na msuko changamano, mandhari ya uhalisia na

uhalisiajabu na muundo wa lugha na uwiano wa lugha kimasimulizi.

(29)

2.3.1 MCHANGANYIKO WA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI

Watunzi wa riwaya ya kisasa hutumia vipera vya fasihi simulizi kama vile visasili,

maghani na nyimbo kuyawasilisha maudhui yao. Kisasili ni kipera cha fasihi simulizi kinachoeleza kuhusu asili ya kitu au hali katika jamii. Nayo maghani ni hadithi za kihistoria kuwahusu mashujaa katika jamii. Katika riwaya ya

Kidagaa Kimemwozea,

kuna kisasili kinachoeleza sababu za watu wa Sokomoko kutoyanywa maji ya mto Kiberenge (uk 4). Maji ya mto huu yaliogopwa kwa vile iliaminika kuwa mtu mwenye Kifafa alifia humo na miili ya waliopigania uhuru ilitupwa mle ndani.

Kuna kisasili kingine kinachoeleza kuhusu asili ya kuwachukia walemavu (uk 7). Hili linatokana na ulemavu kuchukuliwa kuwa mwiko katika eneo la Sokomoko. Jamii inauona ulemavu kama laana au aibu. Mwalimu Majisifu anataka kuwatupa watoto wake walemavu mtoni kwa sababu anajua ni mwiko katika jamii yake. Mke wake, Bi. Dora na Imani wanavunja mwiko huu kwa kuwalea watoto hao kwa upendo mwingi. Jamii yetu inashuhudia visa vya watoto walemavu kuchukuliwa kama laana. Kwa hivyo, wanafungiwa ndani na kunyimwa fursa ya kutangamana na watu.

(30)

mchezaji wa Songoa FC, Chwechwe Makweche, anayeifungia timu yake magoli mengi

ila anaishia kuwa kiguru na kusahaulika. Katika jamii halisi tuna mashujaa watajika kama

vile: Dedan Kimathi, Nelson Mandela, Jomo Kenyatta na Tom Mboya. Mashujaa hawa

wanapigania uhuru wa mataifa yao. Baadhi yao wanatambuliwa ilihali wengine

wanasahaulika.

Katika riwaya ya Mhanga Nafsi Yangu, kuna matumizi ya wimbo unaotumiwa kupitisha

ujumbe maalamu (uk 55-57). Wimbo huu ni jazanda. Unatumiwa kuyaibua masuala ya

ubaguzi, usaliti na mitazamo isiyo ya uhalisia kuyahusu maisha. Aidha, unaangazia

mabadiliko ya maisha yanayomkumba Afida anapofika Peponi. Matarajio yake kuihusu

Peponi yanasalitiwa. Hii ni kwa sababu taswira halisi ya Peponi ni ya kutamausha.

Wapeponi wamejaa ubaguzi, ubinafsi na udhalimu. Utashi wa vitu umewatawala na

hawayajali maslahi ya wengine kinyume na kule Motoni ambapo jamii inaishi kwa

umoja. Maisha ya Peponi yanamtaka mtu ajikakamue na kufanya bidii ili ajiendeleze.

Hali hii inamsukuma Afida kushawishika kuolewa na Neshboch ili apate uraia wa Peponi

na arithi,., mali yake. Ndoa hii inaanza kwa raha ila baadaye inajawa karaha. Afida

anasononeka na kujuta kuvutwa na mawimbi yamabadiliko ya Peponi.

Kipera kingine cha fasihi simulizi kinachoangaziwa ni kile cha miviga na ngomezi. Afida

anasimulia sherehe za harusi kule Motoni. Anaeleza kuwa harusi za kule zina mpangilio.

Zinaanza kwa kuchumbiana, kupelekwa kwa posa na mshenga na kisha utafiti wa kina

unafanywa kuhusu mposaji na anayeposwa. Baadaye mahari yanalipwa, nguo

zinanunuliwa, vyakula mbalimbali vinapikwa na harusi inafungwa msikitini na

(31)

nyumbani. Baada ya harusi, watu wanacheza ngoma mbalimbali na kuwafurahia

wanaharusi (uk 150). Miviga hii inaonyesha kuwa shere he ya harusi kule Motoni ni ya

jamii nzima kinyume na kule Peponi ambapo shughuli hiyo ni ya familia husika tu. Tunaelezwa kuwa harusi kati ya Neshboch na Afida inahudhuriwa na watu wachache: Bw. Bawa, Bi. Mameti, wazazi wa Neshboch na dada zake wawili; She- shaiza na

Bendelheib. Hapakuwa na sherehe baada ya harusi. Jamii nyingi za Kiafrika zina miviga inayofanywa nyakati mbalimbali kama vile mtoto anapozaliwa na kupewa jina, vijana

wanapopashwa tohara, harusi zinapofungwa na mtu anapokufa. Katika jamii hizi, miviga inaishirikisha jamii. Hata hivyo, jamii za Kimagharibi zinazichukulia sherehe hizo kama shughuli ya kifamilia na haifai kuishirikishajamii.

Hali kadhalika, kuna visasili vinavyosambaa Motoni kuwa baba yake Afida ni kuhani,

walii au gwiji wa miujiza. Hili linatokana na visa vya miujiza anavyovifanya akiwa hai

na anapokufa. Anapokuwa hai anawafundisha watu masuala ya dini ya Kiislamu ndiposa wanamwita kuhani au wali. Anapokufa anamtembelea Afida kule Peponi kama kizuu ila anaonekana kama binadamu kamili mwenye nyama na mifupa. Hili linamfanya Afida

I'

amwone kama gwiji wa miujiza (uk 115).

2.3. 2MTINDO WA UTANZU NDANI YA UTANZU

Hii ni mbinu ya kuingiza utanzu mwingine katika utanzu wa riwaya. Riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea ni masimulizi yanayohusu jamii ya Watornoko kwa ujumla. Kwa hivyo,

(32)

vinavyojengana kutoka mwanzo hadi mwisho. Vilevile, katika riwaya hii kuna hadithi

kuhusu wizi wa mswada wa Kidagaa Kimemwozea. Amani anasimulia namna Majisifu

anauiba mswada wake na kuuchapisha kwa jina lake. Riwaya hiyo inampa sifa ilihali

Amani anazama katika umaskini. Utanzu huo wa ndani unachangia kuibua maudhui ya

ufisadi na ukosefu wa utu katika jamii inayozingatiwa na mwandishi wa riwaya.

Aidha, kuna vitabu vingi vinavyorejelewa riwayani. Kuna tawasifu ya Amani ambayo

ataiandika baada ya kusajilishwa na Imani. Madhubuti naye ataandika kitabu. Mwandishi

anarejelea riwaya yake ya 'Siku Njema' na kuwalinganisha Kazikwisha na Mtemi Nasaba

Bora. Wote wanachimba makaburi yao kabla ya kifo chao. Nao Madhubuti na Amani

wanafanya mijadala mingi kuhusu maandishi yanayohusiana na hali halisi ya Tomoko na

hali zao binafsi. Vitabu wanavyovirejelea ni: Viumbe Walia laan iwa, Anthills of

Savannah, On the Posteolony, Mshale wa mungu, Season of Migration to the North,

Midnights Children, Revolution, The Dark Child naUtenzi wa Uhuru wa Tomoko.

Katika riwaya ya Mhanga Nafsi Yangu, Afida anachambua riwaya nyingi ili aweze

kujisaili, kujielewa na kuulewa ulimwengu anamoishi. Riwaya hizo ni pamoja na: Kiu,

The Yaeoubian Buildings, Blindness,End of History and the last man na The Argument

Culture. Pia, anarejelea diwani nyingi: Sauti ya dhiki, Song of Lawino naSong of Deal

2.5.3 UKA TIZAJI W A MKONDO W A MASIMULIZI

Usimulizi ni hali ya kueleza matukio katika hadithi. Kuna usimulizi aina mbalimbali.

Usimulizi katika nafsi ya kwanza,~pili na tatu. Pili, usimulizi wa kiwakati. Usimulizi huu

hurejelea wakati uliopo au uliopita. Hatimaye, ni usimulizi maizi. Hapa ni pale ambapo

(33)

mhusika huwa na sifa za kiungu za kuweza kuona kinachoendelea akilini mwa mtu.

Riwaya ya kisasa huchanganya mitindo wa kisimulizi na hivyo kuifanya kazi kuwa

changamano; isiyoeleweka moja kwa moja. Katika

Mhanga

Nafsi Yangu

,

masimulizi

katika sura ya kwanza hadi tano ni katika nafsi ya tatu ilihali masimulizi katika sura ya

tano na saba ni katika nafsi ya kwanza. Masimulizi ya kiwakati ni katika wakati uliopo na

uliopita. Vilevile, usimulizi maizi unatumiwa. Sauti ya ndani ya Afida inarnzungumzia

Afida kila wakati anapokumbwa na matatizo kule Peponi. Hili linadhihirika pale ambapo

analia baada ya Bi. Marneti kumsingizia kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mume

wake. Inamuuliza:

Afida unalia nini? Ujue kwamba uko Peponi, na Peponi si mahali pa kuendeleza kilio. Maneno ya Bi. Marneti yasikutishe. Kwa sababu si maneno ya Kipeponi. Wenyewe Wapeponi hawatumii matusi na masimango kama anavyotumia Bi. Marneti. wakizungumza. Ya Bi. Marneti ni maneno ya mtu anayedhani kwamba kafika Peponi. Na kwa sababu anadhani amefika Peponi,

basi yeye ni Mpeponi kamili pia. Ikiwa ni hivyo, na wewe umeshafika Peponi kwa hivyo ni Mpeponi uliyekamilika kama yeye. (uk 44-45)

Katika dondoo hili Afida anafahamishwa awe na ukakamavu ili amudu kukabiliana na

rfiazingira yake mpya ya Peponi ambayo yana ubaguzi na dhuluma mbalimbali. Sauti

inamsisitizia umuhimu wa kuwa mvumilivu na ajiandae kwa mengi yatakayojiri akiwa

ugenini. Aidha, kizuu cha baba yake Afida kinamweleza anavyobadilika na kupotoka

kimaadili pindi tu anapofika kule Peponi. Mabadiliko hayo yanatokana na utashi wa vitu

(34)

Masimulizi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea yanasimuliwa katika nafsi ya tatu.

Mtunzi anayaeleza mandhari na mazingira ya wahusika kwa maneno yake mwenyewe.

Masimulizi ni katika wakati uliopita.

2.5.4 UPUUZAJI W A KAIDA ZA KIMSINGI ZA USA WIRI W A W AHUSIKA

Wahusika ni viumbe wa kubuniwa katika utanzu wowote wa fasihi. Wasanii wa riwaya

hutumia wahusika ambao ni binadamu ili kuibulia muktadha wa uhalisia. Wahusika hao

wanakula, wanakunywa, wanacheka, wanalia, wanakuwa wagonjwa na wanakufa kama

binadamu wa kawaida. Kwa hivyo, matendo yao ya hadithini yanaaminika. Katika riwaya

yaMhanga Nafsi Yangu, tunamwona Shuhuda na Afida wakikula, wakikunywa, wakiwa

wagonjwa na Shuhuda anakufa. Katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, tunaelezwa

kuwa Dj, Uhuru na Arnani wanapelekwa hospitalini baada ya kuugua. Aidha, wahusika hawa wanafanya kazi katika nyanja mbalimbali za jamii. Katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, tuna walimu kama Fao na Majisifu. Kuna wachungaji kama Arnani na DJ. Vilevile, kuna wanafunzi kama Mashaka, Madhubuti na Arnani. Wahusika hawa wanatenda mambo na kuzungumza kwa uhalisia ambao unaweza kuaminika. Majina ya

I'

wahusika wa riwaya teule yanalingana na ya watu halisi ulimwenguni. Wahusika hawa

wanapewa majina kama binadamu anavyopewa ili kujitambulisha. Katika riwaya ya

Mhanga Nafsi Yangu kuna wahusika kama Afida, Bi. Mwamda. Bi. Mameti, Neshboch,

Yakrobich, She-shaiza, Shuhuda, Shaabani na Bw. Bwawa. Majina haya yanapatikana

katikajamii tunamoishi. Khamis (2012) anaeleza kuwa wahusika katika riwaya ya kisasa

wanachukua mwelekeo wa ufantasia na uhalisiamazingaornbwe. Fantasia ni dhana

inayoelezea njia ya kutumia lugha kwa kutia chumvi mno hadi kuvuka uhalisia. Fantasia

(35)

katika riwaya ya kisasa ni ya kueleza ukweli kama ulivyo katika jamii ya sasa. Katika fantasia wahusika wanachorwa wakiwa katika safari ili kutafuta ukweli kuhusu maisha. Katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, tunaelezwa kuhusu safari ya Amani na Imani kuelekea Sokomoko. Hii ni safari halisi na tena ya kisaikolojia inayohusu kujisaka na kurekebisha mambo yaliyoharibika hapo zamani. Mwandishi anaifananisha na 'kutingisha kibiriti aone kama kuna njiti' na pia 'kutia mkono kizani'. Dhana ya kwanza inatumiwa mwishoni mwa riwaya kurejelea ndoa yao. Ndoa ya Amani na Imani ni kama

safari wanayoandamana kama wanavyofanya wanapokuja Sokomoko. Naye Madhubuti anafunga safari kwenda Urusi kusoma. Anarudi mwasi machoni pa baba yake ila ni rnzalendo halisi anayesaidia kuikomboa Tomoko kutoka kwa uongozi wa kidhalimu wa

baba yake. Aidha, kuna safari ya Majisifu kwenda Wangwani kutoa mhadhara katika chuo cha Mkokotoni. Safari hii inamchochea Majisifu kujirudi na kujirekebisha. Anaposhindwa kutoa hotuba jukwaani analia kama mtoto kutokana na majuto yanayomkumba. Anaanza kuwaonea wengi huruma, kwa mfano, rnkewe kwa kuwalea watoto wao walemavu, watoto wake walemavu, Imani, Mashaka na Amani.

,-Anawahurumia waandishi ambao mawazo yao yanaibwa kama anvyofanyiwa Amani. Katika riwaya ya Mhanga Nafsi Yangu, kuna safari ya Afida kutoka Motoni kuelekea Peponi ili kujitafutia riziki. Hata hivyo hana uhakika na maisha ya kule Peponi. Anajiuliza maswali mengi:

(36)

kwenyewe? Kukoje enhe? Kumekaaja? Kutampokeaje? Kutamchukuaje? Kutamchukuliaje? (uk 5)

Katika kauli hii tunaelezwa kuwa Afida hana uhakika juu ya ari yake ya kwenda ugenini kwa mwaliko wa shangazi yake anayemtangulia kule. Hajui Wapeponi ni watu wa aina gani. Hana uhakika kuhusu mapokezi yao na namna atakavyoishi kule. Anapotua katika uwanja wa ndege Peponi anaona kila kitu kikiwa cheupe na hili linamkosesha uhakika kuhusu weupe huo. Anajiuliza:

...weupe maana yake nini kama si weupe? Hasa ukitofautishwa na weupe ...Kwani weupe si sitiari ya usafi na unadhifu kwa kila mtu? Si ishara ya mafanikio? Sio ishara ya Peponi na kuingia kwenye ukamilifu wa mambo ya kidunia? Si afueni ya kuingia kwenye afueni na kuwemo katika ubora wa kila kitu? (uk 23)

Kauli hii ni kinaya cha matarajio ya Afida. Hii. ni kwa sababu anakaribishwa na mazingira ya ubaguzi na udhalilishaji badala ya ufanisi anaoutarajia. Shangazi yake anambagua na kumdhalilisha nyumbani na hospitalini. Wanafunzi na wahadhiri wenzake wanamtenga na kumdunisha. Naye, Neshboch na jamaa zake wanamdharu na kumpa talaka. Aidha, sheria za Peponi zinambagua na kumpendelea mume wake katika kesi inayomhusu mtoto wao. Afida anayanganywa fursa ya kumlea mtoto wao kwa

"

kusingiziwa ulevi. Madhila haya yanamchochea kuingia katika ulevi na uasherati. Safari hii inamfanya Afida atambue kuwa nafsi ya mtu inaweza kutolewa mhanga kwa matarajio ambayo mwanzo hayakuwa na msimamo.

Wahusika katika riwaya ya kisasa hujengwa kwa msingi wa uhalisiamazingaombwe. Hapa ni pale ambapo wanapewa uwezo wa kutenda mambo ya kiungu. Katika riwaya ya

Mhanga Nafsi Yangu tuna wahusika ambao wanatenda mambo yasiyo ya kibinadamu .

.25

(37)

Baba yake Afida, ana uwezo wa kufanya matendo ya kiajabu anapokuwa hai. Msimulizi anasimulia:

Babake hakusoma sana hata hivyo, aliweza kutambua mambo ya kidunia yaliyomsaidia sana katika kazi yake ya uaguzi na uganga ... Aliweza hata kuruka hewani na kusafiri pahala popote alipoenda wakati wowote. Mara ngapi Afida wakati wa utoto wake alipolala na babake kitandani aligutuka usingizini na kumshutukia bwana huyo akizunguka kama pia na halafu akining'inia hewani kama tiyara isiyofungwa uzi. Halafu kufumba na kufumbwa alimwona huyo baba yake katoweka. Na kisha alipopata lepe na baadaye kuzindukana tena, alimkuta ubavuni pake anakoroma. Vipi alijitokeza miujiza hii, hawezi kueleza Afida hadi leo. (uk 21).

Masimulizi haya yanaeleza matendo ya kimiujiza ya baba yake Afida. Binadamu halisi hawezi kuruka angani au kuning'inia hewani kama tiara bila ya kuanguka. Hili huwezekana tu kwa malaika na ndege. Kwa hivyo, baba yake Afida anasaidiwa na nguvu zake za kiganga kufanya vitendo hivi. Matendo haya yanamfanya kuheshimiwa na kuogopwa na wengi. Aidha, tunasimuliwa visa vingi ambapo kizuu cha baba yake Afida kinajibizana naye (uk 18). Kizuu cha baba yake Afida kinamweleza Afida sababu za watu kutoroka kwao kuelekea katika mataifa mengine. Wanasukumwa na umaskini na maisha duni katika nchi zao.Wanaenda katika nchi zingine ili watajirike na kuyakamilisha maisha yao.

(38)

Kiswahili kule Motoni, mzee Dawamu, ambaye ni marehemu anajitokeza akiwa hai. Mwalimu huyo anawasaidia wanafunzi wake kuchambua shairi la majira ya baridi

Peponi. (uk 60)

Katika Kidagaa Kimemwozea tunaelezwa kuwa Mtemi Nasaba Bora anaanza kufikiria

suala la kifo akiwa hai. Mawazo haya yanamtatiza anapolala na anapokuwa macho. Anajiona kama marehemu mtarajiwa na anaamua kujipangia mazishi yake kwa kuchimba

kaburi lake. (uk 128)

2.5.5 MSUKO CHANGAMANO

Wamitila (2003) anaeleza kuwa msuko ni mshikamano wa vitushi. Visa na matukio

hujengwa katika hadithi kupitia kwa mpangilio wa mantiki au ufundi unaoongoza katika

uwasilishaji wa utanzu wa riwaya. Kuna msuko sahili na changamano. Katika msuko

sahili, matukio husimuliwa yakifuatana na huwa mtiririko wa moja kwa moja. Katika

msuko changamano mtunzi husimulia matukio yanayoingiliana na kukosa kufuatana ila

hukamilishana. Hili linafanikishwa kwa kutumia viona mbele, viona nyuma na vitabiri.

~ilevile, matukio mengi yanaachwa pembeni na kuibua mengine kisha ya awali

yanarejelewa na kuleta ukamilifu.

Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, inafumwa kwa viona nyuma na mbele. Mtiririko wa

hadithi si wa moja kwa moja. Hadithi inapoanza, Amani na Imani wako kwenye ukingo

wa mto Kiberenge. Baadaye, maisha yao kabla wafike Sokomoko yanabainishwa.

Hadithi ya Majununi inafafanuliwa kwa kuzingatia historia ya jamii inayosawiriwa kabla

ya uhuru. Vipengele hivyo ndivyo vinavyojenga vitushi ambavyo vinabainisha muktadha

(39)

wa jamii hiyo. Kuna nyadhifa nyingi wanazopewa wahusika Mtemi Nasaba Bora na

nduguye, Mwalimu Majisifu. Mtemi anakuwa karani wakati wa enzi ya wakoloni na

kisha kuwa kiongozi wa Sokomoko. Naye nduguye anaajiriwa kwingi lakini pombe

inamfanya apigwe kalamu.

Suala la ulemavu ni sugu katika jamii lakini inasemekana kuwa kabla ya Imani kufika

Sokomoko, walemavu wanachukuliwa visivyo katika jamii. Mbinu hii inatumiwa na

mwandishi kuunda taswira ya uhalisia wa mambo yanayowasilishwa kwa kuoanisha na

yale ya awali. Vilevile, mtunzi wa riwaya ya

Kidagaa Kimemwo

ze

a

,

anatumia vitabiri kuendeleza maudhui yake. Katika sura ya tano, mtunzi anaeleza, "miaka kadhaa baadaye

walipopata kitoto chao wenyewe Imani alikumbuka siku hiyo kilipokata roho kitoto

chao ..." (uk 78). Hapa mtunzi anaeleza kuwa Amani na Imani wanafunga ndoa ingawa

suala hila lipo mwishoni mwa riwaya. Naye Bi. Zuhura anapopelekewa mtoto, Uhuru, anamtazama kwa makini, "kilifanana na mtu fulani pale kwenye kasri la Majununi" (uk

38). Mwandishi anaichochea hadhira yake kuwa huyo ni mtu wanayemfahamu lakini

jambo hila halikuelezwa kwa kina wakati huo. Katika riwaya pia inaelezwa kuwa Dj,

"Alitaka kuficha utarishi wake kwa Mheshimiwa Mtemi Nasaba Bora kupeleka barua ..."

(ukl12). Kinachodokezwa hapa ni kwamba, wahusika hao wawili; Lowela na Mtemi

Nasaba Bora, walikuwa na uhusiano wa kimahaba. Katika sura ya tisa, mwandishi

anaisawiri hali ya kisaikolojia ya MtemiNasaba Bora kuwa, " kila alipolala aliota kifo na

alipokuwa macho aliwaza kifo pia" (uk 127). Mazingira ya kifo hicho yanafafanuliwa hapo baadaye anapoamua kujitia kitanzi katika sura ya ya kumi kwamba, "walikuta

(40)

yanasimuliwa na kuachwa pembeni kisha mengine yanaibuliwa. Baadaye, mtunzi

anarejelea matukio ya awali na kuyakamilisha. Kwa mfano, mtunzi anataja tu kuhusu barua anayopewa Mashaka na Ben Bella katika sura ya tano. Ujumbe wa barua hiyo

unaelezwa kwa kina katika sura ya sita.

Mtiririko wa matukio katika riwaya ya

Mhanga Naf

s

i Yangu

si wa moja kwa moja.

Matukio hayafuatani japo yanaingiliana na kukamilishana. Mtunzi anasimulia matukio

kwa ufupi, anayakatiza na kuibua mengine kisha anayarejelea baaadaye. Hadithi inaanza

Afida akiwa ndegeni akielekea Peponi. Anaonekana kama hana uhakika kuhusu

anakokwenda. Katika sura ya pili, msimulizi anaanza kwa kueleza yanayoj iri katika

uwanja wa ndege kabla ya Afida kuabiri ndege. Anaagwa na ukoo wake na kupewa

maagizo mengi ambayo anatarajiwa kuyatimiza akifika Peponi. Baada ya hayo

masimulizi, msimulizi anarejelea safari ya Afida akiwa ndani ya ndege hadi anapotua Peponi.

Vilevile, kuna matumizi ya viona mbele, viona nyuma na vitabiri. Kizuu cha baba yake Afida kinamkumbusha ahadi anazoipa jamii yake katika uwanja wa ndege kule Motoni. Kinamtahadharisha kuwa kutotimiza ahadi zile kunaweza kumpa majuto mwishoni. (uk 93). Katika sura ya mwisho tunaelezwa kuwa Afida anajuta kuwapuuza wazazi wake. Anawataka wamsamehe. ( uk 190). Afida anapoagana na mpenzi wake, Shaabani , anaeleza, "Watu husema wakati na masafa marefu yana nguvu nyingi za kugeuza na kubadilisha" (uk 14-15). Kauli hii inadhihirika pale ambapo Afida anamsahau Shaabani anapofika Peponi. ( uk 68-69)

(41)

Naye Shuhuda anamweleza Afida, "Bora tunyamaze tu shoga, utakuja kuona mwenyewe. Nitakuona hapahapa Peponi utakapokuwa mwanamke uliyebadilika. Nitakuona na mimi niangue kicheko nikucheke. Niseme Afida huyu amebadilika kiasi hiki?" (uk 79). Kauli hii inakuja kudhihirika maishani mwa Afida. Anapotoka kimaadili na kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na mzee anayemzidi umri na kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Afida anazama katika ulevi na kuuza mwili wake kwa yeyote ilimradi apate pesa.

2.5.6 MANDHARI Y A UHALISIA NA UHALISIAJABU

Mandhari ni wakati au mahali maalumu ambapo matendo katika riwaya hutendeka. Mandhari ya riwaya teule yanaweza kupatikana katika ulimwengu halisi. Mandhari hayo ni kama nyumbani, shuleni, ofisini, mijini, vijijini, maeneo ya stare he kama mikahawa na baa, gerezani na hospitalini. Kijiografia, riwaya ya

Kidagaa Kimemwozea

inasimulia matukio yanayotokea katika nchi ya Tomoko, barani Afrika. Kihistoria, inaeleza hali kabla na baada ya uhuru kule Tomoko. Wakati wa ukoloni, maisha ya jamii ni magumu. Hii ni kwa sababu walowezi kama vile, Bwana Foti na Majununi wanajitengea mashamba yenye rotuba nao wenyeji Waafrika wanaachiwa maeneo yasiyotamanika

,-kama vile Ulitima, Baraka, Umoja na Mabondeni. Baada ya uhuru, viongozi Waafrika wanaochukua hatamu za uongozi kama Mtemi Nasaba Bora wanauendeleza ukoloni mambo leo. Tamaa, ubinafsi na usaliti unawatawala. Wanajilimbikizia mali na kuwaacha wananchi katika umaskini. Maisha ya mjini yanasawiriwa kupitia kwa wahusika kama

vile Mtemi Nasaba Bora na mkewe, Mwalimu Majisifu na Dora, Bw. Maozi na aila yake,

(42)

Imani. Mandhari mengine ni zahanati ya Nasaba Bora, shule ya Upili ya Nasaba Bora

nagereza la Sokomoko. Mandhari haya yanapatikana katika jamii halisi.

Mandhari ya Kijiografia ya Mhanga Nafsi Yangu ni Motoni na Peponi. Dhana ya Motoni

naPeponi zinahusishwa na mazingaombwe. Kidini, Motoni, panaaminika kuwa ni mahali

ambapo watenda dhambi wataenda kuchomeka daima siku ya kiama ifikapo. Kwa hivyo,

kule Motoni watu wanapitia uchungu mwingi kutokana na makali ya moto. Nako Peponi,

ni mahali ambapo wafu huenda kupumzika baada ya kufa. Nchi hizi zinatumiwa kistiari.

Motoni, ni nchi inayopatikana barani Afrika ilihali Peponi ni mojawapo ya nchi za

ngambo zilizoendelea. Mazingira ya Motoni yanasawiriwa kama ya umaskini, magonjwa,

njaa na ujinga. Ni nchi ambayo inasalia nyuma kimaendeleo na inayategemea mataifa ya

nje kama Peponi kuiauni. Kwa upande mwingine, mazingira ya Peponi ni yenye ufanisi

mwingi. Inasawiriwa kama nchi inayoenda na usasa. Wamotoni wanajiimarisha

kiuchumi, kijamii, kielimu na kiteknolojia. Hata hivyo, wanauendeleza ubaguzi dhidi ya

wageni weusi wanaofika kule. Hadithi inasimulia kisa cha Afida anayetoka kwao Motoni;

mahali pa dhiki, kuelekea Peponi; mahali pa utulivu. Hata hivyo, anapofika huko,

anakaribishwa na mazingira ya ubaguzi na udhalimu hadi anaamua kujitolea rnhanga

nafsiyake.

2.5.7 MUUNDO WA LUGHA NA UWIANO WA LUGHA KIMASIMULIZI

Lugha ya riwaya mpya ya Kiswahili ni tofauti na riwaya tangulizi.Watunzi wa riwaya ya

kisasa huitia lugha uvuguvugu ili ionekane mpya kuliko ilivyokuwa. Kwa hivyo,

wanawapa wahusika wao matumizimaalumu ya matamshi, tashtiti, sitiara, utohozi,

(43)

kejeli na kuchanganya ndimi.Lengo lao huwa ni kumteka msomaji auone ujumi wa lugha

ambao unachukua makini yake na kumvuta kisanaa na kumfanya afikirie zaidi. Katika mazungumzo ya kawaida si ajabu kuona kauli ambazo zimetoholewa na zingine

kuchanganywa. Matumizi ya sheng' yameshika kasi miongoni mwa vijana. Watu hujitambulisha kupitia kwa maongezi yao. Wahusika katika riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea wanatumia ucheshi, kejeli, sitiari, tashtiti, kuchanganya ndimi na kuhamisha msimbo ili kuyawasilisha maudhui yanayokusudiwa na mtunzi.

Ucheshi ni mbinu ya kutumia kauli, sentensi au maneno yanayosaidia kujenga

kichekesho .cha aina fulani. Mbinu hii hutumiwa katika kupunguza machovu na pia kueleza namna maneno hayo huweza kumchoma mhusika au wahusika katika kazi ya

fasihi. Ucheshi unaotumiwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ni kama vile: "...viraka viwili vikubwa vya urujuani vilichungulia makalioni kama pazia kwenye

madirisha ya nyumba" (uk 1). Kauli hii inarejelea umaskini unaomzingira Amani. "Wee

mwizi?" (uk 21). Usemi huu unatolewa na Mtemi Nasaba Bora akimrejelea Amani ilihali

yeye ndiye mwizi wa mali na mashamba ya umma. "Weye nitokeje na hata sijanywa

I'

chai?" (uk 86). Kauli hii inadhihirisha narnna haki za wafungwa kama Matuko Weye

zinavyokiukwa. Hawapati chakula.

Kejeli ni usemi wenye dharau unaositiri maana inayokusudiwa. Mifano ya kejeli katika

riwaya hii ni: "Wazungu walipoondoka (inasemekana kuwa hawakuondolewa) waliacha

(44)

Batulurnayo. Katika hali halisi, ni kwamba mkoloni anapoondoka, viongozi weusi

wanauendelza ukoloni mamboleo. "Aliwahurumia waandishi waliotunga vitabu vikatoka,

nao hawana habari navyo maana vyatolewa kwa majina ya wengine" ( kur. 136-137).

Anayeyasema maneno haya ni Mwalimu Majisifu ambaye pia aliuiba mswada wa

Kidagaa Kimemwozea.

Sitiari ni mbinu ya lugha ambapo kifananishi huwa hakitumiwi kutaja kitu kile

kinacholinganishwa kupitia kwacho. Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, inatumia sitiari

nyingi: Kidagaa Kimemwozea inatumika kueleza maisha magumu ya Tomoko. Vilevile,

inarejelea maisha ya watu binafsi kama vile Mtemi Nasaba Bora, Mwalimu Majisifu,

Amani, Mashaka na Dj Bob. "Fahali mmoja mweusi mkubwa akawa analisha karibu na

,

kaptura moja kuukuu na kuizoa yote kinywani" (uk 7). Hili ni tukio halisi ila tunaweza

kupata fasiri mwafaka kwa kulinganisha utawala wa Mtemi Nasaba Bora ambaye

anatumia mamlaka yake kuizoa rslimali yote ya wanyonge wa Tomoko.

Kuchanganya ndimi ni mbinu ya uandishi ambapo mwandishi huchanganya kauli au

I'

maneno ya lugha tofauti katika uwasilishaji wa kazi yake. Katika riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea, mhusika Dj Bob anatumia sheng' ili kujitambulisha na kundi la vijana.

Mtunzi anaibua mhusika anayetumia sheng' ili kuonyesha namna vijana wa mijini

wanavyoboronga lugha ya Kiswahili kwa kuturnia mseto wa Kingereza katika mfumo wa

lugha ya Kiswahili. Mifano:

Mazee 'usinywe maji hayo jo, ni haramu jo (uk 6) Mdosi- tajiri (uk 10)

Kubonga- kuzungurnza (uk 43) Mazee fanya faster jo (uk 73)

(45)

Mambo si fit (uk 73)

Mazee umezaa mtoto? (uk 42)

Mtoi (uk 42)

Kamwite sistee (uk 42)

Dame (uk 42)

Vilevile, Mtemi Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu wanatumia kauli za Kingereza ili kujitambulisha na kundi la wasomi. Aidha, wahusika hawa wanatumiwa kubainisha mielekeo ya watu kuhusu lugha ya kigeni na lugha ya Kiswahili. Mifano, Mtemi Nasaba Bora anatoa hotuba ya Kingereza katika siku ya Wazalendo huko Sokomoko (kur 69-70).

Vilevile, katika mazungumzo baina yake na rnkewe, Bi. Zuhura, anatumia maneno ya Kingereza kama: 'Shut up!' (uk 41), ' It is a straight forward case' (uk 41) na ' What is this?' (uk 40). Mwalimu Majisifu anapogombana na mkewe, Bi. Dora, anamtukana kwa Kingereza, ,Bloody bastard' (uk 44).

Kwa upande mwingine, riwaya ya

Mhanga

N

af

s

i Yan

g

u

imesheheni sitiari, kejeli na kuchanganya ndimi. Nchi zinazorejelewa Motoni na Peponi zinatumiwa kisitiari. Motoni

inarejelea nchi za bara la Afrika zinazokabiliwa na umaskini, magonjwa, njaa na ujinga. Nayo Peponi, inayarejelea mataifa ya kigeni ambayo yana utulivu wa maisha. Afida anasukumwa na hali duni ya kwao, Motoni, kuelekea Peponi ili kujitafutia riziki. Weupe

wa mandhari ya Peponi na rangi nyeupe ya Wapeponi inadhihirisha ukamilifu,

maendeleo na usasa. Weupe huu wa Peponi unawafanya wawabague watu weusi kutoka

Motoni. Wana mwelekeo hasi kuwahusu weusi kwa vile wanaumithilisha weusi na hali duniya maisha. Sitiara nyingine ni pale ambapo ndege anayoabiri Afida inapotua Peponi.

(46)

Peponi. Kutikisikia kwa ndege kunaashiria kupotoka kwa maadili ya Afida anapotua

Peponi. Hili linachangiwa na usasa wa kule.

Aidha, lugha ya riwaya hii imesheni mbinu ya kuchanganya ndimi na utohozi mwingi.

Mbinu hizi zinatumia kuangazia utandawazi na mwingiliano wa utamaduni wa Kiafrika

na kigeni. Tunaelezwa kuwa Bi. Mameti ana vitu vya kisasa: cooker, friji, microwave,

freezer grinder, na blender. Masuala ya usasa yanarejelewa: Middle ages, the civilized

world, miss world, sexual harassment, recreation, imitation, reinvention, appropriation,

reinventions, readjustments, jazz, funk, soul, blues na Rock n' roll.

2.6 HITIMISHO

Sura hii imeangazia dhana ya usasa na riwaya ya kisasa. Tumebainisha kuwa riwaya ya

kisasa ni riwaya inayotumia mbinu na mitindo mipya kuwasilisha maudhui yake. Mbinu

hizo huiteka hadhira na kuifanya ifikirie, ijisaili na kujisakura. Watunzi wa riwaya hizi

huchopeka vipera vya fasihi kama vile visasili na mighani kuelezea masuala

yanayoiathiri jamii ya sasa. Masuala hayo ni pamoja na uongozi mbaya, unyanyasaji,

utamaduni na umaskini. Msuko wa riwaya hizi ni changamano kwa vile zinatumia viona

nyuma, viona mbele na vitabiri. Nayo mandhari ni ya kiuhalisia na kimazingaombwe.

Lugha inayotumiwa imejaa jazanda, sitiara, ucheshi, kuchanganya ndimi, utohozi na

kejeli.Riwaya teule ni za kisasa kwa vile zinasimuliwa kwa misingi ya sifa hizi.

(47)

SURA YA TATU

3.0 MASUALA IBUKA KATIKA RIWAYA

YAKIDAGAA KIMEMWOZEA

3.1 UTANGULIZI

Sura hii inajadili masuala ibuka katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea (2012).

Tunaongozwa na nadharia ya uhalisia. Lukacs (1963) anaeleza kuwa uhalisia sharti

ujihusishe na mambo halisi yanayotokea katika mazingira halisi kupitia kwa wahusika. Wahusika ni vielelezo yakini vya binadamu wa kawaida kwa vile wao wanatumia lugha yabinadamu. Hali halisi ya wahusika na lugha wanayoitumia humwezesha mwanadamu kujifafanulia uwezo wake wa kutenda mambo na mtazamo wake kuhusu maisha. Njogu

(1997) anasema kuwa kazi ya msanii ni kiungo chake na jamii anayoilenga. Walibora

anaibua masuala yanayoiathiri jamii ya kisasa katika ngazi zote za maisha. Masuala

anayoyajadili yanalenga kumfanya binadamu awe mwanajamii mwema anayewajali

wenzake. Anagusia nyanja za kijamii, kisiasa, kielimu, kitamaduni na kiuchumi. Nyanja

hizi humsaidia binadamu kukuza hisia zake, tabia zake na kuyaelewa mazingira yake.

Masuala ibuka yanayoibuliwa ni pamoja na ulemavu, ukiukaji wa haki za binadamu,

kutowajibika kazini, ufisadi, elimu, uongozi wa kimla na lugha ya Kiswahili.

3.2 ULEMAVU

Jamii nyingi za Kiafrika zina imani potovu kuhusu ulemavu. Siva (2015) anaeleza kuwa

ulemavu unachukuliwa kama laana katika jamii. Walemavu hawaonyeshwi upendo,

wanadharauliwa, wanapuuzwa na kuchukiwa. Katika riwaya, tunaelezwa kuwa katika

(48)

nchi ya Sokomoko, ulemavu unachukuliwa kuwa mwiko. Mwalimu Majisifu na Dora

wanapobarikiwa na watoto wanne walemavu inaonekana kama ni miujiza au ni laana ya

kimapokeo kutoka kwa kizazi cha mke. Majisifu anamwona mke wake kama mwenye laana kutokana na dhambi alizozifanya kwao ndiposa anamzalia walemavu.

Anasononeshwa na ulemavu wa watoto wake; anataka kuwatupa majini ili

kuwaangamiza. Rata hivyo, anaghairi nia hiyo baada ya Dora, mkewe, kumshauri,

"Mtoto ni mtoto hata likiwa bonge la nyama. Mtu hupata ajaaliwalo sio alitakalo. " (uk

31 )

Kauli hii inadhihirisha kuwa jamii inauchukulia ulemavu kama laana kubwa. Wazazi

wanatamauka wanapojaliwa watoto walemavu. Mwanamume anajitakasa na kumlaumu

mwanamke kwa kuj ifungua watoto walemavu. Licha ya lawama hizo, mwanamke

anajitolea kuwapenda na kuwaenzi. Anawaona kama baraka kuu kutoka kwa mungu.

Katika jamii, walemavu wanachukuliwa kuwa mzigo. Lang'at (2015) anaeleza kuwa

katika kaunti ya Uashini Gishu, Kenya, walemavu wanaonekana kama watu wa

kuombaomba. Kwa hivyo, wanatengwa na kutelekezwa. Naye Kakai (2014) anasimulia

I'

kisacha mzee anayeitoroka familia yake yenye watoto watatu walemavu katika kaunti ya

Pokot, Kenya. Mama yao anawachiwa jukumu la kuwalea watoto hao katika dhiki nyingi.

Wanakosa lishe na makazi bora hadi pale ambapo msamaria mwema anapojitokeza na

kuwasaidia. Riwayani, Mwalimu Majisifu, anawaona watoto wake kama mashata

yasiyokuwa na faida maishani mwake ndiposa anamwachia mke wake jukumu la

kuwalea. Binamu yao, Mashaka, anawadharau na kuwacheka. Anawaona kama

(49)

madubwasha yasiyofaa kitu duniani na kuwalinganisha na sanamu kwenye maduka ya

Wahindi. Naye Mtemi Nasaba Bora, anabadili nia ya kumwoa msichana mmoja baada ya

kugundua ni kiguru. Banati huyu hashutushwi na uamuzi huo kwa vile anaikubali hali

yake. Msichana huyu anatumika kuonyesha kuwa walemavu ni watu wa kawaida na

wanahitaji nafasi sawa kama watu wengine.

Katiba ya Kenya (2010) inasisitiza kuwa walemavu wanafaa kufurahia haki zote za

kimsingi kwa vile ni washiriki wakamilifu katika jamii. Haki hizo ni pamoja na elimu.

Kuna shule maalumu zinazokidhi mahitaji ya walemavu. Shule hizo zinawapa vifaa maalumu vinavyowasaidia kuukabili ulemavu wao. Wangari (2013) anaeleza kuwa Wizara ya Elimu inahimiza kubuni mpango ambapo shule zinahitajika kujenga darasa

moja kuyakidhi mahitaji ya watoto walemavu. Riwayani, tunaelezwa kuwa Mwalimu

Majisifu, anawanyima watoto wake haki ya kupata elimu na kutangamana na wenzao.

Anawafungia ndani na kuwatenga na ulimwengu mpana. Nayo maoni ya Matuko Weye

katika Siku ya Wazalendo yanapuuzwa kwa vile ni mwendawazimu. Mtemi Nasaba Bora

anayaona maneno yake kama uchochezi kwa wananchi na kuamuru awekwe rumande.

,-Licha ya ulemavu wake, anachangia kwa kiasi kikubwa kuwazindua Wanasokomoko

kuhusu dhuluma za Mtemi Nasaba Bora. Hii ni ishara kuwa hata walemavu wana sehemu

muhimu katika ukombozi wa nchi. (uk 71-72). Kusambaratika kwa uhusiano baina ya Ben Bella na Mashaka kunamfanya Mashaka kuwa mwendawazimu. Hali hii inamfanya

akatize masomo yake na kuiua ndoto yake ya kuwa mwandishi. Katika jamii nyingi

watoto wenye ulemavu hufungwa kwa kamba na kufungiwa ndani. Fatma (2014)

(50)

kaunti ya Tana River, Kenya, wanatishia kuishtaki serikali kwa kuwanyima furs a ya kufanya kazi katika ofisi za umma. Hili linatokana na dhana potovu kuwa walemavu ni watu dhaifu wasioweza kuchangia katika maendeleo yajamii.

3.3MAPENZI NA NDOA

Burke (1999) anaeleza kuwa baadhi ya watu hujiingiza katika uhusiano kutokana na msukumo wa ubinafsi na unafiki. Kuna ukosefu wa mapenzi ya dhati miongoni mwa

wanajamii. Riwayani, tunaelezwa kuwa mapenzi baina ya Michelle na Majinuni ni ya

matumaini kabla ya Majinuni kwenda kupigana Uingereza katika Vita vya pili vya Dunia. Hii ni kwa sababu Michelle anatarajia kuwa baada ya vita, Majununi angerudi na pesa nyingi na kujenga nyumba ya kifahari ambamo wangeishi baada ya kufunga ndoa. Baaada ya vita, uhusiano huu unakumbwa na changamoto nyingi. Michelle anapoalikwa na Majinuni mara ya kwanza anasema:

Monsieur Major Noon nasikitika sana sitakanyaga chini wayo wa mguu

wangu. Jenga nyumba acha ujuba. Siwezi kuishi hemani humu mwituni

kama maskini sina sinani nikiulizwa siungami. (uk 17)

Dondoo hili linaonyesha kuwa Michelle hakuvutiwa na hali ya mpenzi wake. Anamwona I'

maskini kwa vile anaishi hemani. Majununi anajitahidi kujenga nyumba ya vyumba

vinne. Michelle anapoalikwa anasita kuishi kule. Baadaye, Majununi anajenga kasri na

kumwalika Michelle. Michelle anachukizwa na idadi ya vyumba katika kasri lile.

Anaeleza kuwa nambari ya kumi ni hatari. Hatimaye, anamwambia:

Monsieur Major Noon, ruwie radhi lakini naona hatufaani. Pengine imeandikwa kwamba tusioane. Narudi kwetu, katafute mwanarnke kufu yako. (uk 17)

(51)

Kauli hizi zinadhihirisha kuwa Michelle ana matarajio mengi ya kibinafsi ambayo

Majununi hayatimizi. Anajenga mapenzi yake kwa msingi wa mali. Anaamua kuuvunja

uhusiano wake na Majununi kwa vile anamwona maskini. Boss (1988) anashadidia hali

hii kwa kueleza kuwa wingi wa kuvunjika kwa mahusiano katika jamii unatokana na

wanajamii kuwa na matarajio makubwa ya kibinafsi ambayo ni vigumu kutimizwa.

Njogu (1997) anaeleza kuwa uhusiano unaojengwa katika misingi ya ubinafsi na unafiki

unaleta majonzi mengi kwa wahusika. Riwayani, tunaona kuwa kuvunjika kwa uhusiano

baina ya Majununi na Michelle, kunamwachia Majununi majonzi mengi. Anasema:

Mademoiselle Michelle umenigusa chembe cha moyo. Umeniachia donda ambalo halitaweza kupona alaa kulihali. Ndoa ni hiari ya mtu si msusumo. Kumbuka kwamba hiari. ni mukhitari ni juu yako mwenyewe. Haijaandikwa popote kwamba mimi nawe tusifunge ndoa. Unanipasha simanzi najitimai. Nenda sina ngoa nawe. (uk 17)

Katika dondoo hili, tunaelezwa kuwa Majununi anahisi uchungu kwa kuwachwa na

mchumba wake. Upweke na huzuni unamvaa. Hatimaye, anakubali kuwa hayakuwa

mapenzi ya mungu waoane. Usaliti huu unamfanya awachukie wanawake wote na

anaamua kutooa maishani.Matheka (2014) anaeleza kuwa pete tu haitoshi kukamilisha

"

ndoa. Wanandoa wanafaa kuweka msingi wa mapenzi ya dhati kabla ya kuvishana pete

iwapo wanataka wadumu pamoja milele. Mshauri wa ndoa katika shirika la wanandoa la

"Families for tomorrow" anaeleza kuwa ni muhimu kupata mchumba anayekupa furaha

maishani kwa sababu ndoa inahusu maisha ya mtu. Watu wakioana wakiwa na msingi

thabiti wanaishi kwa furaha na amani. Riwayani, tunaelezwa kuwa uhusiano baina ya

Amani na Imani unajengeka katika mapenzi ya dhati, heshima na uaminifu. Mapenzi

(52)

Imani shairi la mahaba (uk162). Amani anamwomba Imani wafunge pingu za maisha ili

waiendeleze jamii yao. Uhusiano wao unaanza kwa kuelewana na kufahamiana. Baada ya

kufahamiana, suala la uchumba na ndoa linajengeka katika nyoyo zao. Hii ni ishara tosha

kuwa mapenzi niyale ambayo kila mtu hujitolea mhanga kuyafanikisha.

Jamii inafaa kuwajibika kuwaelekeza vijana kuhusiana na suala la mapenzi. Ni jukumu la

wazazi, walimu na viongozi kuwashauri watoto kuhusiana na athari za kujiingiza katika

mapenzi ya kiholela wakiwa shuleni. Athari hizo ni pamoja na mimba zamapema, kupata

magonjwa ya zinaa na kukatiza masomo. Hivi karibuni visa vya wasichana wanaopata

mimba katika shule za msingi na upili vimeongezeka. Manyindo (2014) anaeleza kuwa

wanafunzi saba katika shule ya upili ya Taita Taveta, wanafukuzwa shuleni baada ya

kupatikana na mimba. Baadhi yao, wanapachikwa mimba hizo na walimu. Naye Lubanga

(2014) anaeleza kuwa wanafunzi thelatini na tisa katika kaunti ya Ushin Gishu,

wanalazimika kuwacha shule kutokana na ujauzito.Wanafunzi hao ni wa kati ya umri wa

miaka kumi na mitano na ishirini. Shule zinazoathiriwa ni pamoja na: Boinet, wanafunzi

kumi na wawili, Chepsait, wanafunzi kumi na watano na Soin, wanafunzi kumi na

wawili. Katika riwaya, tunaelezwa kuwa Fao anapokuwa mwalimu katika shule ya

sekondari ya Kinondoni anampachika msichana wa shule mimba na hawajibika katika

malezi ya mtoto yule. Walimu kama Fao wanafaa kufutwa kazi na kufikishwa

mahakamani ili wawajibike kwa matendo yao. (uk 37)

Kiongozi wa Sokomoko, Mtemi Nasaba Bora, si kielelezo bora kwa vijana. Anajiingiza

katika uhusiano wa kimapenzi na msichana wa shule, Lowela. Hili linadhihirika katika

References

Related documents

Avail- ability of the full genome sequence and use of another popula- tion will allow determining more precisely hot and cold regions in bread wheat because, in light of

The fuzzy based expert system applied to the battery scheduling based on the measured real time data or forecasted data as follows: Time(T), The Battery State of

The mutation type formed at the highest rate (mDEL1) is most frequent in the plated population (10 5 mutants cells per 10 8 parental cells), but grows so slowly under selection that

Further work will involve the modification of the sliding mode controller using a time-varying switching gain and improvement in modeling of the actuator over a broader

between the gonad signal that stimulates mate search- ing and daf-12 activity, we examined the leaving behavior of daf-12 mutants after ablation of the gonad (germ line plus

Table A.1: Diameter ratios for binary hard-sphere mixtures that exhibit solid-liquid phase diagrams of the solid solution, azeotrope, and eutectic types..

The propulsion mechanism used is completely mechanical, if the electrical counterpart has to be provided, the system will have to rely on external source of

Android is the most popular OS in all over the world.The android OS has captured the 79.3 percent market share.But there are lots of security issues related to smart phones and