Upokezi wa wanafunzi wa shule za upili kuhusu mashairi ya kisw ahili katlka Jimbo la Nakuru

107 

Full text

(1)

CHUO KIKUU CHA KENYATTA

SHULE YA FANI NA SAYANSI ZA JAMII

IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA

UPOKEZI WA W ANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI KUHUSU

MASHAIRI YA KISW AHILI KATlKA JIMBO LA NAKURU

NA

KARANI JOHN OJUMA CSO/CE/20924/2010

TASNIFU HII IMEWASILISHWA ILl KUTOSHELEZA BAADHI YA MAIDTAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATlKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA.

(2)

IKIRARI

Tasnifu hii ya uzamili ni kazi yangu asilia na haijawahi kuwasilishwa kwa madhumini ya shahada yoyote katika chuo kikuu kingine.

Sahihi ~ Tarehe

o

d

oS

po/,6

KARANI JOHN OJUMA

(MT AHINIW A)

Tasnifu hii ya uzamili imewasilishwa kwa idhini yetu kama wasimamizi walioteuliwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Sahihi __ 11lI-.=:....!....!:-I-__ fr::....:....- Tarehe

DKT. EDWIN WANYONYI MASINDE

NA

sahih~ Tarehe

1/1Wk

DKT. JOSEPH NYEHITA MAlT ARIA

IDARA YA KISWAHILI

CHUO KIKUU CHA KENYA TTA

(3)

TABARUKU

(4)

SHUKRANI

Kwanza, ningependa kutoa shukrani zangu kwa Maulana kwa kunipa siha njema tangu nilipoanza masomo yangu katika shahada ya uzamili hadi nilipoyakamilisha.

Isitoshe, shukrani zangu za kipekee na za dhati ziwaendee wasimamizi wangu Dkt. Edwin W. Masinde na Dkt. Joseph Nyehita Maitaria kwa uelekezi wenu wa kitaaluma. Nawatakieni siha njema na Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki kwa ukarimu wenu.

Pia, ningependa kutoa shukrani zangu kwa wahadhiri wote katika Idara ya Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa kunifunza vyema na kunipa moyo kila nilipoelekea kupoteza matumaini. Ahsanteni sana.

Isitoshe, ningependa kutoa shukrani zangu kwa walimu wakuu, walimu wa Kiswahili na wanafunzi wa shule za upili za Moi Kabarak, Rongai, Mary Mount na A.LC. Morop kwa kunifaa pakubwa nilipokuwa nikikusanya data shuleni mwenu.

Ninawashukuru pia wanafunzi wenzangu wa darasa la uzamili kwa ushirikiano tuliokuwa nao tangu tulipoanza masomo yetu. Kama si nyinyi kunipa moyo, huenda masomo haya ningeyaachia njiani. Mungu awabariki.

Mwisho, ningependa kutoa shukrani zangu kwa familia yangu, marafiki wangu na wote waliochangia kwa namna moja au nyingine kuhakikisha kuwa nimekamilisha masomo yangu ya uzamili bila usumbufu wowote. Ahsanteni.

(5)

IKISIRI

(6)

ABSTRACT

Both the classical and the modem Kiswahili poems have always been examined in

the Kenya Certificate of Secondary Education since the inception of the 8-4-4

system of education. However, the classical Kiswahili poems has been examined

more compared to the modem Kiswahili poetry in the last ten years. Because of

this reason, this research was conducted so as to examine and distinguish the

reception of Kiswahili poems in general amongst secondary school students. This

research was guided by Reader Response Theory whose key proponents are Fish

(1980), Tompkins (1980), Iser (1974, 78), Haus Robert Jauss and Roland Barthes

amongst others. This theory was used to examine the reception of Kiswahili

poems amongst secondary school students as readers based on their own personal

attitudes and experiences. This research was carried out in four secondary schools

in Nakuru county namely: Moi High School Kabarak, Rongai Boys High School,

Mary Mount Girls High School and A.I.C. Morop Girls Secondary School. The

form three and form four students were used in this research. Data was collected through the use of poetry tests based on Kiswahili poems, questionnaires and

interview methods. Data was also collected though reading of books, journals,

newspapers and thesis.

(7)

UFAFANUZI WA ISTILAHI MUHIMU

Arudhi :Ni kanuni zinazofuatwa katika utunzi wa ushairi kama vile vina, mizani

na mishororo.

Mashairi huru : Haya ni mashairi ambayo hayajifungi kwenye kaida za utunzi wa mashairi ya jadi kama vile: vina, mizani, idadi maalum ya mishororo, vipande

katika mishoro na mpangilio wa beti. Mashairi haya hujulikana pia kama mashairi

ya kimapinduzi.

Mashairi ya kimapokeo: Ni aina ya mashairi yanayofuata kaida na arudhi za utunzi wa mashairi kama vile: vina, vipande, mizani, mishororo na mpangilio

maalum wa beti. Mashairi haya yanajulikana pia kama mashairi ya arudhi.

Mwelekeo : Hii ni dhana inayotumiwa kuelezea mtazamo au rnkabala anaouchukua msanii au unaochukuliwa na jamii kuhusiana na jambo, tukio, swala

au wahusika fulani.

Upokezi: Ni rnkabala wa kifasihi unaojishughulisha na jinsi kazi za kifasihi zinavyopokelewa na wasomaji wakati fulani au katika mpito wa wakati

(8)

viii YALIYOMO

MADA i

IKlRARI ii

TABARUKU <,,•••••••••••••••••••••• iii

SHUKRANI , iv

IKISIRI v

ABSTRACT , vi

UF AF ANUZI WA ISTILAHI MUHIMU vii

YALIYOMO , viii

SURA YAKWANZA

1.0 Utangulizi 1

1.1 Usuli 1

1.2 Suala laUtafiti .4

1.3 Maswali ya Utafiti 6

1.4 Madhumuni ya Utafiti 6

1.5 Sababu za Kuchagua Mada 7

1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti 9

1.7 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 11

1.8 Misingi ya Nadharia : 16

(9)

1.9 Mbinu za Utafiti " 19

1.9.1 Muundo wa Utafiti 19

1.9.2 Mahali pa Utafiti . ... . . ... . ... . . ... . . . 19

1.9.3 Sampuli Lengwa na Uteuzi Wake 20

1.9.4 Ukusanyaji wa Data 20

1.9.5 Uchanganuzi wa Data 21

1.9.6 Uwasilishaji wa Matokeo 22

SURA YAPILI

DHANA YA USHAIRI

2.0 Utangulizi 23

2.1 Dhana ya Ushairi na Chimbuko Lake 23

2.2 Mgogoro katika U shairi wa Kiswahili 26

2.3 Ufundishaji na Utahini wa Ushairi katika Shule za Upili 31

2.4 Muhtasari 35

SURA YA TATU

UPOKEZI WA MASHAIRI YA KISWAHILI MIONGONI MWA

WANAFUNZI W A SHULE ZA UPILI

3.0Utangulizi 36

3.1 Maana ya Upokezi 36

3.2 Viwango vya Upokezi 36

(10)

3.2.2 Shairi la Kimapokeo la Kiswahili Sanifu 40

3.3.3 Shairi Huru la Kilahaja 43

3.3.4 Shairi Huru la Kiswahili Sanifu 47

3.3 Mambo Yaliyoathiri Upokezi wa Mashairi ya Kiswahili miongoni mwa

Wanafunzi 50

3.3.1 Ufunzaji, Ujifunzaji na Utahini wa Mashairi ya Kiswahili 50

3.3.2 Mielekeo ya Wanafunzi 53

3.3.3 Lugha katika Mashairi ya Kiswahili 55

3.3.4 Aina ya Mashairi ya Kiswahili 62

3.3.5 Misingi Tofauti ya Mashairi miongoni mwa Wanafunzi wa Shule

za Upili 63

3.4 Muhtasari 65

SURA YANNE

ATHARI YA VIWANGO VYA UPOKEZI WA MASHAIRI KWA

MATOKEO YA MITlHANI

4.0 Utangulizi 64

4.1 Athari ya Viwango vya Upokezi kwa Mashairi ya Kimapokeo 64

4.2 Athari ya Viwango vya Upokezi kwa Mashairi Huru 69

4.3 Muhtasari 71

(11)

SURA YATANO

MUHTASARI, MATOKEO, MAPENDEKEZO NA MCHANGO WA

UTAFITI

5.0 Utangulizi 72

5.1 Muhtasari wa Sura 72

5.2 Matokeo ya Utafiti 74

5.3 Mapendekezo 78

5.4 Mchango wa Utafiti 80

MAREJELEO 82

KIAMBATISHO A 86

KIAMBATISHO B 88

KIAMBATISHO C 90

KIAMBATISHO D 92

KIAMBA TISHO E 93

KIAMBATISHO F 95

(12)

SURA YAKWANZA

1.0 Utangulizi

Sura hii .imeangazia usuli wa utafiti huu, suala la utafiti, maswali ya utafiti,

madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada hii pamoja na upeo na mipaka ya

utafiti. Vilevile, sura hii imemulika yaliyoandikwa kuhusu mada pamoja na

nadharia iliyoteuliwa kuwa msingi wa utafiti huu, yaani Nadharia ya Mwitikio wa

Msomaji. Aidha, mbinu za utafiti ikiwa ni pamoja na muundo wa utafiti, mahali

pa utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data, uchanganuzi wa data na

uwasilishaji wa matokeo zimefafanuliwa hapa.

1.1 Usuli

Ushairi wa Kiswahili una historia ndefu katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili.

Kwa sababu hiyo, ushairi wa Kiswahili umekuwa ukifundishwa na kutahiniwa

katika mtihani wa fasihi ya Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya tangu

mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulipoanzishwa. Kutokana na haya, kumekuwa na

upokezi wa viwango tofauti tofauti wa mashairi hayo miongoni mwa wanafunzi

wa shule za upili nchini Kenya. Baadhi ya wahakiki wa Kiswahili kama vile

Knappert (1979), Mazrui na Kazungu (1981), Kezilahabi (1983), Senkoro (1988),

Njogu na Chimerah (1999) na King'ei na Kemoli (2001) wamegawa ushairi wa

Kiswahili katika vipindi vinne vya kihistoria:

(i) Kipindi cha Urasimi Mkongwe.

(ii) Kipindi cha Utasa.

(iii) Kipindi cha Urasimi Mpya.

(13)

(iv) Kipindi cha Ushairi wa Sasa wa Kiswahili.

Mashairi ya Kipindi cha Urasimi Mkongwe - kinachokadiriwa kuanza mwaka wa

1728 - yalizingatia zaidi muundo wa beti, mikarara, urari wa vina na urari wa

mizani.Katika kipindi hiki,kulikuwa na mashairi ya tarbia, tathlitha, takhmisa na

malumbano ambayo yalizingatia kanuni za utunzi wa mashairi. Rata hivyo,

mashairi ya Kiswahili yaliyokuwa maarufu zaidi katika kipindi hiki ni tenzi.

Baadhi ya tenzi hizo ni kama vile: Utenzi wa Tambuka (1728), Utenzi wa

Hamziya (1849), Utenzi wa Al Inkishafi (1810-1820), Utenzi wa Fumo Liyongo,

Utenzi wa Mwana Kupona na Utenzi wa Mikidadi miongoni mwa tenzi

nymgmezo.

Katika Kipindi cha Utasa (1885 - 1945), kulikuwa na maandishi machache mno

na kanuni za utunzi wa mashairi zilianza kufifia katika kipindi hiki. Rata hivyo,

mashairi yaliyotungwa katika kipindi hiki yalizidi kuzingatia sifa za mashairi

yaliyotungwa katika Kipindi cha Urasimi Mkongwe. Tenzi za Vita vya Majimaji

na Vita vya Uhuruziliandikwa katika kipindi hiki.

Katika Kipindi cha Urasimi Mpya, kanuni za utunzi wa mashairi zilizoanzishwa

katika Kipindi cha Urasimi Mkongwe zilianza kufufuliwa. Mashairi katika kipindi

hiki yaliainishwa kulingana na kanuni zilizoorodheshwa na Amri Kaluta Abedi

(1954).Sheria hizi zilihusisha idadi ya mishororo katika kila ubeti,urari wa vina,

urari wa mizani na vipande miongoni mwa zingine. Washairi waliosifika katika

kipindi hiki ni kama vile Amri Abedi, Mathias Mnyampala, Shaaban Robert na

(14)

Kipindi cha Sasa cha Ushairi wa Kiswahili kimeshirikisha tungo ambazo

zimekuwa zikitungwa na wasanii wa Kiswahili kuanzia mwishoni mwa miaka ya

1960 (Maitaria 2012:2). Hivyo, ushairi katika kipindi hiki hushirikisha mashairi

ambayo huzingatia zaidi arudhi, yale ambayo hayazingatii sana arudhi na yale

yasiyozingatia arudhi katika uwasilishaji wake. Baadhi ya washairi wa kipindi

hiki ni kama vile: Euphrase Kezilahabi, Alamin Mazrui, Ebrahim Hussein,

Mugyabuso Mulokozi, Jared Angira na Kulikoyela Kahigi. Baadhi ya washairi wa

kipindi hiki wanadai kuwa si lazima kwa mashairi ya Kiswahili kuzingatia sheria

za utunzi wa mashairi na kwa hivyo wanapinga sheria za kutunga mashairi

zilizowekwa na wanamapokeo.

Kutokana na historia hii fupi ya ushairi wa Kiswahili, ni dhahiri kuwa kuna aina

mbili kuu za mashairi ya Kiswahili:mashairi ya kimapokeo yanayozingatia sheria

za utunzi wa mashairi na mashairi hum ambayo hayafuati sheria za utunzi wa

mashairi. Hata hivyo, ni bayana kuwa mashairi ya kimapokeo yana historia ndefu

katika fasihiya Kiswahili yakilinganishwa na mashairi hum.

Licha ya kuwa mashairi ya kimapokeo yana historia ndefu katika fasihi ya

Kiswahili yakilinganishwa na mashairi hum, mashairi yote mawili yamekuwa

yakifunzwa na kutahiniwa katika shule za upili nchini Kenya. Katika shule za

upili, mashairi haya hutahiniwa katika mitihani ya kitaifa ya kila mwaka katika

karatasi ya tatu (102/3) ambayo hushughulikia fasihi ya Kiswahili kwa jumla.

Hata hivyo, tangu mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulipoanzishwa, imedhihirika wazi

kuwa mashairi ya kimapokeo yametahiniwa zaidi katika karatasi ya Kiswahiliya

102/3 ya mtihani wa kitaifa wa fasihi katika shule za upili nchini Kenya

(15)

yakilinganishwa na mashairi huru. Jambo hili limetokana na kuwa mashairi ya kimapokeo yamekuwepo kwa muda rnrefu katika historia ya fasihi ya Kiswahili yakilinganishwa na mashairi huru. Isitoshe, mashairi ya kimapokeo ndiyo maarufu zaidi miongoni mwa walimu na wanafunzi, katika diwani ya mashairi na katika vyombo vya habari kama vile redia na gazeti la Taifa Leo nchini Kenya. Aidha, mashairi hum yanahitaji uchambuzi wa kina na hivyo basi yanafaa sana kwa wanafunzi wa ngazi za juu za elimu kama vile wanafunzi wa vyuo vikuu hata ingawa hufunzwa na kutahiniwa katika mitihani ya shule za upili. Kwa sababu hiyo, utafiti huu umechunguza, umebainisha na ·umetathmini viwango vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili. Vilevile, utafiti huu umebainisha mambo yaliyotatiza na kufanikisha upokezi wa wanafunzi hawa kuhusu mashairi hayo pamoja na kuweka wazi athari ya upokezi wao dhidi ya mashairi hayo katika matokeo ya mtihani wa fasihi na lugha ya Kiswahili kwa jumla.

1.2 Suala la Utafiti

Utafiti huu umechunguza viwango vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili katika jimbo la Nakuru. Upokezi wa mashairi ya Kiswahili umekuwa tatizo ambalo limedumu kwa muda rnrefu na hivyo kuathiri matokeo ya wanafunzi wa shule za upili katika mitihani ya kitaifa

(16)

Vilevile, kumekuwa na tafiti nyingi ambazo zimefanywa kuhusu ushairi wa

Kiswahili zikiangazia vipengele vyake vingine kama vile maudhui, dhamira na

mtindo katika mashairi ya Kiswahili, ufundishaji na ujifunzaji wa mashairi,

vigezo badalia vya uainishaji wa mashairi ya Kiswahili na changamoto za

uchanganuzi na ufasiri wa ushairi katika shule za upili nchini Kenya. Hakuna

utafiti ambao ulikuwa umefanywa kuhusu upokezi wa mashairi ya Kiswahili

katikajimbo la Nakuru. Kwa hivyo, kulikuwa na haja ya utafiti kufanywa kuhusu

upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili ili

kuziba pengo hili kwa mihimili ya nadharia ya Mwitikio wa Msomaji. Nadharia

hii inazingatia kuwa mwanafunzi kama msomaji huipokea kazi ya fasihi kwa

kuzingatia mielekeo yake binafsi.

Katika utafiti huu, upokezi wa wanafunzi wa shule za upili katika jimbo la

Nakuru kuhusu mashairi ya Kiswahili umechunguzwa kwa kina. Jimbo hili ni

mojawapo kati ya majimbo arobanne na saba nchini Kenya lenye shule za kitaifa,

za kimaeneo na za wilaya ambapo mashairi ya Kiswahili hufunzwa na

kutahiniwa. Kwa hivyo, viwango mbalimbali vya upokezi miongoni mwa

wanafunzi wa shule za upili katika jimbo hili, mambo yaliyofanikisha na kutatiza

upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwao pamoja na athari ya upokezi

wao katika mtihani wa fasihi wa karatasi ya 102/3 hasa katika sehemu ya ushairi

imewekwa wazi.

Kutokana na ushairi wa Kiswahili kuwa sanaa muhimu kwa walimu, wanafunzi

na jarnii kwa jumla, kulikuwa na haja ya upokezi wa utanzu huu miongoni mwa

wanafunzi wa shule za upili kufanyiwa utafiti ili kuirnarisha upokezi wake

(17)

miongoni mwa wanafunzi. Mashairi ambayo yametumiwa katika utafiti huu yametolewa katika karatasi ya 102/3 ya mitihani ya awali ya kitaifa.

1.3 Maswali ya Utafiti

Katika kutathmini upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili, utafiti huu uliongozwa na maswali yafuatayo:

(a) Mashairi ya Kiswahili yalipokewa vipi na wanafunzi wa shule za upili za jimbo la Nakuru?

(b) Ni mambo yapi yaliyotatiza na kufanikisha upokezi wa mashairi haya miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili?

(c) le, upokezi wa wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili umeathiri vipi matokeo yao katika mitihani ya fasihi na hasa sehemu ya ushairi?

1.4 Madhumuni ya Utafiti

Utafiti huu ulinuia kutirniza malengo yafuatayo:

(a) Kubainisha na kueleza viwango mbalimbali vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili zajimbo la Nakuru.

(b) Kufafanua mambo yaliyotatiza na kufanikisha upokezi wa mashairi ya Kiswahili rniongoni mwa wanafunzi wa shule za upili katika jimbo hili.

(18)

1.5 Sababu za Kuchagua Mada

Mashairi ya Kiswahili ni mojawapo ya fani na nguzo kuu ya fasihi ya Kiswahili

yenye umuhimu mkubwa kwa wanafunzi, walimu na jamii kwa jumla. Kwa

sababu hiyo, mashairi ya Kiswahili yamekuwa yakifunzwa katika shule zote za

upili nchini Kenya na kutahiniwa katika mitihani ya kitaifa ya fasihi katika

karatasi ya tatu ya Kiswahili ya 102/3, kabla na baada ya mfumo wa elimu wa

8-4-4 kuanzishwa. Jinsi wanafunzi hupokea mashairi ya Kiswahili huathiri pakubwa

matokeo yao katika mtihani wa fasihi na lugha ya Kiswahili kwa jumla. Utafiti

huu basi ulichochewa na azma ya kutathmini viwango tofauti tofauti vya upokezi

vya wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili ili kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji

wake.

Vilevile, ingawa tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ushairi wa Kiswahili, hakuna

utafiti ambao umefanywa kuhusu upokezi wa wanafunzi wa shule za upili katika

jimbo la Nakuru kuhusu mashairi ya Kiswahili hasa uliohusisha ukusanyaji wa

data kutoka nyanjani. Kwa mfano, Chacha (1980) na (1987), Momanyi (1991) na

(1998), Masinde (1992) na (2003) na Mwangi (2005) miongoni mwa wengine ni

kati ya waliofanya utafiti kuhusu ushairi wa Kiswahili wakiegemea kwenye

vipengele kama vile maudhui, mtindo, dhamira, wahusika, maana na ufasiri wa

ushairi, ufunzaji na ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili.

Kwa mujibu wa Gibbe (1978), mashairi ni zao la jamii na kwa hivyo yana dhima

kubwa katika jamii. Hali kadhalika, kwa mujibu wa Wizara ya Elimu (2002),

ushairi hufunzwa shuleni ili wanafunzi wapate maadili na mafunzo yaliyomo

(19)

katika mashairi. Hii ni kwa sababu mashairi yamefungamana na maadili na tamaduni za jamii mbalimbali. Isitoshe, mashairi hutekeleza majukumu mengine kama vile kuburudisha, kuelimisha, kueneza na kuhifadhi utamaduni wa jamii, kuonya na kutoa mawaidha. Kwa sababu ya majukumu haya yanayotekelezwa na mashairi, upokezi wa wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili yalihitaji kubainishwa ili kutambua iwapo majukumu haya yalifikiwa au la.

Utafiti huu utakuwa na manufaa mengi katika taaluma ya fasihi kwa kuboresha, kubadilisha na kurekebisha viwango vya upokezi wa wanafunzi wa shule za upili kuhusu mashairi ya Kiswahili. Kubadilika na kuimarika kwa viwango vyao vya upokezi kutafanya utanzu huu kuwa maarufu na hivyo kupendwa sio tu na wanafunzi pekee bali walimu na wanajamii kwa jumla. Hali hii itaimarisha matokeo ya wanafunzi katika mitihani ya kitaifa ya fasihi na ya lugha ya Kiswahili kwa jumla pamoja na kuwaadilisha wanafunzi na wanajamii kwa kuwa mashairi yamefungamana

.

na tamaduni za jamii mbalimbali katika taifa letu .

(20)

1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti

Kuna aina mbili kuu za mashairi:mashairi ya kimapokeo na mashairi huru. Utafiti

huu umechunguza upokezi wa aina zote mbili za mashairi ya Kiswahili miongoni

mwa wanafunzi wa shule za upili katika jimbo la Nakuru kwa kuwa mashairi yote

mawili yamekuwa yakifunzwa na kutahiniwa katika karatasi ya tatu ya Kiswahili

ya 102/3 (Karatasi ya fasihi) ya mitihani ya mwigo na ya kitaifa kwa zaidi ya

mwongo mmoja uliopita.

Shule za upili za jimbo la Nakuru zilitumiwa katika utafiti huu. Huku kumetokana

na jimbo hili kuwa na shule nyingi za umma na za kibinafsi zenye hadhi ya

kitaifa, kieneo na kiwilaya na nyingi ya shule hizi huzingatia mfumo wa elimu

wa 8-4-4 ambapo mashairi ya Kiswahili hufunzwa na kutahiniwa katika mitihani

ya mwigo na ya kitaifa. Aidha, shule nne za upili zimeshirikishwa katika utafiti

huu: Shule ya Upili ya Moi-Kabarak, Shule ya Upili ya Wavulana ya Rongai,

Shuleya Upili ya Wasichana ya Mary Mount na Shule ya Upili ya Wasichana ya

A.Le. Morop.

Shule ya Upili ya Moi-Kabarak ilichaguliwa kutumika katika utafiti huu kwa

kuwa ni shule mseto yenye hadhi ya kitaifa na wanafunzi ambao husajiliwa katika

shule hii hutoka katika majimbo yote arobanne na saba nchini Kenya. Shule hii

ilitumika katika utafiti wetu kutokana na matokeo mazuri katika mitihani ya

kitaifa hasa katika somo la Kiswahili kwa miaka mitano iliyopita. Kwa hivyo,

viwango vya wanafunzi wa shule hii vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili

(21)

vilitusaidia kueleza sababu ya kuwepo kwa matokeo mazuri katika mitihani ya

kitaifa katika somo la Kiswahili.

Vilevile, Shule ya Upili ya Wavulana ya Rongai na Shule ya Upili ya Wasichana

ya Mary Mount zenye hadhi ya shule za majimbo ziliteuliwa kwa kuwa shule hizi

huwasajili wanafunzi kutoka kwa maeneo mbalimbali ya jimbo la Nakuru. Aidha,

Shule hizi mbili zimekuwa na matokeo ya wastani katika mitihani ya kitaifa ya

somo la Kiswahili kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kwa hivyo, utafiti huu

ulinuia kutambua iwapo matokeo haya yalichangiwa na viwango vya upokezi vya

wanafunzi hawa.

Pia, Shule ya Upili ya Wasichana ya A.I.e. Morop yenye hadhi ya shule ya

wilaya iliteuliwa kwa kuwa shule hii huwasajili wanafunzi kutoka katika wilaya

ya Rongai katika jimbo la Nakuru. Matokeo ya shule hii ya mitihani ya kitaifa

has a katika somo la Kiswahili hayajakuwa ya kuridhisha kwa muda mrefu. Kwa

sababu hiyo, shule hii ilichaguliwa kutumika katika utafiti huu ili kuonyesha

uhusiano uliopo kati ya viwango vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili na

matokeo katika mitihani ya Kiswahili.

Wanafunzi ishirini wa kidato cha tatu na ishirini wa kidato cha nne kutoka kwa

kila shule waliteuliwa na kushirikishwa katika utafiti huu. Utafiti huu ulichukulia

kuwa wanafunzi wa vidato hivi katika shule za upili walikuwa wamefunzwa

mashairi ya Kiswahili na hata kutahiniwa mara kadha na walimu wao.

(22)

kueleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika shairi, kutambua namna

washairi mbalimbali walivyotumia uhuru wao, uteuzi wao wa swali la ushairi

wanapoandika mtihani wa fasihi na matokeo yao katika mijarabu ya mashairi ya

Kiswahili tuliyowapa rniongoni.

1.7Yaliyoandikwa Kuhusu Mada

Baadhi ya watafiti wameshughulikia uchunguzi wa vipengele mbalimbali katika

utanzu wa mashairi ya Kiswahili. Tafiti zao ni muhimu kwa kuwa zimetuelekeza

kwenye masuala yaliyohusiana na utafiti huu. Rata hivyo, tafiti chache

zimefanywa kuhusu upokezi wa wasomi, wanafunzi na wadau kuhusu lugha ya

Kiswahili hasa fasihi ya Kiswahili.

Onyango (1990) alichunguza mielekeo ya wasomi kuhusu maturnizi ya lugha ya

Kiswahili nchini Kenya. Katika kutathmini mielekeo ya wasomi kuhusu lugha ya

Kiswahili, alitaja mielekeo yao kuhusu fasihi ya Kiswahili ambapo alitambua

kuwa wasomi wengi walikuwa na mielekeo chanya kuhusu ushairi wa Kiswahii

kwani walipohojiwa walisema kuwa ushairi wa Kiswahili ni wa kuvutia sana na

una mdundo wa kipekee. Ugunduzi wake uliufaa utafiti huu kwani tulitambua

kuwa mielekeo ya wanafunzi wa shule za upili kuhusu ushairi wa Kiswahili ni

mojawapo wa mambo yaliyoathiri upokezi wao wa mashairi hayo. Rata hivyo,

kazi hizi mbili ni tofauti kwa kuwa japo zote mbili ni tafiti za nyanjani, kazi hii

ilijishughulisha zaidi na jinsi wanafunzi wa shule za upili walivyopokea ushairi

wa Kiswahili kwa kuzingatia jinsi wanavyoyasoma mashairi na kujibu maswali.

(23)

Kanja (1985) alichunguza sababu za ushairi kukosa kuwa maarufu katika shule za upili nchini Kenya. Katika utafiti wake, alitambua kuwa mielekeo ya walimu na wanafunzi ni chanzo mojawapo kinachotatiza ufunzaji wa ushairi katika shule za upili. Alieleza kuwa walimu walikuwa na imani kuwa wanafunzi hawakuwa na uwezo wa kuelewa mashairi kwa kuwa ni magumu. Kulingana naye, jambe hili ndilo huchangia pakubwa matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa. Utafiti huu ulitofautiana na wake kwa kuwa alishughulikia ushairi wa Kiingereza na huu ulishughulikia ushairi wa Kiswahili. Isitoshe, alitaja tu kuwa mielekeo ya wanafunzi hutatiza ufunzaji wa ushairi ilhali huu ulibainisha kuwa mielekeo ya wanafunzi ni jambe mojawapo lililoathiri upokezi wa wanafunzi kuhusu ushairi wa Kiswahili. Vilevile, Kanja alitumia mtazamo wa kielimu ilhali utafiti huu umeongozwa na mtazamo wa kifasihi kando na ule wa kielimu.

Tafiti zilizofanywa kuhusu ushairi wa Kiswahili katika nyanja zake tofauti tofauti ni kama vile Chacha (1980) ambaye alishughulikia mashairi ya Abdilatif na (1987) maana na ufasiri wa ushairi wa Kiswahili. Ndungo (1985) alitafiti kuhusu usawin wa mwanamke katika Utenzi wa Mwanakupona. Momanyi (1991) alichunguza matumizi ya taswira katika Utenzi wa Al-Inkishafi na (1998) alipambanua jinsi mwanamke wa Kiislamu alivyosawiriwa katika ushairi wa Kiswahili.

(24)

kuhusu maendeleo na mabadiliko ya maudhui katika ushairi andishi wa Kiswahili

kwa kuonyesha kuwa maudhui katika ushairi wa Kiswahili huathiriwa na

mabadiliko ya kihistoria na ya kitamaduni katika jamii.

Njogu na Chimera (1999) walionyesha namna ya kuyachambua mashairi ya

Kiswahili kwa kuzingatia vipengele vya maudhui, wahusika, fani, muundo,

mtindo na muktadha. Kazi yao ilitofautiana na hii kwa kuwa kazi yao ilizingatia

uchambuzi wa mashairi ilhali kazi hii iliangazia upokezi wa wanafunzi kuhusu

mashairi ya Kiswahili. Hata hivyo, utafiti huu ulifaidika kutokana na kazi yao

kwani vipengele walivyobainisha vilibainika kuwa na athari kubwa kwa upokezi

wa wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili.

Mwandoe (2002) alifanya uchunguzi kuhusu ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi

wa Kiingereza katika shule za upili katika tarafa ya Voi. Alitambua kuwa

wanafunzi wa shule za upili katika tarafa hiyo waliuona ushairi ukiwa mgumu

kwa kuwa una mafumbo mengi kwa sababu ya matumizi ya lugha ya kijazanda.

Tofauti na utafiti wake ulioshughulikia ushairi wa Kiingereza, utafiti huu

ulijihusisha na kutathmini upokezi wa wanafunzi wa shule za upili kuhusu

mashairi ya Kiswahili katika jimbo la Nakuru. Utafiti huu ulichukua mwelekeo

wa kifasihi na kielimu ilhali wake ulichukua mwelelekeo wa kielimu pekee.

Nyanchama (2005) alieleza kuhusu matumizi ya taswira na ishara katika Sauti ya

Dhiki. Alitambua aina mbalimbali za ishara kama vile taashira, tanakali za sauti

na ishara kamili. Aidha, alichunguza na kutambua taswira zinazotokana na

tashibihi, sitiari na jazanda. Kazi yake ilisaidia katika utafiti huu katika

(25)

kubainisha namna upokezi wa wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili

ulivyoathiriwa na matumizi ya taswira na ishara katika ushairi husika. Wekesa

(2008) naye alitathmini matumizi ya taswira katika ushairi huru wa Kiswahili.

Kazi yake sawia na ya Nyanchama (2005)ilisaidia kubainisha iwapokulikuwa na

uhusiano wowote kati ya upokezi wa wanafunzi kuhusu ushairi huru na matumizi

ya taswira katika ushairi husika. Rata hivyo,kazi yetu ilihusisha mashairi huru na

mashairiya kimapokeo tofauti na yake iliyoangazia shairi huru pekee.

Mwangi (2005) alishughulikia ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi katika shule za

upili wilayani Murang'a. Katika utafiti wake, alikusudia kuonyesha mambo

yaliyofanya ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi katika shule za upili kuwa

mgumu. Alitambua kuwa wasomaji wengi wa ushairi wa Kiswahili hususan

walimu na wanafunzi walidai kwamba ushairi ni mgumu na haueleweki kwa

urahisi. Alitaja kuwa mielekeo hasi ya walimu na wanafunzi kuhusu ushairi wa

.Kiswahili ndiyo ambayo imetatiza ufunzaji na ujifunzaji wake. Utafiti huu ulifaidika kutokana na utafiti wake kwani baadhi ya mambo aliyotambua kuwa

huathiri ufunzaji na ujifunzaji wa ushairi katika shule za upili yalikuwa pia ndiyo

yaliyoathiri upokezi wa ushairi wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule

za upili.

Babusa (2005)alibainisha vigezo badalia vya uainishaji wa mashairi ya Kiswahili

kwa lengo la kuepuka mgogoro kati ya wanamapokeo na wanamapinduzi .

.Alizingatia vigezo kama vile maudhui, fani na idadi ya mishororo. Kazi yake

(26)

alichanganua mielekeo na umilisi wa lugha ya Kiswahili wa wanafunzi katika

mkoa wa Pwani na Nairobi. Utafiti wake ulisaidia katika utafiti huu kubainisha

jinsi mielekeo ya wanafunzi dhidi ya lugha ya Kiswahili ilivyoathiri upokezi wao

wa mashairi ya Kiswahili.

Tafiti za hivi karibuni zilizofanywa kuhusu ushairi wa Kiswahili ni kama wa

Mung'athia (2011) ambaye alitafiti kuhusu ufumbuaji wa mashairi ya Kiswahili

akizingatia Malenga wa Mvita na Malenga wa Vumba. Utafiti wake ulilenga

kufumbu~ mafumbo yaliyo kwenye mashairi hayo. Kazi yake ilitofautiana na hii

kwa kuwa yake ilifanyiwa maktabani ilhali hii ilifanyiwa nyanjani. Hata hivyo,

kazi yake ilisaidia katika utafiti huu katika kubainisha iwapo upokezi wa

wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili ulitokana na uwezo wao wa kufumbua

au kutofumbua mafumbo katika mashairi haya.

Naye Maitaria (2012) alichunguza uainishaji wa ushairi wa Kiswahili kwa

kuzingatia dhima ya methali katika Jicho la Ndani, Bara Jingine, Chembe cha

Moyo, Usanifu wa Ushairi, Kichomi naSauti ya Dhiki. Tungo hizi zote zimekuwa

zikitungwa kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1960. Kazi yake ilitumika

kuonyesha jinsi matumizi ya methali katika ushairi wa Kiswahili yalivyoathiri

upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili

katika eneo la Nakuru.

Utafiti wa Gakuo (2014) ulihusu changamoto za uchanganuzi na ufasiri wa

ushairi wa Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya. Alichunguza ufasiri na

uelewekaji huo kwa mtazamo wa Ki-Hemanitiki na Uhistoria mpya katika kaunti

(27)

za Transnzoia na Mombasa kwa kuhusisha uchunguzi wa muktadha wa

kiutamaduni na jinsi unavyoathiri uelewekaji wa mashairi.

Kutokana na udurusu wa tafiti zilizopitiwa, imedhihirika kuwa licha ya tafiti

nyingi kufanywa kuhusu mashairi ya Kiswahili, hakuna tafiti zilizofanywa ili

kutathmini Il:akubainisha viwango vya upokezi vya wanafunzi wa shule za upili

kuhusu mashairi ya Kiswahili kwa jumla.

1.8 Misingi ya N adharia

Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya mwitikio wa msomaji. Nadharia hii

imeteuliwa kwa kuzingatia kuwa mwanafunzi kama msomaji alitazamiwa

kuipokea kazi ya fasihi kwa kuzingatia mielekeo yake binafsi.

1.8.1 Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji

Nadharia hii ilianza miaka ya sitini na sabini ya kame ya ishirini hasa kule

Marekani na Ujerumani. Waasisi na watetezi wakuu wa nadharia hii ni Stanley

Fish (1980), Jane Tompkins (1980), Wolfgang Iser (1974, 78) Haus Robert Jauss,

Roland Barthes na wengine. Nadharia hii inamtambua msomaji kama mshiriki

mkuu ainbaye anakamilisha maana ya kazi ya fasihi kutokana na ufasiri wake.

Vilevile, nadharia hii inadai kuwa fasihi inafaa ichukuliwe kama sanaa ya utendaji

ambapo kila msomaji huwa na njia yake ya kipekee ya utendaji katika matini.

Waasisi wa nadharia hii wanaamini kwamba maana ya kazi yoyote ya fasihi

inamtegemea msomaji wa kazi hiyo kwa kiasi kikubwa. Kwa hivyo, msomaji wa

(28)

Kimapokeo, msomaji huwa na mawazo kuhusu matini anayopitia. Kutokana na

tajribaya usomaji, msomaji hupata hisi maalurn.

Wamitila (2003) anasema kwamba istilahi hii huturniwa kurejelea mkabala wa

kifasihi unaojishughulisha na jinsi kazi za kifasihi zinavyopokelewa na wasomaji

wakatifulani au katika mpito wa wakati. Nadharia hii inamtambua msomaji kama

kiungo muhimu katika fasihi na ambaye hukarnilisha maana ya fasihi kutokana na

ufasiri wake binafsi. Wafula na Njogu (2007) wakizungurnzia nadharia hii,

wanasema kwamba msomaji anatazamiwa kuipokea kazi ya fasihi kwa kuzingatia

mieleko yake binafsi. Senkoro (1988:3) anaeleza kuwa nadharia hii inakiri na

kutambua nafasi muhimu ya hadhira ya wasomaji wa kazi ya fasihi. Anaongeza

kuwa nadharia hii inasisitiza urnuhimu wa hadhira wakati nadharia zingine

zilizotangulia hii ya upokezi zilisisitiza urnuhimu wa mtunzi wa kazi ya fasihi.

Kwa mujibu wa wananadharia hii, hadhira huyabashiri na kuyahusisha

wayakutayo hurno na yale waliyokwisha kushuhudia maishani mwao. Kimsingi

basi, nadharia hii inajaribu kuchunguza kile kitendo cha usomaji kwa

kurnchukulia msomaji kama ajaye na dhana, amali na imani ambazo

huthibitishwa na yale anayoyakuta katika kazi ya fasihi. Msomaji huyachuja na

kuyapanga yale yanayomzukia kuwa na maana kwake kutoka kwa yale

anayokurnbana nayo katika usomaji wake.

(29)

Mihimili ya nadharia hii

Mihimili ya nadharia hii na ambayo imetumika katika utafiti huu m kama

ifuatayo:

1. Nadharia hii inazingatia usomaji, msomaji na upokezi. Kushadidia haya,

Huck (1976) aneleza kuwa lengo kuu hapa ni kuwabainisha wasomaji

pamoja na tendo zima la usomaji.

2. Msomaji huikamilisha kazi ya sanaa kwa kuijaliza kwa usomaji makini au

kuidhalilisha kwa usomaji wa kiholela.

3. Nadharia hii inasisitiza athari za kazi za fasihi juu ya akili na maarifa ya

msomaji. Kwamba wasomaji mbalimbali hufasiri athari hizi kupitia njia

tofauti tofauti kutegemea tofauti kati ya matini na hisia zao za kibinafsi.

4. Nadharia hii pia inasisitiza narnna matini inavyoelekeza au kutatiza

mwitikio wa msomaji, sifa inayozua usomaji mzuri au mbaya wa kazi

inayohusika.

5. Msomaji ni mtu ajaye na dhana, amali na imani ambazo huthibitishwa na

yaleanayoyakuta katika kazi ya fasihi.

Mhimili wa kwanza ulitumiwa na mtafiti kutambua viwango mbalimbali vya

wanafunzi vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili ilhali mhimili wa pili, wa tatu,

wa nne na watano ulitumika kubainisha mambo yaliyoathiri upokezi wa mashairi

ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili na hivyo kuathiri

(30)

1.9.0 Mbinu za Utafiti

Utafiti huu umehusisha utafiti wa maktabani na wa nyanjam ili kupata data

inayohusiana na mada.

1.9.1 Muundo wa Utafiti

Utafiti huu ni wa kimaelezo na umefanyiwa nyanjani na matokeo yametolewa

kwa njia ya kimaelezo na ufafanuzi.

1.9.2 Mahala pa Utafiti

Utafiti huu umefanywa katika shule teule za upili za Moi Kabarak, Rongai, Mary

Mount na A.LC. Morop zilizo katika jimbo la Nakuru.

1.9.3 Sampuli Lengwa na Uteuzi Wake

Sampuli lengwa katika utafiti huu ilikuwa ni wanafunzi wa kidato cha tatu na cha

nne kutoka shule teule za upili za Moi- Kabarak, Rongai, Mary Mount na A.LC.

Morop za jimbo la Nakuru. Wanafunzi ishirini wa kidato cha tatu na ishirini wa

kidato cha nne kutoka katika kila shule waliteuliwa kimaksudi na kushirikishwa

katika utafiti huu. Shule ya Upili ya Moi-Kabarak yenye hadhi ya shule ya kitaifa

iliteuliwa kimaksudi kwa kuwa matokeo ya wanafunzi wa shule hii katika

mitihani ya kitaifa hasa katika somo la Kiswahili yalikuwa mazuri na ya

kuridhisha. Zaidi ya hayo, wanafunzi waliosajiliwa katika shule hii walitoka

katika maeneo yote nchini Kenya.

Shule ya Upili ya Wavulana ya Rongai na Shule ya Upili ya Wasichana ya Mary

Mount zenye hadhi ya shule za kimaeneo ziliteuliwa kutumika katika utafiti huu

(31)

kwa kuwa wanafunzi waliosajiliwa katika shule hizi walitoka katika jimbo zima

la Nakuru. Zaidi ya hayo, matokeo yao katika mitihani ya kitaifa katika somo la

Kiswahili yalikuwa ya wastani lakini yenye kuridhisha.

Hatimaye, uteuzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya A.LC. Morop yenye hadhi ya shule ya wilaya ulitokana na matokeo ya kutoridhisha ya wanafunzi wa shule

hii katika mitihani ya kitaifa na hasa katika somo la Kiswahili. Ilichukuliwa kuwa

tofauti katika matokeo ya mitihani ya kitaifa miongoni mwa wanafunzi wa shule

hizi ilitokana na viwango tofauti tofauti vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili.

1.9.4 Ukusanyaji wa Data

Data iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani.

1.9.4.1 Ukusanyaji wa Data Maktabani

Utafiti huu umefanywa katika maktaba kuu ya Chuo Kikuu cha Kenyatta,

maktaba ya shule zilizotumika katika utafiti huu na maktaba ya Idara ya Kiswahili

ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Maktaba hizo zina hifadhi za tasnifu, majarida,

makala na vitabu muhimu vilivyohusiana na mada ya utafiti. Kupitia kwa

usomaji, mtafiti aliweza kuteua mashairi yaliyotumiwa kama mijarabu ya

wanafunzi katika utafiti huu. Pia, vitabu mbalimbali kuhusu nadharia na vile

vilvyohusiana na mada vilisomwa ili kupata udurusu. Isitoshe, tasnifu, majarida,

(32)

1.9.4.2 Ukusanyaji wa Data Nyanjani

Ukusanyaji wa data nyanjani ulihusisha wanafunzi wa shule teule za upili kupewa

mijarabu ya mashairi huru na ya kimapokeo ya Kiswahili. Mijarabu hii

ilimwezesha mtafiti kukadiria viwango tofauti tofauti vya upokezi wa mashairi ya

Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili. Mijarabu hii pia

ilimwezesha mtafiti kubainisha mambo yaliyoathiri upokezi wa mashairi haya

pamoja na kutambua jinsi viwango vyao vya upokezi vilivyoathiri matokeo yao.

Vilevile, hojaji za maswali mseto zilitumika kukusanya data nyanjani. Maswali ya

hojaji yalimwezesha mtafiti kutambua mambo yaliyotatiza na yaliyofanikisha

upokezi wa mashairi kwa wanafunzi wa shule za upili. Mahojianao yalikuwa

muhimu ili kupata ufafanuzi wa mtazamo wa wanafunzi kuhusu mashairi ya

Kiswahili kwa jumla. Kadhalika, walimu wanaofunza Kiswahili katika shule hizi

walihojiwa ili kutambua jinsi walivyowafunza wanafunzi wao mashairi ya

Kiswahili na maoni yao kuhusu upokezi wa wanafunzi wao kuhusu mashairi ya

Kiswahili kwa jumla.

1.9.5 Uchanganuzi wa Data

Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia maswali na malengo ya

utafiti kuhusu mada ya upokezi wa wanafunzi wa shule za upili kuhusu mashairi

ya Kiswahili. Uchanganuzi vilevile uliongozwa na mahitaji ya utafiti na mihimili

ya nadharia ya mwitikio wa msomaji. Katika kuchanganua data, viwango vya

upokezi wa wanafunzi wa shule za upili kuhusu mashairi ya Kiswahili na mambo

yaliyoathiri upokezi wa wanafunzi hawa kuhusu mashairi ya Kiswahili

(33)

yalibainishwa. Aidha, mtafiti alionyesha namna upokezi wa wanafunzi wa shule

za upilikuhusu mashairi ya Kiswahili yalivyoathiri matokeo yao katika mitihani

ya fasihi.

1.9.6 Uwasilishaji wa Matokeo

Data iliyopatikana katika utafiti huu ilichanganuliwa kwa kuzingatia maswali na

malengo ya utafiti kwa uelekezi wa mihimili ya nadharia iliyotumiwa na kisha

matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa lugha ya nathari katika sura tano. Mtafiti

(34)

SURAYAPILI

DHANA YA USHAIRI WAKISWAHILI

2.0 Utangulizi

Sura hii imefafanua maana ya dhana ya ushairi wa Kiswahili pamoja na kutoa

maelezo kuhusu chimbuko lake. Aidha, mgogoro kati ya watunzi wa mashairi ya

kimapokeo na watunzi wa mashairi huru umejadiliwa kwa kifupi. Isitoshe,

historia ya ufunzaji na utahini wa mashairi ya Kiswahili katika shule za upili

nchini Kenya imeangaziwa. Vilevile, viwango vya elimu na tajriba za walimu

wanaofundisha mashairi katika jimbo la Nakuru zimeelezwa. Utafiti huu

umetumia vigezo hivyo ili kubainisha viwango vya upokezi wa mashairi ya

Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili katikajimbo la Nakuru.

2.1 Dhana ya Ushairi na Chimbuko Lake

Ushairi wa Kiswahili umetolewa fasiri na wataalamu mbalimbali. Hata hivyo,

kutokana na mitazamo, maelezo na mawazo ya washairi na wataalam mbalimbli

kama vile Shaaban Robert (1968), Mnyampala (1970), Abedi (1954), Abdilatif

Abdalla (1973), Farouk Topan (1973), Massamba (1983), Msokile (1993) na

Wamitila (2003), ni bayana kuwa tungo za ushairi huwa na sifa bainifu kama

ifuatavyo:

(a) Fani na maudhui ni viungo muhimu sana katika mashairi na kwamba kila

mojawapo lina jukumu lakemahsusi.

(b) Fikira nzito au hisi za ndani ni vitu muhimu kabisa katika shairi.

(35)

(c) Maneno na lugha katika ushairi hufuata mpangilio fulani tofauti na

mpangilio wa maneno katika tungo nyinginezo.

(d) Lugha ya shairi ni sharti iwe ya mkato, yaani iweze kueleza mambo mengi

kwa muhtasari.

(e) Shairi linaweza kufuata kanuni za utunzi wa mashairi kama vile vina na

mizani au likakosa kufuata kanunihizi. Hata hivyo, vina namizani ndivyo

vinavyojenga umbo la shairi.

Kwa hivyo, ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha ya mkato kuelezea

hisia za ndani za binadamu kwa mpangilio fulani wa maneno. Lugha ya ushairi

hivyo basi inatokana na kuyapanga maneno na mawazo kwa njia bora ili

wasomaji au wasikilizaji waweze kutambua maudhui makuu. Hii ina maana kuwa

maudhui ndiyo kiini cha ushairi na maudhui hutegemea hali ya mazingira ya

utamaduni.

Kulingana na Sheikh Alamin katika makala yakeArusi ya Kiswahili (1940),Amri

Abedi katika utangulizi wa Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri

(1954), Mnyampala katika Waadhi wa Ushairi (1965), Shihabdin Chiraghdin

katika utangulizi wa Diwani ya Ahmed Nassir,Malenga wa Mvita (1972)na Ruo

Kimani Ruo (1989) katika Nguzo za Ushairi wa Kiswahili, ushairi wa Kiswahili

ulianzishwa kama nyimbo na wenyeji wa Pwani ya Afrika Mashariki kabla ya

kufikakwawageni.

Kuimbwa kwa. nyimbo hizi hapo mwanzoni kulikuwa hakufuati utaratibu

(36)

kama kaida za ushairi zilivyozowewa hadi sasa zinavyohitaji. Nyimbo hizi

ziliimbwa katika magoma ya harusi, katika pungwa, jandoni na unyagoni, wakati

wa kuwabembeleza watoto, wakati wa kuomboleza na wakati wa kutekeleza

shughuli mbalimbali za kijamii.

Jinsi manju walivyozidi kuziimba nyimbo zao ndivyo ilivyotokea haja ya kutumia

utaratibu maalumu wa kuziimba; utaratibu wa kutumia urari wa vina vya mwisho.

Utaratibu wa kuwa na urari wa vina vya kati na ulinganifu wa mizani ukawa

hauzingatiwi. Ruo Kimani (1989:8) katikaNguzo za Ushairi wa Kiswahili anatoa

mfano ufuatao:

Nipa kitambuu na kipopoo Na tumbaku njema yenye kileo Mahaba ya mume kula na nguo Na maneno mema yenye kituo

Baadaye, kukaja nyimbo zenye mistari mingi na mizani nyingi vilevile

zilizolingana katika kila mstari lakini bado hazikuwa na ulinganifu wa vina vya

kati na nyingine zilikuwa na vina ambavyo havikuwa na urari wowote. Nyimbo

za aina hii zilikuwa ni za kutumbuiza tu nazo zilijulikana kama tumbuizo.

Nyimbo hizi zilianza kugawanywa katika vifungu vyenye mistari michache

michache na kila mstari wa ubeti ukawa na mizani sawa na mizani ya mstari

mwingine. Hatua hii iliendelezwa na beti za nyimbo zikafanywa kuwa na urari wa

vina vya kati na vina vya mwisho. Nyimbo nyingi katika utanzu huu zilikuwa ni

zile za tathlitha na tathnia ingawa kulikuwa na nyingine yenye mistari zaidi ya

(37)

hiyo iliyotajwa. Baada ya maendeleo haya, ndipo kulitokea tungo zingine ambazo

sasa tunaziita mashairi.

Utungaji wa mashairi uliposhamiri, miundo mbalimbali ya mashairi ilianza

kuibuka lakini muundo uliokuwa maarufu na uliopendwa sana ni ule wa mistari

minne na mizani kumi na sita katika kila mstari. Umaarufu wa mashairi

uliwafanya watunzi waanze kuyatumia katika kusimulia matukio makubwa ya

kihistoria kama vile: vita, njaa, ukame na ujasiri wa watu fulani katika jamii

kupitia kwa tungo ndefu za kishairi zilizojulikana kama utenzi. Tungo hizi za

utenzi zilikuwa na sifa bainifu kama vile: kuwa na beti nyingi (mia mbili hivi au

zaidi) na mizani chache katika kila mstari (aghalabu zilikuwa nane katika kila

mstari). Isitoshe, mistari ya tenzi haikugawanywa katika vipande kama ilivyo

katika mashairi mengi na kila ubeti una mistari minne.

Kwa muhtasari, ushairi wa Kiswahili ulitokana na nyimbo zilizoirnbwa katika

shughuli, nyakati na mahali tofauti tofauti katika jamii za Afrika Mashariki kabla

ya kufika kwa wageni.

2.2 Mgogoro katika Ushairi wa Kiswahili

Kulingana na Kezilahabi (1983), ill vigumu kueleza lini hasa mashairi ya

Kiswahili yalianza kuchukua umbo lake la kimapokeo na ni vigumu pia kueleza

lini hasa shairifulani lilianza kuonekana katika hali ya maandishi. Anasema kuwa

haya yametokana na kuwako kwa mashairi hayo katika hali ya fasihi simulizi

(38)

Hata hivyo, ni dhahiri kuwa mashairi ya Kiswahili yaliyotungwa katika kipindi

cha Urasimi (1728 1885) yalizingatia kanuni za utunzi wa mashairi kama vile:

muundo wa beti, mikarara, urari wa vina na urari wa mizani. Ushairi wa

Kiswahili ambao unahusishwa na kipindi hiki ni utenzi. Baadhi ya watunzi wa

mashairi ya kipindi hiki ni kama vile: Muyaka Bin Haji, Bwana Mataka, Ali Koti,

Muhammad Kijumwa na Hemedi Abdalla. Mashairi ya tarbia, tathlitha, takhmisa

na malumbano ambayo yalizingatia kanuni za utunzi wa mashairi yalikuwepo pia

katika kipindi hiki. Kipindi hiki ndicho kilichoweka msingi wa ushairi andishi.

Katika miaka ya 1945 - 1960, kanuni za utunzi wa ushairi wa Kiswahili

zilizoanzishwa katika kipindi cha urasimi rnkongwe zilianza kufufuliwa. Kipindi

hiki kilijulikana kama kipindi cha Urasimi Mpya kichoshuhudia utunzi wa

mashairi mengi yaliyojulikana kama mashairi ya kimapokeo. Washairi

waliochipuka katika kipindi hiki ni Shaaban Robert, Said Karama, Mathias

Mnyampala, Ahmed Nassir, Amri Abedi, Khamis Amani Khamis (Nyamaume),

Abdalla Baruwa, Mdanzi Hanasa, Hassan Mwalimu Mbega na wengine. Shairi

lililoenea sana katika awamu hii ni shairi la tarbia lenye mishororo minne katika

kila ubeti na mizani kumi na sita katika kila mshororo, mtindo uliotumiwa sana na

Muyaka Bin Haji katika karne ya kumi na nane. Wanamapokeo wakiongozwa na

Amri Abedi (1954), walishikilia kuwa kutunga mashairi mazuri ya aina hii

kulihitaji mambo yafuatayo:

(i) Mizani iwe sawa katika kila mstari na mashairi ya aina hii yalihitaji

mizani ya kila mstari iwe kumi na sita, bila kupungua, bila kuzidi; kila

mstari ukiwa na sehemu mbili zenye mizani nane kila sehemu.

(39)

(ii) Vina viwe katika mizani ya nane na ya kumi na sita katika mistari mitatu ya kwanza ya mashairi yenye mistari minne katika kila ubeti na kwamba kuwe na mtiririko wa vina vya mwisho.

(iii) Kituo ambao ni mstari wa mwisho katika kila ubeti huwa ama ni kiini cha habari au kimalizio; nao hubadilika: kina cha mwisho huja kati na cha kati huenda mwisho kwa mujibu wa desturi nzuri ya utungaji. (iv) Kutosheleza. Kwamba kila ubeti ujitosheleze kadri iwezekanavyo,

yaani, uwe na maana kamili na usingoje kutimizwa na ubeti ufuatao.

Cv) Shairi lazima liimbike.

Ili kuwa na urari wa vina na mizani, washairi wa kimapokeo walikuwa na uhuru wa kupunguza silabi katika maneno, kuongeza silabi katika maneno, kubadilisha maendelezo ya maneno na hata kutumia maneno ya kizamani, lengo kuu likiwa kuzingatia kanuni za utunzi wa mashairi ya Kiswahili.

(40)

Baadhi ya washairi wa kipindi hiki wanadai kuwa si lazima kwa mashairi

kuzingatia sheria za utunzi wa mashairi na kwa hivyo wanapinga sheria

zilizowekwa na Wanamapokeo. Kwa sababu hiyo, mashairi mengi katika awamu

hii hayafuati kanuni za utunzi wa mashairi na hii ndio sababu yanajulikana kama

mashairi huru. Baadhi ya washairi wa kipindi hiki ni kama vile: Euphrase

Kezilahabi,M.Mulokozi,K. Kahigi,Ebrahim Hussein na S.A.Mohamed,Alamin

Mazrui na Kyalo, Jared Angira, Kithaka wa Mberia, W. Wamitila na Wallah bin

Wallah miongoni mwa wengine.

Kuzuka kwa mashairi huru katika historia ya ushairi wa Kiswahili kulitokana na

mabadiliko ya kisiasa, kiutawala, kiutamaduni, kiuchumi na kielimu

yaliyoshuhudiwa Afrika Mashariki katika miaka ya sitini. Jared Angira kwa

mfano, alijishughulisha na suala la mgongano wa tamaduni za zamani ambazo

'ziliharibiwa' na kuja kwa Wazungu na dini ya Kikristo naye Ebrahim Hussein

alijishughulisha na suala la mgongano wa tamduni jadi 'zilizoharibiwa' na kuja

kwa Waarabu na dini ya Kiislamu. Kutokana na mabadiliko haya, kulikuwa na

haja pia ya kubadilisha ushairi wa Kiswahili ili uende na wakati.

Kwa mujibu wa Delville (1998), mashairi huru yalianzishwa na Charles

Baudelaire katika kame ya kumi na tisa kule Ufaransa na aliyaita mashairi haya

Mashairi yasiyo na mizani. Baadaye,mtindo huu wa kutunga mashairi ulisambaa

katika mataifa mengine ya Ulaya. Wengi wa watunzi wa mashairi huru

walipoenda kusoma Ulaya, walisoma mashairi huru ya Ulaya na waliporejea

wakawa wameathiriwa na utunzi wa narnna hiyo na hivyo wao pia wakaanza

kutunga mashairi ya Kiswahili yasiyofuata arudhi. Mbali na kuwa mashairi haya

(41)

hayafuati kanuni za utunzi wa mashairi, huwa na sifa bainifu kama vile matumizi

ya takriri na mishata, mambo yanayoyatofautisha na tungo nyinginezo. Isitoshe,

mashairi haya hutumia jazanda, taswira na lugha ya mkato kama ilivyo katika

mashairi ya kimapokeo.

Utunzi wa mashairi hum ulisababisha mgogoro mkubwa kati ya watunzi wa

mashairi ya kimapokeo na watunzi wa mashairi hum. Kwa mfano, katika kutetea

mashairi ya kimapokeo,Shaaban Robert (1968), alisema kwamba:

Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache na muhtasari.

Akiunga mkono wazo hili,Mnyampala (1970) alieleza kuwa:

Ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale. Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongozi ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata yaliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalumu kuwa shairi.

Vilevile,Abdilatif Abdalla (1973) alishadidia mawazo haya kwa kusema kuwa:

Utungo ufaao kupewa jina 'ushairi' si utungo wowote tu bali ni utungo ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenziye; wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala zisizozidi; na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalumu na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni telezi kwa ulimi wa kuitamka, lugha ambayo ina uzito wa fikra, tamu kwa mdomo wa kusema, tumbuizi kwa masikio ya kuisikia na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ulivyokusudiwa.

Kwa mujibu wa Shaaban Robert, Mathias Mnyampala, Abdilatif Abdalla na

(42)

kimapokeo, utungo usiokuwa na man wa vma na mizam S10 ushairi, wazo linalopingwa vikali na watunzi wa ushairi wa sasa. Kwa mfano, Farouk Topan (1973), akiwapinga Wanamapokeo, katika utangulizi wa Kichomi, alisema kuwa:

Ukosefu wa vina na mizani umewafanya wataalamu fulani wa Kiswahili wayakaripie mashairi haya ... mimi sikubaliani nao kwani kitu kuitwa shairi si lazima kiwe na muundo huo huo tu ndipo kistahili kuitwa hivyo. Nionavyo mimi hadhi ya shairi haitegemei muundo au umbo fulani bali hutegemea yale yasemwayo na maneno ya shairi na vile yanavyosemwa.

Maneno ya Farouk Topan yana maana kwamba shairi si lazima liwe na muundo teule na kwamba hadhi ya ushairi haitegemei muundo au umbo fulani bali hutegemea maneno yasemwayo na maneno ya ushairi na vile yanavyosemwa. Mgogoro huu kati ya Wanamapokeo na Watunzi wa sasa wa mashairi ya Kiswahili umeathiri mtazamo wa walimu na wanafunzi kuhusu mashairi ya Kiswahili na hiki ndicho chanzo cha ufunzaji na ujifunzaji wa mashairi ya Kiswahili kuegemezwa kwenye mashari ya kimapokeo. Hali hii bila shaka ina mchango wake kwenye upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili.

2.3 Ufundishaji na Utahini wa Ushairi katika Shule za Upili

U shairi wa Kiswahili nchini Kenya umekuwa ukifunzwa katika shule za upili na kutahiniwa katika mitihani ya fasihi ya kitaifa kabla na hata baada ya mfumo wa elimu wa 8-4-4 kuanzishwa hadi sasa. Ufundishaji na utahini wake umetiliwa mkazo zaidi katika shule za upili ambapo ushairi wa Kiswahili hufunzwa kama somo la lazima na kama mojawapo wa utanzu wa fasihi na kutahiniwa katika

(43)

vile riwaya, tamthilia, hadithi fupi na fasihi simulizi. Katika shule zote za upili

nchini Kenya zinazofuata mfumo wa 8-4-4, mashairi yote ya Kiswahili, yaani

ushairi wa kimapokeo na ushairi huru, hufunzwa kuanzia kidato cha kwanza hadi

cha nne kutegemea shule, tajriba ya walimu na viwango vya upokezi vya

wanafunzi wa shule hizi.

Ufundishaji wa ushairi unamhitaji mwalimu mwenye tajriba na uzoefu wa

kufundisha mashairi. Zaidi ya hayo, unamhitaji mwalimu makini na mwenye

mwelekeo chanya kuyahusu mashairi hayo ili kuimarisha viwango vya upokezi

miongoni mwa wanafunzi. Mahitaji haya yanatokana na ukweli kuwa mashairi

hutumia lugha ya mkato tofautina tanzu nyinginezo za fasihi kamavile riwaya na

hadithi fupi ambazo hutumia lugha nathari. Kwa sababu hiyo, utafiti huu

uligundua kuwa walimu wengi wanaofunza somo la Kiswahili na fasihi ya

Kiswahili kwajumla katika shule za upili nchini Kenya na hasa katika jimbo la

Nakuru tulimofanyia utafiti huu wamehitimu kwa shahada ya kwanza katika

elimu huku wachache wakiwa na stashahada. Wachache wamehitimu kwa

shahada ya uzamili. Hata hivyo, wengi wao wana tajriba ya zaidi ya miaka kumi

katika ufunzaji wa somo la Kiswahili linalohusisha ushairi wa Kiswahili katika

fasihi.

Mbinu tofauti tofauti zimekuwa zikitumiwa kufunza mashairi ya Kiswahili katika

shule za upili nchini Kenya na hasa katika jimbo la Nakuru na hutofautiana

kutoka shule moja hadi nyingine kutegemea tajriba ya walimu, diwaniya mashairi

(44)

ya Kiswahili ni kama vile kusoma shairi darasani na wanafunzi kisha kujibu

maswali yaliyoulizwa. Wakati mwingi mashairi haya husomwa kwa sauti na

wanafunzi wote kwa mahadhi teule lakini wakati mwingine wanafunzi walio

mahiri katika kusoma huchaguliwa kuyasoma.

Vilevile, wanafunzi huyaimba mashairi hayo kwa mahadhi tofauti tofauti kabla ya

kuyajibu maswali waliyoulizwa wakielekezwa na walimu wao. Maswali

yanayoulizwa katika mashairi hayo hutumiwa kama msingi wa kuwafanya

wanafunzi wayaelewe mashairi hayo. Istilahi za mashairi ya Kiswahili kijumla

kama vile maana ya ushairi, ubeti, mishororo, vipande, vina na mizani hufunzwa

ili wanafunzi wawe na uzoefu wa kutumia istilahi hizi kila wanapojibu maswali

katika ushairi unaotahiniwa. Istilahi zinazohusiana na mishororo ni kama vile:

mwanzo, mloto, mleo, kiishio na mkarara. Vilevile, wanafunzwa hupewa maelezo

kuhusu dhana kama vile ukwapi, utao, mwandamizi na ukingo zinazohusiana na

vipande katika mishororo ya mashairi.

Isitoshe, wanafunzi huelekezwa kuhusu jinsi ya kuainisha mashairi ya Kiswahili

kutegemea vigezo mbalimbali kama vile: idadi ya mishororo katika kila ubeti,

idadi ya vipande katika kila mshororo, mpangilio wa vina, idadi ya mizani katika

mishororo na mpangilio wa maneno kati ya vigezo vingine vilevile. Aidha, istilahi

zinazohusiana na idhini ya kishairi kama vile tabdila, inkisari, mazida, utohozi,

kusongoa lugha na matumizi ya msamiati wa kale na lahaja hufunzwa. Wanafunzi

wa shule za upili pia huonyeshwa jinsi ya kuyachambua mashairi ya Kiswahili

kwa kuzingatia umbo la shairi, dhamira na maudhui.

(45)

Utafiti huu uliweza kubainisha kuwa ushairi wa Kiswahili hutahiniwa katika karatasi ya tatu ya 102/3 katika mitihani ya Kiswahili ya mwigo na ya kitaifa kote nchini Kenya katika shule za upili zinazofuata mfumo wa elimu wa 8-4-4. Karatasi hii hujumuisha maswali kutoka kwenye vitabu viteule vya riwaya, tamthilia na hadithi fupi. Vilevile, hujumuisha maswali kutoka kwenye utanzu wa fasihi simulizi na ushairi wa Kiswahili. Kila swali katika karatasi hii huwa na jumla ya alama ishirini na mtahiniwa huhitajika kujibu jumla ya maswali manne

pekee huku swali la kwanza likiwa lalazima.

Utafiti huu uligundua kuwa mambo ambayo yamekuwa yakitahiniwa katika ushairi wa Kiswahili ni kama vile watahiniwa kuhitajika kulipa shairi anwani mwafaka, kutambua na kueleza aina na bahari ya shairi lililotahiniwa pamoja na kueleza umbo la nje la shairi. Vilevile, watahiniwa hutarajiwa kufafanua dhamira na maudhui katika shairi husika, kubainisha jinsi idhini ya kishairi ilivyotumika, kuandika ubeti wa shairi katika lugha nathari, kufasiri jinsi msamiati teule ulivyotumika katika shairi na kulinganisha na kulinganua mashairi ya Kiswahili kimaudhui, kimuundo na kimtindo. Vipengele hivi vyote huchangia jumla ya alama ishirini katika swali la shairi.

(46)

huendeleza maadili ya kijamii na kitamaduni kwa kukashifu hulka hasi za

wanajamii. Kwa sababu hiyo, mwanafunzi hupata fursa ya kujifunza maadili.

Kielimu, mashairi ya Kiswahili hufunzwa katika shule za upili kama sehemu ya

fasihi ili yatahiniwe katika mtihani wa kitaifa wa Kiswahili katika karatasi ya tatu

ya 102/3 inayojumuisha riwaya, tamthilia, hadithi fupi, fasihi simulizi na ushairi.

Lengo kuu la kutahiniwa kwake ni kujaliza mahitaji ya kielimu ya kumwandaa na

kumkomaza mwanafunzi katika nyanja zote za fasihi ili aweze kuhitimu vyema

katika mtihani wa Kiswahili na hivyo kumwezesha kusomea taaluma mbalimbali

nchini Kenya.

2.4 Muhtasari

Sura hii, imeweza kufafanua dhana ya ushairi kwa mujibu wa wataalamu

mbalimbali. Vilevile, imeangazia chimbuko la ushairi wa Kiswahili pamoja na

kueleza kwa ufupi mgogoro uliopo kati ya Wanamapokeo na watunzi wa ushairi

wa sasa. Aidha, imetoa maelezo mafupi kuhusu ufunzaji, ujifunzaji na utahini wa

mashairi ya Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya kwa kurejelea jimbo la

Nakuru.

(47)

SURA YA TATU

UPOKEZI WA MASHAIRI YA KISWAHILI MIONGONI MWA

W ANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI

2.0 Utangulizi

Sura hii imeeleza maana ya upokezi pamoja na kutathmini viwango mbalimbali

vya upokezi wa mashairi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za

upili. Pia, imebainisha mambo yaliyoathiri upokezi wa mashairi hayo miongoni

mwa wanafunzi wa shule za upili zajimbo laNakuru.

3.1 Maana ya Upokezi

Upokezi ni rnkabala wa kifasihi unaojishughulisha na jinsi kazi za kifasihi

zinavyopokelewa na wasomaji wakati fulani au katika mpito wa wakati. Kwa

hivyo, mwanafunzi kama msomaji anatazamiwa kuipokea kazi ya fasihi kwa

kuzingatia mielekeo yake binafsi.

3.2 Viwango vya Upokezi

Viwango tofauti vya upokezi wa wanafunzi wa shule za upili kuhusu mashairi ya

Kiswahili katika jimbo la Nakuru viligunduliwa katika utafiti huu kwa kutumia

alama walizopata watafitiwa katika mijarabu ya mashairi waliyopewa. Kila

mjarabu wa shairi ulikuwa na jumla ya alama ishirini na watafitiwa walihitajika

kujibu maswali kutoka kwa mashairi manne waliyotahiniwa; mawili yalikuwa ya

(48)

3.2.1 Shairi la Kimapokeo la Kilahaja

Shairi A

Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Moyoni furaha sina, ningaitaka sinayo, Si usiku si mtana, ni mamoja kwangu hayo, Mateso nnayoona, yaujuwa wangu moyo, Simwako na wayowayo, uliyonifikiliya!

Nna jipu lintunza, linipalo tabu mno, Tangu liliponianza, kamwe sipati usono,

Kwamba ni mara ya kwanza, kuuguwa ndwezi hino, Latoma kama sindano, utunguwe nakwambia.

Sijana wala si juzi, liliponianza tangu, Ni mingi mno miezi, nnadhofu hali yangu, Nnakonda kama uzi, kwa kushitadi utungu, Kubwa tumaini langu, ni mwishowe nangojeya.

Hitaka keti siwezi, kwamba li makaliyoni, Kutwa huwa yangu kazi, kusimama; ntendeni? Na usiku usingizi, siupati aswilani,

Kutwa nakesha mwendani, kwa utungu kuzidiya.

Kili kipele mwilini, ndiyo mwanzo wake kuwa, Sikujuwa aswilani, kuwa jipu chaja kuwa, Ningekijuwa zamani, ningekitangiya dawa, Ni kwamba sikutambuwa, ndipo hakiwatiliya.

Siku ya kuiva kwake, hiyo ndiyo siku kweli, Huo ndiwo mwisho wake, na mwisho wa idhilali, Idhilali in'ondoke, mimi nayo tuwe mbali,

Siku hiyo ni mawili, kuteka au kuliya.

'Taliminya litumbuke, lisinisumbuwe tena, Usaha wote utoke, utoke nikiuona,

Midamu itirirke, kama ng'ombe alonona, Jipu hili mwana lana, Mn'gu mbwalipa hizaya.

Baada ya yote haya, jaraha niliuguze, Kwa madawa kutiliya, ili kwamba yalipoze, Irudi yangu afiya, na zaidi niongeze,

Nirukeruke niteze, kwa furaha kuningiya.

(49)

Maswali

(a) Andika ubeti wa pili katika lugha nathari. (alama 4)

(b) Katika ubeti wa 5 mshairi anajuta. Eleza. (alama 3)

(c) Tambua matumizi yoyote sita ya maneno ya kilahaja katika shairi hili

kisha uyaandike katika Kiswahili sanifu. (alama 6)

(d) Mbali na matumizi ya lahaja, fafanua matumizi mengine ya idhini ya

mshairi katika shairi hili. (alama 4)

(e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi.

(alama 3)

(i) Wayowayo

(ii) Kushitadi

(iii) Idhilali

Katika shairi hili, viwango vitatu vya upokezi vya wanafunzi wa kidato cha tatu

na cha nne waliotafitiwa vimebainishwa katika majedwali A na B kutegemea

alama walizopata watafitiwa katika shairi hili. Viwango hivi vya upokezi ni

kiwango cha chini, kiwango cha kati na kiwango cha juu.

Jedwali A

Shairi la Kimapokeo la Kilahaja, Kidato cha Tatu

Kiwango cha Chini Kiwango cha Kati Kiwango cha Juu

(Alama 1-5) (Alama 6-14) (Alama 15-20)

Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi Asilimia

MoiKabarak .)..., 15% 14 70% 3 15%

Mary Mount 2 10% 17 85% 1 05%

Rongai 3 15% 15 75% 2 10%

A.I.C. Morop 1 05% 19 95% 0

(50)

Jedwali B

Shairi la Kimapokeo la Kilahaja, Kidato cha Nne

Kiwango cha Chini Kiwango cha Kati Kiwango cha Juu (Alama 1-5) (Alama 6-14) (Alama 15-20) Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi Asilimia

Moi Kabarak 1 05% 14 70% 5 25%

Mary Mount 1 05% 14 70% 5 25%

Rongai 3 15% 13 65% 4 20%

A.I.e. Moron 4 20% 15 75% 1 05%

JUMLA 9 11.25% 56 70% 15 18.75%

Kulingana na data ambayo imeonyeshwa katika Jedwali A na B, ni bayana kuwa jumla ya watafitiwa tisa kati ya watafitiwa themanini wa kidato cha tatu sawia na wanafunzi tisa kati ya wanafunzi themanini wa kidato cha nne walioshiriki katika utafiti huu walikuwa wa kiwango cha chini cha upokezi katika shairi hilo. Hii ni asilimia kumi na moja nukta mbili tano (11.25%) ya wanafunzi wote wa kidato cha tatu sawa na wanafunzi wa kidato cha nne walioshirikishwa katika utafiti huu waliodhihirisha kiwango cha chini cha upokezi katika shairi hilo.

Kiwango cha kati kimejumuisha watafitiwa waliopata kati ya alama sita na kumi na nne juu ya ishirini katika shairi hili. Kwa kurejelea Jedwali A, jumla ya wanafunzi sitini tano wa kidato cha tatu kati ya wanafunzi ,themanini ambao ni asilimia themanini na moja nukta mbili tano (81.25%) na wanafunzi hamsini na

sita waliochangia asilimia sabini (70%) ya wanafunzi wa kidato cha nne

waliotafitiwa kwa mujibu wa jedwali B, walidhihirisha kiwango hiki cha upokezi katika shairi A.

(51)

Hata hivyo, asilimia saba nukta tano (7.5%) anibao ni wanafunzi sita tu kati ya

wanafunzi themanini wa kidato cha tatu ikilinganishwa na asilimia kumi na nane

nukta saba tano (18.75%) ambayo ni wanafunzi kumi na watano kati ya

watafitiwa wote wa kidato cha nne walikuwa wa kiwango cha juu cha upokezi.

Kiwango hiki cha upokezi kimejumuisha watafitiwa waliomudu kupata alama

kumi na tano au zaidi juu ya alama ishirini katika shairi hilo.

3.2.2 Shairi la Kimapokeo la Kiswahili Sanifu

Shairi B

Soma shairi hili kisha ujibu maswali

Kukipenda kitu chako, huo ndio uzalendo Mtu anapenda chake, japo hakina thamani Hatamani cha mwenzake, na kukitia rohoni Chake ni furaha yake, kingakuwa kitu duni.

Kuipenda nchi yako, huo ndio uzalendo Kuwa tayari daima, taifa kutumikia Uzukapo uhasama, haraka kupigania Adui kuwasakama, mbali kuwatupilia.

Kuwapenda watu wako, huo ndio uzalendo Uzalendo ndio ngao, ni silaha kamilifu Tuwe nao moyo huo, tusiwe nyoyo dhaifu Wale wakilinda kwao, nasi tuwe timilifu.

Kuipenda kazi yako, huo ndio uzalendo Kazi tusitegee, ni uhai na afia

Mzalendo jitolee, hasa shamba kulimia Fanya kazi harambee, kwa uchumi kuinua.

(52)

Kupenda taifa lako, huo ndio uzalendo

Uzalendo ni upole, mapenzi kwa nchi yako Si ubishi wa kelele, vituko na maudhiko Nchi haisongi mbele, uzalendo sipoweko.

Maswali

(a) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4) (b) Shairi hili lina umuhimu gani kwa taifa la Kenya. (alama 4)

(c) Eleza sifa za kiarudhi zilivyotumiwa katika ubeti wa sita. (alama 4)

(d) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi.

(alama 3)

(i) Thamani

(ii) Uhasama

(iii) kuwasakama

(e) (i) Tambua tamathali ya usemi iliyotumika katika mshororo: "Uzalendo ndio ngao, ni silaha kamilifu"

(ii) Eleza sababu ya jibu lako kwa swali la (i).

(alama 1) (alama 1) (f) Tambua uhuru wowote wa ushairi katika shairi hili na uutolee mifano

miwili. (alama 2)

(alama 1)

(g) Andika methali moja inayooana na shairi hili.

Jedwali C

Shairi la Kimapokeo la Kiswahili Sanifu, Kidato cha Tatu

Kiwango cha Chini Kiwango cha Kati Kiwango cha Juu

(Alama 1-5) (Alama 6-14) (Alama 15-20)

Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi Asilimia

MoiKabarak 1 05% 17 85% 2 10%

Mary Mount 3 15% 16 80% 1 05%

Rongai 1 05% 18 90% 1 05%

A.I.C. Morop 3 15% 17 85% 0

-JUMLA 8 10% 68 85% 4 05%

(53)

Jedwali D

Shairi la Kimapokeo la Kiswahili Sanifu, Kidato cha Nne

Kiwango cha Chini Kiwango cha Kati Kiwango cha Juu

(Alama 1-5) (Alama 6-14) (Alama 15-20)

Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi Asilimia

Moi Kabarak 0 0 16 80% 4 20%

MaryMount 0 0 17 85% 3 15%

Rongai 0 0 17 85% 3 15%

A.I.C. Morop 7 35% 13 65% 0

-JUMLA 7 8.75% 63 78.75% 10 12.5%

Viwango vya upokezi katika shairi B vya watafitiwa wa kidato cha tatu na cha

nne vimeonyeshwa katika jedwali

e

na D. Shairi hili la kimapokeo tofauti na shairi A, limetumia Kiswahili sanifu.

Miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha tatu kama ilivyoonyeshwa katika jedwali

C, jumla ya watafitiwa wanane kati ya watafitiwa themanini walipata kati ya

alama moja na alama tano juu ya ishirini katika shairi B. Idadi hii ni asilimia kumi

(10%) ya watafitiwa wa kiwango cha chini cha upokezi katika shairi hilo. Kwa

upande mwingine, asilimia nane nukta saba tano (8.75%) ya watafitiwa wa kidato

cha nne walikuwa katika kiwango hiki cha upokezi. Huku kulitokana na

wanafunzi saba kati ya wanafunzi themanini wa kidato cha nne na ambao wote

walikuwa wa Shule ya Upili ya A.Le. Morop. Haya yameonyeshwa katika

jedwali D.

(54)

walipata kati ya alama sita na kumi na nne katika shairi hilo. Hii ni asilimia

themanini na tano (85%) ya wanafunzi wote wa kidato cha tatu waliotafitiwa.

Kwa upande mwingine, asilimia sabini na nane nukta saba tano (78.75%) ya

wanafunzi wa kidato cha nne waliojibu maswali ya shairi B walimudu kupata

alama zizo hizo. Hii ilikuwa jumla ya watafitiwa sitini na tatu kati ya themanini

wa kidato cha nne.

Hatimaye, jumla ya wanafunzi wanne ambao ni asilimia tano (5%) ya wanafunzi

themanini wa kidato cha tatu walimudu kudhihirisha kiwango cha juu cha upokezi

katika shairi hilo kama ilivyoonyeshwa katika jedwali C. Hii ni idadi ndogo

ikilinganishwa na jumla ya watafitiwa kumi wa kidato cha nne waliochangia

asilimia kumi na mbili nukta tano (12.5%) ya watafitiwa wote wa kidato hicho.

Rejeleajedwali D.

3.2.3 Sbairi Huru la Kilabaja

Shairi C

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:

KIBARUW A: Abdilatif Abdalla

Kwenye shamba hili kubwa asilani hakunyi mvuwa Ni kwa mitilizi yajasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa

Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa Ndipo mte ukatipuza!

(55)

Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa

Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa

Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa

Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao

Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao

Uulize na upepo rnkali kwa ghadhabu

uvumao-Viulize: Ni nani arukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?

Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?

Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?

Halafuye hana faida moja apatayo wala malipo yanayotosheleza

-Isipokuwa kusudungwa na kutupiliwa matambara na vyakula vilivyooza?

Viulize: Ni nani huyo ni nani?

Viulize: Ni nani ayalimaye mashamba na kuyapaliliya?

Na rnimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinarniya?

Hatimaye nani atajirikaye mali yakarnmiminikiya

Akaota na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya

Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?

Viulize: ni nani huyo ni nani!

Na hac ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao

Nayo hiyo mito kwa furaha maji itiririkao

Na huo upepo rnkali wenye ghadhabu uvumao .

Vyote hivyo vitatu vitakujibu kwa umoja wao:

"Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!"

Maswali

(a) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari.

(b) Eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi.

(alama 4)

(56)

(c) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu

vibarua. (alama 3)

(alama 2)

(d) Eleza dhamira ya shairi hili.

(e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi.

(alama 3)

(i) ~itilizi

(ii) Kusundugwa

(iii) Nyanana

(f) Tambua tamathali za usemi zilizotumika katika ubeti wa tano. (alama 4)

Jedwali E

Shairi Huru la Kilahaja, Kidato cha Tatu

Kiwango cha Chini Kiwango cha Kati Kiwango cha Juu

(Alama 1-5) (Alama 6-14) (Alama 15-20)

Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi .Asilimia

MoiKabarak 8 40% 12 60%

-

-Marv Mount 9 45% 11 55%

-

-Rongai 5 25% 15 75% -

-A.I.e. Moron 8 40% 12 60% -

-JUMLA 30 37.5% 50 62.25%

Jedwali F

Shairi Huru la Kilahaja, Kidato cha Nne

Kiwango cha Chini Kiwango cha Kati Kiwango cha Juu

(Alama 1-5) (Alama 6-14) (Alama 15-20)

Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi Asilimia

MoiKabarak 2 10% 17 85% 1 05%

Mary Mount 5 25% 15 75% -

-Rongai 4 20% 15 75% 1 05%

A.I.e. Morop 6 30% 14 70%

-

-JUMLA 17 21.25% 61 76.25% 2 2.5%

Figure

Updating...

References

Updating...

Download now (107 pages)