• No results found

Umilisi na utendaji: tathmini ya changamoto na uimarikaji wa kiswahili katika baadhi ya shule za upili, Eneo la Nyanza

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Umilisi na utendaji: tathmini ya changamoto na uimarikaji wa kiswahili katika baadhi ya shule za upili, Eneo la Nyanza"

Copied!
132
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

UMILISI NA UTENDAJI: TATHMINI YA CHANGAMOTO NA UIMARlKAJI 'NA KISWAHILI KATlKA BAADHI YA SHULE ZA UPILI, ENEO LA NYANZA.

TASNIFU YA

KOKO AS CA MONICA

TAS. IFU RH IMETOLEWA 10VA MADHUMUNI YA KUTOSHELEZA

BA.-\.DHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZA~IILI K-\TIKL\ CHUO KIKUl: eHA KENYATTA.

(2)

UNGAMO

TASNIFU HIl NI KAZI YANGU MWE YE"VE 1 A HAIJATOLEWA K"VA MAHITAJI YA SHAHADA KATlKA CHUO KINGINE.

Sahihi ---~---- T areh e---

.£2'1

Lt

.---

I

a» {

£,

Koko Asca Monica

C50/CE/22433/20 11

TASNIFU HIl IMETOLEWA I(WA IDHINI YETU KAMA "VASIMAMIZI

"VALIOTEULIWA NA CHUO KIKUU CHA KENYATTA.

~~

_

o~

Sahihi~~--- Tarehe

o?:>

,

_

lo~/rw/b

I-~

l-~

_

Daktari Jacktone Okello Onyango

IDARA YA KIS"VAHILI ~A LUGHA ZA KIAFRlKA

CHUO KIK1T CHA KE~YATTA

Sahihi --~--- T

are

h

e

--

.

0

.

2:

:.

j

-

QJ;

:_

/_of

I

JJ,

,

__-Mwalimu Evelyne S. Mudhune

IDARA YA KIS"VAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKi\

(3)

SHUKRA I

Ningependa kumshukuru Mungu kwa nguvu na uhai na kwa kuniwezesha kukamilisha

utafiti huu. Vile vile ningependa kuwashukuru wasimamizi wangu Daktari Jacktone

Onyango na Mwalimu Everlyne Mudhune kwa maelekezo merna, mashauri na usimamizi mzuri uliofanikisha kazi hii kukamilika.

Ninawashukuru wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika kama

Profesa Kitula King'ei, Daktari Pamela Ngugi pamoja na Mkuu wa Idara Daktari Richard Wafula. inawashukuru Daktari Alice Mwihaki na Daktari Leonard Chacha Mwita kwa

ushauri mwema na maelekezo.

(4)

T.\B .\Rl'KL'

Kazi hii ninaitabaruku kwa wanangu:

Felix Ochieng'

Winnie Achieng

Denick Jude

Eugine J avan

(5)

\BSTRACT

(6)

ABSTRACT

(7)

IKISIRI

Utafiti huu ulinuia kuchunguza umilisi na utendaji wa wanafunzi katika .lugha ya Kiswahili katika baadhi ya shule za upili mkoani yanza (Eneo la Ziwa) na kuchanganua sababu za kuimarika kwa matokeo katikamitihani ya Kiswahili ya kitaifa ya KCSE kwa miaka minn~ iliyopita (2009-2012). Utafiti huu unatokana na sa~abu kwamba shule za Eneo la Ziwa zimekuwa zikifanya vibaya katika mitihani ya Kiswahili

katika kiwango cha kitaifa yaani KCSE. Hata hivyo shule ya Wavulana ya Maranda na shule ya Wasichana ya Kisumu, zilionyesha matokeo mazuri katika miaka miwili mtawalia (2010 na 2011). Utafiti uliangazia iwapo matokeo haya yalijitokeza kighafla

ama yaliimarika kihatua. Utafiti huu ulizingatia matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne katika mtihani wa KCSE kwa miaka minne iliyopita 2009-2012. Uteuzi wa sampuli kimakusudi ulitumiwa kuteua shule nne katika magatuzi manne ambayo ni; Kaunti ya Migori, Homabay, Kisumu na Siaya. Shule hizo zilijumuisha shule za kitaifa na za

magatuzi, shule za wavulana pekee na wasichana pekee. Utafiti ulilenga; kubainisha viwango vya umilisi na utendaji wa wanafunzi wa shule za upili, kueleza changamoto zinazokumba ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili katika Eneo la Ziwa na kuchunguza sababu za kuimarika kwa utendaji wa Kiswahili katika eneo hilo. Nadharia ya Sarufi Zalishi na nadharia ya Kijurnuia na Kibinadarnu zilirumiwa. Data za utafiti zilikusanywa nyanjani na maktabani. Data zilikusanywa kwa kujaza hojaji, mahojiano na kukusanya matokeo ya shule husika. vlbinu ya utafiti ya kimaelezo ilitumiwa kuchanganua sababu za kuimarika kwa matokeo ilhali mbinu ya kitakwimu ilitumiwa kuchanganua matokeo. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kuainisha mada tofauti

(8)

YALIYOMO

ungalTIO 11

Shukrani iii

Tabaruku ., iv .

Abstract. v

Ikisiri vi

Yaliyomo vii

Ufafanuzi wa dhana xi

Orodha ya vifupisho xii

Orodha ya vielelezo na majedwali xiv

Viambatisho xvi

Sura ya kwanza: Utangulizi. 1

1.0 Utangulizi 1

1.1 Usuli wa mada 1

1.2 Suala la Utafiti 6

1.3 Maswali ya utafiti : 8

1.4 Malengo ya utafiti 8

1.5 Sababu za kuchagua mada ya utatiti 8

(9)

1.7 Yaliyoandikwa kuhusu mada 12

1.8 Misingi ya nadharia 18

1.9 Mbinu za utafiti 22

1.9.1Mahali pa utafiti 23

1.9.2 Uteuzi wa Sampuli 24

1.9.3 Ukusanyaji wa data 25

1.9.4 Uchanganuzi wa data 25

1.9.5 Uwasilishaji wa data 26

1.9.6 Hitimisho 26

Sura ya pili: Viwango vya umilisi na utendaji.. 27

2.0 Utangulizi 27

2.1 Viwango vya umilisi 27

2.1.1 Umilisi wajuu 28

2.1.2 Umilisi kiasi 33

2.1.3 Umilisi hafifu 34

2.2 Viwango vya utendaji 35

2.2.1 Utendaji wajuu 36

2.2.2 Utendaji kiasi 39

(10)

Sura ya tatu : Changamoto katika ujifunzaji wa Kiswahili.. .43

3.0 Utangulizi 43

3.1 Uongozi wa shule 43

3.2 Sera za shule 44

3.3 Mielekeo ya wanafunzi 45

3.4 Upungufu wa vifaa vya masomo 46

3.5 Athari za lugha ya kwanza .47

3.6 Idadi ya vitabu 48

3.7 Uhaba wa tafiti na rnachapisho .49

3.8 Walimu , 50

3.9 Athari za sheng' : 53

3.10 Makosa yanayofanywa na baadhi ya wanafunzi 55

3.11 Hitimisho 58

Sura ya nne: Sababu za kuimarika kwa matokeo ya Kiswahili .59

..to

Utangulizi 59

4.1 Uongozi wa shule 61

4.2 Sera ya lugha yaKiswahili shuleni 61

4.3 Shughuli za idara ya Kiswahili 64

(11)

~.5 Uimarishaji wa vifaa vya masomo 74

4.6 Athari za lugha ya kwanza 76

4.7 Vitabu vingi na bora : 77

4.8 Ongezeko latafiti na machapisho 79

4.9 Walirnu waliohitimu 79

4.10 Kukabiliana na sheng' 82

4.11 Mbinu! mikakati mipya 85

4.12 Vipindi vya ziada : 89

4.13 Hitimisho 90

Sura ya tano :Muhtasari, Matokeo na Mapendekezo 91

5.0 Utangulizi 91

5.1 Muhtasari 91

5.2 Matokeo ya utafiti 94

5.3 Mapendekezo 96

504 Mapendekezo ya tafiti nyingine 97

Marejeleo 99

(12)

UFAFANUZI WA DHANA

Baaclhi ya istilahi ambazo zilitumiwa ni kama;

Chamcha/chajio/ Kiamsha kinyw

a-Mitihani mifupi kuhusu mada moja inayofanywa kwa muda

mfupi kila siku wakati wa jioni, asubuhi ama mchana.

Gatuzi - Eneo la utawala lenye kufuata mfumo wa uhawilishaji wa madaraka na ugavi wa matumizi ya rasilimali kutoka serikali

kuu kwenda kwa serikali ndogo, lenye kuongozwa na gavana ;

Pia huitwa kaunti aujimbo.

Kategoria za maneno- Aina tofauti za maneno kulingana na sifa za kisarufi. utaratibu wa kugawa maneno katika makundi mbalimbali

kulingana na kazi zinazofanywa na maneno hayo katika lugha

na sifa zao.

Mkoa wa Nyanza- Kwa sasa ni Eneo la Ziwa

Sintaksia- Ni tawi la isimu arnbalo huchunguza kanuni na namna maneno yanavyopangwa karika rnaandishi au rnazungumzo ili kuleta miundo na mifumo mizuri va maneno kama vile virai, vishazi

na sentensi.

Vmilisi- I i mfumo wa kiasili unaomwezesha mtumiaji wa lugha

kuzalisha na kuelewa idadi isiyo kikomo ya sentensi za lugha.

Utendaji- Ni utumiaji wa ule uwezo wa kiisimu katika muktadha halisi.

(13)

AGORO-

BORDETA-

CHAKIBO-

CHAKINYA-

CHAKIRACPE

-

FDSE-

HAW

K-

KCE-KCPE

-KC

SE-

KG-KIE/

KICD-

KK-

KLB-

~EC-ORODHA YA VIFUPISHO

Agoro Sare High School

Bondo Rarieda District English Teachers Association

Chama cha Kiswahili cha Bondo

Chama cha Kiswahili cha N yanza

Chama cha Kiswahili cha Rarieda

Certificate ofPrimary Education

Free Day Secondary Education

Jina la mtihani wa muungano wa shule zifuatazo; Homabay, Agoro

Sare, Kaplong', Ramba, Litein na Siongoroi.

Konsonanti

Kenya Certificate of Education

Kenya Certificate of Primary Education( cheti cha darasa la 8)

.enya Certificate ofSecondary Education Icheti cha kidato 4)

Kisumu Girls National School

Kenya Institute of Curriculum Development

Nadharia ya Kijumuiya na Kibinadamu

Kenya Literature Bureu

(14)

KSSHALl

L2

-

MAR-

NK-RA

P-gw,

SZ

-

$Taz

TSC

-

v-

x-

y-

z-Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Upili. Kenya.

Lugha yakwanzal mama

Lugha yapili! Kiswahili

Maranda National School

Na kadhalika

St. Joseph' s Rapogi High School

Swali

Nadharia ya Sarufi Zalishi

Mpaka wa silabi

Tazama .

Teachers Service Commission

Vokali

Watahiniwa waliokosa kufanya mitihani

Wale ambao hawakumaliza mitihani yote

(15)

ORODHA YA VIELELEZO NAMAJED\;VALI

Ukurasa

(1.1)Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (KCSE), Bondo 2006--- 4

(1.2)Kielelezo eha shule hamsini bora nehini Kenya, 2007, Kiswahili--- 3

(1.3) Matokeo ya mitihani yaKiswahili KCSE 2009 - 2012--- 5

(lA) Kielelezo eha viwango vya umilisi na utendaji katika SZ--- 21

(2.1) Matokeo ya wanafunzi waliojaza hojaj i--- 28

(2.2) Jedwali: Lo! Uwanja wa kuehezea kandanda umelowa maji--- 30

(2.3)Kielelezo eha kurekebisha sentensi---. 31

(2A) Kielelezo katika Jedwali: kuandika kwa umoja--- 31

(2.5) Alama za wanafunzi katika viwango vya umilisi--- 33

(2.6) Kiel elezo eha matokeo ya utendaj i--- 36

(2.7) Kielelezo katika Jedwali: viwango vya utendaji--- 36

t2.~i Kielelezo eha kugeuza sentensi katika kauii ya kutendewa--- 37

(2.9) Kielelezo eha matokeo ya viwango vya umiiisi na utendaji--- 41

(2.10) Kielelezo ehajedwali eha matokeo ya viwango vya umilisi nautendaji--- 41

(3.1)Kielelezo eha uongozi--- 43

(3.2)Kielelezo eha idadi yavitabu---

48

(16)

(3.4)Kielelezo cha makosa yawanafunzi------------------------------ 58

(4.1)J edwali la matokeo ya KCSE 2009- 2012---------------------- 59

(4.2)Matokeo ya mitihani ya Kiswahili KCS E2009 - 2012---------------- 60

(4.3)Kielelezo cha idadi ya walimu----------------------------- 80

(17)

VIAMBATISHO

A. Idhini ya Utafiti kutoka Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya Kitaifa--- 105 B. Idhini ya Utafiti kutoka Wizara ya Elimu, Gatuzi laKisumu--- 106 C. Hojaji--- I07 D. Tuzo Gaz, eti laTaifa Leo---

.

--- 110 E. Tuzo, Gazeti laTaifa Leo--- 111 F. Kongamano la walimu wa Kiswahili nchini, Alliance--- 112

G. Orodha ya shule 50bora ,KCSE, 2012--- 113 H. Ramani ya Kenya--- 114 I. Ramani ya Eneo la Zi wa--- 115

(18)

SURA YA KWANZA:

VTANGULIZI

1.0 Utangulizi

Sura hii inaeleza usuli wa mada, suala la utafiti, maswali yaliyoongoza utafiti, malengo ya

utafiti, sababu za kufanya utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada,

nadharia pamoja na mbinu za utafiti.

1.1Usuli wa Mada

Kwa muda mrefu, eneo la Nyanza lilihusishwa na matokeo duni katika somo la Kiswahili.

Hali kadhalika ilidaiwa kuwa watu kutoka Nyanza hasa wanaozungumza Dholuo kama Ll

wana matatizo katika umilisi wa lugha ya Kiswahili. Wanyoike (1978:36) na Mbaabu

(1985), wanaeleza kuwa Dholuo ni lugha ya Kinailoti, na kwamba mara nyingi, wanafunzi

wa Kinailoti hasa Dholuo hupata matatizo katika ujifunzaji wa Kiswahili ambayo ni lugha

ya Kibantu. Ritchie (1978), anaeleza kuwa kila lugha huwa na upekee wa mfumo wa

mawasiliano. Upekee huu husababisha tofauti kubwa baina ya lugha tofauti. Tofauti hizi

husababisha ugurnu wa kujifunza lugha ya pili (L2). Baadhi ya matatizo ambayo wanafunzi

hupata katika ujifunzaji wa lugha ya pili hujitokeza katika viwango tofauti tofauti vya

kiisimu King'ei na Musau (2002), Mudhune (1994), 01al (2008) na wengineo. Wanyoike

(1978), Musau (1993) na Mbaabu (1985), wanaeleza kuwa baadhi ya wazawa wa lugha

nyingine karna ya Kinailoti huwa na matatizo katika ujifunzaji wa Kiswahili kwa sababu ya

athari za lugha ya kwanza.

Nchini Kenya, mitihani ya kitaifa husimarniwa na Baraza la Mitihani la Kenya (K EC).

Mitihani hutumiwa kupima kiwango cha ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi. Kwa sababu

hiyo utafiti huu uliangalia matokeo ya Kiswahili katika eneo la Ziwa kwa miaka minne

(19)

hiki ambapo kwa mara ya kwanza eneo la Ziwa liliongoza katika mtihani wa

Kiswahili.Matokeo hayo pia yalionekana kuimarika kwa kipindi kirefu.(Taz. kielelezo-l.l ).

Ubora wa matokeo hayo haukuwa wa kisadfa tu. Mikakati mingi na harakati mbalimbali

zilihusishwa. Kwa mfano, katika mwaka wa 2006, kamati ya kuchunguza chanzo na athari

za matokeo duni na kupendekeza masuluhisho iliundwa . Kiswahili kilikuwa mojawapo ya

masomo ya kuchunguzwa. Mojawapo ya mapendekezo ya kamati hiyo kuhusu somo la

Kiswahili yalikuwa ni kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili kwa kuandaa

warsha za kupiga msasa kwa walimu wa Kiswahili. Pili, ilisisitizwa kuwa Chama cha

Walimu Wakuu wa Shule za Upili (KSSHA) kiwe na mpangilio na shughuli za kulenga

kubadilisha mielekeo ya wanafunzi kuhusu Kiswahili, kuboresha utendaji wa Kiswahili na

vile vile kuboresha uwezo wa walimu wa Kiswahili.

Watafiti wengi wamezungumzia mbinu tofauti za kuimarisha ujifunzaji wa Kiswahili kama

vile Njogu (2005), Ndalu (1997), Gesaga (1986), Gichura (1999), Eshiwani (1988) na

Fraser (1959). Njogu (2005), akichangia mjadala kuhusu matokeo duni ya Kiswahili kama

lugha ya taifa katika gazeti la Daily Nation, alielezea kuwa umilisi katika Kiswahili si

kuvumbua misamiati ya kikale na maneno magumu bali ni kufuata sheria na uteuzi

mwafaka wa msamiati. Alijadili baadhi ya matatizo yanayosababisha kutoimarika kwa

matokeo ya Kiswahili kuwa; ufahamu mdogo wa umilisi wa kiisimu, kuzuka kwa kilugha

cha 'sheng', kuwa na mielekeo hasi, ukosefu wa motisha wa kujua lugha vizuri katika

kiwango cha kitaifa na akasisitiza ufunzaji wa Kiswahili nchini. Kulingana na tarakimu za

Education Watch Juzuu 24, 2008, matokeo ya somo la Kiswahili yalikuwa chini m110.Kwa

mfano, katika kielelezo cha gatuzi dogo la Bondo, matokeo ya Kiswahili katika mwaka wa

2006 yalikuwa kama yafuatayo: Taz jedwali la

Cl.

1).

Katika Mkoa wa Nyanza kulikuwa na shule tatu pekee miongoni mwa shule hamsini

(20)

KCSE. Miongoni mwa shule takriban 5,000, shule ya Rapogi ndiyo iliyokuwa katika

orodha hiyo kutoka eneo la Luo Nyanza. Taz jedwali la (l.2).

(1.2) Kielelezo cha Shule Hamsini Bora Nchini Kenya (2007), Kiswahili

Nambari 39 46 48

kitaifa

Shule Kisii High St.Joseph Rapogi Nyambaria

Wastani 9.2413 9.1096 9.0751

Baadaye pakatokea mabadiliko arnbapo, katika mwaka wa 2010 Maranda ilipata wastani

wa 11.3512 na kuibuka washindi katika mtihani wa Kiswahili. Pia ilikuwa nambari ya nne

kitaifa kwa alama wastani ya 10.5578. Shule ya Wasichana ya Kisumu ilinyakua taji hilo

kutoka kwa Maranda na kuwa washindi katika matokeo ya Kiswahili kwa alama 11.185 na

kwa jumla kuwa nambari sitini na sita miongoni mwa shule takriban 5,000 wastani wa

(21)

(1.1) Matokeo ya Mtihani wa Kiswahili (KCSE), Bondo 2006

Jinsia Alama A A-

B

+

B

B-

C

+

C

C

-

D

+

D D- E X WASTANI

Usajili

Wavulana

1

2

7

0

3

6

6

8

11

0

1

24

1

04

1

75

l

39

11

8

1

00

2

11

7

9

5

1

6

.

3567

Asilimia (%) 2.8 5.4 8.7 9.8 8.2 13.8 10.9 9.3 7.9 16.6 6.2 0.4 0.08 53%

Wasichana

7

1

7

6

1

7

53

6

8

6

2

1

3

5

9

7

7

5

5

6

117

29

2

0

6

.

1

8

4

Asilimia (%) 0.8 2.4 7.4 9.5 8.6 18.8 13.5 10.5 7.8 16.3 4 0.3

-

51.5%

2006

6.2976

(22)

Na.

MWAKA SHULE USAJILI WASTANI KlTAIFA

2009 KG 234 8.252

MAR 219 9.0868

RAP 171 9.257

AGORO 251 5.1315 2010

KG 241 8.407

MAR 261 11.3512 1

RAP 186 9.1989

AGORO 307 6

.

2011

KG 233 11.185 1

MAR 261 11.0536

RAP 194 10.3927

AGORO 193 9.3367

2012

KG 234 10.047 8

MAR 283 9.8481 16

RAP 207 9.2899

AGORO 217 9.235

(1.3)Matokeo ya Mitihani ya Kiswahili KCSE (2009 - 2012)

Katika matokeo ya mitihani ya 2012, shule kumi na mbi1i za yanza, zikiwemo tisa za Luo Nyanza zilikuwa miongoni mwa shule 50 bora nchini Kenya. Shule ya Wasichana ya

Kisumu ilikuwa nambari 8 na Maranda 16.( Tazama kiambatisho G). Utafiti huu ulinuia kubaini sababu za kuimarika kwa matokeo hayo.

Kulingana na Chomsky (1965), umilisi ni mfumo wa kanuni unaowawezesha watumiaji wa lugha kuzalisha na kuelewa sentensi zisizokuwa na kikomo. Mtazamo wa kiasili wa ujifunzaji lugha unasema kuwa binadamu ana uwezo wa kiasili wa kuelewa sarufi za

Jugha tofauti tofauti (Radford, 1997). Kwa upande mwingine alieleza utendaji ni mfumo wa namna lugha inavyotumiwa katika mawasiliano. Somo la Kiswahili ni la lazima kwa

(23)

na KCSE nchini Kenya. Kiswahili ni mojawapo ya masomo muhimu katika kuhitimu

alama za kuingia katika chuo kikuu. Waluo pia hutumia na kuzungumza Kiswahili kwa

vile ni lugha ya taifa. Kiswahili ni lugha rasmi kulingana na Katiba ya Kenya (2010).

Kwa mud a mrefu shule za Nyanza zimehusishwa na Kiswahili kibovu. Shule ya Maranda

ilipoibuka mshindi katika mtihani huu lilikuwa ni jambo la kushangaza. Mwaka wa 2010

na 2011, tulishuhudia washindi wa lugha ya Kiswahili kuwa shule za en eo la Ziwa

ambazo ni Shule ya Upili ya Maranda na ya Wasichana ya Kisumu mtawalia.

Utafiti huu ulichunguza viwango mbalimbali vya umilisi na utendaji katika lugha ya

Kiswahili katika baadhi ya shule za upili eneo la Nyanza. Changamoto zilizokuwa katika

somo hilo la Kiswahili ambazo sasa zimerekebishwa zilichunguzwa na sababu za

kuimarika kwa matokeo hayo katika Kiswahili. Kulingana na Chomsky kiungo

muhimu zaidi katika umilisi wa kiisimu ni kile cha sintaksia. Kwa hivyo; utafiti

ulizingatia kiwango cha sintaksia. Mtihani wa Kiswahili unajumuisha karatasi tatu

ambazo ni insha, lugha na fasihi. Utafiti huu ulizingatia karatasi ya lugha.

1.2 Suala la Utafiti.

Utafiti ulidhamiria kutuelekeza kuthibitisha iwapo wanafunzi wa eneo la Ziwa

wanaweza kuwa na umilisi na utendaji wa Kiswahili wa kuwawezesha kupita mtihani.

Shule za Nyanza zimehusishwa na Kiswahili kibovu kwa muda mrefu. Inaaminika kuwa

si jambo rahisi kwa wanafunzi wa Kiluo kuwa na umilisi wa Kiswahili. Sababu

zilizotolewa ni madai ya Wanyoike (1978), na Mbaabu (1985), kuwa baadhi ya wazawa

wa lugha ya Dholuo huwa na matatizo katika ujifunzaji wa Kiswahili kwa sababu ya

athari za L1.

Chomsky (1965), anafafanua dhana ya umilisi na utendaji katika nadharia yake ya SZ

ambapo anadai kuwa umilisi ni mfumo wa kiasili unaomwezesha mtumiaji wa lugha

(24)

kwamba katika ujifunzaji wa lugha mwanafunzi anahitaji kuwa na ujuzi wa sheria na

ufahamu wa L2. Anaeleza kujua viambajengo vya sarufi hufuata hatua zinazotabirika,

vingine hupatikana mapema na vingine baadaye bila kujali L1 ya mzungumzaji.

Kulingana na Mogambi (2007), kanuni ya lugha ya kwanza huathiri lugha nyingine

anayojifunza mzungumzaji.

Utafiti huu ulinuia kuchunguza kuimarika kwa umilisi wa wanafunzi Waluo

wanaojifunza Kiswahili kama L2 miongoni mwa wanafunzi wa baadhi ya shule za eneo

la Nyanza. Kutokana na matokeo mazuri katika somo la Kiswahili, utafiti ulichunguza

mikakati ambayo iliweza kuwekwa ili kufikia kiwango hicho. Matokeo ya viwango hivyo

yalitupa mwangaza kuhusu changamoto ambazo zilikumba shule teule miaka ya nyuma na

namna ambavyo shule hizo zi1iweza kukabiliana na changamoto hizo na kuimarisha

matokeo yao ya Kiswahili.

Momanyi (2009), alidai kuwa mojawapo ya sababu kuu za kufundisha Kiswahili katika

mtalaa wa shule za upili ni kuwapa wanafunzi stadi za kimsingi za kuzungumza, kusoma,

kusikiliza na kuandika miundo ya kimsingi ya lugha ya Kiswahili. Utimilifu wa stadi hizi

za kimsingi zinafaa kudhihirika katika matokeo ya mitihani ya KCSE. Wanafunzi

wanafaa kuonyesha umilisi wao wa lugha katika utendaji.

Kufikia sasa watafiti wengi wamechunguza sababu za matokeo duni katika baadhi ya

masomo na katika maeneo mbali mbali kama; (Gesaga, 1986), (Gichura, 1999),

(Kipkorir, 2005), (Ndalu, 1997) na (Njogu, 2005). Hawa wote walichunguza tu sababu

za kuwa na matokeo duni kwa hivyo pengo ambalo utafiti huu ungependa kujaza ni

kwamba tafiti hizi hazikuangazia sababu za kuimarika katika masomo hayo. Mapitio ya

vitabu yalionyesha kuwa watafiti wengi waliegemea sababu za kijamii na tofauti za Ll na

L2. Pia hawakuzingatia viwango vya umilisi wa wanafunzi katika lugha kwa ukamilifu.

(25)

Kiswahili wa wanafunzi katika shule za upili kutoka Luo Nyanza katika kiwarigo cha

sintaksia, changamoto na sababu kuu za kuimarika kwa matokeo ya Kiswahili .

.1.3Maswali ya Utafiti

Utafiti uliongozwa na maswali yafuatayo;

1. Kuna viwango vipi vya umilisi na utendaji wa wanafunzi wa shule za upili katika eneo la

Ziwa katika lugha ya Kiswahili?

2. Ni changamoto zipi hukabili ujifunzaji wa wanafunzi wa sehemu ya Luo Nyanza katika

lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili?

3. Ni nini ilisababisha kuimarika kwa matokeo ya wanafunzi katika mitihani ya Kiswahili

katika eneo la Ziwa?

1.4 Malengo ya Utafiti

Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo;

1. Kubainisha viwango vya umilisi na utendaji wa wanafunzi wa shule za upili zilizoteuliwa

katika sehemu ya Luo Nyanza katika Kiswahili.

2. Kueleza changamoto ambazo hukumba ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili katika

sehemu ya LlIO Nyanza.

3. Kuchunguza sababu za kuimarika kwa matokeo ya wanafunzi kutoka eneo la Ziwa

katika mitihani ya kitaifa ya Kiswahili.

1.5 Sababu za Kuchagua Mada ya Utafiti

Mada ya utafiti huu ilichaguliwa kwa sababu zifuatazo; kwanza, kupitia mikakati

maalumu ya ujifunzaji iliyotumiwa katika shule teule, inatarajiwa kwamba wanafunzi

wataweza kuinua ujuzi wao katika sarufi. Kufahamu sarufi ya lugha fulani ni muhimu

kwani hujumuisha urnilisi na tajiriba za wasemaji wa lugha hiyo kuhusu miundo yake.

(26)

ujumbe usiwafikie watu vizuri. Peck (1988), anaeleza kuwa bila sheria mazungumzo

yatakuwa tu sauti na maandishi kuwa tu michoro.

Sababu ya pili ni kwamba mtafiti alitaka kuchunguza majibu ya wanafunzi na kuwaweka

katika viwango vya umilisi na utendaji. Viwango hivi vilinuiwa kusaidia walimu kuandaa

mbinu zinazofaa kwa kila kikundi ili wanafunzi wote darasani waweze kushughulikiwa

kulingana na uwezo wao ili kufurahia huo umilisi mpya.

lnatarajiwa kuwa matokeo ya utafiti yanaweza kuchochea kuundwa kwa mikakati ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wanafaulu katika kujenga umilisi na utendaji wao wa

somo hili. Bloomfield (1927), anaamini kuwa kuna viwango vya umilisi na utendaji baina

ya wanajamii lugha moja. Anaeleza kwamba utendaji unaathiriwa na hali ya maisha ya

mtu.

Sababu nyingine ya kufanya utafiti huu ni kuwahamasisha walimu pamoja na wanafunzi

kuhusu mbinu bora za kuimarisha umilisi wa wanafunzi katika lugha ya Kiswahili. Hii

ni kwa sababu wasomi wengi wanaamini kuwa kuanguka kwa wanafunzi katika somo la

lugha kunasababisha kuanguka kwa masomo kwa jumla (Martha King, 1984). Kwa hivyo

mbinu ambazo hutumiwa na shule ambazo ni vielelezo bora zitatupa mwangaza kuhusu

namna ya kuimarisha somo la Kiswahili.

Mtafiti alinuia kuwachochea walimu wa lugha kuyatambua matatizo ya wanafunzi wao.

Anavyoeleza Non-ish (1983 :80), kuwa walimu wazingatie mbinu zinazofaa za ufunzaji.

Wanaweza

k

u

fa

h

a

mu

vipengele wanavyostahili kusisitiza katika ufunzaji wao na mbinu

wanazofaa kutumia. Johnson na Johnson (2001: 173), walipendekeza njia bora za ufunzaji

kuwa faafu na kuzingatia kiini cha ujumbe.

Sababu nyingine ya mtafiti kufanya utafiti huu ilikuwa ni kuchochea washika dau wa

elimu na Wakurugenzi wa Magatuzi wa TSC kuweza kuandaa mafunzo au semina kwa

(27)

Kiswahili. Hatua zinazofaa zikichukuliwa, wanafunzi wanaweza kupata umilisi na

utenclaji katika lugha ya Kiswahili bila kuzingatia lugha yao ya kwanza.

1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti

Utafiti huu ulijikita katika umilisi na utenclaji wa wanafunzi wa shule za upili kutoka eneo

la Luo Nyanza katika somo la Kiswahili. Umilisi ulipimwa kupitia hojaji finyu na wazi

kuhusu matumizi ya lugha ambayo iliclhihirishwa katika utendaji. Umilisi una kanuni na

sheria za kufuatwa katika tungo na hizi huonyeshwa katika utenclaji. Anavyoeleza

Chomsky (1965), umilisi ni mfumo wa sheria za lugha. Wanafunzi walipewa maswali

katika sarufi kutoka mitihani ya kitaifa iliyopita. Data za sekondari zilitolewa .kutoka

matokeo ya mitihani ya kitaifa kuanzia mwaka wa 2009 hadi 2012 ili kufanyia

uchanganuzi.

Mbali na viwango vya umilisi na utendaji, utafiti ulichunguza hasa sababu za kuimarika

kwa matokeo katika Kiswahili. Hii ni kwa sababu kipindi cha kati ya mwaka 2009 hadi

2012 kilidhihirisha uimarikaji wa somo hili katika eneo la Nyanza. Suala la kutoimarika

kwa matokeo limegusiwa na Njogu (2005) na Ndalu (1997). Vile vile limejadiliwa katika

sura ya tatu karna changamoto katika ujifunzaji wa Kiswahili. Utafiti ulinuia kuchunguza

namna shule za Nyanza ziliweza kukabiliana na changamoto hizi ili kuimarisha matokeo

yao.

Matokeo ya Somo la Kiswahili hutegemea kufaulu katika mtihani wa karatasi ya insha,

lugha na fasihi. Utafiti huu ulijifunga katika mtihani wa karatasi ya lugha. Sehemu ya

matumizi ya lugha na sarufi. Hii ni kwa sababu sintaksia inadhihirisha vipengele vya

mofolojia. Kulingana na Chomsky kiungo muhimu zaidi katika umilisi wa kiisimu ni kile

cha sintaksia. Finch (2003), anaeleza kuwa sintaksia inahusu namna maneno

yanavyopaugwa katika maanclishi au mazungumzo ili kuleta miundo nu mifumo mizuri

(28)

Sampuli lengwa ilikuwa wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama Ll kwani wao

hawajaathiriwa na lugha nyinginezo za kiasili. Walichaguliwa kwa sababu ya madai ya

Wanyoike (1978:36) na Mbaabu (1985), kuwa wazungumzaji wa Kinailoti kama vile

Waluo wana matatizo katika ujifunzaji wa Kiswahili.

Wanafunzi hutagusana na Kiswahili kila mahali lakini utafiti ulishughulikia shule za upili

katika Eneo la Luo Nyanza. Kwa hivyo matokeo si jumlifu kwa shule zote nchini.

Ingawa shule ya Maranda na Shule ya Wasichana ya Kisumu ndizo zinazotambulika

kufanya vizuri. Kuna shule nyingine nyingi ambazo pia zinapata matokeo mazuri katika

mitihani ya Kiswahili (tazama kiambatisho G). Eneo la Ziwa lina Magatuzi sita;

Nyamira, Kisii, Siaya, Migori, Hornabay na Kisumu (tazarna kiambatisho J). Magatuzi

manne yalijumuishwa kwa sababu sehemu hii ya Luo Nyanza imegawanywa katika

magatuzi marine. Shule moja kutoka kila gatuzi ilitumiwa kama sampuli wakilishi.

Uteuzi clhamirifu ulitumiwa kuchagua shule nne kutoka magatuzi ya Luo yanza kwa

sababu ni zile zilizopata matokeo mazuri zaidi. Hizi ni; Shule ya Wasichana ya Kisumu

(gatuzi la Kisumu), Shule ya Maranda (Siaya), Rapogi (Migori) na Agoro Sare katika

gatuzi la Homa Bay. Wenyeji wa gatuzi la Kisii na yamira ni Wabantu na lugha zao

zinatokana na nasaba moja na Kiswahili. Shule ya wasichana ni moja kwa sababu utafiti

ulinuia sampuli ya wateule zaidi yaani ubora wa matokeo yake katika mtihani. Kama

anavyoeleza Labov (1966), kwarnba sio ukubwa wa sarnpuli bali ni ubora wa data

unaohitajika katika uteuzi wa sarnpuli.

Sampuli ilikuwa ya wanafunzi 100; ishirini na watano kutoka kila shule. Walimu

walikuwa 20; watano katika kila shule walijaza hojaji na kujibu mahojiano. Wanafunzi

asilimia tano waliteuliwa kutoka kila darasa kujaza hojaji. Vidato vya pili na vya tatu

vilitafitiwa kwani hapo ndipo pan a mafunzo ya msingi. Kidato cha pili wangali

(29)

utangulizi wa somo nacho cha nne ni kudurusu. Mbinu ya uteuzi dhamirifu ilitumiwa

kuteua wahojiwa kwa kuchukua matokeo ya mtihani wa muhula. Orodha ya wanafunzi

arobaine bora iliturniwa na kuteua wale ambao ni wazawa Waluo.

Utafiti ulifanywa shuleni palipo na mafunzo rasmi darasani kwa sababu wao ndio

wanaojifunza Kiswahili kama L2.

1.7 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 1.7.1 Maandiko Kuhusu adharia

Chornsky katika kitabu chake cha Syntactic Structures (1957), anashikilia mtazamo

kwamba kila binadamu ana uwezo wa kupata na kujifunza lugha. Chomsky (1965),

anaendelea kueleza dhana ya umilisi na utendaji katika nadharia yake ya Sarufi Zalishi

ambapo anadai kuwa umilisi ni mfumo wa kiasili unaomwezesha mtumiaji wa lugha

kuzalisha na kuelewa idadi isiyo kikomo ya sentensi za lugha. Nadharia ya Sarufi Zalishi

ilitumiwa katika utafiti huu. Chomsky anaeleza kuwa kuna tofauti baina ya kile

tunachokij ua na kile tunachokitenda. Akijadili tofauti kati ya umilisi na utendaj ianaeleza

kuwa mazungurnzo yetu ya kila siku si njia mwafaka ya kuakisi uwezo wetu wa kiisimu.

Tunaweza kufanya makosa kwa sababu ya utelezi wa ulimi. Umilisi wa kiisimu huwa

ubongoni ilhali utendaji wa kiisimu ni kile kinachotoka mdomoni. Hymes (1967),

anaeleza namna ambavyo umilisi unavyotofautiana na utendaji. Anadai kuwa umilisi

huathiri tu utendaji iwapo mzungumzaji ana kasoro fulani katika mawasiliano.

Radford (1997), anadai kwamba mtoto anazaliwa na uwezo wa kijenetiki wa kupata

lugha. Upataji wa lugha unatokea wakati kitivo cha lugha ubongoni mwa mtoto

kinapotagusana na tajiriba ya kiisimu katika mazingira ya kijamii. Mtagusano huu

unavyaza sarufi ya lugha husika. Anaongeza kwamba mtazarno kuhusu upataji wa lugha

ya kwanza unaweza kuelekezwa kwenye ufunzaji wa lugha ya pili. Katika ufunzaji wa

(30)

atakayornwandalia mwanafunzi. Hivi ni kuserna kwarnba rnsernaji wa lugha ya pili

atakuja kurnulika vigezo vya kanuni zinazotawala rnaana na rnaumbo ya lugha

anayojifunza. Kazi hii ilichangia ufahamu wetu kuhusu upataji wa L2 rniongoni rnwa

wanafunzi Waluo wanaojifunza Kiswahili.

Onyango (2006), aliyechunguza toni ya vitenzi katika Olunyala, alitumia mihirnili rninne

ya nadharia ya Sarufi Zalishi kueleza tofauti hizo; Kwanza, tofauti baina ya urnilisi

ambao ni ule ujuzi walio nao wazungurnzaji ilhali utendaji ni matumizi halisi ya lugha

katika miktadha rnbalimbali. Pili, sarufi ya lugha huchukukuliwa kuwa kieleiezo cha

umilisi wa rnzungumzaji. Tatu, isirnu hujishughulisha na utazarnaji wa sifa bainifu za

lugha na sarufi iwe na sheria na muundo bainifu za tungo. Kazi hii iiichangia utafiti wctu

katika kubainisha tofauti kati ya umilisi na utendaji.

Chacha na Musau (2001), katika Mbinu za Kisasa za Kufuiidisha Kiswaliili kwa Walimu

wo Shule za Msingi, Upili na Vyuo Vi/ant wanaelezea baadhi ya nadharia za ufundishaji

wa lugha ya pili. Wanajadili nadharia ya KK na mihimili ya nadharia hiyo. Kazi hiyo ni

tofauti na utafiti wetu kwani wao waliangazia nadharia zote za ufunzaji wa lugha ya pili

kwa ujumla. Utafiti huu uiiangazia nadharia rnoja ya KK. Kazi hii ilichangia pakubwa

kueleza namna wanafunzi wa eneo la Ziwa wameweza kuboresha utendaji na matokeo

yao katika mitihani ya kitaifa ya KCSE katika Kiswahili.

1.7.2 Maandiko Kuhusu Ugumu wa Upataji wa Kiswahili kama L2 kwa Wanafunzi

Waluo

Lugha ya Kiswahili na Dholuo ni tofauti kwa namna nyingi. Mbaabu (1985), akieleza

muundo wa sauti za Kiswahili, anaeleza binadarnu ana uwczo wa kutamka sauti zote za

lugha za ulimwengu. Wanyoike (1978:36), Musau (1993) na Mbaabu (1985), wanaeleza

kuwa Dholuo ni lugha ya Kinailoti na wanafunzi wa Kinailoti wana matatizo katika

ujifunzaji wa Kiswahili ambayo ni lugha ya Kibantu. Baadhi ya matatizo ambayo

13

(31)

Lt

.

wanafunzi hupata katika ujifunzaji wa L2 hujitokeza katika viwango tofauti vya kiisimu.

Wanaeleza kuwa baadhi ya wazawa wa lugha ya Dholuo huwa na matatizo katika

ujifunzaji wa Kiswahili kwa sababu ya athari za L1. Wanyoike anapendekeza kuwa

wanaotaka kufanya utafiti wa kina wawe walio na umilisi mzuri wa lugha ya Kiswahili na

Mbaabu (1985:75), anaeleza namna ujuzi wa Dholuo kama L1 unavyoingilia Kiswahili.

Anaeleza wakati wa kuongea lugha ya Kiswahili watu wengi huingiza maneno ya L1

katika sentensi za Kiswahili. Baadhi ya sababu zikiwa; ukosefu wa umilisi kamili wa

lugha ya Kiswahili husababisha utata. Kwa mfano, kila lugha ina methaJi zake tofauti.

shida kutafsiri methali kutoka lugha moja hadi nyingine bila kugeuza maana na mpangilio

wa sauti katika kuunda maneno. Matokeo ya utafiti wake kuhusu Dholuo ni kuwa; majina

ya Luo hayajapangwa katika makundi ya umoja na wingi kama yalivyopangwa katika

Kiswahili. Hakuna viambishi vinavyotofautisha vitu vilivyo hai na visivyo hai na Mjaluo

anapozungumza Kiswahili huwa amepanga fikira zake kwa mpangilio wa lugha ya

Dholuo. Yeye hutafsiri kwa Kiswahili na neno moja la Dholuo huwa na matumizi mengi

kuliko tafsiri yake katika Kiswahili. Kwa mfano, {kendo} - {oal tenal mekoni} ..

King'ei na Musau (2002), wanaongeza kuwa matatizo ya kimatamshi miongoni mwa

wazungumzaji wa Kiswahili yanatokana na lugha za mama za wazungumzaji. Sauti za

lugha ni tofauti na kila lugha ina idadi fulani ya vitamkwa. Matokeo ya utafiti wao ni

kwamba; kwanza, Kijaluo hakina sauti zifuatazo; lvi, Iz/,1 shl na /gh/, kwa mfano, kutofautisha [shuka/suka] huwatatiza. Pili, vokali za Dholuo ni nyingi kuliko tano za

Kiswahili - li,e,a,o,u,E,J,O,U/. Jambo la tatu ni kurefusha vokali. Lugha zote mbili

huweka shadda kwenye silabi ya pili kutoka mwisho wa neno. Hata hivyo, zinatofautiana

(32)

Kwa mfano, $ja $te $do$ (mpishi). [ ja'tedo ]. Neno [ugali] katika Dholuo litakuwa [uga:li]. Vile vile lugha nyingi huwa na mipangilio tofauti ya konsonanti na vokali.

Upekee wa Dholuo ni kuwa hupendelea zaidi mpangilio wa konsonanti vokali (KV)

mwanzoni mwa kila neno. Kwa hivyo, wazungumzaji hutatizika wanapokumbana na

mfuatano wa konsonanti konsonanti (KK) mwanzoni mwa neno kwa mfano,

Kiswahili Dholuo

Mtu, mbwa mutu, umbwa

Wilkins (1974), alibaini kuwa mtoto atachukua miaka mitatu au minne kujifunza Ll ili

kufikia umilisi bora. Hivyo basi, yule anayejifunza L2 ili kufikia kiwango hicho

kutategemea muda anaotumia katika matumizi ya L2. Kazi hizi zinafaidi utafiti huu

kwani zinafafanua ugumu ambao wanafunzi Waluo hupata katika ujifunzaji wa Kiswahili

kama lugha ya pili. Tofauti ni kwamba kazi hii ilichunguza namna wanafunzi Waluo

waliweza kukabiliana na matatizo hayo.

Komora (1971), katika A Kiswahili Course Teachers Book J anadokeza kuwa wanafunzi

ambao huzungumza lugha sawa au iliyo karibu na Kiswahili watajifunza haraka zaidi

kuliko wale ambao huzungumza lugha tofauti na Kiswahili. Crispus na Kamal (1984),

katika Mbinu za Kufundisha Kiswahili, wanaeleza kuwa wanafunzi wanapoenda shuleni

wanafaa kuandaliwa kujifunza Kiswahili. Wengine watachukua wiki mbili kujifunza hasa

wale wanaozungumza Kiswahili nyumbani kama watoto wa pwani na wale wa mjini.

Wanaozungumza Kibantu watachukua wiki sita ilhali kutoka lugha nyingine kama

Dholuo na Kikalenjin watahitaji wiki nane au zaidi. Kazi hii ilidhihirisha tofauti iliyopo

baina ya lugha hizi mbili.

Tofauti nyingine zilionyeshwa na Mudhune (1994), katika A Contrastive Analysis

Approach to the Learning of Swahili Morphosyntax by Luo Learners. Tasnifu hiyo

(33)

Kiswahili yalihusu vivumishi, vihusishi, vimilikishi na tarakimu kwa vile hakuna

upatanisho wa kisarufi. Alionyesha kuwa makosa hayo huhamishwa hadi Kiswahili

ambapo Kiswahili . ni mojawapo ya lugha za Kibantu. Kiswahili sanifu (na lugha

nyingine za Kibantu) huwa na ngeli za nomino. Nomino ndizo hutawala sentensi yote.

Kwa mfano, {m}

+

{tu} ni ngeli ya kwanza, {watu} ni ngeli ya pili. Kisha hakuna

uhusiano wowote wa kimofolojia kati ya nomino na maneno mengine. Kwa mfano,

dhok ariyo - ng'ombe wawili. Kazi yake ni tofauti na utafiti wetu kwani utafiti wetu

haulinganishi lugha hizo mbili bali inaeleza ugumu ambao wanafunzi wanaweza kupata

katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili.

Olal (2008), alishughulikia utohozi wa maneno mkopo ya Dholuo kutoka Kiswahili.

Alionyesha kuwa mageuzi ya kifonolojia katika maneno mkopo ya Dholuo hudhihirisha

istilahi zinazotofautiana na maneno asilia ya Kiswahili. Anaeleza kuwa Dholuo ni lugha

toni. Kazi yake ilisaidia kufafanua tofauti kati ya lugha hizi mbili na matatizo ya

wanafunzi Waluo wanaojifunza Kiswahili.

1.7.3 Maandiko Kuhusu Mbinu za Ufunzaji naUboreshaji wa Matokeo ya Kiswahili

Njogu (2005), alichunguza matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa na kuelezea

matatizo ya Kiswahili kama lugha ya taifa. Alidokeza baadhi ya matatizo kuwa; ufahamu

mdogo wa umilisi wa kiisimu, kuzuka kwa kilugha cha 'sheng', kuwa na mielekeo hasi

kuhusu uwezo wa Kiswahili, ukosefu wa motisha wa kujua lugha ya Kiswahili vizuri

katika kiwango cha kitaifa na akasisitiza ufunzaji wa Kiswahili nchini. Kazi yake

ilisaidia kujua ni kwa namna gani shule za Nyanza zilisuluhisha baadhi ya matatizo hayo

ili kuboresha matokeo yao katika KCSE.

Kulingana na Ndalu (1997), mbinu za kufundisha Kiswahili ni kama vile; kuwafunza

(34)

kurekebisha makosa pale yanapotokea na kujua viwango na asili ya wanafunzi ili kujua

ni wanafunzi gani watahitaji muda mrefu zaidi kujifunza. Kazi yake ilisaidia kufafanua

baadhi ya changamoto zinazokabi1i lugha hii ya Kiswahili.

aye Gesaga (1986), alichunguza mambo yanayoathiri utendaji wa lugha ya Kiingereza.

Alishughulikia uhusiano baina ya alama za CPE (mtihani wa darasa la nane) za

wanafunzi wanapoingia katika kidato cha kwanza na a1ama wanazopata katika KCE

(mtihani wa kidato cha nne), tajiriba za walimu, vifaa na mbinu za ufunzaji na ujifunzaji.

Utafiti wake unatofautiana na kazi yetu kwani eneo la utafiti wake 1ilikuwa Kiambu,

katika sorno la Kiingereza na pia aligawa kazi yake katika shu1e bora, wastani na dhaifu

na utafiti huu ulifanywa kati ya miaka 1983-1985. Tofauti zilizoko ni kwamba kwa sasa

mfumo wa elirnu umebadi1ika na mitihani inayofanywa sasa ni KCPE, darasa la nane na

KCSE kidato cha nne. Vile vile shule zimeainishwa katika vitengo vinne hasa mtihani wa

KCSE mwaka wa 2011 ambazo ni shu1e za kitaifa, shule za magatuzi, shule za wi1aya na

za kibinafsi. Utafiti wetu ulizingatia shule zilizofanya vyema katika lugha ya Kiswahili

pekee. Kazi yake ilisaidia mtafiti kujua vipenge1e vya kuchunguza hasa anapomnukuu

Martha King (1984), anayesema:

"Kwajinsi kufaulu kwa elimu kunahusiana na umilisi wa lugha basi pia kuanguka

kwa shule kunahusiana na kuanguka kwa 1ugha'. Kufaulu na kuanguka kwa

wanafunzi kunategemea na kufungamana na jinsi wanavyoshirikiana na kuunda

maana kupitia lugha."

Mtafiti anakubaliana naye kuwa ni muhimu kupunguza matokeo mabaya katika 1ugha

mwanafunzi anapotaka kufau1u katika mtihani. Kulingana na Gichura (1999), jambe

muhimu zaidi linaloathiri masomo hasa ya wasichana ni mielekeo yao. Alipendekeza

umuhimu wa kuchunguza rnazingira katika elimu kama nadharia ya Dewey inavyosema

(35)

Kipkorir (2005), na Eshiwani (1988), walichunguza sababu za kijamii na kiuchurni na

namna zinavyoathiri matokeo bora. Kazi ya Kipkorir inachangia kazi hii pale

anapowanukuu Cohen and Marion (1994), wanapoeleza kuwa uteuzi wa sampuli

kimaksudi hutumiwa pale mtafiti anapokuwa na sababu ya kufinya sampuli kwa

madhumuni ya kupata sampuli iliyokusudiwa kuwa na habari zinazohitajika hasa

ukizingatia malengo ya utafiti. Kipkorir alitumia nadharia ya Mgawanyiko wa Kitabaka

katika jamii lakini utafiti wetu unatumia nadharia ya KK. Hata hivyo, Fraser (1959),

anadai kuwa katika kila kiwango cha uwezo kutakuwa na tofauti katika matokeo ambayo

huweza kuelezwa kwa sababu tofauti tofauti.

Kwa jumla, mapitio ya maandiko haya yalitumiwa kufafanua tofauti kati ya umilisi na

utendaji, kueleza changamoto zinazowakabili wanafunzi katika ujifunzaji wa Kiswahili

kama L2 katika eneo la Ziwa na jinsi ya kuimarisha matokeo ya Kiswahili.

1.8 Misingi ya N adharia

Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni Sarufi Zalishi (Chomsky, 1965) na nadharia ya

Kijumuia na Kibinadamu (Richards na Rodgers, 2001).

1.8.1 Nadharia ya Sarufi Zalishi

Chomsky (1957), katika kitabu chake cha Syntactic Structures anashikilia mtazamo

kwamba kila binadamu ana uwezo wa kupata na kujifunza lugha. adharia ya Sarufi

Zalishi (SZ) iliasisiwa nu Noam Chomsky katika chapisho lake la (1965), Aspects of the

Theory ofSyntax. Umilisi wa kiisimu unahusiana na ujuzi wa muundo wa lugha. Umilisi

huo hautegemei sifa za kijamii bali mazingira faafu ya mtoto kukua. Chomsky

ametofautisha umilisi kuwa ubongoni ilhali utendaji ni kile kinachotoka mdomoni.

(36)

1.8.1.1 Mihimili ya Nadharia ya Sarufi Zalishi

Mihimili ya nadharia ya SZ ni kama ifuatayo:

1. Sarufi Zalishi hunuia kueleza uwezo au umilisi wamzawa wa lugha. Umilisi na

Utendaji ni dhana za kimsingi katika SZ.

I!. SZ inaeleza tungo zote ambazo zinaweza kuzalishwa katika lugha fulani.

111. Hueleza sentensi ambazo si sahihi na zile ambazo ni sahihi katika lugha husika.

IV. Sifa za SZ ni kwamba inajieleza kinaganaga na kwa uwazi kupitia kanuni hi vi kwamba

rnsomaji wa sarufi hii hapaswi kutumia makisio yoyote au ujuzi wowote kujaribu kubaini

yanayoelezwa na sarufi hii.

v. Sheria za SZ ni kielelezo na maagizo yake ni kama yale yanayopewa kompyuta.

Maagizo hayo hayaelezwi. Kwa mfano, maagizo yanayosema;

S KN

+

KT (yaani iandikwe hivi; Sentensi ni kirai nomino na kirai tenzi)

VI. Sarufi Zalishi inaweza kubashiri hivi kwamba haielezei tu tungo ambazo tayari

zimezuliwa au kutungwa. SZ inaweza kuzua kwa kubashiri tungo zote ambazo kuna

uwezekano wa kuzitoa katika lugha husika au pengine sentensi ambazo hazijawahi

hata kamwe kutolewa.

Vii Nadharia ya SZ inaweza kuonyesha sentensi ambazo sio za lugha husika.

Viii Ina uwezo wa kufasiri baadhi ya semi kuwa na usarifu japo hatujawahi kuzisikia hapo

mbeleni.

Nadharia hii ilitumiwa kukadiria na kuchanganua data za matokeo ya wanafunzi katika

shule teule. Kutokana na matokeo ya zoezi la sarufi katika Kiswahili, wanafunzi

waliwekwa katika viwango mbalimbali vya urnilisi na utendaji. Mihimili yote hapo juu

ilitumiwa katika kuchanganua majibu ya wanafunzi katika sura ya pili. Upungufu wa

nadharia hii ni kutoweza kueleza utendaji wa wanafunzi ambao ulijalizwa na nadharia ya

(37)

8.1.2 Dhana za Sarufi Zalishi

Umilisi- ni uwezo wa kiisimu. Chomsky (1965), anaueleza kama ule uwezo wa

mzungumzaji asilia wa lugha wa kuimudu lugha yake. Kupitia umilisi mzungumzaji

asilia wa lugha anaweza kudondoa sentensi ambazo ni sahihi na ambazo si sahihi kisarufi. I-Iumwezesha mzungumzaji asilia kudondoa zile sentensi ambazo zinawezekana kutolewa katika lugha hiyo na zile ambazo haziwezekani kutolewa. Pia anaweza kutambua maumbo

na miundo tofauti ya tungo moja na aweze kutambua utata katika sentensi.

Kwa mujibu wa Radford (1997:274), Sarufi Bia ni ujuzi wa umilisi lugha uliowakilishwa

ubongoni mwa msemaji lakini kushirikiwa na wanadamu wote. Umilisi wa L2 ulipimwa

kupitia majibu ya sarufi na matumizi ya lugha ya wanafunzi, alama walizopata na

uzingativu wa sheria za kisintaksia.

Bloomfield (1927), anaamini kuwa kuna viwango vya umilisi na utendaji baina ya

wanajamii lugha moja. Bloomfield anaeleza kwamba utendaji unaathiriwa na hali ya

maisha ya mtu. Finch (2003), alieleza kuwa uwezo wetu wa kuzalisha mifumo mizuri ya

uundaji wa maneno unategemea; kwanza, umilisi wetu wa aina za maneno. Pili, uwezo

huo umo ndani/ ubongoni.

Utendaji - Ni yale matumizi ya lugha katika muktadha halisi (Chomsky, 1965). Ni uturniaji wa ule uwezo wa kiisimu katika muktadha halisi. Utendaji humwezesha mzungumzaji asilia wa lugha kubadilisha tungo na kuzitumia vilivyo kutoka mtindo

mmoja hadi mwingine. Kwa mujibu wa Dell (1965), utendaji wa kiisimu 111 kama

mwangwi unaoakisi umilisi kamili. Huweza kuathiriwa na sababu za kijamii.

Kwa mujibu wa nadharia ya SZ pamoja na mihimili yake kama ilivyoelezwa 'hapo juu, mtafiti aliweza kuzua kiele1ezo kifuatacho ili kufafanua viwango vya umilisi na utendaji

(38)

(1.4) Kielelezo cha Viwango vya Umilisi na Utendaji katika SZ

Mawasiliano

Umilisi utendaji

1

1

Viwango vya umilisi viwango vya utendaji

Umilisi wajuu umilisi kiasi umilisi hafifu utendaji wa juu utendaj kiasi

(tafsiri yangu)

1.8.2 Nadharia ya Kijumuia na Kibinadamu

Naclharia hii iliasisiwa na Jack C. Richarcls and Rodgers, T. S. (200 I),katika kitabu chao

cha Approaches and Methods in Language Teaching. Mct'afferty, Jacobs na Icldings

(2006), pamoja na Richards (2001), wanapendekeza namna ya ufundishaji wa lugha ya

pili ambapo mwalimu ana jukumu la mshauri na msaiclizi wa mwanafunzi, naye

mwanafunzi ni mshauriwa na msaidiwa. Wanaeleza kuwa ujifunzaji wa L2 uchukuliwe

kama utoaji wa ushauri na nasaha wa kimatibabu. Mwalimu anafaa kuchukua nafasi ya

daktari na kumsikiliza mwanafunzi, ampe nafasi ya kujieleza na kisha kuonyesha ule ujuzi

mpya. Naclharia hii inasisitiza ufunzaji ulio na utu na ubinadarnu. Chacha na Musau

(200 t), wakimnukuu Richards wanaeleza kuwa kuna mitazamo mbalimbali ya ufunzaji

(39)

1.8.2.1 Mihimili ya Nadharia

Mihimili ya nadharia ya KK ilifupishwa kama ifuatayo;

I. Usalama wa wanafunzi ni muhimu kwani wakiwa na wasiwasi na kutojisikia salama

hawawezi kujifunza lugha vizuri.

11. Kutomakinika kwa wanafunzi kupunguzwe kwa kuwapa majukumu tofauti tofauti

darasani.

Ill. Wanafunzi wakijifundisha mada au stadi fulani wanapaswa kuhimizwa kuonyesha ujuzi

huo mpya darasani kwa mazungurnzo au maandishi.

IV. Wanafunzi wanafaa kuwa na fahari na kufurahia ujuzi huo na mwalimu anafaa awape

nafasi hiyo.

v. Wanafunzi wanafaa kujifunza lugha kwa njia rnbalimbali karna vile tafsiri, kujirekodi

katika kanda za kunasia sauti, vikundi, ucharnbuzi, usikizaji na rnazungumzo yajumla.

VI. Mwisho ujifunzaji ni jukumu la jumuia ya wanafunzi pamoja na mwalirnu. Washiriki

wanafaa kujifunza kwa kutangamana na wenzao. Kwa hivyo kujifunza ni jukumu la

ushirikiano wa jumuiya.

adharia hii ilitumiwa katika utafiti huu ili kuonyesha changamoto katika ujifunzaji wa

Kiswahili, kufafanua utendaji wa rnzungumzaji au rnwanajamii, na narnna wanafunzi

waliweza kuboresha utendaji wao katika mitihani ya Kiswahili ya kitaifa.Walimu

walihojiwa na wanafunzi walijaza hojaji kueleza rnbinu za ufunzaji kama rnatumizi ya

vifaa, vitabu, idadi ya walimu pamoja na vipindi vya ziada au ratiba maalumu na hii

ilionyesha namna mihimili hiyo inavyotenda kazi.

1.9 Mbinu za Utafiti

Orodho (2003), alieleza mbinu za utafiti kuwa mwongozo au utaratibu unaotumiwa kuzua

majibu kwa maswali ya utafiti. Utafiti huu ulifanywa maktabani na nyanjani. Mbinu za

(40)

ambapo hojaji zilitungwa mapema na kupewa wanafunzi na walimu kujibu. Kulingana na

Kombo na Tromp (2006), hojaji hutumiwa kwa sampuli teule na kubwa na katika maeneo

mbalimbali kwa hivyo huokoa wakati. Majibu hupatikana baadaye. Hii inaaminiwa kutoa

majibu haraka na kwa uhakika. Wanafunzi wanachukuliwa kuwa wahojiwa faafu.

Wanafunzi wanatoka katika jamii na katika shule ambapo Kiswahili kama L2

inayochunguzwa inatumiwa. Inaaminika kuwa wao wanaweza kutoa data muhimu na za

kuaminika kwa utafiti huu.

Walimu walijaza hojaji na wasrmarruzi wa somo la Kiswahili walihojiwa. Walimu

wanachukuliwa kama watekelezaji wa sera za lugha shuleni. Wao ndio wanaomiliki mada

za kufundisha kwa wanafunzi kwa hivyo, wanachukuliwa kuwa wahojiwa wanaofaa

Zaidi katika utafiti kwani wanaweza kutoa maoni yao, ya wanafunzi wao na hata kuhusu

sera za lugha shuleni kama anavyoeleza (Kembo- Sure, 1996).

Utafiti pia ulifanywa maktabani ambapo vitabu mbalimbali vinavyoelezea nadharia

vilitumiwa. Tasnifu mbalimbali zilichunguzwa na machapisho mengine muhimu. Vitabu

hivi vilitumiwa kufafanua mada hii ya utafiti.

1.9.1 Mahali pa Utafiti

Utafiti ulifanywa eneo la Luo Nyanza kwa sababu wakazi wa eneo hili ni wazungumzaji

wa Dholuo wanaojifunza Kiswahili kama L2. Inaaminika kwamba Waluo hawana umilisi

kamili wa Kiswahili kama wanavyodai Wanyoike (1978) 11aMbaabu (1985), kuwa

baadhi ya wazawa wa lugha ya Dholuo huwa na matatizo katika ujifunzaji wa Kiswahili

kwa sababu ya athari za L1.

Mbinu ya uteuzi kimaksudi ilitumiwa kuchagua shule nne ambazo ni; Maranda, St.

Joseph's Rapogi, Agoro Sare na KisUI1111Girls kwa kuangalia ufaulu wazo wa kiwango

(41)

Vidato vya pili na vya tatu vilitafitiwa kwani hapo ndipo pana mafunzo kamili, kidato cha

tatu wako tayari kwa mtihani. Kidato cha kwanza ni utangulizi wa somo nacho cha nne ni

kudurusu. Mbinu hiyo ilitumiwa ili kupata data kamili za kuaminika na zilizohitajika.

1.9.2 Uteuzi wa Sampuli

Kombo na Tromp (2006), wanaeleza kuwa sampuli kusudi huwa mwafaka pale ambapo

kundi au sehemu fulani inaaaminiwa ndiyo ina data mwafaka inayoafiki malengo ya

utafiti. Mbinu hiyo ilihakikisha mtafiti ametumia shule bora katika mitihani ya kitaifa.

Uteuzi wa sampuli dhamirifu ulitumiwa katika utafiti huu. Kipkorir akiwanukuu Cohen

na Marion (1994), anaeleza kuwa uteuzi wa sampuli kimakusudi hutumiwa pale .mtafiti

anapokuwa na sababu ya kufinya sampuli kwa madhumuni ya kupata sampuli

iliyokusudiwa kuwa na habari zinazohitajika hasa ukizingatia malengo ya utafiti. Utafiti

ulifanywa katika shule nne za upili ambazo ziliteuliwa kwa kufanya vyema katika

Kiswahili kutoka eneo la Luo Nyanza, ambao hawajaathiriwa na lugha nyingine za

Kibantu.

Labov (1966:283), anaeleza kuwa kanuni katika uteuzi wa sampuli ni kuwa upana na

usawa wa uteuzi unafaa kuwa wakilishi kwa sampuli yote. Hivi ni kusema kwamba shule

zilizoteuliwa zinawakilisha shule zote za eneo hilo. Shule moja ya wasichana pamoja na

shule tatu za wavulana zilifanyiwa utafiti. Shule ya wasichana ni moja kwa sababu utafiti

ulinuia sampuli dhamirifu, yaani shule zinazofanya vyema katika Kiswahili. Shule hizo

zilijumuisha zile za kitaifa ambazo ni Maranda na Kisumu Girls na za magatuzi ambazo

ni; Agoro Sare na St.Joseph's Rapogi. Kabla ya mwaka 2012 shule zote nne zilikuwa

katika kategoria ya shule za mikoa.

Kulingana na Du Plooy (2002), Cohen na Marion (1994) na Canale (1983),

walipendekeza mbinu ya uteuzi wa sampuli dhamirifu kuwa mbinu bora katika kuteua

(42)

kutoka kila shule na walimu 20; watano kutoka kila shule walijaza hojaji. Wanafunzi

asilimia tano waliteuliwa kutoka kila darasa.

1.9.3 Ukusanyaji wa Data

Ubora wa kazi yoyote ya utafiti hutegemea ubora wa data iliyokusanywa ili

kuchanganuliwa (Kombo na Tramp, 2006). Data zilikusanywa kutoka shule nne teule

kwa kutumia hojaji na mahojiano. Wanafunzi walipewa mtihani wa matumizi ya lugha

kujibu. Majibu hayo yalitumiwa katika uchanganuzi.

Vifaa vingine vya ukusanyaji data vilivyotumiwa ni kama vile; hojaji, mahojiano,

utazamaji, vitabu, kalamu na vipakatalishi. Walimu walipewa hojaji kujaza, wasimamizi

wa somo la Kiswahili walihojiwa. Data ya matokeo ya mitihani ya kitaifa kutoka shule

hizo zilirejelewa katika uchanganuzi.

1.9.4 Uchanganuzi wa Data

Matokco yalioanishwa na kupangwa. Kombo na Tromp (2006), wanapendekeza data

kupangwa kutoka ghafi hadi taarifa, taarifa hadi ukweli uliothibitishwa na ukweli huo

kuwa elimu. Uhifadhi wa data ulifanywa katika karatasi, daftari, tarakilishi na majedwali.

Uchanganuzi ukaongozwa na nadharia ya SZ na nadharia ya KK. Mihimili ya SZ ilisaidia

katika kubainisha viwango vya umilisi na utendaji wa wanafunzi. Mihimili ya KK

ilisaidia kutathmini changamoto katika ujifunzaji wa Kiswahili na jinsi walivyoboresha

matokeo ya Kiswahili. Data hizo zilipangwa kulingana na mada tofauti tofauti kwa

kurejelea malengo ya utafiti.

Uchanganuzi ulifanywa kwa kutumia mbinu za kimaelezo na za kitakwimu. Maelezo

yalitolewa kuhusu mada tofauti na kutoa muhtasari wa kiini. Brown (1990); anaeleza

umuhimu wa idadi ya utukiaji na viwango vya asilimia katika mbinu ya kitakwimu.

(43)

kiisimu kwa kutumia nambari. Kuonyesha kipashio fulani cha kiisimu kilitokea mara

ngapl.

Majibu ya hojaji na mahojiano yalitumiwa. Hii ni kwa sababu hojaji na mahojiano hutoa

majibu yenye uwazi na kwa undani. Hojaji za wanafunzi zilisahihishwa. Baada ya kupewa

alama juu ya 30, alama hizo ziliwekwa katika asilimia. Ili kufikia malengo ya utafiti huu,

uchunguzi ulilenga kujibu maswali yanayoongoza utafiti huu.

1.9.5 Uwasilishaji wa Data

Data ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo kwa kiasi kikubwa. Maelezo ni kuandaa ripoti

ya muhtasari wa mada zote muhimu na kuonyesha uhusiano wao (Kombo na

Tromp,2006). Picha, jedwali, na michoro pia zilitumiwa pale palipohitajika. Data kutoka

alarna za wanafunzi na matokeo ya shule mbalimbali zilitumiwa. Picha zilitumiwa

kulinganisha shule teule katika majibu yao. Michoro na majedwali yalitumiwa kuonyesha

asilimia ya alama ya wanafunzi. Maelezo yalitolewa kuhusu majedwali hayo. Matokeo ya

utafiti yamejadiliwa kwa kurejelea maswali ya utafiti, malengo ya utafiti na mihimili ya

nadharia iliyoongoza utafiti huu.

Hitimisho

Sura hii imeeleza kiini cha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti 11UU.

Katika sura hii mbinu za utafiti zilionyeshwa. Data zilizopatikana zilipangwa na

kutumiwa katika uchanganuzi. Katika sura inayofuata, viwango vya umilisi na utendaji

vitashughulikiwa kwa kuangazia sifa mbalimbali za kila kiwango kwa kuchunguza majibu

ya wanafunzi katika hojaji. Kielelezo cha viwango vya umilisi na utendaji (1.4)

(44)

SURA YA PILI

VIWANGO VYA UMILISI NA UTENDAJJ

2.0 Utangutizi

Sura hii inachunguza viwango mbalimbali vya umilisi na utendaji wa wanafunzi katika

shule zilizoteuliwa katika eneo la Nyanza. Wanafunzi walipewa maswali katika sarufi ili

kubainisha na kuwaweka katika viwango vya umilisi na utendaji. Matokeo yalichunguzwa

kwa muktadha wa sifa za viwango vya umilisi na utendaji. Rejelea kielelezo (1.4).

2.1Viwango vya Umilisi

Umilisi ni ule uwezo wa mzungumzaji asilia wa lugha kuimudu lugha yake (Chomsky,

1965). Kupitia umilisi mzungumzaji asilia wa lugha anaweza kudondoa tungo ambazo si

sahihi na zile ambazo ni sahihi kisarufi katika lugha husika. Anaweza pia kutambua

maumbo na miundo tofauti ya tungo moja. Vile vile, anaweza kutambua utata katika

sentensi za lugha yake husika. Bloomfield (1927), anadai kuwa kuna viwango vya umilisi

na utendaji baina ya wanajamii lugha moja. Kwa mujibu wake Bloomfield, utendaji

huathiriwa na hali ya maisha ya mtu na hata umilisi wake wa ndani. Kutokana na

maelezo yaliyotolewa hapo juu mtafiti aliweza kuzua vigezo kadhaa vya kuonyesha

umilisi kwa jumla. Kulingana na Chomsky (1965), umilisi umo ubongoni wala

hauonekani. Kwa hivyo, vigezo hivi vinaweza kudhihirishwa tu katika utendaji wa

wanafunzi. Vigezo vya umilisi ni kama ifuatavyo;

I. Mwanafunzi awe na uwezo wa kuonyesha tungo zote ambazo zinaweza kuzalishwa

katika lugha fulani.

11. Awe na ujuzi wa sheria zinazotawala lugha husika. Chomsky (1965), anaeleza umilisi

ni mfumo wa sheria za lugha, unaeleza ujuzi wa sheria.

(45)

IV. Mwanafunzi aweze kuzua kwa kubashiri tungo zote ambazo kuna uwezekano wa

kuzitoa katika lugha husika au pengine sentensi ambazo hazijawahi hata kamwe

kutolewa.

v. Mwanafunzi aweze kudondoa sentensi ambazo si sahihi na zile ambazo ni sahihi katika

lugha husika.

VI. Aweze kuonyesha sentensi ambazo sic za lugha husika.

VII. Awe na uwezo wa kufasiri baadhi ya semi kuwa na usarifu japo hajawahi kuzisikia hapo

awali.

VIII Aweze kutambua utata katika sentensi husika.

VIII. Aweze kubainisha sentensi zilizo na ukubalifu na zisizo na ukubalifu.

Kwa mujibu wa vigezo hivi, wanafunzi walipewa mazoezi katika sarufi na matumizi ya

lugha na kutokana na majibu waliwekwa katika viwango vitatu vya umilisi ambavyo ni;

umilisi wa juu, umilisi kiasi na umilisi hafifu. Viwango hivi vinajadiliwa hapa chini;

2.1.1 Umilisi wa Juu

Umilisi wa juu ndio upeo wa juu katika umilisi wa lugha. Katika sehemu hii wanafunzi

walipewa maswali na wengi wao walidhihirisha kuwa na umilisi wa ha1i ya juu kwa

kupata alama kati ya 20- 30 kwa jumla ya a1ama 30. Ni wawili tu waliokuwa na alama

40% na 26.67%. Fraser (1959), anadai kuwa katika kila kiwango cha umilisi kutakuwa

na tofauti katika matokeo ambayo huweza kuelezwa kwa sababu tofauti tofauti. Haya

ndiyo matokeo ya wanafunzi wa1iojibu hojaji;

(2.1) Marokco ya Wanafunzi Waliojaza Hojaji (katika asilimia)

shule Jdadi ya Alama ya juu Wastani Alama ya

wanafunzi chini

KisumuGirls 25 86.66 70 50

Maranda 25 91.67 59.03 40

Rapogi 25 93 76.69 56.66

(46)

Matokeo haya pia yameonyeshwa kwa alama mbalimbali kama yafuatayo:

Alama A A- B+ B B- c+ C c- D+ D D- E

Shule

KG

7 8 2 4 2 ".) 0 0 0 0 0 0

MAR 4 2 2 4 2 2 4 4 0 0 0 0

RAP 13 3 2 2 1 2 1 0 0 0 0 0

ACORO 6 7 4 5 0 2 0 1 0 0 1 0

Jumla

30

20

10

15

5

9

5

5

0

0

1

0

Matokeo ya utafiti yalibaini kwamba, kati ya wanafunzi 100, wanafunzi 80 walipita

vizuri, 9 walikuwa na alama za wastani na 11 walipata alama za chini. Katika kitengo

hiki, wanafunzi wana ujuzi wa hali ya juu ya lugha yaani wana umilisi bora wa lugha.

Burke (1966), anaeleza kuwa kila mtoto anazaliwa na uwezo wa kupata lugha yoyote

kimiujiza kwa urahisi na kwa kasi mno. Si kwa kuwekewa masharti au kupewa

vishawishi, kwamba kwa kutafsiri usemi anaokumbana nao baadaye anakuwa mweledi.

Wanafunzi hawa hujipata katika mazingira ambapo wao huzungumza na kuandika kwa

Kiswahili kila wakati. Zifuatazo ni baadhi ya sifa za wanafunzi katika kiwango hiki:

1. Wanafunzi wana uelewa wa hali ya juu wa lugha husika, Chomsky (1965), anaeleza

kuwa Saruf Zalishi (SZ) inaeleza tungo zote ambazo zinaweza kuzalishwa katika lugha

fulani, Wanafunzi waliweza kudhihirisha kwa kuzalisha sentensi tofauti tofauti. Katika sw.

la 17 la kueleza aina za sentensi, mwanafunzi 67 alitunga sentensi sahili kuwa; Mama

analima. Scntensi ambatano kuwa; Baba anakula huku Maria anatazama runinga.

Sentensi changamano kuwa; Ng'ombe aliyepotea amepatikana.

11. Wanafunzi wana uwezo wa kutumia miundo tofauti tofauti ya tungo. Wanafunzi

waliweza kubainisha aina za maneno katika sentensi. Finch (2003), anaeleza kwamba

(47)

aina za maneno. Pili, uwezo huo umo ndanil ubongoni. Kwa mfano, katika swali la 14

(kiambatisho

La! Uwanja wa

C); Bainisha aina za maneno katika sentensi hii;

maji sana

I

N

v

kuchezea kandanda umelowa

T N T N E

(2.2) Jedwali: Lo! Uwanja wa Kuchezea Kandanda Umelowa Maji

Alama Utukiaji Asilimia

2 2

2 2

3 3

9 9

13 13

19 19

36 36

17 17

100 100

o

1.5

2

2.5

3

3.5

4

Jumla

Katika jedwali hili, asilimia 36 ya wanafunzi walipata alama tatu na nusu, asilimia kumi

na saba ndio waliopata alama zote nne. Hata hivyo, kuna asilimia mbili pekee ambao

hawakupata jibu sahihi dhihirisho kuwa viwango ni tofauti. Asilimia 84 walipita ilhali

16% pekee ndio walioanguka.

Ill. Ni wale walio na ubunifu mkubwa katika matumizi ya lugha. Mhimili wa kwanza

unasema kuwa SZ hunuia kueleza uwezo au umilisi wa mzawa wa lugha. Kulingana na

Dell (1962), umilisi kamili huonyeshwa kwa ubunifu mkubwa katika matumizi ya lugha.

(48)

(2.3) Kielelezo cha Kurekebisha Sentensi. Rekebisha sentensi ifuatayo;

---Waya yangu imepotea

13

• Nunge

• Mbili

87

Katika swali hili 87% walipata jibu sahihi. Asilimia 13 wakakosa jibu. Kwa mfano, wengi

walipata jibu kuwa; Waya wangu umepotea.

IV. Wana ujuzi wa sheria zinazotawala lugha husika. Chomsky (1965), umilisi ni mfumo wa

sheria za lugha, unaeleza ujuzi wa sheria. Kwa mfano, hali ya umoja na wingi,

mnyambuliko wa vitenzi na kadhalika. Kwa mfano, katika swali la 15 (kiambatisho c),

majibu yalikuwa hivi;

(2.4) Kielelezo katika Jedwali: Kuandika kwa Umoja

Miche hii ni mizuri sana, itafaa

100

90

80 .~ 70

.2 60

IU

s:: 50

;

!:

.

40 I

!Q 30 ~

IU 20 :E 10

1

o

~~---~----~--~---87 .Idadi 9 3 1

o

1 1.5 2

Alama

Katika swali hili wanafunzi 87% walipata alama zote mbili ilhali 9% hawakupata jibu

sahihi.

(49)

Awe na uwezo wa kufasiri baadhi ya semi kuwa na usarifu japo hajawahi kuzisikia

hapo awali. Katika kategoria hii, ni wale ambao kulingana na Berko (1958):

a. Hawajaathiriwa na vigezo visivyofaa kisarufi. Kwa mfano, swali la 13 (iii) Rekebisha

sentensi hii: Humu ndio natokapo. Wengi wao walipata jibu kuwa; Humu ndimo

natokamo au Hapa ndipo natokapo. 56% walipata alama zote, 28% wakapata alama

mojana nusu na 16% wakapata alama moja.

b. Berko aliongezea kuwa wazungumzaji wenye umilisi wa juu ni wale hawajaathiriwa

na vikwazo vya kumbukumbu. Wanafunzi wengi waliweza kukumbuka mada zote

walizofundishwa siku moja, mbili au wiki moja au mbili zilizotangulia. Wanafunzi

wana uwezo wa kukumbuka kanuni na sheria za lugha ya Kiswahili.

c. Kigezo kingine ni kutomakinika darasani. Wanafunzi kuwa na usikivu wa hali ya juu

ndiposa waweze kuelewa na kukumbuka mafunzo. Kwa mfano, katika swali la 10; Je,

unawcza kukumbuka mada ulizofundishwa jana--- juzi ---- wild i1iyopita?----

-Majibu yao yalionyesha kuwa wengi waliweza kukumbuka waliyofundishwa hata

wiki iliyopita. Kwa mfano, mwanafunzi na. 67 alijibu; Jana- Aina za nyimbo, juzi

-Shairi, Wiki i1iyopita - Muhtasari.

d. Wanafunzi hawa pia hawajaathiriwa na kuhamisha uzingativu na matarajio yao. Kuna

wale wanafunzi ambao hawawezi kutulia katika somo kwa saa moja au mbili

mfululizo. Wakati mwingine wao hukinai somo hila na kufunga bongo zao.

VI. lsitoshe, wanafunzi katika kiwango hiki ni wale wanaoweza kudondoa sentensi

ambazo si sahihi na zile ambazo ni sahihi katika lugha husika. Kwa mfano, swali la 13

(ii) Rekebisha sentensi: Chumvi kiko katika mezani. Matokeo ya utafiti

yalionyesha kuwa asilimia 70 waliweza kupata alama zote mbili. Walidondoa kosa la

(50)

vii. Waliweza kutambua utata katika baadhi ya sentensi husika. Kwa mfano, katika swali la 14

la kubainisha aina za maneno katika sentensi, waliweza kubaini neno Lo! Kuwa ni

kihisishi.

Vlll. Kulingana na uchunguzi alioufanya Cazden (1967), miongoni mwa watoto Wanegro, anadai

kuwa watoto wa tabaka la juu huwa na umilisi wa lugha zaidi ya wale wa tabaka la chini.

Aghalabu umilisi huu hupatikana hasa watoto wanapovunja ungo ama wanapobaleghe.

Wakati huu huwapata watoto wengi wakiwa katika shule za upili kwa hivyo wao hujenga

umilisi wa hali ya juu.

IX. Watoto wanaozaliwa katika familia za uwililugha au wingi lugha pia huwa na nafasi nzuri ya

kuwa na umilisi bora kuliko wanafunzi wengine (Cazden, 1967). Wanafunzi wengi waliojaza

hojaji walikuwa katika kiwango hiki kama inavyoonyeshwa katikajedwaii hili;

(2.5) Alama za Wanafunzi katika Viwango vya Umilisi

Shule Umilisi wajuu Umilisi kiasi Umilisi hafifu

Ala. kati ya 20-30 Alama 15 -19 Alama 01 -14

Kisumu Girls (%) 88% 8 3.8

Agoro sare (%) 88 8 4

Rapogi H. (%) 84 12 4

Maranda (%) 84 12 4

Matokeo yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi walipata zaidi ya 84%.

2.1.2 Umilisi Kiasi

Hawa ni wanafunzi ambao walidhihirisha umilisi wa wastani yaam umilisi wao 111

wastani. Walionyesha sifa zifuatazo;

I. Katika kiwango hiki, wanafunzi walipata alama kati ya 15 - 19 juu ya alama 30

11. Katika kiwango hiki, wanafunzi wanaweza kutazama na kuelewa kanuni za kiisimu lakini

(51)

anaeleza kuwa katika kila kiwango cha uwezo kutakuwa na tofauti katika matokeo

ambayo huweza kuelezwa kwa sababu tofauti tofauti.

Ill. Uelewa wa wanafunzi huwa wa kiasi tu. Kwa mfano, waliweza kutambua aina mbili za

sentensi na kueleza vizuri lakini wakashindwa kueleza aina ya tatu.

IV. Ubunifu wao ni wa kiwango cha wastani. Kwa mfano, katika kuandika aina za sentensi,

baadhi yao walishindwa kutunga sentensi changamano. Asilimia 64 walipata aina zote

tatu za sentensi, 20% walipata alama za wastani na 16% walipata alama mbili pekee.

v. Wanafunzi hujifunza kwa kukariri, baadaye wanakuwa na mazoea. Kwa mfano, baadhi

ya wanafunzi waliandika aina za maneno kwa maneno wala sin kwa ishara. Kwa mfano,

mwanafunzi na. 58 aliandika, Lo!- kihisishi, uwanja- nomino, wa- kivumishi,

kuchezea- kitenzi, kandanda- nomino, umelowa- kitenzi, maji- nomino na s

ana-kielezi,

VI. Wanafunzi wana uwezo wa kutumia baadhi ya sheria za lugha. Leech (1974), alisisitiza

umilisi wa sheria za lugha. Kwa mfano, kuandika hali ya umoja ya sentensi. Waliweza

kubainisha aina za maneno katika sentensi. Kwa mfano, asilimia tatu za wanafunzi

walipata alama moja na nusu katika swali 15 katika kielelezo (2.4). Katika swali la 14

asilimia tisa walipata alama mbili na asilimia kumi na tatu walipata alama mbili na nusu

kama ilivyo katika kielelezo (2.2).

VII. Huweza kukumbuka mada walizofundishwa katika siku chache kama siku mbili

zilizopita,

2.1.3 Umilisi Haflfu

Hiki ni kiwango cha umilisi mdogo wa mzungumzaji wa lugha husika. Wanafunzi walio

na umilisi hafifu walionyesha sifa zifuatazo;

1. Katika kiwango hiki, wanafunzi wana uelewa mdogo sana wa lugha. Kwa rnfano; wengi

(52)

11. Hawa walipata alama kati ya 0- 14 juu ya jurnla ya alama 30.

111. Wanafunzi hawana ubunifu wa kutosha kwani wana makosa ya kufanya tafsiri si si si.

Kwa mfano, katika jedwali (2.4) 13% walikosa jibu. Wengi walipendelea kuandika

majibu yao katika ngeli ya I-ZI. Asilimia 27 walikuwa na kosa la kutozingatia nge1i.

IV. Kutoweza kutumia miundo tofauti tofauti ya tungo. Walivuruga muundo wa sentensi.

Kwa mfano, katika swali la 12,wengine walitoajibu lifuatalo; Ng'ombe yule alizalishwa

ndama mkubwa jana badala ya Ndama mkubwa alizaliwajana na ng'ombe yule.

v. Kutozingatia baadhi ya sheria zinazotawala lugha. Katika sw. "la 12 (ii), wengine walitoa

jibu kama; Mavu hawa wamemsumbuliwa Nyatoge kwa muda mrefu sana.

VI. Kukosa kudondoa sentensi ambazo si sahihi na zile ambazo ni sahihi. Kwa mfano, katika

sw 13 (ii), asilimia 13 walipata sufuri. Taz. Jedwali la (2.3).

2.2 Viwango vya Utendaji

Utendaji ni utumiaji wa ule uwezo wa kiisimu katika muktadha halisi. Kulingana na

Bloomfield (1927), anaamini kuwa kuna viwango tofauti tofauti katika umilisi na utendaji

baina ya wanajamii lugha moja. Anaeleza kuwa viwango vya utendaji huathiriwa sana na

hali ya kijamii. Kategoria hii imegawanywa katika viwango viwili ambavyo ni; utendaji

wa juu na utendaji kiasi. Matokeo ya wanafunzi waliohojiwa yalionyesha kuwa wanafunzi

wengi walijua kuzungumza na kuandika vizuri kwa Kiswahili. Pia walidhihirisha umilisi

wao wa lugha katika majibu waliyotoa. Kuna vigezo kadhaa ambavyo vinadhihirisha

viwango vya utendaji kama vile:

1. Wanafunzi wanaweza kudhihirisha umilisi wao wa lugha katika utendaji.

11. Alama za wanafunzi katika hojaji zilitumiwa kuonyesha viwango vya utendaji ..

111. Utendaji humwezesha mzungumzajr kubadilisha tungo na kuzitumia vilivyo kutoka

mtindo mmoja hadi mwingine.

References

Related documents

Since most of the work related to traffic and transportation planning requires an effective framework for the analysis of the present and future travel demand pattern, a model

The proportion of eyed beans is somewhat too large to result from two recessive factors and too small t o result from a single factor, but other- wise the theoretical

I n Petunia the cells of the white area are much smaller than the colored cells in the center of the purple spot. The light purple cells are intermediate as to their sizes between

Following the collection of the first harvests the F1 plants were again selfed and then all of the leaves and side branches were removed so that second harvests of seed were

was  utilized  to  evaluate  professional  development  manuscripts,  collected  based  on  their   focus  of  professional  development  for  community

In image analysis technique textures of liquid crystal complexes are captured from the solid phase of the sample to the isotropic phase using POM and the changes in

The full load performance with VGT was compared with the case of mechanically controlled waste-gated turbocharger, so that the potential for a higher Brake Mean

In our examination, we have tried different inside and outside releases like void, surface and crown utilizing factual parameters, for example, skewness and