• No results found

Matatizo katika ujifunzaji wa silabi za kiswahili katika shule za upili wilayani Rarieda, Kaunti ya Siaya

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Matatizo katika ujifunzaji wa silabi za kiswahili katika shule za upili wilayani Rarieda, Kaunti ya Siaya"

Copied!
123
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

NA

MOSES JARED OWINO

TASNIFU IDI IMETOLEW A KW A MADHUMUNI YA KUTOSHELEZA

MAIDTAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATlKA CHUO KIKUU CHA

KENYATTA

APRILI2016

(2)

11

UNGAMO

Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika chuo kikuu kingine.

..

dj~

2zlolfJ

~016

Sahihi: Tarehe: .

MOSES JARED OWINO C50lCE/26291/20 11

Tasnifu hii imetolewa kwa Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa idhini yetu kama wasimamizi.

Sahihi: ~ Tarehe:

~~(:?.'t.f.&.9lb.

OKT. L.M. CHACHA

CHUO KIKUU CHA KENYATTA

IDARA Y A KISW AHlLI NA LUGHA ZA KIAFRlKA

Sahihi: ..~ Tarehe: ~~ ..Q.lt·I·.l·~···.

MWL. MUDHUNE E. S.

CHUO KfKUU CRA KENY ATTA

(3)

TABARUKU

(4)

IV

SHUlmAN I

Namshukuru Mola aliyeniwezesha kufanya kazi hii. Ningependa pia kuwapa shukrani za dhati wasimamizi wangu, Dkt. Leonard Mwita Chacha na Mwl. Everlyne Mudhune. Miongozo yao yenye busara iliniwezesha kukamilisha kazi hii. Nawashukuru vilevile wahadhiri wote katika ldara ya Kiswali na Lugha zaKiafrika kwa ushauri wao wa dhati tangu mwanzo wa shahada yangu ya uzamili.

(5)

lKISIRI

Utafiti huu ulilenga kubaini iwapo wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda wana matatizo katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili. Dhana ya silabi imefanyiwa utafiti na watafiti pamoja na wasomi mbalimbali. Utafiti huu hivyo basi umechangia kwa maarifa yaliyotafitiwa. Tulitumia nadharia ya lugha kadirifu (Selinker 1972) na nadharia ya silabi ya KV (Clements na Keyser 1983). Data ilikusanywa kwa kuwashirikisha walimu na wanafunzi kujaza fomu za hojaji kuhusu silabi. Vilevile wengine walishirikishwa katika mahojiano ya moja kwa moja yaliyolenga aina na miundo ya silabi za Kiswahilli. Mazungumzo ya wanafunzi pia yalisikilizwa ili kubaini namna matamshi ya baadhi yao yanavyodhihirisha miundo ya silabi za Kiswahili wanazounda. Aidha vitabu kuhusu nadharia ya lugha kadirifu na silabi ya KV vilisomwa maktabani na makala mengine kusornwa kwenye tovuti. Shule na wanafunzi walioshirikishwa ziliteuliwa kutumia mtindo wa sampuli za kimaksudi. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa misingi na mihimili ya nadharia ya lugha kadirifu na nadharia ya silabi ya KV. Utafiti wetu ulibaini kuwa baadhi ya wanafunzi wa Kiswahili wanaozungumza Dholuo kama L1 wanatatizwa katika rnatamshi ya silabi za Kiswahili kutokana na tofauti za miundo ya silabi kati ya Dholuo na Kiswahili. Matatizo haya husababisha matamshi yasiyo sahihi ya maneno, makosa ya hijai katika maandishi na utata katika maana ya baadhi ya maneno hayo. Matokeo ya utafiti mzima yaliwasilishwa kwa maelezo. Utafiti huu uliazimia kuwafaa wanafunzi wanaozungumza lugha mbalimbali za kwanza, wanaojifunza lugha ya Kiswahili kwa jumla, ikizingatiwa kwamba silabi ni kipashio muhimu sana katika muundo wa lugha.

(6)

VI

ABSTRACT

TITLE: THE DIFFICULTIES IN THE LEARNING OF SWAHILI SYLLABLES IN SECONDARY SCHOOLS IN RARIEDA DISTR[CT, SIA VA COUNTY

This research study aimed at establishing whether secondary school students in Rarieda District have difficulties in learning Swahili syllables. Various scholars and researchers have done research and published about the concept of the syllable. This research therefore has given contribution to the already established knowledge. The research was conducted based on the theoritical framework of the Interlanguage theory (Selinker 1972) and the CV phonology theory (Clements and Keyser 1983). Data was collected from teachers and students by use of questionnaire, interviews and participatory field observation. Stuctures of Swahili syllables were the main target by the researcher by listening to the conversations of the students as they spoke Swahili. The library and internet were also useful in reading about Interlanguage theory, CV phonology theory and other literature on the syllable. Schools and the students who took part in the reseach were chosen using probability sampling technique. The data collected was analysed based on the foundations of Interlanguage theory and the CV phonology theory, followed by descriptive presentation of the results. The results of our research study showed that some of the Swahili students who speak Dholuo as L1 have difficulties in learning Swahili syllables due to the difference syllable structure between Dholuo and Swahili. The difficulties were seen to affect pronunciation in speaking, spelling in writing and meaning of words. This research study is useful to students of various first languages backgrounds learning Swahili as a second language as well as to linguists in dealing with the syllable and second language learning.

(7)

$ #

o

.cr K· K1 KKKV KKV KMS KO KS1L KV KVK

L1

L2

LE-LK

MW

RMC

S

T

V VK

VIFUPJSHO NA ISHARA Mpaka wa silabi

Mpaka wa neno Kapa

Rusu silabi Konsonanti Kilele

Konsonanti, Konsonani, Konsonanti, Vokali Konsonanti, Konsonanti, Vokali

Kanuni za Muundo Silabi Koda

Kamusi Sanifu ya lsimu na Lugha Konsonanti, Vokali

Konsonanti, Vokali, Konsonanti Lugha ya kwanza

Lugha ya pili Kilele

Lugha Kadirifu Mwanzo

Rarieda Mock Committee Silabi

Vokali

(8)

VIII

ISTILAHI MUHIMU

Fonimu: Kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachobadili maana ya neno.

Lugha ya pili: Lugha yoyote anayojifunza mtu na kuitumia kuongezea kwa lugha ya kwanza.

Lugha ya kwanza: Lugha aipatayo mtu anapozaliwa na kuanza kuitumia katika mawasiliano.

Ruwaza: Sampuli:

Mpangilio maalumu wa sauti katika lugha.

Idadi ndogo ya walengwa inayoteuliwa kwa utafiti kuwakilisha walengwa wote.

Kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti au muungano wa sauti hutamkwa kama fungu moja.

(9)

YALIYOMO

UNGAMO , ~ ii

TABARUKU ii

SHUKRANI iii

IIZlSIRI v

ABSTRACT vi

ORODHA YA VIFUPISHO NA ISHARA vii

ISTILAHT MUHlMU viii

Y ALIYOMO ix

ORODHA YA VIELELEZO xiii

SURA YA I(WANZA: UTANGULIZI 1

1.0Usuli wa mada I

1.0.1Ujifunzaji wa lugha I

1.0.2 Ujifunzaji wa fonolojia na silabi 2

1.1 Suala la utafiti 4

1.2 Malengo ya utafiti 5

1.3Maswali ya utafiti 5

1.4 Sababu za kuchagua mada : 6

1.5Upeo na mipaka 8

1.6 Yaliyoandikwa kuhusu mada 8

1.7 Misingi ya Nadharia 13

1.7.1 Nadharia ya Lugha kacliri fu 13

(10)

x

1.8Mbinu za utafiti 20

1.8.1 Eneo la Utafiti 21

1.8.2 Mbinu za Ukusanyaji Data : 21

1.8.2.1 Mahojiano 22

1.8.2.2 Hojaji 23·

1-.8.2.3 Uchunzaji · 23

1.8.3 Usampulishaji 24

1.8.4 Uchanganuzi wa Data 26

1.8.5 Uwasilishaji wa Matokeo ~7

1.9 Muhtasari 28

SURA YA PILI: MATATIZO KATlKA UJIFUNZAJI WA SILABI ZA

KISW AHILI 28

2.0 Utangulizi 29

2.l Dhana ya silabi 29

2.2 Dhima ya silabi 31

2.3 Uwakilishaj iwa silabi 34

2.4 Silabi za Kiswahili 35

2.4.1 Miundo ya silabi za Kiswahili 36

2.4.2 Aina za silabi za Kiswahi li .41

2.5 Si1abi za Dholuo 43

2.5.1 Miundo ya silabi za Dholuo .43

2.5.2 Aina za silabi za Dholuo 49

2.6 Muhtasari : 51

SURA YA TATU: MIUNDO YA SILABI ISIYO SAHIHI : S2

(11)

3.1 Uchopekaji wa vokali mwanzoni mwa neno 53

3.1.1 Uchopekaji wa vokali lul mwanzoni mwa neno 53

3.1.2 Uchopekaji wa vokali awali Iii 56

3.1.3 Uchopekaji wa vokali lul kwenye silabi 60

3.1.4 Uchopekaji wa vokali Iii katikati ya neno 62

3.2Udondoshaji wa vokali 68

3.2.1 Udondoshaji wa vokali katikati mwa neno 69

3.2.2 Udondoshaji wa vokali tamati katika neno 72

3.3 Udondoshaji wa konsonanti 74

3.3.1 Udondoshaji wa konsonanti I1n/

75

3.3.2 Udondoshaji wa konsonanti Ih/ 77

3.4 Muhtasari : 80

SURA YA NNE: ATHARI ZA MATATIZO KATIKA UJIFUNZAJI WA SILABL81

4.0 Utangulizi 81

4.1 Maendelezo mabaya ya maneno katika maandishi 81

4.2 Matamshi yasiyo sahihi 83

4.3 Utata katika rnaana 87

4.4 Muhtasari 89

SURA YA TANO: IIITIMISI-.lO 90

5.0 Utangulizi 90

5.1 Utaratibu wa

Uchanganuzi

92

5.2 Matokeo ya Utafiti 94

5.3 Mahitimisho ya Utafiti 98

(12)

XII

5.5 Tamati 99

Marejeleo 100

Kiambatisho i:Fomu ya Hojaji 106

Kiambatisho ii: Maswali ya kuongoza Mahojiano 109

(13)

ORODHA YA VIELELEZO

Kielelezo I: Uhusiano wa konsonanti na vokali katika silabi kwa rusu 19

Kielelezo 2: Uwakilishaji silabi kwa rusu (silabi ya KV) 35

Kielelezo 3: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa KV 36

Kielelezo 4: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa V 36

Kielelezo 5: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa K kwa matawi. 37

Kielelezo 6: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa KKV kwa matawi 39

Kielelezo 7: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa KKKV kwa matawi 39

Kielelezo 8: Uwaki1ishaji wa silabi ya muundo wa KVK kwa matawi 41

Kielelezo 9: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa VK kwa matawi .40 Kiele1ezo 10: Uwakilishaji wa muundo wa KVK kwa matawi .45

Kielelezo 11: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa KV kwa matawi 46

Kielelezo 12: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa V kwa matawi .47

Kielelezo 13: Uwakilishaji wa silabi za muundo wa VK kwa kielelzo matawi 47

Kielelezo 14: Muundo wa silabi yenye kilele cha vokali mbili 48

Kiele1ezo 15: Uchopekaji wa vokali awali lul katika neno #m$bu# 55 Kielelezo 16: Uchopekaji wa silabi awali lul katika neno #m$bwa# 55 Kielelezo 17: Uchopekaj iwa vokali awali Iii katika neno 'nchi' kuwa 'inji' 57 Kielelezo 18: Uchopekaji wa vokali awali lul katika neno #mwananchi# kuwa 59

Kielelezo 19: Uchopekaji wa vokali tamati Ilil katika neno 'mmemwacha' kuwa 61

(14)

XIV

Kielelezo 22: Uchopekaji wa vokali tamati Iii kwenye neno 'skrubu' kuwa 'sikurubu' 66 Kielelezo 23: Uchopekaji wa vokali tamati Iii kwenye neno 'daktari' kuwa "dakitari' 67 Kielelezo 24: Udondoshaji wa vokali ya katikati Iii kwenye neno 'badilisha' kuwa 71

Kielelezo 25: Udondoshaji wa fonirnu lul katika neno 'rnakamu' na kuwa 'rnakam ' 73

Kielelezo 26: Udondoshaji wa fonimu Iml katika neno 'mvua' kuwa 'vua' 77

Kielelezo 27: Udondoshaji wa konsonanti Ihl kwenye neno 'harufu' na kuwa 'arufu' 79

(15)

1.0 Usuli wa mada

Ujifunzaji wa silabi za Kiswahili ni sehemu ya ujifunzaji mzima wa lugha ya Kiswahili, Ujifunzaji wa lugha unahusiana na lugha ya pili kwani mtu hupata lugha ya kwanza nayo ya pili anajifunza. Katika mchakato wa ujifunzaji wa lugha ya pili mwanafunzi huweza kukumbana na matatizo kutokana na tofauti zilizopo kati ya ruwaza za Ll na L2. Hivyo basi, katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahli wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama LI huweza kukumbana na matatizo kutokana na tofauti za miundo kati ya silabi za lugha hizo mbili,

1.0.1 Ujifunzaji wa lugha

Lugha ni mfumo wa maumbo ya sauti, ambao huwasilisha maana huku ukifuata kanuni bayana za sarufi (Buliba na wenzake 2006). Watoto hupata ruwaza za lugha ya kwanza akilini na kutokana na ujuzi huu wanaweza kuunda na kutumia maumbo sahihi. Kila binadamu hupata ujuzi wa Ll anapozaliwa na kukaa katika jamii yake na ana uwezo wa kujifunza lugha ya pili. Chomsky (\959) anasema kwamba kila binadamu ana ujuzi jumulifu wa lugha. Watoto hujifunza lugha ya kwanza kwa kuunda kanuni za narnna lugha

(16)

2

Ujifunzaji wa L2 unahitaji maelekezo rasmi katika muktadha wa kiusomi, kutagusana nayo nje ya muktadha huo na mazoezi yanayozingatia stadi zote za lugha ili kupata ruwaza

mpya (Garza 2008). Hivyo basi, mwanafunzi huweza kurejelea tajiriba na ujuzi wake wa

sifa na mifumo ya L1 ili kupata ujuzi wa L2. Kwa mujibu wa Lado (1957), wanafunzi

huweza kuwa na athari ya kuhamisha miundo ya L1 hadi L2 na kuhamisha huku

hudhihirika mwanafunzi anapojaribu kuongea lugha ya pili. Athari hutegemea mfanano au

tofauti za miundo ya lugha hizo mbili. Mwanafunzi hivyo basi anastahili kuelewa namna

ya kuhusisha ujuzi mpya wa L2 na ujuzi wa awali wa L1 hatua kwa hatua ili kuunda

maumbo sahihi ya lugha ya pili. Ujifunzaji wa lugha unajumuisha ujuzi wa fonetiki,

fonolojia, mofolojia na sintaksia yake. Utafiti huu ulilenga ujifunzaji wa silabi za Kiswahili, kipashio cha kifonolojia.

1.0.2 Ujifunzaji wa fonolojia na silabi

Fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza na kuchanganua mfumo wa sauti katika lugha

(Yule 1985). Kila mtu mjua lugha fulani ana umilisi wa ruwaza za sauti za lugha hiyo

akilini mwake na ndipo anaweza kutamka maneno ipasavyo anapozungumza. Fonolojia

huchunguza ruwaza za sauti katika lugha mahususi, kuziorodhesha sauti hizo na kuangalia zinavyoungana kuunda vipashio vikubwa. Katika ujifunzaji wa fonolojia ya lugha

mahususi, mwanafunzi anajifunza mfumo wa sauti za lugha hiyo kwa kiasi kwamba aweze

kufahamu namna sauti hizo zinavyoungana kuunda silabi, kisha maneno. Hii ni kwa

(17)

Fonolojia ina matawi mawili: fonolojia vipande sauti na fonolojia arudhi. Suala la miundo

ya silabi hushughulikiwa katika fonolojia vipande sauti. Fonolojia inahusisha kuchunguza

na kuorodhesha idadi ya fonimu katika lugha mahususi na namna zinavyotamkwa (Buliba

na wenzake 2006). Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachobadili maana

ya neno (TUKI 1990). Katika uzungumzaji wa lugha watu hutamka maneno na hivyo basi,

fonolojia inajihusisha na mpangilio wa sauti unaokubalika katika lugha fulani kuunda

silabi za maneno.

Silabi ina dhima kuu katika ujifunzaji wa L2 kwani mwanafunzi wa L2 anastahili kumudu

silabi zake kwa vile kuongea lugha kunahusisha kutamka silabi zake katika maneno.

Ujifunzaji wa silabi za lugha hivyo basi unahusu mwanafunzi kujifunza umilisi wa

utamkaji wa miundo sahihi ya silabi hizo. Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu

matamshi ambacho kwacho sauti au muungano wa sauti hutamkwa kama fungu moja

(Massamba 2006). Sauti za lugha zina uhusiano wa kuweza kufuatana kuunda silabi

ingawa kila lugha ina mfumo wa namna sauti zake zinavyoungana kuunda silabi. Mtu

anapojifunza lugha ya pili, umilisi wa ruwaza zake katika mchakato wa kuunganisha sauti

kuunda silabi zinazokubalika ni muhimu. La sivyo mwanafunzi wa L2 ataunda miungano

ya silabi na kisha maneno yasiyo sahihi.

Silabi huweza kuwa wazi au funge. Dholuo ni lugba ya Kinailoti iliyo na silabi funge

(18)

4

Katika wilaya ya Rarieda, wanafunzi wengi wanazungumza Dholuo kama L1. Hivyo basi, kuna uwezekano wa kuwa na matatizo wanapojifunza Kiswahili kama L2, hasa wanapozungumza kwa sababu ya tofauti hizi za silabi.

1.1 Suala la utafiti

Wanyoike (1978) anaeleza kwamba wanailoti hukumbwa na matatizo wanapojifunza Kiswahili sanifu. Dholuo ni lugha ya Kinailoti. Tatiti za awali zinazohusisha Dholuo na Kiswahili zimeonyesha kujitokeza kwa makosa katika viwango tofauti tofauti kama

f

o

n

%

jia

j

mof%jia

na

s

intak

s

ia

wanafunzi

wanapojifunza

Kiswahili

.

Makosa

bado yanajitokeza licha ya baadhi ya mapendekezo kutekelezwa. Kuna uwezekano wa kuwepo kwa tatizo la kifonolojia ambalo laweza kuwa linahusu silabi na hasa kutokana na tofauti za silabi za Dholuo ambayo ni lugha ya Kinailoti na za Kiswahili ambayo ni lugha ya Kibantu. Nia ya utafiti huu ilikuwa kuchunguza iwapo tatizo hili lipo, kiwango chake na athari yake kwa Kiswahili sanifu.

Kutokana na Ripoti ya Kamati ya Mwigo ya Wilaya ya Rarieda iRarieda Mock Comittee) (2013), wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mtihani wa mwigo walionyesha udhaifu katika karatasi ya kwanza na ya pili katika Kiswahili. Maendelezo ya baadhi ya maneno hayakuwa sahihi kwani miundo ya silabi ilivurugwa. Suala hili lilistahili kuchunguzwa ili kuboresha kiwango cha Kiswahili katika eneo hili. Hili ni suala muhimu kwa sababu Kiswahili ni Lugha ya Taifa na Lugha Rasmi nchini Kenya. Vilevile Kiswahili ni somo la lazima katika shule za upili na hivyo kukuza ujuzi wake nijambo linalohitaji umakini sana (Apopo20.1 0).

(19)

1.2Malengo ya utafiti

Kwa ujumla, utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo:

l. Kubainisha matatizo ya wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda katika ujifunzaji

wa silabi za Kiswahili wanapozungumza na kuandika.

2. Kutambua kiwango cha makosa ya miundo ya silabi za Kiswahili na wanafunzi hawa wa

Dholuo kama L1 katika kuzungumza na kuandika Kiswahili.

3. Kutathmini athari ya matatizo ya ujifunzaji wa silabi za Kiswahili miongoni mwa

wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda katika matumizi ya Kiswahili.

Kwa mujibu wa malengo haya utafiti ulinuia kujibu maswali kadha kuwezesha malengo

yote kufikiwa.

1.3 Maswali ya utafiti

Utafiti huu uliongozwa na maswali yafuatayo:

1. Ni matatizo yapi waliyonayo wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda katika

ujifunzaji wa silabi za Kiswahili?

2. Wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda huzua miundo rpi ya silabi

wanapozungumza na kuandika Kiswahili?

3. Matatizo wanayopata wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda katika ujifunzaji

(20)

6

1.4 Sababu za kuchagua mada

Tafiti ambazo zimefanywa kuhusiana na Kiswahili na lugha za kijamii zimelenga maneno

mkopo ya Kiswahili katika lugha hizo, makosa ya kisaruf yanayofanywa na wanafunzi katika Kiswahili, sintaksia na fonolojia ya Kiswahili na ujifunzaji wa aina za maneno kama

vile nomino, vibainishi, vivumishi na vitenzi. Nafasi ya silabi katika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 haijazingatiwa na tafiti hizi. Utafiti huu kwa hivyo umeziba pengo hili kwa kulenga ujifunzaji wa silabi za Kiswahili na wanafunzi wanaozungurnza Dholuo kama Ll katika wilaya ya Rarieda.

Wanafunzi wengi wa shule za upili nchini Kenya hujifunza Kiswahili kama L2 kwani wengi wao wanazungumza lugha za kijamii kama LJ. Purcell na Suter (\980), wakizungumzia ujifunzaji wa lugha ya pili, wanaserna kwamba ujifunzaji wake huathiriwa sana na muundo wa lugha ya kwanza. lkiwa miundo ya lugha hizi mbili inafanana, athari za Ll kwa L2 ni chanya na ikiwa ni tofauti ujifunzaji wa L2 hutatizwa na tajiriba za muundo wa lugha ya kwanza. Kwa vile utafiti huu ulilenga ujifunzaji wa silabi za Kiswahili na wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama L1, tulilenga miundo ya silabi za lugha hizi mbili kama ruwaza muhimu.

(21)

muundo wa silabi wa jumla wa KV kama zilivyo lugha zote, muundo wa KVK unapatikana katika silabi nyingi sana za maneno yake ikilinganishwa na Kiswahili. Katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili kuna uwezekano wa baadhi ya wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama Ll kuhamisha miundo ya silabi funge za Dholuo na kuichanganya kwenye silabi za Kiswahili ambazo ni wazi. Mojawapo ya malengo ya kufunza Kiswahili katika shule za upili ni kuwawezesha wanafunzi kutambua makosa yanayotokana na athari ya L1 na lugha nyingine katika kuzungumza na kuandika Kiswahili

(KNEe 2012). Utafiti huu ni muhimu kwani utawezesha wasomi na walimu wa Kiswahili kujua makosa na chanzo chake na hivyo basi kuwa rahisi kuyarekebisha.

(22)

8

1.5Upeo na mipaka

Utafiti huu ulilenga wilaya ya Rarieda ili kubaini iwapo wanafunzi wa shule za upili

wanaozungumza Dholuo kama

L

l

wana matatizo katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili.

Hii ni kwa kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda ni

wazungumzaji wa Dholuo kama L1. Maeneo mengine ya Nyanza panaweza kuwa na hali

kama hii ita Rarieda imepakana na wilaya ambazo wakazi wake asilia ni wazungumzaji wa

Dholuo (Bondo, Kisurnu, Gem). Maongezi ya wanafunzi yalilengwa zaidi kwa kuwa

mawasiliano hufanyika zaidi kwa maongezi.

Ujifunzaji wa silabi za Kiswahili katika shule za upili ni mojawapo ya masomo ya msingi

ambayo hufunzwa katika vipindi vya mwanzo katika kidato cha kwanza. Somo hili

huhusisha maana ya silabi na miundo ya silabi. Hivyo utafiti huu ulihusisha wanafunzi wa

kidato cha tatu ambao wamekwisha kupata umilisi wa kutosha wa Kiswahili.

Tuliwahusisha wanafunzi wa kidato cha tatu kwa sababu katika kiwango chao, wamesoma

Kiswahili kwa muda mrefu na hivyo basi, inatarajiwa kuwa wammepata umilisi wa

kutosha wa Kiswahili.

1.6 Yallyoandikwa kuhusu mada

Dhana ya siJabi na suala la ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 limeshughulikiwa na

wanaisimu pamoja na watafiti mbalimbali. Katamba (1989) anasema kuwa silabi ni

(23)

silabi inaweza kuwa mofimu, mofimu mbili, neno au hata fonimu. Katamba ameeleza

muundo wa ndani wa silabi. Silabi hugawanywa kwenye mwanzo na kina ambapo kina

huweza kuwa na kilele na koda. Anasema kuwa kilele huwa irabu iliyo katika silabi na

ndiyo sehemu muhimu zaidi katika silabi kwani silabi huweza kukosa mwanzo na koda

lakini kilele lazirna kiwepo. Vilevile ameangazia umuhimu wa silabi katika lugha pamoja

na usilabishaji. Jambo lingine alilojadili ni hatua za usilabishaji na aina za silabi.

Makosa ya wanafunzi wanapojifunza lugha ni muhimu sana kwa sababu humpa mtafiti

ushahidi kuhusu jinsi lugha inavyopokelewa au jinsi mtu hujifunza lugha. Katika kujifunza

L2, wanafunzi hukiuka kanuni za lugha hiyo (Corder 1981). Alipendekeza kuwa

kuwatahini wanafunzi huweka wazi makosa hayo. Utafiti huu unahusiana na kazi ya

Corder na Katamba kwa sababu unahusu matatizo katika ujifunzaji wa silabi kwa msingi

wa miundo ya silabi. Rata hivyo, upekee wa utafiti wetu ni kuwa ulilenga matatizo waliyo nayo wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda katika ujifunzaji wa silabi.

Hodne (1985) alichunguza miundo ya silabi za Kiingereza na wazungumzaji wa Kipolandi

kama LI. Katika utafiti wake alikusanya silabi za Kiingereza kwa kuwasikiliza wazungumzaji wenye asili ya Kipolandi. Matokeo ya utafiti wake yalionyesha kuwa

makosa katika miundo ya silabi za Kiingereza yalitokana na uhamishaji wa miundo ya

silabi za Kipolandi (Ll) hadi Kiingereza (L2). Utafiti wa Hodne (1985) unahusiana na

(24)

10

Wazungumzaji wa lugha fulani huweza kusilabisha upya maneno ya lugha ya pili wanapojifunza. Kazi ya Breslow (1983), inaonyesha makosa ya usilabishaji katika Kiingereza na wazungumzaji wa Kiarabu kama Ll. Wazungumzaji hawa walisilabisha upya maneno ya Kiingereza kulingana na muundo wa silabi za Kiarabu. Tafiti za Hodne (1985) na Breslow (1983) zinadhihirisha athari za miundo ya silabi za Ll kwa L2.

Mudhune (1994), Musau (1993) na Chepkwony (2011) walichunguza athari za Ll kwa L2. Tafiti zao zililenga kubaini matatizo ya wasemaji wa L1 za Kinailoti wanapojifunza kuzungumza Kiswahili kutokana na tofauti za Ll na L2. Mudhune (1994) alichunguza ujifunzaji wa mofosintaksia ya Kiswahili na wazungumzaji wa Dholuo huku Musau (1993) na Chepkwony (2011) wakizingatia fonolojia ya Kiswahili na matatizo ya Kiswahili sanifu mtawalia na wazungumzaji wa Kikipsigis. Utafiti huu unatofautiana na tafiti hizi ambazo zililenga ujifunzaji wa fonolojia kwa jumla na sarufi, kwa kulenga tu matatizo ya wanafunzi wa shule za upili katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili wilayani Rarieda, ambao ni wazungumzaji wa Dholuo. Rata hivyo, unahusiana na tafiti hizi kwa ambavyo unazingatia Dholuo ambayo ni lugha ya Kinailoti.

(25)

kubaini matatizo ya wanafunzi katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili. Lugha ya kwanza

ya wanafunzi hawa ni Dholuo, si Kinyala. Hata hivyo unahusiana kwa vile tafiti zote mbili

zinahusisha kulinganisha kanuni za lugha ya kwanza na lugha ya pili.

Karingi (2012) alichunguza ufunzaji na ujifunzaji wa vivumishi na vibainishi katika shule

za upili wilayani Kirinyaga. Alihusisha kategoria za maneno kwa mujibu wa sintaksia

finyizi. Lengo lake lilikuwa kubainisha mbinu za ufunzaji wa vivumishi na vibainishi,

kuchanganua matatizo wanayopata wanafunzi na walimu katika kujilunza na kufunza

vivumishi na vibainishi na kutathmini chanzo cha matatizo hayo. Ingawa utafiti wake

ulilenga ujifunzaji wa vipashio vya Kiswahili kama utafiti huu ulivyolenga, tofauti ni kuwa

utafiti wetu ulilenga tu matatizo ya wanafunzi katika ujifunzaji wa silabi. Vilevile wilaya

ya Rarieda iliteuliwa, tofauti na utafiti wa Karingi uliohusisha ya Kirinyaga.

Olal (2008) alibaini kuwa utohozi wa maneno ya Kiswahili katika Dholuo unafanikishwa

kwa udondoshaji wa silabi na uchopekaji wa fonimu. Utafiti wake ulilenga utohozi

fonolojia wa maneno- mkopo ya Dholuo kutoka Kiswahili. Alilinganisha aina na maumbo

ya silabi za Dholuo na za Kiswahili. Vilevile alichunguza usilabishaji wa maneno ya

Dholuo yaliyotoholewa kutoka lugha ya Kiswahili. Utafiti wake unahusiana kwa karibu na

utafiti huu kwa vile utafiti huu pia ulizingatia miundo ya silabi za Dholuo na za Kiswahili.

Rata hivyo unatofautiana kwa ambavyo utafiti huu ulilenga kubaini namna tofauti za

miundo ya silabi za Dholuo na za Kiswahili unavyoathiri ujifunzaji wa Kiswahili kama L2,

(26)

12

Utafiti wa Onditi (1994) ulihusu ujifunzaji wa kiulizi cha Kiingereza 'WH-' na wanafunzi

wa shule za upili wanaozungumza Dholuo kama Ll. Alibainisha kuwa wanafunzi hawa

waliathiriwa na mfanano wa maumbo ya Dholuo na ya Kiingereza. Tofauti ya utafiti huu

na wa Onditi (1994) ni kuwa utafiti huu unaweka msingi wake kwa tofauti za maumbo ya

silabi za Kiswahili na za Dholuo.

Nyamasyo (1985) alichunguza athari ya mazingira ya kiisimu kwa upataji wa sintaksia na

mtoto wa umri wa miaka minne aliyekuwa na msingi wa uwingi lugha (Dholuo, Kikamba,

Kiswahili na Kiingereza). Alibaini kuwa mtoto huyu alipata zaidi sintaksia ya Kiswahili

kuliko lugha zile nyingine kwa sababu Kiswahili ndiyo lugha aliyotagusana nayo zaidi.

Utafiti wa Nyamasyo (1985) unahusiana na huu kwa vile eneo la utafiti (Rarieda)

liliteuliwa kwa msingi wa Dholuo pekee kama Ll bila mtagusano na lugha nyingine hadi

wanafunzi wanapojifunza Kiswahili kama L2.

Tafiti na maandishi ambayo yametajwa yanaonyesha kuwa utafiti huu utaendeleza na

kuchangia katika juhudi za watafiti na wasomi kuhusu silabi na ujifunzaji wa lugha ya

Kiswahili kama L2. Tafiti hizi zimechunguza ujifunzaji wa vipashio mbalimbali vya

Kiswahili. Hata hivyo kuna pengo lililoachwa ambalo ni ujifunzaji wa silabi za Kiswahili

miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama LI. Kwa hivyo, ni tumaini letu

kwamba utafiti huu utaziba pengo hili kwa namna tumechunguza matatizo ya wanafunzi

(27)

1.7 Misingi ya Nadharia

Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili; nadharia ya lugha kaclirifu na naclharia zalishi ya

silabi ya KV. Nadharia ya lugha kadirifu ilitusaiclia kuonyesha namna ambavyo baaclhi ya

wanafunzi wa Kiswahili wanaozungumza Dholuo kama L1 wanavyotatizwa kujifunza

silabi za Kiswahili. Vilevile ilitusaidia kueleza namna wanafunzi hawa wanavyohamisha

miundo ya silabi kutoka Dholuo hadi Kiswahili na kupelekea kuunda maneno ya Kiswahili

yaliyo na miundo ya silabi isiyo sahihi. Nadharia zalishi ya rnuundo wa silabi ya KY

ilitusaidia kuwakilisha miundo ya silabi kwa rusu ili kuonyesha miundo sahihi ya silabi za

Kiswahili na miundo ya silabi isiyo sahihi kutokana na athari ya miundo ya silabi za

Dholuo kama LI.

1.7.1 Nadharia ya Lugha kadirifu

Nadharia bii iliasisiwa na Selinker (1972). Lugha kadirifu (LK) ni maumbo ya muda rnfupi

ya kisarufi yanayoundwa na wanafunzi wa L2. LK ni mfumo wa kiisimu unaojisimamia na

unatokana na juhudi za mwanafunzi kuzungumza L2. Ni ujuzi unaodhihirisha batua

badilifu za mchakato wa mwanafunzi wa L2 unaokua na kuwa changamani kwa rnpito wa

wakati. Maumbo ya LK yanajisimamia kwa sababu hayalingani na L1 au L2 ya

mwanafunzi. Kumpf (1982) anasema kwamba lugha kadirifu si mchanganyiko wa L I na

L2 ingawa kuna sifa za ama L1 au L2 au zote zinazoweza kudhihirika katika LK. Mfumo

(28)

14

Kwa mujibu wa Nemser (1971), lugha ya mwanafunzi hupitia viwango kadhaa kabla ya kufika kwenye ukamilifu wa ujuzi wa L2. Watu wanaojifunza L2 kila mara wanahamisha ruwaza za L1 kabla ya kupata umilisi kamili wa ruwaza za L2. Corder (1967) anasema kuwa LK ni mfumo katika lugha ya mwanafunzi na fasiri kuhusu mchakato wa ujifunzaji ambazo huweza kutolewa kwa kufafanua hatua zinazofuatana za lugha hiyo ya mwanafunzi. Muundo unaoibuka katika lugha ya mwanafunzi hutokea kwa sababu ya tofauti za miundo kati ya LI na L2. Maoni haya yalikuwa muhirnu sana katika utafiti huu kwa vile wanafunzi waliolengwa ni wazungumzaji wa Dholuo kama LI. Dholuo ni lugha ya Kinailoti na miundo ya silabi zake ni funge ikilinganishwa na lugha ya Kiswahili ambayo silabi zake ni wazi.

Lugha kadirifu huendelea kubadilika na kukaribia L2. Makosa katika L2 ni ithibati kuwa mwanafunzi anapanga ujuzi anaopata katika kipindi kinachohusika. Selinker (1972) anasema kwamba ujifunzaji wa L2 hukwama katika kiwango fulani. Hivyo LK huwa madhubuti. Katika kiwango hiki, mifumo fulani ya LI huhamishwa na kudumu katika L2. Maoni haya yalikuwa muhimu zaidi katika utafiti huu kwani tulinuia kubaini matatizo ya wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama Ll wanapojifunza silabi za Kiswahili kwa kuchunguza miundo isiyo sahihi wanayoibua na kutathmini athari yake kwa Kiswahili sanifu.

Kwa mujibu

.

wa Selinker (1972), LK hufikia kiwango madhubuti kwa hatua mbalimbali. .

(29)

midogo midogo ya Ll katika LK kuhusiana na L2 licha ya kuendelea na ujifunzaji zaidi wa L2. Mwanafunzi anaweza kujaribu kuzungumza L2 kwa ufasaha lakini atarejelea miundo madhubuti ya LK anapokabiliwa na masuala magumu kushughulikia akilini au akiwa na kiwewe, msisimko au katika hali ya mapumziko. Kiwango hiki madhubuti hufikiwa kwa sababu mwanafunzi anaweza kuwasiliana vizuri licha ya kuwa na makosa katika LK (Selinker 1992). Kwa msingi huu utafiti huu ulitumia mada za kuzua msisimko kwa wanafunzi wa kidato cha tatu wilayani Rarieda kama sherehe za Krismasi, siku ya kwanza shuleni ili kusikiliza matamshi yao ya silabi za Kiswahili.

Kwa mujibu wa Powell (1998), mwanafunzi wa L2 hufanya makadirio anavyosikia katika mchakato wa ufundishaji. Anatumia ujuzi wake wa L1 katika LK ingawa bade kuna uwezekano wa kuathiriwa na LK nyingine alizo nazo kutokana na ujifunzaji wa lugha nyingine. Hata hivyo LK haivunji mipaka au kanuni za lugha halisi za sarufi jumulifu. Hivyo basi, LK ni mchakato endelezi akilini mwa kila mwanafunzi. Powell (1998) na Garza (2008) wana maoni sawa kwamba ujifunzaji wa L2 huweza kutegernea tofauti za kibinafsi. Hivyo LK ya mwanafunzi mmoja huweza kuwa na tofauti kidogo na za wengine ingawa athari zajumla za L1 zinadhihirika.

Hatua za lugha kadirifu

(30)

16

1.Uhamishaji lugha. Katika hatua hii, mwanafunzi anafahamu vyema kuwa kuna mifumo

katika L2 lakini hana habari kuhusu mifumo hiyo. Kwa hivyo, vipengele au mifumo

midogo midogo hudumu katika lugha ya mwanafunzi kutokana na uhamishaji kutoka L1.

Hali hii vilevile inajumlisha kanuni za LI ambazo mwanafunzi anadumisha katika L2.

2. Ujumlishaji wa kanuni za L2. Mwanafunzi huanza kutambua mfumo fulani wa L2 na

kuanza kuzindua kanuni ambazo anazitumia kwajumla kuwasilisha maana katika L2.

Wanafunzi wa kidato cha tatu wamejifunza Kiswahili kwa muda mrefu tangu shule ya

msingi. Kwa hivyo, wanaelewa kanuni sahihi za fonolojia katika kiwango cha silabi.

Katika kiwango chao wana umilisi wa kutosha ingawa baadhi yao huenda wanajumlisha

kanuni za

Ll.

Hatua hizi mbili hivyo basi zilikuwa muhimu katika utafiti huu hasa kueleza

namna baadhi ya wanafunzi wanapohamisha kanuni za silabi za Dholuo na kuzijumlisha na

zile za Kiswahili katika ujifunzaji wao.

Utafiti huu ulichukulia kwamba wanafunzi hawa wanaozungumza Dholuo kama Ll

wametambua mfumo wa Kiswahili akilini mwao na baadhi ya silabi wanazozua katika

Kiswahili zinafuata kanuni zenye uhusiano na Ll. Mtazamo huu ulichukuliwa kwa msingi

wa mhimili wa pili. Kanuni hizi wanazozindua zenye uhusiano na Dholuo huenda ikawa

tatizo lao katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili kwani silabi za Dholuo ni funge

(31)

3. Uhamishaji wa mafunzo ya L2. Mwanafunzi wa L2 anaweza kuathirika na mbinu

zinazotumika katika ufundishaji wa L2. Hii huwezekana kwa mwanafunzi kuhamisha

vipengele vinavyotokana na mafunzo ya L2 anayopata. Kuna mitelezo zaidi ya makosa katika L2 anayojifunza. Hatua hii iliufaa utafiti huu kwa vile walimu watajaza hojaji ili kubaini ikiwa wan a matatizo yoyote katika ufundishaji wa silabi za Kiswahili. Habari hizi zilikuwa

muhirnu

katika kuandika ripoti ya matokeo ya utafiti.

4. Mikakati ya ujifunzaji. Katika hatua hii, mwanafunzi huweka mikakati ya ujifunzaji wa vipengele vya L2. Hatua hii humwezesha mwanafunzi kuzingatia kanuni imara zinazokaribiana na lugha anayojifunza. Hata hivyo anaweza kuathiriwa na mwelekeo wake kuhusu L2 hivi kwamba akajifunza L2 kwa utepetevu na kudumisha miundo fulani isiyo sahihi. Hatua hii ilikuwa muhimu kwa utafiti huu kwani katika kukusanya data kwani wanafunzi wa Kiswahili wanaozungumza Dholuo kama Ll waliombwa kueleza mikakati yao ya kujifunza silabi za Kiswahili. Habari hizi zilitumika katika kuandika ripoti ya utafiti kwa kueleza matokeo ya utafiti.

5. Mikakati ya mawasiliano ya L2. Mwanafunzi huweza kufikia kiwango cha kutosheka

katika ujifunzaji wa L2 kwa kuichukua LK kama njia ya kuwasiliana na wazawa wa L2.

(32)

18

Hatua hizi tano humfanya mwanafunzi kufikia hatua madhubuti ya LK ambapo anazingatia kanuni za L2 ingawa bado kuna makosa machache anayoyafanya. Hivyo basi ataendelea kuzungumza LK iliyo na miundo ya L2 isiyo sahihi. Hatua hizi ni muhimu kwa ambavyo utafiti huu ulilenga kubaini makosa ya wanafunzi wanaozungumza Dholuo katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili kwa kubainisha miundo isiyo sahihi wanayozua kutokana na athari ya L1.

1.7.2 Nadharia zalishi ya silabi ya KV

Nadharia hii iliasisiwa na Clements na Keyser (1983). Wawili hawa walibuni muundo wa fonolojia wa KV ambao kimahususi unashughulikia silabi. Kwa mujibu wa Clements na Keyser (1983), nadharia ya silabi inastahili kutekeleza majukumu matatu. Katika utafiti huu, tulichukulia majukumu haya waliyoainisha kama mihimili ya nadharia ya silabi ya KV ifuatavyo:

i) Kutaja kanuni jumulifu zinazotawala muundo wa silabi.

ii) Kue1eza mipaka na kiwango cha namna muundo wa silabi huweza kutofautiana kutoka lugha moja hadi nyingine.

iii) Kutaja kanuni zinazotawala silabi katika lugha mahususi.

Kwa msingi wa mhimili wa kwanza, silabi inachukuliwa kuwa na muundo wa rusu tatu: rusu silabi, rusu msingi na rusu ya fonimu. Hii ndiyo kanuni jumulifu inayotawala muundo

(33)

wa silabi. Rusu msingi ndiyo inayoelekeza sehemu ambazo konsonanti na vokali huchukua

kwenye muundo wa silabi. Clements na Keyser (1983) wanaeleza kwamba vokali ndiyo

inayowakilisha kilele cha silabi kwani ina mvumo wa juu ikilinganishwa na konsonanti.

Rusu hizi zinaunganishwa na mistari inayoonyesha uhusiano kati yake. Sehemu ya K

huunganishwa na fonimu za konsonanti ilhali V huunganishwa na fonimu za vokali.

Uhusiano huu unaweza kuwakilishwa kwa kielelezo matawi ifuatavyo tukitumia silabi

$Ia$:

Kielelezo 1:Uhusiano wa konsonanti na vokali katika silabi kwa rusu.

rusu silabi

A

I

V

1

1

rusu msingi

rusu fonimu

Mhimili huu ulitusaidia katika kuwasilisha miundo ya silabi za Dholuo na za Kiswahili

kwa njia ya vielelezo matawi. Vilevile, iwapo tulipopata miundo isiyo sahihi ya silabi za

maneno ya Kiswahili inayobuniwa na wanafunzi wa Kiswahili wanaozungumza Dholuo

(34)

20

Mhimili wa pili wa nadharia hii ni kueleza mipaka na kiwango cha namna muundo wa

silabi huweza kutofautiana kutoka lugha mmoja hadi nyingine. Clements na Keyser (1983)

wanapendekeza kuwa silabi ya KV ndiyo silabi pendwa ya lugha zote duniani. Katamba

(1989), akizungumzia nadharia hii, anasema kwamba hakuna lugha yoyote duniani ambayo

imepatikana kukosa muundo wa silabi ya KV. Kila lugha ina miundo mingine ya silabi

ambayo huweza ama kufanana au kutofautiana na miundo ya silabi katika lugha nyingine.

Mhimili wa tatu unahusu kanuni za lugha mahususi zinazotawala muundo wa silabi.

Clements na Keyser (1983) wanasema kwamba, kuna lugha ambazo zinaruhusu

mwambatano wa konsonanti au vokali kwenye silabi na zipo ambazo haziruhusu

miambatano fulani ya konsonanti au vokali. Mhimili huu ulitufaa katika utafiti wetu kwa

kutusaidia kueleza kanuni zinazoelekeza namna konsonanti au vokali huweza kuambatana

katika silabi za Dholuo na za Kiswahili.

1.8 Mbinu za utafiti

Sehemu hii inaeleza mbinu ambazo zilitumiwa kukusanya data nyanjani na namna mbinu

hizo zilivyotumiwa. Vilevile inaeleza idadi ya sampuli iliyotumiwa katika utafiti naaina ya

usampulishaji uliotumiwa kuteua sampuli hiyo pamoja na vigego geu vilivyozingatiwa.

Mbali na hayo eneo ambalo utafiti utafanywa limeelezwa katika sehemu hii. Mbinu

zilizotumiwa .katika uchanganuzi wa data iliyokusanywa na uwasilishaji wa matokeo

(35)

1.8.1 Eneo la Utafiti

Eneo la utafiti lilikuwa wilaya ya Rarieda iliyo katika Kaunti ya Siaya mkoani Nyanza.

Eneo hili linapakana na Ziwa Victoria, wilaya za Bondo, Gem na Kisumu Mashariki.

Wakazi wake ni wazungumzaji wa Dholuo kama Lt. Kwa ambavyo wilaya ya Rarieda

haina mji wowote mkubwa, haina wakazi wengi wageni. Hivyo wengi wa wanafunzi

katika shule za upili hasa za kutwa ni wazungumzaji wa Dholuo. Sababu nyingine ya

kuhusisha shule za kutwa ni kuwa asilirnia themanini na tano ya shule za upili wilayani

Rarieda ni za kutwa.

Wilaya ya Rarieda imepakana na maeneo yaliyo na shule ambazo matokeo yake ya

Kiswahili yamekuwa bora zaidi ikiwemo Maranda (en eo la Bondo) na Shule ya wasichana

ya Kisumu (eneo la Kisumu). Shule za Rarieda hazijaonyesha matokeo bora kama haya.

lli\l'j'Q huenda kuna tatizo linalostahili kuchunguzwa katika Rarieda. Eneo hili limeachwa

katika tafiti zinazohusu lugha ya Kiswahili. Utafiti huu uliainisha makosa kwa kiwango

cha fonolojia (silabi) hasa katika uzungumzaji na kupendekeza njia za kurekebisha. Utafiti

wamwigo ulionyesha maneno kadha yakivurugwa.

1.8.2Mbinu za ukusanyaji data

Hizinimbinu mbalimbali zilizotumiwa kupata data kutoka kwa walengwa nyanjani.

Utafiti huu ulitumia mahojiano, hojaji na uchunzaji kukusanya data kutoka kwa wanafunzi

(36)

22

Data muhimu zinazoweza kuhusishwa na ujifunzaji wa L2 ni matamshi ya mwanafunzi

katika L1, matamshi yake ya LK na matamshi sahihi ya L2 na wazungumzaji wake

(Selinker 1972). Kwa hivyo, data iliyokusanywa nyanjani ni maneno ya Kiswahili

yanayotamkwa na wanafunzi wa Kiswahili wanaozungumza Dholuo kama L1 kudhihirisha

miundo isiyo sahihi ya silabi za Kiswahili.

1.8.2.1Mahojiano

Mahojiano ni mbinu ya kukusanya data kwa kuwauliza walengwa maswali na kupata

majibu kutoka kwao (Mugenda na Mugenda 1999). Katika utafiti huu, mahojiano ya ana

kwa ana yalitumiwa kuwauliza wanafunzi maswali. Mahojiano wazi yalitumiwa, ambayo

yaliongozwa na maswali yaliyoandaliwa mapema. Tulipanga na walimu ili kukutana na

wanafunzi walengwa shuleni.

Maswali haya yalilenga maana ya silabi, aina za silabi wanazofunzwa, miundo ya silabi

wanayojua, matatizo wanayokumbana nayo katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili na

baadhi ya maneno yanayotatiza kutamka kwa mujibu wa silabi zake. Majibu yao

yalinakiliwa kwa kalamu na kuainishwa baada ya kazi ya nyanjani. IIi kuondoa athari ya

mtazamaji au mtafiti kwa walengwa tulizua mada za kusisimua kabla na wakati wa

mahojiano, kama maadhimisho ya Krismasi, siku

ya

kwanza shuleni na ujuzi wa teknolojia

(37)

1.8.2.2 Hojaji

Hojaji ni mbinu ya ukusanyaji data ambapo mtu anayelengwa kutoa habari hupewa fornu

za maswali yanayomwongoza kutoa habari lengwa (Mugenda na Mugenda 1999).

Mlengwa huyajaza majibu yake kwenye fomu ya hojaji. Hojaji huweza kuwa wazi au funge. Hojaji funge ni hojaji ambayo humpa mlengwa mipaka ya kutoa majibu yake kwa

ambavyo inapendekeza majibu yanayotarajiwa ili achague mojawapo kwa kila swali. Hojaji wazi ina maswali ambayo mlengwa ana uhuru wa kutoajibu anavyojua bila kupewa

orodha ya majibu ya kuchagua.

Katika utafiti huu, hojaji wazi ilitumiwa kwa walimu. Maswali ya hojaji yaliyotungwa

yalikuwa mafupi ili waweze kuyajibu kwa urahisi. Maswali haya yalipigwa

chapa

na

nakala za kutosha za fomu za hojaji kutolewa. Tulizuru shule lengwa mapema na kupanga

miadi na walimu kuhusu siku ya data kukusanywa, hivyo walengwa walijaza fomu hizo na

tukakusanya siku iyo hiyo ili kuzuia hatari ya kupotea kwa fomu na kusahau kujaza.

1.8.2.3 Uchunzaji

Uchunzaji ni mbinu ya kukusanya data kwa kuchuja habari lengwa kutokana na jumla ya

habari fulani kwa kusikiliza au kutazama. Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchunzaji

kuwasikiliza wanafunzi wanavyotamka silabi za maneno wanapozungumza Kiswahili. Hili

lilifanyika kwa kuwashirikisha wanafunzi wa kidato cha tatu katika mijadala ya Kiswahili.

(38)

24

mahojiano. Mada za mazungurnzo zilihusisha afya na mazingira, habari na mawasiliano na

nidhamu. Maneno ishirini na moja yalilengwa na matamshi yake kusikilizwe kwa makini.

Kanda na hayo maneno mengine yanayodhihirisha miundo ya silabi isiyo sahihi

yalinakiliwa kwa uchanganuzi baadaye.

Baadhi yao walipewa insha kuhusu faida na hasara za teknolojia. Tulisoma insha hizo na

kunakili maneno yaliyo na miundo ya silabi isiyo sahihi. Insha hizi ziliandikwa kabla ya

mahojiano na hojaji ili matatizo waliyo nayo yadhihirike bila kufahamu mapema kuwa

makosa yao yanalengwa. Hivyo tuliwasiliana na walimu katika shule zilizotafitiwa kwa

simu ili wawape wanafunzi insha. Jumla ya shule sita zilihusishwa. Wanafunzi wanne

katika kila shule waliteuliwa kuandika insha na tukasafiri hadi shuleni kuzichukua insha

hizo, tukasahihisha na kutoa nakala.

1.8.3 Usampulishaji

Kwa mujibu wa Mugenda na Mugenda (1999), usampulishaji ni hatua ya kuteua idadi

ndogo ya walengwa katika mchakato wa.utafiti ili kuwatumia kukusanya data. Sampuli ni

sehemu ndogo inayoteuliwa kuwakilisha jumuiya nzima ya walengwa katika utafiti. Data

inayokusanywa kutokana na sampuli huchukuliwa kuwa kiwakilishi cha ukweli kuhusu

(39)

Utafiti huu uliteua sampuli za kimaksudi kwa msingi wa mada ya utafiti, Sampuli za

kimaksudi ni sampuli zinazoteuliwa kwa kulenga sehemu ya idadi nzima ya walengwa

ambayo inajulikana kuwa ina habari zinazotatitiwa. Mugenda na Mugenda (1999)

wanasema kuwa sampuli za kimaksudi huteuliwa kwa sababu mtafiti anajua kuwa data

anayotaka inapatikana kwa watu mahususi wenye sifa fulani lengwa. Jcladi ya sampuli

iliteuliwa kulingana na maoni ya Milroy na Gordon (2003) kuwa sampuli ndogo ndiyo

mwafaka katika utafiti. Shule sita za upili ziliteuliwa kufanyiwa utafiti kwa sababu

walengwa ni wanafunzi wa shule za upili. Kwa ambavyo wilaya ya Rarieda imegawanywa

kwenye maeneo sita kila shule iliteuliwa kutoka kila eneo.

Shule za kutwa ziliteuliwa kwani wanafunzi wake ni wakazi wa wilayani na wanakaa

vijijini. Shule za bweni zina wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na wengi wa

wale wanaozungumza Dholuo kama L1 huencla wanakaa mijini. Wanafunzi kumi wa

kidato cha tatu waliteuliwa katika kila shule kwa sababu wana uzoefu wa mazingira ya

shule na tajiriba ya kutosha ya mafunzo na matumizi ya Kiswahili. Wanafunzi kumi

kuteuliwa ni kwa msingi wa maoni ya Wolfram na Schilling (1998) kuwa katika utafiti wa

lugha katikajamii kila kundi liwakilishwe na angaa watu watano na idadi ya wanaohojiwa

iwe kati ya 48- 120. Wanafunzi wa kidato cha nne hawakuhusishwa kwa vile huenda

walikuwa na kazi nyingi na hivyo hawangepata muda wa kutosha kushirikishwa katika

(40)

26

Vigego geu muhimu tulivyozingatia ni jinsra na L1. Wanafunzi watano walikuwa wavulana na watano wasichana katika kila shule ili usawa wa kijinsia uzingatiwe. Wanafunzi wote kumi tulioteuwa kama sampuli walikuwa wazungumzaji wa Dholuo kama Ll kwa sababu utafiti ulilenga matatizo yanayotokana na tofauti za miundo ya silabi kati ya Dholuo (Ll) na Kiswahili (L2). Walimu walitusaidia kuwateua wanafunzi hao ambao wazazi wao (baba na mama) ni Waluo. Wanafunzi wanne kati ya kumi katika kila shule waliandika insha; mvulana na msichana bora katika Kiswahili na mvulana na msichana aliye na udhaifu katika Kiswahili. Walimu walisaidia kupima ubora na udhaifu huu kutumia matokeo ya awali ya mitihani Kiswahili. Uteuzi huu ulihakikisha kuwa wanafunzi wote wanaozungumza Dholuo kama Ll wamewakilishwa kikamilifu. Mwalimu mmoja wa Kiswahili kutoka kila shule iliyoshirikishwa alijaza hojaji.

Vilevile sampuli za kubahatisha zilitumiwa kuwasikiliza wanafunzi wowote wa shule za upili ili kukusanya data ya maneno ambayo miundo ya silabi zake imevurugwa.

1.8.4 Uchanganuzi wa Data

(41)

Mhimili wa kwanza (uhamishaji lugha) ulitumiwa kuainisha maumbo ya silabi yasiyo

sahihi ambayo yametokana na kuhamisha maumbo ya silabi za Dholuo. Mhimili wa pili

(ujumlishaji kanuni) wa tatu (uhamishaji wa mafunzo) ulitumiwa kuainisha maoni ya

walimu kuhusu matatizo wanayokumbana nayo katika ufunzaji wa silabi ambayo huweza

kuathiri wanafunzi. Mhimili wa nne nao (mikakati ya ujifunzaji) ulitumiwa kuonyesha

kiwango cha makosa ya silabi ambayo wanafunzi wamedumisha katika uzungumzaji wao

na uandishi wa Kiswahili katika kiwango chao cha umilisi wa Kiswahili. Nao mhimili wa

pili (ujumlishaji wa kanuni) ulitumiwa kueleza namna baadhi ya wanafunzi walivyojipata

katika hali ya kurekebisha baadhi ya maneno isivyostahili.

Mhimili wa tano (mikakati ya mawasiliano) ulitumiwa kutathmini iwapo wanafunzi hawa

wametosheka na umilisi wao wa Kiswahili ama wanafanya jitihada zaidi kuuboresha.

Tumeandika ripoti kwa maelezo kuhusu matatizo ya wanafunzi katika ujifunzaji wa silabi

za Kiswahili. Mapendekezo yaliolewa kuhusiana na matatizo yaliyoelezwa.

1.8.5 Uwasilishaji wa Matokeo

Hii ni hatua ya kueleza kwa kina namna data iliyochanganuliwa ilivyotokea. Matokeo

yatawasilishwa kwa maelezo kwa kuzingatia malengo ya utafiti. Maelezo yametolewa

kuhusu matatizo ya wanafunzi wa shule za upili wilayani Rarieda katika ujifunzaji wa

silabi za Kiswahili, miundo ya silabi inayoundwa na wanafunzi hawa na athari ya matatizo

(42)

28

za LK. Vilevile tumetumia michoro ya vielelezo matawi kuonyesha miundo mbalimbali ya silabi kwa mujibu wa Nadharia ya muundo wa silabi wa KY (Clements na Keyser, 1983).

1.9 Muhtasari

(43)

SURA YA PILI

MATATIZO KATlKA UJIFUNZAJI WA SlLABl ZA KrSWAHILI

2.0 Utangulizi

Sura hii inaeleza dhana ya silabi, dhima ya silabi na uwakilishaji wa silabi kwa rusu kwa

msingi wa Nadharia ya silabi ya KY. Yilevile innaeleza miundo na aina za silabi za

Kiswahili na kisha miundo na aina za silabi katika silabi za Dholuo. Kutokana na maelezo

haya, sura hii inadhihirisha tofauti zilizopo hasa katika miundo ya silabi za Dholuo na zile

za Kiswahili. Tofauti hizo ndizo chanzo cha matatizo katika ujifunzaji wa silabi za

Kiswahili na wanafunzi wanaozungumza D holuo kama L 1.

2.1 Dhana ya silabi

Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti moja au

muungano wa sauti hutamkwa kwa pamoja kama fungu moja (Massamba 2006). Wakati

mtu anapozungumza au kusoma, matamko ya silabi ndiyo yanayosikika. Hivyo basi silabi

kama kipashio cha lugha huwezesha mawasiliano kutendeka. Kwa mujibu wa Buliba na

wenzake (2006), silabi ni kipashio muhimu katika fonolojia ambacho kinaweza kutumiwa

kueleza muundo wa lugha. Muundo wa lugha yoyote ile unaweza kuelezwa kuzingatia aina

zake za silabi na namna sauti zinavyopangwa kuunda silabi hizo. Kwa mfano Kiingereza ni

lugha inayokubali mkururo wa konsonanti ama mwanzoni au mwishoni mwa silabi ilhali

(44)

30

Dhana ya silabi ni ya msingi sana katika lugha. Katamba (1989) anasema kwamba silabi ndicho kipashio kinachotumika kupanga mifumo ya lugha. Umuhimu wa silabi unadhihirika katika kushughulikia sifa arudhi za lugha kama shadda, kiimbo na wakaa. Sifa hizi zote huwekwa kwenye neno kuzingatia silabi. Mwansoko (1995), akishughulikia shadda katika Kiswahili, anaeleza sifa nyingine kama kidato na muda wa matamshi ambazo zinategemea silabi katika maelezo yake.

Barbara (2011) anasema kwamba silabi huwa upeo wa matamshi mtu anapozungumza. Hivyo basi uwezo wa kumudu silabi za lugha yoyote ile hupatikana mtu anapojifunza lugha hiyo. Mgawanyo wa silabi hubainika zaidi katika mazungumzo ya watoto wanapojifunza kusema lugha (Buliba na wenzake, 2006). Kwa njia hii watoto huupunguza ugumu wa kuyamudu maneno marefu kwa kuyavunja katika silabi. Mtoto anapojifunza lugha ya kwanza anajihusisha zaidi na kupata fonolojia yake bali si sauti binafsi za lugha hiyo. Kwa mujibu wa Jacobson (1969), watoto hupata muundo wa silabi za LI kwa kuanza kutamka silabi ya KV ambayo ndiyo silabi pendwa ya lugha zote duniani.

(45)

Kiingereza. Kauli hii inathibitisha umuhimu wa L1 ya mtu katika kuathiri ujifunzaji wa

L2.

2.2 Dhlma ya silabl

Kwa jumla silabi mara nyingi huwa na dhima ya fonimu, mofimu na neno (Buliba, na

wenzake 2006). Silabi zote zinazoundwa kwa irabu pekee na zile zinazoundwa kwa

konsonanti Iml na Inl huwa na dhima ya fonimu kwani zinaweza kubadilisha maana ya neno. Kwa mfano, tukitumia jozi ya mlinganuo finyu:

Mfano 1:Maneno yanayodhihirisha dhima ya silabi kama fonimu.

a) n-chi: sehemu ya ardhi iliyozungukwa na maji

m-chi: mtwangio

b) o-za: vunda/ kabidhi mtoto katika harusi

u-za: badilisha kitu kwa fedha au kitu kingine

c) ta-i: ndege mkubwa alaye mizoga/ kitambaa kivaliwacho shingoni juu ya ukosi

ta-o: pindo

Kunazo silabi ambazo ni

mo

f

imu,

Mofirnu ni kipashio kidogo zaidi katika lugha ambacho

kinabeba maana ya kisarufi na hakiwezi kugawanywa bila maana kupotea. Kwa mfano

katika neno #mto# kiambishi {m} cha umoja na mzizi {to} ni mofimu ambazo pia ni

(46)

32

mwanafunzi akibadili mmundo wa silabi ambayo ina dhima ya fonimu katika neno, maana

yaneno hilo iliiyokusudiwa itabadilika. Kwa mfano, silabi {m} ikibadilishwakuwa {mil neno hila litabadilika kuwa mito. Pia kuna silabi ambazo ni sehemu ya mofimu, kwa mfano katika neno #mama# silabi zake ni ma$ma na {mama} ni mofirnu moja. Hivyo basi

ikiwa mzungumzaji wa Kiswahili atazua miundo ya silabi isiyo sawa kuna uwezekano mawasiliano kutatizwa.

Silabi vilevile inaweza kuwa na dhima ya neno katika lugha. Maana yake ni kwamba kuna maneno ambayo yanaundwa kwa silabi moja. Kwa mfano neno #la# lina silabi moja tu

ambayo ni $la$, neno #kwa# vilevile lina siabi moja ambayo ni $kwa$. Maneno mengine

yanayoundwa kwa silabi moja ni vitenzi vya silabi moja kama: #Ia#, #pa#, #fa#, #ja#,

#pwa#, #nya#.

Silabi pia huchukua nafasi kubwa kama kiarnbajengo cha sifa arudhi katika isimu. Arudhi

ni sifa ambazo huzingatiwa katika utamkaji wa maneno mtu anapozungumza na zinahusiana na namna sauti zinavyotamkwa ili kuleta maana iliyokusudiwa. Sifa hizi

ambazo ni kidatu, mkazo na nguvumsikiko katika neno huelezwa kwa kuzingatia ni silabi ipi ambayo sifa hizi huwekwa. Katamba (1989), akizungumzia dhima ya silabi, anasema kuwa kuna sheri a ambazo zinahitaji shadda msingi kuwekwa kwenye silabi fulani katika

neno. Kwa hivyo, ili kutia sifa arudhi hizi kwenye neno ipasavyo, mtu yeyote yule anayezungumza lugha fulani anastahili kuwa na miundo sahihi ya silabi ili miundo ya

(47)

Uwekaji wa shadda kwa maneno huzingatia silabi. Katika Kiswahili shadd a hutiwa kwenye silabi ya pili kutoka mwisho wa neno. Shadda inapotiwa kwenye silabi inayostahili maana ya neno iliyokusudiwa huwasilishwa. Vilevile kiimbo kikiwekwa sawa kwenye neno huwezesha kusudi la mzungumzaji kueleweka kwa urahisi, kwa mfano kusudi huweza kuwa kuuliza swali, kuonyesha mshangao au kutoa tu taarifa. Kuna maneno ambayo maana yake hubadilika namna silabi inayotiwa shadda inavyobadilika. Kwa mfano:

Mfano 2: Maneno yanayodhihirisha kubadilika kwa maana kutegemea silabi inayotiwa shadda.

a) a'la: neno la kuonyesha mshtuko au mshangao

'ala: zana za kufanyia kazi au za vita

b) bara'bara: njia kuu

ba'rabara: sawasawa

(48)

34

Buliba na wenzake (2006) wanasema kuwa mada ya silabi ni hatua muhimu sana katika

ufunzaji wa lugha. Wakitumia Kiswahili kama mfano wanaserna kwamba katika kujifunza

kutamka maneno ya Kiswahili watoto huanza kwa kutarnka silabi ili kurahisisha uzito wa

kutamka maneno marefu. Athari ya L1 kwenye miundo ya silabi za L2 ni suala la kutiliwa

maanani kwani huweza kumfanya mtu akawa na matatizo katika kujifunza L2 ikiwa

miundo hiyo inatofautiana.

Kwa ambavyo umilisi wa lugha huambatana na ruwaza za miundo akilini mwa

mzungumzaji, miundo hii isiyo sahihi huenda ikawa sehemu ya ruwaza za mtu. lwapo

atafikia usukuku katika ujifunzaji wake inamaanisha kuwa hatafikia miundo sahihi ya L2

(Ping 2008). Matokeo yake ni kwamba atatumia lugha isiyo sahihi katika mawasiliano

yake. Utafiti huu unalenga ujifunzaji wa silabi za Kiswahili kwa sababu wanafunzi

wakimudu ujuzi sawa wa miundo ya silabi za Kiswahili, uzungumzaji wao pamoja na

kuandika kutaboreshwa.

2.3 Uwakilishaji wa silabi

Silabi huweza kuwakilishwa kwa kielelezo matawi ambacho kina ngazi (rusu) tatu: rusu

silabi, rusu msingi na rusu ya fonimu (Clement na Keyser 1983). Wanaendelea kusema

kuwa silabi ni kipashio msingi katika hairakia ya kifonolojia kwani sifa za kifonolojia

huweza kuelezwa kwa msingi wa silabi. Katika uwakilishaji huu, rusu ya kwanza amabayo

niyajuu zaidi inawakilisha silabi. Rusu ya pili inaitwa rusu msingi na inaonyesha muundo

(49)

katika silabi hiyo. Rusu ya mwisho ambayo ni ya kiwango cha chini zaidi inaonyesha

fonimu mahususi ambazo zinaunda silabi inayowakilishwa. Kila kipashio cha rusu ya chini

zaidi (rusu fonimu) huunganishwa na kipashio cha rusu ya pili kwa mistari wima. Vipashio

vya rusu ya pili (rusu msingi) huunganishwa na rusu silabi kwa mistari mishazari. Mistari

hii mishazari hukutana na kushikana inapofika kwenye rusu silabi, kama inavyoonyeshwa

kwenye mchoro ufuatao:

Kielelezo 2: Uwakilishaji silabi kwa rusu (silabi ya KV).

o rusu silabi

=,

K V rusu msingi

I

I

m a rusu fonimu

Utafiti huu ulitumia vielelezo matawi kueleza miundo ya silabi za Kiswahili na Dholuo,

Hii ni kwa sababu njia hii inaonyesha maelezo kamilifu ya sehemu zinazounda silabi.

2.4 Silabi za Kiswahili

Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa na zaidi ya watu milioni themanini katika

maeneo ya Afrika Mashariki na Kati (Bosha 1993). Kimsingi, lugha za Kibantu

zimetawaliwa na silabi wazi, ambazo huishia kwa vokali. Kwa mujibu wa Massamba

(2006), silabi za .lugha ya Kiswahili zina muundo msingi wa KV, ambayo ndiyo silabi

(50)

36

maneno ya Kiswahili. Vilevile lugha ya Kiswahili ma silabi funge. Hizi m silabi

zinazoishia kwa konsonanti.

2.4.1 Miundo ya silabi za Kiswahili

Kama ilivyotajwa katika 2.3, tumeeleza kuwa lugha ya Kiswahili ina KY kama muundo

wake wa kimsingi wa silabi. Muundo huu unapatikana katika maneno mengi zaidi ya

Kiswahili, Kwa mfano, katika neno #ba$ba#.

Kielelezo 3: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa KY

b a

A

K

Y

I

I

b a

A

I

I

Muundo mwingine unaopatikana katika silabi za maneno ya Kiswahili ni muundo wa Y.

Katika muundo huu vokali moja pekee huunda silabi, kwa mfano katika neno #o$a#.

Kielelezo 4: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa Y.

(J (J

I

I

V

V

I

I

(51)

Kuna muundo wa silabi za K ambapo konsonanti moja huunda silabi. Konsonanti

zinazounda silabi za K ni nazali pekee. Kimsingi ni kwamba katika lugha ya Kiswahili konsonanti za nazali Iml na In! zina usilabi. Sifa hii ya usilabi ipo kwa sababu nazali ndizo

konsonanti zilizo na usonorari mkubwa baada ya viyeyusho. Hata hivyo zinaposimama

peke yake kuunda silabi zitatokea mwanzoni I11waneno tu kama vile:

Mifano 3: Maneno yaliyo na silabi za konsonanti ya nazali pekee.

Mkulima #m$ku$li$ma# Msichana #m$si$cha$na#

Mti #m$ti#

Mtu #m$tu#

Nchi #n$chi#

Nta #n$ta#

Kielelezo 5: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa K kwa matawi.

0-I

K

I

K V

I

I

m t

Muundo mwingine ni wa mwambatano ya konsonanti mbili zikifuatwa na vokali, kwa

mfano KKV. Muundo wa KKV hutokea hasa kwa konsonanti kufuatwa na nusu vokali.

KEYA

(52)

-38

Kwa hivyo muundo huu unaweza kuchukuliwa kama muundo wa KY2KY. Kwa mfano

katika maneno yafuatayo:

Mfano 4: Maneno yaliyo na muundo wa silabi K

Y2

KY. Fyeka #fye$ka#

Gwara #gwa$ra#

Shwari #shwa$ri#

Swara #swa$ra#

Tupwa #tu$pwa#

Tweka #twe$ka#

Twiga #twi$ga#

Yilevile muundo wa KKY hutokea katika maneno yenye asili ya kigeni yaliyosimilishwa hasa kutoka lugha ya Kiingereza. Kwa mfano:

Mfano 5: Maneno yaliyo na muundo wa silabi wa KKY.

Klabu #kla$bu#

Kreti #krc$ti#

Stethoskopu #ste$tho$sko$pu#

Stimu #sti$mu#

Trei #tre$i#

(53)

Kielelezo 6: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa KKY kwa matawi.

(J

~

K

12K

V

I

I

I

f y e

(J

.>.

K

Y

I

I

k a

Muundo wa KKKY hutokea tu katika maneno machache ya mkopo ambayo

yamesimilishwa kutoka Kiingereza. Maneno haya ni kama vile:

Mfano 6: Maneno yaliyo na muundo wa silabi wa KKKY.

Skrubu #skru$bu#

Stroberi #stro$be$ri#

Kielelezo 7: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa KKKY kwa matawi.

KKK Y K Y

s

k

r u b u

Silabi za muundo wa KYK hutokea aghalabu katika maneno mkopo katika Kiswahili kwa

mfano kutoka Kiingereza na Kiarabu, Maneno haya ni kama yale yaliyoonyeshwa katika

(54)

40

Mfano 7: Maneno yaliyo na muundo wa silabi wa KVK.

Daftari #daf$ta$ri#

Daktari #dak$ta$ri#

Labda #lab$da#

Kielelezo 8: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa KVK kwa matawi.

(J

~

K V K

I

I

I

I a b

A

K V

I

I

d

a

Vilevile kuna maneno ya Kiswahili yaliyo na muundo wa silabi wa VK. Mengi ya rnaneno

ya Kiswahili yenye silabi za muundo huu wa VK yana asili ya Kiarabu. Maneno haya ni

kama yafuatatyo:

Mfano 8: Maneno yaliyo na muundo wa silabi wa VK.

Tksiri #ik$si$ri#

Iktisadi #ik$ti$sa$di#

llhali #il$ha$li#

(55)

Kielelezo 9: Uwakilishaji wa silabi ya muundo wa VK kwa matawi.

-.

I

1

(J

m

/\

K V

I

I a

2.4.2Aina za Silabi za Kiswahili

Lugba ya KiswahiJi ina silabi wazi na siJabi funge. Silabi wazi ni silabi zinazoishia na vokali ilhali silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti. Kwa hivyo, maneno mengi ya Kiswahili yameundwa kwa silabi wazi. Kwa mfano:

Mfano 9: Maneno yaliyo na silabi wazi.

Jina #ji$na#

Kiti #ki$ti#

Paka #pa$ka#

Meza #me$za#

Ngozi #ngo$zi#

Karatasi #ka$ra$ta$si#

(56)

42

Hata hivyo, kuna maneno ambayo yana silabi funge, hasa maneno mkopo ya Kiswahili ..

Baadhi ya maneno haya yanaposimilishwa katika Kiswahili yanabakia kutamkwa yalivyo

katika lugha zake asilia na hivyo basi baadhi ya silabi kubakia funge. Kwa mfano:

Mfano 10: Maneno mkopo ya Kiswahili yaliyo na silabi funge.

Maktaba #mak$ta$ba#

lksiri #ik$si$ri#

Alhamisi #al$ha$mi$si#

Maksai #mak$sa$i#

lktisadi #ik$ti$sa$di#

Ilhali #il$ha$li#

Abadan #a$ba$dan#

Kuna kundi la silabi ambazo zinaishia na konsonanti za nazali Iml na In!pekee. Silabi hizi zinaundwa na nazali moja pekee na aghalabu hutokea mwanzoni mwa neno. Katika utafiti

wetu tumezishughulia chini ya silabi funge kwa sababu zinapotamkwa hakuna vokali

inayohusishwa. Rata hivyo, katika miundo yake ya ndani, silabi kama hizi hazina koda

kwani nazali hiyo huwa ndicho kilele chake. Kwa mfano:

Mfano 11: Maneno yaliyo na silabi funge ya nazali pekee.

Mtu #m$tu#

Mv! #m$vi#

Nta #n$ta#

(57)

2.5 Silabi za Dholuo

Dholuo ni lugha ya Kinailoti inayozungumzwa na jamii ambayo kwa ukubwa ni ya tatu

nchini Kenya. Lugha hii inazungumzwa takribani watu milioni 3.8 wanaopatikana katika

eneo la Ziwa Viktoria (Borowsky na Avery 2009). Wazungumzaji hawa asilia wa Dholuo

kama Ll wanapatikana katika Kaunti nzima ya Kisumu, Siaya, Homa Bay na sehemu ya

Kaunti ya Migori katika eneo laNyanza. Baadhi ya maeneo katika kaunti hizi yamepakana

na wazungumzaji wa lugha nyingine kama vile lugha za Kikalenjin, Kiluhya, Kikisii na

Kikuria. Wilaya ya Rarieda, Kaunti ya Siaya ni moja wapo ya maeneo ambapo

wazungumzaji wa Dholuo wamezungukwa na wazungumzaji wa Dholuo pekee kama

Iugha ya kwanza.

2.5.1 Miundo ya silabi za Dholuo

Idadi ya miundo ya silabi za Dholuo imechukuliwa kuwa tofauti na watafiti mbalimbali.

Kwa mfano, Olal (2008) anatambua miundo mitatu ya silabi za Dholuo. Naye Owino

(2003) anatambua miundo minne. Kwa kuzingatia maoni ya hawa wawili, utafiti huu

ulizingatia miundo minne ya silabi za Dholuo ifuatayo: KY,V,YK, KYK.

ldadi ya silabi zilizo na muundo fulani mahususi inatofautiana kutoka aina moja ya

maneno hadi nyingine. Browsky na Avery (2009: 176) wanasema kuwa silabi nyingi za

(58)

44

yenye muundo wa KVK. Mbali na vitenzi vya Dholuo, maneno ya aina nyingine pia

yameundwa kwa silabi moja yaKVK. Kwa mfano:

Mfano 12: Maneno ya Dholuo yanayoundwa kwa silabi moja ya KVK.

Dholuo Mgao wa Silabi Kiswahili

Dum $dum$ ruka

Wer $wer$ imba

Tok $told pakua

Ling' $lilJ$ nyamaza

Bet $bet$ keti

Sin $sin$ kasirika

Tam $tam$ kataa

Dok $dok$ rudi

Chop $cop$ fika

Duok $duok$ rudisha

Maneno mengine yaliyo na silabi za KVK mbali na vitenzi ni kama:

Dholuo Mgao wa silabi Kiswahili

Lak $lak$

m

e

n

o

Nam $nam$ ziwa

Wich $wic$ kichwa

Ler $Ier$ safi

Lit $lit$ chungu

(59)

Asilimia kubwa ya maneno ya Dholuo ni yenye silabi za KVK. Hii ni kwa sababu

kulingana na maoni ya Owino (2003) silabi ya KVK ndiyo muundo upeo katika Dholuo. Muundo wa silabi wa KVK unaweza kuwakiliishwa kwa kielelzo matawi kama ifuatavyo:

Kielelezo 10: Uwakilishaji wa muundo wa KVK kwa matawi

o

~

K

V

K

I

\

I

k 0 8 mvua

Kwa hivyo kutokana na data hizi silabi za KVK ni nyingi katika Dholuo. Hata hivyo katika Kiswahili silabi za muundo wa KVK zinapatikana katika maneno yenye asili ya kigeni na

ni chache. Hivyo basi suala hili linaweza kuwa changamoto kwa wanafunzi wa Kiswahili

wanaozungumza Dholuo kama Ll wanapojifunza silabi za Kiswahili.

Muundo wa silabi za KV unapatikana katika maneno ya Dholuo kwani huu ndio muundo

pendwa wa silabi za lugha zote. Aghalabu silabi za KV zinapatikana katika maneno yaliyo

na silabi mbili au zaidi na zinaweza kutokea mwarizoni au mwishoni rnwa neno. Kwa

mfano:

Mfano 13:Maneno ya Dholuo yaliyo na silabi ya muundo wa KV. Dholuo

Mgao

wa Silabi

Kiswahili

Goyo

#go

$y

o#

piga

(60)

46

Anguru #a$lJgu$ru#

#o$to$yo#

#ki$di#

nguruwe

Otoyo

Kidi

fisi

jiwe

Puro #pu$ro# lima

Kielelezo 11: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa KV kwa matawi

o

/\

i I

c

.

>

.

f

I

p u r o lima

Muundo mwingine ni wa V, ambapo silabi huundwa kwa vokali pekee. Silabi za muundo

huu zinajitokeza katika nomino. Silabi za aina hii si nyingi sana katika vitenzi vya Dholuo,

isipokuwa tu kwamba zinapatikana sana vokali zinapotumiwa kama viambishi kwenye

vitenzi. Mifano ya maneno yenye silabi za V ni kama:

Mfano 14: Maneno ya Dholuo yaliyo na silabi ya muundo wa V.

Dholuo Mgao wa Silabi Kiswahili

Ong'er #o$l)er# nyani

Apwoyo #a$pwo$yo# sungura

Apar #a$par# kumi

Opuk #o$puk# kobe

Aora #a$o$ra# mto

(61)

Kutokana na mifano hii inabainika kuwa wingi wa silabi za V hutokea mwanzoni mwa

rnaneno, Kwa upande

mwingin

e,

katika Kiswahili silabi za

muundo

huu

hu

weza

kutokea

popote katika neno; mwanzoni, kati au mwishoni. Hii pia huweza kuwa changamoto kwa

wanafunzi wanaozungumza Dholuo kama Ll wanapojifunza silabi za Kiswahili.

Kielelezo 12: Uwakilishaji wa muundo wa silabi wa V kwa matawi.

r

I

a

I

I

o r a mto

Silabi za muundo wa VI( hutokea katika maneno ya Dholuo. Aghalabu maneno haya ni ya

silabi moja pekee. Rata hivyo maneno haya si mengi na agbalabu ni nomino, Katika

Kiswahili, silabi za muundo huu zinatokea mwanzoni mwa maneno yenye asili ya kigeni

ilivyoelezwa awali

(

t

aza

m

a

2.3.4). Maneno ya Dholuo yaliyo na silabi za

muund

o

wa VK

ni kama vile:

Mfano 15: Maneno ya Dholuo yaliyo na muundo wa silabi wa VK.

Dholuo Mgao wa Silabi Kiswahili

Ot $ot$ nyumba

Icb $ic$ tumbo

(62)

48

Kielelezo 13: Uwakilishaji wa silabi za muundo wa VK kwa kielelzo matawi

0'

.>.

V K

.

I

1

I C tumbo

Tofauti inaonekana katika miundo ya silabi za Kiswahili na Dholuo kwa ambavyo muundo

wa KVK na VK unapatikana katika maneno mengi asilia ya Dholuo lakini unapatikana

katika maneno machache ya Kiswahili. Vilevile silabi za muundo wa K zinazopatikana

katika maneno ya Kiswahili hazipatikani katika maneno ya Dholuo. Hii ni kWH sababu

hakuna konsonanti

ya

Dholuo iliyo na usilabi.

Mbali na hayo vokali zinapofuata!la katika Dholuo mara nyingi hazijisimamii kuunda

silabi bali zinakuwa kilele cha silabi hiyo. Kwa mfano, katika maneno kama $dicl$

(mbuzi), $ruo0$ (mwokozi).

Kielelezo 14: Muundo wa silabi yenye kilele cha vokali mbili

(63)

Rata hivyo kunapokuwa na mwambatano wa vokali ambapo vokali ya chini inatangulia

basi vokali hizo zitaunda silabi mbili. Kwa mfano, katika neno #a$o$ra# (mto).

Mwambatano wa konsonanti katika silabi za Dholuo hufanyika tu nazali zinapotangulia au

konsonanti zinapofuatwa na viyeyusho. Kwa mfano:

Mfano 16: Maneno ya Dholuo yaliyo na muundo wa silabi wa KKV.

Dholuo

Rombo

Mgao wa Silabi Kiswahili

Olwenda

#ro$mbo#

#o$lwe$nda#

kondoo

mende

2.5.2 Aina za silabi za Dholuo

Dholuo ina mchanganyiko wa silabi funge na silabi wazi katika maneno yake. Maneno

mengi yaliyo na silabi funge yanaundwa kwa silabi moja pekee. Mifano ya silabi runge za

Dholuo:

Mfano 17: Maneno ya Dholuo yaliyo na silabi runge.

Dholuo Mgao wa silabi Kiswahili

an $an$ mum

lel' $ler$ sati

pun $pim$ pima

duok $duok$ rudisha

(64)

50

tok

yuak

bad

$tok$

$yuak$

$bad$

pakua

lia

mkono

Aina nyingine ya silabi za Dholuo ni silabi wazi. Silabi hizi zinatokea mwanzoni, kati au

mwishoni mwa maneno kama ilivyo katika Kiswahili. Mifano ya silabi wazi katika Oholuo

ni:

Mfano 18: Maneno ya Dholuo yaliyo na silabi wazi.

Dholuo Mgao wa silabi Kiswahili

puro #pu$ro# lima

nyaroya #]la$ro$ya# ndama

ariyo #a$ri$yo# mbili

rombo #ro$mbo# kondoo

buru #bu$ru# maJ1VU

kendo #ke$ndo# tena

ng'olo #1)0$10# chora

Dholuo haina maneno mengi yenye silabi wazi

z

in

az

ofuat

a

n

a.

Hii ni tofauti na lugha ya

Kiswahili ambayo maneno yake mengi yenye asili ya Kibantu yana silabi wazi. Maneno

(65)

2.6 Muhtasari

Katika sura hii turneangazia tofauti zilizopo kati ya silabi za Kiswahili na za Dholuo kwa kuonyesha miundo na aina za silabi katika Dholuo na Kiswahili. Tofauti hizi ndizo chanzo cha matatizo ya baadhi ya wanafunzi wa Kiswahili wanaozungumza Dholuo kama Ll

katika ujifunzaji wa silabi za Kiswahili. Sura hii hivyo basi ilishughulikia dhana ya silabi,

dhima ya silabi na uwakilishaji na silabi. Mbali na hayo imeshughulikia miundo ya silabi

za Kiswahili, aina za silabi za Kiswahili, miundo ya silabi za Dholuo na aina za silabi za

Dholuo. Kutokana na sura hii tofauti zilizopo kati ya aina na miundo ya silabi za Kiswahili

na Dholuo zimedhihirika na hivyo basi kuonyesha uwezekano wa wanafunzi hao kutatizwa wanapojifunza silabi za Kiswahili. Katika sura inayofuata tumejadili na kuonyesha miundo isiyo sahihi ya silabi za Kiswahili inayoundwa na baadhi ya wanafunzi wanaozungumza

Dholuo kama Ll kutokana na matatizo ya tofauti za miundo ya silabi kati ya Kiswahili na

References

Related documents

The proportion of eyed beans is somewhat too large to result from two recessive factors and too small t o result from a single factor, but other- wise the theoretical

Results show that the Lyapunov-type inequality gives the worse and the Cauchy-Schwarz-type inequalitygives the best lower bound estimates for the smallest

Following the collection of the first harvests the F1 plants were again selfed and then all of the leaves and side branches were removed so that second harvests of seed were

was  utilized  to  evaluate  professional  development  manuscripts,  collected  based  on  their   focus  of  professional  development  for  community

In our examination, we have tried different inside and outside releases like void, surface and crown utilizing factual parameters, for example, skewness and

the spatial relevance’s to the query, They focused on the efficiency issue of geographic document search and proposed an efficient indexing structure, namely, IR-tree, along

(1) Slump test: fresh concrete was test under slump for different proportions as 0%, 5%, 10% & 15% replacement of fine aggregate with waste plastic granules, the results

We therefore screened for gain-of-function enhancers of jing gain of function in the eye and identified the Drosophila homolog of the disease gene of human a