• No results found

Mofosintaksia ya yambwa katika kishazi cha kiswahili

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Mofosintaksia ya yambwa katika kishazi cha kiswahili"

Copied!
168
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

'. . ". . . .

~OFOSINTAKSIA YAYAMBWA KATIKA IDsijAzI

eHA

KISWAHILI

TASNIFU

YA

BRENDA MIDIKA EGARA

TASNIFU HII

IMETOLEW A KATIKA IDARA YA KISW AHILI

KA TIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA KW A MADHUMUNI YA

KUTOSHELEZA BAADHI YA

MAHITAn

YA SHAHADA YA

(2)

IKIRARI

Tasnifu hii ni kazi yangu asilia na haijawahi kuwasilishwa katika chuo kikuu chochote kwa madhumuni ya kutuzwa shah ada yoyote.

EGARA BRENDA MIDlKA TAREHE

Tasnifu hii imetolewa kwa Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa idhini yetu kama wasimamizi:

2?Jos--/

ew

l

h

/

7

TAREHE DAKTARl ALICENY AMBURA MWIHAKI

IDARA YAKISWAHILl

DAKTARl JACKTONE OKELLO ONYANGO TAREHE

IDARA YA KISWAHILl

(3)

IKIRARI

Tasnifu hii ni kazi yangu asilia na haijawahi kuwasilishwa katika chuo kikuu chochote

kwa madhumuni ya kutuzwa shah ada yoyote. >-

.

Ifi.h

i

\U-.~

EGARA BRENDA MIDlKA TAREHE

Tasnifu hii imetolewa kwa Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa idhini yetu kama wasimamizi:

DAKTARI ALICE NYAMBURA MWlHAKI IDARA YA KISWAHILI

DAKTARI JACKTONE OKELLO ONYANGO TAREHE

(4)

TABARUKU ",-. j," . Kwa wazazi wangu wapendwa

Nawashukuru kwa kunihimiza na kunitia moyo niendelee na masomo.

Kwa mwanangu Ezekiel Imani Muyaka .. Kazi hii iwe kichocheo kwako kuthamini masomo.

(5)

SHUKRANI

Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake na kunipa afya njema wakati wa kukamilisha utafiti huu.-Shukrani zangu za dhati ziwaendee wasiniamizi wangu Dkt. Alice Mwihaki na Dkt. Jacktone Onyango kwa kunielekeza na kunipa

mwongozo. Mungu awabariki na awape moyo na uvumilivu wa kuendelea kuwasimamia na kuwaelekeza wanafunzi wengine. Shukrani zangu pia ziwaendee wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili kwa kunifundisha katika masomoyangu ya uzamili. Miongoni mwao

ni Prof. King'ei, Prof. Mbaabu, Prof. Ndung'o, Dkt.Wafula, Dkt. Masinde, Dkt. Ngugi, "-.<.. Dkt. Osore, Dkt. Arege, Dkt. Gakuo, Bi Mudhune na Mwl. Gathenji ambaye alinisaidia

-' -

..

sana kwa kuniazima vitabu vyake mwenyewe. Shukrani zingine ziendee Chuo Kikuu cha

Kenyatta kwa kunipa ufadhili wa kimasomo wa 'Vice Chancellor's Scholarship'.

Shukrani kwa babangu na mamangu kwa kunipa moyo, kuwa karibu na-kunivumilia wakati wa uandishi wa kazi hii. Nawashukuru kwa msingi wa elimu rnIioniwekea. Kwa ndugu zangu: Kabaji Egara, Ian Kilavuka, Nneka Kagai na Bahati Egara na binamu wangu Sheila Ozengo asanteni kwa kunitia mwoyo na kunifariji nilipokuwa ninakata tamaa. Nawashukuru kwa kunivurnilia na kunitia motisha kumaliza kazi hii. Mungu awe nanyi daima.

(6)

Lenna Nyandwaro, Festo Haule, Dorothy Kabaka, Kellen Muthoni, Joseph Kitheka, .Charless Omutimba, Benson Sululu, Hassan Makombo, Elizabeth Mue , Esther Chari,

. Nimrod Mburia, Cecilia Kihara, Oginda, Celestine Nanjala, Ntawiyanga Sylvain, James Mwilaria, Everlyne Onyango na Eliud Msusotsi. Kuwepo kwenu kulichangia katika ufanisi wa masomo yangu. Kila la heri mnapoendelea na safari hii ya usomi.

v

.,,~':.

..''.::.. ',.:' -"<.<'~: " .

(7)

IKISIRI

Utafiti huu ulinuia kuchanganua sifa za kimofosintaksia za yambwa katika kishazi cha Kiswahili. Vipengele vya kimofolojia hutangamana na sintaksia na kuibua michakato .inayochanganuliwa katika mofosintaksia.. Mofosintaksia kwa hivyo,··. ni.·utanzu

unaochunguza uhusiano uliopo kati ya mofolojia na sintaksia. Yambwa katika utafiti huu inafafanuliwa kama kirai nomino au kirai bainishi katika kishazi ambacho kuwepo kwake hutegemeamuundo wa kiarifu. Tafitiza yambwa katika lugha za Kibantu zimepatwa na changamoto .hasa katika kutumia dhana za kimapokeo 'yambwa' na 'yambiwa' katika kurejelea yambwa. Katika Kiswahili, kiarifu kinaweza kuchukua hadi vipengele vitatu vinavyokifuata bila kuwepo kwa ushahidi wowote wa kimofolojia unaofafanua viperigele husika. Vipengele vinavyokuja baada ya kitenzi ambavyo huchukua mfumo wa kirai nomino au kirai bainishi huwa ni yambwa au chagizo. Kutokana na haya, sifa za kisintaksia hutofautiana katika vishazi vilivyo na yambwa moja nalau mbili. Aidha, katika Kiswahili hadhi ya yambwa kama yambwa msingi au yambwa upili haijazingatiwa katika tafiti. Katika kuchanganua uasimetrialugha, dhana za "yambwa msingi" na "yambwa upili" hutumiwa kurejelea vipengele vya kishazi chenye yambwa changamano. Utafiti huu ulilenga kutambulisha uamilifu na sifa za kisintaksia za yambwa ya Kiswahili. K wa kutumia data ya Kiswahili, utafiti wetu ulinuia kubainisha sifa za .yambwa msingi na yambwa upili kwa kutumia vigezo vya majaribio vilivyotolewa vya uwakilishi yambwa na mpangilio wa maneno. Data iliyotumiwa katika utafiti ilikuwa ni vishazi sahili vilivyotolewa kutoka kwa vitenzi elekezi vya Kiswahili· ambavyo viliteuliwa kimaksudi. Vishazi huru vilitungwa na watafitiwa watatu baada ya kuwasilishiwa vitenzi elekezi. Nadharia ya Sintaksia Finyizi ilitumiwa kuchanganua vishazi husika. Uboreshaji wa nadharia ya Sintaksia Finyizi wa mwaka wa 2000 ili kuchunguza data ya upatanisho ndio ulituongoza katika uchanganuzi wa data. Utafiti huu una sura tano. Suraya kwanza inatoa utangulizi wa utafiti kwa kutoa maelezo ya usuli wa utafiti, suala lautafiti, malengo na maswali ya utafiti, tahakiki ya maandishi, misingi ya nadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili inachambua muundo wa kishazi cha Kiswahili. Katika sura ya tatu, utafiti unachunguza muundo na uamilifu wa yambwa katika Kiswahili. Sura ya nne inashughulikia uwakilishi yambwa katika Kiswahili. Sura ya mwisho inatoa. mahitimisho na mapendekezo ya utafiti zaidi. Uchanganuzi unaowasilishwa una umuhimu kwa isimu ya Kiswahili, wanafunzi wa lugha ya Kiswahili na isimulinganishi.

..; .

...:.

(8)

ABSTRACT·

This research examined the morpho syntactic properties of syntactic objects within the Kiswahili clause. Morphological properties of a language interact with syntax giving forth processes that are analyzed through morphosnytax. Morphosyntax is therefore defined as the interface between morphology and syntax. An object is

a

post verbal noun .. ··phrase/determiner phrase whose existence depends on the verbal structure. The study of

syntactic objects. in Bantu languages has encountered problems when applying the traditional notions of "direct" and "indirect" objects. The Kiswahili verb can take up to .three post verbal positions with the absence of morphological case or clearly definable

positions. Other post verbal elements that appear inthe form of noun phrases" or determiner phrases are either adjuncts or locatives. Additionally, in Kiswahili the primary hood and secondary hood of objects has not received considerable research. The terms ."primary object"and "secondary object" are sometimes used to refer. to the two .complements in a double object construction when speaking of asymmetric and.

symmetric languages. This research sought to identify features of Kiswahili syntactic objects from other post verbal elements. U sing the Kiswahili data, our study aimed at distinguishing the properties of secondary and primary objects using the criteria laid out of: word order and object-agreement. The data for the study was in the form of independent clauses generated from Kiswahili transitive verbs purposively selected. Independent clauses used in the study were generated by three respondents after being presented with the verbs. The clauses were analyzed using the Minimalist Program. The 2000 revision of the Minimalist Program to accommodate agreement phenomena guided the data analysis: The research is divided into five chapters. Chapter one gives the preliminary details of the research, that is, the background to the study, the research . problem, the objectives, literature review and the research methodology. Chapter two

analyzes the clausal structure of Kiswahili. In chapter three, the study discusses the . structure and function of the Kiswahili objects. In chapter four, Kiswahili object marking

is discussed. The last chapter gives the conclusion of the study and areas for further research. The analysis presented has theoretical, applied and practical benefits to Kiswahili linguistics, Kiswahili language learners and comparative linguists.

....:. ., ,',...<

. .j

(9)

B: Kibainishi

E: Kielezi

Ele: Elekezi

H: Kihusishi

ha: Hamo

KB: Kirai Bainishi

KE: Kirai Elezi

KH: Kirai Husishi

KN: Kirtti Nomino

KNJ: Kirai Njeo

KP: Kirai Patanishi

KSH: Kirai Shamirishi

KV: Kirai vumishi

N: Nomino

NJ: Njeo

P:Patanishi

T: Kitenzi

SF: Sintaksia Finyizi

SH: Kishamirishi

V: Kivumishi

ORODHA YA VIFUPISHO

(10)

Anafora: . . Dhima: Kanuni: Kiarifu: . Klima: Kisabaki: Kishazi: Mofolojia:

MAELEZO YA DHANA MUHIMU

Kijenzi cha kisarufi ambacho huhitaji kufungwa kwa kisabiki chake ili

maana ifasirike. .~.

.Uamilifu wa kipengele cha kisintaksia kulingana na nafasi yake katika kishazi. Dhima huwa ni uhusiano wa kisintaksia au kisemantiki baina ya virai nomino au virai bainishi na kiarifu katika muundo wa kishazi huru. Sifa bia zinazotawala mifumo ya sarufi za lugha zote za binadamu, kwa mujibu wa Sarufi ZaIishi.

. ~;

Kundi la maneno au neno linaIotoa taarifa kuhusu kiima.

Mojawapo ya dhima za kisintaksiakatika muundo wa kishazi huru . Kipashio ambacho hurejelewa na kipashio kingine ili kipate maana.

Fungu la maneno lenye muundo wa kiima na kiarifu ambaIo limo ndani ya sentensi au umbo la sentensi sahili.

Taaluma ya kiisimu inayoshughulikia uchambuzi na uchunguzi wa kanuni na mifumo inayohusu upangaji wa mofimu mbalimbali ili kuunda maneno

katika lugha. .

Mofosintaksia: Taaluma ya kiisimu inayoshughulikia uchaganuzi wa uhusiano uliopo baina ya mofolojia na sintaksia.

pro: Viwakilishi nafsi viambata.

Semantiki: Taaluma ya kiisimu inayohusu uchanganuzi wa maana inayojitokeza katika leksimu nalau sentensi

Sintaksia: Taaluma ya kiisimu inayochuguza kanuni zinazotumiwa katika muundo wa maneno, virai na vishazi

Yambwa: Istilahi inayorejelea kitendwa au kitendewa katika muundo wa kishazi huru. Istilahi hii hurejela kirai nomino au kirai bainishi ambacho huja baada ya kiarifu. Yambwa hujidhihirisha kama yambwa msingi au yambwa upili katikakishazi huru.

Yambwa msingi: Kipashio kinachodhihirisha sifa ya kuwa kirai nomino kinachokuja mara tu baada ya kiarifu, na kinawakilishwa kwenye kiarifu kupitia mofimu wakilisho yambwa.

Yambwa upili: Kirai nomino kinachokuja baada ya kirai nomino cha kwanza cha yambwa, hakiwakilishwi kwenye kiarifu kupitia mofimu wakilishi yambwa.

(11)

ORODHA YAMAJEDWALINA VIELELEZO.·

(1.2) Kielelezo cha Uidadishi ; :.:~ ~ .22

(1.2) Vielelezo vya Muungano wa Virai ..~ : : :: .24

(1.3) Kielelezo cha Muungano wa Virai :..: : ~ · , ~ 25

(1.4) Kielelezo cha Hatima ya Uhamisho ; : . : 27

(2.1) Jedwali la Ngeli za Kisintaksia : .41

(2.2) Jedwali la Vijikategoria vya Kitenzi ::.: : : .: .43

(2.3) Jedwali la Vijikategori vya Kivumishi ,..~ .45

(2.4) Jedwali la Vijikategoria vya Kielezi .46

(2.5) Jedwali la Vijikategoria vya Kihusishi : .47

(2.6) Jedwali la Vijikategori vya Kibainishi .49

(2.7) Jedwali la Vijikategoria vya Kipatanishi : 50 (2.8) Jedwali laVijikategoria vya Kishamirishi 51 '

(2.9) Jedwali la Maumbo ya Kirai Nomino 53

(2.10)Jedwali la Maumbo ya Kirai Tenzi ~ 56

(2.11) Jedwali la Maumbo ya Kirai Vurnishi : 59

(2.12) Jedwali la Maumbo ya Kirai Husishi 61

(2.13) Jedwali lei Maumbo ya Kirai Bainishi 63

(2.14) Jedwali la Maumbo ya Kirai Patanishi 65 (3.1) Jedwali la Maumbo ya Kirai Nomino Yanayowakilisha Yambwa 78 (3.2) Jedwali la Maumbo ya Kirai Bainishi Yanayowakilisha Yambwa 85 (3.3) Jedwali la Dhima Maana ya Mtendewa au Kitendewa , 92

(12)

(3.6) Jedwali la Dhima Maana ya Mfaidi

.

.

,...•...

>:.:...• ,

95 (3.7) Jedwali la Dhima Maana ya.Lengo.. : ; : :...•..~ ,~; ~.~.96.

. . . .

(3,.8)Jedwali -la Dhima Maana ya Mahali : ~..•...: 97

. -.' .

(3.9) Jedwali la Dhima Maana ya Mpokezi

au

Kipokezi . , : 98

(4.1) Jedwalila Wakilisho Yambwa katikaKiswahili.: : :..:;.: ;...•.... : " :..J02·

" . .' . .

(4.2) Jedwali la Wakilisho Yambwa Sahili katika Yambwa Sahili ~..: ~ : :104 . (4.3) Jedwali la Wakilisho Yambwa na Vibainishi vya Kipronomino ..: : 105

(4.4) Jedwali la Mpangilio wa Hoja za Yambwa : 112

(4.1) Kielelezo cha Udhihirikaji wa Yambwa Msingi na Yambwa Upili .115

(4.2) Kielelezo cha Upatanishi wa Kisintaksia wa Yambwa ; 117

(4.3) Kielelezo cha Upatanishi wa Kisintaksia wa Yambwa 117 .

(13)

YALIYOMO .~;.,

Ikirari , ii

.. Tabaruku : . ·iii

Shukrani.- . iv

Ikisiri ~ . vi

Abstract vii

Orodha ya Vifupisho , : ~ viii

Orodha ya Majedwali na Vielelezo : ; · x

Yaliyomo , xii

SURA YA KWANZA: UT ANGULIZI ~ 1

1.0Usuli wa Utafiti 1

1.1 Suala la Utafiti 4

1.2 Maswali ya Utafiti 5

1.3Malengo ya Utafiti 6

1.4Upeo na Mipaka ya Utafiti 6

1.5 Sababu za Kuchagua Mada : : 9

1.6Tahakiki ya Maandishi 11

1.6.1Tafiti Bayana zaMofosintaksia katika Kiswahili na Lugha nyingine zaKibantu ...12

1.6.2 Tafiti Bayana za Yambwa katika Kibantu .15

1.7Misingi ya Nadharia 20

1.7.1 Hatua za U changanuzi wa Sentensi 21

1.7.1.1 Uidadishi 22

(14)

1.7.1.3 Uharnisho : 26

. ,

(1.4) Kielelezocha Hatima ya Uhamisho : : : ~ ~ 27

1.7.2 Kanuni za Sintaksia Finyizi : · : 28

.

1..

8.0

Mbinu

za Utafiti

31

.

.

~

1.8.1 Mbinu za Ukusanyaji wa Data 32

1.8:2 Mbinu za Uchanganuzi Data 35

1.8.3 Mbinu za Uwasilishaji Data 37.:

Hitimisho 38

SURA YA PILI: KISHAZI CHA KISW AHILI : 39

2.0 Utangulizi : : 39

2.1 Kategoria za Maneno ya Kiswahili ~ : .39

2.1.1 Jopo la Kategoria Leksia .40

2.1.1.1. Kategoria yaNomino 40

2.1.1.2 Kategoria ya Kitenzi .42

2.1.1.3 Kategoria ya Kivumishi .44

2.1.1.4 Kategoria ya Kielezi .45

2.1.1.5 Kategoria ya Kihusishi .47

2.1.2.Jopo la Kategoria Sarifu : 48

2.1.2.1.Kategoria ya Kibainishi , .48

2.1.2.2 Kategoria ya Kipatanishi 49

2.1.2.3 Kategoria ya Kishamirishi 50

2.2 Muundo Kirai 52

2.2.1 Jopo la Kirai Leksia 52

2.2.1.1 Kirai Nomino : 53

(15)

2.2.1.2

.

Kirai Tenzi : :

55

.

2.2.1.3

KiraiVumishi ·...•....: i•••••••••••••.•••••••••••••••. :•••••.•• ; ••.~•••••.••••••.•• 58

2.2.1.4

Kirai Elezi : : ;

60

2.2.1.5

.

Kirai Husishi :

61

2.2.2

Jopo la Kirai Sarifu ;

62

2.2.2:1 Kirai

Bainishi

63

2.2.2.2

Kirai Patanishi

,65

2.2.2.3

Kirai Sharnirishi ;

67

2.3

MuundoKishazi 68

2.4

Uamilifu wa Kisintaksia katika Kishazi ;

73

2.4.1

Dhima ya Kiima : ;

73

2.4.2

Dhima ya Yambwa ~

74

Hitimisho

74

SURAYA TATU: MUUNDO NA UAMILIFU WA YAMBWA KATlKA KISWAHILI 76

3.0

Utangulizi

76

3.l Muundo wa Yambwa katika Kiswahili

76

3.1.1 Yambwa kama Kirai Nomina katika Kiswahili

77

3.1.1.1 Noniino Pekee 78

3.1.1.2 Nomina naNomina · 79

3.1.1.3 Nomina na Kivumishi 80

3.1.1.4 Nomina na Kibainishi 81

3.1.l.5 Nomina naKirai Husishi 82

3.1.2

Yambwa kama Kirai Bainishi katika Kiswahili 85

3.1.2.1-Kibainishi Pekee 86

" . .:. :.,

(16)

3.1.2.2 Kibainishi na Nomino 87 .-...

3.1.2.3 Kibainishi na Kirai Nomino 88 ,.

~...•

. . '.

3.2Uamilifu wa Yarribwa katika Kiswahili : ~ ~.., 90

3.2.1Dhima Maana ya Mtendewa au Kitendewa ~ 91

3.2.2Dhima Maana ya Maudhui ~ 92

3.2.3Dhima Maana ya Hisifu 94

3.2.4Dhima Maana ya Mfaidi 95

3.2.5 Dhima Maana ya Lengo : 96

3.2.6 Dhima Maana ya Mahali 97

.3.2.7 Dhima Maana ya Kipokezi au Mpokezi 97

Hitimisho ; : ...;..99

SURA YA NNE:

UWAKILIsm

YAMBWA KATlKA KISWAHILI

101

4.0Utangulizi ·..: .: 101

4.1 Wakilisho Yambwa Sahi1i katika Kishazi 101

4.2.Wakilisho Yambwa Changamano katika Kishazi 106

4.3 Utambuzi wa Yambwa Msingi na Yambwa Upili 110

4.3.1 Kigezo cha Uambishaji Wakilisho Yambwa 110

4.3.2. Mpangilio wa Hoja za Yambwa kwenye Kishazi 112

4.3.3Ufafanuzi wa Uasimetria Yambwa Kisintaksia 114

4.4 Upatanishi Yambwakatika Kiswahili 116

Hitimisho 120

SURA YA TANO: HITIMISHO

121

5.0 Utangulizi 121

5.1 Matokeo yaUtafiti 124

(17)

5.2 Mahitimisho ya Utafiti .- 132

5.3Mapendekezo ya Utafiti Zaidi 134

Marejeleo : 137

KIAMBATISHOA: DATA YA UTAFITI , 143

KIAMBATISHO B:VIGEZO VY A KUTA THMINI W AKILISHO YAMBWA 151

(18)

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI ':'..:;'.

1.0 Usuli wa Utafiti

Dhana ya mofosintaksia inarejelea kiwango cha uchanganuzi wa kisarufi kinachozingatia

baadhi ya mahitaji ya mofolojia kuegemea utanzu wa sintaksia. Mofosintaksia imetokana

na mabadiliko katika mitazamo ya kiisimu kutoka enzi ya Sarufi Muundo kufikia Sarufi

Zalishi.Chomsky (1965) aliasisi dhana ya mofosintaksia katika jitihada .za kukosoa mtazamo wa Umuundo kuhusu upeo wa sarufi katika isimu jumulifu. Umuundo

ulisisitiza uchanganuzi wa lugha bila ufafanuzi wa sheria zinazotawala lugha. Mtazamo

huu wa Umuundo ulipingwa na Chomsky (ibid) kwa kuwa ulifafanua vipengele vya

kisarufi bila kueleza sheriahusika.

Sayansi jarabati .iliyoendelezwa katika kame ya ishirini iliwasisimua wanaisimu waliotumia mbinu za kijarabati kuchanganua lugha. Wanamuundo, wakiongozwa na

Mwanaisimu wa Marekani, Leonard Bloomfield (1933) walijikita katika ujarabati.

Wanaisimu wa Umuundo walitambulisha viwango vinne vya muundo wa kisarufi:

fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Mofolojia katika umuundo ilitambulishwa

kama kiwango mahsusi cha uchanganuzi wa sarufi.

Chomsky (ibid) katika kuasisi nadharia ya Sarufi Zalishi hakutarnbulisha mofolojia kama

kiwango bayana cha kisarufi. Badala yake, aligawa kiwango cha uchanganuzi cha

mofolojia ili fungu moja lichanganuliwe katika fonolojia na lingine lichanganuliwe na

(19)

sintaksia. Tangu mgawanyiko huo, fungu lililohusishwa na sintaksia lilipelekea kuzaliwa

kwa dhana ya mofosintaksia. Anderson (1992:99) akifafanua dhana ya mofosintaksia

:..,.

.anaeleza: .". :

Maneno yana muundo wa kimofosintaksia. Muundo huu wa kimofosintaksia

hujumuisha sifa zote (na sifa mahsusi) ambazo huwa ni muhimu katika sheri a za

uundaji wa maneno na sintaksia. Maelezo msingi kuhusu neno ambayo

yamejumuishwa katika muundo wa kimofosintaksia ndio hupatikana katika

michakato ya kisintaksia. Yale maelezo rrisingi kuhusu sintaksia yanayotolewa

katika muundo wa kimofosintaksia ndio hupatikana katika mofolojia. Muundo wa

kimofosintaksia wa neno ndio kipengele pekee ambacho huonekana kwa

sintaksia. Njia pekee ambayo sintaksia inaweza kuathiri muundo wa neno ni kwa

kubadilishabadilisha muundo wa kimofosintaksia wa neno hilo.· (Tafsiri ya

mtafiti)

Maelezo haya yanadhihirisha kuwa sifa za kimofolojia za neno huathiriwa na mazingira

ya kisintaksia ambamo neno hilo linapatikana. Maneno pia lazima yaonekane katika

michakato ya kisintaksia ili yaweze kutenda kazi katika lugha. Maelezo haya ya

Anderson (ibid), kwa hivyo ni ushahidi msingi kuwa sintaksia huathiri muundo wa neno

na uamilifu wake.

Baada ya kuasisiwa na Chomsky (ibid) dhana ya mofosintaksia imeendelezwa zaidi na

wataalamu mbalimbali kuhusiana na mada za ufunzaji na ujifunzaji wa lugha, upatanisho

wa kiima, upatanisho wa yambwa, mnyambuliko wa vitenzi, na dhima mbalimbali za

kisintaksia na/au kisemantiki (Alexidou 1997, Bearth 2003, Buell, 2005, na Riedel 2009).

Linalodhihirika katika tafi~i zilizotajwa ni kuwa mofosintaksia inachunguza mwingiliano

(20)

..Tafiti za awali za kimofosintaksia kama Greenberg (1963) na Nicholas (2008) zililenga kuchunguza vipengele vipana zaidi vya kimofolojia. Vipengele hivi vilidhihirika kwa

'uwazi zaidi vikiwemo sifa za lugha ambishi au lugha ambishi bainishi. Maendeleo ya

mtazamo wa Sarufi Zalishi uliotenganisha sifa bia na kanuni za lugha yamechangia

katika kukuza tafiti za kanuni za lugha. Tafiti zinazotumia Sarufi Zalishi kama mtazamo

.wa uchanganuzi hulenga kuchanganua vipengele finyu vya kimofosintaksia katika lugha.

Kulingana na Marten, Kula, na Thwala (2007) tafiti nyingi za kimofosintaksia katika

lugha za Kibantu kwa misingi ya Sarufi Zalishi zinalenga vipengele vidogozaidi

ambavyo hudhihirika zaidi katika lugha hizi. Mojawapo ya vipengele hivyo ni yambwa.

Kwa hivyo, uchanganuzi wa kimofosintaksia utakuwa msingi mwafaka wa utafiti kuhusu

yambwa.

Yambwa ill mojawapo ya dhima za kisintaksia ambayo huwakilishwa kwa kirai nomino au kirai kibainishi kinachofuata kitenzi (kiarifu) katika sentensi sahili (Morolong na

Hyman 1977, Hyman and Duranti 1982, Kimenyi 1978, Baker 1988 na Riedel 2009).

Sentensi sahili (kishazi huru) inaweza kujumuisha virai nomino au virai bainishi .viwili

vinavyofuata kiarifu. Katamba (1993) anaeleza kuwa kimuundo, kishazi huru huwa na

aina tatu za yambwa: yambwa msingi, yambwa upili, na yambwa husishi. Iwapo kuna virai nomino/bainishi viwili au zaidi vinavyokuja baada ya kiarifu katika kishazi huru,

mara nyingi mojawapo huwakilisha yambwa msingi na nyingine yambwa upili (Katamba, 1993). Idadi ya yambwa hutegemea muundo wa kiarifu. K wa hivyo, kiarifu kina jukumu la kupanga dhima yambwa na uhusika kwa jumla. Mbali na jukumu la

(21)

kisintaksia la kukamilisha kishazi kwa madhumuni ya usarifu katika lugha, Y1lIIlbwaina

thamani ya kuwasilisha dhima maana. Dhima maana ni dhana za kisemantiki kama vile

maudhui yanayoweza kuhusishwa na yambwa au kiima.

'...~.. .' ..

Tafiti za yambwa ya Kibantu zimeshughulikia aina za yambwa, yambwa katika tungo

zenye yambwa changamano, yambwa na mofimu wakilisho yambwa, yambwa katika

kudhihirisha: uasimetria lugha, na yambwa katika tungo rejeshi miongoni mwa nyingine.

Wataalamu wengi wamefanya utafiti kuhusu yambwa ya Kibantu katika kushughulikia

mada zilizotajwa, (Mchombo 1987, Bresnan na Moshi 1990, Marten, Kula, na Thwala

2007a na 2007b, Riedel 2009, na Marten na Kula 2012). Vipengele ambavyo vinazua

ukosefu wa maafikiano katika usomi kuhusu yambwa ya Kibantu ni: muundo wa

yambwa, hadhi ya yambwa msingi na yambwa upili katika vishazi vya Kibantu, aina za

yambwa katika vishazi vya Kibantu, upatanisho wa yambwa, uwakilishi yambwa na

dhima maana za yambwa ya Kibantu. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa kutafiti vipengele

mbalimbali vya yambwa katika Kiswahili ili kuchangia ufahamu wa yambwa katika

kishazicha Kibantu.

1.1 Suala la Utafiti

Utafiti huu ulikusudia kuchanganua muundo na uamilifu wa yambwa katika Kiswahili.

Muundo wa kiarifu katika kishazi cha Kiswahili huathiri vijenzi vinavyokifuata. Kwa

kurejelea mofosintaksia, kiarifu cha Kiswahili kinaweza kudhibiti virai nomino/virai

(22)

huwakilisha yambwa rnsingi na yambwa upili. Tafiti zirnehusisha yambwa na rnuundo

wa kisintaksia wa kishazi ingawa kuna utata katika kutambua rii kirai nomino kipi

. . . .' . '. . ;." .

kinawakilisha yarnbwa rnsingi na yarnbwa upili katika kishazi cha Kiswahili. Utata wa

ukosefuwa rnaafikiano urnetokana na rnuundo ambao yarnbwa huchukua katika vishazi

vya Kibantu. Kuwepo kwa utata huu kurneashiria kuwa utafiti zaidi kuhusu ubainishi wa

yarnbwa rnsingi na yarnbwa upili katika Kiswahili illrnuhirnu.

Tafiti rnbalirnbali zirnefanyiwa vigezo vya kutarnbulisha yarnbwa rnsingi na yarnbwa

upili katika kishazi cha Kibantu (Morolong na Hyman 1977, HYman na Duranti 1982,

Bresnan na Moshi 1990, Marten, Kula na Twala 2007). Vigezo husika hata hivyo

havijajaribiwa katika sintaksia ya Kiswahili. Utafiti huu ulitathrnini na kubainisha vigezo

vya kutarnbulisha yarnbwa rnsingi na yarnbwa upili kwa kujaribisha vigezo husika

kwenye data ya Kiswahili. Hivyo basi, uchanganuzi wa kanuni za kisintaksia na

kisemantiki za yarnbwa ya Kiswahili ulielezwa kwa kuzingatia rnisingi ya nadharia ya

Sintaksia Zalishi Finyizi (Sintaksia Finyizi). Katika kuangazia suala hili, utafiti huu

uliazirnia kujibu rnaswali rnanne yanayohusiana na rnofosintaksia ya yambwa ya

Kiswahili

1.2 Maswali ya Utafiti

Utafiti huu ulinuia kujibu maswali rnanne yafuatayo:

1. Kuna aina ngapi za yarnbwa katika kishazi cha Kiswahili?

2. Yarnbwa inawakilishwa narnna gani katika kiarifu cha Kiswahili?

(23)

3.Kanuni zipi zinatawala matumizi ya yambwa katika kishazi cha Kiswahili?

4. SintaksiaFinyizi ina utoshelevu upi katika uchanganuzi wa yambwa ya Kisw. . ahili? .

1.3 Malengo ya Utafiti

Utafiti huu ulidhamiria kutimiza malengo yafuatayo:

1. Kubainishaaina za yambwa katika kishazi cha Kiswahili

2. Kuchanganua uwakilishi yambwa katika kiarifu cha Kiswahili

3.Kujadili kanuni zinazotawala matumizi ya yambwa katika kishazi cha Kiswahili

4. Kutathmini utoshelevu wa Sintaksia Finyizi katika Uchanganuzi wa yambwa ya

Kiswahili.

1.4Up eo na Mipaka ya Utafiti

Utafiti wa kimofosintaksia ungetarajiwa kuchunguza vipengele vyote vya

kimofosintaksia katika lugha. Ilivyodokezwa hapo awali (Tazama 1.1) vipengele

vinavyoweza kufanyiwa utafiti wa kimofosintaksia ni pamoja na upatanisho wa kiima,

upatanisho wa yambwa, ujifunzaji lugha, mnyambuliko ya vitenzi, urejeshi, na

uambishaji, miongoni mwa mada zingine. Kazi hiihaikuzingatia vipengele vyote vya

kimofosintaksia bali ilijikita katika yambwa katika kishazi huru cha Kiswahili. Mada za

kimofosintaksia za ujifunzaji lugha, urejeshi na uambishaji ziliaachwa kwa sababu

zinahusu zaidi vipengele vingine vya lugha ya Kiswahili bali sio kipengele cha yambwa.

Kazi hii ilijikita katika kuchunguza muundo na uamilifu wa yambwa, wakilisho yambwa

(24)

viwango vya kimofolojia, kisintaksia, na kisemantiki. Mada hizi zilichaguliwa kutokana

na upekee wake katika kushughulikia mofosintaksia ya yambwa ya Kiswahili kikamilifu.

Utafiti huu ulijikita katika. kutathmini muundo wa yambwa. Kigezo ambacho

kilidhihirisha maumbo ya kirai riomino au kirai bainishi ambayo huwakilisha yambwa.

Uamilifu wa yambwa ulitathminiwa kwa ubainishaji wa dhima maana za yambwa katika

.Kishazi. Muundo na uamilifu wa yambwa ulibainishwa katika vishazi sahili ambavyo

matumizi yakeyalionyesha mahusiano ya vijenzi kwa uelekevu zaidi kuliko vishazi

vingine.

Uchanganuzi wa mofosintaksia ya yambwa ulifanywa kwa kuzingatia tanzu tatu za

kisarufi za: mofolojia,sintaksia, na semantiki. Tanzu hizi zinachangiana na

kukamilishana ingawa kwa kadiri tofauti. Katika utafiti huu, tulitambulisha kuwa

muundo wa kimofolojia wa neno ni muhimu kwa sintaksia, kwa vile sintaksia ndio

imehusishwa zaidi katika tafiti za kimofosintaksia. Hivyo basi, sintaksia ilizingatiwa

zaidi katika kuchunguza yambwa kwa kurejelea kishazi huru cha Kiswahili. Kwa kuwa

yambwa huwasilishwa kwa kirai nomino au kirai bainishi, utafiti ulihusisha semantiki

kutokana na hoja kuwa kirai nomino au kirai bainishi kinachodhibitiwa na kiarifu

hutekeleza dhima tofauti za kisemantiki katika kishazi.

Kama wanavyoshadidia Marten, Kula, na Thwala (2007a), utafiti wa mofosintaksia ya

yambwa unahitaji uzingatie kipengele cha uwakilishi yambwa ili kutoa mwanga zaidi

(25)

katika kuchunguza na kuelewa kimuundo na kiuamilifu mofosintaksia ya yambwa ya

Kiswahili. Lengo mojawapo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza uwakilishi yambwa

katika kishazi huru cha Kiswahili. Marten, Kula na Thwala (ibid)m wanaviainisha vigezo

kumi na tisavya kutafiti mofosintaksia ya yambwa kwa mujibu wa uwakilishi yanibwa

katika Kibantu. Vigezo hivi vinaainishwa katika makundi matano: muundo wit wakilishi

yambwa, mofimu wakilishi katika:: yambwa changamano, tungo rejeshi, upatanisho wa

virai nomino, nit wakilisho yambwa, na toni ya lugha. Katika utafiti wetu tulichunguza

vigezo kumi na vinne kama vinavyoanishwa katika utafiti wa Marten, Kula na Thwala,

(ibid). Vigezo hivi vilijumuishwa katika makundi mawili ya muundo wa wakilishi, na

wakilishi yambwa katika yambwa changamano. Uteuzi wa vigezo hivi ulifanywa

kutokana na jinsi vigezohivi viwili vilivyoshughulikia mada yetu ilhali vigezo vitatu

vilivyosaliavinarejelea vijenzi vingine vya kishazi.

Kiswahili kina lahaja kumi na nane ambazo hutofautiana kimsamiati na kwa kiwango

kidogo kisarufi (Stigand 2013). Kwa kurejelea matumizi ya wakilishi yambwa kuna

tofauti ambayo hupatikana kati ya lahaja za Tanzania Bara na Pwani ya Kenya. Lugha

iliyotumiwa katika utafiti huu ilikuwa ni Kiswahili Sanifu (Mbaabu 2007). Kiswahili

Sanifu kilihusika katika uchunguzi kwa kuzingatia malengo ya utafiti huu pamoja na

kutolea mifano husika. Idadi ya vigezo vilivyojadiliwa vya mofosintaksia ya yambwa

vilitegemea jinsi vinavyodhihirika katika Kiswahili Sanifu. Kuna madai kwamba

mahitimisho yaliyoafikiwa kuhusu Kiswahili Sanifu yanatosheleza mahitaji ya uchunguzi

(26)

1.5 Sababu za Kucbagua Mada

Utafiti huu una umuhimu wa kisarufi, kinadharia, kitumikizi na kiutendakazi katika . Kiswahili. Kwa upande wa sarufi ya Kiswahili, uchaguzi wa madahii ulitokana na

mchango wake katika usomi wa isimu ya Kiswahili. Kisintaksia, utafiti huu ulikusudia kupambanua na kudhihirisha wazi zaidi kanuni za mofosintaksia yayambwa ya Kiswahili kwa kutumia vishazi vya Kiswahili. Maumbo tofauti ya vishazivyenye yambwa yalidhihirishwa katika utafiti. Kutokana na maumbo hayo, ilionekana kuwa; yambwa huathiri muundo ya sintaksia ya Kiswahili. Utafiti huu pia ulibainisha njia ambazo yambwa huwakilishwa katika kishazi cha Kiswahili. Katika hali hii utafiti huu ulipata nafasi yake katika ufafanuzi wa sarufi ya Kiswahili kupitia uchanganuzi wa kipengele cha yambwa katika kishazi.

Kwa upande wa nadharia, utafiti huu uliitathmini nadharia ya Sintakisia Zalishi Finyizi katika kuchanganua kipengele cha yambwa ya Kiswahili. Nadharia yoyote ya kisarufi hunuia kueleza kanuni za lugha ya mwanadamu. Hata hivyo, wazungurnzaji huchagua kanuni wanazotumia pamoja na sheri a husika. Tafiti zimeonyesha kuwa baadhi ya vipengele vya sarufi huathiri sintaksia ya Kiswahili. Kwa kuwa yambwa huathiriwa na vijenzi vya kishazi, utafiti huu ulichanganua kipengele cha yambwa kinadharia kwa kutumia nadharia ya Sintaksia Finyizi (Chomsky 2000 na 2001) ambayo hujumuisha kipengele cha upatanisho yambwa. Kuna umuhimu wa kutafiti lugha za Kiafrika ili kutathmini nadharia zinazotumiwa kuchanganua vipengele vya lugha. Kwa ambavyo, nadharia nyingi ambazo zimeibuka zimetumiwa zaidi katika kutathmini Kiingereza,

(27)

utafiti huu ulionyesha utoshelevu wa nadharia ya Sintaksia Finyizi katikakutathmini

yambwa ya Kiswahili. Utafiti umechangia katika kukuza mofosintaksia ya Kiswahili kwa

kudhihirisha kanuni za upatanisho yambwa. kama inavyoelezwa katika rmsmgi ya

Sintaksia Finyizi.

Kwa kuzingatia tafiti zilizopo katika lugha za Kibantu, ilionekana kuwa kuna tafiti

chache ambazo zimeshughulikia mofosintaksia ya.vipengele vya kisarufi vya Iugha za

Kibantu. Tafiti nyingi kuhusu yambwa katika Kibantu zimetafiti uwakilishi yambwa.

Tafiti zingine zimehusika na kuchunguza na kulinganisha yambwa kwa mtazamo

linganishi na lugha kama vile Kichichewa na Kirundi. Ingawa tafiti hizi hazichanganui

lugha ya Kiswahili kimahsusi, maelezo muhimu yalitokana na tafiti hizo. Kwa kutumia

data ya vishazi vya Kiswahili, uchunguzi huu uliweza kutoa uchanganuzi wa yambwa

katika vishazi .mbalimbali vya Kiswahili. Kulingana na Meinhof (1915) ipo haja ya

kutafiti lugha mahsusi ili kutoa ujuzi bora zaidi wa lugha hasa za Kibantu. Matokeo ya

utafiti huu yataweza kutumiwa kwa madhumuni ya isimu linganishi na watafiti wengine

na kuchangia katika weledi wa isimu ya lugha za Kibantu.

Maelezo muhimu kuhusu ujifunzaji na ufundishaji wa lugha ya pili yalitolewa katika

utafiti huu. Kiswahili ni lugha ifunzwayo katika shule za msingi nchini Kenya, Uganda,

Tanzania na Rwanda. Lugha ya Kiswahili pia ni lugha rasmi ya Kenya na Tanzania.

Isitoshe, Kiswahili hufunzwa katika nchi za Magharibi na Mashariki kama vile Marekani,

(28)

hujumuisha somo la Kiswahili kama somo la lazima. Utafiti huu kwa hivyo, ulichangia

katika weledi wa vipengele vya kisintaksia ambavyo hudhihirisha matumizi ya yambwa.

Kipedagojia, utafiti huuulichangia katika ufuridishaji wa masomo ya uchanganuzi wa

sentensi na vijenzi vya sentensi ya Kiswahili. Matokeo ya utafiti huu yatachangia katika

kusaidia kufunza Kiswahili kama lugha ya pili.

Utafiti huu una mchango katika kuifahamu zaidi yambwa ya Kiswahili kimuundokwa

namna inavyodhihirika katika vishazi. Mtazamo wa kimofosintaksia umeongeza maarifa

zaidi kuhusu vipengele finyu zaidi vya kiisimu vya Kiswahili kwa ujumla. Wataalamu

wengine watahamasika zaidi kuendeleza tafiti za kiisimu katika usomi wa vipengele vya

kimofosintaksia katika Kiswahili. Vilevile utafiti huu utawawezesha wataalamu

kuendeleza taaluma ya nadharia za kiisimu kwa kurejelea Kiswahili kutokana na

mofosintaksia yake ya yambwa. Umuhimu wa utafiti huu kinadharia na kitumikizi, na

kimaandishi umetokana na tahakiki ya maandishi mbalimbali kuhusu mofosintaksia na

yambwa.

1.6 Tahakiki ya Maandishi

Tahakiki ya maandishi ilijikita katika vipengele viwili vikuu: maandishi kuhusu tafiti

zinazofafanua mofosintaksia katika Kibantu na Kiswahili, na maandishi kuhusu tafiti za

yambwa katika Kibantu na Kiswahili. Tahakiki kuhusu mofosintaksia ilitambua kuwa

kunazo tafiti ambazo zimefanywa zinazoonyesha uwiano na utangamano wa mofolojia na

sintaksia. Tafiti zingine zilijikita katika mofosintaksia kama kipengele mahsusi cha

11

KE

... ","-rr •.... /'·-~··f\R

(29)

uchanganuzi wa kisarufi. Katika tahakiki hii, tafitikatika baadhi ya lugha za Kibantu na

Kiswahili kuhusu mofosintaksia na yambwa zilichaganuliwa kwa kurejelea malengo ya

mtafiti,matokeo na mahitimisho ya utafiti wake.

1.6.1 Tafiti Bayana za Mofosintaksia katika Kiswabili naLugha nyingine za Kibantu

Mofosintaksia ni mseto wa tanzu sarufi za lugha ambazo hufuma misingi ya kimofolojia

katika sintaksia (Taz 1.0). Tahakiki kuhusu maandishi ya mofosintaksia ilichunguza

maswali matatu ambayo yalifafanua dhana ya mofosintaksia katika utafiti wa lugha:

maeneo ya utafiti wa mofosintaksia, lengo la uchanganuzi wa kimofosintaksia, na athari

zauchanganuzi wa kimofosintaksia katika lugha.

Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu mofosintaksia katika Kiswahili na baadhi ya lugha

za Kibantu. Kuna tafiti ambazo zimejikita katika mofosintaksia moja kwa moja

(Mudhune 1994, Buell 2005, Mwangi 2001, na Kariuki 2012), ilhali tafiti zingine

zimelenga kufafanua uwiano na utangamano wa mofolojia na sintaksia (Vitale 1981).

Baadhi ya tafiti zimeshughulikia ufundishaji wa vipengele vya kimofosintaksia na

mnyambuliko wenye athari za kimofosintaksia katika lugha za Kibantu. Wataalamu wa

tafiti hizi wanaafiki ana kuwa katika kuchanganua vipengele mbalimbali vya

(30)

Buell (2005) alichunguza mada mbalimbali za kimofosintaksia na jinsi huathiri muundo

wa.kiarifu cha Kizulu. Baadhi ya masuala ya kimofosintaksia ya kitenzi cha Kizulu

aliyoyashughulikia BUell (ibid) ni pamoja na mizizi ya vitenzi, kauli za mnyambuliko

kama vile kauli ya usababishi na kauli ya kutendeana, uhusiano baina ya kauli za

mnyambuliko na uambishaji katika mizizi ya vitenzi. Uchunguzi huu unaafiki kuwa

maneno hutokea na kuathiriwa na mazingira ya sintaksia. Kutokana na uundaji wa

maneno, ilidhihirika kuwa kadiri mnyambuliko wa vitenzi unavyoongezeka kwenye

mzizi wa kitenzi cha Kizulu ndivyo muundo wa kishazi unavyoathirika. Muundo huu

huathirika aidha, kwa kuongeza au kupunguza hoja zinazokuja baada ya kiarifu. Utafiti

wa Buell (ibid) ulikuwa na umuhimu kwa sababu ulihusu taratibu za athari za

kimofosintaksia za muundo wa kiarifu katika Kizulu. Tofauti na utafiti wetu, kazi yake

ilichanganua athari za mnyambuliko kwenye kishazi, huku utafiti wetu unalenga

kuchunguza namna ambavyo vipengele ambavyo huja baada ya kia~ifu huathiriwa na

kuathiri sintaksia.

Kazi ya Vitale (1981) iliwasilisha uwiano na utangamano wa mofolojia na sintaksia

katika Kiswahili kwa kutumia nadharia ya Sarufi Geuza Maumbo. Vitale (ibid)

alitathmini vipengele ambavyo hushughulikiwa na mada ya mofosintaksia vikiwemo

kauli tenda, kauli ya kutendeana na kauli tendewa, usababishi, urejeshi, uundaji wa

maneno, sintaksia ya umoja na wingi na upatanisho wa kisarufi. Utafiti wa Vitale (ibid)

ulichanganua vipengele hivi kwa kuonyesha umuhimu wake kwa mofolojia na sintaksia.

Uchariganuzi huu ulitathmini kila kipengele katika kiwango cha mofolojia, sintaksia, kwa

(31)

kutolea sheria na vielelezo matawi. Vitale (ibid) aligundua kuwa mofolojia na sintaksia

huwiana na kutangamana. Utafiti huu ulikuwa na umuhimu kwa utafiti wetu kwa kuwa

ulifafanua hatua za kiuchanganuzi katika kuelewauwiano na utanganiano wa mofolojia

na sintaksia lakini haukugusia mofosintaksia ya yambwa.

Mudhune (1994) alishughulikia ujifunzaji wa vipengele vinne vya kimofosintaksia kwa

msingi wa nadharia ya Uchanganuzi Linganuzi. Katika kazi hiyo, Mudhune (ibid)

anatambulisha vipengele vya nomino, viwakilishi nomino, upatanisho nomina wa

viwakilishi na vimilikishi kama vipengele vya kimofosintaksia vinavyoweza kuwatatiza

wanafunzi wa lugha ya Kiswahili. Kulingana na utafiti wake baadhi ya wanafunzi

wanaojifunza Kiswahili wenye asili ya Kidholuo walitatizika kujifunza upatanisho wa

kisarufi katika sentensi za Kiswahili. Mudhune (ibid) anapendekeza kuwa utafiti zaidi

kuhusu mofosintaksia ya kategoria zingine za kisarufi kama vile vitenzi, vielezi na tungo

rejeshi unahitajika. Kutokana na hoja za Mudhune (ibid), tulitambua kuwa mofosintaksia

yaKiswahili inaweza kuathiri wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha ya

pili.

Kithuku (2012) alifanya utafiti kuhusu mofosintaksia ya ngeli ya 9110 (N/N) kwa

kuchunguza vipengele vya kimofolojia vya nomino za kundi hili. Katika uchunguzi

wake, Kithuku (ibid) alitathmini namna ambavyo wanafunzi hupatanisha sarufi katika

kundi la ngeli la 9110 wanapotunga sentensi za Kiswahili kwa kutumia misingi ya

(32)

wa kundi la ngeli la 9110 (N/N) huathiriwa iwapo mwanafunzi hazifahamu nommo

ambazo huwekwa katika ngeli ya 911O. Utafiti wa Kithuku (ibid) pia ulidhihirisha kuwa

.baadhi ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili hujumulisha kanuni za upatanisho wa

kisarufi ambapo ngeli ya 9110 ilitumika kama ngeli suluhishi. Ingawa kazi ya Kithuku

(ibid) ilijikita katika mofosintaksia, kazi hii ni tofauti na utafiti wetu kwa kuwa ilijikita

katika rnada ya upatanisho wa kiima katika ngeli ya 9110 ilhali utafiti wetu ulilenga

mofosintaksia ya kipengele cha yambwa ya Kiswahili.

Maandishi katika sehemu hii yamefafanua mada mbalimbali za kimofosintaksia ambazo

zimeshughulikiwa katika Kibantu na Kiswahili. Mada hizi zimedhihirisha matatizo katika

baadhi ya vipengele vya sarufi vinavyohusisha uchanganuzi wa kimofosintaksia. Tafiti

hizi zimeonyesha kuwa utafiti zaidi wa vipengele vya kimofosintaksia katika Kiswahili

na lugha za Kibantu kwa ujumla utatoa mwanga zaidi katika kufafanua dhana ya sarufi.

Tahakiki ya tafiti za kimofosintaksia ni msingi rnzuri wa kazi hii kwani ilituwekea

bayana baadhi ya vipengele vinavyochanganuliwa katika mofosintaksia. Ingawa tafiti hizi

za kirnofosintaksia zirnerejelewa katika tahakiki ya maandishi bayana ya mofosintaksia,

tafiti bayana kuhusu yambwa zilihitajika ili kuangazia zaidi mada ya utafiti.

1.6.2Tafiti Bayana za Yambwa katika Kibantu

Zipo tafiti kadha za wataalarnu wa Kibantu zinazozungumzia rnasuala mbalimbali ya

yambwa (Morolong na Hyman 1977, Bresnan na Mchombo, 1987, Bresnan na Moshi

1990, Marten, Kula na Thwala 2007, na Riedel 2009). Wataalamu hawa

(33)

wameshughulikia uchambuzi wa mada za muundo wa yambwa, yambwa changamano na

wakilisho yambwa (Taz 1.1). Kila mmoja wa waaandishi hawa anazungurnzia yambwa

na uamilifu wa yambwa katika lugha husika ya Kibantu. Katika tafiti hizi yambwa

inaelezwa kama sifa bia ya lugha kote ulimwenguni. Kwa kuwa utafiti wetu ulihusu

Kiswahili ambayo illmojawapo yalugha za Kibantu, kuna umuhimu wa kutathmini tafiti

kuhusu yambwa katika lugha za Kibantu na Kiswahili ..

.Hyman na Morolong (1977) wananachambua sifa ambazo huipa yambwa hadhi ya

yambwa msingi katika Kibantu. Katika utafiti wao, Hyman na Morolong (ibid)

walitambulisha kuwa mtazamo wa kufafanua yambwa ya Kibantu kwa misingi wa

Kiingereza unaibua utata wa udhihirikaji wa yambwa msingi na yambwa upili katika

Kibantu. Utafiti wa Hyman na Morolong (ibid) unapinga mtazamo wa kuzilazimishia

lugha za Kibantu ubia kwa kutumia dhana za kimapokeo za uchanganuzi wa Kiingereza,

hasa katika kufafanua vipengele ambavyo huja baada ya kiarifu. Kulingana na wataalamu

hawa, lugha za Kibantu hazina ushahidi wowote wa kimofolojia ambao hutambulisha

vipengele vinavyofuata kiarifu. Hyman na Morolong (ibid), wanatambulisha hatua mbili

za kumwongoza mtafiti katika kutambua yambwa msingi. Hatua hizi ni: kutambulisha

sifa za kijumla za yambwa na kisha kutathmini ni hoja zipi katika kishazi zinaweza

kupewa sifa hizi. Hatua hizi zilihitajika katika utafiti wetu ili kuangazia zaidi kuhusu

(34)

Tafiti za Hyman na Morolong (ibid) na Hyman na Duranti (1982) zililenga kutoa njia za

kutambulisha yambwa msingi katika Kisotho. Kwa kutathmini data ya Kisotho kupitia

majaribio ya unominishaji, mpangilio wa maneno katika kishazi, uhai wa yambwa

husika, uambishaji wakilishi yambwa na urejeshi, uchanganuzi wa watafiti hawa

.unaweka mfumo wa kingazi unayoitambulisha yambwa msingi katika lugha. Katika

mfumo huu sifa ya uhai ndio sifa ya kwanza ya kutambulisha yambwa msingi huku

dhima za kisarufi ambazo yambwa hubeba ndio kiwango cha pili katika kutambulisha

yambwa msingi na yambwa upili katika Kibantu. Matokeo ya tafiti zao yana umuhimu

katika utafiti, kwa kuwa kupitia kutathmini data ya Kiswahili, vigezo vya majaribio

wanavyovitoa vilibainisha wazi yambwa msingi na yambwa upili.

Kioko (2000) alifanya utafiti kuhusu kutambulisha yambwa msingi katika Kikamba.

Katika utafiti huu, Kioko (ibid) anaeleza kuwa lugha za Kibantu zinaweza kuwa na virai

vibainishi vitatu vikija baada ya kiarifu. Mahitimisho ya utafiti wa Kioko (ibid) yaliafikia

kuwa yambwa msingi huwa na sifa zake. Kwa kutumia vigezo vinavyoturniwa na Hyman

na Morolong (ibid), na Hyman na Duranti (ibid). Utafiti wa Kioko (ibid) unaonyesha

kuwa yambwa msingi hutambulishwa kutokana na utangamano wake wa vipengele vya

mfumo ngazi wa kisemantiki. Ingawa utafiti wa Kioko (ibid) ulilenga kutambulisha

yambwa msingi katika Kikamba, utafiti wetu unalenga kutambulisha sifa za yambwa

msingi katika yambwa changamano ya Kiswahili.

Bresnan na Moshi (1990) wanachambua na kutoa tofauti kati ya lugha asimetria na lugha

isoasimetria kwa kulinganisha Kihaya, Kirundi, na Kichichewa. Utafiti wa Bresnan na

(35)

Moshi(ibid) unachunguza sifa za yambwa msingi na yambwa upili za kuweza kuchukua

nafasi inayokuja baada ya kiarifu, yambwa inayochukua mofimu wakilisho yambwa

katika kiarifu na yambwa ambayo huchukua kauli tendi katika kishazi. Kulingana na

utafiti wao, Kichichewa ni lugha isoasimetria ilhali Kirundi na Kihaya ni lugha simetria.

Tofauti kati ya lugha simetria na isoasimetria imezua mjadala kwa sababu ni vigezo

vichachevya uasimetrialugha ambavyo hutumika katika uainishaji wa lugha mbalimbali

za Kibantu.

.Utafiti

wa Bresnan na Moshi (ibid) unaibua haja ya kutafiti zaidi vigezo vya

uasimetria lugha katika Kiswahili. Katika utafiti wetu, tulijadili vigezo vinavyotumika

zaidi kutofautisha uasimetria wa lugha ya Kiswahili.

Hadhiya kinadharia ya wakilisho yambwa katika Kibantu imeshughulikiawa katika tafiti

za Kibantu zinazochunguza yambwa. Bresnan na Mchombo (1987) wakitumia nadharia

ya Sarufi Amilishi Leksia, wanaeleza kuwa mofimu wakilisho yambwa ya lugha ya

Kichichewa ipo kwa madhumuni ya uwakilishi. Mofimu hii husimamia kirai nomino au

kirai bainishi katika kishazi. Kwa kulinganisha lugha tatu za Kisambaa, Kihaya na

Kiswahili, Riedel (2009) anadai kuwa wakilisho yambwa zote katika Kibantu ni za

madhumuni ya upatanisho wa kisarufi. Dai la Riedel (ibid) limezua mjadala wa maoni

kuwa sio lugha zote za Kibantu hudhihirisha upatanisho wa wakilisho yambwa. Mjadala

huu umeendelezwa na tafiti kama Siedl na Dimitriadis (1997), Diercks na Sikuku (2011),

na Adams (2010) wanaodai kuwa wakilisho yambwa ya lugha za Kiswahili, Kibukusu na

Kisotho ipo kwa sababu ya uwakilishi wa kirai nomino au kirai bainishi katika kitenzi.

(36)

kuhusu sifaza wakilisho yambwa. Tofauti na tafiti zilizojadiliwa ambazo zililengalugha

zingine za Kibantu na kulinganisha na Kiswahili, utafiti huu ulitumia misingi ya

Sintaksia Finyizi kufafanua hadhi ya kinadharia ya wakilisho yambwa katika vishazi vya

Kiswahili.

Katikauchanganuzi wa yambwa ya Kiswahili, tafiti kadha zimelenga kulinganisha

kipengele cha mofimu wakilisho yambwa ya Kiswahili na lugha nyingine za Kibantu.

Seidelna Dimitriadis (1997) wakitumia nadharia ya Sarufi Amilishi Leksia wanafafanua

uamilifu na muundo wa mofimu wakilishi yambwa ya Kiswahili bila kuchukua mtazamo

linganishi. Ingawa utafiti wa Siedl na Dimitriadis (ibid) hauchukui mtazamo linganishi,

utafiti hUQ ulitofautiana na utafiti wetu kwa kuwa utafiti wetu haukurejelea kipengele

kimoja cha yambwa cha wakilisho yambwa bali ulitathmni vipengee kadhaa vya yambwa

kulingana na mofosintaksia katika Kiswahili.

Tahakiki hii imechambua masuala ya kimsingi katika yambwa ya Kibantu na Kiswahili.

Maandishi ya tafiti bayana kuhusu mofosintaksia na yambwa katika Kibantu na Kiswahili

ni muhimu kwa kuwa maandishi yalionyesha masuala ya utafiti katika maeneo ya

yambwa na mofosintaksia. Masuala haya yalirejelea utambuzi wa yambwa msingi na

yambwa upili, uasimetria lugha katika lugha za Kibantu, na wakilisho yambwa katika

Kibantu. Kulingana na tahakiki ya tafiti hizi, hakuna ukubaliano kuhusu yambwa ya

Kibantu. Masuala ya yambwa ya Kibantu yanaendelea kuzua mjadala hasa katika kuamua

hadhi ya uwakilishi na upatanisho wa wakilisho yambwa. Kutokana na tahakiki hii,

(37)

vijinadharia sita: Eksi Baa, Utawala, Uhusika, Dhima maana, Ufungami na Ufundani

katika uchanganuzi wa sintaksia (Culicover, 1997). Pamoja na vijinadharia sita, mtazamo

wa Utawala na Ufungami ulijumuisha miundo

miwiliya

sentensi: rnuundo ndani na

muundo nje. Nadharia ya Utawala na Ufungami ilikosolewa kutokana na uchangamano

uliozuka .katika utaratibu wake wa kuchanganua sintaksia. Upungufu mwingine wa

nadharia ya Utawala na Ufungami ulikuwa ni udhahania wa hali ya juu. Kwa madhumuni

ya kupunguza uchangamano na udhahania katika uchanganuzi wa kisintaksia, Chomsky

(1995) alitumia Sintaksia Finyizi.

Sintaksia Finyizi ni mtazamo uliorahisisha uchanganuzi wa kisintaksia kwa kuondoa

dhanaya muundo wandani wa sentensi na kufasiri upya vijinadharia sita vya Utawala na

Ufungami. Uchanganuzi wa Sintaksia Finyizi unazingatia kanuni mbalimbali linganifu

zinazotawala uchanganuzi wa kishazi. Utafiti wa mofosintaksia ya yambwa ya Kiswahili

ulizingatia nadharia ya Sintaksia Finyizi kutokana na uwezo wake wa kuoanisha

mofolojia na sintaksia katika uchanganuzi wa kishazi. Uchanganuzi ulitegemea mihimili

miwili ya Sintaksia Finyizi; hatua za uchanganuzi wa kishazi na mfumo wa kanuni.

1.7.1 Hatua za Uchanganuzi wa Sentensi

Hatua ya kuondoa muundo ndani iliashiria kuwa Sintaksia Finyizi italenga muundo wa

nje pekee (Taz 1.7.0). IIi kufidia nafasi ya muundo wa ndani, Sintaksia Finyizi

ilipendekeza hatua tatu za uchanganuzi wa kishazi. Hatua za uchanganuzi wa kishazi

(38)

1.7.1.1 Uidadishi

Uidadishi ni hatua ya kwanza katika uchanganuzi wa muundo wa kishazi kulingana na

Sintaksia Finyizi. Dhana ya uidadishi inarejelea zoezi lakuoanisha maneno yaliyounda

kishazina kategoria za kisarufi. Sintaksia Finyizi ilitambulisha kategoria nane za kisarufi

za nomino (N), vivumishi (V), vitenzi (T), vihusishi (H), vielezi (E), vibainishi (B),

. .

vishamirishi (SH) na vipatanishi (P). Hata hivyo, ni nadra sana kishazi kimoja

kijumuishe kategoria zote,

Kishazi <Walimu wachangamfu waliwatungia wanafunzi wao maswali mengi>kwa

mfano, kina kategoria tano ambazo ni nomino (N), kivumishi (V), kibainishi (B),

kipatanishi (P), na kitenzi (T). Kielelezo kifuatacho kinadhihirisha namna maneno ya

kishazi <Walimu wachangamfu waliwatungia wanafunzi wao maswali mengi>

yanavyoidadishwa.

(1.1) Kielelezo cha Uidadishi

N

1

wlimU

wachangamfu wa iwa

Kielelezo hiki kinadhihirisha kuwa ingawa kishazi kina maneno saba, uidadishi

unahusisha kategoria tano. Neno la kwanza #walimu#, la tano #wanafunzi#, na la sita

#maswali# yanawakilisha kategoria ya nomino, neno #wachangamfu# linawasilisha

kivumishi ilhali maneno #wao# na #mengi# yanawakilisha kibainishi. Maneno haya

(39)

huhifadhiwaakilini mwa mwanadamu kulingana na sifa zake za kisarufi (Chomsky

1995).Kategoria za maneno huunda vijenzi vikubwa katika hatua ya muungano.

1.7.1.2Muungano

Muunganohureje1ea hatua ya kuunganisha kategoria za kisintaksia na kuunda vijenzi

vikubwazaidi (Radford 1997). Katika muungano, kategoria za maneno huungana na

kuundavirai na virai huungana kuunda vishazi. Kategoria za virai vilivyopo katika lugha

ni kirai nomino (KN), kirai bainishi (KB), kirai tenzi (KT), kirai vumishi (KV), kirai

elezi (KE), kirai husishi (KH), kirai patanishi (KP), na kirai shamirishi (KSH). Kirai

huundwakutokana na neno moja au muungano wa maneno mawili au zaidi. Neno moja

huwani kichwa cha kirai kilichoundwa.

Mahusiano ya kategoria zinazounda virai na vijenzi vikubwa zaidi katika Sintaksia

Finyizi hudhihirika wazi zaidi kwa njia ya vielelezo matawi. Kielelezo matawi

kinaonyesha uhusiano wa kihirakia katikamuundo wa kishazi. Kwa kuzingatia kishazi

<Walimu wachangamJu waliwatungia wanafunzi wao maswali

mengi

>

virai vinadhihirika

(40)

(1.2)Vielelezo vya Muungano wa Virai

a)

b)

l\

~l

wahwa tungia

c)

Walimu wach gamfu

Wanafunzi wao maswali mengi

Vielelezo vya(a) na (c) vinaonyesha jinsi nomino inavyoungana na kijenzi kingine

kuunda kirai nomino (KN). Kirai nomino (KN) naiau Kirai Bainishi (KB) hubeba dhima

mojawapo ya kisintaksia: kiima au yambwa. Nomino ndio inabeba kichwa cha kirai.

Kielelezo (c) kinaonyesha kuwa kirai kinaweza kufumwa ndani ya kirai kingine, kirai

nomino finyu <maswali mengi>kimejitokeza katika kirai nomino panuzi zaidi. Kirai

patanishi (kP) katika muundo wa kishazi cha Kiswahili hukitwa katika uhusiano baina ya

vipatanishi na kategoria ya kitenzi. Sifa za upatanisho kama vile umoja na wingi na njeo

huandamana na kitenzi cha Kiswahili na kudhibitiwa katika kirai patanishi (KP). Baada

ya muungano wa kuunda virai, muungano wa kishazi kizima hufuata.

Kishazi cha Kiswahili lazima kiwe na kiarifu. Kiarifu hujitokeza kama muungano wa

kipatanishi na kitenzi na kuunda kirai patanishi finyu (pI) <waliwa

+tungia>

. Kirai

patanishi finyu hupanuliwa kwa kufanyiwa uchomozi. Uchornozi wa kirai patanishi finyu

(pI) katika hatua ya muungano huzalisha kirai patanishi (KP) kipana zaidi ambacho

hubeba virai vingine. Uchorriozi hujumuisha kuongeza virai vingine kama kirai nomino,

(41)

·kirai elezi, kirai bainishi na kirai husishi kwenye kirai patanishi finyu (pI). Katika mfano

wetu<walimu wachangamfu walitungia wanaJunzi wao maswali mengi> kirai nomino,

<walimu wachangamfu>kinaunganishwa kwenye kirai patanishi finyu

(1)')

na

kuzalisha

kirai patanishi <vialiwatungia walimu wachangamfu>. Shamirisho inayowakilishwa na

<wanafunzi wao>inachopekwa kwenye kirai patanishi na kuunda kirai patanishi (KP)

<waliwatungia walimu wachangamfu wanafunzi wao>. Kirai nomino <majibu mengi>

kinachopekwa mwishoni. Kifuatacho ni kielelezo cha hatirna yamuungano uliohusika.

(1.3) KieJeJezo cha Muungano W3 Virai

tungia

(42)

· . . . . Kielelezo hiki kinadhihirishajinsi virai vinaungana na kuunda kishazi kamili. Mbali na

kudhihirisha uhusiano wa vijenzi kuunda virai, kielelezo hiki kina kategoria tupu(tu) ya

KN ambayo haijajazwa. Kwa kawaida nafasi hii hujazwa na kiima. Kiima cha kirai

patanishi pana <walimu wachangamfu>kimo katika nafasi ya baada ya kitenzi. Nafasi ya

kirai nomino (KN) tupu itajazwa kupitia hatua ya uhamisho.

1.7.1.3 Uhamisho

Uhamisho unarej elea mchakato wa faridi kuhama kutoka pahali pa awali hadi pengine

katika muundo wa kishazi. Uhamisho ni wa aina nyingi, lakini ule unaodhihirika

waziwazi katika Kiswahili ni uhamisho wa kijenzi na uhamisho wa hoja. Katika

uhamisho wa kijenzi, faridi huhama kutoka nafasi ya awali hadi nafasi nyingine

inayopewa hadhi ya faridi ile ile (Culicover 1997, Radford 1997, na Haegeman 1991).

Uhamisho dhima hutokea katika michakato ya ukanusho na uhamisho wa dhima maana.

Mchakato wa uhamisho katika Sintaksia Finyizi huanzia sehemu ya chini (hame) na

kuelekea sehemu ya jiiu. Kijenzi kinapohama huacha hame (ha) mahali ambapo kimetoka.

Katika KP <waliwatungia walimu wachangamfu wanafunzi wao maswali mengi> kirai

nomino <walimu wachangamfu> kinahama na kuchukua nafasi ya kiima cha kirai

patanishi, ambayo ipo mbele ya kirai patanishi finyu.

(43)

(1.4) Kielelezo cha Hatima ya Uhamisho

~

I

waliwa

1

tungia

~(ha)

I

I

I

I

I

I

I

I

I

I

I

I-

I

I

I

I

I

ali mengi

1_- _I wana nZIW o mas

---Katika kishazi<waliwatungia walimu wachangamfu wanafunzi wao maswali mengi>kirai

nomino (KN) <walimu wachangamfu> kinajitokeza kama kiima cha kiarifu ilhali

shamirisho ill KN <wanafunzi wao>_ Kirai nomino kinachowasilisha kiima kimehama

katika nafasi yake ya kiima cha kirai patanishi pan a<walimu wachangamfu waliwaambia

(44)

Hatua ya uhamisho huongozwa na kanuni za aina tatu: kanuni ya masafa mafupi, kanuni

ya ulafi, na kanuni ya ucheleweshi. Kanuni ya masafa mafupi inaeleza kuwa kijenzi

kihamie pahali palipo karibu iwezekanavyo. Kanuni ya ulafi pia hutawala uhamisho wa

vijenzi kwa kusisitiza uhamisho ufanyike ili kutimiza mahitaji ya kijenzi kinachohama

wala sio vijenzi vinavyokaribia. Kanuni ya ucheleweshi inaeleza kuwa uhamisho

unangojea hadi inapobidi. Kanuni za uhamisho zinawiana na kanuni bia zingine za

Sintaksia Finyizi.

1.7.2 Kanuni za Sintaksia Finyizi

Kanuni ni kaida za kijumla ambazo hutawala mahusiano katika muundo wa kishazi.

Sintaksia Finyizi ilipofasiri upya dhana ya sintaksia, ilididimiza dhana ya vijinadharia na

kutukuza dhana ya kanuni (Taz 1.7.0). Ufasiri mpya wa kanuni za kisarufi unadhihirika

katika maendeleo ya Sintaksia Finyizi. Kanuni maarufu zaidi ni saba: utegemezi muundo,

utawala, uhusika, dhima maana, uarifu, ufasiri karnili, na ufungami.

Kanuni ya utegemezi muundo huzingatia kwamba muundo wa maneno na virai

hutegemea kategoria za maneno, wala sio maneno yanayotumika katika kuunda kishazi.

Izingatiwe kuwa ubainishaji wa kategoria za maneno katika utegemezi muundo ni hatua

muhimu katika kufanikisha uidadishi (Tazama 1.7.1). Hatua ya kubainisha kategoria za

maneno ina umuhimu katika utafiti wa mofosintaksia ya yambwa kwa sababu yambwa

hubainishwa kulingana na kategoria yake ya kisarufi. Yambwa ni kijenzi cha kishazi

(45)

kinachowakilishwa kwa kirai nomino au kirai bainishi na dhima yake hutawaliwa na

kiarifu.

Utawala ni kanuni inayofafanua uhusiano uliopo kati ya vijenzi sanjari vya kisintaksia.

Uhusiano uliopo kati ya kichwa cha kirai na shamirisho kwa mfano, hudhihirishwa

.kupitia utawala. Kanuni ya utawala hurejelea uhusiano wa kijenzi kimoja mtawala kikiwa

na kingine mtawaliwa. Kanuni hii inatuwezesha kubainisha namna kiarifu hudhibiti

dhima nyingine katika kishazi huru. Kiarifu ndicho kichwa cha kirai kinachojumuisha

vipengele vinavyokifuata. Virai nomino ambavyo hufuata kitenzi huwa ni yambwa.

Hivyo basi, kanuni ya utawala ilitupelekea kubainisha kanuni ya uhusika katika hatua ya

muungano.

Kanuni ya uhusika inaeleza kuwa kirai bainishi au kirai nomino huwa na dhima katika

kishazi. Dhima mbili kuu zinazotambulishwa katika uhusika ni uhusika kiima na uhusika

yambwa. Uhusika kiima huwekwa kwenye kirai nomino (KN) au kirai bainishi (KB)

ambacho huwa ni mtenda au maudhui ya kishazi nao uhusika yambwa huonyesha nomino

inayotendewa au inayotendwa. Katika utafiti wa mofosintaksia ya yambwa, kanuni ya

uhusika ilitumiwa kubainisha idadi ya virai nomino (KN) au virai bainishi (KB)

vinavyotekeleza dhima maana katika kishazi cha Kiswahili.

Kanuni ya dhima maana hueleza dhima za kisemantiki za kirai nomino (KN) au kirai

(46)

nomino au kirai bainishi na kiarifu. Kulingana na aina ya kiarifu, majukumu ya dhima

maana yafuatayo yametambulishwa: kiini, kitendi, hisifu, pokezi, chombo, pahala, hatirna

na chanzo. Kanuni ya dhima maana inaeleza kuwa kila kirai nomino katika kishazi kina

jukurnu moja.Muundo wa kiarifu huamua idadi ya virai nomino ambavyo hukifuata.

Katika uchanganuzi wa mofosintaksia ya yambwa,kanuni ya dhima maana inafaa katika

kutambulisha dhima za kisemantiki za kirai nomino na kirai bainishi kinachokuja baada

yakiarifu kulingana na kanuni ya uarifu.

Kanuni ya uarifu inaeleza kuwa kila kiarifu lazima kiwe na kiima. Uundaji wa virai

katika hatua ya muungano huongozwa na kanuni ya uarifu. Katika muungano wa

<waliwatungia walimu wachangamfu wanafunzi wao maswali mengi>tunaona kuwa

kanuni ya uarifu inasababisha muungano kuanza na kitenzi. Kitenzi kinafuatwa moja kwa

moja na kiirna <walimu wachangamfu>. Kutokaria na kanuni ya uarifu, kirai nomino

<walimu wachangamfu>kinahama na kuchukua nafasi yake ya kiirna cha kirai patanishi

pana <walimu wachangamfu waliwatungia wanafunzi wao maswali mengi>. Katika

uarifu, ikiwa kishazi hakina kiirna nafasi ya kiima huwa ni tupu. Kanuni ya uarifu

ilituwezesha kueleza tungo zenye wakilisho yambwa.

Kanuni ya ufasiri kamili inaeleza kuwa kila kijenzi katika kishazi kimepewa maana ya

kisarufi au kileksia. Kila kijenzi cha kishazi lazima kiwakilishe maana fulani kimofolojia,

kisintaksia na/au kisemantiki. Majukumu ya yambwa na mofimu wakilisho yambwa

30

(47)

yanabainishwa kwa kurejelea kanuni ya ufasiri kamili ikishirikiana na kanuni ya

ufungami.

Kanuniya ufungami hueleza uhusiano uliopo kati ya anafora na kisabaki chake. Katika

uhusiano huo, anafora inafungama kwa kisabaki ndivyo maana yake ifasiriwe. Uhusiano

kati ya yambwa na mofimu wakilisho yambwa unalingana na uhusiano wa kisabiki an

anafora. Kanuni ya ufungami ilifaa utafiti huu kwa sababu ilituwezesha kuonyesha

mahusiano ya yambwa kwa kurejelea jinsi wakilisho yambwa huturnika kuirejelea

yambwa katika kishazi.

Misingi ya nadharia imewakilishwa kwa kuegemea hatua za uchanganuzi wa kisintaksia

na kanuni 'za Sintaksia Finyizi. Hatua ambazo zilibainishwa ni uidadishi, muungano, na

uhamisho. Kanuni za nadharia ya Sintaksia Finyizi saba: kanuni za utegemezi muundo,

utawala, uhusika, dhima maana, uarifu, ufasiri kamili na ufungami zirnefafanuliwa.

Pamoja na kubainisha mihimili ya Sintaksia Finyizi, sehemu hii imejadili jinsi kanuni na

hatua za Sintaksia Finyizi ziliongoza mbinu za utafiti kuhusu mofosintaksia ya yambwa

katika kishazi cha Kiswahili.

1.8.0Mbinu za Utafiti

Utafiti huu ulizingatia mawanda mawili: utafiti wa maktabani na utafiti wa njanyani.

Katika utafiti wa maktabani, mtafiti alisoma vitabu, majarida, tasnifu na kutafiti kwenye

(48)

· .

ulimwezesha mtafiti kudhibiti ubora zaidi wa taarifa za kinadharia kWlUSU mada za

mofosiritaksia na yambwa na kuweka msingi wa utafiti. Baada ya kuweka msingi wa

utafiti,mtafiti alitekeleza utafiti wa nyanjani kuhusu mada za mofosintaksia na yambwa.

Utafitiwa nyanjani ulihusisha hatua tatu za kijumla: ukusanyaji wa data, uchanganuzi wa

data,na uwasilishaji wa data.

1.8.1Mbinu za Ukusanyaji wa Data

Data lengwa katika utafiti huu ilijumuisha vishazi hum vyenye yambwa na wakilisho

yambwa.Kishazi huru kilicho na yambwa moja au zaidi ndicho kilikuwa mwafaka katika

utafiti wa mofosintaksia ya yambwa kwa kuegemea· Sintaksia Finyizi. Vishazi hum

vilichaguliwa kutokana na uwezo wake wa kudhihirisha vyema uhusiano uliopo baina ya

kiarifu na vijenzi vya kisintaksia ambavyo hukifuata. Vishazi hum vyenye yambwa

vilichaguliwa kulingana na uwezo wa kiarifu kudhibiti yambwa moja au zaidi. Vishazi

vilivyo na mofimu iliyoambishwa kwenye kiarifu kuwakilisha yambwa vilichaguliwa

kudhihirisha namna yambwa huwakilishwa katika kishazi hum cha Kiswahili (Riedel

2009). Matumizi ya kishazi huru yalituwezesha kugawanya vijenzi vya kisintaskia vya

Kiswahili vinavyokifuata kiarifu kwa welekevu zaidi.

Vishazi vilivyoteuliwa vilijumuisha vishazi vyenye vitenzi elekezi. Uamuzi wa kutumia

hali yauelekezi wa vitenzi vya Kiswahili katika kukusanya data yetu ulitokana na hali ya

uwezo wa vitenzi elekezi kuweza kudhibiti yambwa moja au zaidi katika muundo wa

kishazi (Carnie 2012). Kishazi cha kitenzi elekezi hudhihirisha kwa uwazi zaidi vijenzi

(49)

vinavyokifuata kiarifu. Uteuzi wa vitenzi elekezi ulikuwa wa kimaksudi kwa kutilia

. maanani asili ya kitenzi. Lugha ya Kiswahili ina aina mbili zavitenzi: vitenzi vya

Kiswahili vya asili ya Kibantu na asili ya kigeni. Vitenzi katika aina hizi mbili

vilizingatiwa katika ukusanyaji wa data ili kuweza kupata data yenye upana zaidi. Uteuzi

vya asili hizi mbili ulituwezesha kudhihirisha athari ya muundo wa kiarifu katika kishazi

c

ha

kitenzichenye asili ya Kibantu na chenye asili ya Kigeni katika Kiswahili.

Vitenzi vilivyoteuliwa ili kuzalisha data ya utafiti vilitolewa katika Kamusi ya Kiswahili

Sanifu (TUKl 2004). Uteuzi wa vitenzi ulitegernea idadi ya kauli za mnyarnbuliko kitenzi

kinaweza kunyambuliwa huku kikidhirisha muundo wa yambwa katika Kiswahili.

f

Kulingana na Buell (2005) kadri kauli za mnyambuliko zinavyoongezwa kwenye kitenzi

i

ndivyo rnuundo wa kisintaksia wa vijenzi vya kishazi huathirika au kuathiriana.

I

I

Baada ya hatuaya uteuzi wa vitenzi, hatua ya kuwateua watafitiwa ilifuata. Samarin

(1967) anaeleza kuwa watafitiwa katika usorni wa isirnu huhakikisha kuwa data

inayokusanywa ni miundo ambayo wazungumzaji asilia hutarnka. Watafitiwa

walichaguliwa kwa sababu ya umilisi wao wa lugha ya Kiswahili. Chomsky (1965)

anaeleza kuwa data iliyotolewa kwa wazungurnzaji asili inaweza kutoa hali halisi ya

lugha. Urnuhirnu wa kujurnuisha watafitiwa katika utafiti huu ni kuwa watafitiwa hutoa

(50)

Usampulishaji wa watafitiwa ulifanywa kimaksudi. Watafitiwa watatu walishiriki katika

utafiti huu kwa kuzalisha .vishazi vyenye yambwa. Milroy (1967) .anapendekeza

. matumizi ya sampuli ndogo katika utafiti wa kiisimu kwa sababu sampuli kubwa katika

utafiti wa lugha huzua data yenye urudufu mwingi. Walimu watatu walichaguliwa kwa

sababu idadi chache ingezua data toshelevu kwa kazi hii. Katika kusampulisha walimu,

kigezo cha tajriba ya watafitiwa kutumia na kufundisha lugha ya Kiswahili ndicho

kilituongoza. Ufundishaji wa kipengele cha mtalaa wa Kiswahili wa shule za upili cha

muundo wa sentensi ya Kiswahili kilitumiwa. Kipengele hiki hufundishwa katika kidato

cha tatu na cha nne. Hivyo basi, walimu wa kidato cha tatu na cha nne waliteuliwa.

Usamplishaji pia ulijumuisha uteuzi wa wazungumzaji asilia watatu ambao

waliwasilishiwa data iliyotoka kwa walimu waliozalisha vishazi ili kutoa uamuzi wao

kuhusu vishazi hivyo. Kulingana na Chomsky (1986) lengo kuu la utafiti wa kiisimu ni

kuchunguza urnilisi sarufi wa rnzungurnzaji asilia wa lugha fulani. Umilisi sarufi

unalenga kuchunguza maarifa ya mzungurnzaji katika kuamua ni sentensi zipi sahihi na

sentensi zipi sio sahihi katika lugha yake. Maturnizi ya kigezo cha uzungumzaji asilia na

ufundishaji wa kipengele cha muundo wa kishazi cha Kiswahili uliongozwa na haja ya

kupata data asilia. Pamoja na hayo, matumizi ya wazungumzaji asilia kuamua ukubalifu

wa vishazi vilivyozalishwa yaIituwezesha kupata vishazi asili zaidi.

Vitenzi vilivyochaguliwa viliwasilishwa kwa watafitiwa. Kila mtafitiwa aliwasilishiwa

vitenzi elekezi vinne. Mtafiti aliwapelekea walimu teuliwa vitenzi na kuwapa muda wa

(51)

kuzalisha vishazi vyenye yambwa katika kauli za minyambuliko kwa kuanzia kauli ya

kutenda. Uzalishaji .wa vishazi vyenye yambwa ulitegemea uwezo wa kitenzi

kunyambuliwa katika kaulizinazokubalika na wazungumzaji asilia. Katika kuibua

vishazi vyenye mofimu wakilisho yambwa, mtafiti aliwaelekeza walimu ipasavyo kuibua

maumbo ya wakilisho yambwa. Baada ya kuzalisha vishazi husika, wazungumzaji asilia

waliwasilishiwa vishazi hivyo na wakatoa maoni yao kuhusu ukubalifu wa vishazi

vilivyozalishwa.

Vishazivilivyotathminiwa vilikuwa 60: 20 vyenye tungo za yambwa changamano, na 10

vyenye yambwa sahili. Vishazi 20 vilitumiwa kuonyesha uamilifu wa yambwa katika

Kiswahili, ilhali vishazi 10 vilidhihirisha mofimu wakilisho yambwa ya Kiswahili. K wa

kuzingatia idadi hii, tunaweza kusema kuwa vishazi hivi ni kiwakilishi cha sentensi

zinazozungumzwa zenye sifa zilizochanganuliwa.

1.8.2 Mbinu za Uchanganuzi Data

Uchanganuzi wa data ulianza kwa kubainisha muundo wa kishazi cha Kiswahili. Sifa za

kimofosintaksia zilizodhihirika katika uchanganuzi wa kishazi cha Kiswahili zilielezwa

hatua baada ya hatua. Uchanganuzi wa data uliainisha vishazi vya Kiswahili kulingana

na muundo wa kirai nomino au kirai bainishi kinachowakilisha yambwa, vishazi vyenye

yambwa sahili na yambwa changamano, vishazi vilivyojumuisha wakilisho yambwa

kwenye kiarifu na hatimaye sifa ambazo huipa yambwa hadhi ya yambwa msingi katika

(52)

vimeainishwa na baadhi ya wataalamu wa lugha za Kibantu (Tazama 1.6.3). Vigezo hivi

vinavyotambulishwa vilijaribiwa katika data yetu ili kutambulisha sifa na hadhi ya

yambwa katika Kiswahili.

Katika kuchunguza ama za yambwa katika Kiswahili, data ilichanganuliwa ili

kudhihirisha uamilifu wa yambwa ya Kiswahili. Carnie (2012) anaeleza kuwa yambwa

huwa na dhima maana za kisarufi. Utambuzi wa dhima maana ya yambwa katika

Kiswahili ulijikita katika kanuni ya dhima maana ya Sintaksia Finyizi. Baada ya

kuchanganua yambwa, uwakilishi yambwa ulibainishwa kulingana na udhihirikaji wake

katika kishazi huru cha Kiswahili.

Uwakilishi yambwa katika Kiswahili ulibainishwa kwa madhumuni ya kufafanua

muundo na dhima ya uwakilishi yambwa. Vigezo kumi na vinne vilivyotambulishwa na

Marten, Kula na Thwala (2007) kuhusu mofosintaksia ya yambwa kwa kuzingatia

wakilisho yambwa viliongoza ubainishaji wa muundo wa wakilisho yambwa ya

Kiswahili (Tazama 1.4:7). Katika kuchanganua data, utawala wa mofimu wakilisho

yambwa na kiarifu wa kudhibiti yambwa katika kishazi huru ulibainishwa na

kulinganishwa. Hatimaye, utafiti ulifafanua muundo wa wakilisho yambwa na kiarifu

katika kutawala yambwa na mabadiliko yake ya kimofosintaksia kwenye kitenzi cha

Kiswahili katika sehemu ya uwasilishaji wa data.

References

Related documents

I n Petunia the cells of the white area are much smaller than the colored cells in the center of the purple spot. The light purple cells are intermediate as to their sizes between

Results show that the Lyapunov-type inequality gives the worse and the Cauchy-Schwarz-type inequalitygives the best lower bound estimates for the smallest

Following the collection of the first harvests the F1 plants were again selfed and then all of the leaves and side branches were removed so that second harvests of seed were

Our results show that, although tetrasomic inheritance creates additional con fi gurations of lineages that have unique probabilities of coalescence compared to those for

In our examination, we have tried different inside and outside releases like void, surface and crown utilizing factual parameters, for example, skewness and

Further work will involve the modification of the sliding mode controller using a time-varying switching gain and improvement in modeling of the actuator over a broader

During this analysis work numerous agglomeration strategies even have been used for segmentation for neoplasm detection in resonance imaging (MRI).MRI attributable to its give

Table A.1: Diameter ratios for binary hard-sphere mixtures that exhibit solid-liquid phase diagrams of the solid solution, azeotrope, and eutectic types..