UWIANO WA PICHA NA MATINI KATIKA MABANGO
YA MATANGAZO YA UKIMWI: MTAZAMO WA
KISEMIOTIKI
TasnifuYa
~MANI
HELLENWANJlKU
lliyotolewa kwa madhumuni
ya kutosheleza baadhi ya
mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu
cha Kenyatta
2006
KENYATIA UNlVERSi
I
1 RA
UNGAMO
Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijatolewa kwa mahitaji ya Shahada katika Chuo Kikuu kingine chochote.
KIMANI HELLEN WANJlKU
Tasnifu hiiimetolewa kwa Chuo Kikuu kwa idhini yetu kama wasimamizi.
~...>.,..l.--O
--DKT. C. M. NDUNGO
TABARUKU
Kwa mume wangu mpendwa Philo, na watoto wangu Eddy, Chris na Diana! Mapenzi yenu yalinitungisha nia ya kuendelea kuchuana na vitabu hata pale mambo yalipokaribia kunichusha, kuniatilisha, kunisikitisha na kunishawishi kukata tamaa. Tulijua tulipotoka lakini hatukujua tulipokwenda ... tukapiga hatua kujaribu! Sasa hapa tulipo ...
SHUKRANI
Ahimidiwe Mwenyezi Mungu! Tasnifu hii ni zao la rehema na baraka zako.
Shukrani zangu ziwaendee wasimamizi wangu waadhama, Dkt. C. M. Ndungo na Dkt.A.N. Mwihaki kwa wasaa wao walioutwaa kuniongoza, kunishauri na kunitia moyo kila hatua ya utafiti huu. Dkt. Mwihaki, nimefarijika na msaada wa vitabu na kazi zako tangu nillpoanza utafiti. Nawashukuru wote wawili kwa maoni na maarifa mlionipa ill kuituja tasnifu hii hadi kufikia kiwango ilivyo sasa.
Nawashukuru wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika kwa kunielimisha na kunitia shime katika kila hatua ya masomo yangu. Wahazili, Mary Khaemba na Ann Kimotho, twaeni shukrani zangu kwa mahimizo yenu wakati wa kozi hii.
Nawashukuru wasomi wengine tulioanza pamoja safari hii ya usomi, tukafaana kwa vitabu na mawazo. Tulikuwa masahibu tukaoneana imani na kuhimiliana katika yote tuliyoyafanya. Nitawezaje kuwasahau akina Kea, Nelly, Salome, Kihara, Mungai na Wachira. Mlinishajiisha kila nilipokaribia kufa moyo. Shukrani zisizo kifani ziwaendee, Munuku Ann, King'ori Ann, Karuga Mary, Gitau Elizabeth na Savala kwa kunifaa kwa vitabu na mawazo. Nawaombea kila la heri.
Kutimia kwa tasnifu hii kusingefikiwa pasi mchango wa watafitiwa walioshirikishwa nyanjani, kwa maswali ambayo kwao wao yalikuwa hayana faida bali udhia na usumbufu wangu. Haiyumkiniki kumtaja kila mmoja kwa jina katika nafasi hii. Kwa hivyo, wote nawashehenezea shukrani zangu kwa mchango wenu.
Maelezo ya Istilahi Muhimu
Bango Ishara Maana Matini Msimbo Semiotiki Stiari Uchanganuzi MatiniUchanganuzi Picha na Ishara
Ukinzano
Utata
Kipande cha karatasi ngumu kama kadi, au bati lililoangikwa mahali - kwenye barabara au maeneo mengineo. Katika muktadha huu ni ilani/tangazo.
Alama, kidokezi au kielekezi chochote katika tangazo.
Fahiwa za neno na picha.
Kifungu cha maandishi au taarifa
inayojisimamia katika kueleza dhana fulani. Mfumo wa mawasiliano.
Taaluma inayoshughulikia ishara za mawasiliano.
Maana fiche inayoweza kufasiriwa kutokana na matini na picha katika kazi.
Uhakiki unaotumia mbinu za kiisimu katika kuangalia jinsi visehemu mbalimbali
vilivyosawiriwa ili kuwasilisha maana na ujumbe. Uhakiki unaotumia mbinu zisizo za kiisimu katika kuangalia jinsi viunzi tofauti vya picha na ishara vilivyosawiriwa ili kufanikisha uwasilishaji wa maana na ujumbe.
Hali ya maana katika kipashio fulani au picha fulani kupingana au kukosa upatanifu.
VIFUPISHO
AAWORD Association of African Women for Research and Development. (Ushirika wa Wanawake wa Afrika wa Utafiti na Maendeleo.)
ART Antretroviral Therapy.
(Huduma ya Tiba ya Kupunguza Makali ya UKIMWI.)
ARV Antiretrovirals.
(Madawa ya Kuimarisha Afya ya Wagonjwa wa UKIMWI.)
DASCOP District AIDS/STD Coordinating Programme. (Washirikishi wa Ngazi za Wilaya wa Mipango ya kupambana na UKIMWI na Magonjwa ya Zinaa.) KDHS Kenya Demographic and Health Survey.
(Uchunguzi wa Demografia na Afya ya Jamii Nchini.)
KNASP Kenya National HIV/AIDS Strategic Plan.
(Mikakati ya Kitaifa ya Kupambana na UKIMWI.) NACC National AIDS Control Council.
(Baraza la Taifa la Kupambana na UKIMWI.) NASCOP National AIDS/STD Control Programmme.
(Mpango wa Taifa wa Kupambana na UKIMWI na Magonjwa ya Zinaa.)
UNAIDS United Nations Programme on HIV/ AIDS. (Ushirika wa Kimataifa katika Mipango ya Kupambana na UKIMWI.)
IKISIRI
Lengo la kazi hii ni kuchanganua uwiano wa maana za picha na matini katika mabango ya matangazo ya UKIMWI kwa kuzingatia tathmini za wapokezi. Watafitiwa ambao walishirikishwa katika utafiti huu waliteuliwa kutoka maeneo ya Githurai na Kiandutu katika wilaya ya Thika, Vitengo vya watu wenye umri, kazi, elimu, tajriba, falsafa na mielekeo tofauti vilihusika. Kwa kurejelea misimbo ya nadharia ya Semiotiki kwa mujibu wa Barthes uchanganuzi wa ishara zote za kisanaa na kiisimu katika mabango thelathini na matano yanayohusu ugonjwa hatari wa UKIMWI yamechanganuliwa.
Kazi hii imegawanyika katika sehemu tano. Sura ya kwanza imetanguliza kazi yote kwa kuangazia mada ya utafiti, maswali, malengo, upeo na mipaka ya utafiti. Mengine yaliyoshughulikiwa katika sura hii ni misingi ya nadharia, tahakiki za maandishi yanayohusiana na mada hii, ukusanyaji na uwasilishaji wa data. Sura ya pili imeshughulikia viunzi vya matangazo kwa nia ya kupata maana msingi katika mabango ya UKIMWI, kwa kutalii yale yanayojidhihirisha wazi pasi kuhusisha tajriba, mielekeo na falsafa za mtu binafsi na za kijamii. Sura ya tatu, imeangazia ujumbe katika mabango ya matangazo ya UKIMWI pamoja na kuhakiki dhamira za miguso tofauti. Uhakiki huo uliegemea upande wa yaliyomo kwenye tangazo kama vile: mada, maudhui, wahusika, pamoja na msuko wa picha na matini kwa kurejelea maoni ya watafitiwa.
YALIYOMO
Ukurasa
Mada
i
..
Ungamo 11
b
k
...
Ta aru u
111Shukrani
:
iv
Maelezo ya Istilahi v
Vifupisho .
......•••.•.•....••...•.••..•.•.••.••..• ~.
lki . .
..
slrl ~l
I·
...
Ya
iyomo
V111SURA YAKWANZA: UTANGULIZI
1.0
Usuli wa Utafiti
c
11.1 Swala la Utafiti 5
1.2
Maswali ya Utafiti
.
7
1
.
3
Malengo ya Utafiti
.
7
1
.
4
Tahadhania 81
.
5
Sababu za Kuchagua Mada
8
1.6
Upeo na Mipaka ya Utafiti
.
101.7 M··
ismgi
.ya Na
dh
arra
.
111.8.0
Udurusu wa Maandishi
.
161.8.2
Tafiti katika Lugha Zingine
181.8.3
Tafiti katika Lugha ya Kiswahili..
221.9.0
Mbinu za Utafiti
251.9.1
Sampuli
261.9.2
Ukusanyaji wa Data
281.9.3
Uchanganuzi wa Data
281.9.4
Uwasilishaji wa Data
29SURA YA PILI: VIUNZI VYA MATANGAZO
2.1.0
Picha na Ishara
312.1.1
Maana za Picha na Ishara
342.2.0
Vichwa Vikuu
412.2.1
Matangazo Yanayoshirikisha Vichwa Vikuu
-412.2.2
Matangazo Yasiyo na Vichwa Vikuu
-472.3
Wakala wa Tangazo
54SURA YA TATU: UJUMBE KATIKA MATANGAZO
3.1.0
Ujumbe katika Picha na Matini..
633.1.1
Maafa ya kuambukizwa UKIMWI
693.1.2
Matumizi ya Kondomu
793.1.3
Ususiaji wa Ngono
883.1.5
Hiari katika Ushauri na Uchunguzi..
96SURAYANNE: UWIANOWA MAANANAUJUMBE
4.1.0
Uangavu
1064.1.1
Amali ya Anwani
.
1074.2.0
Matini Ndefu
1184.2.1
Kiashiria
1194.2.2
Kihimili Maana
1214.2.3
Kielekezi
.
1234.2.4
Kihisishi
.
1284.3
Muktadha
1324.4.0
Muwala na Mshikamano
1344.4.1
Mshikamano Tegemezi
.
1364.4.2
Mahusiano Linganuzi
.
1404.5
Uakifishi
.
1424.6.0
Tamathali za Semi
.
1454.6.1 Stiari 145
4.6.2
Usafid
i.
1464.7.0
Mbinu za Kipekee
1504.7.1
Takriri
.
1504.8.0
Kuchanganya Msimbo
156
4.8.1
Kujitambulisha na Jamii- Lugha
157
4.8.2
Kurejelea Dhana
159
4.8.3
Mwingiliano wa Mifumo- Lugha
160
SURA YA TANO: HITIMISHO
5.1.0 Matokeo ya Utafiti 171
5.2.0
Mahitimisho ya Utafiti..
176
5.3.0 Mapendekezo
179
]V(Cllr~j~l~()•••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••1~1
SURA
YA KWANZA
UTANGULIZI
1.0
Usuli wa Utafiti
Mawasiliano ni kipengele muhimu zaidi kinachodhihirisha ustawi wa teknolojia na sayansi katika nchi yoyote He. Mawasiliano mwafaka yanahitajika ili kuharakisha uimarishaji wa afya ya jamii. Maendeleo na uvuvumkaji wa nchi yoyote hutegemea afya ya wananchi wake na uwezo wa wananchi kukabiliana na jukumu la ujenzi wa
taifa (NASCOP2005).
Kuna ukosefu wa ujuzi na maarifa ya kujikinga na kuzuia magonjwa sugu yanayokuwa kikwazo katika ujenzi wa taifa. Kumakinisha mtu na jamii kwa jumla ni jukumu la wizara ya afya, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali ambayo yanahusiana moja kwa moja na ustawi wa afya ya mtu binafsi au jamii kwa ujumla
(NACC2005).
Mwaka 1999 mwezi Desemba, ugonjwa wa UKIMWI ulitangazwa kuwa janga la kitaifa, kutokana na jinsi ulivyoangamiza watu wengi nchini. Kwa mujibu wa ripoti ya NACC (2005), katika muda wa dakika tano, ugonjwa huu sugu, huangamiza watu watatu. Idadi ya watu wanaokufa kutokana na UKIMWI ni takribani watu
105,000 kila mwaka. Hii ni idadi ya zaidi ya watu 350kwa kila siku (NACC2005).
Ugonjwa huu unaendelea kuangamiza mamilioni ya watu kila uchao. Kwa mujibu
wanawake, wanaume na watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI wakati huu.
Zaidi ya asilimia 95 wakiwa katika mataifa yanayoendelea. Nchini Kenya, mmoja
kati ya kila watu tisa ana virusi vya UKIMWI. Idadi ya visa hivi inazidi kuongezeka
kutoka 10,000 mnamo 1987 na kufikia visa 96,000 vipya, mnamo 2003. Hili ni
ongezeko la zaidi ya mara kumi katika kipindi cha miaka 15.
Katika harakati za kumakinisha umma, mbinu nyingi za mawasiliano hususan
mabango yanayoangikwa katika maeneo tofauti zimetumika. Matangazo ya
UKIMWI katika mabango ni njia ambayo imehusisha masuala tofauti katika
mazingira ya wasanii mbalimbali, kwa kusudi la kuzindua, kushawishi,
kutahadharisha, kufahamisha, kuelimisha na kurekebisha mielekeo na mitazamo
ya wananchi. Mashirika mengi ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yamechukua
hatua ya kutumia mabango kama mkondo wa uwasilishaji wa masuala nyeti
nchini. Mkondo huu wa uwasilishaji wa ujumbe umewezesha wananchi kuusoma
ujumbe mara kwa mara wapitiapo mahala palipoangikwa mabango
yanayotangazia masuala mbalimbali. Hivyo njia hii imejibainisha kama yenye
uwezo wa kutahadhalisha na kudhibiti mielekeo ya wananchi.
Suala hili la utangazaji hufuma majukumu mapya kufungamana na maisha na
maendeleo ya jamii kwa mujibu wa wakati. Matangazo ni kipengele muhimu
katika mfumo wa kumakinisha umma ill kumaizi mengi yanayowazunguka. Hili
litaweza tu kutokea pale tu, maana na ujumbe unaolengwa na mwasilishi
unamfikia mpokezi pasi utata au upotoshi. Kuwasilisha dhana fulani kwa jamii
la ugonjwa sugu wa UKIMWI lafaa kuzingatiwa kwa uwazi zaidi kwa vile
limefungamanishwa na masuala ambayo jamii nyingi huyaona mwiko kuyataja
kwa udhahiri (Gachara 2005).
Msukumo wa utafiti huu ni kuchunguza uhusiano kati ya picha na matini katika
mabango ya UKIMWI. Mtafiti anachukulia kwamba maana halisi au ambazo
zinaibuliwa huweza kuzungukiwa na utata na upotoshi wa ujumbe iwapo
hakutakuwepo na uwiano wa ishara za kisanaa na ishara za kiisimu kwenye
mabango na pia iwapo picha na matini zitazua fasiri zaidi ya moja. Isitoshe
utoshelevu wa mabango ya matangazo ya UKIMWI utategemea ujuzi wa wananchi
wa kusoma na kujua yanayoelezwa.
Mtafiti amejaribu kutafuta ni kwa njia gani mabango ya matangazo ya UKIMWI
yanaweza kuwasilisha maana na ujumbe kwa njia toshelevu. Mtafiti amekusudia
kuwa kwa kubainisha wazi vigezo vya uwiano wa picha na matini katika
uwasilishaji wa maana na ujumbe katika mabango, utafiti huu umechangia katika
utatuzi wa matatizo yanayokumba taaluma ya mawasiliano hasa kuhusiana na
suala ibuka la ugonjwa wa UKIMWI.
Uamilifu wa taaluma ya semiotiki, katika uchanganuzi - miundo ya maana katika
kazi ulianza na wanaprague mwaka 1920-1930 hususan, Jan Mukaravosky. Hata
hivyo, semiotiki ilianza kutumikizwa katika uchanganuzi wa ishara na vielelezo
picha katika kazi ya Roland Barthes ya mwaka 1955. Kazi zake Barthes ziliipa
taaluma ya semiotiki msukumo mkubwa katika uchanganuzi wa maana za ishara
alipoainisha fasiri za maana katika Pasta ya Panzani (Tanaka, 1994). Kwa mujibu
wa Barthes, matangazo huwasiliana na wapokezi kwa nia ya kuwapasha ujumbe na
maana fulani. Matangazo ni mwafaka zaidi kama kichocheo cha fasiri za kisemiotiki kwa vile huhusisha ishara za kiisimu na pia kisanaa katika kufikisha
ujumbe kwa hadhira. Mtazamo wa kisemiotiki unafaa zaidi katika kufasiri maana
na ujumbe, kueleza utaratibu na njia za ubunifu na uzuaji wa maana na pia
matatizo ya ufasiri, katika matangazo.
Barthes (1964) anaeleza kuwa, mfumo wa ishara kama vile picha, vielelezo,
michoro na hata lugha hushughulikiwa kama vipengele vinavyozua ujumbe na
fasiri mbalimbali za maana. Picha huchunguzwa kama mfumo lugha, na lugha
huchunguzwa kama mfumo ishara. Hivyo mifumo ya kiisimu na mifumo ya
kisanaa huchunguzwa kama mifumo ya kiishara inayotegemeana katika kuibua
mifumo ya maana na ujumbe.
Wazo hili linashadidiwa na Gombrich (1977) anayesisitiza umuhimu wa kuangalia
picha na ishara zinazornzunguka mwanadamu katika vipengele vyote vya maisha.
Umuhimu wa picha umo katika uwezo wake wa kuwasillsha ujumbe ambao
haungesimbwa kwa njia nyinginezo. Katika kazi zinazohusisha ishara anuwai,
mtazamo wa kisemiotiki huchunguza amali na uamilifu wa kila kipashio cha
ishara, na kuvifungamanisha katika kukamilisha uzima wa mifumo ya maana na
ujumbe kikamilifu.
Mtazamo wa kisemiotiki unachukulia kuwa katika mawasillano huwa kuna ishara
zinazosimbwa, na ung'amuzi wa maana na ujumbe wa ishara husika utafikiwa pale
tu ishara zenyewe zitasimbuliwa ipasavyo (Barthes, 1986b). Barthes anadokeza
kuwa, kuna aina tatu za ishara za kisemiotiki zinazochangia fasiri za maana na
ujumbe: ishara za kiisimu au umbo lugha linalowakilisha dhana katika mfumo
lugha, hizi huwa ni kigezo bainifu; ishara-lugha fiche na stiari picha. Ishara hizi
husimba maana na ujumbe ambao husimbuliwa tu na wapokezi kwa mujibu wa
tajriba na amali mbalimbali za kijamii. Ni katika mkabala huu, tumetathmini umuhimu wa ishara za kisanaa ambazo zinafanikisha mawasiliano sawa na ishara
za kiisimu.
1.1Swala la Utafiti.
Utafiti huu umechanganua uhusiano kati ya picha na matini katika mabango ya
matangazo ya UKIMWI. Tumetathmini uwiano kati ya maana za picha na matini
katika mabango ya matangazo ya UKIMWI. Mtafiti ameibusha kutokana na matini
na picha miktadha tofauti inayozalisha uwiano wa maana na ujumbe katika
mabango ya UKIMWI. Kipengele hiki cha ishara za kisanaa kama vile picha
kubeba maana na ujumbe. Watafiti wengi kama vile, (Ojwang 1986, Michira 1993, Aloo 2002), wamebobea katika kipengele cha matangazo ya biashara kwa kuzingatia zaidi mwingiliano wa matini na muktadha. Katika tafiti zilizotangulia, uwiano kati ya picha na matini haujaonyeshwa namna unavyofanikisha mawasiliano kwa kuimarisha ufasiri wa maana na ujumbe unaofikia hadhira.
1.2 Maswali ya Utafiti.
Uafiti huu umeongozwa na maswali haya:
• Je, picha na matini zilizotumika katika mabango ya matangazo ya UKIMWI,
zinawasilisha ujumbe na maana sawa?
• Msuko wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya UKIMWI
umefanikisha vipi ufasiri wa maana na ujumbe?
• Ni vigezo vipi vya uwiano wa picha na matini vinavyofanikisha ufasiri wa
maana na ujumbe?
• Ni mbinu zipi zinazoweza kuboresha ufasiri wa maana na ujumbe katika
mabango ya matangazo ya UKIMWI?
1.3 Malengo ya Utafiti
• Kuchanganua picha na matini zilizotumika katika mabango ya matangazo
yaUKIMWI.
• Kuchanganua namna muundo wa picha na matini unavyofanikisha ufasiri
wa maana na ujumbe.
• Kutathmini vigezo vya uwiano wa picha na matini vinavyofanikisha ufasiri
wa maana na ujumbe.
• Kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha ufasiri wa maana na ujumbe
1.4 Tahadhania
• Kuna uwiano kati ya matini na picha katika mabango ya matangazo ya
UKIMWI.
• Kuna utata wa maana za picha na matini katika mabango ya matangazo ya
UKIMWI.
• Msuko wa picha na matini hufanikisha, ufasiri wa maana na ujumbe katika
mabango ya matangazo ya UKIMWI.
• Mabango kama mkondo wa mawasiliano yanaweza kuboreshwa zaidi ili
yawasilishe maana na ujumbe kwa njia mwafaka.
1.5 Sababu za Kuchagua Mada
Utafiti huu umefanywa kwa kuzingatia kwamba matangazo ni kipengele muhimu
kinachohusika katika kuizindua, kuishawishi, kuimakinisha, kuiongoza na
kuirekebisha mielekeo na mitazamo ya jamii. Matangazo huhusisha masuala
mbali- mbali katika nyanja tofauti - siasa, elimu, afya na maadili katika mifumo ya
kijamii.
Matangazo yamekuwa kwa kiwango kikubwa dhihirisho la ulimwengu
unaobadilika haraka mno hasa katika maendeleo ya kisayansi na teknolojia ya
mawasiliano. Ni katika sajili hii ya matangazo, tunaweza kuona jinsi lugha
inavyopanuliwa ili kupambana na mabadiliko kwa mujibu wa uhalisi wa maisha ya
Mtafiti amezingatia mabango ya matangazo ya UKIMWI yaliyoandikwa kwa Kiswahili kwani anachukulia kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya wote- wasomi na wasiosoma. Lugha hii ina uwezo wa kuhamasisha wote kuhusu masuala ibuka kama vile ugonjwa wa UKIMWI kwa kuwa hutumika na hueleweka na idadi kubwa
ya watu nchini. Isitoshe, Kiswahili ni lugha ya taifa na pia ndiyo lugha inayotumiwa na Wakenya wengi katika mawasiliano. Mbali na hayo, mabango kama njia ya utangazaji, yanaweza kutapakazwa kote nchini na hivyo kufikia idadi kubwa ya watu katika maeneo tofauti .
amechukulia kuwa mabango ni njia ya utangazaji inayoweza kutanda kote nchini katika kuhamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa UKIMWI na kwa hivyo palikuwa na haja ya kutathmini utoshelevu wake kama njia mojawapo ya mawasiliano inayohusisha ishara za kisanaa pamoja na zile za kiisimu.
1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti
Ingawa njia za utangazaji kuhusu suala la UKIMWI ni nyingi, utafiti huu umelenga tu mabango pekee, yaliyotundikwa kwenye barabara, vituo vya afya na maeneo mengine tofauti nchini. Mabango yameteuliwa kutokana na uwezo wa njia hii ya utangazaji kufikia idadi kubwa ya watu katika maeneo tofauti. Vilevile uteuzi wa mabango umezingatia kusudi la mtafiti la kutathmini utaifa katika upokezi wa matangazo ya UKIMWI. Picha na matini za mabango ya matangazo ya UKIMWI zimetathminiwa ili kuchunguza fasiri za maana za wapokezi tofauti kwa vile hili ni suala linaloathiri kila mtu kwa njia moja au nyingine nchini. Mtafiti amejikita tu
kwa fasiri za wapokezi kwa vile mabango hayo yanaashiria wasomaji tofauti na msomaji ndiye wa mwisho aliye na nafasi na mchango katika kuyachambua na kuelewa maana. Hivi ni kusema kuwa, nia na maoni ya waasilishi wa mabango husika hayakuakisiwa na utafiti huu.
Mabango yamechanganuliwa, kwa kuzingatia maudhui tofauti yanayozingatiwa na
ushirika wa wote katika kuangarniza UKIMWI. Kwa kila kitengo mabango saba yameshughulikiwa. Jumla, mabango thelathini na matano yaliyoendelezwa zaidi kwa lugha ya Kiswahili yamechanganuliwa. Katika mabango mengi imebainika kuwa hata iwapo lugha ya Kiswahili ilihusishwa pakubwa, vilevile maneno ya Kiingereza na Sheng yalichopekwa. Maneno au kauli zilizochopekwa zimetolewa kisawe chake katika Kiswahili na kuchanganuliwa. Hata hivyo, mtafiti hakuhusika katika kurekebisha mifumo ya sarufi na makosa ya hijai yaliyojidhihirisha katika
matangazo kama vile- *mjaa-rnzito. Mifumo yote ya mawasiliano ikiwemo ishara za kiisimu na kisanaa imeehanganuliwa jinsi ilivyojitokeza katika tangazo ili kudhihirisha fasiri za maana.
1.7
Misingi ya Nadharia
Nadharia ambayo ni mwafaka zaidi na ambayo imetoa msingi maridhawa wa uchanganuzi wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya UKIMWI ni nadharia ya semiotiki. Semiotiki ni neno lililotoholewa kutoka neno lenye asili ya Kiyunani lenye maana ya uhakiki wa ishara. Hii ni nadharia yenye historia ndefu, yenye mielekeo ya uchunguzi wa ishara iliyozuka katika karne ya tano, wakati wa
Kushika kasi kwa nadharia ya semiotiki katika miaka ya 1960-1970 kumeambatana
na mwelekeo wa kuuasi na kuacha umuundo, ulioonekana kama uliofungika au
usiobadilika (Royle, 1995). Mikabala hii inahusishwa sio tu na Jacques Derrida,
mbali pia na wahakiki wengine kama Julia Kristeva, Michael Foucalt, Jacques
Lacan, Loius Althusser na Paul De Mann (Blamires, 1991). Nadharia ya semiotiki
katika kuangaza suala la uashiriaji humulika jinsi kazi hizo zinavyowasiliana na
wasomaji. Nadharia hii inajishughulisha na jinsi mpokezi anavyoipokea kazi fulani
anayoisoma (Innis, 1985).
Nadharia hii haisisitizi tu masuala ya kifasiri au jinsi tunavyofasiri kazi fulani tu
mbali pia usomaji wetu wa kazi na kujiuliza kwa nini kazi hizo huwa na maana
zilizo nazo kwa wasomaji tofauti. Kama wanavyosema Andrew Bennet na Nicolas
Royle (1995), jamii hushiriki mfumo wa kanuni na taratibu zinazokubalika na
jamii husika. Jamii moja huweza kutumia ishara za aina sawa na kuelewana katika
ufasiri wa maana na ujumbe. Hata hivyo ufasiri hutofautiana kwa watu binafsi.
Kwa mfano, neno 'mvinyo' linapotajwa huenda likatoa wazo au ishara tofauti
miongoni mwa watu wenye tajriba tofauti.
Aidha, kama wasemavyo wahakiki wa Chuo Kikuu cha Yale - Geoffrey Hartman, Hillis Miller, Paul De Mann na Harold Bloom, kuna uwezekano wa matini kuwa na
fasiri nyingi zinazolingana au kukinzana na zote zikakubalika. Mhakiki ana wajibu wa kupasua ishara za kisanaa na kiisimu,vipengele vyake vyote ili kuweka wazi
matumizi ya kiashirii na kiashiriwa chake na maana yaks huhamishwa au
huahirishwa (Blamires, 1991).
Licha ya nadharia ya semiotiki kufaidi na mikabala hiyo, imefaidi pia kutokana na
mawazo ya mwana-isimu wa Ki-Swizi, Ferdinard de Saussure, pamoja na
mwanafalsafa wa Ki-Marekani anayejulikana kama Charles Pierce (1977). Pierce
anahusishwa na kielelezo cha ishara kinachohusishwa na pembe tatu: ishara,
yambwa na kifasiri. Zingatia mchoro unaodhihirisha aina hizo za ishara kwa
mujibu wa Pierce ambao tofauti na mchoro wa Ferdinard de Saussure uliozingatia
zaidi isimu huu umejikita kwa ishara za kisanaa.
Ishara
Yambwa Kifasiri
Kwa mujibu wa mwanafalsafa huyu, kila ishara huwa na yambwa au kitendwa
kinachorejelewa. Kifasiri ni kile kinachochochewa katika akili ya anayefasiri ishara
hiyo. Pierce anaamini kuwa kila ishara ina misingi inakotegemezwa ili kufasiriwa
kwake kuwezekane. Misingi hiyo huzua ishara aina tatu: kielekezi, ishara stiari na
taashira. Misingi hii mitatu ya ishara itawekea misingi ya uchanganuzi wa matini
kudhihirisha fasiri nyingi za maana na ujumbe. Mtafiti ameweza kuhakiki kwa
kina ishara tofauti zilizoko katika mabango tofauti na kutambua maana
zinazosemwa wazi na kudhihirisha jinsi zinavyopingana ki-itikadi na yasiyosemwa
wazi.
Mhakiki mwingine aliyewekea misingi nadharia hii ni Barthss (1964, 1977, 1981,
1984b, 1986b). Barthes, anadokeza kuwa, lengo kuu katika kuhakiki matini, ni
kuivunja katika sehemu ndogo alizoziita leksia. Hivi ni kama vitengo vidogo vya
usomaji vinavyodhihirisha misimbo au kanuni fulani ambazo huwa muhimu
katika kuifasiri kazi fulani. Alizitambua aina tano kuu za misimbo ambazo
zitawekea misingi maridhawa utafiti huu.
Kwanza, kuna msimbo wa matukio. HUll unahusu msuko wa kazi. Msimbo huu
umemsaidia mtafiti katika uhakiki wa usanii wa picha na matini katika mabango
ya matangazo ya UKIMWI, na kutathmini jinsi picha zinavyoambatishwa kwenye
matini ki-athari na ki-sababishi,
Pili, ni msimbo wa kihemenitiki. Huu unahusu uchunguzi wa matendo ya
binadamu kama vile - upendaji, uchukiaji wa kazi kutokana na taharuki
zilizojengwa. Msimbo huu umemsaidia mtafiti katika kuchunguza kufumbatwa
kwa maana katika viunzi mbalimbali vya tangazo na namna vinavyojengeana
katika kutaharukisha wapokezi katika ufasiri wao wa maana na ujumbe. Msimbo
Tatu, kuna msimbo wa kisemu. Neno semu hutumika kuzielezea sifa bainifu za kisemantiki. Hizi ni sifa zinazotuwezesha kuipata picha fulani katika kazi, kwa
kuibua fahiwa za maana. Msimbo huu umemwezesha mtafiti kufafanua picha na
matini kwa kutumia unasibishi wa maana kwa kiwango kikubwa. Aidha,
umetuwezesha kugundua kuwa maana nasibishi ina uzito kuliko maana msingi ya
maneno, kwa vile hufafanua yale yasiyosemwa wazi na maneno, ishara na picha
katika mabango tuliyoyashughulikia ya UKIMWI.
Nne, upo msimbo wa ki-ishara. Huu ni msimbo muhimu katika usomaji na uhakiki wa kazi yoyote. Ishara huwakilisha viashiriwa fulani. Uhusiano kati ya ishara na kiashiriwa hujengewa na dhana zilizoko mawazoni. Msimbo huu umemsaidia mtafiti kutathmini viwakilishi na viwakilishwa vya maana katika
mabango ya matangazo ya UKIMWI.
Tano, kuna msimbo wa kirejelezi. Msimbo huu unajengwa kutokana na viashirii vya utamaduni na tajriba ya maisha. Kiashirii huweza kuwa kile kile bali
kinachorejelewa kikawa tofauti kwa mujibu wa utamaduni na tajriba ya maisha.
Msimbo huu umeupa utafiti huu nguzo imara katika kutathmini jinsi wapokezi wa
mabango ya matangazo ya UKIMWI nchini wanavyofasiri maana na ujumbe kwa
mujibu wa tajriba zao za maisha na falsafa za kitamaduni na kijamii.
Misimbo hii ya nadharia ya semiotiki imemsaidia mtafiti kuibusha fasiri tata
katika picha na matini za mabango ya matangazo ya UKIMWI. Aidha, kwa
ya UKIMWI mtafiti ameweza kujumulisha maoni ya watafitiwa ili kupendekeza
namna ya kuboresha mabango yanayohusu masuala ibuka kama suala la UKIMWI
nchini.
1.8.0
UDURUSU
WAMAANDISHI
Udurusu huu utahusu maandishi ya kijumla kuhusu semiotiki, tahakiki za tafiti
bayana za lugha zingine na kisha tafiti katika lugha ya Kiswahili.
1.8.1MaandishiyaJumla kuhusu Semiotiki
Semiotiki kama ilivyosemwa hapo awali, ni utohozi wa neno linalotokana na lugha
ya Kiyunani lenye maana ya ishara. Neno hili linatokana na muungano wa
maneno mawili. Maneno haya ni 'Logos'(maneno) na Semeion (yanayohusiana na
ishara). Hivyo semiotiki ni sayansi inayojihusisha na mifumo ya ishara na
uashiriaji. Baadhi ya wataalamu wanaiita semiolojia badala ya semiotiki.
Watalamu wengi kama vile: Pierce 1931, 1977, Stokoe 1972, Voloshinov 1973,
Guiraund 1975 Eco 1976 Barthes 1964, 1977, 1984b, Innis 1986 wamekubaliana
kuwa semiotiki hujishughulisha na namna waandishi wanavyowasilisha ishara
zinazofumbata na kusimba maana, hivi kwamba wasomaji wanafanya juhudi
kupata na kusimbua maana iliyosimbwa.
Ishara zote ziwe za kiisimu au za kisanaa hushughulikiwa kisemiotiki. Ishara hizo
huwa na maana iliyo dhahiri. Maana hii dhahiri hurejelewa kama maana halisi au
maana msingi ya ishara. Maana hii haihusishwi na hisia au mahusiano
kijamii. Mtazamo wa kisemiotiki uliohusiana na mwana isimu wa kiswizi,
Ferdinard de Saussure, ulijikita zaidi katika maana hii msingi bila kuingilia maana
batini ya ishara husika.
Wataalamu kama vile: (Pierce 1931, Eco 1976, 1977, 1978 , Barthes 1977, Innis
1986) wanahusisha ishara na maana msingi na pia maana batini kwa kuegemea
mantiki. Maana msingi wanasema ni kile kilichomo katika matini, picha, mchoro,
kibonzo, bango na kadhalika. Maana batini husimbuliwa na mpokezi kwa kufasiri
namna picha, mchoro, kibonzo au bango husika lilivyosawiriwa. Hata hivyo
wanasema kuwa maana hizi huingiliana hivi kwamba hakuna mipaka mwafaka
inayoweza kuwekwa waziwazi. Hili linatokana na wazo linaloelezwa na Voloshinov
(1973: 105) ya kuwa, maana msingi ni gari la kusafirishia fasiri za maana batini na
nasibishi, hivi kwamba ung'amuzi na ufasiri wa maana hizi hauwezi
kutenganishwa kwa njia yakinifu.
Semiotiki husaidia kuangazia ufasiri wa maana kwa kuwa ishara haziwasilishi tu
maana lakini huwa zenyewe kifaa cha kuibulia maana. Ishara lazima ziwasiliane na
kuwasilisha maana pale tu, wapokezi wenyewe watajishughullsha kwa mapana na
marefu kupata na kusimbua maana kwa vile haziwasiliani kidhahiri.
Ni kutokana na sayansi hii inayojishughullsha na ishara, tunatambua kuwa lugha
zote hukusudia kuwasiliana lakini sio mawasiliano yote hutokea kutokana na
lugha. Barthes (1984b) amedhihirisha mchango wa semiotiki katika kuhusisha
Semiotiki, hivyo basi hutudhihirishia kuwa hakuna njia ya mawasiliano inayofaa
kudunishwa au kuonekana bora zaidi ya nyingine. Ukweli ni kuwa maana haiwi
katika njia au mkondo wa mawasiliano kama vile, matini, bango, picha na
kadhalika. Maana hupatikana tu iwapo imewekezwa na kukabidhiwa kwa ishara
fulani ya kisanaa au ya kiisimu. Hakuna kitu ambacho ni ishara hadi pale
tunakifasiri kama ishara. Chochote kinaweza kuwa ishara iwapo kinachukuliwa
kama chenye uashiriaji fulani. Hivi ni kusema kuwa ishara na uashiriaji
huambatana na hali kubalifu za mahusiano ya ishara kwa mtu binafsi na jamii
kwa ujumla. Semiotiki imeainishwa katika mitazamo kama vile:
• Semiotiki jumu1ifu inayoshughulikia nyanja zote zinazohusisha ishara na
uashiriaji.
• Semiotiki ya ldjamii inayohakiki ishara na kuzihusisha na mitazamo na
falsafa za kitamaduni na kijamii. Uchanganuzi huu hutuwezesha kufahamu
kuwa tofauti katika ufasiri wa maana za ishara hutokana na mawazo na hali
kubalifu za mtu binafsi na zile za kijamii zinazopokezanwa kizazi hadi
kizazi na hutofautiana kutegemea tamaduni mbalimbali.
• Semiotiki mawasiliano. Huchanganua matini za televisheni, radio,
filamu, vibonzo, magazeti, matangazo katika majuzuu na mabango na picha
ili kusimbua maana zilizosimbwa. /
Mitazamo hii ndiyo dira inayotawala na kuelekeza utafiti wetu.
1.8.2 Tafiti katika Lugha Zingine
Hams ndiye mtaalamu wa kwanza kuwekea msingi utafiti katika uwanja wa
lugha ya utangazaji aligundua kuwa lugha hutokea katika muungano fulani na
hivyo basi akatafiti aina za miungano hiyo kwa kutumia mtazamo wa uchanganuzi msambao. Utafiti wake ulihusisha kipengele cha mshikamano katika mipangilio ya
kauli au sentensi katika matangazo ya biashara. Utafiti huu umejengea utafiti wetu
hasa katika kuchunguza mipangilio ya maneno katika matini zilizoko katika
mabango ya matangazo ya UKIMWI, ili kubainisha maana kinzani na fasiri tata.
Tofauti iliopo ni kuwa, utafiti huu haukuzingatia tu mshikamano wa matini pekee
bali umechunguza:
• Utendakazi wa matini.
• Maana na ujumbe unaowasilishwa na matini.
Isitoshe, mbali na kuzingatia kipengele cha lugha ya maneno (ishara za kiisimu),
utafiti huu umeshughulikia ishara zisizo za kiisimu kama picha na ishara, ambazo
zina uwezo wa kuwakilisha maneno zaidi ya elfu moja katika uwasilishaji wa
maana na ujumbe.
Lambert (1989) alifanya utafiti juu ya sarufi na uamilifu wa muktadha katika
matini. Alinuia kueleza mwingiliano wa sarufi na muktadha katika kutunga na
kufasiri matini kimuktadha. Alifanya hivyo kwa kuzingatia vigezo vya uchanganuzi
wa muktadha kisha akaainisha aina za miktadha inayobuni matini mbalimbali.
Utafiti huu unahusiana na utafiti wake kwa sababu unatafiti muktadha kama
mojawapo ya vipengele vinavyochangia ung'amuzi na ufasiri wa maana na ujumbe katika matini na picha katika mabango. Hata hivyo, utafiti wetu haukujikita katika
kigezo toshelevu cha kuibua maana ya ujumbe, bali kuna vigezo vingine vingi
vinavyochangia ung'amuzi na ufasiri wa maana na ujumbe katika matini na picha
(Guiraund.uczs).
Wataalamu wengine kutoka maeneo mengine waliosaidia kuwekea msingi utafiti
huu ni Vestergaard na Schr0eder (1985). Katika kazi yao, wamedhihirisha kuwa lugha ya matangazo ya kibiashara huambatana na hali, wakati mielekeo na
matarajio ya jamii. Lugha inayotumika kushawishi na kuiathiri jamii kuhusu
bidhaa fulani huzingatia bidhaa zenyewe zinazotangazwa, zinalenga hadhira gani
-kiumri, kiellmu, jinsia na daraja la kiuchumi. Wanaeleza namna lugha
inavyotumiwa katika matangazo ya biashara ill iweze kutimiza malengo fulani.
Watangazaji wanazingatia suala la mahitaji ya kijamii ya hadhira yao ill kuweza
kuyatumia mahitaji yale kuiathiri na kuishawishi hadhira ile. Kazi hii imekuwa
muhimu katika utafiti wetu. Tofauti ni kuwa walishughulikia kipengele cha
matangazo ya kibiashara ilhali utafiti wetu umejikita zaidi katika kipengele cha
matangazo ya huduma, hususan huduma za afya katika jamii.
Mtafiti mwingine aliyeshughulikia swala la utangazaji ni Inglis (1972) anayesema kwamba matangazo ya biashara huunganisha bidhaa au huduma zinazotangazwa
na mielekeo na matarajio ya jamii husika. Kuweza kuathiri na kushawishi jamii,
tangazo lolote linafaa kuzingatia hall na hisia za hadhira kuambatana na mazingira
na muktadha wa wakati na utamaduni. Kazi hii imekuwa nguzo imara ya utafiti
wetu, tofauti ni kuwa alizingatia matangazo ya biashara ilbali utafiti wetu
Mtafiti mwingine aliyechanganua lugha ya matangazo ya biashara ni Barthes (1984b). Aligundua fasiri tata na polisemi za maana katika matangazo na
akapendekeza matumizi ya lugha elekezi inayoambatana na misingi ya jamii
husika. Judith Williamson (1983) alichunguza maana ambazo hazisemwi wazi katika matangazo. Maana hizi nasibishi huibuliwa na wapokezi wa matangazo
yenyewe. Tanaka (1994) alitathmini utata katika matangazo unaoweza kuibua
farakano kati ya hali halisi, miongoni mwa hadhira na jamii kwa ujumla kutokana
na fasiri potovu. Forceville (1996) alichunguza stiari picha katika matangazo ya biashara katika mabango kutoka nchi mbalimbali kama vile: Ulaya, Ujerumani, Ufaransa na kadhalika. Alikusudia kudhihirisha kuwa picha hubeba tamathali
kadhaa zikiwemo tashibiha, stiari, jazanda na taashira. Tafiti hizi zote zimeupa
msingi imara utafiti huu. Tofauti ya tafiti hizo na utafiti huu ni kuwa, utafiti huu
umeshughulikia kipengele mahsusi cha utangazaji kinachoonekana kupuuzwa na
watafiti hao - kipengele cha matangazo ya huduma.
Gachara (2005) ameshughulikia lugha ambayo inatumiwa katika kampeini za
kuhamasisha umma kuhusu ugonjwa sugu wa UKIMWI. Alilinganisha na
kulinganua utoshelevu wa matini zilizoandikwa na zile za kiusemi katika uwasilishaji wa ujumbe kwa umma. Katika utafiti wake aligundua kuwa matini
zilizoandikwa zilikuwa toshelevu zaidi ya zile zilizokuwa katika hall ya usemi.
Utafiti wake umejengea utafiti huu kwa kubainisha ni nini kinachochofaa
kusemwa wapi, lini na kwa akina nani. Hata hivyo utafiti huu unatofautiana na
yaliyotolewa kwa Kikuyu hasa nyimbo na matangazo katika redio na televisheni.
Isitoshe utafiti wake ulikuwa jumulifu katika kuelezea utoshelevu wa matini zote
zilizoandikwa pasi kutujulisha ni gani illyo toshelevu zaidi na kwa sababu gani, na
zile ambazo si toshelevu ni nini hasa kinachofaa kufanywa ill pia ziwe toshelevu.
Utafiti wetu umechunguza kipengele kimoja mahsusi - mabango ill kutathmini
utoshelevu wake kwa watu wote nchini, kwa kuoanisha muktadha, ishara za
kiisimu na zile za kisanaa katika uibuaji wa maana na ujumbe.
1.8.3Tafiti katika Lugba ya Kiswabili
Kitsao (1975) alifanya utafiti wa kimtindo kuhusu maandishi katika uandishi wa
barua, magazeti na riwaya. Alitumia nadharia ya mtindo ill kubainisha mitindo ya
matumizi lugha katika viwango vya sarufi na semantiki. Utafiti huo umejengea
utafiti huu kwa kuzingatia usanii wa matini katika mabango, hasa kwa kuzingatia
kuwa, katika kuchunguza maana, msomaji anaanza kwa hatua ya kukisia maana za
kazi nzima. Msomaji hawezi kuzielewa au kuzifahamu sehemu za kitu (matini na
picha) bila kuelewa kitu kizima chenyewe, na pia hawezi kukielewa hicho kizima
bila ya kuzifahamu sehemu zake. Sehemu za kazi na ukamilifu wa maana
unategemeana. Tofauti, ni kuwa utafiti huu haujikiti kwa riwaya na magazeti na
barua ball umezingatia usanii wa matini na picha katika kufanikisha ung'amuzi na
ufasiri wa maana na ujumbe katika mabango ya matangazo ya UKIMWI.
Habwe (1999), alifanya utafiti kuhusu uchanganuzi usemi katika hotuba za
Kiswahili nchini Kenya. Alitumia mitazamo ya Halliday na Hassan (1976) na
sana katika hotuba hizo. Pia allgundua kwamba maana katika hotuba hizo huwa
zaidi ya maneno yanayotumiwa. Hivyo maneno yallbeba maana fiche. Wanasiasa
waligeuza maana ill kutosheleza hall tofauti, matarajio yao pamoja na yale
wanayoyadhania kuwa matarajio na mahitaji ya hadhira zao. Utafiti huo
umetumiwa kama msingi wa utafiti huu hasa katika kubainisha kuwa yasiyosemwa
wazi hupingana na yasemwayo wazi. Hata hivyo kazi hii imetofautiana na yake
kwani alishughulikia lugha ya kisiasa.
Michira (1993) allchunguza lugha ya wachuuzi na matangazo redioni. Utafiti wake
ulijikita katika misingi ya nadharia ya elimu-mitindo. Alishughulikia uteuzi na
matumizi ya msamiati katika mitindo hiyo miwili ya matumizi lugha. Aligundua
kuwa aina zote mbill za matumizi lugha huonyesha mchanganyiko wa misimbo,
sintaksia na lugha sahili ambayo ina makosa mengi ya kisarufi. Utafiti huu
umefaidi kutoka kwa utafiti huo hasa katika kubainisha mbinu, mikakati na
vipengele vya matini katika mabango, vinavyofanikisha ufasiri wa maana na
ujumbe. Kazi hii imetofautiana na utafiti huo kwa vile alishughulikia lugha ya
usemi.
Mtafiti mwmgme allyeshughulikia swala la matangazo ni Ojwang' (1986)
aliyechunguza matini za matangazo ya uajiri wa kazi katika magazeti. Ojwang'
alishughulikia matangazo kutoka magazeti na majarida matano, kutoka nchini
Kenya na kuchunguza jinsi lugha ya matangazo haya illvyokuwa kielelezo cha
muktadha wa mawasillano na utamaduni chipukizi wa mashirika na makampuni
wapi na kwa nani huathiriwa pakubwa na muktadha wa mawasiliano na
utamaduni wa wale ambao wanahusika (Dittmar, 1976).
Aloo(2002) alichunguza matangazo ya biashara katika redio na televisheni. Utafiti wake ulidhihirisha jinsi matangazo ya biashara yanavyoshawishi hadhira bila
kuifahamisha vya kutosha kuhusu bidhaa zinazotangazwa. Utafiti wake pia
ulidhihirisha mbinu mbalimbali za ushawishi pamoja na mbinu za lugha
zinazotumiwa na watangazaji katika matangazo ya biashara. Utafiti huo umejengea
utafiti huu hasa kwa kubainisha mbinu za lugha zilizotumika katika usanii wa
maandishi katika mabango ya matangazo ya UKIMWI. Tofauti ni kuwa utafiti
wake ulishughulikia matangazo ya biashara na hasa matangazo katika hali ya
usemi bali sio matini zilizoandikwa.
Uhakiki wa tafiti za humu nchini na ziIe za maeneo mengine, umebainisha kuwa
kipengele cha matangazo ya huduma kinafaa kushughulikiwa ili kudhihirisha
kama mbinu zinazotumika katika matangazo ya biashara hutumika pia kufanikisha
matangazo ya huduma. Aidha, tafiti nyingi zimechukulia kuwa lugha ya maneno
ndiyo pekee inayowasilisha maana na ujumbe. Imebainika kuwa tafiti hizi bayana
zimechunguza sifa na kanuni za muktadha na matini katika uwasilishaji wa maana
na ujumbe. Tafiti hizo zimetuwezesha kuona uhitaji wa kuchunguza ishara zisizo
za kiisimu kama picha na ishara za kisanaa, kama msingi wa uwasiIishaji wa
muktadha hazijashughulikiwa katika tafiti hizo ili kudhihirisha namna
vinavyochangiana na kutegemeana katika kuwasilisha maana na ujumbe.
1.9.0
Mbinu za Utafiti.
Utafiti huu ulihusisha mbinu za aina mbili.
Utafiti Maktabani ulihusu usomaji wa mapana wa makala, machapisho,
majarida na tasnifu zinazohusiana na mada yetu ya utafiti ili kuimarisha hoja za
utafiti huu. Vitabu ambavyo waandishi wameshughulikia matangazo tofauti
tofauti, makala yanayohusu uchanganuzi matini na yale yanayozingatia
uchanganuzi wa picha na ishara mbalimbali vimerejelewa. Mtafiti amerejelea pia,
vitabu ambavyo vinaelezea zaidi kuhusu nadharia ya semiotiki. Huduma za
mtandao zimemfaa vilevile.
Utafiti Nyanjani ulifanywa kwa nia ya kutathmini ufasiri wa maana na ujumbe
katika mabango ya matangazo ya UKIMWI kwa wapokezi tofauti tofauti.
Watafitiwa walioshirikishwa walitoka katika maeneo ya miji katika wilaya ya
Thika. Maeneo ya Thika yaliteuliwa kwa kuwa tarakimu zilidhihirisha kuwa, mji
huu una idadi kubwa ya maambukizo ya UKIMWI nchini ambayo ni 34% (NACC
2005). Maeneo yaliyoshughulikiwa ni Githurai kuwakilisha maeneo ya kimji yaliyo
na mseto wa watu wa makabila na biashara anuwai na maeneo ya Kiandutu
yaliyowakilisha maeneo yenye umaskini uliokidhiri. Hivi ni kumaanisha kuwa,
mtafiti alijaribu kupata fasiri za maana kutoka kwa watu wenye falsafa na mielekeo
tofauti nchini kwa kuwa suala la UKIMWI huhusishwa na hadhi ya kiuchumi, na
1.9.1Sampuli.
Mtafiti amechanganua mabango thalathini na matano kuambatana na mada kuu,
maudhui na malengo tofauti, kwa mujibu wa Baraza la Kupambana na UKIMWI
Nchini (NACC2005).
Mada
Matumizi Ya Kondomu
Ususiaji Wa Ngono
Maafa Ya UKIMWI
Kuishi Na Waliougua UKIMWI
Huduma Za HUU
Jumla
Idadiya Mabango.
7
7
7
7
7
35
Mabango haya yamekusanywa kwa njia mbili. Mabango yaliyotundikwa kwenye
barabara na maeneo mengine, na ni makubwa zaidi, yamepigwa picha. Pili, yale
madogo yaliyoangikwa katika maeneo tofauti; mtafiti ameyakusanya kwa minajili
ya uchanganuzi katika utafiti huu.
Hatua ya pili ilihusu uteuzi wa mabango mawili kutoka kwa kila kategoria
yaliyopatiwa watafitiwa walioteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio kwa vile kuna
masuala mengi ambayo mtafiti alitilia maanani kama yaliyoweza kuathiri ufasiri
wa maana na ujumbe katika mabango husika. Mbinu ya hojaji ilitumika. Hojaji
iliyotumika katika utafiti huu ni hojaji wazi iliyomtaka mtafiti kuibua fasiri tofauti
iliandikwa na kuwasilishwa kwa watafitiwa kwa lugha ya Kiswahili kwani mtafiti
alichukulia kuwa, lugha ya Kiswahili inaweza kutumika kama chombo cha
mawasiliano nchini kwa wote. Sampuli ya watafitiwa waliohusishwa, walitoka
eneo la Thika kutokana na ithibati kuwa maenezi ya ugonjwa wa UKIMWI katika
eneo hili umekuwa janga kwa muda mrefu, Isitoshe, kwa mujibu wa ripoti ya
NACC(2005) inadhirisha wazi, kuwa miji yenye idadi kubwa zaidi ya maambukizo
ni kama vile: Thika - 34%, Busia - 29%, Nakuru - 26% na Kisumu - 29%. Katika
vituo vya kukagua akina mama waja- wazito, miji hii hususan mji wa Thika
umedhihirisha kiwango kikubwa cha maambukizo katika mwaka 1990-2004.
Mtafiti aliteua maeneo mawili ya Wilaya ya Thika - Githurai ikiwakilisha sehemu
za miji yenye mchanganyiko wa makabila mengi na pia kutokana na umaarufu
wake kama kituo cha biashara anuwai hivyo tulipata sampuli wakilishi ya vitengo
mbalimbali vya watu. Maeneo ya Kiandutu yaliteuliwa kuwakilisha maeneo duni
na yenye umasikini uliokithiri. Umaskini ni kigezo muhimu kinachodhihirisha
ukosefu wa maendeleo katika masomo na tajriba zinginezo zinazoathiri uwazaji wa
mtu na jamii kwa ujumla. Uchaguzi wa maeneo haya ulizingatia shabaha ya utafiti
hasa kuhusiana na ung'amuzi na ufasiri wa maana na ujumbe katika mabango ya
matangazo ya UKIMWI kuambatana na vitengo mbalimbali vya watu nchini,
wenye matarajio, mielelekeo na falsafa tofauti. Watafitiwa ishirini kutoka kila
eneo la Kiandutu na Githurai walishirikishwa, jumla ya watafitiwa waliotoa fasiri
1.9.2 Ukusanyaji wa Data.
Watafitiwa walikabidhiwa mabango kumi kila mmoja kati ya mabango yote thalathini na matano yaliyokuwa yamepigwa picha na kukusanywa, ili kuyatathmini na kuyafasiri. Fasiri zote za maana na ujumbe zilizoibuliwa zilijazwa kwenye hojaji wazi zilizokuwa zimetayarishwa na mtafiti. Wale ambao hawakuweza kusoma na kuandika, mtafiti aliwaongoza kwa kutumia hojaji hiyo hiyo.
1.9.3 Uchanganuzi wa Data
Mtafiti amechanganua picha na matini kwa kuongozwa na misimbo ya nadharia ya semiotiki kwa mujibu wa Barthes, (1964, 1977, 1981, 1984b) iliyokuwa dira ya kuongoza uhakiki wa:
• Yaliyomo katika mabango.
• Maana ashiriwa na maana husishi katika picha na matini kwa kurejelea maoni ya watafitiwa.
• Maoni na hisia za watafitiwa kuhusu maana wazi na maana fiche katika matini.
• Vigezo vya uwiano wa picha na matini.
Pili, mtafiti amechanganua miktadha inayosaidia katika ufasiri na welewa wa maana na ujumbe katika mabango. Maoni ya watafitiwa yamerejelewa ili kuondoa unafsishi wa maoni ya mtafiti. Fasiri na maoni ya watafitiwa kuhusu mabango ya UKIMWI yamekadiriwa kufuatia asilimia ya watafitiwa waliotoa mchango wao ifuatavyo:
X= Idadi ya watafitiwa wote arubaini.
Takwimu hizi zimechangia katika kudhihirisha fasiri za watafitiwa, ung'amuzi na
ufasiri wao wa mahusiano ya ishara, maana na ujumbe katika mabango ya
UKIMWIpamoja na hisia zao kuhusu picha na matini zilizoshirikishwa.
1.9.4 Uwasilisbaji wa Data
Matokeo katika tasnifu hii yamewasilishwa kwa njia ya maelezo yaliyojumuisha
mabango yaliyohakikiwa. Aidha, matokeo yote kutokana na hojaji wazi ambazo
zilikabidhiwa watafitiwa yamechanganuliwa, yakapangwa na kuwasilishwa kwa
kutumia majedwali. Uwasilishaji wa data ni elezi kwa kiasi kikubwa. Maelezo haya
yamejumulisha na kudhihirisha fasiri za watafitiwa wote walioshirikishwa katika
utafiti nyanjani na kujumuisha utangulizi na mahitimisho ya sura mbalimbali ili
kuonyesha ukamilifu wa maelezo kwa kuzingatia malengo ya utafiti.
Hitimisho.
Katika sura hii tumeshughulikia vipengele muhimu katika utangulizi wa utafiti
vikiwemo swala la utafiti, malengo na maswali ya utafiti, mbinu za kukusanya,
kuchanganua na uwasilishaji wa data. Misingi ya nadharia mwafaka kuongoza na
kuelekeza utafiti huu zimeelezwa. Msingi wa nadharia na mbinu za utafiti
zinasisitiza nafasi ya picha na ishara katika kuwasilisha maana na ujumbe na
namna mpokezi anavyofasiri picha na ishara zilizoshirikishwa katika mabango ya
matangazo ya UKIMWI. Katika sura inayofuata tumeshughulikia maana halisi,
SURAYAPILI
VIUNZI VYA MATANGAZO
Utangulizi
Sura hii tumeangalia jinsi mtazamo wa kisemiotiki unavyoshughulikia maana
msingi katika picha na matini. Katika kazi zinazohusisha ishara anuwai kama
vile matangazo, mtazamo wa kisemiotiki huchunguza mfumo wa maana kupitia
kwa uratibu wa viunzi tofauti katika matangazo (Barthes 1984b). Msisitizo huwa
katika msuko wa picha na ishara zinazochukuliwa kama kiini kinachofuma
maana na ujumbe katika matangazo husika. Maana msingi ni maana halisi ya
picha ambayo haihusishi hisia, tajriba na falsafa za mtu binafsi na za kijamii. Hii
ni maana ambayo yeyote ataipata kwa kuwa inapatikana waziwazi kutoka kwa
tangazo husika na ndiyo huhimili ujumbe unaoibuliwa na wapokezi mbalimbali
(Williamson, 1978).
Tumetathmini maana msingi katika matangazo ya UKIMWI kwa kujikita kwa
viunzi vyote vinavyoshirikishwa kwenye bango vikiwemo: picha na ishara kwa
kuzingatia namna zilivyosukwa pamoja na matini zilizoambatishwa. Matini
zimetengwa katika vitengo vifuatavyo:
• Vichwa vikuu.
• Wito.
Imehalisi kuchunguza ni vipi utangamano mwafaka wa viunzi hivyo vyote
vinavyohusishwa, unavyokuwa nguzo imara ya kujengea maana msingi
zinazojidhihirisha katika mabango ya matangazo mbalimbali ya UKIMWI.
2.1.0 Picha na Ishara
Picha na ishara zimechukua nafasi kubwa katika mabango ya matangazo mengi
ya UKIMWI ili kuiteka nadhari ya hadhira. Picha na ishara zinazoshirikishwa
ndizo zinazochukua sehemu kubwa ya mawazo yanayopitishwa, kwa kuwa
yanayoonwa hukumbukika na kubakia katika nadhari ya hadhira kuliko yale
yanayosomwa (Jefkins 2002).
Msanii wa picha na ishara katika matangazo huwajibika kuziwasilisha kwa njia
inayoeleweka kwa kuakisi tajriba na matarajio ya hadhira yake. Kwenye data
zetu picha na ishara zimesaniiwa kwa njia inayodhihirisha umakinifu katika
uteuzi, kwa kuhakikisha kuwa picha zinaoana na ujumbe unaotolewa. Mabango
haya yamesukwa kwa njia yenye mvuto, rangi za kupendeza na kwa uratibu
unaoitaharukisha hadhira. Mpokezi anapolitazama bango fulani, linamvutia
toka mwanzo mpaka mwisho ill apate maana yake kikamilifu. Hivi ni kusema
kuwa, kuna mwingiliano fulani, kati ya yaliyomo katika tangazo na wapokezi,
kwa mujibu wa uwezo wao wa utambuzi wa mahusiano ya ishara. Mfano mzuri
wa tangazo linaloiteka nadhari ya kila mpokezi, kutokana na muktadha
mwafaka unaoakisi matarajio ya jamii ya wakati huu, rangi zenye mvuto, lugha
Katika tangazo hili, maana msingi inajidhihirisha wazi, hata rwapo matini
zilizoambatishwa ni haba ambapo tunapata ni kauli moja fupi:
JIKINGE..AIDS isReal!
JIKINGE...UKIMWI niUhaIisi!
Picha hii imeratibiwa kwa njia ambayo mpokezi anaipata maana msingi pasi
kutegemea ufafanuzi wa matini. Sawia, picha na ishara ambazo zimeambatishwa zinaonekana kutimiza majukumu yafuatayo kulingana na
maoni ya watafitiwa:
• Kuvuta tabasuri ya wapokezi.
• Kusaidia msomaji wa tangazo kukumbuka kiini cha ujumbe hata
baadaye.
• Kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala linalotangazwa.
• Kuboresha muktadha na kumtamanisha msomaji kwa yaliyomo katika
tangazo.
• Kuhimili maelezo ya matini.
• Kuimarisha vidokezi muhimu na imara ili kuvibaidi na vidokezi hafifu na
sadifu.
• Kubainisha hadhira lengwa na kuitenga kutokana na hadhira sadifu.
Kwa kuzingatia yaliyomo katika bango, kwa mbali tanapata mastakimu ya
kifahari iliyozingirwa kwa ua imara. Mazingira yametunzwa vyema, kuashiria
haiba na utukufu wa wenyeji wa makazi hayo. Hata hivyo, haya yote hayaipi
familia iliyosawiriwa naima yoyote, kwa vile sononeko na majonzi yanashamiri
nyusoni za wahusika katika bango hili. Inaonekana wazi wameondokewa na
mmoja hasa kutokana na pengo lililoko baina ya mama na mtoto wao msichana.
Mikono yao imewekwa katika namna inayodhirisha hali ya kukata tamaa. Asili
ya simanzi kuu walionao wahusika hawa inaelezewa kinaganaga na jeneza lililo
kando nyuma yao, linalodhihirisha kuwa kifo kimewapokonya mwandani wao
kutokana na janga la UKIMWI. Matini imeambatishwa kudhihirisha kuwa
UKIMWI ni uhalisi bali si ugonjwa wa kupuuzwa na kufanyiwa masihara na
Ni dhahiri kuwa picha na ishara zinazoshirikishwa katika tangazo huweza
kuwapa shauku wasomaji au pia kuwapunguzia shauku zao kulingana na jinsi
zilivyowasilishwa na kutumiwa.
2.1.1 Maana za Picha na Ishara
Katika uchanganuzi wa kisemiotiki, picha na ishara huchukullwa kama kitengo
mojawapo cha usemi, kinachotarajiwa kuwasiliana na wapokezi kwa kuchochea
au kusaili dhana fulani (Tanaka 1994). Katika hall hii, usemi sio kifaa cha
unenaji bali umbo la kijamii la kuwasilisha ujumbe na kuingiliana. Hivyo basi,
picha huwa na sura na sifa za usemi zinazojidhihirisha katika msuko au
muundo wa tangazo. Msuko wa picha huwa na mchango mkubwa katika
kuathiri mkondo wa maana na ujumbe kwa wapokezi. Matangazo husomwa
kufuata mpangilio wa juu chini unaojengea mshikamano wa mifumo ya maana
(Gombrich 1977).
Matangazo mengi yaliyoambatishwa picha yameathiriwa pakubwa na mazoea ya
usomaji wa matini hivi kwamba msuko wa picha zenyewe katika mabango
hufuata mkondo wa usomaji kutoka kushoto kuelekea kulia. Msuko huu ni
muhimu katika kuelekeza jicho la wapokezi katika kutalii na kutathmini
yaliyoshughulikiwa katika tangazo. Miundo ya matangazo yanayoshirikisha
picha hullnganishwa na miundo ya sentensi. Kwa mfano, katika sentensi
yanayofahamika hutangulia mwanzo ili kuelekeza wapokezi kwa mapya
Halima ni mhadhiri.
Halima kama mhusika anafahamika, lisilojulikana ni kuhusu kazi anayoifanya ambayo sasa inabainishwa. Mpangilio huu umetumika katika mabango mengi
ya matangazo ya UKIMWI.
Kichwa kikuu kinadokeza hususan yale yanayofikirika kufahamiwa na hadhira
lengwa na kuambatishwa picha inayochukua nafasi kubwa ya tangazo Hi
kukijadili na kukihimili. Picha hii inafafanua mambo ambayo yamedokezwa katika kichwa kwa kina, na kumwelekeza msomaji wa tangazo kulitalii na
kulielewa swala linalojadiliwa vyema.
Mushkili katika ung'amuzi wa maana unaoweza kuibuliwa na picha,
unasuluhishwa kwa matini zinazoambatishwa Hi kumwezesha mpokezi kujikita tu kwa vidokezi imara asije akayumba sana na kupotosha maana. Matini hizi
zinazoambatishwa kuihimili picha na kutoa ufafanuzi zaidi zinakuja baadaye,
aghalabu upande wa kulia au chini ya picha zenyewe. Vestergaard na Schr0eder
(1985) wanadokeza kuwa matangazo mengi yanayoambatisha picha katika
kufafanua maana na ujumbe hufuata mpangilio huu unaozingatiwa katika lugha andishi.
Wasanii wa matangazo yanayohusisha picha na ishara, hutanguliza kwa kiini
cha tangazo katika kichwa, hatimaye picha huambatishwa na kutolewa
huu wakutanguliza yanayofahamika na kukubalika katika jamii ya wakati wa
leo, na kuyafafanua zaidi kwa picha na ishara zinazofuatiliwa na matini fafanuzi
BANGONA.2
ni bango hili la Na. 2.Tangazo hili linadhihirisha mwambatano fulani wa viunzi
mbalimbali ambavyo vinashirikishwa katika tangazo vikiwemo:
• Kichwa cha tangazo.
• Picha.
• Wakala wa tangazo.
• Picha ndani ya picha.
Kichwa kinalenga moja kwa moja kwenye maana lengwa
Picha ambayo imeambatishwa inaonyesha umoja wa
wote: wanaume kwa wanawake, wazee kwa vijana, na Wakristo kwa Waislamu
katika juhudi za kupambana na janga la UKIMWI. Umoja huu wa wote
unadhihirishwa na picha ya wanaume watatu na wanawake wawili
waliounganisha viganja vya mikono ishara ya umoja ni nguvu na utengano ni
udhaifu hususan katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Katika kufafanuamaana kwa kina na kwa uwazi zaidi, picha hii ina wanaume
watatu. Mmoja ni Mwislamu kwa mujibu wa kofia aliyojivika kichwani. Wa pili,
ni Mkristo kutokana na tasbihi aliyoiweka shingoni inayotofautiana na tasbihi
za kiislamu. Tasbihi yenyewe imening'inia kifuani. Mwanamume wa tatu
haifahamiki yeye ni muumini wa dini gani na pia wanawake wawili waliomo
kwenye picha. Wote wameunda nusu mduara kwa kushikanisha viganja vya
mikono yao pamoja ill kusawiri haja ya ushirika. Macho yao yamekondolewa na
kuangazwa kuashiria umakinifu wa kila mmoja katika kadhia hii ya kuangamiza
UKIMWI nchini. Picha hii imeambatishwa matini:
Msisitizo unatokea kwa urejeleshi wa mada hizo tatu kusudio chini ya picha, na
1. Usifanye mapenzi kabla ya ndoa.
2. Kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja daima.
3. Kama huwezi kufanya mawili hayo,jildnge nakondomu.
Kiunzi cha tangazo hili kinachofuata ni wito. Wito unaotolewa ni marudio ya
maneno yaliyotolewa katika kichwa. Hivi ni kusema kuwa, wito huu ni
msisitizo bayana wa mada kuu katika tangazo kwa vile ni marudio tu ya
maneno yale yale yaliyo kwenye kichwa kikuu, lakini wakati huu yameandikwa
kwa herufi ndogo zikilinganishwa na hati zilizotumiwa kwenye kichwa kikuu
cha tangazo hili.
Chini ya wito huu ni picha ndogo iliyo ndani ya picha kubwa, inayodhihirisha
muumano wa viganja vya mikono vinavyounda aina ya mzunguko. Duara
lililoundwa kwa kushikarnanisha viganja vya mikono linashadidia maana
iliyotangulizwa katika kichwa kuhusu juhudi za pamoja kuangamiza UKIMWI.
Katika kuhitimisha msuko wa tangazo, ni wakala wa tangazo hili unaochangia
uimarishaji na kuaminika kwa maana na ujumbe katika tangazo:
National AIDS Control Council.
Baraza La Kupambana na UKIMWI.
Kila kijisehemu kina ujumbe mdogo kinachochangia kitengo kikuu cha mfumo
kamilifu wa maana msingi katika tangazo. Hivyo, kuna utegemeano na
ujengano wa vipashio tofauti katika ujenzi wa maana msingi inayojidhihirisha
katika tangazo. Kwa mfano, wito wa tangazo unasisitiza tu, yaliyotangulizwa
katika kichwa, ilhali wakala wa tangazo unaimarisha vidokezi muhimu katika
tangazo. Tangazo lingine ambalo linadhihirisha mwambatano na ujengano wa
viunzi tofauti katika kuimarisha welewa wa wapokezi ni bango hili la Na. 3.
Tangazo hili lina viunzi vifuatavyo:
Kichwa kikuu ambacho kimeandikwa kwa muundo wa nusu duara,
MEN: CAST THE WINNING DICE AGAINST AIDS.
WANAUME: WATUPA DADO YA USHINDI DHIDI YA UGONJWA WA
UKIMWI.
Picha inayoambatishwa tangazo hili ni ya mshumaa unaowaka uliozingirwa na
ni mweusi na umezingirwa na duara dufu lililokoza rangi ya kijivu. Kuzingira
mshumaa wenyewe ni dado nyingi zilizotupwa na kurusharushwa kwenye
maeneo yote katika tangazo. Dado zenyewe zinadhihirisha sehemu za juu zenye
madoa mawili na matano na ubavuni, madoa mawili au matatu. Ishara
inayowakilisha jitihada za umoja wa wanaume katika mapambano dhidi ya
UKIMWI imeambatishwa kote katika tangazo hili. Kuhimili ishara hii ni picha
ndogo ya mchoro wa wanaume wawili walioshikana bega kwa bega na
kufuatana hatua kwa hatua kudhihirisha umoja katika juhudi za wanaume
kuushinda ugonjwa wa UKIMWI. Kuhitimisha viunzi vya tangazo hili ni wito
unaotoa arifa kwa wanaume kuhusu yanayotarajiwa:
NI JUKUMU LA WANAUME KUUSHINDA UKIMWI.
Wakala wa tangazo hili ni:
INTERNATIONAL AIDS CANDLEliGHT MEMORIAL.
SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KUPAMBANANA UKIMWI LA MNARA WA
MISHUMAA.
Tangazo hili linadhihirisha mwambatano na uhusiano kati ya picha na wakala
wa tangazo. Picha ya mshumaa unaowaka na kuangaza kote imehimiliwa na
wakala: SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KUPAMBANA NA UKIMWI LA MNARA
WA MISHUMAA. Wakala huu unalenga kwenye maana ya tangazo kwa
kushirikiana na ishara ya juhudi za wanaume katika mapambano dhidi ya
UKIMWI inayojengea na kuhimili maana msingi inayodhihirika katika kichwa
cha tangazo. Ishara hii ilionekana haifahamiwi na hadhira kubwa. Takribani
kuchangia maana. Hili ni dhihirisho kuwa utambuzi wa maana msmgi hutegemea uhusiano baina ya tajriba ya mpokezi na yale yaliyomo kwenye tangazo na inafaa yale yote yanayoshirlkishwa kwenye tangazo yaakisi tajriba na matarajio ya wapokezi.
Matangazo haya pia, yanadhihirisha kuwa maana msingi katika mabango ya matangazo ya UKIMWI, inaibuka kutokana na mjengeano wa viunzi tofauti katika kuibusha maana zinazoshamiri waziwazi. Yeyote ambaye angekumbana na matangazo hayo angeweza kuzitambua na kuzisoma bila shida yoyote. Maana hizi za kimsingi hazihimiliwi na utamaduni, imani au chukulizi awali mbalimbali ila hujidhihirisha wazi katika kazi za kisanaa (Barthes 1964). Sehemu inayofuata tutatathmini kila kipengele ili kuona jinsi kinavyochangia katika mshikamano wa maana msingi inayodhihirika katika tangazo.
2.2.0 Vichwa VIkuu
Ushahidi unaojitokeza katika data zetu ni kuwa kuna aina mbili ya matangazo:
• Matangazo yanayoshirikisha vichwa vikuu.
• Matangazo yasiyo na vichwa vikuu.
2.2.1 Matangazo Yanayoshirikisha Vichwa Vikuu
Vichwa vikuu vingi katika matangazo huwa ni vifupi. Huwa ni kauli za neno moja au sentensi fupi. Maneno katika vichwa hivi yamepambwa kwa fonti kubwa yakiazimia kutimiza malengo yafuatayo:
• Kufuatisha welekevu wa tangazo.
• Kuleta uangavu wa tangazo.
Aidha, vichwa hutoa ujumbe jumulifu wa yaliyomo katika tangazo kwa njia ya
iktisadi. Kichwa huweza kubainisha moja kwa moja kiini cha tangazo. Mfano
rnzuri ni tangazo hili la bango Na. 4.
Kichwa cha tangazo hili, kimeandikwa kwa hati zenye kuvuta nadhari ya
hadhira kwa mbali kutokana na jinsi kilivyokoza rangi ya majivu na kunakshiwa
vizuri huku kikizingirwa kwa rangi ya kahawia nyepesi:
CONDOM
KONDOMU
Kichwa hiki kimehimiliwa na picha iliyosawiri vibonzo vinne. Kibonzo kilicho
katikati mwa picha kimebeba na kusheni maana msingi inayoshadidiwa na
matini:
ASKARI WA WOTE: TUMIA VIZURI KILA WAKATI UKIFANYA MAPENZI.
Kibonzo hiki kimechorwa kikiwa tambo la jitu ambalo limetutumka misuli.
Hakijadhihirisha uana vizuri, hivi kwamba iliwachukua muda watafitiwa
kuamua kama kimewakilisha mwanamke ama mwanamume. Watafitiwa
asilimia 62 hawakufikia uamuzi mahsusi kama kibonzo chenyewe ni mwanamke
au ni mwanamume. Mushkili huu unajitokeza kwa vile uso unadhihirisha sura
za kiume, viatu pia ni vikubwa mno hivi kwamba vinaonekana kama vya kiume.
Machoni kimevalia miwani. Vazi kilichojivika linaonekana kama kanzu ya kike
lililopindwa kwa mkunjo unaoligeuza umbo na kulifanya kuonekana kama
kondomu. Hili ni dhihirisho wazi kuwa suala la matumizi ya kondomu linahusu
wote. Kimeshika fimbo mbili kubwa, kila mkono una fimbo. Kimetanua miguu
kama kinachopiga hatua kufikia kitu fulani. USQ una ishara ya tabasamu na
Vibonzo vingine vitatu vilivyosawiriwa vinaonekana kama vitoto
vikilinganishwa na pande la kibonzo kinachowakilisha askari. Kibonzo cha
kwanza kilichosawiriwa na tumbo kubwa kimepewa jina mahsusi la:
'Pregnancy'
Uja uzito
Mikono yote miwili inakuna kichwa, macho pima kimekondoa, na machozi
yanakitiririka. Uso unadhihirisha fadhaa na wahka mkubwa. Aidha, kimeduwaa
na hakina raha kamwe. Miguu vilevile imetanuliwa pasi kufahamu njia gani
inayofaa kufuatwa. Kimekolezwa rangi ya samawati.
Kibonzo cha pili kinachoonekana nyuma ya kibonzo cha askari kimepewa jina la
HIV- virusi vya UKIMWI. Kibonzo hiki ni kimbaumbau na hakiri zaidi
kikilinganishwa na kile cha askari. Miguu kimetagaza pia ishara ya makeke na
mbio za kasi zaidi. Kina rangi ya kahawia iliyoiva na kupakana na kijivu.
Kibonzo cha tatu, kimepewa jina la STIs - Sexually Transmitted
Infections-Magonjwa ya Zinaa. Vilevile kibonzo hOOkinakimbilia usalama na rangi yake ni
kijani hafifu. Tangazo hili limeambatishwa wito: Tumia oizuri kila wakati
unapofanya mapenzi. Wito huu unahitimisha yaliyoanzishwa na kichwa kikuu
cha tangazo hili.Wakala wa tangazo hili ni:
GOal International Humanitarian Organization.
Shirika la Mataifa la Ufadhili wa Binadamu, la al.
Ndani ya herufi 0 kuna picha ya ramani ya ulimwengu ishara wazi kuwa
uwiano kati ya viunzi mbalimbali vya tangazo hili tunapata uhusiano jenzi na
tegemezi. Aidha, wito unatilia mkazo mada kuu inayojitokeza katika kichwa cha
tangazo na kuhimiliwa vyema na picha.
Uwiano wa viunzi mbalimbali katika uimarishaji wa maana msmgi za
matangazo ya UKIMWI pia unajitokeza katika bango hili la Na. 5. Kichwa kikuu
katika tangazo hili kimeandikwa kwa hati kubwa:
TULlZA BOLI!
BANGONA.S
Kichwa chenyewe kinalenga moja kwa moja kwenye shabaha ya tangazo. Picha
iliyoambatishwa katika tangazo hili inaonyesha mchezaji nambari kumi (10)
mwenye rnzubao na wasiwasi kwa kufika kwenye ukingo wa uwanja. Inambidi
kuukanyanga mpira ghafla ili kuutuliza usitoke nje ya uwanja. Mkono mmoja
nyongani na mwingine unakuna kichwa. Anaonekana kutanzwa na kuvotana na
mawazo asijue la kufanya. Nyuma yake kuna nguzo za lango la goli. Goli lenyewe
linaonekana halina mlinzi. Katika kuimarisha maana msingi, ni matini
iliyoambatishwa:
UWANJA MDOGO: KAMDUDU KAKO, TUMIA CD.
Tell it straight! ...Sema wazi!...
Tangazo hili limekolezwa rangi ya nili inayojitokeza pia katika ramani ya Kenya
ambayo imeambatishwa kama picha ndogo ndani ya picha kubwa. Ramani hii
imezingirwa kwa duara. Katikati mwa ramani kuna duara lingine ndogo
lililoambatishwajina la wakala wa tangazo. Wakala wa tangazo ni:
Family Planning Association of Kenya
Shirika la Mpango wa Uzazi Nchini Kenya.
Viunzi tofauti vya tangazo hili vinadhihirisha uhusiano rejeleshi na sisitizi wa
maana msingi. Kichwa kikuu kinarejelea yaliyomo kwenye picha
yanayosisitizwa na kufafanuliwa na matini fupi iliyoambatishwa.
Muundo wa picha pia unajumuisha taipografia, vielelezo kama vile rangi,
ujalidi, aina ya karatasi, mfumo wa hati za maandishi na msuko wa vijisehemu
mbali mbali na jinsi vinavyofumana ili kufanikisha uwasilishaji wa maana kwa
mifumo ya kisemiotiki. Uratibu wa mifumo hii ya kisemiotiki ndiyo ambayo inaiwezesha na kuielekeza hadhira katika ufasiri wa maana na ujumbe.
Matangazo mengi katika mabango ya UKIMWI yametumia vichwa vikuu ili kutoa muhtasari wa yale yaliyomo kwenye picha hivi kwamba mpokezi asiye na muda wa kutathmini yaliyohusishwa kwenye matini fupifupi zilizoambatishwa chini au kando ya picha, ataweza kuelewa maana ya tangazo kwa kusoma kichwa tu cha tangazo. Aidha, matini fafanuzi zinazoambatishwa zinaandikwa kwa hati ndogo zisizoonekana kwa umbali. Vichwa vikuu vinawasilisha maana kwa njia yenye iktisadi lakini iliyo na uzito na uwezo wa kujumuisha hoja kuu za tangazo.
2.2.2 Matangazo Yasiyo na Vichwa Vikuu
matini fupifupi ambazo hazitoi ufafanuzi wowote kuhusu dhana
zinazowasilishwa.
Wapokezi wanaachiwa uhuru wa kuibua maana kutegemea UJUZl wao wa
mahusiano ya ishara za kisanaa. Matangazo ya aina hii katika data, ni yale
yanayohusisha maswala ya ngono na pia yale yanayohimiza matumizi ya mipira
ya kondomu katika kujikinga. Mfano mzuri ni tangazo katika bango la Na. 6a.
Tangazo hili limesawiri vijana wawili ambapo kuna mwanamume na
mwanamke wa umri wa kati. Kijana mwanamume amevalia kizibao cha rangi
nyeupe kilichopindwa kwa rangi nyeusi ambacho kimewacha sehemu ya kifua
wazi. Amevalia mkufu. Mdomo ameufumba na macho yake hayaonekani
kutokana na miwani aliyoivalia. Mikono yake imetanuliwa kama iliyoshika
sehemu za nyonga yake ishara ya kujithamini na mbwembwe za ujana. Kando
yake kuna miwani ambayo imeambatishwa picha ndogo ya pakiti ya Trust.
Msichana naye amevalia fulana ambayo nyororo yake imefunguliwa kiasi. Uso
wake hauna raha na midomo imekolezwa rangi ya kahawia iliyoiva na
ameufumbua kiasi. Kichwa chake kimeinamishwa. Mavazi yao na marembo
yanadhihirisha kuwa wao ni vijana wa kisasa, waliolelewa mjini. Nyuma yao
wawili kuna wavu usioonekana vizuri. Picha hii imeambatishwa matini:
Maisha iko sawa
na Trust.
Matini hii imeambatishwa matangazo mengi yanayohimiza matumizi ya mipira
ya kondomu kuzuia maenezi ya UKIMWI. Kile ambacho kinabadilishwa ni
picha pekee. Mfano mzuri wa mabadiliko tu ya picha unadhihirika katika bango
Tangazo hili limesawiri wanaume wawili na wanawake wawili wa umri wa
makamo. Mwanamume mmoja ameketi huku yuamvuta mwenzake kama
kwamba yuarnzuia asiurushe mpira. Mkono mmoja ameutumia kujihimili.
Amevalia shati jeusi na bushuti la rangi ya manjano. Raha inadhihiri usoni