FANI NA MAUDHUI KATIKA MASHAIRI YA MAGAZETI YA TAIFA LEO
NA
MOGENI MAGOMA ERICK C50/CE/22694/2010
TASNIFU ILIYOWASILISHWA KATIKA IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA KATIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA KWA MINAJILI YA
KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI
ii UNGAMO
Kazi hii ni yangu mwenyewe na haijawahi kutolewa katika Chuo Kikuu kingine kile.
Sahihi:________________________ Tarehe:________________________
Mogeni Magoma Erick
C50/CE/22694/2010
Tasnifu hii imewasilishwa kwa idhini yetu kama wasimamizi wa kazi hii wa Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Sahihi:____________________________ Tarehe:_________________________
Profesa Kitula King‟ei
(Idara ya Kiswahili na lugha za Kiafrika)
Sahihi:__________________________ Tarehe:_________________________
Daktari Edwin Masinde
iii TABARUKU
Kazi hii naitabarukia marehemu mamangu Bi. Paskalia Kerubo ambaye ndiye nguzo
iv SHUKURANI
Shukrani zangu za dhati kwanza nazitoa kwa Maulana kwa kunijalia afya wakati wote
nilipokuwa nikishughulikia kazi hii. Pili ningependa kutoa shukurani zangu za dhati kwa
waelekezi na wahadhiri wangu, Profesa Kitula Kinge‟i na Daktari Edwin Masinde kwa
uelekezi wao ambao ndio nguzo kuu katika matokeo ya kazi hii.
Mbali na wasimamizi, shukrani ziwaendee wahadhiri wote katika idara ya Kiswahili kwa
kunifundisha, kuielekeza na kunipa dira kamili katika safari hii ndefu na yenye
misukosuko. Nyote Mungu awabariki.
Pia nawashukuru ndugu zangu Risper, Dennis, Lilian, Videlis na Charles kwa kunipa
moyo na kwa maombi yenu. Shukrani zingine zimwendee Bi. Mildred kwa kuipiga chapa
kazi hii.
Vilevile namshukuru mke wangu Bi Everline Kemunto kwa kusimama nami kwa hali na
mali hasa kwa kuzidi kuniombea kwa kipindi chote nilipokuwa naishughulikia kazi hii.
Shukurani zangu pia ziwaendee watoto wangu Brian na Kerubo.
Aidha ningependa kuwashukuru wanafunzi wenzangu kama Kiange, Gladys, Joy,
Nyandoro, Onsarigo, Karani na wengine wote waliochangia kwa njia moja au nyingine
v IKISIRI
vi ABSTRACT
vii YALIYOMO
UNGAMO... ii
TABARUKU ... iii
SHUKURANI ... iv
IKISIRI ...v
ABSTRACT ... vi
YALIYOMO ... vii
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI ...1
1. 0 Usuli ...1
1. 1 Suala la utafiti ...2
1.2 Malengo ya utafiti ...3
1.3 Maswali ya utafiti ...3
1.4 Sababu za kuchagua mada ...4
1.5 Upeo na mipaka ya utafiti ...4
1.6 Yaliyoandikwa kuhusu mada ...5
1.8.0 Mbinu za utafiti ...13
1.8.1 Muundo wa utafiti ...13
1.8.2 Mahala pa utafiti ...14
1.8.3 Sampuli lengwa ...14
1.9.0 Ukusanyaji wa data ...14
1.9.1 Upangaji wa Data ...14
1.9.2 Uchanganuzi wa Data ...15
1.9.3 Uwasilishaji wa data ...15
1.9.4 Hitimisho...15
SURA YA PILI: FANI NA MAUDHUI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI ...16
2.0 Utangulizi ...16
2.1.0 Fani Katika Utunzi Na Uwasilishaji Wa Ushairi ...16
2.1.1 Taswira. ...22
2.1.2 Jazanda ...24
2.1.3 Chuku ...24
viii
2.1.5 Takriri ...26
2.1.6 Tashhisi ...27
2.1.7 Kuchanganya ndimi ...29
2.1.8 Inkisari ...29
2.1.9 Mazida...30
2.1.10 Tabdila ...31
2.1.11 Kuboronga Sarufi ...31
2.1.12 Methali ...34
2.1.13 Utohozi. ...34
2.1.14 Tashbihi...36
2.1.15 Tanakali za sauti /onomatopoeia ...36
2.1.16 Misimu ...37
2.1.17 Nidaa/Siyahi ...37
2.1.18 Nahau ...38
2.1.19 Isitiari. ...38
2.2.0 Maudhui Katika Ushairi Wa Kiswahili...39
2.2.1 Dhana ya Maudhui ...39
SURA YA TATU: UCHAMBUZI WA FANI NA MAUDHUI YA MASHAIRI YA MAGAZETI YA TAIFA LEO ...45
3.0 Utangulizi ...45
3.1 Uwasilishi wa fani na maudhui ya kijamii ...49
3.1.1 Shairi la Tupate Fahamu ...49
3.1.2 Shairi la Napinga utoaji mimba ...51
3.1.3 Shairi la Jongoo na Jogoo ...53
3.1.4 Shairi la Ni Nani Changudoa ...56
3.1.5 Shairi la Tafakari ewe msichana ...58
3.2. Uwasilishi wa Maudhui ya Kiuchumi...61
3.2.1 Shairi la Ukosefu wa Ajira ...61
3.2.2 Shairi la Nikawalisha ...63
3.2.3 Shairi la Nchi Iko Kilindini...66
ix
3.2.5 Shairi la Maskini Wateseka ...74
3.3 Uwasilishi wa Fani na Maudhui ya Kisiasa ...77
3.3.1 Shairi la Majimbo Yatufaa ...77
3.3.2 Shairi la Katiba Gani Itazaliwa. ...81
3.3.3 Shairi la Haki iko Hegi ...85
3.3.4 Shairi la Niwanauliza, Siasa ni Vita ...88
3.3.5 Shairi la Kura Tusiuze. ...94
SURA YA NNE: DHIMA YA GAZETI LA TAIFA LEO KATIKA KUENDELEZA UTANZU WA USHAIRI NCHINI KENYA ...101
4.0 Utangulizi ...101
4.1 Dhima ya gazeti la taifa leo katika maendeleo ya ushairi nchini Kenya ...103
4.2 Mchango katika fani ...103
4.2.1 Taswira ...103
4.2.2 Balagha / Mbalagha ...105
4.2.3 Tashbihi...105
4.2.4 Tashhisi / uhaishaji ...106
4.2.5 Takriri ...106
4.2.6 Inkisari na mazida ...107
4.3.0 Mchango kimaumbo ...108
4.4.0 Mchango kimaudhui ...108
4.4.1 Maudhui ya kijamii ...108
4.4.2 Maudhui ya kisiasa ...109
4.4.3 Maudhui ya kiuychumi ...109
4.4.4 Mchango wa umbuji wa wahusika ...110
4.5.0 Hitimisho...110
SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ...111
5.0 Utangulizi ...111
5.1 Hitimisho...113
5.2 Mapendekezo kwa utafiti zaidi ...116
MAREJELEO ...118
x
KIAMBATISHO B: NAPINGA UTOAJI MIMBA ...123
KIAMBATISHO C: JONGOO NA JOGOO ...124
KIAMBATISHO D: NI NANI CHANGUDOA? ...125
KIAMBATISHO E: TAFAKARI EWE MSICHANA ...126
KIAMBATISHO F: UKOSEFU WA AJIRA ...127
KIAMBATISHO G: NIKAWALISHA ...128
KIAMBATISHO H: NCHI IKO KILINDINI ...129
KIAMBATISHO I: SHEREHE AU TWAPORA...130
KIAMBATISHO J: MASIKINI WATESEKA ...131
KIAMBATISHO K: MAJIMBO YATUFAA ...132
KIAMBATISHO L: KATIBA GANI ITAZALIWA? ...133
KIAMBATISHO M: HAKI IKO HEGI ...134
KIAMBATISHO N: NIWANAULIZA, SIASA NI VITA? ...135
1
SURA YA KWANZA UTANGULIZI
1. 0 Usuli
Magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili yamekuwa yakiendeleza mashairi ya
Kiswahili kwa muda mrefu sasa. Waandishi, wachapishaji pamoja na wahariri huwa na
malengo maalum ambayo wanatarajia kuyatimiza.
Mashairi haya yanatarajiwa kuwa na hadhira pana katika jamii nchini Kenya hasa
ikizingatiwa kwamba gazeti la Taifa Leo ndilo tu ambalo huchapishwa kila siku katika
lugha ya Kiswahili. Pia, kutokana na ukweli kuwa somo la Kiswahili ni la lazima katika
shule za msingi na upili nchini Kenya bila shaka wengi wa wanafunzi na wakufunzi
hutarajiwa kulisoma gazeti hili.
Pia vyuo vyote vya ualimu hasa wa shule za kimsingi hufunza somo hili kama la lazima.
Aidha vyuo vikuu nchini Kenya hufunza somo la Kiswahili. Hivi leo nchini Kenya
kikatiba Kiswahili kimepewa hadhi ya lugha ya taifa na rasmi (Katiba ya Kenya, 2010).
Ulimwenguni Kiswahili kimekuwa lugha ya kimataifa. Hii ina maana kuwa vipengele
vyote vya lugha hii vinafaa kuendelezwa ili kukidhi mahitaji ya jamii nchini Kenya.
Katika mashairi haya maudhui mbalimbali hudhihirika. Ni dhahiri kuwa hamna fasihi
ambayo inaibuka katika ombwe tupu. Mashairi yana uhusiano na maisha katika jamii.
King‟ei, K. Na Kisovi, C. (2005) fasihi hutumia fani au ufundi fulani wa kimasimulizi ili
kuwasilisha maudhui fulani kuambatana na matakwa ya mwanafasihi. Maudhui ya fasihi
huchochewa na hali halisi katika jamii ya mwanafasihi na mazingira yake. Isisahaulike
2
kuelimishwa katika jamii yake na bila shaka, ameathiriwa sana kimawazo na maisha ya
jamii yake. Pale anapotunga kazi ya fasihi, mwanafasihi huweza kushughulikia maudhui
ambayo ni muhimu kutokana na hali halisi katika jamii anamoishi na anamojifunza.
Ingawa hivyo kuna haja ya kufanya utafiti wa kina ili kuonyesha ni maudhui yapi
yanaendelezwa katika mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili,
maudhui hayo huendelezwa vipi na ni ipi nafasi ya gazeti hilo katika maendeleo ya jamii
nchini Kenya. Miongoni mwa masuala ambayo hushughulikiwa na mashairi haya ni yale
ibuka kwa hivyo utafiti huu utayashughulikia yanayohusu siasa, jamii na uchumi.
1. 1 Suala la utafiti
Kuna tafiti nyingi ambazo zimetangulia utafiti huu na kugusia swala la fasihi na vyombo
vya habari. Kirichia (2012) amegusia usawiri wa wanasiasa kama wahusika katika
makala za habari kwenye gazeti la Taifa Leo Nchini Kenya yeye katika utafiti wake
alilenga kudhihirisha taswira mbalimbali za wanasiasa namna zinavyochorwa katika
gazeti la Taifa Leo. Ingawa utafiti huo unatumia gazeti la Taifa Leo kama wetu, wetu ni
tofauti kwa vile unaangazia fani na maudhui katika mashairi yanayowasilishwa katika
gazeti la Taifa Leo. Ushairi magazetini unadhihiri mabadiliko makubwa katika fani na
maudhui.Ingawa hivyo kuna haja ya kufanya utafiti ili kuonyesha maendeleo hayo.Kwa
hivyo utafiti huu utapata fursa ya kuonyesha fani na maudhui katika mashairi ya magazeti
ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili mwaka wa 2010-2012.
Utafiti huu ulidhamiria kuonyesha ni maudhui yapi yanavyoendelezwa katika ushairi
3
yanaendelezwa vipi na ni ipi dhima ya gazeti hili katika usawiri wa masuala nchini
Kenya.
Vilevile utafiti huu uliangazia ushairi magazetini kwa vile kuna baadhi ya mashairi
ambayo huchapishwa katika magazeti na hayapati fursa ya kuchapishwa vitabuni. Kupitia
utafiti huu jamii ilipata fursa ya kufahamu maswala nyeti ambayo hawangeyafahamu kwa
kutegemea vitabu vya ushairi pekee
magazeti ni njia muhimu ya kuwafahamisha wanajamii.Wale ambao hawawezi kupata
fursa ya kusoma mashairi vitabuni wanaweza kupata fursa kupitia kwa usomaji wa
magazeti. Hivyo, utafiti huu ulipata fursa ya kuonyesha ni maudhui yapi yanaendelezwa
katika ushairi unaochapishwa katika Magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili,
yanaendelezwa vipi na hatimaye kuonyesha dhima ya gazeti la Taifa Leo katika kusawiri
masualaibuka nchini Kenya.
1.2 Malengo ya utafiti
1. Kuchunguza fani na maudhui katika mashairi ya gazeti la Taifa Leo.
2. Kubainisha namna gazeti la Taifa Leo linavyosawiri maudhui hayo.
3. Kuonyesha dhima ya gazeti la Taifa Leo katika kusawiri masuala-ibuka nchini
Kenya.
1.3 Maswali ya utafiti
1. Je, ni maudhi gani yanashughulikiwa katika mashairi ya gazeti la Taifa Leo?
2. Maudhui hayo hushughulikiwa vipi?
4 1.4 Sababu za kuchagua mada
Sababu za kuchagua mada hii ni pamoja na ukweli kwamba gazeti la Taifa Leo ni la
kipekee la Kiswahili na kwa hivyo inatarajiwa kuwa inafikia hadhira pana na hivyo
hushughulikia maswala mbalimbali yanayoathiri jamii.Pia ushairi magazetini unadhihiri
mabadiliko katika fani na maudhui hasa ikizingatiwa kuwa jamii ya kisasa inakumbwa na
changamoto zinazotokana na matokeo ya mabadiliko katika sekta ya sayansi na
teknolojia.Kwa hivyo kuna haja ya kufanya utafiti ili kuonyesha mabadiliko katika fani
na maudhui yanayodhihirika katika utanzu huu wa ushairi magazetini na hatimaye
kuonyesha nafasi ya gazeti la Taifa Leo katika kuakisi mabadiliko hayo.
Dhima ya fasihi ni pamoja na kuonya, kuelimisha, kuhifadhi utamaduni, kuburudisha,
kuadilisha na kadhalika. Kwa hivyo kupitia kuonyesha masuala-ibuka haya dhima ya
fasihi itadhihirika. Utanzu huu wa ushairi umetengewa nafasi maalum katika gazeti hili
hivi kwamba huwa na ukurasa wake kila siku ya Jumamosi na Jumapili.
Ulimwengu wa sasa umekumbwa na mabadiliko mengi kwa sababu ya maendeleo
kiwakati, na hayo mabadiliko yamezua masuala mengi yakiwemo yale ibuka. Kwa
misingi hiyo tunataka kufanya utafiti ili kubainisha maswala ibuka hayo na kuonyesha
changamoto zake katika maendeleo ya jamii; na hivyo kuwawezesha watu kujua namna
ya kukabiliana na changamoto hizo. Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaonyesha umuhimu
wa mashairi haya. Utafiti huu utawanufaisha wanafunzi wote wa Kiswahili, walimu,
washirikadau katika vyombo vya habari na jamii kwa ujumla.
1.5 Upeo na mipaka ya utafiti
Magazeti ni mengi nchini Kenya kama vile „The Standard‟, „The Daily Nation‟, „The
5
Utafiti huu utashughulikia masualaibuka katika mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo
Jumamosi na Taifa Jumapili nchini Kenya mwaka 2010-2012. Sababu za kuyachagua
magazeti haya ni pamoja na kuwa yanaandikwa kwa Kiswahili na pia ni katika siku hizo
mbili katika juma ambapo mashairi huchapishwa. Sababu kuu ya kuchagua kipindi cha
mwaka wa 2010-2012 ni kuwa ni kipindi cha kisasa ambapo masuala mengi yakiwemo
yale ibuka hudhihirika
Utafiti huu umezingatia mashairi yaliyochapishwa katika Magazeti ya Taifa Leo
Jumamosi na Taifa Jumapili za mwaka 2010-2012.
Mtafiti atachagua magazeti ambayo yana maudhui ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Mtafiti angependa kushughulikia masualaibuka mengi kama vile yanayohusu sayansi na
teknolojia, mazingira, utandaridhi na kadhalika lakini kutokana na ukosefu wa muda hili
halitafanyika.
Mathalan ni dhahiri kuwa mashairi yanayochapishwa katika Magazeti ya Taifa Leo
Jumamosi na Taifa Jumapili hudhihiri mgogoro uliopo baina ya mashairi huru na yale
yanayozingatia arudhi. Lakini utafiti huu hautajishughulisha na mgogoro huu kwa vile
malengo yake ni tofauti.
1.6 Yaliyoandikwa kuhusu mada
Suala la fani na maudhui katika fasihi limeshughulikiwa na waandishi, wahakiki na pia
watafiti mbalimbali. Senkoro (1988) alitafitia maudhui na mtindo katika mashairi ya
watunzi mbalimbali huku akitumia nadharia ya umaksi kama dira yake. Yeye katika
utafiti wake alipata kuanganzia vipengele mbalimbali vya mtindo huku akionyesha jinsi
6
mtindo ni namna ambavyo msanii huipa kazi ya fasihi sura ya kifani na kimaudhui kwa
njia ambayo msanii asingeweza kuipa hata kama jambo linalozungumziwa na wasanii
hawa ni lile moja. Katika kiwango hiki utafiti huu una mshabaha mkubwa na wetu lakini
tofauti ni kuwa utafiti wetu ulijikita katika mashairi yaliyochapishwa katika gazeti la
Taifa Leo katika kipindi cha 2010-2015. Tofauti nyingine pia inajitokeza kupitia kwa
matumizi ya nadharia iliyotumiwa. Wakati utafiti wa Senkoro ulitumia nadharia ya
umaksi utafiti wetu ulitumia mihimili ya nadharia ya kimtindo ya kirasimi iliyoasisiwa
na Leech na Short (1981).
Vilevile Nyongesa (2015) naye alifanya utafiti kuhusu mtindo na dhamira katika mashairi
ya washairi chipukizi kutoka Bungoma. Kwa ambavyo utafiti huu ulizingatia mtindo
pamoja na dhamira kuna mshabaha unaodhihirika baina ya matokeo yake na yale ya
utafiti wetu. Ingawa hivyo utafiti huu wa Nyongesa ulipungukiwa katika upande wa
kudhihirisha vipawa vya chipukizi ambao hawapati fursa ya kuchapisha mashairi yao
katika diwani. Kuna chipukizi wengi ambao hupata kuchangia maendeleo ya ushairi
nchini kupitia utunzi wao wa mashairi ambayo yanapata fursa ya kuchapishwa katika
gaziti la Taifa Leo kwa hivyo utafiti huu ulipata fursa ya kujaza pengo hilo.
King‟ei, K. na Kisovi, C. (2010) wanaeleza kuwa sanaa ya kifasihi inatokana na usanifu,
ufasaha au ufundi wa kuwasilisha mawazo au fikra za mwanadamu. Nia hasa ya
kuwasilisha mawazo kama hayo ni kudhihirisha hali fulani za maisha yake kama vile
furaha, huzuni, matatizo, fanaka, utetesi, kashfa, sifa, maelekezo au uchambuzi.
Wanazidi kuelezea kuwa ufundi huu wa kisanaa huwasilishwa kwa maneno yaliyoteuliwa
7
kwa hivyo fasihi hutumia fani au ufundi fulani wa kimasimulizi ili kuwasilisha maudhui
fulani kuambatana na matakwa ya mwanafasihi.
Kulingana nao fasihi ni zao la jamii kwa kipindi fulani katika historia. Hii ina maana
kuwa maudhui ya fasihi huchochewa na hali halisi katika jamii ya mwanafasihi na
mazingara yake. Pia ikumbukwe kuwa msanii ni zao la jamii yake kwani yeye
amezaliwa, kukuzwa na kuelimishwa katika jamii yake. Bila shaka atakuwa ameathiriwa
sana kimawazo na maisha ya jamii yake. Pale anapotunga kazi ya fasihi mwanafasihi
huweza kushughulikia maudhui ambayo ni muhimu kutokana hali halisi katika jamii
anamoishi na anamojifunza.
Maudhui ya jamii hukuwa na kubadilika kulingana na hali ya maisha ya jamii
inayohusika. Mwisho tunakubaliana kwa dhati na waandishi hawa kuhusu majukumu
yanayotekelezwa na fasihi kama vile:
i. Kukuza, kueneza, kuboresha na kuhifadhi utamaduni.
ii. Kukuza, kueneza, kupanua na kuhifadhi lugha.
iii. Kuitumbuiza jamii
iv. Kuhifadhi historia ya jamii.
v. Kuwahamasisha wanajamii kujikomboa kisiasa na kitamaduni.
vi. Kusifia viongozi au asasi za kijamii zilizo bora.
8
Waandishi hawa wanadai kuwa fasihi inafungamana sana na mitindo ya maisha ya kila
siku na ni dhahiri kwamba maudhui yake yanagubika kila kipengele cha maisha ya
mwanadamu.
Mlacha (1995) akiandika kuhusu vyombo vya habari na usambazaji wa fasihi alieleza
kuwa vyombo vya habari vina uhusiano mkubwa sana na fasihi hasa kwa vile vyote hivi
vimetawaliwa na lugha ambayo hasa ndio njia muhimu ya mawasiliano baina ya
binadamu.
Kwa maneno mengine mtu anaweza kusema kuwa vyombo vya habari na fasihi ni
vyombo vinavyotumiwa na binadamu kwa mawasiliano ingawa kimoja (ambacho ni
vyombo vya habari) kinatumiwa pia kama chombo cha kuiwasilisha fasihi kwa
binadamu.
Kwa njia hiyo pia gazeti la Taifa Leo likiwa chombo mojawapo la vyombo vya habari
huchapisha mashairi ambamo lugha hutumika kwa njia ya kipekee ili kuwasiliana na
binadamu.
Mathalan mwandishi huyo anaeleza kuwa vyombo vya habari na fasihi kimuktadha na
kiutekelezaji vina dhima sawa ingawa vinatofautiana. Mantiki inayoweza kuvifanya
vyombo hivi viwili vifanane zaidi na au hata vilingane ni ile ya kuelimisha.
Kuhusu vyombo vya habari Mlacha anaeleza kuwa vina nafasi kubwa sana katika kukidhi
lengo la mawasiliano katika jamii. Aidha, hii ndio njia mojawapo ya kuwafanya
wanajamii waweze kuyafahamu matukio tofauti ya kila siku katika jamii yao, waifahamu
9
Kuhusu mawasiliano Mlacha (1995) anaeleza kuwa vyombo vya habari, vikiangaliwa
katika ujumla wake, vina majukumu mawili muhimu sana. La kwanza ni lile la
kuielimisha jamii kunakotokana na hayo mafanikio ya kuwasiliana ambayo nayo
yanatokana na binadamu kuelewana katika ishara zao. Hii ndiyo maana wataalamu kama
akina Parry J. (1967:29) wanasisitiza kuwa ni katika ndani ya mfumo mzima wa
mawasiliano ambamo kuelimisha kunajitokeza kuwa jambo linalotawala. Hii inatokana
na hali ya kuwa mfumo wa kuwasiliana umekitwa zaidi katika kueleweshana na
kuhakikisha kuwa kile ambacho hakifahamiki au hakijaeleweka vizuri kinafafanuliwa na
kufikishwa kwa watu wote wanaohusika na wanaostahili kukifahamu. Lengo kuu sio
katika kubadili tabia au maisha ya yule anayepokea ujumbe moja kwa moja, bali kumpa
taarifa aweze kutafakari ishara zake na kuelewa kutokana na tafsiri yake ya ishara hizo.
Wapo wataalamu ambao wameonyesha kuwa upo uhusiano baina ya fasihi na vyombo
vya habari. Upubor (1985:159) ameviona vyombo vya habari kama namna ya kuchangia
ujuzi na uzoefu ambapo idadi kubwa ya watu wanaweza kuhusishwa kwa wakati mmoja.
Fasili hii ya Upubor anadhihirisha kuwa upo uhusiano unaoweza kubainika baina ya
vyombo vya habari na fasihi.
Kwa upande mwingine wataalamu wengine kama vile Igbenedion (1985:115) wanadhani
kuwa vyombo vya habari vinaweza pia kuwa na athari mbaya kwa hadhira, bado ni
vyombo ambavyo, kama asemavyo konde (1984:239), vinaweza kuwa silaha ya kulinda
hadhi ya binadamu, hasa tunapozingatia kipengele cha kuelimisha jamii.
Kuhusu fasihi Mlacha (1995) anaeleza kuwa inaweza kuangaliwa pia kama chombo cha
10
kwa hakika fasihi hukusanya habari na matukio ya muda mrefu katika jamii ambayo
yamechukuliwa kama sehemu ya utamaduni wa jamii hiyo. Lengo kuu la fasihi ni lile la
kuielimisha na hata kuiburudisha jamii, kama vile lilivyo lengo kuu la vyombo vya habari
gazeti la Taifa Leo likiwa miongoni mwao.
Fasihi huelezwa kwa kutumia lugha na ishara kama vile ujumbe wowote ule
unaopitishwa kwenye vyombo vingine vya habari. Lakini zaidi ya hayo, ndicho chombo
kinachouwakilisha utamaduni wa jamii na hapo ndipo ulipo umuhimu wa kuisambaza
fasihi ili iwafikie na kueleweka kwa wanajamii wote. Yenyewe haiwezi kujisambaza bila
msaada wa vyombo vya habari vinavyojitokeza kama vyombo muhimu sana katika
usambazaji na ukuzaji wa fasihi.
Hapa nchini vyombo vya habari vimeipa fasihi nafasi kubwa sana na hivyo kuipanua
hadhira yake. Kwa mfano katika uchapishaji wa gazeti la Taifa Leo ambamo kurasa
maalum zimetengwa ili kuendeleza vipengele vya fasihi siku ya Jumamosi na Jumapili
kila juma. Hii inaonyesha kuwa, jamii ambayo ndiyo yenye vyombo hivyo vya habari,
imeona umuhimu wa kuisambaza fasihi na njia bora ilivyojitokeza ni kutumia vyombo
kama vile redio, magazeti, televisheni na hata video.
Ni muhimu kuzingatia aliyoyaelezea Wasberg (1988:21) alipotaka kuonyesha nafasi ya
vyombo vya habari katika kuikuza fasihi. Yeye ameeleza wazi kuwa waandishi wengine
wamelazimika kutumia vyombo vya habari kusambaza kazi zao hasa kwa vile
11 1.7 Misingi ya kinadharia
Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kimtindo ya kirasimi iliyoasisiwa na
Leech na Short mwaka wa (1981). Kulingana na nadharia hii mawazo ya mtunzi
huwa yameumbwa kitambo. Huwa yapo na ni juu ya mtunzi huyo kuyanasa kwa
njia bora itakayomwezesha katika kueleza matukio hayo kwa njia mwafaka. Kila
mtunzi hujitokeza na kunasa ujumbe kwa njia yake ya kipekee. Hii ina maana
kuwa iwapo mtunzi atanasa ujumbe kwa njia isiyofaa basi hivyo ndivyo
atakavyouwasilisha. Vilevile iwapo ataunasa kwa njia bora ndivyo
atakavyouwasilisha.
Nadharia hii inaeleza kwamba kazi ya fasihi haiwezi kueleweka bila lugha. Kwa
hivyo, jinsi mtu atumiavyo lugha husaidia kutoa ujumbe wake kwa wasomaji au
wasikilizaji. Hivyo, lugha huwa ndiyo chombo muhimu cha mawasiliano katika
jamii zote za wanadamu.
Chambilecho Leech: (1969:4).
Kazi ya fasihi haiwezi kueleweka vizuri bila ya
lugha ambayo hutumiwa kuieleza. Ni vyema
kuelewa uhusiano ulioko kati ya lugha ya ushairi
na ujumbe wa mwandishi. (Tafsiri yetu)
Nadharia hii inasisitiza uhusiano kati ya ujumbe na lugha. Kulingana na Leech
(ibid) kazi ya fasihi hukusudia kuwasilisha hisi au tajriba fulani kwa wasomaji
au wasikilizaji. Aeleza kuwa nadharia hii ina vigezo vinavyotumiwa kuchambua
12
Leech aeleza kuwa mshairi hutumia lugha "kiajabu" na a thari za uchumi
haziwezi kutenganishwa na matumizi ya lugha kisanaa.
Kuyatilia uzito maelezo haya Senkoro (1982) aeleza kwamba ushairi ni utanzu
wa fasihi unaotumia mpangilio wa lugha ya mkato, ya picha, na yenye mapigo
mahususi katika kutoa maudhui. Anarudi kueleza kuwa ushairi hutumia lugha ya
mkato yenye kueleza maudhui yake kimuhtasari, na mara nyingi huya ficha
maudhui hayo ndani ya taswira na ishara.
Ngara (1982) aeleza kwamba matumizi ya lugha katika kazi ya sanaa ni njia moja
ya kuvuta hisi na hadhira. Kwa hivyo tutachambua muundo wa lugha katika
kujenga na kutoa ujumbe wa mwandishi.
Leech, N. (1981:15) akimrejelea Aristotle na Plato anaeleza kuwa yaliyomo na
jinsi yaliyomo yanavyowasilishwa ni kama mwili na roho. Hii ina maana ya
kuwa maudhui na namna yanavyowasilishwa ni mambo mawili yanayotegemeana
na kuathiriana.
Aidha Leech (ibid) anaeleza kuwa katika matini tunaweza kuchunguza muundo
kwa kina ili kuona ni maneno/sauti zipi zinazopendelewa zikilinganishwa na
zingine. Hili limetuwezesha kupata maan a aliyokusudia mtunzi wa kazi ya sanaa.
Mhimili huu umetufaa katika utafiti wetu kwa vile tumeutumia katika kuchambua
na kuhoji sababu za baadhi ya watunzi wa mashairi kutumia takriri ya sauti au
maneno katika kazi zao.
Mhimili mwingine ni kuwa maudhui na mtindo katika kazi ya kirasimi ni mambo
13
uliokamilika kati ya kinachoelezwa na jinsi kinavyoelezwa (Wafula R. na Njogu
K. 2007). Mhimili huu umetufaa katika utafiti wetu kwa vile tum eutumia katika
kutathmini yaliyomo na jinsi yaliyomo yanavyowasilishwa. Kwa mfano katika
kuchambua yaliyomo tumeongozwa na mambo matatu ambayo n i mada, maudhui
na mielekeo. Pia katika kuchambua jinsi yaliyomo yanavyowasilishwa
tumeongozwa na mambo kama vile vipengele vya lugha ambavyo vimejumuisha
maelezo ya moja kwa moja, kejeli, na sadfa miongoni mwa vingine.
Pia tumezingatia mbinu za kisarufi kama vile, matumizi ya vina, mizani, takriri,
inkisari, mazida n.k. Aidha tumezingatia namna kila mtunzi anavyotu mia
tamathali za usemi kama vile: stiari, tashbihi, tashhisi, balagha na kisengere
nyuma miongoni mwa zingine. Mhimili mwingine katika nadharia hii ambao
umekuwa wa manufaa katika utafiti wetu ni ule ambapo mwanasanaa anayetunga
kazi ya kirasimi humezwa na mkondo wa fikra uliomzunguka. Mhimili huu
umetuwezesha katika kutambua maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo
ndiyo humwathiri kila mtunzi katika maisha yake ya kila siku.
1.8.0 Mbinu za utafiti 1.8.1 Muundo wa utafiti
Utafiti huu ni wa kimaelezo. Utafiti wa kimaelezo ni ule ambao hutegemea maelezo
katika uwasilishi na uchanganuzi wake. Utafiti huu utajikita katika maktaba. Mtafiti
amesoma magazeti ya Taifa Leo, makala, majarida, vitabu na tasnifu mbalimbali
14 1.8.2 Mahala pa utafiti
Utafiti huu umejikita maktabani na nyanjani sababu kazi hizi zinapatikana huko. Pili,
katika maktaba tumepata makala ya kusoma yanayoeleza misingi ya nadharia ya uhalisia
kwa uwazi na pia yaliyoandikwa kuhusu mada.
1.8.3 Sampuli lengwa
Sampuli lengwa katika utafiti huu, ni magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili
na kinacholengwa ni fani na maudhui. Kwa hivyo magazeti na masuala hayo
yameteuliwa kimakusudi. Uteuzi wa kimakusudi ni mbinu ya kutoa sampuli wakilishi
kutokana na idadi kubwa ya watu, au vitu ambavyo haviwezi kuchunguzika vyote kwa
pamoja. Mbinu hii humwezesha mtafiti kuchagua sampuli inayowakilisha kila aina ya
tabia inayopatikana kundini. Utafiti wetu umeazimia kuzingatia magazeti ya Taifa Leo
Jumamosi na Taifa Jumapili kuanzia mwaka wa 2010 hadi 2012. Kwa ambavyo gazeti
hizi ni nyingi hatungeweza kuzichunguza zote kutokana na ukosefu wa muda. Kwa hivyo
mbinu hii ya uteuzi kimaksudi itakuwa ya manufaa kwa vile ilituwezesha kuchagua na
kuchunguza tu yale mashairi ambayo yatakuwa na masuala ya kiuchumi, kijamii na
kisiasa.
1.9.0 Ukusanyaji wa data
Data itaainishwa kulingana na masualaibuka pamoja na malengo ya utafiti. Data
imekusanywa kupitia kusoma kwa kina na kuchagua masuala-ibuka ya kisiasa, kiuchumi
na kijamii. Mtafiti amesoma kwa kuzingatia namna masuala hayo yanavyoshughulikiwa.
1.9.1 Upangaji wa Data
Tumepanga data yetu kulingana na :
15
ii. Malengo yetu kwa mfano lengo la kwanza limetuwezesha kuona masuala-ibuka,
la pili limetuelekeza katika kuangalia namna masuala hayo yameshughulikiwa
ilhali lengo la tatu limetuwezesha kudhihirisha dhima ya gazeti la Taifa Leo
katika maendeleo ya jamii nchini Kenya.
1.9.2 Uchanganuzi wa Data
Tumechanganua data kwa kuzingatia: malengo, maswali ya utafiti na mihimili ya
nadharia ambayo imeongoza utafiti wetu.
1.9.3 Uwasilishaji wa data
Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kupitia kwa njia ya maelezo.
1.9.4 Hitimisho
Sura hii imeshughulikia mambo ya kimsingi kuhusiana na utafiti huu. Haya ni pamoja na
maelezo ya masuala muhimu kama vile: usuli, swala la utafiti, malengo ya utafiti na
maswali ya utafiti. Zaidi ya hayo, sababu za kuchagua mada na upeo wa utafiti ni
vipengele ambavyo vimeelezwa kwa kina. Pia, uhakiki wa yaliyoandikwa kuhusu mada,
misingi ya nadharia, mbinu za kukusanya; kuchanganua na kuwasilisha data
zimeshughulikiwa katika sehemu hii. Katika sura inayofuata tumechunguza fani na
16
SURA YA PILI
FANI NA MAUDHUI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI 2.0 Utangulizi
Katika sura hii tumechunguza fani na maudhui katika ushairi wa Kiswahili. Sura hii ni
muhimu kwa ambavyo ndiyo imetuwekea msingi thabiti wa kuegemea tunapochambua
fani na maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kama yanavyowasilishwa katika
mashairi yanayochapishwa katika magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili.
Kupitia sura hii mtafiti amepata fursa ya kufafanua maana ya fani na kueleza kwa kina
mbinu mbalimbali za fani pamoja na tamathali za usemi zinazotumiwa na wasanii katika
kazi zao. Aidha maelezo kabambe yametolewa kuhusu maudhui yanayoendelezwa katika
utanzu wa ushairi wa Kiswahili. Jambo hili pia ni muhimu kwa vile linajenga msingi
imara katika kutathmini maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kama
yanavyowasilishwa katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo.
2.1.0 Fani Katika Utunzi Na Uwasilishaji Wa Ushairi
Ushairi ni chombo mwafaka kinachowezesha mwandishi kuufumbata upana na urefu wa
maisha katika maneno teule machache yaliyofinyangwa kisanaa. Uteuzi huo wa maneno
hupangiliwa kama vito kwenye kazi ya sonara anayefua chombo cha dhahabu hukuza
heba ya mkufu huo kwenye jicho la mvaaji na mtazamaji. Mpangilio wa maneno mateule
katika ushairi hujenga picha na tashbihi inayojenga maana na mantiki inayochorwa na
mshairi, lakini heba yake imo katika kukamilisha hisi kwa msomaji au msikilizaji; kama
hisi za mapenzi au chuki, dhiki na faraja, ari au mapuuza, ujinga au werevu, sifa au
17
vilivyorejelewa hapo juu kama mtindo, mkufu kama maudhui na mvaaji na mtazamaji
kama hadhira. Kwa mujibu wa King‟ei na Amata (2001) ingawa ushairi ni pambo la
lugha na usanifu, mashairi hayawezi kuwa yenye mvuto na mnato iwapo hayatahusu hisi
na mambo yanayofahamika na wote wanaoishi katika jamii husika.
Sehemu kubwa ya sifa na msisimuo wa shairi ni kwa msikilizaji wake kuweza kulielewa
kimaudhui na pia katika kitengo cha lugha. Ushairi ni utanzu wa fasihi ambao
hutofautiana na riwaya na tamthilia hasa katika umbo na matumizi maalum ya lugha.
Wakati ambapo fasihi ya kinathari kama vile tamthilia na riwaya hutumia lugha ya mjazo
au mtiririko, ushairi hutumia zaidi lugha ya mkato kama nyenzo muhimu ya kuwasilisha
maudhui kitaswira, kimafumbo na kimuhtasari (Gibbe 1990 na Senkoro 1988). Hali hiyo
imetokana na hoja kwamba, mshairi huwa hana wakati mwingi wa kujieleza au kufafanua
zaidi maelezo na mifano iliyotolewa. Kadhalika ushairi wa Kiswahili una matumizi ya
upeo wa juu wa lugha hasa ukilinganishwa na aina zingine za fasihi andishi.
Kwa hivyo, kila kipengele cha lugha kilichoteuliwa na kutumiwa katika utungo huo,
hushikilia nafasi muhimu katika uwasilishaji wake. Kwa sababu utamu wa lugha haupo
tu katika maudhui au ujumbe bali pia katika ujumi wa lugha unaotokana na umbuji au
ustadi uliotumiwa katika uwasilishaji wa ujumbe (Kunemah 2008 na Khatib 1999).
Wataalam mbalimbali wanatumia msamiati tofauti tofauti katika kurejelea mtindo.
King‟ei (2005:40) anauita mbinu za usanifu. Nao Ndung‟o na Wafula (1993:44)
wameuita fani. Mogambi (2005:19) naye anauita mtindo. Ndung‟o na Wafula (1993)
wakimnukuu Senkoro (1982:8) wanasema kuwa:
18
Kutokana na maelezo haya tunaweza kusema kuwa huu ni ustadi au ubingwa ama mbinu
ambazo msanii wa kazi ya fasihi hutumia katika kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira
lengwa. King‟ei (2005) anasema kuwa mbinu za usanifu ni maarifa au ufundi wa kisanaa
kwa jumla anayoshirikisha mtunzi ili kufanya kazi yake ya kifasihi kuwa na mvuto kwa
msomaji wake.
Mogambi (2005) anasema kwamba mtindo ni ufundi wa kuwasilisha mawazo yaliyomo
katika kazi ya msanii. Ndung‟o na Wafula (1993:45) wakimnukuu Mulokozi na Kahigi
(1979:53) katika kuchangia mjadala huu wa maana ya fani wanasema:
Fani ni sanaa, ni jumla ya vipengele vya lugha vilivyowekwa katika mpangilio mahsusi ili kutoa kwetu maana fulani.
Wanaendelea kusema kuwa mtindo ni jumla ya vipengele vya lugha msanii hutumia
katika kutoa maana fulani kwa hadhira. Maelezo haya yana utata kwa vile yatubidi
kuelewa maana ya lugha na zaidi ya hayo vipengele vyake.
Wakiendelea, wananukuu Taasisi ya ukuzaji mitaala (1988:168) ambayo nayo imeeleza
kuwa:
Fani ni umbo lililofasiriwa ili kuelezea hisia za fanani.
Maelezo haya yanatuelekeza kwa dhana kuwa mtindo ni jinsi msanii anavyofinyanga
kazi yake ya sanaa ili kuelezea mawazo na hisia zake kwa lugha ya ufasaha. Kutokana na
maelezo ya wataalamu tuliorejelea tunaona kuwa mtindo ni ujumla wa vipengele vyote
vya fasihi ambavyo msanii hutumia katika juhudi zake za kuelezea mawazo, maoni au
19
Miundo na vipengele mahsusi vya lugha ambavyo hutumiwa katika ushairi sharti kuweza
kusaidia katika uwasilishaji wa ujumbe uliokusudiwa. Ujumbe unapomfikia msomaji
ndipo hueleweka kwa yakini kwamba, mtunzi ameweza kufanikiwa katika kuwasiliana
na hadhira yake (Maitaria 2012). Aidha, mshairi wa Kiswahili ambaye hupuuza uteuzi
mwafaka wa miundo ya lugha huenda shairi lake likawa chapwa, chakavu na la
kuchosha. Matokeo ni kwamba, shairi linalowasilishwa huenda lisiwe lenye kugusa hisia.
Hadhira isipopata kishawishi cha kuupenda ushairi kwa kuuga zilizotumiwa, ujumbe
kusudiwa hautakuwa umewasilishwa ipasavyo (Darvin na Wamuhu 1994 na Mulokozi na
Kahigi 1982).
Kulingana na nadharia ya Semiotiki ni kuwa, miundo mwafaka ya lugha ni ile husheheni
sitiari, ishara na tamathali za semi zinazochochea usaili na tafakuri ya hadhira. Kwa
hivyo ni muhimu hadhira kuweza kupata kichocheo cha kujiuliza maswali ya kiutafakuri
kila wakati inaposema kazi hiyo ya kisanaa. Katika utunzi, miundo mahususi ya kauli
zilizotumiwa huwa ni ile ambayo husaidia katika ufasiri wa ujumbe kwa kuzingatia
miktadha mbalimbali ipatikanayo ndani ya ushairi na ile iliyopo katika uhalisi wa maisha
ya jamii.
Kwa kutumia kauli mahsusi hususan methali, hadhira huweza kufunuliwa kwa ubanifu
ukweli wa maisha ambao huafiki miktadha ya uhalisi wa maisha na utamaduni wa jamii
(Wamitila 2008 na Lo Liyong 1972). Lugha ya Kiswahili kama zilivyo lugha zingine
ulimwenguni, ina ukwasi mkubwa wa semi kama vile; methali, nahau, misemo, misimu
na kadhalika. Semi zitumiwazo katika uwasilishaji, huufanya utungo kutajirika zaidi
kiuchambuzi (Mosha 2002 na Senkoro 1988). Kwa hivyo msomaji anapoichambua
20
Ifahamike kuwa mfano kwamba mshairi anapotumia semi kama vile methali kama
chombo chake cha utunzi na uwasilishaji isichukuliwe kuwa ni hali ya kubainisha tu
weledi au ukwasi wake wa lugha, bali pia ni msingi wa kufaulisha upokezi wa ujumbe
(Hawkes 1977, Oslen 1973 na Nowottny 1968).
Kutokana na matumizi ya semi, ushairi wa Kiswahili huweza kuwa ni utanzu wenye
dhima maalum ya kuelimisha, kutafakarisha, kuonya, kuliwaza, kuzindua na kuhifadhi
amali adimu za utamaduni wa jamii. Iwapo uhalisi wa maisha na utamaduni wa jamii
umeathirika au umebadilika kwa namna fulani, semi hizi pia hushabihi mabadiliko hayo.
Kwa mtazamo huo basi ushairi wa Kiswahili ni utanzu ulio hai. Kwa mantiki hiyo, kunga
au fani zitumikazo huweza kubadilika kutegemea mabadiliko yanavyojiri katika jamii.
Kwa hivyo, semi hutumiwa mno katika miktadha ya kitamaduni, kijamii na kihistoria.
Endapo pana mabadiliko ya kitamaduni na kijamii watunzi hutumia semi ambazo
huchukuana vyema ma miktadha ya mabadiliko hayo. (Jalala 2008 na Kitogo 2002).
Mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura
ambayo kimaudhui huainisha kanuni na kaida zilizofuatwa kama ni zilizopo (za
kimapokeo) au ni za kipekee. Kwa mujibu wa maelezo haya tunaweza kusema kuwa
mtindo ni upangaji wa maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hatimaye
hubainisha au kuonyesha nafsi na labda upekee wa mtunzi wa kazi hiyo. Kutokana na
mtindo wa kazi ya fasihi inakuwa vigumu kubadili sentensi au hata kidahizo katika kazi
hiyo bila kubadili mtindo wenyewe. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa mtindo ni ile
namna ambayo mtunzi huipa kazi yake ya kifasihi sura kimaudhui kwa njia ambayo
21
Kinachosisitizwa hapa ni kuwa hata kama watunzi wawili watashughulikia mada moja au
maudhui sawa ni sharti mitindo yao iwe tofauti. Mtindo ndio unaowawezesha
watazamaji, wasikilizaji na hata wasomaji kung‟amua mtunzi wa kazi bila kumwona au
kumtambulisha kwa jina.
Ndung‟o na Wafula (1993) wanasema kuwa pengine lugha ndicho kipengele muhimu
zaidi katika fani ya fasihi. Wanamnukuu Khatib (1981:16) anayedokeza kuhusu lugha
katika fasihi iwe simulizi au andishi:
Lazima iwe na utanashati na ulimbwende wa kipekee wenye mvuto na mnato na kuteka na kusisimua hisi za wasikilizaji, wasomaji au watazamaji.
Lugha ndiyo malighafi ya fasihi. Lugha inayotumika katika fasihi ni lugha ya kisanaa
inayopamba na inayokusudia kuibua hisia fulani kwa hadhira kulingana na jinsi
inavyotumiwa kwa lengo na kuchekesha, kukejeli, kusuta, kuchokoza, kutia hamasa au
kushawishi. King‟ei (2000: xii) anasema kuwa lugha ya kishairi ni ya mkato au
muhtasari. Mshairi hujaribu kuelezea fikira zake katika lugha iliyofinyangika, yenye
uchache wa maneno kama iwezekanavyo. Isitoshe, lugha ya ushairi ni lugha iliyo teule,
ni maneno yaliyochaguliwa kiufundi, kwa makini, ili kuleta athari, hisia na matokeo
maalum yaliyokusudiwa.
Tamathali za usemi za aina tofauti tofauti hutumika kujenga picha. Mifano ya tamathali
hizi ni kama; sitiari, tashhisi, takriri, misemo, methali, kejeli, ishara, tauria, simo,
ndimi-mseto, mbinu rejeshi/kisengere-nyuma, utohozi na kadhalika. Mbinu hizi tumezifafanua
22 2.1.1 Taswira.
Taswira ni mkusanyiko wa picha mbalimbali ambazo huundwa kwa njia ya maelezo na
wasanii katika kazi ya fasihi. Katika taswira twaweza kubainisha matumizi ya ishara
mbalimbali zinazowakilisha mawazo, dhana, vitu au watu (Ndung‟o na Wafula 1993:51).
Taswira huwa ni lugha ambayo inachora picha ya watu, vitu, wanyama au mahali kwa
kutumia ishara.
Katika taswira twaweza kubainisha maelezo ambayo jinsi yanavyopangwa na msanii
huweza kufanya hadhira zipate aina mbalimbali za hisi za kunusa, kusikia, kuona, kuonja
na kugusa.
Mbinu hii ya fani hutumiwa na washairi ili kunasa na kuteka hisia za hadhira zao.
Wasanii hutumia maneno ambayo huumba picha kamili ya mtu, kitu, hali, wazo, dhana
au uzoefu fulani wa jamii husika. Matumizi ya picha aghalabu huenda sambamba na yale
ya ishara. Tunatumia ishara hapa kwa maana ya dhana au mawazo mbalimbali
yanayotumiwa na wasanii katika kazi zao za fasihi kuwasilisha vitu, dhana au mawazo
mengine.
Matumizi mema ya taswira na ishara hutegemea ubingwa wa msanii wa kuchota mambo
mbalimbali katika mazingira ya jamii anayohusisha katika sanaa yake. Lengo kuu la
kutumia taswira ni kusisitiza maudhui yanayojadiliwa. Hiyo ina maana kuwa kufaulu au
kutofaulu kwa matumizi ya taswira kutatathminiwa kwa mizani ya jinsi taswira hizo
husaidia kuwasilisha au kuzuia maudhui yaliyokudiwa.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Jumapili 18-07-2010 kuna shairi lililo na anwani ya
23
mshororo wa tatu kuna taswira ya ukunguni kubishana kufanya ukata kutotoka. Taswira
ilidhamiriwa kumwezesha msomaji kupata kuelewa kwa undani namna uzembe
ulivyojongea na kufanya umaskini kupiga kambi kwa mtu anayependa kulaza damu.
Katika ubeti wa pili, mshororo wa pili kuna taswira ya hilako na aibu kumwandama
mzembe. Ubeti wa nne mshororo wa kwanza kuna taswira ya mtu aliye na bidii
anavyozidiwa na miliki na ile ya adui kutishwa na mafanikio ya mwenye bidii.
Katika ubeti wa mwisho mshororo wa tatu kuna taswira ya kuaga dhiki na kudidimisha
umaskini. Kwa jumla mtunzi Kimani Wa Mbogo amefanikiwa kuwasilisha maudhui yake
ya faida za bidii kupitia usawiri wa picha zinazoonyesha namna ambavyo mtu mkunguni
anavyoteseka maishani ilhali mwenye bidii anayafurahia maisha.
Aidha katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi tarehe Saba Mei, mwaka wa elfu mbili na
kumi na moja kuna shairi lenye kichwa “Ogopa pia ni Ngao” ambamo malenga Rono
Leonard amewachorea taswira mbalimbali. Katika ubeti wa kwanza mshororo wa nne
kuna taswira ya ogopa kuwa ngao ya kujiepusha na majanga. Mshairi alidhamiria
kuonyesha namna mwoga anavyojiepusha na matatizo mengi. Katika ubeti wa pili
mshororo wa tatu kuna taswira ya mapenzi kumkaba mtu na daima kuwa msiba. Hadhira
imewezeshwa kuona nguvu za mapenzi na athari zake. Katika ubeti wa tatu mshororo wa
kwanza kuna taswira ya mtu aliyejiingiza utandoni. Mtunzi alidhamiria kuonyesha namna
mtu anayejiingiza katika mapenzi ni sawa na aliyejiingiza mtegoni. Vilevile katika ubeti
huo mshororo wa tatu mshairi anasawiri picha ya mtu anayebeba mambo mazito kwa
24
Katika ubeti wa sita mshororo wa tatu mshairi anasawiri taswira ya nyoyo
zilizokirihishwa kutokana na kuchushwa kwa dawa. Malenga alitumia mbinu hii ili
kuwaelimisha hadhira dhidi ya ubaya wa dawa za kulevya.
2.1.2 Jazanda
Hii ni hali ya kulinganisha uhalisi na hali fulani kwa kutumia maelezo (King‟ei 2005:41).
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 23-10-2010 kuna shairi lililo na anwani
ya “Jongoo na Jogoo” ambamo mna matumizi ya jazanda. Malenga Hamisi Babusa
amelipa shairi lake anwani kwa kuzingatia mbinu ya jazanda. Katika shairi lake neno
jogoo ni jazanda. Neno hilo limetumika katika kuwarejelea watu wenye nguvu au walio
na ushawishi mkubwa. Vilevile katika shairi hilo neno jongoo limetumika kijazanda
kuwarejelea watu wanyonge.
Aidha katika shairi lenye anwani ya “Tafakari Ewe Msichana” lililochapishwa katika
gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 05-03-2011 mna matumizi ya jazanda. Katika ubeti wa
tatu mshororo wa pili, nyota yako ni muma, malenga Muge Kipkemboi ametumia mbinu
ya jazanda iliyo na maana ya mafanikio ya anayerejelewa katika elimu. Pia katika ubeti
huohuo kipande cha utao kuna kauli, inayo mwangaza bora iliyo na maana ya matokeo
mazuri.
2.1.3 Chuku
Ni matumizi ya lugha kutoa maelezo yaliyotiwa chumvi ili kuyafanya mambo yaonekane
ni ya ajabu kupita kiasi. Msanii anatumia chuku ili kuongeza ladha katika kazi yake. Vile
vile anaweza kutumia mbinu hii ya fani ili kuchekesha au kusisitiza. Lengo kuu huwa ni
25 2.1.4 Balagha
Ni matumizi ya maswali ambayo hayahitaji au hayana majibu. Lengo kuu la kutumia
balagha au mbalagha ni kuwazindua wasomaji ili wazingatie na kuyafikiria
yanayorejelewa. Maswali ya balagha hukusudia kuleta uchochezi akilini mwa msomaji
(Mogambi 2005:22).
Kwa mfano katika shairi la “Maskini Wateseka” lililochapishwa katika gazeti la Taifa
Leo Jumamosi, 07-05-2011 mshairi Edison Wanga ametumia mbinu ya balagha kwa
ufanisi mkubwa ili kuwachochea hadhira kutafakari kuhusu maudhui ya hali ya kiuchumi
nchini. Katika ubeti wa kwanza kuna mshororo wa pili, “bei mepanda ki shari, mafukara
tule nini”. Hapa mshairi alifanikiwa kuichochea hadhira kuona taswira halisi ya namna
maskini wanavyoteseka. Pia katika ubeti wa tatu mshororo wa tatu, “Lini itaja nafuu, tena
bila pingamizi”. Hapa mshairi amefanikiwa kuzua taharuki kwa hadhira ili kujaribu
kutofakari ni lini hali itabadilika na kuwa nzuri. Vile vile katika ubeti wa tano mshororo
wa kwanza, “Kodi za nyumba zapanda, fukara tulale wapi”. Hapa mshairi alikuwa na nia
ya kuonyesha malazi ambalo ni hitaji la kimsingi. Pia katika mshororo wa pili, “Wanalia
kina dada, wana wanywe maji yapi”. Mshairi anazidi kuchochea hadhira kutafakari kwa
undani mateso yanayokumba maskini. Pia katika mshororo wa tatu, “Zaingia zino shida,
serikali iko wapi”. Mtunzi amefanikiwa katika matumizi ya balagha ili kuonyesha namna
serikali inakosa kuwajibika raia waliowachagua.
Vilevile katika gazeti la Taifa Jumapili la 29-04- 2012 kuna shairi lenye anwani Mvua ni
heri au balaa? Ustadh Nuhu Zubeir Bakari amefanikisha ujumbe wake kupitia mbinu ya
balagha au mbalagha. Ametumia mbinu hii ili kuifanya hadhira kupiga darubini kuhusu
26
“Mvua ni heri au balaa?” Kupitia kwa mbinu hii ya balagha hadhira inapata kutafakari
kupitia kwa taharuki ni kwa vipi mvua ni heri au balaa. Vilevile mshairi ametumia mbinu
hii katika kuunda kibwagizo chake, “Mvua kuanza kunyesha, ni heri au balaa?” Mbinu
hii ni ya manufaa kwa vile imemwezesha mshairi kutilia uzito dhamira yake. Pia katika
ubeti wan ne mshororo wa tatu, “Sasa wapi pana heri, ni mvua ama ni jua?” Mshairi
amefanikiwa kuwatafakarisha hadhira na kutathmini ni wapi penye heri iwapo ni kwa
mvua ama kwa jua. Vile vile katika ubeti wa saba mshororo wa tatu, “Wako wapi
manyapara, wakenya tuna huzuni” Mshairi ameweza kuwafanya hadhira wake kupiga
darubini viongozi na kuonyesha naman wanavyokosa kuwajibikia raia na matokeo yake
ni kuwa raia wanazama katika mateso.
2.1.5 Takriri
Ni marudiorudio ya sauti, silabi, neno, sentensi, wazo au ridhimu; ili kuleta athari kwa
msomaji wa shairi linalohusika (Mbunda 1993:6). Marudio haya hufanywa ili kutilia
mkazo jambo ama wazo.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Jumapili, 05-06-2010 malenga Kimanga Bismark
amefanikisha ujumbe wake katika shairi lenye anwani ya “Tupate Fahamu” kupitia
matumizi ya mbinu ya takriri. Mshairi anafanikisha dhamira yake kupitia mbinu ya
takriri. Kila mshororo umeanza kwa maneno mwalimu funza. Takriri hii ililenga
kusisitiza dhamira ya shairi.
Pia, mfano mwingine u katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 13-02- 2010 ambamo mna
shairi lenye anwani “Ukosefu wa Ajira”. Ustadh Omar Bonge ametumia mbinu ya takriri
katika shairi hili ili kusisitiza dhamira yake kwa hadhira. Mifano ya matumizi ya mbinu
27
kazi hayawani” na katika ubeti wa pili mshororo wa kwanza,”Hayawani mso kazi, japo
awe sultani.” Katika mishororo hii miwili maneno mso kazi yamerudiwa. Pia katika ubeti
wa pili mshororo wa tatu, “Aamuru uvamizi, kuhatarisha amani” na katika ubeti wa tatu
mshororo wa kwanza, “Amani huhatarisha, watu wakiwa magadeni.” Katika mishororo
hii miwili maneno kuhatarisha amani yamekaririrwa. Vile vile katika ubeti wa tatu
mshororo wa tatu, “Mwishowe hujifundisha, kukaba watu gizani” na katika ubeti wa nne
mshororo wa kwanza, “Hukabwa gizani watu” katika mishororo hii miwili mbinu hii ya
takriri inabainika.
Katika ubeti wa nne mshororo wa tatu,”Haibadiliki katu, hali hii duniani” na katika ubeti
wa tano mshororo wa kwanza “Duniani hii hali, iko tele mitaani” katika mishororo hii
miwili maneno duniani hali hii yamekaririwa.
Katika ubeti wa tano mshororo wa tatu,”Ndipo huja wafadhili, kuwasajili vitani” na
katika ubeti wa sita mshororo wa kwanza,”Vitani kisajiliwa na kuingia kambini”. Katika
mishororo hii miwili maneno kuwasili vitani yamekaririwa.
Hatimaye malenga kupitia matumizi ya takriri amepata kusawiri kibwagizo
chake,”Ukosefu wa ajira, huchangia uhalifu” jambo linalomwezesha kufanikisha dhamira
yake kwa hadhira.
2.1.6 Tashhisi
Huu ni mtindo ambapo vitu ambavyo havina uhai au pia mawazo hupewa sifa au tabia za
binadamu. Mbinu hii hutumika kwa nia ya kuleta mawazo hayo na vitu hivyo karibu na
maisha ya binadamu kwani katika hali kama hiyo, msomaji atavielewa au atapata ujumbe
28
Kwa mfano katika shairi lenye kichwa “Jongoo na Jogoo” lililochapishwa katika gazeti la
Taifa Leo Jumamosi, 23-10-2010 mshairi Hamisi Babusa ametumia mbinu ya tashhisi
kwa nia ya kumwezesha hadhira kupata ujumbe wake kwa urahisi. Katika ubeti wa
kwanza mshororo wa kwanza, “Nasema nawe jongoo, ulojaa fondogoo”. Hapa neno
jongoo limepewa sifa za ubinadamu kwani ingawa hasemi katika muktadha huu ni kama
anashirikishwa katika mazungumzo kama binadamu.
Katika ubeti wa pili mshororo wa pili, “Acha wako uchokoo, hutamudu mtondoo” Hapa
mshairi anaonya jongoo kuacha uchokozi.
Katika ubeti wa tano mshororo wa kwanza, “Kwa jogoo udondoo, hatakuamba haloo”
Hapa bado mshairi anazidi kudhihirisha mbinu hii ya tashhisi anapowapa jogoo na
jongoo tabia za kusema kama binadamu. Katika ubeti wa mwisho mshororo wa pili,
“Jitizame kwa kioo, jione vyema jongoo” hapa jongoo anapewa sifa ya ubinadamu ya
kujitazama katika kioo.
Mfano mwingine u katika shairi lenye kichwa “Nikawalisha” lililochapishwa katika
gazeti la Taifa Jumapili, Julai 18, 2010. Malenga Kimani Wa Mbogo ametumia tashhisi
ili kumwezesha hadhira kupata taswira kamili ya maudhui ya uzembe na faida za bidii.
Kwa mfano katika ubeti wa kwanza mshororo wa tatu, “Ukata haukutoki, ukunguni
ukibisha” hapa neno ukunguni limepewa uwezo wa kubisha kama binadamu. Katika ubeti
wa nne mshororo wa pili, “Adui awe chuki, jasho langu kumtisha” hapa neno jasho
limepewa sifa za binadamu. Vilevile katika ubeti wa mwisho mshororo wa tatu, “Milele
29 2.1.7 Kuchanganya ndimi
Hali hii hutokea mzungumzaji au mwandishi anapotumia lugha mbili au zaidi
kuwasilisha maoni yake. Katika mashairi teule ya gazeti la Taifa Leo ingawa
yameandikwa katika lugha ya Kiswahili pana matumizi ya maneno kutoka lugha zingine.
Lengo kuu huwa ni kuonyesha kiwango cha elimu cha mtunzi au hadhira yake.
2.1.8 Inkisari
Hii ni mbinu ya kishairi ambapo mtunzi wa shairi anafupisha baadhi ya maneno. Lengo
kuu la matumizi ya inkisari ni ili kuafikia urari wa mizani katika shairi. Mbinu hii
hujitokezea aghalabu katika mashairi mengi.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 31-07-2010 mshairi Kevin Wamalwa
ameandika shairi lililo na kichwa “Nchi iko Kilindini” na katika shairi hili maneno
mbalimbali yamefupishwa kama vile:
(i) Kisikia badala ya ukisikia.
(ii)Miye badala ya mimi yeye.
(iii)Likuwa badala ya ilikuwa
(iv)Waso badala ya wasio
(v) Metupa badala ya wametupa
(vi)Litujia badala ya walitujia
(vii) Kajitia badala ya wakajitia
(viii) Nyusao badala ya nyuso zao
(ix)Sa‟ badala ya sasa
(x) Metuachia badala ya wamtuachia
30
Vilevile katika shairi la “Sherehe au Twapora?” Lililochapishwa katika gazeti la Taifa
Jumapili, 5-09-2010 malenga Wa Nyika Aggrey Juma ametumia vifupisho kama vile:
(i) Yalonichoma badala ya yaliyonichoma
(ii)Waloachwa badala ya walioachwa
(iii) Umbole badala ya umbo lake
(iv) Ndo badala ya ndio
2.1.9 Mazida
Hii ni mbinu ya kurefusha baadhi ya maneno kwa lengo la kupata urari wa mizani.
Vilevile sababu kubwa ya kurefusha huku ni kuwezesha kudhibiti uwiano wa mdundo
katika ushairi (Mazrui na Syambo 1992:37).
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, Julai 31, 2010 kuna shairi lenye anwani
“Nchi iko Kilindini” ambamo mshairi Wamalwa Kevin ametumia mbinu hii ya mazida ili
kuafikia urari wa mizani. Mifano ya mazida katika shairi hilo ni kama vile:
(i) Hawanayo badala ya hawana
(ii)Tukazamilie badala ya tukazame
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 31-07- 2010 kuna shairi la Nchi iko
Kilindini ambamo mshairi Wamalwa Kevin amedhihiri matumizi ya mbinu hii ya
mazida. Kwa mfano katika ubeti wa tatu mshororo wa tatu, “Ndio zinayo mambo,
mashimo kila mwahali” hapa neno mwahali limetumiwa badala ya mahali. Pia katika
ubeti wa tano mshororo wa kwanza, “Waja wala makombo, hawanayo hata hali”. Hapa
neno hawanayo limerefushwa. Vilevile katika ubeti wa sita mshororo wa tatu, “Sa‟
31 2.1.10 Tabdila
Ni mbinu ya kubadilisha mpangilio wa sauti katika neno. Lengo kuu la kutumia tabdila ni
ili msanii aweze kuafikia urari wa vina.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Jumapili, 29-04-2012 kuna shairi lenye anwani “Mvua
ni heri au balaa?” Mbinu hii inadhihirika. Maneno yaliyobadilishwa mpangilio ni kama
vile:
(i) Tuyapigilie badala ya tuyapige.
(ii)Wafile badala ya wafa
Pia katika shairi “Tupate Fahamu” lililochapishwa katika gazeti la Taifa Jumapili, 5-06-
2010 kunadhihirika matumizi ya mbinu ya tabdila kwa lengo la kupata urari wa vina.
Neno lililobadilishwa utaratibu wake ni karimu badala ya karima.
2.1.11 Kuboronga Sarufi
Ni mbinu ya kubadilisha miundo ya sentensi katika shairi. Wasanii hutumia mbinu hii ili
kulipa shairi ridhimu au keleta uwiano wa mpigo.
Kwa mfano katika shairi lenye anwani ya “Ogopa pia ni Ngao” lililochapishwa katika
gazeti la Taifa leo Jumamosi, 7-05- 2011 pana matumizi ya kuboronga sarufi kwa lengo
la kulipa shairi ridhimu.
Mifano.
(i) Ubeti wa kwanza mshororo wa kwanza, “Ninalo jambo moyoni, nikilificha ni
deni” badala ya moyoni ninalo jambo, ni deni nikilificha.
(ii)Ubeti wa kwanza mshororo wa pili “Napanga yangu mizani, nikujuze kwa yakini”
32
(iii)Ubeti wa pili mshororo wa tatu, “Mapenzi yakikukaba, daima kwako msiba”
badala ya mapenzi yakikukaba, msiba kwako daima .
(iv)Kibwagizo,”Ogopa ni ngao pia, hukuepusha majanga” badala ya ogopa pia ni
ngao, majanga hukuepusha.
(v) Ubeti wa tatu mshororo wa kwanza,”Kujitosa mahabani, mejitosa utandoni”
badala ya mahabani kujitosa, utandoni mejitosa.
(vi)Ubeti wa tatu mshororo wa pili, “Tasabilia kanuni, sirini na hadharani” badala ya
kanuni tasabilia, hadharani na sirini.
(vii) Ubeti wa tatu mshororo wa tatu,”Mazito yaso kifani, tayabeba kwa imani”
badala ya mazito yaso kifani kwa imani tayabeba.
(viii) Ubeti wa nne mshororo wa kwanza, “Naogopa kuwa jizi, kuiba katu
siwezi” badala ya naogopa kuwa jizi, katu siwezi kuiba.
(ix)Ubeti wa tano mshororo wa pili, “Kuitimiza ahadi, kwangu sawa na marudi”
badala ya ahadi kuitimiza, kwangu sawa na marudi.
(x) Ubeti wa sita mshororo wa pili, “Siogopi kukanusha, lolote linalochusha” badala
ya kukanusha siogopi, linalochusha lolote.
(xi)Ubeti wa saba mshororo wa pili, “Hikiki change kifurushi, napulizia marashi”
badala ya kifurushi hiki changu, marashi napulizia
Pia katika shairi la “Kuruhusu Ukahaba” lililochapishwa katika gazeti la Taifa Leo
Jumamosi, 11-02- 2012 malenga Nuhu Zubeir Bakari amesheheni matumizi ya
33 Mifano.
(i) Ubeti wa nne mshororo wa kwanza, “Tuyalinde maadili, ili tuhepuke dhambi”
badala ya maadili tuyalinde ili dhambi tuhepuke.
(ii)Ubeti wa nne mshororo wa tatu, “Amekataza Jalali, nakufahamisha „jombi‟
badala ya Jalali amekataza „jombi‟ nakufahamisha.
(iii)Ubeti wa tano mshororo wa kwanza, “Msitangulize pesa, dhidi ya utu na dhima”
badala ya pesa msitangulize dhidi ya utu na dhima.
(iv)Ubeti wa tano mshororo wa pili,”Wengine kuwanyanyasa, kwa tabia za kinyama”
badala ya kuwanyanyasa wengine, kwa tabia za kinyama.
(v) Ubeti wa sita mshororo wa pili, “Umeijosea njia, kufanya ubarakala” badala ya
njia umeikosea, ubarakala kufanya.
(vi)Ubeti wa sita mshororo wa tatu, “Itakumeza dunia, utupwe kwenye jalala” badala
ya dunia itakumeza, utupwe kwenye jalala.
(vii) Ubeti wa saba mshororo wa kwanza, “Tunajua „Koinange”, wanapoliwaza
moyo” badala ya „Koinange” tunajua, moyo wanapoliwaza.
(viii)Ubeti wa nane mshororo wa kwanza “Twajua mwatka kodi, kuwatoze
makahaba” badala ya kodi mwataka tajua makahaba kuwatoza.
(ix)Ubeti wa nane mshororo wa pili, “Lakini kwa “saa-Godi”, hamtaipata toba”
badala ya kwa “saa-Godi” lakini, toba hamtaipata.
(x) Ubeti wa tisa mshororo wa kwanza,”Nakomelea komeo, hapa nafunga kiriba”
34 2.1.12 Methali
Ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiriwa na jamii kuwa kweli na unaotumiwa
kufumbia au kupigia mfano na huwa umebeba maana pana kuliko maneno yenyewe
yanayotumiwa (TUKI, 2004). Methali katika ushairi wa Kiswahili hutumiwa kwa
malengo mbalimbali kama vile: kichepuo cha kufafanulia maelezo ya msingi, kulenga
mapigo ya ridhimu na udhibiti wa mwendo, chombo cha kufumbia fumbo, kuwezesha
hadhira kukumbuka kwa urahisi maudhui ama dhamira ya shairi, kudhibiti kaida za
kisarufi, kujenga taharuki, chombo cha kuwasilishia hisi na kubainisha itikadi ya mtunzi,
kuelekeza na kuiadilisha jamii na kadhalika.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa leo Jumamosi, 2-06- 2012 kuna shairi la “Pengine
CCTV” ambamo mshairi Faith Suzen katika ubeti wa tatu mshororo wa kwanza,
ametumia methali sio ndwele yalopita, tuyagange yausoni. Pia katika ubeti wa tano
mshororo wa kwanza, ametumia methali anyolewapo mwenzio, maji ukitie chako.
Aidha katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 9-07-2011 kuna shairi la “Waukwepaje
Ushuru” ambamo mshairi Salim Kalime Salim katika ubeti wa sita mshororo wa kwanza,
ametumia methali kwa binadamu mchungu, ni wa nguruwe mkuki. Pia katika ubeti wa
saba mshororo wa kwanza, ametumia methali haba na haba huleta, tukajikaza kibaba.
2.1.13 Utohozi.
Ni mbinu ya kuunda msamiati kutokana na msamiati wa lugha nyingine kwa kuzingatia
kanuni za kisarufi za lugha pongezi. Kwa mfano lugha ya Kiswahili imezua msamiati
mpya kutokana na maneno ya Kiingereza kama vile:
(i) Kompyuta kutokana na computer
35 (iii) Ofisi kutokana na office na kadhalika.
Lengo kuu la kutohoa maneno ni kuonyesha namna utanzu wa ushairi kama sanaa
unavyobadilika kiwakati na kuathiriwa na mifumo mipya katika jamii.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 11-02-2012 kuna shairi la “Kuruhusu
Ukahaba” ambamo Ustadh Nuhu Zubeir Bakari katika ubeti wa tatu mshororo wa tatu,
“Linapoanguka giza, waigawe „gudi-gudi‟. Hapa neno gudi-gudi limetoholewa kutokana
na lile la Kiingereza good-good. Pia katika ubeti wa nane mshororo wa pili,”Lakini kwa
„saa-Godi‟,hamtaipata toba” hapa neno Godi limetoholewa kutokana na lile la Kiingereza
God.
Aidha katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 18-08-2012 kuna shairi la “Wanjiku sasa
Nafurahi” ambamo mshairi Elvis Ondieki katika ubeti wa pili mshororo wa
pili,”Wanangu walo sikuli, watezaanza kushaini”. Hapa maneno sikuli na kushaini
yemetoholewa. Neno skuli limetoholewa kutokana na lile la Kiingereza school ilhali
kushaini limetoholewa kutokana na yale ya Kiingereza to shine. Pia katika ubeti huohuo
mshororo wa tatu, “Na upishi wa makuli,‟tarejesha sitovuni” hapa neno stovu
limetoholewa kutokana na lile la Kiingereza stove. Vilevile katiba ubeti wa tatu mshororo
wa kwanza, “Nimeipata sababu, kumugombeza kondakta” hapa neno kondakta
limetoholewa kutokana na lile la Kiingereza conductor. Pia, katika ubeti wa nne
mshororo wa kwanza,”Kesho nikienda pampu, nitazidisha madaha” hapa neno pampu
36 2.1.14 Tashbihi
Hii ni tamathali ya ufananisho au mlinganisho wa vitu viwili au zaidi. Ni mtindo wa
kifani ambao kwao kitu kimoja au zaidi hulinganishwa au hufananishwa. Tamathali hii
hutumika ili kuwezesha hadhira kupata kwa urahisi dhamira ya mtunzi.
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 11-06-2011 kuna shairi la “Mayatima
Tumekosani?” Ambamo mshairi Clare na Wanalela katika ubeti wa pili mshororo wa
pili,”Wanajamii wanatugemea, mfanowe ibilisi” hapa mtunzi aeleza kuwa wanajamii
wanalinganisha mayatima na shetani.
Vilevile katika gazeti la Taifa leo Jumamosi, 23-10- 2010 kuna shairi la “Jongoo na
Jogoo” ambamo malenga Hamisi babusa katika ubeti wa kwanza mshororo wa tatu,
“Wewe ni kama mnyoo ni dhaifu yako moo” hapa mshairi analinganisha jongoo na
mnyoo. Vilevile katika ubeti wan ne mshororo wa pili, “Akule ja poopoo, pamwe na
wako ukoo” hapa mshairi analinganisha jinsi jogoo anavyoweza kumla jongoo kama
poopoo.
2.1.15 Tanakali za sauti /onomatopoeia
Ni matumizi ya neno ambalo kwalo likitamkwa huelekea kutoa maana. Ni neno ambalo
kimsingi huiga sauti ya kitu (Msokile 1993: 38).
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 23-10-2010 kuna shairi lenye anwani
“Jongoo na Jogoo” ambamo mshairi Hamisi Babusa anadhihirisha matumizi ya taharuki.
Kwa mfano, katika ubeti wa pili mshororo wa tatu, “Ikikohoa kohoo, utabaki uko foo”.
37 2.1.16 Misimu
Ni maneno au misemo inayozuka ghafla katika jamii kufuatana na matukio maalum
katika jamii hiyo (Msokile 1993).
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 11-02-2012 kuna shairi lenye kichwa
“Kuruhusu Ukahaba” ambamo mna matumizi ya misimu. Kwa mfano katika ubeti wa
pili, “Uzinsi sio halali, hata ungepiga chambi” hapa neno chambi limetumika kwa maana
ya kukita mizizi au kukithiri. Pia, katika ubeti huohuo mshororo wa tatu, “Amekataza
Jalali, nakufahamisha „jombi‟”. Hapa neno jombi limetumika kwa maana ya adinasi.
Vilevile katika ubeti wa tano mshororo wa tatu, “Mnadunga mkinusa, kitawafika
kiyama”.hapa neno mnadunga ni la kimsimu lenye maana ya mnapachika.
2.1.17 Nidaa/Siyahi
Hii ina maana ya mwito fulani. Mwito wa sauti atoayo mtu kama ishara ya furaha,
masikitiko, chuki au hasira. Aidha huonyesha hali ya kushangaa au kukataa kitu (Kalome
na Maria 2001).
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Jumapili, 12-02-2012 katika shairi lenye anwani “Bei
kuumiza watu Maskini!” Mshairi Swaleh Suheil Abeid amedhihiri matumizi ya nidaa.
Kwa mfano katika anwani “Bei kuumiza watu maskini! mbinu hii inadhihirika. Pia katika
kibwagizo, “Twaumia maskini, bei za vitu kupanda!” pia nidaa inadhihirika vilevile
katika ubeti wa pili, msohororo wa tatu, “Tungaupika mchuzi, kitoweo kina zani!” Pia
kunadhihirika matumizi ya siyahi. Pia katika ubeti wa tatu, mshororo wa kwanza,
“Kukicha bei za vitu, zapandishwa madukani!” Hapa pia mbinu hii imetumika kuonyesha
38 2.1.18 Nahau
Ni msemo uliojengwa kwa kutumia maneno ya kawaida, aidha aghalabu, huwa umesitiri
maana tofauti na ile iliyobebwa na maneno ya nahau yenyewe (Msokile 1993).
Kwa mfano katika gazeti la Taifa Leo Jumamosi, 9-10-2011 kuna shairi lililo na anwani
“Waukwepa je Ushuru” ambamo mshairi Kalim Kasim amedhihiri matumizi ya nahau
kama vile katika ubeti wa kwanza mshoro wa kwanza, “Swala lanikereketa, moyo lanipa
udhia” hapa msemo swala lanikereta kwa maana ya suala linalonisumbua. Pia katika
ubeti huohuo mshororo wa tatu, “Ulimi sitaufyata, nanyi nawaulizia” hapa msemo ulimi
sitaufyata umetumika kwa maana ya kuwa sitaacha kusema. Pia katika ubeti wa pili
mshororo wa kwanza, “Ni jambo lilokuwepo, toka enzi za azali”. Hapa msemo enzi za
azali umetumika kwa maana ya wakati wa zamani. Katika ubeti huohuo mshororo wa
tatu, “Jambo hili likiwepo, tukaona ni aali.” Hapa msemo jambo la aali umetumika kwa
maana ya jambo bora. Pia katika ubeti wa nne mshororo wa kwanza, “Migongo
tunaipinda, mashambani tukifika” Hapa nahau migongo tunaipinda imetumika kwa
maana ya kujikaza kazini. Katika ubeti wa tano mshororo wa tatu,”Wakenya ndio ni taka,
waso na wakuwakimu”. Hapa msemo waso na kuwakimu umetumika kwa maana ya
kukosa wa kuwatimizia mahitaji yao. Vilevile katika ubeti wa sita mshororo wa pili,
“Wakenya twala machungu, wao na pesa lukuki”. Hapa msemo wakenya twala
machungu umetumika kwa maana ya wakenya kuteseka sana na pia pesa lukuki kwa
maana ya pesa nyingi. Hatimaye katika ubeti wa saba mshororo wa tatu, “Sa tujazeni
kibaba, sikatae katakata” hapa msemo sikatae katakata kwa maana ya kutokataa kamwe.
2.1.19 Isitiari.
Tamathali ya usemi ya aina hii hulinganisha vitu vya aina mbili au zaidi vyenye sifa