• No results found

Ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa shule za msingi

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa shule za msingi"

Copied!
134
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

UFASIRI WA NGANO ZA KIFANTASIA MIONGONI MWA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI

NA

DOROTHY AKINYI ODHIAMBO C50/22706/2011

TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI CHUO KIKUU CHA KENYATTA

(2)
(3)

iii TABARUKU Kwa wazazi wangu wapendwa,

Marehemu Baba Richard Odhiambo Ondula na Roseline M. Odhiambo.

Nawashukuru kwa kunihimiza na kunitia moyo niendelee na masomo.

Kwa mume wangu mpendwa James Kabaka Obonyo,

Mungu azidi kukubariki.

Kwa wanangu wapendwa, Elton Otieno, Annette Achieng’ na Nicole Faith.

(4)

iv SHUKRANI

Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema na kuniwezesha kukamilisha kazi hii. Shukrani zangu pia ziwaendee wasimamizi wangu Dkt. M. Osore na Dkt. P. Ngugi kwa kunielekeza. Mungu azidi kuwahifadhi na kuwabariki. Shukrani zingine pia ziwaendee wahadhiri wa Idara ya Kiswahili kwa kunifundisha katika masomo yangu ya uzamili.

Namshukuru sana mume wangu mpendwa James Kabaka na wanangu Elton, Annette na Nicole. Mlivumilia mengi nilipokuwa chuoni. Maombi yenu yalinitia moyo hasa nilipokaribia kukata tamaa. Mungu awe nanyi daima.

Pia, nawashukuru wanafunzi wenzangu: Nyandwaro Lena, Brenda Egara, Festo Haule, Kellen Muthoni, Cecilia Kihara, Joseph Kitheka, Charles Omutimba, Esther Chari, Elizabeth Mue, Hassan Makombo, Nimrod Mburia, Benson Sululu na Pamela Anyango. Kuwepo kwenu kulichangia katika ufanisi wa masomo yangu. Mungu awabariki sana.

(5)

v

IKISIRI

Utafiti huu ulinuia kuchunguza ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa darasa la tatu katika shule za msingi nchini Kenya. Lengo kuu lilikuwa kubainisha jinsi watoto wanavyofasiri maudhui, wahusika na mandhari yanayotokana na ngano teule za kifantasia. Vitabu vilivyosomwa na kufasiriwa ni: Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998) Paka na Panya (Nyakeri, 2006), Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) na Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006). Kazi hii iliongozwa na nadharia mbili ambazo zilichangiana katika kufanikisha madhumuni. Nadharia hizo ni Mwitikio wa Msomaji na Uhalisiajabu. Utafiti ulifanyika maktabani, mtandaoni na nyanjani. Utafiti huu ulifanywa katika manisapaa ya Homabay. Shule moja ya kibinafsi nay engine ya uma ziliteuliwa kwa kutumia mbinu bahatishi. Watoto walishirikishwa katika kusoma ngano teule katika vikao. Aidha, mtafiti aliandaa majadiliano na watoto huku wakijibu maswali walioulizwa. Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kulingana na madhumuni ya utafiti na mihimili ya nadharia. Data zote zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili, mtafiti ameandika muhtasari wa ngano zilizoteuliwa. Pia, ufasiri wa maudhui katika ngano hizi umeshughulikiwa. Katika sura ya tatu, ufasiri wa wahusika umejadiliwa. Sura ya nne imeshughulikia ufasiri wa mandhari yanayojitokeza katika ngano zilizosomwa. Sura ya mwisho ni muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Utafiti huu umechangia katika taaluma ya fasihi ya watoto. Washikadau watakaonufaika kutokana nayo ni kama wahakiki, wakufunzi vyuoni, wachapishaji, wazazi, waandishi na miongoni mwa wengine.

(6)

vi

ABSTRACT

This research examined how standard three primary school pupils interpret fantasy tales as a genre in children’s literature. It’s main objective was to find out children’s interpretation of themes, characters and settings of the four chosen books namely: Kuku na Mwewe (Mpesha 1998), Paka na Panya (Nyakeri, 2006), Safari ya Mbinguni

(7)

vii

ORODHA YA VIFUPISHO KIE- Taasisi ya Elimu Nchini Kenya

KICD- Taasisi ya Ukuzaji Mitaala Kenya

(8)

viii

MAELEZO YA ISTILAHI MUHIMU

Mtoto: Maoni ya Hunt (1994), ni kuwa mtoto ni binadamu ambaye hajakomaa kimwili na kiakili. Katika utafiti huu, mtoto anayerejelewa ni wa kati ya miaka 8 na 10. Pia, anatarajiwa kuwa katika darasa la tatu.

Ngano za kifantasia: Hadithi zinazoelezea matukio yaliyokiuka mantiki. Matendo na wahusika katika pia yamekiuka uhalisia.

Uhalisiajabu: Kazi za kifasii zinazoeleza matukio ambayo si ya uhalisia bali ya kifantasia. Matukio yakiajabu hutawala.

(9)

ix YALIYOMO

UNGAMO ... ii

TABARUKU ... ii

SHUKRANI ... iv

IKISIRI ... v

ABSTRACT... vi

ORODHA YA VIFUPISHO ... vii

MAELEZO YA ISTILAHI MUHIMU... viii

YALIYOMO ... ix

SURA YA KWANZA: UTANGULIZI ... 1

1.0 Utangulizi... 1

1.1 Usuli wa Mada ... 1

1.2 Swala la Utafiti ... 5

1.4 Malengo ya Utafiti ... 6

1.5 Sababu za Kuchagua Mada ... 6

1.6 Manufaa ya Utafiti ... 7

1.7 Upeo na Mipaka ya Utafiti... 7

1.7.1 Eneo la Utafiti ... 8

1.7.2 Vitabu Vilivyochambuliwa katika Utafiti... 9

1.8 Yaliyoandikwa kuhusu mada ... 9

1.9 Misingi ya Nadharia... 14

1.9.1 Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji ... 15

1.9.2 Mihimili ya Mwitikio wa Msomaji ... 16

1.9.3 Nadharia ya Uhalisiajabu ... 18

1.9.4 Mihimili ya Uhalisiajabu ... 19

1.10 Mbinu za Utafiti ... 20

1.10.1 Uteuzi wa Sampuli ... 20

1.10.2 Ukusanyaji wa Data ... 21

1.10.3 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Matokeo ... 21

(10)

x

SURA YA PILI : UFASIRI WA MAUDHUI KATIKA NGANO ZA

KIFANTASIA ... 23

2.0 Utangulizi... 23

2.1 Dhana ya Maudhui ... 23

2.1.1 Muhtasari wa Hadithi ya Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2007) ... 27

2.1.2 Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006) ... 28

2.1.2 Muhtasari wa Hadithi ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) ... 33

2.1.3 Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) 34 2.1.4 Muhtasari wa Hadithi ya Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998) ... 37

2.1.5. Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Kuku na Mwewe(Mpesha, 1998) ... 38

2.1.4 Muhtasari wa Hadithi ya Paka na Panya (Nyakeri, 2006). ... 43

2.1.5 Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Paka na Panya ( Nyakeri, 2006) ... 43

2.1.6. Hitimisho ... 47

SURA YA TATU: UFASIRI WA WAHUSIKA KATIKA NGANO ZA KIFANTASIA ... 49

3.0 Utangulizi... 49

3.1 Dhana ya Wahusika ... 50

3.2 Ufasiri wa Wahusika katika Ngano ya Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998) ... 52

3.2.1 Mama Mwewe ... 52

3.2.2 Mama Kuku ... 56

3.2.3 Wanawe Kuku... 59

3.3 Ufasiri wa Wahusika katika Ngano ya Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006). ... 62

3.3.1 Sungura ... 62

3.3.2 Fisi ... 66

3.4 Ufasiri wa Wahusika katika Ngano ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) .. 70

3.4.1 Tembo ... 70

3.4.2 Chozi ... 73

3.5 Ufasiri wa Wahusika katika Ngano ya Paka na Panya ( Nyakeri, 2006) ... 77

3.5.1 Paka ... 77

(11)

xi

3.6 Hitimisho ... 83

SURA YA NNE: UFASIRI WA MANDHARI KATIKA NGANO ZA KIFANTASIA ... 86

4.0 Utangulizi... 86

4.1 Dhana ya Mandhari ... 86

4.2 Ufasiri wa Mandhari katika Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006) ... 90

4.3 Ufasiri wa Mandhari katika Paka na Panya (Nyakeri, 2006) ... 94

4.4 Ufasiri wa Mandhari katika Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998) ... 97

4.5 Ufasiri wa Mandhari katika Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) ... 100

4.6 Hitimisho ... 102

SURA YA TANO: HITIMISHO ... 104

5.0 Utangulizi... 104

5.1 Muhtasari ... 104

5.2 Matokeo ya Utafiti ... 105

5.3 Changamoto katika Utafiti ... 110

5.4 Mapendekezo ya Utafiti wa Baadaye ... 111

MAREJELEO ... 112

VIMBATISHO ... 116

KIAMBATISHO A: Maswali ... 116

KIAMBATISHO B: Picha Zinazofafanua Mandhari ... 118

(12)

1

SURA YA KWANZA UTANGULIZI 1.0 Utangulizi

Sura hii inajadili usuli wa mada. Pia mtafiti ameshughulikia swala la utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada. Kuna maelezo kuhusu upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada na misingi ya nadharia. Mtafiti pia ameshughulikia mbinu za utafiti ambapo maeneo ya utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data, uchanganuzi na uwasilishaji wa data umejadiliwa.

1.1 Usuli wa Mada

Fasihi ya watoto ni kazi ya kifasihi iliyokusudiwa hadhira ya watoto (Davies, 1973). Kulingana na Hunt (1994), mtoto ni binadamu ambaye hajakomaa kiakili na kimwili. Tanzu za fasihi hii hujumuisha ngano, vitendawili, vitanzandimi, maigizo, mafumbo, mashairi na nyimbo. Ngano ni utanzu wa fasihi simulizi ijapokuwa siku hizi zimehifadhiwa katika maandishi. Godek (2005), anasema kuwa kuna ngano za kihalisia na za kifantasia. Ngano za kihalisia zinahusu matukio ya kawaida yanayoeleweka kwa urahisi. Matukio yaliyokiuka mantiki hayazingatiwi katika ngano za aina hii. Kwa upande mwingine, ngano za kifantasia hueleza matukio yasiyoweza kutendeka katika hali ya kawaida.

(13)

2

(2008), anaeleza kuwa katika fasihi za kifantasia, mazingaombwe yanachukua nafasi kubwa na hivyo kuchukua misingi ya kihalisiajabu.

Kulingana na Tunnel na Jacob (1997), kuna fantasia za kimapokeo na fantasia za kisasa. Fantasia za kimapokeo hazina waandishi wanaojulikana na zinatokana na tamaduni mbalimbali kote ulimwenguni. Zilipokezanwa kwa njia ya mdomo kwa karne nyingi kabla ya kutiwa katika maandishi. Fantasia za kisasa zimeibuka kutokana na fantasia za kimapokeo na zina waandishi wanaojulikana. Fantasia hizi zimepitia mabadiliko kulingana na mahitaji ya watoto wa kisasa na kipindi cha wakati.

Kuna vigezo muhimu vinavyotumiwa kutathmini ngano za kifantasia. Stewig (1980), anaeleza kuwa vigezo hivi ni wahusika wa namna ya kipekee kama wanyama, majitu na vifaa mbalimbali vilivyohaishwa, kuwepo kwa uganga au sihiri, wema dhidi ya uovu, nguli na mandhari ya kipekee. Tunnel na Jacob (1997), wanamuunga mkono kwa kusema kuwa vigezo hivi ni kuwepo kwa wahusika wasiokuwa wa kawaida, kuwepo kwa uchawi, shujaa, ulimwengu wa kufikirika na matukio yaliyokiuka sheria asilia ya wakati au muda. Wanasema kuwa si lazima vigezo vyote vijitokeze katika ngano moja. Kuwepo kwa kigezo hata kimoja katika ngano inaitosheleza kuitwa ya kifantasia.

(14)

3

Wataalamu wa fasihi ya watoto wameeleza umuhimu wa ngano za kifantasia katika malezi ya watoto. Kwa mfano, Cass (1967), anasema kuwa ngano hizi huwasaidia watoto kuelewa mazingira yao. Wao hufurahia hadithi zinazohusu wahusika wanyama. Wanafikiri kuwa wanyama au hata magari huwa na hisia za kibinadamu. Ni jambo la kawaida kwa mtoto kusikia katika ngano kwamba wanyama fulani wanaongea, wanaenda kazini, wanavaa nguo na hata kusoma. Jambo hili huzua fikra na mawazo katika nafsi ya mtoto.

Ijapokuwa Montessori (1949), anapinga kuwa watoto hawapaswi kusomewa ngano za kifantasia bali za kihalisia, kulingana na Tucker (1981), ngano hizi humwezesha mtoto kuelewa matukio mengi katika mazingira yake kuliko maelezo yoyote ya kisayansi. Maoni ya Bettelheim (1975), ni kwamba ngano hizi humsaidia mtoto kujibu maswali mengi yanayomzonga kuhusu ulimwengu wake mpya na humtayarisha kukumbana na ukatili wa ulimwengu kwani huo ndio ukweli wa maisha. Maudhui ya kutisha na kuogofya katika ngano humtayarisha kihisia kuelewa dhana za kifo, ugonjwa, upweke na maovu yanayopatikana katika maisha.

Ngano kadhaa za kifantasia zimeteuliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala Kenya (K.I.C.D) ili kutumiwa kufunza fasihi katika shule za msingi. Kupitia kwa ngano hizi, stadi za kusoma na kusikiliza huimarishwa. Stadi ya kusoma ni muhimu kwani humtayarisha mwanafunzi kuelewa na kufasiri yale anayoyasoma. Stadi hii inahusishwa na kusoma kwa sauti na kusoma kimya kimya (K.I.E, 2002).

(15)

4

(1989) anaendelea kueleza kuwa mwanasaikolojia Piaget, ameainisha viwango vinne vikuu katika ukuaji wa bongo za watoto. Mtoto aliye chini ya miaka miwili ana uwezo wa kusogeza viungo vyake vya mwili na pia kuwa na kielelezo cha kifaa akilini licha ya kuwa hakiko karibu naye. Watoto kati ya miaka 2 na 7 nao hujali sana maslahi yao zaidi ya watu wengine. Utafiti huu unawarejelea watoto wa kiwango cha tatu walio na kati ya miaka 7 na 11. Akimnukuu mwanasaikolojia Piaget, Bee (1989) anaendelea kueleza kuwa watoto hawa wana uwezo wa kufikiria kwa kina na huelewa bayana mazingira yao.Wenzao wa kiwango cha nne yaani walio na miaka 12 na zaidi wamepevuka zaidi yao na hufasiri mambo kwa undani. Ikiwa ngano za kifantasia hueleza kuhusu matukio yaliyokiuka uhalisia na yasiyo na mantiki, pana haja basi ya kuchunguza ikiwa watoto wa darasa la tatu wanazifasiri ipasavyo.

Cass (1967:36) anasema yafuatayo kuhusu ufasiri wa ngano za kifantasia:

Fantasia nyingi za kisasa zinaweza kufasiriwa kwa njia kadha kwani zimesheheni ukweli uliofichika, istiari na mawazo ya kifalsafa. Haya yamejikita kwenye maajabu, sihiri, na maudhui yake asilia.

(16)

5 1.2 Swala la Utafiti

Mtindo wa kifantasia huondoa vitu kutoka hali ya kawaida hadi hali ya kiuhalisiajabu. Baadhi ya vitabu vinavyosomwa na watoto wa darasa la tatu ni vile visivyoeleza uhalisia moja kwa moja bali kwa njia fiche. Mifano ya vitabu hivi ni kama; Mpesha, N. (2005) Mende Mdogo na Mpesha, N. (1997) Nyani Mdogo. Wahusika, mandhari na maudhui yanayolengwa yanatolewa kwa njia ya kifalsafa na sharti yafichuliwe ili yabainike.

Utafiti huu umechunguza ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa shule za msingi. Aidha umechunguza jinsi maudhui katika ngano za kifantasia yanavyofasiriwa na watoto. Pia, ufasiri wa wahusika na mandhari umechunguzwa ili kubainisha ikiwa watoto wanaelewa ujumbe na maadili yanayotokana na ngano teule za kifantasia.

Ili kubainisha ikiwa watoto wana uwezo wa kufasiri ngano za kifantasia, hadithi teule zilisomwa katika kikao. Baada ya kusoma, watoto waliulizwa maswali kisha majibu yao kuchanganuliwa. Maoni ya watoto yalipangwa kulingana na wanavyofasiri maudhui, wahusika na mandhari katika ngano za kifantasia.

1.3 Maswali ya Utafiti

Utafiti huu unajibu maswali yafuatayo:

i. Je, watoto wanafasirije maudhui yanayojitokeza katika ngano za kifantasia? ii. Wahusika wa ngano za kifantasia wanafasiriwaje na watoto?

(17)

6 1.4 Malengo ya Utafiti

Malengo ya utafiti huu ni:

i. Kuchunguza jinsi watoto wanavyofasiri maudhui yanayojitokeza katika ngano za kifantasia.

ii. Kubainisha jinsi wahusika wanavyofasiriwa na watoto katika ngano za kifantasia.

iii. Kuchunguza jinsi watoto wanavyofasiri mandhari yanayopatikana katika ngano za kifantasia.

1.5 Sababu za Kuchagua Mada

Kiswahili ni somo la lazima nchini. Fasihi inafunzwa kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu. Mtaala wa elimu ya shule za msingi nchini (KIE, 2002) unasisitiza stadi za kusoma na kuandika. Wanafunzi wanapaswa kusoma na kufahamu taarifa, hadithi na mashairi mbalimbali na kisha kuyafasiri ili waweze kunufaika kutokana na maadili yanayojitokeza.Wao hupewa fursa ya kujibu maswali au kujadiliana na walimu wao ili kubainisha haya. Kulingana na Mtaala wa Elimu nchini (KIE, 2002) kuwepo kwa maadili mema miongoni mwa wanafunzi ni lengo la nne la elimu nchini. Utafiti huu ni mchango katika kufanikisha malengo ya elimu nchini.

(18)

7

watoto kama vile mafumbo, mashairi, nyimbo na vitanza ndimi. Utafiti huu basi utachangia katika kuimarisha fasihi ya watoto na hasa Kiswahili kama somo la lazima.

Aidha, fasihi kama somo la lazima ina tanzu mbalimbali. Tanzu za fasihi huweza kuwa na maana ya ndani au ya wazi. Huck na wengineo (2001), wanasema kuwa ngano za kifantasia huwa na maana ya ndani na hurejelea jamii kijazanda. Matokeo ya utafiti huu yataonyesha ikiwa watoto wananufaika kutokana na ngano za kifantasia kwa kuzifasiri inavyokusudiwa. Fasihi ya watoto ni muhimu katika malezi yao na ni muhimu ifasiriwe vilivyo na watoto wenyewe ili wanufaike kutokana nayo.

1.6 Manufaa ya Utafiti

Utafiti huu utawanufaisha washika dau mbalimbali wa maswala ya watoto kama wakufunzi vyuoni, waandishi wa vitabu, wachapishaji, wapangaji wa sera za elimu ya watoto, wazalishaji wa fasihi katika vyombo vya habari, wahakiki, wazazi na makanisa. Kupitia kwa matokeo ya utafiti huu, washikadau wanaweza kuendelea kuimarisha uwanja huu wa fasihi ya watoto kwa kufanya utafiti zaidi ama kuandika ngano zaidi.

1.7 Upeo na Mipaka ya Utafiti

Fasihi ya watoto ina tanzu nyingi ambazo pia zina vipera mbalimbali. Utanzu wa ngano una ngano za kihalisia na ngano za kifantasia. Utafiti wa awali ulidhihirisha kuwa wanafunzi wengi wa shule za msingi wanazifurahia ngano hizi.

(19)

8

cha juu cha shule ya msingi. Baada ya darasa la nane kiwango kinachofuata ni shule ya upili.

Utafiti huu umechunguza jinsi watoto wa shule za msingi wanavyofasiri maudhui, wahusika na mandhari katika ngano za kifantasia. Watoto wa darasa la tatu katika Manispaa ya Homa-Bay wameshirikishwa katika utafiti huu. Darasa la tatu lilichaguliwa kimaksudi kwa sababu ni muhimu kuchunguza ikiwa watoto hawa wadogo wamazielewa ngano hizi. Silabasi ya shule ya msingi nchini inasisitiza mafunzo ya fasihi kuanzia viwango vya chini vya elimu. Ngano za kifantasia zimejumuishwa katika masomo ili kukuza stadi mbalimbali kama kusoma na kusikiliza. Watoto wa kiwango hiki pia wanaweza kusoma ngano walizoandikiwa na maoni yao ni muhimu ili kubainisha ikiwa wananufaika kutokana nazo.

1.7.1 Eneo la Utafiti

(20)

9 1.7.2 Vitabu Vilivyochambuliwa katika Utafiti

Baada ya kupitia vitabu kadhaa, vifuatavyo viliteuliwa kwani vilikuwa na data ambazo zingesaidia katika kufanikisha malengo ya utafiti huu kwa wanafunzi wa kiwango hiki. Vitabu hivi ni: Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998), Paka na Panya (Nyakeri, 2006), Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) na Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006). Vitabu hivi ni miongoni mwa vile vilivyopendekezwa na kupitishwa na Taasisi ya Elimu Kenya (KIE, 2012) kwa wanafunzi wa darasa la tatu. Viliteuliwa kimakusudi kwani vilirejelea watoto wa darasa la tatu na ni vya kifantasia.

1.8 Yaliyoandikwa kuhusu mada

(21)

10

Tucker (1981), anaeleza kwamba umri wa miaka saba ndio unaofaa zaidi kwa watoto kuanza kusimuliwa ngano za kifantasia. Anatoa mfano wa utafiti wa Arnold Gesell uliofanyiwa watoto wa Marekani. Utafiti wa Gessel unaonyesha kuwa katika umri huu, bongo za watoto zinazidi kuimarika kiasi cha kuweza kumudu ngano ndefu kiasi. Watoto huhitaji ngano zinazojibu maswali yanayotokana na matukio ya kihalisia yanayopatikana katika mazingira yao. Majibu yanapopatikana kutoka kwa ngano, humridhisha mtoto kuliko maelezo yoyote ya kisayansi. Haya yanaonyesha kuwa ngano za kifantasia huchangia katika kukua kwa mtoto.

Vilevile, Tucker (1981) anasema kuwa ufasiri wa ngano hizi hutegemea hali ya kisaikolojia ya msomaji. Fasiri huweza kutofautiana ama kulingana baina ya wasomaji wawili tofauti kutegemea tajriba zao maishani. Utafiti wa Gessel ni muhimu kwani unachangia kwa upande wa umri unaofaa kwa watoto kuanza kusimuliwa ngano za kifantasia. Utafiti huu utahusisha watoto wa darasa la tatu ambao wana umri wa kati ya miaka minane na kumi.

(22)

11

Kwa mujibu wa Stewig (1980), ngano za kifantasia huonyesha uhalisia kwa njia ya kinyume. Japo matukio yake yamekiuka mantiki, yanapaswa kufasiriwa ipasavyo ili kuweza kuelewa ulimwengu wa kihalisia. Pia anasema kuwa ngano hizi ni muhimu sana katika malezi ya mtoto. Utafiti wake unaonyesha kuwa watoto waliosoma ngano hizi kwa wingi walikuwa na uwezo wa kuthibiti hasira walipokosewa. Watoto waliokosa kuzisoma ngano hizi walishindwa kuthibiti hasira na walipokosewa walikasirika kwa muda mrefu. Maoni ya Stewig ni muhimu kwa utafiti huu kwa kusisitiza umuhimu wa ufasiri wa ngano na mchango wake katika malezi ya mtoto. Hata hivyo, utafiti wake ulifanyiwa watoto wazungu. Utafiti huu nao umefanyiwa watoto wa Kiafrika huku ngano za kifantasia za Kiswahili zikirejelewa.

Matokeo ya utafiti wa Kamera (1983), ni kuwa, watoto wa shule za msingi wako katika umri unaotawaliwa na ari na hamasa za visa vya kupiga chuku. Ngano za kifantasia huwafurahisha kuliko ngano za kihalisia. Kamera (1983), anaendelea kusema kuwa katika usimulizi mzuri, watoto huona jinsi lugha, wahusika na maudhui yalivyojitokeza na mazoea haya hukuza ubunifu miongoni mwao. Vilevile watoto hawapendi tu kusikiliza ngano bali pia wanafurahia wanapopewa fursa ya kusimulia. Jambo hili huleta ushupavu na kuondoa hali ya unyonge unaowakumba wanapokabiliwa na jukumu la kujieleza hadharani. Katika utafiti huu, watoto watapewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maudhui, wahusika na mandhari.

(23)

12

wahusika na matukio ya kiajabu katika mandhari tofauti tofauti. Jambo hili huwapa watoto hamu ya kutaka kujua mengi na pia huzua fikra nyingi katika bongo zao. Maoni yake yana mchango katika utafiti huu kwani mawazo yanayoibuka katika fikra za watoto baada ya kusoma ngano huwapa fursa ya kutafakari kuhusu maudhui au maadili yanayotokana nazo, jambo litakalojitokeza katika utafiti huu.

Upokezi wa watoto katika tanzu mbalimbali za fasihi ya watoto nchini Tanzania umeshughulikiwa na Mpesha (1995). Ametumia nadharia ya mwitikio wa msomaji. Mpesha (1995), alikusanya data yake katika maktaba mbalimbali nchini Tanzania. Pia alitumia mahojiano na hojaji zilizojibiwa na watoto wa kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Matokeo yake ni kwamba watoto wanaweza kutoa maoni yao kuhusu aina mbalimbali za fasihi na maoni hao yana umuhimu katika kuikuza fasihi yao. Utafiti huu unatofautiana na wa Mpesha kwani umeshughulikia utanzu wa ngano za kifantasia pekee. Aidha, utafiti wa Mpesha (1995) ulifaa kwani maoni ya watoto yalishughulikiwa kwa undani kama yalivyo katika utafiti huu.

Utafiti wa Karuga (2005), ulifanyiwa watoto wa darasa la 5 na 6. Lengo lake lilikuwa kuchunguza upokezi wao wa vitabu vya hadithi za kihalisia na zile za kifantasia kwa kuzingatia vigezo maalum. Alitambua kuwa watoto huwa na mahitaji na matarajio yao wenyewe kuhusu vitabu wanavyoandikiwa. Karuga alitumia nadharia ya Mwitikio wa Msomaji na uhakiki wa Kimtindo. Kinyume na utafiti wa Karuga uliolenga kuchunguza upokezi wa watoto, utafiti huu umechunguza ufasiri wa maudhui, wahusika na

(24)

13

Mtindo wa nyimbo za watoto wa shule za chekechea ulifanyiwa utafiti na Mwanza (2007). Lengo lake lilikuwa kuvichambua vipengele vya kimtindo vinavyochangia katika uwasilihaji wa maudhui. Pia alitumia nadharia ya uhakiki wa kimtindo na ile ya umuundo. Mbinu alizotumia katika kukusanya data ni mahojiano na uchunzaji. Utafiti wake ulidhihirisha kuwa baadhi ya maudhui yanayojitokeza katika nyimbo hizi ni kuonyesha nafasi ya mama katika malezi, lishe bora, umuhimu wa masomo miongoni mwa mengine. Utafiti wake ni tofauti na huu kwani alishughulikia utanzu wa nyimbo ilhali huu umejikita katika ngano za kifantasia. Aidha, utafiti huu umechambua maoni ya watoto ili kuonyesha ufasiri wao wa wahusika, maudhui na mandhari. Ijapokuwa alishughulikia utanzu wa nyimbo, utafiti wake una umuhimu kwa upande wa uchambuzi wa maudhui yanayowaadilisha watoto.

(25)

14

Magaju (2004), alihakiki uhalisiajabu katika riwaya za Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002). Alikuwa na lengo la kubainisha jinsi uhalisiajabu unavyojitokeza

katika riwaya za Kiswahili. Pia alitumia mbinu ya usomaji maktabani ili kupata data za utafiti. Utafiti wake ni muhimu kwani uliongozwa na nadharia ya Uhalisiajabu sawa na utafiti huu. Vigezo vya kifantasia pia vimeainishwa katika utafiti wa Magaju (2004), jambo ambalo ni muhimu katika utafiti huu. Aidha, utafiti huu unatofautiana na wa Magaju kwani ulichunguza ufasiri wa maudhui, wahusika na mandhari miongoni mwa wanafunzi wa darasa la tatu, Kaunti ya Homabay katika utanzu wa ngano za kifantasia. Data zilizotumika katika utafiti huu pia zilikusanywa nyanjani tofauti na za Magaju (2004) zilizopatikana maktabani. Utafiti huu pia ulishughulikia maudhui kama yalivyofasiriwa na watoto, jambo ambalo halikushughulikiwa na Magaju.

1.9 Misingi ya Nadharia

Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili zifuatazo:

a) Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji b) Nadharia ya Uhalisiajabu

(26)

15

katika ulimwengu halisi, japo mafunzo hulenga binadamu katika maisha yake ya kiuhalisia.

1.9.1 Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji

Nadharia hii inalenga kubaini uhusiano uliopo kati ya msomaji na kazi ya fasihi. Msomaji anapopitia kazi ya fasihi anaweza kuifasiri kulingana na tajriba yake ya maisha au usomaji. Mielekeo ya kibinafsi pia ina athari kubwa kuhusu namna msomaji hupokea kazi fulani.

Louise Rosenblatt alipendekeza nadharia hii kwa mara ya kwanza mnamo 1938. Baadhi ya watetezi wake wakuu ni Stanley Fish (1970), Jane Tompskin (1980) na Wolfgang Iser (1974, 1978). Iser anaeleza kuwa muundo wa kazi fulani ndio utakaoathiri jinsi msomaji atakavyoipokea. Anachomaanisha ni kuwa matini yoyote ya kifasihi ni aina ya malighafi ambayo msomaji ni sharti aifanyie kazi ingawa muundo na sifa za matini huchangia katika kuathiri kazi ya msomaji. Iser (1974) anaeleza kuwa muktadha wa msomaji, ufahamu wake, mazingira yake pamoja na sifa zinazomzunguka huathiri maana atakayoipa kazi ya fasihi.

(27)

16

kwenye misingi ya kijamii. Yaani, akili ya msomaji haiwezi kufanya kazi ya kufasiri matini bila kuathiriwa na misingi ya kijamii.

1.9.2 Mihimili ya Mwitikio wa Msomaji

Ifuatayo ni baadhi ya mihimili ya nadharia ya Mwitikio wa Msomaji kulingana na Iser (1974) na Tompkins (1980):

1. Maarifa ya kimsingi na tajriba aliyo nayo msomaji huathiri namna ambavyo ataifasiri matini (Tompkins 1980). Mwitikio wa Msomaji huongozwa na asili mielekeo na maadili yake wala si maoni ya mwelekezi au mwalimu wake. Kwa hivyo, kazi ileile inaweza kufasiriwa kwa njia tofauti na wasomaji tofauti au ikafasiriwa kwa njia tofauti na msomaji yuleyule ikiwa ataisoma katika vipindi tofauti.

2. Katika uhakiki wa kazi ya fasihi, msomaji ndiye mwenye umuhimu mkubwa wala si matini. Kazi ya fasihi haiwezi kupata uhai wake hadi inaposomwa. Iser (1974), aliibua wasomaji wa aina tatu ambao ni:

a) Msomaji anayelengwa

Huyu ni anayelengwa na mtunzi wa kazi ya fasihi. Kazi inaweza kulenga watoto, vijana au watu wazima.

b) Msomaji wa kukisiwa

(28)

17 c) Msomaji bora zaidi

Huyu ni msomaji wa kiwango cha juu ambaye ana uwezo wa juu kabisa wa kuifasiri kazi ya fasihi.

3. Katika kusoma kazi ya fasihi darasani, kuna usomaji wenye nia ya kutaka kupata mawazo au kutaka kujua tu matini hiyo inasema nini na usomaji wa kumchochea au kumhamasisha msomaji atake kujigundulia mengi kutokana na tajriba yake ya kipekee aliyoipata maishani.

Mihimili miwili ya nadharia hii ndiyo imetumika katika utafiti huu. Mhimili wa kwanza umetumiwa kuhakiki maoni ya watoto kuhusu maudhui, mandhari na wahusika wa ngano teule za kifantasia. Baada ya kuulizwa maswali, majibu yaliyotolewa na watoto yalichanganuliwa na kisha kufasiriwa. Hii ni kwa sababu mhimili huu unasisitiza kuwa tajriba mbalimbali za wasomaji ndizo huongoza namna watakavyofasiri kazi yoyote ya kifasihi. Watoto wanaosoma katika shule moja huenda wakafasiri ngano kwa njia tofauti kutegemea hisia zao, jinsia, malezi, dini, maarifa ya kimsingi.

Mhimili wa pili wa nadharia ya mwitikio wa msomaji pia umetumiwa katika utafiti huu kwani unasisitiza umuhimu wa msomaji aliyelengwa na kazi ya fasihi. Utafiti huu unawalenga watoto wa darasa la tatu. Kwa hivyo, maoni yao kuhusu ufasiri wa maudhui, wahusika na mandhari yana umuhimu. Haya yanaafikiana na malengo ya utafiti. Maoni ya mtafiti hayana uzito katika utafiti huu.

(29)

18

Ngano hizi husheheni maajabu, miujiza na matukio ya kimazingaombwe. Nadharia inayotosheleza mahitaji ya uhakiki wa kazi kama hii ni ya uhalisiajabu.

1.9.3 Nadharia ya Uhalisiajabu

Nadharia hii iliasisiwa mnamo 1925 na Mjerumani aliyejulikana kama Franz Roh (Roh, 1968). Aliitumia uhalisiajabu katika muktadha wa kisanaa kusawiri aina fulani ya miujiza iliyomo kwenye uhalisi unaotokana na ujarabati (Zamora 1995). Zamora anaendelea kueleza kuwa katika aina hii ya sanaa matukio ya kifantasia na kichawi huelezwa kwa namna ya moja kwa moja kama kwamba ni ya kawaida. Hii ni kwa sababu uhalisiajabu haujajitenga na matukio ya kawaida ya jamii zetu bali unatokana nayo. Pia, hakuna mpaka baina ya uhalisi na ndoto katika uhalisiajabu. Katika aina hii ya fasihi, matukio hayafuatani kimantiki, vilevile, mandhari ni muhimu kwani mazimwi, mito, mimea, wanyama na hata misitu huhusishwa.

Cooper (1998), naye anahusisha aina hii ya fasihi na waandishi kutoka Afrika Magharibi. Anasema kuwa sababu za kisiasa ndizo ziliwachochea kutumia mtindo huu katika kazi zao. Huu ulikuwa mfumo wa uongozi wa kibepari uliozungumziwa na waandishi kama Anderson na Jameson. Hii inaonyesha kuwa uhalisiajabu haujajitenga na matukio ya kawaida ya jamii.

(30)

19 1.9.4 Mihimili ya Uhalisiajabu

Ifuatayo ni baadhi ya mihimili ya nadharia hii kulingana na Franz Roh (Roh, 1968):

1. Katika aina hii ya fasihi, matukio hayafuatani kimantiki kama ilivyo katika maisha ya kawaida. Mandhari ni muhimu na wahusika wanyama, majitu, misitu na hata wachawi hurejelewa.

2. Matukio ya kiajabu, kushangaza na kuogofya huonekana kama ya kawaida. 3. Hakuna mpaka kati ya uhalisi na ndoto, huwa vimechanganyika.

4. Wakati na mahali vina uhusiano ya kiduara, matukio hujirudia katika kazi za kihalisiajabu.

5. Uhalisiajabu umefungamana na sanaa jadi kama vile visaasili, hurafa, ngano za mazimwi.

6. Matukio hayafuatani kimantiki kama katika uhalisia, mtindo wa baadhi ya tanzu za fasihi simulizi hutumika.

(31)

20 1.10 Mbinu za Utafiti

Utafiti huu ulijikita katika maeneo ya nyanjani na maktabani. Usomaji mpana wa vitabu, makala, tasnifu, majarida na machapisho yanayohusiana na mada hii yalirejelewa kwa undani. Usomaji huu ulimsaidia mtafiti kuelewa zaidi kuhusu nadharia za utafiti na maoni ya wataalam mbalimbali kuhusu ngano za kifantasia.

Baada ya usomaji maktabani, mtafiti alielekea nyanjani ili kukusanya maoni ya watoto kuhusu wanavyofasiri mandhari, wahusika na maudhui yanayotokana na ngano za kifantasia. Mtafiti aliwashirikisha watoto katika kusoma na baadaye, katika mjadala walijibu maswali yaliyotokana na ngano walizosoma.

1.10.1 Uteuzi wa Sampuli

(32)

21

Jwan na Ong’ondo (2011), wanaeleza kuwa ili kuwafanyia watoto utafiti, ni sharti

mtafiti apate idhini kutoka kwa wasimamizi wao. Haya yalizingatiwa kwani mtafiti aliomba idhini kutoka kwa walimu ili kuteua sampuli na kufanya utafiti.

1.10.2 Ukusanyaji wa Data

Mbinu ya mjadala elekezi ilitumiwa kukusanya data. Mtafiti, pamoja na wanafunzi walioteuliwa walikuwa na vikao ambapo ngano teule za kifantasia zilisomwa. Mtafiti aliwashirikisha wanafunzi katika kusoma kwa sauti na baadaye kuwauliza maswali. Kama mchunzaji wa kushiriki, mtafiti aliwashirikisha wanafunzi katika majadiliano na kuandika maoni yao. Majibu ya wanafunzi na maelezo yao kuhusu mada ndogondogo kutoka kwa kila ngano yalirekodiwa.

1.10.3 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Matokeo

Utafiti huu ulinuia kuchunguza ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa shule za msingi. Data zilizotoka nyanjani zilichanganuliwa kwa kuzingatia majibu ya wanafunzi na maelezo yao kutokana na mahojiano kati yao na mtafiti. Data ya mtafiti iliyorekodiwa kutokana na uchunzaji wa kushiriki pia ilichanganuliwa. Wakati wa uchanganuzi, data zenyewe zilipangwa kimaelezo kulingana na namna watoto wa darasa la tatu walivyofasiri maudhui, wahusika na mandhari.

(33)

22

uhalisiajabu pia iliongoza utafiti huu hasa ikizingatiwa kuwa ngano za kifantasia zimekiuka mantiki japo zinaelezea matukio halisi ya jamii.

Data zote zilizopatikana zilipangwa na kuainishwa kulingana na malengo ya utafiti huu. Majibu yote yanayotokana na swali moja yaliwekwa pamoja na kufasiriwa. Uchanganuzi huu uliongozwa na malengo, maswali pamoja na mihimili ya nadharia ya mwitikio wa msomaji pamoja na ile ya uhalisiajabu. Hapa tumeonyesha maudhui mbalimbali yanayojitokeza katika ngano husika kwa mujibu wa watoto. Vilevile, ufasiri wa tabia za wahusika mbalimbali na mandhari umeainishwa katika ngano zote zilizorejelewa.

1.11 Hitimisho

(34)

23

SURA YA PILI

UFASIRI WA MAUDHUI KATIKA NGANO ZA KIFANTASIA 2.0 Utangulizi

Lengo la kwanza la utafiti ni kuchunguza jinsi watoto wanavyofasiri maudhui yanayojitokeza katika ngano za kifantasia. Maoni ya watoto yaliyotokana na maswali waliyoulizwa baada ya kusoma kila hadithi yameainishwa na kuchanganuliwa. Ufasiri huu umeongozwa na nadharia ya Mwitikio wa Msomaji na ile ya Uhalisiajabu. Hii ni kwa sababu maoni ya watoto baada ya kusoma hadithi huathiriwa na tajriba zao maishani. Kwa mujibu wa Tompkins (1980), maarifa ya kimsingi na tajriba aliyo nayo msomaji huathiri namna ambavyo ataifasiri matini. Nadharia ya Uhalisiajabu imetumika katika ufasiri wa maudhui katika ngano za kifantasia. Maoni ya Zamora (1995) ni kuwa, katika fasihi kama hii matukio hayafuatani kimantiki kama ilivyo katika uhalisia. Kwa hivyo, imetumika kufasiri maoni ya watoto ili kubaini mitazamo yao kuhusu mafunzo yanayotokana na ngano hizi.

Katika sura hii, dhana ya maudhui imeelezwa. Muhtasari wa kila hadithi pia umetolewa kabla ya kuainisha maoni ya watoto. Baadaye, maoni ya watoto yamechanganuliwa ili kuonyesha wanavyofasiri maudhui katika ngano za kifantasia. Baadhi ya maudhui ambayo yameelezwa ni ya kisasi, ulaghai, ukarimu, msamaha, heshima na imani katika Mungu. Sehemu inayofuata inaeleza dhana ya maudhui.

2.1 Dhana ya Maudhui

(35)

24

kuwasilisha ujumbe kwa hadhira yake, basi ujumbe huo ndio maudhui yake. Maoni ya Wamitila (2003), ni kuwa maudhui ni jumla ya mambo yote yanayozungumziwa katika kazi ya kifasihi. Maudhui hutumiwa kwa upana kujumlisha dhamira, falsafa, itikadi na msimamo wa mwandishi. Jumla ya maswala yanayoshughulikiwa na mwandishi basi ndiyo maudhui yake. Aidha, Wamitila (2008) anaposhughulikia fani na maudhui anasema kuwa maudhui hayawezi kumfikia msomaji bila ya kuwepo na nyenzo za kuyapitisha au kuyawasilisha. Fani ni jumla ya nyenzo zinazotumiwa kuwasilisha maudhui. Uhusiano uliopo basi kati ya fani na maudhui ni wa kutegemeana. Bila fani, maudhui hayapo na maudhui hayawezi kuwasilishwa bila ya kuwepo kwa fani. Mwandishi basi huweza kukuza maudhui yake kupitia kwa mazungumzo ya wahusika, matendo yao na hata nyimbo wanazoziimba.

Ruthiiri (2012), anaeleza maudhui kama chombo muhimu ambacho mwandishi anaweza kutumia kuwapa watoto amali muhimu za kijamii, kielimu na kidini. Maudhui kwa hivyo, huhusu maswala muhimu katika kazi ya msanii. Katika kazi za watoto, wasanii huweza kuzungumzia maudhui yanayolenga kuimarisha ukuaji wa akili, uelewa wa mazingira, kuadilisha au hata kufahamisha mtoto kuhusu matukio ya kihalisia katika maisha (Stewig, 1980).

Wasomaji ndio huipa kazi ya fasihi maana. Kulingana na Wamitila (2002), tunaweza kuivumbua maana ya kazi fulani kwa kuisoma kazi hiyo kwa kina na makini, huku tukiuelewa na kung’amua uhusiano wa visehemu mbalimbali na jinsi visehemu hivyo

(36)

25

umuhimu sana katika kuifanikisha kazi ya mwandishi. Ni katika muktadha huu basi ndipo kuna umuhimu wa kuchunguza jinsi watoto wanavyozielewa ngano za kifantasia.

Cass (1967), anaeleza kuwa katika fasihi ya watoto, mwandishi anapaswa kuteua maudhui kwa makini ili kutekeleza mahitaji ya mtoto. Katika ngano hizi, maudhui ya wema dhidi ya wovu yanapaswa kuzingatiwa ili kuadilisha watoto. Kulingana na Cass (keshatajwa), kuwepo kwa haki ni jambo muhimu sana katika maisha ya mtoto. Ikiwa mhusika fulani anaendeleza wovu katika hadithi, mtoto hutarajia kuona kuwa haki imetendeka kwa kuadhibiwa kwa mhusika huyo. Si lazima adhabu iwe kali lakini kitendo chochote kinachoonyesha kuwa wema umetuzwa na uovu umeadhibiwa ni jambo linalomridhisha mtoto.

Tunnel na Jacob (1997), wanaeleza kuwa maudhui ya kuogofya ni muhimu sana katika kumtayarisha mtoto kukumbana na matukio magumu maishani. Vilevile, Bettelheim (1975), anasema kwamba watoto wana haki ya kufahamishwa kuhusu maudhui ya kufurahisha na ya kuogofya kwani huo ndio ukweli wa maisha. Hakuna haja ya kuwadanganya au kuwapofusha kwa kuwafurahisha pekee. Ni vyema kuwatayarisha kuhusu pande mbili za maisha, furaha na huzuni. Hii ni kwa sababu wao ni sehemu ya jamii ambamo matukio haya huibuka.

(37)

26

kimsingi huzua mgogoro katika hadithi, jambo ambalo hukuza ploti za hadithi hizi. Wakati mwingine maudhui haya hukuzwa kupitia kwa wahusika wa kustaajabisha walio na nguvu za ajabu na uwezo uliopita ule wa binadamu wa kawaida. Wanaweza kuwa wachawi wanaoangamiza au wanyama wazuri wanaofariji na kuleta matumaini.

Kazi za kifantasia zilizokusudiwa watoto huwa na maudhui ambayo yamefichika. Huck na wengineo (2001), wanasema kwamba ili maudhui haya yaweze kufichuliwa, ni sharti yafasiriwe kwani maudhui yenyewe yamejitokeza kwa njia ya kijazanda au kishairi. Ufasiri wa maudhui katika ngano hizi hutegemea umri, jinsia, na malezi ya mtoto miongoni mwa mengine.

Aidha, maudhui kama kipengele cha kimsingi katika fasihi ya watoto ni kiini cha hadithi na huhusu maswala muhimu katika hadithi ile. Ni muhimu basi kwa hayo maudhui kuwa ya wazi na mepesi kulingana na kiwango cha watoto lengwa ili fasihi iweze kutekeleza majukumu yake. Hii ni kwa sababu vitabu vya watoto vinapaswa kuwakuza kijamii na kimaadili.

(38)

27

Fasihi ina majukumu ya kutekeleza katika maisha ya anayeipokea. Ikiwa hadhira lengwa ni watoto, ni muhimu kubaini ikiwa wanaweza kuzifasiri na kupokea mafunzo waliokusudiwa. Kabla ya kufanya hivyo, ni muhimu kushughulikia muhtasari wa hadithi husika kisha kueleza maoni ya watoto.

2.1.1 Muhtasari wa Hadithi ya Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2007)

Hadithi hii inahusu Fisi na Sungura ambao ni marafiki waliopendana sana. Wakati mmoja kulitokea kiangazi na wanyama hawa walikosa chakula cha kuwalisha wanao. Baada ya kujadiliana kwa muda, wote waliamua kwenda kutafuta chakula kwa zamu. Mnyama aliyeachwa nyumbani alikuwa na jukumu la kuwatunza watoto wa mwenzake. Fisi ndiye alikuwa wa kwanza kwenda kutafuta chakula kwa hivyo Sungura alibaki na watoto wake.

Sungura alijitahidi sana katika malezi ya watoto wote na alionyesha upendo sana. Fisi aliporudi nyumbani baada ya kukosa chakula, alilakiwa kwa furaha sana. Alifurahi kuwaona watoto wake wakiwa na afya nzuri kuliko hata alivyowaacha. Zamu ya Sungura ilipofika, Fisi hakuwajibika jinsi Sungura alivyowajibika. Chakula kilipoanza kuadimika aliamua kuwapa watoto wa Sungura chakula kidogo tu ili wasife kwa njaa huku akiwapa watoto wake chakula kingi. Chakula kilipoendelea kuadimika, aliamua kutowapa chakula chochote watoto wa Sungura. Chakula chote aliwapa watoto wake. Hata wanawe Sungura walipokuwa wagonjwa hakujishughulisha.

(39)

28

Sungura pia alikosa mafanikio na kuamua kurejea nyumbani. Alipofika hakuamini macho yake. Watoto wake walikuwa wamelala mekoni.

Sungura alikuwa ameamua kulipiza kisasi. Fisi alipomjia, hakuonyesha dalili yoyote ya kukasirika. Badala yake alimdanganya kuwa alifanikiwa kupata chakula mbinguni kwa hivyo Fisi angeweza kwenda na wanawe ili waweze kula minofu. Sungura alishirikiana na Mwewe katika kutekeleza kisasi.

Alimwambia Fisi kuwa angeweza kushika mkia wa Mwewe hadi mbinguni. Watoto wa Fisi wangeshika mkia wa mama yao na wengine kushika mikia ya wenzao huku wakiwa na sufuria za kubebea minofu mikononi. Mwewe alipaa hadi alipohakikisha kuwa hangeweza kuona chochote kule chini ardhini kisha akaukata ule unyoya wake ulioshikiliwa na Fisi. Fisi na wanawe walianguka chini na kupata majeraha mabaya sana.

Fantasia inayojitokeza katika hadithi hii ni kuwepo kwa matukio yasiyoweza kuwepo katika uhalisia kama kuongea kwa wanyama au hata wanyama kuwa na safari ya kuwafikisha mbinguni. Kulingana na Tunnel na Jacob (1997), ngano ya kifantasia huwa na sifa kadhaa lakini kuwepo kwa sifa moja tu ya maajabu, kama vile kuongea kwa wanyama kunaiwezesha kuitwa fantasia.

(40)

29

A: Fisi alikuwa mbaya kwa sababu aliwatesa watoto wa sungura kwa hivyo Sungura alifanya vizuri kumlipa.

B: Mtu akimfanyia mwenzake vibaya atalipwa jinsi Fisi alifanyiwa.

C: Si vizuri kutenda mabaya kwa sababu ukifanya hivyo ni lazima ulipwe.

D : Mwenzako akikukosea, ni vizuri kumsamehe. Kwa hivyo, Sungura angemsamehe Fisi baada ya

kuwatesa watoto wake.

E: Fisi hakusema asante baada ya kusaidiwa na Sungura kwa hivyo, Sungura alifanya vizuri kumwambia Mwewe ili alipwe vibaya.

F: Hadithi hii inafunza kuwa tusifanyiane mabaya. Tupendane na kusameheana wenzetu wakitukosea.

G: Sungura alisema uongo. Alimdanganya Fisi eti alipata chakula mbinguni.

H: Hadithi hii inafunza eti tuwe na tabia nzuri kama ya Sungura. Yeye aliwapatia watoto wa Fisi chakula na dawa.

(41)

30

J: Mungu anapenda watu wazuri kama Sungura kwa sababu aliwapenda watoto wa Fisi.

K: Fisi alidanganywa kwa sababu ya ubaya wake.

L: Hadithi hii inafunza kuwa tupendane na tusaidiane jinsi sungura alifanya.

M: Fisi ni mbaya sana. Yeye ni mchoyo.

N: Fisi aliangushwa chini kwa sababu ana tabia mbaya. Hakuwapenda watoto wa Sungura

O: Watoto wote wapendane na kusaidiana.

P: Ni vibaya kuwa mwongo kama Fisi.

Q: Ukiwa na tabia mbaya, unalipwa na Mungu kwa mabaya kama Fisi.

R: Marafiki wanapaswa kusameheana.

S: Watoto walio na tabia mbaya hulipwa kwa mabaya kama Fisi.

T: Mungu hapendi waongo. Anataka watu wasameheane.

(42)

31

sababu ya ubaya wake. Waliona kuwa alistahili kwa sababu alikosa kuonyesha ukarimu wake kwa watoto wa Sungura baada ya kutendewa mema. Haya yanaafikiana na maoni ya Madsen (1976), anapoeleza kuwa, watoto hutarajia kuona kuwa uovu umeadhibiwa na wema kutuzwa. Walieleza kuwa Fisi alipata malipo kulingana na maovu aliyowatendea watoto wa sungura na kuwa ni vizuri kutenda mazuri ili usipatwe na mabaya. Aidha, walijifunza kutoshiriki maovu kwani huchangia katika uovu (S). Kwa ujumla, walisisitiza ukuzaji wa maadili mema katika jamii.

Ni watoto 20% pekee (D, F, R na T) waliosisitiza kuwepo kwa msamaha kati ya watu wakieleza kuwa hadithi hii inafunza kuwa watu wanapoishi pamoja ni vizuri wasameheane wanapokosana. Walipendekeza kuwa Sungura angemsamehe Fisi hata ikiwa aliwatesa wanawe. Aidha, mmoja alieleza kuwa watu wakipendana huweza kusameheana kwa urahisi. Maudhui haya ya msamaha japo yalirejelea kisa cha Fisi na Sungura, watoto waliweza kujihusisha nayo. Maoni ya mtoto D yanaonyesha kuwa watoto wana uwezo kuelewa maudhui katika hadithi na kujifunza kutokana nayo. Badala ya kutaja moja kwa moja kuwa majina ya wanyama waliohusishwa, mtoto huyu alisema kuwa “mwenzako akikukosea, ni vizuri kumsamehe”.

(43)

32

anayefurahisha katika hadithi nyingi za Kiafrika na licha ya ulaghai wake, yeye ni maarufu sana.

Aidha watoto 20% (H, I, L na M), walitambua kuwepo kwa ukarimu. Ukarimu wa Sungura ulitambuliwa alipowapa watoto wa Fisi chakula na dawa. Walisema kuwa binadamu wasiwe wachoyo kama Fisi (I). Uzuri wa Sungura ulisisitizwa kwa vile hakuwa mchoyo. Japo anatumia ulaghai baadaye, ukarimu wake wa mwanzoni ulimfanya ajitokeze kama mhusika mzuri miongoni mwa watoto.

Mapenzi yalitambuliwa na watoto 15% (J, O na N). Kulingana nao, watoto wadogo wanahitajika kupendana na kusaidiana katika jamii (O). Wanatoa mfano wa mhusika Sungura aliyewapenda watoto wa Fisi wakati mama yao alikwenda kutafuta chakula. Walieleza kuwa mapenzi ya Sungura yalijitokeza alipowapa watoto wa Fisi chakula na dawa bila kuwabagua. Kwa sababu Fisi alikosa mapenzi, kulingana na watoto, alikuwa mhusika mbaya.

(44)

33

Japo majibu yaliyotambuliwa na watoto yaliegemea katika kutuza wema na kukashifu wovu, watoto waliweza kuhusisha binadamu na yaliyojitokeza hadithini. Haya yanaonyesha kuwa watoto walielewa mafunzo yaliyojitokeza katika ngano hii. Sehemu ifuatayo imeshughulikia muhtasari wa hadithi ya pili ambayo ni Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003).

2.1.2 Muhtasari wa Hadithi ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003)

Hadithi hii inahusu wahusika wawili ambao ni Chozi na Tembo. Chozi alikuwa jirani ya Tembo lakini majirani hawa wawili walikuwa hawaamkiani wala kutembeleana. Nyumba ya Chozi ilikuwa njiani na ndani ya kiota chake mlikuwa na makinda saba. Kila mara Chozi alikuwa akiondoka kwenda kuwatafutia wanawe chakula na kila alipokutana na Tembo kila mmoja wao alikuwa na shughuli zake.

Siku moja Chozi alipoondoka, Tembo alipita karibu na nyumba yake na kuwakanyaga wana wa Chozi hadi wakafa. Chozi aliporudi alisikitika sana. Alipomwuliza Tembo sababu ya kuwaua wanawe, Tembo alimjibu kwa ujeuri na kutomheshimu kama mwenzake. Hakujali kumwomba msamaha.

Ni kweli kuwa Tembo aliwaua watoto wa Chozi bila kujua lakini ujeuri wake ulimsikitisha sana Chozi. Chozi aliwakusanya ndege wenzake na kuwahadithia masaibu yaliyompata. Baada ya kujadiliana kwa muda mrefu waliamua kwenda kulipiza kisasi. Mwewe, Tai na Kipanga walitumwa kwenda kutoboa macho ya Tembo. Walielezwa waende wakatue kwenye kichwa cha Tembo na kudona macho yake.

(45)

34

kisasi walidona macho ya Tembo na akawa hawezi kuona tena. Mara vyura wakatokezea na kupiga kelele nyingi kando ya shimo kubwa. Tembo alifuata kelele hizo akawa anaenda bila kuona na kisha kuanguka shimoni na kuvunjika mguu mmoja. Chozi na mumewe walimwendea na kumwambia kuwa afanyaye mabaya hulipwa. Baada ya kuomba msamaha Tembo alisamehewa na kina Chozi kisha wakamwahidi kuwa wangemtoa shimoni.

2.1.3 Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003)

Baada ya kusoma hadithi, watoto walioshirikishwa katika utafiti walitoa maoni yafuatayo kuhusu maudhui. Maoni haya yalikuwa majibu ya swali lifuatalo:

Hadithi hii inatufunza nini?

A: Tembo hakumwomba Chozi msamaha baada ya kuwaua watoto wake. Chozi alifanya vizuri kutoboa macho yake.

B: Kulipa kwa mabaya ni dhambi mbele ya Mungu. Chozi angemsamehe Tembo.

C: Tuwe na tabia nzuri, ukifanya mabaya, utafanyiwa mabaya.

D: Hadithi hii inatufunza kuwa tuwaheshimu majirani wote na kuwapenda. Tembo hakumheshimu jirani yake.

(46)

35

F: Ndovu alimdharau Chozi kwa sababu alikuwa mdogo.

G: Hadithi hii inafunza kuwa wakubwa wasiwatese wadogo.

H: Ukimkosea mtu, unamwambia pole. Tembo angemwomba Chozi msamaha.

I: Hadithi hii inafunza kuwa majirani wapendane na kusalimiana.

J: Mungu anataka tusameheane halafu hata wewe utasamehewa

K: Hadithi hii inafunza kuwa ukimkosea mwenzako, utalipwa jinsi Tembo alivyolipwa.

L: Chozi alifanya vizuri kutoboa macho ya Tembo kwa sababu aliwakanyaga watoto wake hadi wakafa

M: Watoto wasaidiane vile ndege walimsaidia Chozi.

N: Tembo alikuwa na kichwa kigumu. Alimdharau Chozi na kumjibu vibaya.

O: Wakubwa wasiwatese wadogo.

P: Chozi angemsamehe Tembo asingetoboa macho yake.

Q: Majirani wapendane.

(47)

36 S: Majirani wapendane na kusalimiana.

T: Hadithi hii inafunza kuwa tupendane na kuheshimiana.

Watoto 25% (A, C, E, K na L) walitambua kuwepo kwa tendo la kulipiza kisasi. Walieleza kuwa kitendo kibaya hulipwa kwa mabaya. Hili lilitokana na tabia ya Tembo kuwaua wana wa Chozi na kukosa kumwomba msamaha. Bettelheim (1975), anaeleza kuwa watoto hufurahia kuona kuwa maovu yameadhibiwa. Wana wa Chozi walipouawa na Tembo, watoto hawa waliona umuhimu wa kisasi kutekelezwa. Japo kisasi huwaridhisha watoto, iwapo mtu anaweza kuomba msamaha basi huweza kuepukana nacho (A).

Hata hivyo, jumla ya watoto 25% (B, H, J, R na P) walikashifu tendo la kulipiza kisasi na kuhimiza msamaha. Katika maelezo yao, wanasema kwamba Mungu hapendi kisasi na kwa hivyo unapolipiza kisasi, hiyo ni dhambi mbele yake (B). Watoto hawa wana tajriba mbalimbali kama inavyoelezwa na waasisi wa nadharia ya Mwitikio wa Msomaji. Majibu yao yanaonyesha kuwa waliathiriwa na mafunzo ya kidini yanayoeleza kuwa Mungu hapendi kisasi bali msamaha. Aidha, maoni ya Stewig (1980) yanayohimiza kuwepo kwa kisasi katika hadithi za watoto yalipingwa na maoni ya watoto hawa.

(48)

37

hayangetobolewa. Ikiwa majirani hawa (Chozi na Tembo) wangekuwa wanasalimiana na kupendana hawangechukiana.

Maonevu dhidi ya viumbe wanyonge yalikuwa maoni ya watoto 20% (F, G, N na O). Watoto G na O walieleza kuwa watu wakubwa hawafai kuwatesa wadogo. Maoni haya yanaonyesha kuwa walijinasibisha na mhusika Chozi hadithini kwani kulingana nao, Chozi alidharauliwa na kuonewa na Tembo kwa sababu alikuwa kiumbe mdogo. Katika fasihi ya watoto, watoto huweza kujinasibisha na wahusika wanyonge wasiojiweza au wadogo kama wao (Karuga, 2005). Watoto walijitokeza kama ambao walimhurumia Chozi kwani walimwona Tembo kama aliyejawa na kiburi. Walitambua kuwepo kwa udhalimu katika jamii unaoendelezwa na walio na nguvu dhidi ya wanyonge.

Ushirikiano ulitambuliwa na mtoto mmoja (M) aliposema kuwa watu wanapaswa kusaidiana jinsi ndege walivyomsaidia Chozi. Mtoto huyu alikuwa akiunga mkono hatua ya Tembo kutobolewa macho na Chozi na kwa vile hakuwa anajiweza, ilibidi apate usaidizi kutoka kwa ndege wenzake waliokuwa wadogo kama yeye.

Hadithi ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2006), inahusu maisha ya wanyama porini. Maoni ya watoto yanaonyesha kuwa wana uwezo wa kutambua maudhui na mafunzo. Vilevile, watoto waliweza kuoanisha mafunzo na maisha ya binadamu. Sehemu inayofuata imeshughulikia muhtasari wa hadithi ya tatu, maoni ya watoto na ufasiri wa maudhui.

2.1.4 Muhtasari wa Hadithi ya Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998)

(49)

38

amwazime wembe wa kuwanyolea wanawe. Baada ya kupewa wembe, Kuku aliambiwa aurejeshe jioni ya siku ambayo ingefuata. Kuku alipofika na wembe huo kwake watoto wake waliupoteza walipokuwa wakicheza nao.

Mwewe alipoambiwa na Kuku kuhusu kupotea kwa wembe ule, alipandwa na hasira nyingi na kutaka atafutiwe wembe wake kwani alitaka kuutumia kukata kucha za wanawe. Mama Kuku na wanawe walichakura kila mahali wakiutafuta wembe wa Mwewe. Walijitahidi sana lakini hawakufanikiwa. Mama Kuku alijaribu kumwomba Mama Mwewe msamaha lakini Mwewe hakujali.

Mwewe alipandwa na hasira sana. Jambo hili lilimsikitisha sana Mama Kuku. Hata majirani wengine walikosa kumwelewa Mwewe. Jogoo aliporudi kutoka safarini alisikitika sana kwa yote aliyoambiwa. Alijaribu kwenda kumwomba Baba Mwewe msamaha lakini naye hakusikiliza, badala yake alizidi kumwonya na kumwambia aurudishe ule wembe. Japo jamii ya Kuku ilijitahidi sana kuutafuta ule wembe, haukupatikana.

Siku iliyofuata Mwewe aliwanyanyua watoto wa Kuku na kuwala. Kitendo hiki kiliwahuzunisha sana Baba Kuku na Mama Kuku. Wote waliamua kuhamia mjini lakini masaibu yao hayakuisha bali yaliendelea kuongezeka. Walihuzunika walipokuwa mjini kwani maisha yao yalikuwa hatarini. Mwishowe, walirejea kijijini ambapo Mwewe aliendelea kuwala wana wa Kuku.

2.1.5. Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998)

(50)

39

A: Mwewe ni mbaya sana, alikataa kumsamehe Kuku lakini Kuku alimwomba msamaha.

B: Si vizuri kumfanyia mtu vibaya akikukosea, watu wapendane na kusameheana.

C: Tuwachague marafiki wazuri. Tusikubali kuwa na marafiki ambao hawawezi kusamehe kama Mwewe.

D: Hadithi hii inatufunza kuwa tunapokesewa na wenzetu, ni vizuri kuwasamehe.

E: Mungu anaweza kumsaidia Kuku akimwomba.

F: Hadithi hii inatuonyesha kwa nini Kuku na Mwewe hawasikilizani hadi sasa.

G: Mwewe si mchoyo, alimpa Kuku pilau, kachumbari na wembe.

H: Mwewe ni mbaya. Tusiwe na tabia kama ya Mwewe.

I: Mwewe bado anakula watoto wa Kuku. Yeye ni mbaya sana kwa sababu hakumsamehe.

J: Kuku angewakataza watoto wake waache kucheza na wembe, hiyo ni tabia mbaya.

(51)

40

L: Mwewe anapenda kulipa kisasi mpaka sasa.

M: Hadithi inafunza kwamba Mwewe na Kuku ni maadui.

N: Watoto wa Kuku wana tabia mbaya kwa sababu walicheza na wembe.

O: Mama Mwewe si mzuri.Tusiwe kama yeye.

P: Watoto wote wawe na adabu.Wasiwe kama watoto wa kuku.

Q: Watu wasaidiane vile Mwewe alimsaidia Kuku na Wembe na chakula.

R: Mwewe angemsamehe Kuku.

S: Kuku anawapenda watoto wake kwa sababu aliwapikia na kuwanyoa.

T: Watoto wadogo wasicheze na vitu vya wakubwa.

(52)

41

Licha ya kuwa Mama Kuku aliomba msamaha, Mama Mwewe alikataa kumsamehe. Maudhui ya ukosefu wa utu yanajitokeza hapa hasa watoto wanaposema kwamba Mama Kuku alikosa huruma. Jambo hili linamfanya Mwewe kuwa mhusika mbaya asiyependwa na watoto (O). Haya yanaafikiana na maoni ya Finnegan (1970) anapoeleza kuhusu wahusika waovu wanaopatikana katika ngano za Kiafrika. Kulingana naye, Mwewe ni mhusiki katili asiyekuwa na utu. Anaposema kuwa tusiwe kama Mwewe, mtoto O hapendi kuona chuki na mateso yakiendelezwa katika jamii.

Pamoja na hayo, watoto 20% (F, L, M na I) walitambua uhasama baina ya Kuku na Mwewe. Walionyesha kuwa wanaelewa mazingira yao kwa kuoanisha yanatokea katika uhalisia na matukio katika hadithi. Jambo hili lilibainika walipoeleza kuwa hadithi hii inaeleza kuwa Kuku na Mwewe bado ni maadui. Waliweza kutambua kuwa Mwewe bado anawala watoto wa Kuku. Ufahamu wa mazingira ni jambo muhimu katika kuwaelimisha watoto. Watoto huelewa mazingira yao vizuri kupitia kwa hadithi za kifantasia (Bettelheim 1975). Madai haya pia yanashikiliwa na Tucker (1981), anapoeleza kwamba watoto huhitaji ngano zinazojibu maswali yanayotokana na matukio ya kihalisia. Majibu yanayopatikana kutoka kwa ngano humridhisha mtoto kuliko maelezo yoyote ya kisayansi.

(53)

42

Vilevile, maudhui ya utovu wa adabu na heshima yaliweza kutambuliwa na watoto 20% (J, N, P na T) walioeleza kuwa watoto wa Kuku walikosa heshima kwani walicheza na wembe wa Mwewe hadi ukapotea. Walisema kuwa hii ilikuwa ishara ya tabia mbaya. Tunnel na Jacob (1997), wanaeleza kuwa fasihi ya watoto ina jukumu la kuwaadilisha watoto na kuwafunza kuhusu tabia njema zinazohitajika katika jamii. Watoto walitambua kuwa wana wa Kuku walikosa uadilifu kwa kupoteza wembe, jambo lililowaletea matatizo makuu. Mtoto P alitahadharisha dhidi ya watoto kuwa na tabia kama za wanawe Kuku. Mwewe pia alitambuliwa kama mhusika aliyekosa uadilifu kwa sababu alikataa kumsamehe Kuku hata baada ya kuombwa msamaha. Kinachojitokeza ni kuwa watoto hawakufurahia utovu wa nidhamu kwa kusema kuwa ni ‘tabia mbaya’ ( J na N).

Maudhui ya imani kwa Mungu pia yalitambuliwa na mtoto mmoja (E). Anapoeleza kuwa Mungu angewezakumsaidia Kuku, ina maana kuwa aliathiriwa na mafunzo ya kidini. Bettelheim (1975), anaeleza kuwa hadithi za kifantasia zina jukumu la kuadilisha watoto na pia kukuza imani yake ya kidini. Haya hutokana na maadili yanayosisitizwa na hadithi hizi ambayo pia hutokana na mafunzo ya kidini. Mtoto E aliweza kuoanisha mafunzo yaliyotokana na hatithi hii na tajriba yake ya kidini. Kwa kufanya hivi, uadilifu uliweza kujitokeza kama funzo linalotokana na hadithi hii. Aidha, utovu wa maadili mema ulikashifiwa na mtoto H alipoonya kuwa tusiwe kama Mwewe. Kulingana naye, Mwewe alikuwa mbaya na binadamu yeyote anayeiga tabia yake ni mbaya.

(54)

43

2.1.4 Muhtasari wa Hadithi ya Paka na Panya (Nyakeri, 2006).

Hadithi hii inamhusu mhusika Chaka ambaye ni Paka. Paka alikuwa amekosa chakula kutokana na mvua nyingi iliyokuwa ikinyesha bila kusita. Pia alikaribia kufa kutokana na baridi kali iliyoletwa na mvua. Alimwomba Mungu ili amsaidie asife kwa baridi na njaa. Baada ya maombi, alimwona Panya aliyekuwa akiziba tundu. Chaka alimwendea Panya na kumsihi ili aweze kumsaidia. Panya aliamua kumsaidia Chaka hasa baada ya kuona kuwa alikuwa amezirai. Panya alimwonea huruma na kumbeba hadi alimokuwa akiishi.

Mle ndani, Panya alimwashia moto ili ajipashe joto. Panya pia alimpikia chakula kitamu na kumlisha kwa sababu hakuwa na nguvu. Wanyama hawa wawili waliendelea kuwa marafiki wakubwa sana. Jambo hili liliwashangaza wanyama wenzao waliokuwa wakiishi mwituni. Siku moja walipokuwa wametulia kwao, Chaka alitamani sana kitoweo cha Panya kwa hivyo alipanga kumshambulia.

Paka hakuwa na habari yoyote na aliendelea kuwa mkarimu kwake. Chaka alifunga mlango na kuanza kumshambulia Panya ambaye alilia kwa uchungu sana. Kwa bahati nzuri, Fisi aliyekuwa akipita karibu alisikia kelele hizo na kuingia walimokuwa. Fisi aliyekuwa na njaa alimshambulia Chaka na kumgeuza kitoweo. Hivyo ndivyo panya alivyonusurika.

2.1.5 Ufasiri wa Maudhui katika Hadithi ya Paka na Panya ( Nyakeri, 2006)

(55)

44

A: Panya alikuwa na upendo. Alimpa Chaka chakula na pia kumwashia moto.

B: Paka ni mwongo, alimdanganya Panya kuwa hangemuua.

C: Hadithi hii inatufunza kuwa tuwe na tabia nzuri. Tusiwe waongo kama Paka.

D: Tukisaidiwa, tuseme asante. Paka hakusema asante.

E: Paka alijidanganyisha kuwa Mkristo lakini alikuwa mwongo.

F: Paka alimdanganya Panya kuwa wangekuwa marafiki, lakini alibadilika na kutaka kumla.

G: Ni vizuri kusema ukweli kwa marafiki zetu wanaotusaidia. Tusiwe waongo kama Paka.

H: Hadithi hii inatufunza kuwa Paka na Panya hawaelewani.

I: Panya ni mjinga sana. Kwa nini alikubali kumsaidia Paka na hawasikilizani.

J: Panya hakuwa mchoyo. Alimpa Paka chakula.

(56)

45

L: Mungu anapenda watu. Alimsaidia Panya hadi akakosa kuliwa na Paka.

M: Hadithi hii inafunza kuwa tusaidiane na Mungu atatusaidia. Paka alimwomba Mungu akapata usaidizi.

N: Paka alilipwa na Mungu kwa sababu alitaka kumla Panya, Fisi alimuua.

O: Ukimfanyia mtu vibaya, utapatwa na mabaya.

P: Hadithi hii inafunza kuwa marafiki wengine ni waongo kama Paka.

Q: Paka aliliwa na Fisi kwa sababu alitaka kumla Panya.

R: Tusiwe waongo kama Paka, uongo ni mbaya.

S: Tupendane na kusaidiana jinsi Paka alivyomsaidia Panya.

T: Tuseme asante baada ya kusaidiwa na tusidanganye wenzetu.

(57)

46

kulingana na mtoto T, watu hawapaswi kudanganyana. Watoto walijifunza umuhimu wa uaminifu.

Watoto 15% (J, K na S) walitambua ukarimu ulioendelezwa na Panya. Panya alimwashia Paka moto, akampikia na baadaye kumlisha hadi akapata nguvu. Walieleza kwamba binadamu wanapaswa kusaidiana jinsi Panya alivyomsaidia Chaka (S). Vilevile, mmoja wao alidokeza kuwa Mungu anapenda watu wanaosaidiana. Haya maoni yalionyesha kuwa watoto hawa waliweza kutambua maudhui haya na kuyaoanisha na maisha ya kawaida huku wakujifunza umuhimu wa kusaidiana.

Vilevile 15% ya watoto (L, M na N) walisema kuwa Mungu ndiye aliyemsaidia Paka kwa sababu alimwomba. Mmoja wao (M), alipendekeza kuwa tumwombe Mungu tunapokuwa na mahitaji na atatupa usaidizi. Kile kitendo cha kuliwa kwa Paka kulionyesha kuwa Mungu alilipiza kisasi kwa ubaya wa Paka. Maoni haya ya watoto yanaonyesha kuwa watoto hawa wamekulia katika mazingira yanayoendeleza imani ya kidini katika kukuza maadili. Bettelheim (1975), anaeleza kuhusu umuhimu wa ngano za watoto zinazohimiza imani za kidini kwani kupitia kwa hadithi kama hizi, watoto huweza kujifunza umuhimu wa maadili mema kwani mara nyingi mafunzo ya kidini yanaeleweka zaidi kupitia kwa hadithi.

(58)

47

umuhimu wa shukrani kwani waliamini kuwa anayekosa kushukuru baada ya kusaidiwa hupatwa na balaa jinsi Fisi alivyomwangamiza Paka.

Mtoto I alimlaumu Panya kwa kukosa kuwa mwangalifu. Alieleza kuwa Panya alikuwa mjinga kwa kukubali kumsaidia Paka kwa sababu hawasikilizani. Maoni haya yanaonyesha kuwa mtoto huyu anaelewa yanayojitokeza katika mazingira yake kwani Paka na Panya ni maadui. Asemavyo Tucker (1981), watoto wanahitaji ngano zinazojibu maswali yanayojitokeza katika jamii yao. Ngano hii iliwafahamisha watoto chanzo cha uhasama baina ya Paka na Panya.

Watoto 10% (O na Q), walieleza kuwa yeyote afanyaye ubaya hulipwa kwa mabaya. Kitendo cha Fisi kumla Paka kilikuwa ishara ya kisasi. Kulingana na mtoto Q, Paka aliangamizwa na Fisi kwa sababu ya uovu wake. Walitambua kuwa atendaye mema huandamwa na mema. Maudhui haya ya kisasi basi yalichangia kukuza maadili yao kwa kuwahimiza kutenda mema maishani.

2.1.5. Hitimisho

Sura hii ilidhamiria kuchunguza iwapo watoto wanafasiri maudhui yanayojitokeza katika ngano za kifantasia. Majibu ya watoto yameonyesha kuwa wana uwezo wa kufasiri maudhui yanayojitokeza katika ngano hizi. Katika hadithi ya Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006), watoto 25% (A, B, C, Q na S) walitambua kuwepo kwa

(59)

48

Maudhui ya kisasi pia yalijitokeza katika hadithi ya Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2006). Chozi alilipiza kisasi baada ya Tembo kuwaua wanawe. Kulingana na watoto watano 25% (A, C, E, K na L) haki ilitendeka. Watoto wengine 25% (B, H, J, R na P) waliotambua kuwa Mungu hapendi kisasi na kwa hivyo Chozi angemsamehe Tembo. Maoni haya yalionyesha kuwepo kwa tajriba mbalimbali miongoni mwa watoto. Watoto hawa walipendekeza kuwa majirani wanapaswa kuishi kwa heshima na upendo, sio jinsi ambavyo Chozi na Tembo walivyoishi kwani hawakuwa kakisalimiana.

Katika hadithi ya Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998), walieleza kuhusu maudhui ya utovu wa nidhamu. Watoto 20% (J, N, P na T) walisema kuwa wanawe Kuku walicheza na wembe kwa kujinyoa vibayavibaya na kurushiana na hata kuupoteza. Wawili ( J na N) walieleza kwamba hawapaswi kuwa na tabia mbaya kama za hawa vifaranga.

(60)

49

SURA YA TATU

UFASIRI WA WAHUSIKA KATIKA NGANO ZA KIFANTASIA 3.0 Utangulizi

Sura ya pili imeshughulikia ufasiri wa maudhui katika ngano za kifantasia. Lengo la pili la utafiti ni kuonyesha jinsi watoto wanavyofasiri wahusika katika ngano za kifantasia. Kwa hivyo, maoni ya watoto kuhusu wahusika mbalimbali yameainishwa na kuchanganuliwa. Katika kila ngano, ni wahusika wakuu pekee ndio walioshughulikiwa. Ili kuibuka na data, watoto waliwekwa katika vikao kisha hadithi zikasomwa kwa sauti, maoni yao yalikuwa majibu ya maswali yafuatayo:

Unampenda mnyama yupi? Kwa nini? Humpendi mnyama gani? Kwa nini?

Huck na wengineo (2001), wanaeleza kuwa watoto huonyesha kuwa wameelewa kazi ya kifasihi kwa njia mbalimbali. Wanaweza kutoa muhtasari wa hadithi inayohusika, kujibu maswali wanayoulizwa, kuandika kuhusu hadithi au hata kuchora na kutumia majina ya wahusika wanapocheza. Maoni ya watoto kuhusu wahusika katika hadithi wanazosoma huchangia katika kuwaadilisha na pia kuelewa watu wanaopatikana katika mazingira yao.

(61)

50

Kabla ya kushughulikia maoni ya watoto, ni muhimu kueleza dhana ya wahusika.

3.1 Dhana ya Wahusika

Wahusika ni viumbe mbalimbali au watendaji wanaopatikana katika kazi ya fasihi. Kuna aina mbalimbali za wahusika kama wahusika binadamu, wanyama au vifaa vilivyohaishwa. Stewig (1980) anaeleza kuwa kuwa wahusika binadamu (hekaya) na wahusika wanyama (hurafa) katika fasihi ya watoto.

Mwandishi huwa na lengo la kuwasilisha ujumbe fulani kwa wasomaji. Kupitia kwa wahusika msomaji anaweza kufahamu falsafa ya mwandishi kuhusu jambo fulani maishani. Wao huwa na sifa za kimaadili, kitabia, kiitikadi, kifalsafa ambazo hutambulishwa na wanayoyasema na wanayoyatenda (Wamitila, 2002). Wanaweza pia kutambulishwa na maelezo ya wahusika wengine au msimulizi.

Kazi mbalimbali huwa na aina tofauti tofauti ya wahusika. Kulingana na Finnegan (1970), wahusika huweza kuwa viumbe walio na uhai au vifaa visivyokuwa na uhai. Wahusika wa kifantasia ni kama wale wanyama wanaoweza kuongea. Pia, wanyama wanaoweza kubadili miundo yao au kujigeuza kutoka kwa binadamu wakawa wanyama ama miamba ni wa kifantasia. Vilevile, kuna wahusika wachawi, mazimwi au majitu.

(62)

51

Madsen (1976), anasema kuwa wahusika wanaweza kubuniwa na mwandishi au wakatolewa kwenye matukio ya kihistoria ya jamii fulani. Anatoa mifano ya wahusika wanyama, wachawi, mazimwi, mbilikimo na vichimbakazi. Baadhi ya wahusika katika ngano za kifantasia hutekeleza matendo yao kupitia kwa maajabu yanayotokana na vifaa mbalimbali. Vifaa hivi huwa vimejazwa nguvu na uwezo wa kiajabu ili kuweza kutenda matendo ya kiajabu. Vifaa hivyo vinaweza kuwa vioo, bakora, upanga, mkongojo au chochote kulingana na ubunifu wa mwandishi. Wahusika hawa huweza kupokea sifa zao kulingana na mwingiliano miongoni mwao au matendo yao katika mandhari ya kustaajabisha inayowazingira. Aidha, wahusika wa kihistoria wanaweza kuwa watu walioishi katika kipindi fulani cha kihistoria.

Hata hivyo, Wamitila (2008), anaeleza kwamba fasihi ya watoto hutumia wahusika wanyama kwa kiasi kikubwa. Wanyama hawa wanaingiliana na binadamu katika ulimwengu wa kibunifu kwa njia ya moja kwa moja kama inavyojitokeza katika ulimwengu wa fasihi simulizi. Maingiliano haya hata hivyo yanadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na mwonoulimwengu wa maisha ya binadamu, hivi kwamba wanyama wanafuata tabia za watu. Wanavaa, wanazungumza na wanatenda matendo ambayo kijumla yanahusishwa na watu bali si wanyama.

(63)

52

Wanapozungumzia ngano za kifantasia, Huck na wengineo (2001), wanaeleza kuwa kando na wanyama wanaoongea, watoto wanapenda wahusika kama vidude vya kuchezea kama mwanaserere vilivyohaishwa. Wale wa umri wa miaka 8 na 9 hudhani kuwa vidude hivyo vya kuchezea ni hai. Pia, watoto hao huamini kuwa wanyama na vidude vya kuchezea huwa na fikra kama za binadamu na wanaweza hata kuongea. Wakati mwingine mtoto anapocheza na vidude hivyo, huweza kuongea navyo, kuvilisha na hata kuviadhibu.

Bettelheim (1975), anaeleza kuwa wahusika wa kifantasia ni muhimu kwani mawazo na fikra za kifantasia zinazoibuliwa na wahusika hawa huchangia katika kukuza bongo zao. Mawazo na fikra hizi kuhusu wahusika hawa wa kiajabu humsaidia mtoto kujibu maswali mengi yanayozonga nafsi yake na kumtayarisha kukumbana na mambo mengi katika ulimwengu wake mpya.

3.2 Ufasiri wa Wahusika katika Ngano ya Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998)

Hadithi hii inawahusu wahusika wakuu wawili ambao ni Kuku na Mwewe. Wawili hawa walikuwa marafiki japo baadaye walibadilika na kuwa maadui. Baada ya kusoma ngano, watoto walijibu maswali waliyoulizwa kuhusu wahusika hawa wawili. Majibu yao yalichanganuliwa ili kubaini ikiwa waliweza kufasiri wahusika katika ngano za kifantasia.

3.2.1 Mama Mwewe

References

Related documents

In this study, we have extended the NEKL protein network to include the conserved ankyrin repeat proteins MLT-2 / ANKS6, MLT-3 /ANKS3, and MLT-4 /INVS.. Our data suggest that

Modelling stability analysis and control of a direct AC/AC matrix converter based systems MelakuMihretIEEE (2011) presented about direct and indirect space vector

Since most of the work related to traffic and transportation planning requires an effective framework for the analysis of the present and future travel demand pattern, a model

was  utilized  to  evaluate  professional  development  manuscripts,  collected  based  on  their   focus  of  professional  development  for  community

Our results show that, although tetrasomic inheritance creates additional con fi gurations of lineages that have unique probabilities of coalescence compared to those for

ABSTRACT : In this paper, Model based approach is implemented to control a heat exchanger prototype using optimization technique for parameter tuning of PID

The propulsion mechanism used is completely mechanical, if the electrical counterpart has to be provided, the system will have to rely on external source of

We therefore screened for gain-of-function enhancers of jing gain of function in the eye and identified the Drosophila homolog of the disease gene of human a