• No results found

Mtindo katika mashairi ya kiswahili: Aina na dhima ya kibwagizo tasnifu

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2020

Share "Mtindo katika mashairi ya kiswahili: Aina na dhima ya kibwagizo tasnifu"

Copied!
94
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

ksl,.?>,OOU

MTINDO KATlKA MASHAIRI YA KISW AHILI:

AINA NA DHIMA YA KIBWAGIZO

TASNIFU

YA

SARAH KAMBUA NYAMAI

TASNIFU HII

IMETOLEWA ILl KUTOSHELEZA BAADHI YA

MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATlKA IDARA YA

KISWAHILI, CHUO KIKUU CHA KENYATTA

2015

KENYATTA

UNIVERSITY LIBRARY

(2)

IKIRARI

Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika chuo kikuu kingine chochote

Sahihi ~: __: Tarehe

2-_4-JLQL_~Qr~~

_

SARAH KAMBUA NY AMAI

Tasnifu hii imetolewa kwa chuo kikuu kwa idhini yetu kama wasimamizi.

Sahihi .. .. .

Tarehe2'f/9~~.

DKT JOSEPH

n

MATARIA Idara ya Lugha na Isimu Chuo Kikuu Cha Karatina

Mw. ELIPHAS M. KAMUNDE

(3)

TABARUKU

Kwa mume wangu mpenzi, Stanley Nyamai Musyoka.

K wa watoto wangu wapendwa: Christine Mwende, Donald Musyoka, Emmaculate

Kavutha na Reuben Kongo. Kwenu: elimu ni mali.

(4)

SHUKRANI

Namshukuru Mungu aliyeniwezesha mpaka katika kiwango hiki. Kama si wewe Maulana singeweza kwa nguvu zangu mwenyewe. Aidha, nawashukuru kwa dhati ya moyo wangu wasimamizi wangu katika kazi hii: Dkt. Joseph N. Maitaria na Mwl. Eliphas M. Kamunde kwa ushauri, mwongozo wao wa busara na subira hadi nikafaulu na kuhitimu. Michango na maoni yao muhimu ndio yalinifanikisha na kuivisha kazi hii. Ningependa kuwashukuru wahadhiri wote wa idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika kwa ushauri na mwongozo kwa njia moja au nyingine. Ahsante.

(5)

IKISIRI

Utafiti huu umetathmini mtindo katika mashairi ya Kiswahili kwa kuzingatia dhima na aina ya kibwagizo. Mtafiti amechunguza mashairi yaliyowasilishwa kwa mitindo mbalimbali huku akitilia maanani mashairi ya Kiswahili yanayobainishwa katika matapo matatu: yale yanayozingatia mno arudhi za kimapokeo, yasiyozingatia mno arudhi (ya kati) na yale yasiyozingatia arudhi hizo (huru) ili kudhihirisha haya. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile yamtindo. Nadharia ya mtindo kwa jumla inazingatia matumizi ya lugha kwa kutathmini maana ya kijuujuu katika ruwaza ya sentensi au mfumo wa neno ili kubainisha au kufasiri maana fiche. Tasnifu hii imegawanyika katika sura tano: sura ya kwanza ni utangulizi ambapo mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada na upeo wa utafiti zimeshughulikiwa. Pia, udurusu wa maandishi yanayohusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti huu imejadiliwa. Sura ya pili imechanganua namna watunzi wa mashairi ya kimapokeo wanavyokitumia kibwagizo. Sura ya tatu imechanganua namna kibwagizo kinavyotumika katika mashairi ya kati ilhali sura ya nne imeshughulikia mashari huru ya Kiswahili. Sura ya tano ni hitimisho ambapo muhtasari na matokeo ya utafiti umeshughulikiwa pamoja na mapendekezo ya utafiti.

(6)

UFAFANUZI WA DHANA MUHIMU

Mashairi ya mapokeo - Mashairi ya jadi. Mashairi yanayozingatia urari wa vina na ulinganifu wa mizani kuleta uwiano.

Mashairi ya kati - Mashairi ambayo yanazingatia baadhi ya kaida za kiarudhi na pia kuhusisha mbinu zinazotumika katika uwasilishaji wa mashairi huru.

- Mashairi yasiyozingatia kaida za arudhi za kimapokeo katika uwasilishaji wake.

Mashairi huru

Kibwagizo - Mshororo wa mwisho wa kila ubeti ambao

(7)

YALIYOMO

IKIRARI ii

TABARUKU iii

SHUKRANI iv

IKISIRI v

UFAFANUZI WA DHANA MUHIMU vi

YALIYOMO vii

SURA YAKWANZA 1

Utangulizi 1

Swala la Utafiti 3

Maswali ya Utafiti 4

Sababu za Kuchagua Mada 4

Msingi wa Nadharia 5

Upeo na Mipaka ya Utafiti 11

Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 11

Mbinu za Utafiti 15

Uteuzi wa Data 15

Uteuzi wa Mashairi 16

Ukusanyaj i wa Data 16

Uchanganuzi wa Data 16

Uwasilishaj i wa Data 17

Kiishilio 17

SURA YA PILI 18

MASHAIRI YANAYOZINGATIA ARUDHI ZA KIMAPOKEO 18

2.0 Utangulizi 18

2.1 Shairi: Lipi Litakalokuwa 19

2.2 Shairi: Ukamilifu wa Mja 20

(8)

2.3 Shairi: Telezi 23

2.4 Shairi: Kamliwaze 27

2.5 Shairi: La Mjini Na La Shamba 29

2.6 Kiishilio 33

SURA YA TATU 34

MASHAIRI YAKATIYA KISWAHILI 34

3.0 Utangulizi 34

3.1 Shairi: Nikwambiye 35

3.2 Shairi: Jaribu Kunikukumbuka 39

3.4 Shairi: Anga 44

3.5 Shairi: Mimi Mtupu .47

3.6 Kiishilio 49

SURA YA NNE 51

MASHAIRI HURU YAKISWAHILI 51

4 .0 Utangulizi 51

4.1 Shairi: Jibwa 52

4.2 Shairi: Wazo Nje ya Wakati 55

4.3 Shairi: Bonde 58

I' 4.4 Shairi: Harusi 60

4.5 Shairi: Puuu! 63

4.6 Kiishilio 65

SURA YATANO 67

HITIMISHO LA UTAFITI 67

5.0 Utangulizi 67

5.1 Muhtasari 67

5.2 Matokeo ya Utafiti 69

(9)

MAREJELEO 73

FARAHASA 76

(10)

SURA Y A KWANZA 1.0 Utangulizi

Mashairi ni utanzu wa fasihi ambao hupatikana katika fasihi simulizi na andishi. Hutumiwa na watunzi wengi kujieleza na kuielezajamii wanayoiishi. Ubeti wa shairi la Kiswahili huwa na mshororo mmoja (tathmina), miwili (tathnia), mitatu (tathlitha), minne (tarbia), mitano (takhmisa), au zaidi. Kibwagizo hutumiwa kwa namna tofauti tofauti. ili kusisitiza wazo linaloelezwa na mshairi, hivyo, kinaweza kuwa kinaitikia ujumbe wa mshairi, kitafafanuliwa kwa namna kinavyoweza kusaidia katika kuibulia umbo, muundo, kuelekeza mtindo na ridhimu au maadhi katika ushairi wa Kiswahili. Kibwagizo kama istilahi ya kifasihi, kinafasiriwa kwa uelekezi wa dhima yake katika ushairi wa Kiswahili.

Kwa kuwa jamii ndiyo inayoibua na kuendeleza fasihi yake; inapobadilika, fasihi pia haina budi kubadilika. Kwa sababu chimbuko lake ni mazingira halisi ya jamii. Kwa kuzingatia mabadiliko hayo, mshairi hutunga tungo zake kulingana na wakati. Haya yanadhihirika katika mashairi ya watunzi wa nyakati mbalimbali yakiwemo mashairi ya

kimapokeo (yanayozingatia zaidi arudhi), ya kati (yanayozingatia kwa kiasi arudhi) na

I' mashairi huru (yasiyozingatia kabisa arudhi za kimapokeo). Baadhi ya majukumu ya ushairi wa Kiswahili kama utanzu wa fasihi ni kutumbuiza, kufurahisha, kuadilisha, kuekeza na kuhifadhi utamaduni wajamii, kuonya na kutoa mawaidha.

(11)

wameeleza hisi, matarajio na mahitaji ya jamii zao katika nyakati tofauti kwa kutumika

mitindo tofauti. Kutokana na historia ndefu ya ushairi kuna mabadiliko toka kipindi kimoja hadi kingine. Kuna ushairi wa kimapokeo ambao huzingatia arudhi wa kati, ambao umechanganya utunzi wa mashairi ya kimapokeo na huru, nayo mashairi huru hayafuati kabisa urari wa vina na mizani.

Wanamapokeo wanashikilia urari wa vina na mizani kuwa uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili. Baadhi ya watunzi hao ni K. A Abedi, S. Chiraghdin, J. M Mayoka, S. A. Kandoro, A. Abdallah, A. Snowhite, S. Robert na A. Gibbe (Maitaria 2012). Ushairi wa

kati hauzingatii sana arudhi za mapokeo. Baadhi ya mashairi ya 'kati' yamejumuisha kwa kiasi arudhi; urari wa vina, ilhali mengine hayaufuati urari huu wa vina. Mashairi ya kati, ya washairi kama S. A. Mohamed na A. Mazrui, yanadhihirisha kunga na fani zinazozingatiwa katika mashairi ya mapokeo na huru. Ushairi huru hauzingatii kabisa arudhi za kimapokeo, ingawa huwa na taratibu zake kwa kiasi. Watunzi katika Wakati huu wanaeleza kwamba si lazima shairi liwe linajibanisha katika vina au urari wa mizani ndipo liitwe shairi. Kwamba, shairi halipaswi kuwa na umbo maalum lisilobadilika milele. Baadhi ya watunzi watajika katika mlengo huu ni E. Kezilahabi, K. K. Kahigi na M. M. Mulokozi, E. Hussein, K. wa Mberia na K. wa Mutiso.

Mtunzi wa shairi huratibu na hueleza mawazo yake katika mishororo ambayo huashiriwa kwa majina maalum na hutofautiana kutika aina moja ya shairi hadi nyingine.

Kibwagizo kama mshororo wa mwisho katika mashairi ya kimapokeo hufuata urari wa vina na mizani. Mashairi ya mapokeo hutungwa kwa kuzingatia mpangilio maalum wa beti, idadi fulani ya silabi au mizani, ukamilifu au upatanifu wa vina na mizani. Huwa na idadi maalum ya mishororo kila ubeti inayogawika kwenye vipande. Urari wa vina na

2

KENYATTA UN\VERStTY

L~ERAR'f

(12)

mizani ulioko katika kila mshororo huonekana pia katika kibwagizo. Mashairi kati yamechanganya uzingativu wa urari wa vina na mizani katika utunzi wake huku kwa mengine ule urari wa vina na mizani unaopatikana haupo kabisa. Kibwagizo cha mashairi ya kati hivyo basi wakati mwingine kitazingatia urari wa vina na mizani kama mishororo iliyokitangulia kibwagizo hicho. Endapo mishororo ya awali katika shairi la kati halijazingatia urari wa vina na idadi ya mizani; kibwagizo kitafuata mtindo huo huo

na hakitakuwa na urari wa vina na mizani. Mashairi huru hayana urari wa vina na mizani.

Mizani za mshororo zinaweza kutoshana na zile za kibwagizo; kama ni mizani kumi na katika mishororo ya awali ikawa vivyo hivyo katika kibwagizo. Vilevile kina cha mwisho kinaweza kubadilika na kuja kati au cha kati kwenda mwisho. Kibwagizo kinaweza kuwa ama na kina kimoja tu cha ubeti au kiwe na vina vya namna ya peke

yake au kifuate mpango ule ule wa vina vya mistari mingine. Kutokana na hali hizi tofautitofauti za kibwagizo na mashairi yenyewe; ya kimapokeo, ya kati na huru, basi hiki ndicho kimekuwa kiini cha utafiti huu; kuonyesha vile mashairi ya kimapokeo ya

kati na huru yalivyotumia kibwagizo kuwasilisha ujumbe katika utunzi wao. Utafiti huu umebainisha mtindo anuwai katika mashairi ya Kiswahili kwa kuzingatia aina na dhima ya kibwagizo katika mashairi haya.

1.1 Swala la Utafiti

Utunzi na uwasilishaji wa ushairi ya Kiswahili huzingatia matumizi ya maneno ambayo

(13)

kimapokeo. Matumizi ya kibwagizo si wazi katika ushairi usiozingatia kaida za arudhi. Kimetumika kwa njia na dhima mbalimbali katika kuhitimisha ubeti wa shairi la Kiswahili. Baadhi ya watunzi hueleza kuwa kibwagizo hutumika kudhihirisha dhamira au maudhui ya mshairi. Utafiti huu umeainisha na kuchanganua mashairi ya kimapokeo, ya kati na mashairi huru kuonyesha kuwa kibwagizo kimetumika sio tu kuupitisha ujumbe au kuutilia mkazo bali pia kulipamba shairi la Kiswahili. Watunzi katika enzi

hizi tatu wametumia uhuru wa kuchagua mitindo tofauti katika mashairi yao ili kudhihirisha namna kibwagizo kinavyoweza kusaidia katika kuibulia umbo na muundo kuieleza mtindo na maadhi katika ushairi wa Kiswahili. Aidha, utafiti huu umebainisha matumizi ya kibwagizo katika uainishaji zaidi wa mashairi ya Kiswahili.

1.2 Maswali ya Utafiti

Utafiti huu umelenga kujibu swali lifuatalo:

a) Kibwagizo huwa na dhima gani katika mashairi ya Kiswahili?

1.3 Malengo yaUtafiti

a) Kubainisha kuwa mtindo katika kibwagizo cha mashairi ya Kiswahili hutegemea watunzi na nyakati mbalimbali

b) Kueleza namna kibwagizo kimeweza kutumika katika mashairi ya kimapokeo, ya kati na huru.

c) kutathmini umuhimu wa kibwagizo katika ubeti wa shairi la Kiswahili.

1.4 Sababu za Kuchagua Mada

Ushairi wa Kiswahili umekuwa ukitumia kibwagizo kama kiungo muhimu katika utunzi. Kibwagizo kama mshororo katika ubeti wa shairi ni muhimu katika utunzi na

(14)

uwasilishaji mashairi ya Kiswahili. Baadhi ya wahakiki hueleza kuwa kibwagizo

hutumika na mtunzi katika kutolea maudhui na ujumbe wake. Mwelekeo huu

haujabainisha dhima ya kibwagizo katika mashairi ya Kiswahili hasa kwa kuzingatia

mtindo wa shairi lenyewe. Hivyo, ni muhimu kufanya utafiti kudhihirisha dhima ya kibwagizo kwa kuzingatia mtindo katika mashairi ya Kiswahili.

Pili, utanzu wa ushairi una historia ndefu iliyojikitia kuwili: fasihi simulizi za jamii

zilizohusika. Kutokana na hali hii ni hapana budi kuwepo na mabadiliko fulani ya

kiuwasilishaji toka kipindi kimoja hadi kingine. Baadhi ya mabadiliko hayo ni ushairi

huru. Utafiti huu umebaini jinsi kibwagizo kimeathirika katika utunzi wa rnashairi ya kimapokeo, ya kati na huru.

Tatu, kibwagizo hutumiwa na watunzi kwa nj ia tofauti. Mizani au silabi za mishororo

mingine ya shairi inaweza lingana na kuwa na mshabaha na ile ya kibwagizo. Katika

shairi, kina cha mwiisho cha kibwagizo kinaweza kubadilika na kuja kati ilhali cha kati

huenda mwisho. Kimalizio huwa na mizani michache kuliko ilivyo mishororo

iliyotangulia. Kwa hivyo, utafiti huu umebaini dhima ya kibwagizo na vile kimetumika

katika mashairi ya kimapokeo, ya kati na huru.

1.5 Msingi wa Nadharia

Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ile ya mtindo. Mwasisi wa nadharia hii ni

Buffon (1930) anadai kwamba, mtindo ni mtu mwenyewe, yaani jinsi mtu anavyotumia

lugha kupitisha ujumbe wake. Anasema kuwa kazi ya fasihi hudumu kupitia mtindo

wake na mtindo huo ni mtu mwenyewe. Maoni ya Buffon (keshatajwa), ni kuwa mtindo

(15)

kuita kazi ya mtunzi fulani rntindo wake. Kwa mfano, tunaposema mtindo wa M. S

Mohamed, tuna maana kuwa ametumia lugha yake. Nadharia ya mtindo kwa jumla

inazingatia matumizi ya lugha kwa kutathmini maana ya kijuujuu ya sentensi au neno iIi

kubainisha au kufasiri maana fiche.

Kwa majibu wa Coombes (1953) i1i kuchanganua mtindo katika kazi ya fasihi

inavyowasilishwa, ni muhimu kuzingatia miundo na vipengele vya lugha vinavyofanya

ivutie. Coombes anazingatia vigezo kama vile matumizi ya taswira, wazo la kishairi,

hisia zilizoibuliwa, uteuzi wa maneno, urari wa vina na mahadhi ya shairi. Lengo la

kimtindo anavyodai Leech (1969), ni kuchunguza lugha na kanuni zake ili kubainisha

mbinu na vipengele vinavyotengewa kazi fulani ya jamii.

Crystal na Davy (1969) wanafafanua mtindo kwa njia nne kuu; kwanza wanasema

kwamba mtindo ni tabia ya mtu kuhusu matumizi yake ya lugha yaani namna mtu

anavyotumia lugha kuwasilisha ujumbe wake. Wanaendelea kudai kuwa mtindo ni tabia

ya mtu binafsi kuhusu matumizi yake ya lugha ambayo hudhihirisha hulka na upekee

wake wakutumia lugha. Kwa hivyo, Crystal na Davy wanakubaliana, kwa kiwango

fulani na Buffon ambaye ana maoni kuwa, mtindo ni mtu mwenyewe, yaani jinsi

anavyoitumia lugha kupitisha ujumbe wake na ndiye alikuwa mwasisi wa nadharia hii.

Wanaeleza mtindo kumaanisha mashairi ya namna jamii au kikundi fulani cha watu

wanavyotumia lugha katika kipindi fulani. Kwa mfano, mtindo wa mashairi wa

"kishujaa" wa Kiingereza cha zamani. Hapa, jinsi tunavyochukua hali pana kwa ujumla

ndivyo tutakavyokuwa waangalifu zaidi kueleza hali ya wanaoshiriki ile lugha.

Wanaeleza mtindo kama tabia ya kuyaeleza mambo, hii inadhihirika katika maelezo ya

(16)

mtindo kama kusema kinachofaa kwa njia mwafaka au kama tabia isiyofaa yaani

matumizi mwafaka katika mazingira fulani. Kwa mfano tunaposema mtindo

uliostaarabika au ulio angavu zaidi. Madai yao ni kwamba, mtindo umekuwa ukihusishwa na fasihi kama maandishi mazuri, yenye sifa bora na yenye urembo au

maandishi yaliyopambwa.

Kulingana na Leech (1969), kazi ya fasihi hukusudia kuwasilisha hisi au tajriba kwa

wasomaji au wasikilizaji. Anaeleza kuwa nadharia hii ina vigezo vinavyotumika

kuchambua kazi za kisanaa kwa kuangalia mitindo ya mwandishi. Kuhusu lugha, Leech

anaeleza kuwa mshairi hutumia lugha 'kiajabu' na athari za ufumi haziwezi

kutenganishwa na matumizi ya lugha kisanaa. Kadhalika, Senkoro (1982) amesisitiza

kwamba ushairi ni utanzu wa fasihi unaotumia mpangilio wa lugha mkato, ya picha, na

yenye mapingo mahususi. Kwa hivyo, vigezo vinavyotumiwa kuchangulia na kubainisha

shairi ni umbo lake pamoja na matumizi ya lugha. Anaendelea kueleza kwamba ushairi

hutumia lugha ya mkato yenye kuendeleza maudhui yake kimuhtasari, ambayo aghalabu

huwa katika kibwagizo. Nadharia hii imemsaidia mtafiti kuchambua aina ya lugha

iliyotumika katika vibwagizo vya mashairi ya kimapokeo, ya kati na huru, ili mtunzi

ajieleze mwenyewe na kuiathiri hadhira yake.

Maoni ya Lodge (1981) ni kuwa, mtindo ni jinsi ya kuj ieleza kwa hadhira au wapokezi

wa ujumbe. Anayachangia maoni ya Buffon (keshatajwa), kuwa mtindo ni jinsi mtu

anavyoitumia lugha kupitisha ujumbe. Lodge ana maoni kuwa mwasilishaji huvyaza

kwa usanii kauli zinazopatikana katika mawasiliano ya Jamii ili kuubulia maana fiche.

,

Kauli ya lugha zinazotumika husaidia kujenga taswira ya kimawazo ambayo huweza

kufasiriwa moja kwa moja au kwa njia ya kiistiari. Ngara (1982) akichangia kuhusu

7

I/Chlyfl.TTA

l

'

t

\II\/f-

f

'

{'! 't· I

LIQR

'

\

h;'" "

(17)

lugha anaeleza kwamba matumizi ya lugha katika kazi ya sanaa ni njia moja ya kuvuta

hisi za hadhira. Kwa hivyo tumechambua muundo wa lugha katika kujenga na kutoa

ujumbe wa mtunzi.

Masinde (1992) anaendeleza maoni ya Buffon (keshatajwa), kwa kusema kuwa mtindo

ni jinsi msanii hutunga kazi na kuipa sura fulani kifani na kimaudhui kwa lugha ambayo

inaibusha kwa uzuri zaidi ujumbe anaotaka kuutoa. Mtindo ndio utofautishao mashairi

ya mapokeo, ya kati na huru. Shairi hupata maana na umuhimu wake sio kutokana na

umbo lake lanje tu bali pia matumizi ya lugha katika kujenga dhamira ya mtunzi.

Mtazamo wa Leech (keshatajwa) ni kuwa, tunapozungumzia mtindo, tunamrejelea

mwandishi fulani katika akili zetu nawakati fulani. Anaendelea kusema kuwa uelewa wa

shairi lolote unaweza kuathiriwa na ujuzi na uzoevu wa mashairi mengine na mwandishi

huyo huyo. Lugha inayotumika ikilinganishwa na ya kawaida; kwanza inaweza kukiuka

njia za kawaida za kutumika lugha. Pili, mtunzi na hasa wa shairi ana uhuru kati ya

watumiaji wa lugha kuitumia lugha bila uzingatifu wa kijamii au kihistoria wa watumizi

hao wa lugha. Mtunzi wa mashairi anaweza kutumia lugha ya kale au kuomba sifa za

wengine. Tatu, mengi yanayoonekana kama utabia ya lugha fulani yana misingi yake

~

katika matumizi ya kila siku ya lugha na yanaweza kuchunguzwa kwa kuzingatia

matumizi haya. Uchambuzi wa lugha ndio unaodhihirisha sifa za ndani za shairi na

kuonyesha kuwa upekee wa shairi umo katika kunga za lugha zilizotumiwa. Madai haya

ya Leech yanaafikiana na ya mwasisi Buffon kuwa lugha ni mtu mwenyewe.

Njogu na Chimera (1999) wanadai kuwa mtindo ni ufundi wa kupanga kupangua. Ni

ujuzi wa kujieleza. Wanasema mtindo unatofautisha mtunzi mmoja na mwingine. Mbatia

(18)

(2001) ana maoni kuwa, mtindo ni jinsi mtunzi wa kazi ya kisanaa anavyotumia lugha

katika kujieleza. Mtindo kulingana na Wamitila (2010) huwa ni sifa, fani au miundo

ambazo hubainisha kazi fulani maalum au kazi za mtunzi maalum, jinsi mwandishi

fulani anavyojieleza katika kazi yake. Hata hivyo, inawezekana pia kukawa na mtindo

wa wakati fulani au hata eneo fulani. Nadharia hii inajikita kwenye uchanganuzi wa

lugha kwa kiasi kikubwa. Uchunguzi huu wa lugha unapania kubainisha ubunifu uliopo

kwenye lugha hiyo na kwa kuutekeleza kwa undani, unasaidia katika uelewekaji wa

shairi.

Wanamtindo husisitiza umuhimu wa lugha kama chombo tekelezi kinachosaidia katika

kuelewa ujumbe au maudhui yaliyokusudiwa. Kutokana na mtindo wa kazi ya fasihi,

inakuwa vigumu kubadili sentensi au hata neno katika kazi hiyo bila kubadili mtindo

wenyewe. Nadharia hii husisitiza uwiano kati ya ujumbe na lugha. Ina misingi katika

dhana kwamba lugha huchangia ufanisi wa kazi ya sanaa kwani hutumiwa katika uzuaji

na ubunifu wa kifasihi.

Nadharia ya mtindo inalenga matumizi ya lugha katika kuibusha dhamira za mwandishi

katika uwasilishaji wake. Kwa maana hii dhamira za mwandishi haziwezi kueleweka I'

bila lugha. Jinsi mwandishi atumiavyo lugha husaidia kutoa dhamira yake kwa wasomaji

au wasikilizaji. Hivyo, lugha huwa ndicho chombo muhimu cha mawasiliano katika

jamii. Kwa mujibu wa nadharia hii, uchunguzi wa matumizi ya lugha lazima uchunguze

vile maudhui yamewiana na matumizi ya lugha, kwa hivyo huwezi kutenganisha lugha

na maudhui na ukaelewa ujumbe wa mtunzi. Hivyo basi nadharia hii itatuongoza

kudhihirisha vile mtindo wa mtunzi na lugha yake hujengana na kuwiana katika kuibua

(19)

yale ya wanamabadiliko. Shairi hupata maana na umuhimu wake sio kutokana na umbo

lake la nje bali pia matumizi ya lugha katika kuibua dhima ya mtunzi.

Uchanganuzi wa lugha ndio unaodhihirisha sifa za ndani za shairi na kuonyesha upekee

wake katika kunga za lugha zilizotumika. Katika kuchambua mtindo uliotumika na

watunzi wa mashairi ya kimapokeo, ya kati na mashairi huru tumeona kuwa lugha

hutumiwa na mtunzi kupata kibwagizo cha aina yake na kwa dhima tofauti. Nadharia ya

mtindo imetuongoza kuchambua kibwagizo katika mashairi ya kimapokeo, ya kati na

huru hasa katika ufundi wa kimtindo wa kupanga na kupangua kulingana na watunzi na

nyakati mbalimbali. Imetuongoza kuona hisi au tajriba zinazowasilishwa kwa hadhira

kupitia kwa lugha ya mkato, ya picha na yenye mapigo mahsusi. Katika muktadha huu,

nadharia hii imetuongoza kuchambua mtindo ili kudhihirisha dhima katika kibwagizo

cha mashairi ya Kiswahili.

Mihimili ifuatayo ndiyo imeuongoza utafiti huu:

a) Maudhui na dhamira hushughulikia falsafa ya mtunzi kuhusu jamii anayozungumzia.

b) Muundo wa kazi za kubuni ndio huudhibiti ujumbe unaowasilishwa.

I' c) Umbo na mpango wa kazi huipa kazi ya fasihi sura maalum.

d) Uwasilishaji wa mawazo hutegemea lugha ya kimafumbo iliyotumika katika harakati

za uwasilishaji wa ujumbe na picha kukidhi haja za umbo katika utanzu

unaowasilishwa.

Mihimili hii imetuongoza kuichambua mitindo ya watunzi wa mashairi ya kimapokeo,

ya kati na mashairi huru ili kudhihirisha aina ya kibwagizo na dhima ya kibwagizo

chenyewe katika mashairi ya Kiswahili. Aidha, imetuongoza kudhihirisha kuwa shairi ni

(20)

umbo, na mpango wa kazi ya fasihi yenye uwasilishaji wa mawazo wa kimafumbo

kutegemea kauli teule za mtunzi.

1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti

Utafiti huu umeshughulikia mashairi kumi na matano kutoka kwa Diwani tatu za

washairi wasifika wa Kiswahili. Mashairi hayo yanapatikana katika: Sauti ya Dhiki ya

Abdilatif Abdalla (1973), Jicho la Ndani ya Said A. Mohamed (2002) na Dhifa ya E.

Kezilahabi (2008). Kutoka kila diwani mashairi matano yamechanganuliwa. Mashairi

hayo yamechanguliwa kwa makusudi. Mashairi kutoka Sauti ya Dhiki ni ya kimapokeo,

ni yale yanayozingatia kanuni za kiarudhi. Mashairi katika Jicho La Ndani ni ya kati,

haya yamechanganya ufuasi wa kaida za kiarudhi za utunzi na mengine yasiyofuata

kaida hizo kabisa. Katika Dhifa ni mashairi huru. Haya kabisa hayazingatii kaida za

kiarudhi. Mashairi haya yana aina tofauti za kibwagizo kilichotumika. Utafiti huu

umebaini jinsi watunzi tofauti walivyotumia mitindo tofauti katika mishororo ya shairi

na hasa katika kibwagizo kubainisha dhima ya shairi.

1.7 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada

I' Utafiti mchache umefanywa kuhusu aina na dhima za kibwagizo cha mashairi ya

Kiswahili. Abedi (1954) anayo maoni kuwa desturi iliyoenea ni kukifanya kituo kuwa

kiini cha habari na kukileta mwisho wa kila ubeti bila kubadilisha maneno yake. Katika

muktadha huu maelezo yake ni kuwa yanayoelezwa yanatimia katika mistari mitatu na

wa nne, ulio ni kituo, unakariri kiini cha madhumuni ile. Hiyo mistari ya kwanza

inajenga dibaji au utangulizi kuhusu kiini hicho. Aidha, kibwagizo hubadilika kutoka

(21)

kinachotosheleza ubeti ule kinaoupamba. Ameeleza kwa ujumla aina za vibwagizo na

majina yake. Maoni ya Abedi yametufaa katika utafiti huu.

Mtindo wa shairi ni tabia pekee ya utunzi au uandishi na hutofautiana kutoka mtunzi

mmoja hadi mwingine (Leech 1969). Jambo hili hutegemea ufundi, hisia na unafsi wa

mtunzi. Mtindo haufundishiki bali hutokana na uwezo, mazoea na vitabia pekee vya

mtunzi. Rata hivyo, kazi zilizoshughulikia ushairi ni nyingi nazo ni pamoja na Topan

(1973) anayeuchambua ushairi huru, anaunga mkono maoni ya Kezilahabi kwamba, vina

na mizani ni muhimu ila cha kuzingatia ni kuwa shairi liwasilishe ukweli fulani wa

maisha. Ana maoni kuwa hadhi ya ushairi haitegemei muundo au umbo fulani, bali yale

yasemwayo najinsi yasemwavyo. Anaeleza kwamba, mawazo huletwa na mazingira na

mtu huchagua fani inayoambatana na uwezo wake. Topan (keshatajwa) hajashughulikia

kibwagizo kwa hivyo utafiti wake ni tofauti na wetu.

Kahigi (1975) aneleza kwamba mashairi ya Kiswahili yanafaa kutazamwa kisayansi.

Mtazamo huu ni wa kihalisi ambao huangalia historia nzima ya ushairi kwa jumla

ukiihusisha na mabadiliko ya mfumo wa jamii na kuzingatia dhamira na maendeleo

I' yake. Mtazamo huu hukiangalia kitu kilivyo katika maisha, kama sehemu ya

mchangamano wa mambo mengi katika maumbile na kama kitu kinachobadilika kila

wakati hutegemea mazingira ambayo yamekizunguka. Maoni hayo yamemsaidia sana

mtafiti kuhusu aina na dhima za kibwagizo cha mashairi ya Kiswahili.

Diwani ya Sauti ya Dhiki kwa upande wa maudhui, muundo na matumizi ya lugha

imechunguzwa na Matteru (1975). Utafiti wetu ni tofauti na wa Matteru kwani

umezingatia kibwagizo katika mashairi ya kimapokeo, kati na huru ilhali yeye alizingatia

(22)

ushairi huru. Chacha (1980) amehakiki ushairi wa Abdilatif katika kiwango cha

maudhui, akizingatia Sauti ya Dhiki na UtenziwaHawaa. Utafiti wake ni tofauti na wetu

kwani umejikita katika kibwagizo. Kahigi na Mulokozi (1982) wanaeleza kuwa miundo

mipya katika ushairi wa Kiswahili ni nyongeza ya ile iliyopo na inabeba maudhui ya

kileo. Wanasisitiza kwamba hali ya kushikilia vina na mizani inapingana kimsingi na

kanuni ya sanaa ya umbuji. Wanaeleza kwamba kanuni kuu katika utunzi wa mashairi ni

uwiano kati ya fani na maudhui na kilele chake hudhihirika katika kibwagizo cha

mashairi ya Kiswahili.

Baadhi ya mashairi ya waandishi mbalimbali yamehakikiwa na Senkoro (1988)

akiongozwa na nadharia ya umaksi. Ameshughulikia taswira katika Sauti ya Dhiki

tofauti na utafiti wetu ulioshughulikia vibwagizo vya mashairi ya Kiswahili. Masinde

(1992), ameshughulikia dhamira na mtindo katika mashairi huru. Anasema kuwa

mashairi hutungwa kama sanaa na hutumia lugha yenye kuvutia fikra kama mashairi ya

wanajadi, hata kama hayazingatii arudhi za ushairi wa mapokeo. Utafiti wake unajaribu

kudhihirisha mgogoro uliokita mizizi baina ya watunzi wa jadi na wale wa kisasa.

Hajajihusisha na kibwagizo cha mashairi hayo. Hii iliipa kazi hii nguvu kwamba haja ipo

ya utafiti zaidi kufanywa kwa kuzingatia aina ya kibwagizo na dhima yake katika I'

mashairi ya Kiswahili.

Kutokana na historia ndefu ya ushairi hapana budi kuwepo na mabadiliko fulani toka

kipindi kimoja hadi kingine (Kuvuna S. M. na Maliachi P. A 1992). Wanaendelea kutoa

maoni kuwa baadhi ya mabadiliko ambayo yamechimbuka katika ushairi ni hali ya kuwa

na mashairi huru (zohali) ambayo hayafuati kanuni za kimsingi ambazo washairi wa

(23)

yametufaa katika kuyachunguza mashairi huru yanayotokana na mabadiliko ya kielimu,kisiasa na kijamii.

Kibwagizo kinaweza kuwa kipande tu kinachorudiwarudiwa katika mshororo wa mwisho wa kila ubeti katika shairi nzima (King'ei na Kemoli 2001). Wana madai kuwa sifa muhimu ya mashairi ya tarbia za kijadi ni kuwa na kibwagizo. Wanaeleza umuhimu wa kibwagizo katika shairi, aidha wanatoa maelezo juu ya vibwagizo. Maoni haya ya King'ei na Kemoli yametufaa katika kukichunguza aina ya kibwagizo na dhima yake katika mashairi ya Kiswahili.

Nyanchama (2004) amefafanua matumizi ya taswira na ishara katika Sauti ya Dhiki, ambayo inashughulikia mashairi ya kimapokeo. Utafiti wake ni tofauti na yale

yaliyozingatiwa katika utafiti huu ambao urnelenga kibwagizo cha mashairi ya kimapokeo, ya kati na huru. Babusa (2005) amechunguza vigezo mbadala vya kubainisha mashairi ya kiswahili ili kuepuka mgogoro kati ya wanajadi na wanausasa. Baadhi ya vigezo alivyozingatia ni maudhui, fani, idadi ya mishororo miongoni mwa vigezo vinginevyo. Tofauti kati ya kazi hizi mbili ni kuwa utafiti wa Babusa unashughulikia kuepuka mgogoro kati ya wanajadi na wanausasa ambapo utafiti huu I'

umeshughulikia aina na dhima za kibwagizo katika mashairi ya Kiswahili.

Mulandi (2007) amechunguza matumizi ya usambamba katika mashairi huru. Anajaribu kuonyesha namna mshairi wa kisasa anavyotumia uhuru wake wa utunzi katika kujadili maswali mbalimbali yanayoikumba jamii. Utafiti wake ni tofauti na huu unaochunguza aina na dhima ya kibwagizo katika mashairi ya Kiswahili. Khatib M. S. (2011) mwandishi wa diwani ya Wasakatonge anasema kuwa, hajafungwa na mawazo ya

(24)

kimuhafidhina ya kung'ang'ania dhana kuwa ulimbwende wa mashairi ya Kiswahili

umo katika kupanga vina, mizani na kukamilisha urari wa beti za tarbia na takmisa. Sana

yoyote ile ina uhai, inakua na kubadilika. Maoni haya ya Khatib yametufaa sana katika

uchunguzi wetu wa aina na dhima za vibwagizo has a kuyahusu mashairi huru.

Utafiti huu umechunguza mtindo katika mashairi ya Kiswahili. Tumezingatia aina na

dhima ya kibwagizo kwa sababu ni kipengee ambacho hakijashughulikiwa kwa kina

zaidi. Aidha tumechanganua mitindo mbalimbali ya kibwagizo kama kinavyotumiwa na

watunzi mbalimbali wa mashairi ya kimapokeo, ya kati na huru katika kuupitishia

ujumbe wake. Walioshughulikia mashairi hawajashughulikia mtindo wa mashairi ya

Kiswahili kwa kuzingatia aina na dhima ya kibwagizo kama mshororo maalum katika

mashairi hayo. Wahakiki walioshughulikia mashairi wamefanya hivyo kwa mikabala

tofauti na tuliyotumia katika utafiti huu.

1.8 Mbinu za Utafiti

Utafiti huu umejikita katika mbinu tatu ambazo m usomaji na udurusu maktabani,

upekuzi mtandaoni na mahojiano.

1.8.1 Uteuzi wa Data

Data iliyoongoza utafiti huu ni mashairi ambayo yamehifadhiwa katika vitabu teule

vinavyopatikana maktabani. Usomaji wa vitabu, majarida, tafiti na makala. Nyanjani

tumewahoji wataalamu na watunzi wa mashairi ya Kiswahili ili kupata maoni yao

kuhusu suala hili. Kutoka kwa mtandao tumepata maoni na mawaidha ya watunzi wa

mashairi na wataalamu kwajumla. Maoni haya yamekuwa ya manufaa sana katika utafiti

huu. Data Imekusanywa kwa kuzingatia mada na malengo ya utafiti huku tukiongozwa

(25)

1.8.2 Uteuzi wa Mashairi

Katika utafiti wetu kwa jumla tuliteua mashairi kumi na matano kutoka diwani tatu:

Ambazo ni Sauti ya Dhiki, Jicha fa Ndani na Dhifa. Kutoka Sauti ya Dhiki

tumechunguza mashairi yanayozingatia kaida za arudhi katika utunzi. Mashairi haya ni

ya kimapokeo. Kutoka Jicha fa Ndani tumechunguza mchanganyiko wa mashairi ya

kimapokeo, yanayozingatia kaida za arudhi, na mashairi huru, yasiyozingatia kaida za

arudhi. Kutoka Dhifa tumechunguza mashairi huru yasiyozingatia kaida za arudhi za

kimapokeo. Sababu ya kuyachagua mashairi haya ni kuwa yana kibwagizo

kinachobadilikabadilika na kuwa kina dhima tofauti katika kila shairi.

1.8.3 Ukusanyaji waData

Data iliyotumiwa katika utafiti huu ilitokana na kazi zilizochapishwa hususa diwani za

mashairi, vitabu na machapisho mengine kutoka maktabani hasa za Chuo Kikuu cha

Kenyatta. Aidha, mahojiano na wataalamu na watunzi wa mashairi ya Kiswahili na

mtandao.

a) Mbinu ambayo imetumika sana OJ usomaji wa maktabani-ambapo mtafiti

amepitia vitabu teule vya mashairi na mtandao.

b) Mbinu ya mahojiano-imetumiwa na mtafiti kuwahoji wataalam wa fasihi na

lugha aidha watunzi wa mashairi wenye tajriba tofauti za utunzi kama vile;

mtunzi wa mashairi ya kimapokeo na mtunzi wa mashairi huru.

1.8.4 Uchanganuzi waData

Katika mashairi yote tuliyoyateua, tumechunguza mstari wa mwisho wa kila ubeti katika

shairi unaorudiwa katika kila ubeti katika shairi. Kibwagizo ni mshororo au mstari

unaobeba ujumbe muhimu katika shairi. Tasnifu hii imechunguza mshororo huu ambao

16

(26)

tumeuita kibwagizo katika mashairi yenye mitindo mbalimbali ili kubaini aina na dhima

za vibwagizo katika mashairi ya Kiswahili. Mashairi haya ni ya kimapokeo, ya kati na huru.

1.8.5 Uwasilishaji wa Data

Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia sura

mbalimbali.Sura ya kwanza imetoa maelezo kuhusu swala la utafiti, malengo ya utafiti,

nadharia na mbinu za utafiti zilizotumika. Sura ya pili imeshughulikia mashairi ya

kimapokeo na jinsi kibwagizo kimetumiwa na watunzi mbalimbali kama mbinu ya

kimtindo. Sura ya tatu imeshughulikia mashairi ya kati na vile kibwagizo kimetumika

katika mashairi haya kama mbinu ya kimtindo. Sura ya nne imeshughulikia mashairi

huru na matumizi ya kibwagizo katika mashairi haya kama mbinu ya kimtindo

1.9 Kiishilio

Sura hii imejadili mambo ya kimsingi kuhusiana na utafiti. Haya ni pamoja na ufafanuzi

wa istilahi muhimu, swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada.

Pia, imeshughulikia misingi ya nadharia, upeo na mipaka na yaliyoandikwa kuhusu

mada. Hatimaye tumeshughulikia mbinu za utafiti, uteuzi wa data na uwasilishaji wa

"

(27)

SURA YAPILI

MASHAIRI YANAYOZINGATIA ARUDHI ZA KIMAPOKEO

2.0 Utangulizi

Sura hii imechambua mashairi ya kimapokeo mbalimbali kutoka Sauti ya Dhiki ya

Abdilatif Abdalla. Mashairi yatakayochambuliwa ni 'Kamliwaze' (uk.5), 'Ukamilifu Wa

Mja' (uk. 12), 'TeLezi' (uk.24), 'Lipi litakalokuwa' (uk.35) na 'La Mjini Na La Shamba'

(uk.74). Mashairi haya yanafuata kikamiiifu vigezo vya kiarudhi. Vigezo hivi ni

vipande, mizani, mishororo, vina beti na vituo. Ni mashairi ambayo hayajaathiriwa na

utamaduni wa kigeni. Mashairi haya yana mawazo yanayowasilishwa katika muktadha

wa wenyeji na yameambatana na nyimbo za kienyeji kwajumla. Mengi ya mashairi ya

kimapokeo kulingana na Wallah (1988:xxvii) ni yale ya tarbia ambayo huwa na

mishororo minne katika kila ubeti, ambayo pia huitwa unne. Hivyo, huwasilishwa kwa

mtindo uliozoeleka katika jamii. Hata hivyo, mashairi haya huwasilishwa kwa miundo

mbalimbali. Tofauti hizi za miundo zinatokana na mpangiiio wa vina. Aghalabu, tungo

nyingi za ushairi wa Kiswahili ambazo huwasilishwa kwa kuzingatia arudhi za

kimapokeo: zimekuwa zikitumia kibwagizo kama kipengele cha kimtindo katika kukidhi

mahitaji ya kiutunzi na uwasilishaji. Kibwagizo kama mshororo katika shairi, huwa na

,.

idadi maalum ya mizani na vina. Hivyo, humbainikia msomaji kwa wepesi. Lengo hapa

ni kubaini aina za kibwagizo katika mashairi ya kimapokeo na dhima yake katika baadhi

ya mashairi hayo.

(28)

2.1 Shairi: LipiLitakalokuwa

Hili ni shairi la aina ya tarbia Iinalofuata arudhi za kimapokeo. Kibwagizo cha shairi hili

kinakaririwa toka mwanzo hadi mwisho wa shairi. Mizani katika shairi hili inatoshana

toka mshororo wa kwanza hadi kwa kibwagizo. Ubeti wa kwanza ni:

Lipi mojapo la kuwa? Naliwe lijulikane Liwe tupate lijuwa, tujuwe na tulio Naliwe tupate tuwa, liwapo ndilo tunene

Halitakuwajingine, ima ndilo au silo. (Ubeti wa 1)

Kibwagizo katika shairi hili ni; Halitakuwa jingine, ima ndilo au silo. Vina vya kati

katika shairi hili ubeti wa kwanza ni 'wa' na vya mwisho ni 'ne' katika mishororo mitatu

ya kwanza. Kibwagizo kina kina cha kati kinachofanana na kina cha mwisho cha

mishororo mitatu iliyotangulia, 'ne', kina chake cha mwisho ni '10'. Vina vya shairi hili

ingawa havifanani katika shairi nzima lakini vinafanana katika kila ubeti. Aina hii ya

kibwagizo ni kisichobadilika toka ubeti hadi ubeti. Kwa kawaida, katika mashairi ya kimapokeo, ambayo mtunzi pia ametumia, ni kuwa kibwagizo huwa kiini cha ujumbe wa

mtunzi na huletwa mwisho wa kila ubeti bila kubadilisha maneno yake. Katika hali hii

maelezo ya mtunzi yanatimia katika mishororo mitatu. Mshororo wa nne ambao ndio

kibwagizo unakariri kiini cha ujumbe wa mtunzi. Mtunzi ametumia mtindo wa

kibwagizo kisichobadilika katika ubeti wa kwanza hadi wa nne. Amekikariri kibwagizo

'Halitakuwajingine, ima ndilo au silo'.

Sanaa ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa na mwanadamu ili kudhibitisha uhalisi

(Sanchez, 1973). Hivyo, Ushairi ndiyo sanaa ya Abdallah, kibwagizo kinadhibitisha

uhalisi kwa kutoa wito au wazo msingi mwishoni wa kila ubeti. Aidha, uhusiano kati ya

sanaa na jamii ni wa kihistoria ambapo msanii huwa ni wa wakati wake. Msanii wa

(29)

shairi hili ameongozwa na itikadi katika uelezaji wa matukio ya jamii anayoishughulikia.

Itikadi hiyo imebainishwa kwa namna anavyotoa maelezo yake na kuwasawiri wahusika

wake. ltikadi yenyewe imejitokeza katika maudhui na dhamira ya mwandishi (Njogu na

Chimera, 1999). Katika utunzi wa mashairi, uhalisi huu hutegemea mtindo wa mtunzi

ambao huongozwa na wakati. Uelezaji wa matukio umedhihirika katika mishororo ya

kwanza mitatu katika ubeti. Mshororo wa nne ambao ndio kibwagizo humebeba

maudhui na dhamira ya mwandishi. Huu ndio ukariri wa kiini cha ujumbe wa mtunzi

unaodhihirika katika kibwagizo.

Kibwagizo katika 'Lipi Litakalokuwa', kimekuwa ni dira ambayo humrejesha zaidi

msomaji katika ujumbe ambao umezingatiwa. Ukariri wa kibwagizo ni njia mojawapo

ya kubainisha ujumbe unaowasilishwa katika shairi. Mtunzi amekitumia kibwagizo

kama mtindo kwa lengo la kusisitiza ujumbe. Maelezo huwasilishwa katika mishororo

mitatu ya kwanza ambayo ni maelezo zaidi juu ya kiini kilicho kwenye kibwagizo

kudhihirisha umuhimu wa kibwagizo chenyewe, kibwagizo kinachofunuwa kiini cha

madhumuni yale.

I' 2.2 Shairi: Ukamilifu wa Mja

Shairi hili ni la tarbia. Lina kibwagizo, ambacho ni mshororo wa mwisho,

kinachorudiwa katika sehemu yake ya pili huku Sehemu ya kwanza ya kibwagizo

ikibadilika kutoka ubeti hadi ubeti. Muundo wa ubeti wa kwanza ni:

Twaa nakupa pokeya, pokeya usidharau

Yaliyomo ni ya ndiya, katika waadhi huu Twaa kwa kuzingatiya, mazingatiyo makuu

Mtu kuwa na maguu, si kwamba mekamilika (Ubeti wa 1)

(30)

Shairi hili lina muundo wa ndani na wa nje. Shairi limegawanyika katika ukwapi na

utao. Katika kila kipande kuna vina vinavyotiririshwa; kina cha ndani ni ' ti' na cha nje

'ko' Isipokuwa katika kibwagizo ambapo kina cha kati ni ' ko' na cha mwisho ni ' ti'.

Mashairi mengi yanayofuata arudhi za kimapokeo hufuata mtindo huu ambapo vina vya

mstari wa mwisho (kibwagizo) si lazima vishabihiane na vile vya mishororo ya awali.

Hapa mishororo hubadilishana vina mpaka mwisho. Kina cha mwisho kinakuwa ndicho

kina cha kati cha kibwagizo.

Mtindo unaobainika katika shairi hili ni kuwa kibwagizo kinarudiwa katika kila ubeti

lakini sehemu ya kwanza inabadilika. Kulingana na Kahigi na Mulokozi (1979) ni kuwa

mstari unaorudiwarudiwa husisitiza wazo kuu. Kibwagizo ni mbinu ya kushirikisha

wasikilizaji wakati wa kuliimba shairi. Katika mashairi mengi ya Kiswahili, kibwagizo

huandikwa mwishoni mwa kila ubeti na hakibadiliki toka mwanzo hadi mwisho wa

shairi. Katika shairi hili, sehemu isiyobadilika ni ya pili (utao), ya kwanza (ukwapi),

inabadilika katika kila ubeti.

Uchanganuzi wa msamiati lazima uzingatie namna urudiaji wa maneno

unavyowasilishwa ambao ni msingi mkubwa wa kuendeleza dhamira fulani (Wamitila, I'

2010). Urudiaji pia huweza kutokana na sababu za kimtindo pale ambapo maneno fulani

yanarudiwa kwa sababu ya udumishaji wa vina na mizani (katika tungo za kiarudhi) au

kwa sababu ya kuzua hisia (yaani kuwa kama njia ya kuchimuza) au pale ambapo ile

sanaa inakuwa ni aina ya hatima yenyewe. Sehemu ya pili ya mshororo na kibwagizo

inarudiwa hili kudhihirisha kuwa binadamu hawezi kuwa kamilifu kwa kuyatimiza yote

(31)

Takriri au urudiaj i unaweza kuwa wa nusu mstari. Mtindo huu wa urudiaj i wa nusu mstari una dhima ya kutomkera msomaji maana katika kila mwisho wa ubeti kuna hoja

mpya inayozindua akili ya msomaji. Kibwagizo cha shairi hili ni takriri ya nusu mstari

kwa sababu kipande cha pili cha kibwagizo kinarudiwa kutoka ubeti wa kwanza hadi wa

kumi na nne. Mtindo huu wa kibwagizo una dhima ya kutoa fursa kwa hadhira

kuzingatia mambo mawili katika kituo hicho hicho kimoja; sehemu moja ya kituo

hukariri wazo kuu la ubeti huo nayo sehemu ya pili inakariri wazo kuu la shairi zima.

Tunapokichunguza kibwagizo katika kila ubeti tunaona kuwa kibwagizo ni :

Mtu kuwa na maguu, si kwamba mekamilika Na mtu kuwa na turnbo, si kwamba mekamilika Mtu kuwa na kifuwa, si kwamba mekamilika

(Ubeti wa 1) (Ubeti wa 2) (Ubeti wa 3)

Dhima ya sehemu ya kwanza ya kibwagizo inayobadilika inadhihirika hapa katika kila

ubeti kwa ambavyo kuna jambo jipya linalotajwa. Hii inatokea katika beti kumi na nne

za mwanzo. Sehemu hii ya kwanza ya kibwagizo cha aina hii ina dhima ya kuibua wazo

kuu linalowasilishwa katika kila ubeti. Sehemu ya pili ya kibwagizo inasalia: si kwamba

mekamilika (katika beti zote za shairi).

Sehemu ya pili ya kibwagizo cha aina hii nayo ina dhima ya kuwasilisha wazo kuu la

shairi zima. Wazo kuu analoliwasilisha mtunzi ni kutokamilika kwa mja. Kuanzia ubeti

wa kumi na tano hadi wa kumi na tisa kibwagizo kinabadilika katika kila ubeti. Idhibati

ya hayo ni kama ifuatavyo:

Nikupe yangu maani, ya mja kukamilika Maana yangu 'tatowa, ya mja kukamilika Hapo ndipo huambiwa, mja amekamilika Hiyo ni yangu maana, ya mja kukamilika Kama huyo 'tamkiri, ni mja kukamilika

(Ubeti wa 15) (Ubeti wa 16) (Ubeti wa 17) (Ubeti wa 18) (Ubeti wa 19)

(32)

Katika vibwagizo hivi tunaona kuwa vile kibwagizo kinabadilika nayo dhima

inabadilika. Kwa mfano, katika kibwagizo cha ubeti wa kumi na tano na sita, dhima

inakuwa ni kumpa msomaji maana ya mja kukamilika. Katika kibwagizo cha ubeti wa

kumi na saba hadi kumi na tisa, dhima sasa inakuwa ni kutoa jibu kwa vibwagizo vya

awali. Anatoa maana yake ya mja kukamilika, jambo ambalo hadhira limelingoja kwa

shauku kuu: kujua ukamilifu wa mja ni upi. Hata hivyo, kibwagizo bado ni takriri nusu mstari na kinabadilika kutoka ubeti hadi ubeti. Nusu ya kwanza inabadilika kutoka

nikupe yangu maani, maaa yangu 'tatowa, hapo ndipo huambiwa, hiyo ni yangu maana, kama huyo 'tamkiri,

(Ubeti wa 15) (Ubeti wa 16) (Ubeti wa I 7) (Ubeti wa 18) (Ubeti wa 19)

Hata hivyo dhima inabakia ileile na hapa kuna himizo zaidi kwa msomaji. Kutorudiwa

kwa maneno yale yale kuna dhima ya kutomchosha msomaji au hadhira. Hivyo, Sehemu

ya pili ya kibwagizo nayo inakuwa:

Ya mja kukamilika, Ya mja kukamilika, Mja amekamilika, Ya mja kukamilika, Ni mja mekamilika,

(Ubeti wa 15) (Ubeti wa 16 ) (Ubeti wa 17) (Ubeti wa 18) (Ubeti wa 19)

Katika madondoo hayo mtindo wa mtunzi unajidhihirisha ingawaje mane no machache

yanabadilika lakini nusu ya pili ya kibwagizo inabaki na dhima ya kulikariri wazo kuu la

shairi zima toka mwanzo hadi mwisho.

2.3 Shairi: Telezi

Shairi hili ni la tarbia, linatimiza kaida ya tarbia ya kijadi. Kibwagizo cha shairi hili ni

tofauti katika kiia ubeti. Ubeti wa kwanza na wa pili una muundo ufuatao :

Mvuwa iiiyonyesha, ya maradi na ngurumo Kutwa na kucha kukesha, kuonyesha pasi kikomo

23

\/1\

-r"

"

r. I .

lr;, I/-\ \ / .. /> ..

-'IVi

V

L

:

.R

...

/1

.

' .,.... I

Y

lID./

I'..- '

• I I \/' i \ j

(33)

Haikuwanufaisha, wenye kazi za vilimo

Wenye kazi za vilimo, walifikwa na hasara (Ubeti wa 1)

Mimeya waliopanda, i1itekukatekuka

Kazi ngumu walotenda, yote ikaharibika

Hawakuvuna matunda, waliyo wakiyataka

Waliyo wakiyataka, yakawa ya mbali nao (Ubeti wa 2)

Shairi hili lina vina vya ndani na vya nje. Shairi limegawika katika ukwapi na utao.

Katika kila kipande kuna vina vinavyotiririshwa. Vina vya kati kwa kila ubeti

vinafanana katika mishororo mitatu ya kwanza. Vina vya mwisho pia vinafanana, kwa

hivyo shairi hili linatiririka. Kina cha kati cha kibwagizo ni kile cha mwisho cha

mishororo mitatu ya kwanza katika kila ubeti wa shairi nacho kina cha mwisho cha

kibwagizo ni tofauti katika kila ubeti.

Katika muktadha wa shairi hili, 'Telezi', linalorejelewa, inabainika kuwa mtunzi wa

ushairi huwa ana hiari ya kuteua kauli na miundo mahsusi ya lugha iliyopo katika

mawasiliano ya jamii na kuipuuza ile ambayo huihisi kuwa haitaweza kusaidia katika

ubainishaji na uelekezaji wa mawazo, maono na fikra katika utungo na hasa kwa jamii

husika. Uteuzi huo huzingatia zaidi athari ambayo imekusudiwa kuibuliwa katika akili.

Dhima ya mtunzi ni kuchochea na kuielekeza mielekeo ya hadhira pamoja na

kuiadilisha. Kilele cha uteuzi huu wa kauli na miundo hudhihirika zaidi na uwasilishwa

katika kibwagizo cha shairi husika. Kibwagizo cha aina hii basi huwa na dhima teule ya

kuelekeza na kuadilisha jamii. Kibwagizo cha shairi hili nitofauti katika kila ubeti. Kwa

mfano kibwagizo ni:

Wenye kazi za vilimo, walifikwa na hasara

Waliyo wakiyataka, yakawa ya mbali nao

Hadi mwao majumbani, na kukomeya milango

(Ubeti wa I)

(Ubeti wa 2)

(Ubeti wa 3)

(34)

Kibwagizo kinabadilika na kuwa tofauti katika kila ubeti. Mtunzi ameteua kauli na

miundo ya lugha mahususi katika jamii anayowasiiiana nayo kuielekeza mielekeo ya

hadhira na kuiadilisha kama inavyodhihirika katika kibwagizo.

Kadhalika, baadhi ya mashairi ya Kiswahili huweza kuimbika kwa kuzingatia mpangilio

maalum wa mizani na urari wa vina (Noor, 1988 na Kandoro, 1982). Wanajadi kama

vile Chiraghdin, Mayoka, Kandoro na wengineo wanakubaliana kuwa vina na urari wa

mizani ndiyo vitambulisho vya ushairi wa Kiswahili. Kwa sababu dhima kuu katika

ushairi wa Kiswahili ni kuburudisha na wakati huo huo kuwasilisha ujumbe adhimu kwa

hadhira (Abdallah 1990). Katika muktadha huo shairi hujengewa ukariri ambao

hulifanya kuweza kuimbika, kughaniwa na kusomwa kwa sauti ya kimoyomoyo. Haya

hutimizwa kimtindo katika utunzi wenye maadhi na muwala wa mishororo pamoja na

vibwagizo vinavyoshirikiana kuuibua ujumbe kwa hadhira kusudiwa. Mishororo na

kibwagizo katika shairi hili la 'Telezi' imetimiza dhima hii kama inavyobainika katika

ubeti ufuatao:

Mvuwa iliyonyesha, ya maradi na ngurumo Kutwa na kucha kukesha, kuonyesha pasi kipimo Haikuwanufaisha, wenye kazi za vilimo

Wenye kazi za vilimo, walifikwa na hasara (Ubeti wa 1)

Katika ubeti huu, mizani katika kila mshororo ni kumi na sita, imegawa nane katika

ukwapi na nane katika utao. Kuna urari wa vina katika ubeti huu. Vina vya kati katika

mshororo wa kwanza hadi wa tatu ni 'sha' na kina cha kati cha kibwagizo ni 'mo'.Vina

vya mwisho katika mishororo mitatu ya kwanza ni 'mo' nacho kina cha mwisho cha

kibwagizo ni 'ra'. Katika shairi zima vina vya kati vya mishororo mitatu ya kwanza

vinafanana. Vina vya mwisho katika mishororo ya kwanza mitatu vinafanana. Kina cha

(35)

ya ubeti huo. Kina cha mwisho cha kibwagizo ni tofauti kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Mtunzi amejenga mpangilio maalum wa mizani na urari wa vina ambavyo ni

vitambulisho vya ushairi wa Kiswahili hasa unaozingatia arudhi za kimapokeo.

Kibwagizo cha shairi 'Telezi' ni tofauti katika kila ubeti. Sehemu ya kwanza ya kibwagizo ni sehemu ya mwisho ya mshororo uliotangulia. Dhima ya mtunzi ni kulipamba shairi kwa kurudia maneno yale yale aliyoyatumia awali katika mshororo uliotangulia. Mtindo huu unakifanya kibwagizo kiwe cha aina ya pindu. Kibwagizo

hakifanani katika shairi zima: ni tofauti katika kila ubeti. Mtunzi anatumia aina hii ya

kibwagizo kwa dhima ya kuutilia mkazo ujumbe wake katika kila ubeti. Kwa mfano

katika ubeti wa mwisho mtunzi anabadilisha mtindo wake. Zikanibwaga telezi, sikujuwa kuzendeya

Ningekwenda kwa henezi, yasingenifika haya Lakini tena siwezi, mwendo huo kutumiya

Sitawata kutembeya, ila tabadili mwendo (Ubeti wa 7)

Kwa kuzingatia ubeti huu mtunzi anabadli jinsi alivyokuwa akikiunda kibwagizo chake katika beti zilizotangulia. Hajatumia sehemu ya mwisho ya mshororo wa tatu kukianzishia kibwagizo. Kibwagizo katika ubeti huu ni: Sitawata kutembeya, ila tabadili mwendo.

Kibwagizo hiki kimetumia kina cha kati kinachofanana na vina vya mwisho vya

mishororo iliyotangulia. Mtunzi amekitumia kibwagizo tofauti katika ubeti wa mwisho kimaksudi. Kibwagizo hiki pamoja na kuhitimisha shairi kina ujumbe muhimu wa shairi

zima. Dhima ya kibwagizo cha aina hii ni kuhitimisha shairi pamoja na kupitisha ujumbe muhimu wa shairi zima kwajumla.

(36)

2.4 Shairi: Kamliwaze

Hili ni shairi aina ya tarbia ya bahari ya msuko. Mishororo ya kwanza mitatu ina mizani

kumi na sita kila mmoja lakini kibwagizo chake kimefupishwa na kina mizani nane

kutoka mwanzo hadi mwisho. Beti hizi zinaudhihirisha muundo wa shairi hili.

Tumishi inuka hima, utwae wangu waraka

Huko ninakokutuma, uwenende kwa haraka

Na haya mate natema, hima yasije kauka

Inuka sa sa inuka (Ubeti wa 1)

Nenda kwa mwenzangu mja, kanisalimiye sana

Mwambe ni zetu pamoja, huzuni anzoona

Mambo hwenenda yakija, ni dasituri bayana

'Kipeleleza'taona (Ubeti wa 2)

Katika shairi hili, mishororo mitatu ya kwanza kwa kila ubeti ina vina vya kati

vinavyofanana. Katika ubeti wa kwanza vina vya kati ni 'ma' na vya mwisho ni 'ka'.

Kibwagizo ambacho ni kipande tu, kinachukua kina cha mwisho 'ka' kinachofanana na

kina cha mwisho cha mishororo mitatu iliyotangulia. Katika ubeti wa,pili vina vya kati

vya mishororo mitatu ya kwanza ni 'ja' na vya mwisho ni 'na'. Kibwagizo kinachukua

kina 'na' ambacho ni kina cha mwisho cha mishororo mitatu ya kwanza. Mtindo huu

unaendelea hadi ubeti wa mwisho ambapo kila kibwagizo kinachukua kina cha mwisho

cha mishororo mitatu ya kwanza ya ubeti.

Shairi 'Kamliwaze' ni la aina ya msuko kwa sababu kibwagizo chake kimefupishwa.

Kibwagizo ni kifupi na chenye idadi ya mizani inayoafiki kipande cha mwisho cha

mishororo ya ubeti basi mtunzi ametumia aina hii ya kibwagizo kwa dhima ya kuubulia

muundo wa sehemu hii ya shairi. Ingawaje kibwagizo hiki ni cha msuko lakini

kinabadilika ubeti hadi ubeti. Kwa mfano :

Tnuka sasa inuka (Ubeti wa 1)

'Kipeleza 'taona (Ubeti wa 2)

Nyayo zisife kwa tabu (Ubeti wa 3)

(37)

Ufupishaji huu wa kibwagizo ni wa kimtindo ambapo mtunzi anaitaka hadhira yake

ishiriki katika kujenga sehemu iliyobaki. Ufupishaji pia ni mbinu ya taharuki ili kujenga

muktadha wa usaili na utafakari. Msomaji anajisaili juu ya alichokikusudia mtunzi katika kibwagizo, kuwaza na kuwazua ni utafakari unaojengwa na muktadha anaouzua mtunzi.

Mtunzi pia anaweza kuwa anataka beti za shairi ziwe na maadhi fulani maalum ya umbo

Iililojengwa. Umbo hili la kibwagizo cha msuko Iinadumishwa hadi mwisho wa shairi.

Katika ushairi wenye vina na mizani, kama huu wa kimapokeo, hamu ya msomaji zaidi

hudumishwa na ulinganifu wake wa ridhimu na sauti unaotokana na vina na urari wa

mizani. Mapigo ya shairi la aina hii hufuata mgawanyo wake katika vipande vyenye

mizani sawa, na shairi husomeka upesiupesi bila kuitumikisha sana akili ya msomaji.

Kifani, vina na urari wa mizani katika shairi hufanya kazi ya ala ya muziki katika ushairi

simulizi. Hivyo basi shairi lililodumisha ulinganifu na ridhimu hadi kwenye kibwagizo

huzua hamu kwa msomaji na hadhira kwajumla.

Kama ilivyokwishaelezwa hapo awali, kibwagizo cha shairi hili kimefupishwa na

kinabadilikabadilika katika kila ubeti. Kibwagizo cha aina hii kina dhima ya kujenga

usaili na utafakari kwa msomaji au msikilizaji. Mtunzi ameyateua maneno haya kwa

makini kuwa ishara ya kuufikia ujumbe batini uliofumbwa kwenye shairi, ujumbe huu

unapasa kuifikia hadhira kusudiwa. Wafula na Njogu, (2007) wana maoni kuwa, maneno

yaliyotumika katika kibwagizo ni ishara zinazohitaji kufasiriwa na kupatanishwa na

baadhi ya vipengele vinavyopatikana katika matukio yaliyo katika jamii inayorejelewa.

Jukumu la ushairi si kutumbuiza, kusifu kuonya wala kukosoa tu. Abdalla ana falsafa au

mwongozo katika sanaa yake kama inavyodhihirika katika shairi hili. Itikadi au

mwongozo anaouzingatia ni wa kujihusisha na maoni, mahitaji na matakwa ya walio

(38)

wengi na hasa watu waliomo katika tabaka duni. Mshairi anautetea na kuufafanua uhalisi

na ukweli wa kijamii. Haya yanadhihirika kwa uwazi katika mishororo mitatu ya kwanza

na kusisitizwa katika kibwagizo. Kibwagizo hiki ni himizo kwa msomaji na hadhira

kusudiwa kuwa wana jukumu fulani ambayo iko katika kila ubeti. Maoni, mahitaji na

matakwa ya hadhira yameshughulikiwa na mtunzi hasa katika himizo anyoitoa katika

kibwagizo.

2.5 Shairi: La Mjini Na La Shamba

Hili ni shairi la tarbia lenye muundo wa ngonjera. Kibwagizo cha shairi hili ni swali

katika ubeti wa kwanza linalojibiwa katika kibwagizo cha ubeti wa pili.

Mwateni apige mbawa, na kwingi kutaratamba Nakifutishe kifuwa, na ardhi kuitimba

Ni bure aj isumbuwa, haamshi moja nyumba

Tangu linijimbi shamba, likawikiya mjini? (Ubeti wa 1)

Jawabu la ubeti huu liko katika ubeti ufuatao:

JAWABU

Uliyefumba fumbo, hakujuwa kulifumba

Usibaranganye mambo, simba awapo, ni simba

Si lea tangu kitambo, kwajulikanwa ya kwamba

Lau si huyo wa shamba, wa mjini hangekuwa (Ubeti wa 2)

Katika shairi hili, mishororo ya kwanza mitatu katika ubeti wa kwanza ina vina vya kati

'a' na 'mba' kama vina vya mwisho ilhali kibwagizo kina kina cha kati 'mba' na cha

mwisho ni 'ni'. Katika ubeti wa pili vina vya kati ni 'mbo' na vya mwisho ni 'mba'.

Kibwagizo kina vina vya kati 'mba' na cha mwisho ni 'wa'. Vibwagizo hivi havifanani

(39)

kwa maneno au kwa vina lakini vyote vina dhima inayofanana. Vinamrudisha msomaji

kwa ujumbe muhimu unaopitishwa na mtunzi.

Muundo wa shairi la Kiswahili hubainishwa kupitia kwa mshikamano wa mawazo,

mpangilio wa vipengele vya lugha, maudhui, lengo na mafunzo. Mtunzi ameyazingatia

haya katika mtindo huu wa uwasilishaji wa shairi kwa kushirikisha zaidi vipengele vya

kiarudhi katika shairi hili. Kibwagizo katika ubeti wa kwanza, ambacho ni swali, na kile

katika ubeti wa pili, ambacho ni jibu, ni dira ya kuundia muundo wa beti katika shairi

hili. Kibwagizo kilichotiririshwa huathiri muundo wa shairi kinyume na kile ambacho

hakijatiririshwa. Kibwagizo cha aina hii kinaafiki idadi maalum ya mizani sawa na

mishororo iliyokitangulia. Hivyo basi, aina ya kibwagizo hiki ni yenye dhima ya kuwa

dira ya kuunda beti katika shairi lenyewe.

Lugha iliyotumika katika shairi huhitaji kuchochea hisi za msomaji au msikilizaji. Licha

ya urari wa vina na mizani, kuna umuhimu wa kuteua maneno muhimu yenye kutoa

taswira au picha zinazohitajika (Kuvuna na Maliachi 1992). Abdalla katika shairi hili

ametumia mtindo wa kuyateua maneno yanayochochea hisi na kutoa picha ya kufumba

I' na kufumbua fumbo, katika ngonjera, kama ilivyohitajika katika umbo la shairi hili.

Mulokozi na Kahigi wanasema kuwa ushairi lazima uguse hisi, lazima umsisimue

anayeusema, kuusoma au kuuimba na yule ausikilizaye. Shairi lisilogusa hisi ni kavu na

butu na hata kama limesarifiwa katika vina na urari wa mizani, shairi hilo litaishia katika

kuubiri tu. Mtunzi ametumia maneno kimakusudi katika kila mshororo na kufikia kilele

chake katika kibwagizo cha kila ubeti. Shairi hili linamsisimua anayelisoma au

kulisikiliza na si kavu kwa vile linagusa hisi.

(40)

Jambo ambalo linautenga ushairi wa Kiswahili na tungo nyingine za Kiswahili ni umbo

lake (Chiraghdin, 1977). Shairi la Kiswahili linapokosa vina na mizani hukosa umbo na

hapo huwa haliitwi tena shairi. Kutokana na umbo la shairi linalorejelewa ni wazi kuwa

Iimeafiki kuitwa shairi. Lina vina na mizani ambayo inatiririka katika beti zote mbili.

Kibwagizo chake katika kila ubeti ni tofauti.

Tangu linijimbi shamba, likawikia mjini? (Ubeti wa 1 Lau si huyo wa shamba, wa mjini hangekuwa (Ubeti wa 2)

Mtunzi anatumia kibwagizo katika ubeti wa kwanza (hapo juu) kama swali kwa ujumbe

unaowasilishwa katika ubeti wa kwanza. Anatoa hoja zake katika mishororo mitatu ya

kwanza na kuhitimisha ujumbe huo kwa swali linalopatikana katika kibwagizo.

Kibwagizo hiki ni swali na wakati huo huo ni hatima ya ujumbe wa ubeti wa kwanza.

Katika ubeti wa pili kinakuwa jibu la swali lililo katika kibwagizo cha ubeti wa kwanza.

Mtunzi amezua utafakari kwa msomaji wa shairi katika ubeti wa kwanza na kuumaliza

utafakari huo kwa kutoa j ibu katika kibwagizo cha ubeti wa pili. Kibwagizo cha pili

(kilichorejerewa hapo juu) hivyo basi, kina dhima ya kujibu swali na kuumaliza usaili

wa hadhira. Kibwagizo cha ubeti wa kwanza ni swali nacho kibwagizo cha ubeti wa pili

ni jibu. Mtunzi amekitumia kwa kila ubeti wa shairi moja ili shairi litoshane na

kukamilishana. Kibwagizo hiki kimetosheleza na kuukamilisha ujumbe wa mtunzi katika

I'

shairi hili la aina ya ngonjera.

Lugha ya ushairi huwa na uzito mkubwa na mawazo yake ni mazito. Jinsi lugha

inavyotumiwa inaonyesha sifa ambazo si za kawaida kwa kiwango kikubwa

(Nyembembe, 1977). Mshairi ana uhuru mkubwa zaidi wa kuuchanganyachanganya

msamiati, kuubadilisha, ili uafikiane na mahitaji yake ya kishairi ya kipekee. Mtindo

kulingana na Wamitila (2003) hurejelea sifa maalum za mwandishi au mazoea ambayo

(41)

hujionyesha kwenye fani yake. Mazoea haya hapa yanajidhihirisha katika mtindo wa

fumbo. Mtunzi ameutumia mtindo wa fumbo ili kuikemea, kuizomea na pengine

kuirekebisha jamii. Aidha, fasihi haipaswi kupayuka, inapaswa kusema kwa staha ili

asemwaye asivunjiwe mbeleko. Mtunzi huwataka wasomaji wawe mahiri katika kuiga

utamaduni wa kabila fulani au taifa fulani, kwanza wayachunguze kwa makini, hayo

watakayoyaiga yanaweza kuukuza utamaduni wao au la.

Maana ya shairi inaweza kujibainisha moja kwa moja unapolisoma kwa kuwa mtunzi

ameyatumia maneno waziwazi, yanayoeleweka, au akayatumia mafumbo yanayousetiri ujumbe (Wamitila, 2005:8). Maneno ambayo hutumiwa katika kibwagizo huwa ni yale ambayo yameteuliwa kwa makini kuwa ishara ya kuufikia ujumbe uliofumbwa kwenye

shairi. Mtunzi ameutumia mtindo wa tamathali ya methali katika kuufumba ujumbe wake. Ni jukumu la hadhira kushiriki sio katika usomaji tuli bali pia kushiriki katika

kuliajiri bongo ili kuweza kupambanua maana iliyosetiriwa katika shairi (Senkoro,

1988:viii). Katika muktadha huu basi mtunzi amekitumia kibwagizo cha aina hii kwa

dhima mbili; ya kwanza, kuufumba ujumbe wake, na pili, kuitaka hadhira kushiriki

kuufumbua ujumbe. Maneno yaliyotumika katika kibwagizo huwa ni matini au ishara

zinazohitaji kufasiriwa na kupatanishwa na baadhi ya vipengele vinavyopatikana katika ,

-matukio yaliyo au yanayoshuhudiwa katika jamii inayorejelewa (Wafula na Njogu,

2007:85-86). Haya yanadhibitisha kuwa ushairi wa Kiswahili hufasiriwa kwa mwafaka

zaidi kwa upatanishwa na muktadha mahususi wajamii.

Msokile (1993:45) ana maoni kuwa taswira ni mkusanyiko wa picha ambazo zinaundwa

na maelezo ya msanii katika kazi ya fasihi. Hujengwa kutokana na matumizi ya

tamathali za usemi. Ujenzi wa taswira humfanya msomaji apate aina mbalimbali za hisi

32

(42)

zinazoshughulikiwa na kazi ya kifasihi. Madai ya Njogu na Chimera (1999:91) ni kuwa taswira hutumika kuleta picha au hali fulani akilini mwa msomaji au watazamaji.

Anaweza kuona, kusikia, kuonja, kunusa, kupenda, kuchukizwa au kudharau

kilichosawiriwa kutegemea taswira zilizotumika. Taswira ni picha ambazo hujengwa na

msanii kwa minajili ya kuwasilisha ujumbe wake. Anaweza kuchora picha ya mahali,

hali na vitu kwa kutumia tamathali za usemi hususan tashbihi na sitiari. Pamoja na

kutumia sitiari na tashtabihi, taswira hizi pia hujengwa kwa kutumia methali, vitendawili

na misemo ya kawaida. Mtunzi wa shairi hili ametumia methali kama taswira katika

kibwagizo. Ametumia uhuru wa mtunzi kuibadili methali 'jogoo wa shamba hawiki

mjini'. Methali hii katika kibwagizo imetumiwa na mtunzi kuleta mnato na wakati huo

huo kutoa funzo kwa hadhira.

2.6 Kiishilio

Sura hii imechunguza kibwagizo katika mashairi ya kimapokeo. Imechunguza aina

mbalimbali za kibwagizo na dhima yake katika mashairi ya Kiswahili. Aina iliyoshughulikiwa ni kama kibwagizo kinachorudiwarudiwa katika kila ubeti,

kinachobadilikabadilika katika kila ubeti, kinachorudiwa nusu mstari na nusu ya pili ni

tofauti, kibwagizo ambacho ni kipande tu yaani nusu mshororo na kibwagizo cha

I' mazungumzo ambapo katika ubeti wa kwanza kibwagizo ni swali linalojibiwa katika

kibwagizo cha mshororo wa pili. Dhima ya kila kibwagizo kama kilivyotumika katika

(43)

SURA YATATU

MASHAIRI YA KATIYA KISWAHILI

3.0 Utanguiizi

Sura hii imeshughulikia kibwagizo cha mashairi ya kati ya Kiswahili. Kundi hili la mashairi ya kati huzingatia baadhi ya kaida za kiarudhi na kukaidi zingine. Mashairi haya hayafuati kanuni zote za ushairi wa mapokeo kama mizani, vina, kibwagizo, mishororo na vipande. Mashairi haya yanatokana na athari mbili, ya kiutunzi na uwasilishaji: kuzingatia kwa kiasi mbinu za uwasilishaji wa mashairi ya kimapokeo, pili, ni kutoridhika kabisa na umbo la shairi kutokubalika. Hivyo, hubadili mtindo na kuyapa

mashairi hayo 'sura mpya' ya uwasilishaji ili kukaidi baadhi ya miundo na sifa za ushairi wa kimapokeo wa Kiswahili. Mashairi huru yaliyozuka baada ya uhuru yalitokana na

mazingira mapya ya kisiasa, kielemu na kijamii. Mashairi haya yanaupa ushairi wa Kiswahili sura mpya kutokana na ubunifu wake. Wamitila (2001 :xii) katika utangulizi wa Jicho fa Ndani anasema kuwa, mshairi haridhiki na kaida za mizani tu bali anaonyesha ubunifu mkubwa sio tu katika mipangilio ya tungo hizo bali pia katika idadi ya mizani na mishororo katika beti zake. Wataalam tuliowahoji wanasema kuwa mashairi ya kati yanaonyesha kuwa mtunzi hajui azingatie arudhi au la, huku wengine wakiyakana kabisa kuwa si mashairi. Kadhalika King'ei, (2000) ana mawazo kuwa

" utunzi na uwasilishaji wa ushairi huru usidharau kaida za sanaa wala kufungwa nazo.

Ushairi kama sanaa na utunzi wa fasihi ni lazima ugeuke na kuambatana na wakati bali kule kubadilika kusichukuliwe kumaanisha kubandikiwa ugeni usio na haja wala

usioweza kuingiliana vizuri na kukubalika na maumbile ya sanaa yetu.

Katika kupitia mashairi katika diwani yaJicho faNdani inabainika kuwa imechanganya mashairi jadi na mashairi huru. Aidha, kuna mashairi mengi yaliyotungwa katika

(44)

muundo wa kimapokeo au kijadi. Mshairi anakiri ukweli kuwa sanaa haiwezi kufungika

kwenye kaida za kisanaa zisizobadilika. Mashairi ya kati yatakayoshughulikiwa hapa ni

ya kutoka katika diwani hii ya Jicho la Ndani nayo ni ;' ikwambiye' (uk.5), 'Jaribu

Kunikumbuka' (uk.55), 'Watendewa Jana' (uk.56), 'Anga' (uk.83), na 'Mimi Mtupu'

(uk.157). Mashairi haya si ya aina moja, yamechanganyika ya kimapokeo na mengine ni

huru. Jambo hili linayafanya yasiwe na aina moja ya muundo. Hivyo, kibwagizo

kinachotumiwa huwa hakibainiki wazi wala dhima yake haijitokezi moja kwa moja.

Lengo la sura hii ni kuchambua aina ya vibwagizo vinavyopatikana katika mashairi haya

na dhima ya kila kibwagizo.

3.1 Shairi: Nikwambiye

Hili ni shairi lenye umbo la tarbia lakini lisilofuata kaida za kiarudhi za kimapokeo. Lina

umbo la tarbia kwa sababu ya mishororo yake minne katika kila ubeti, lakini Baadhi ya

kaida hizo hazipo katika idadi ya mizani. i shairi la kati kwa vile inakaidi kaida za

kiarudhi na kufuata zingine kama inavyodhihirika hapa;

Nikwambiye njia ya ukweli ngumu

'sisikiye ina watu maalumu

Kwangu miye njia hiyo naihamu

Nifikiye daraja ya uwalimu (Ubeti wa 1)

Hata iwe

Niigiwe

Nifungiwe

Niraduwe

njia hiyo jahanamu

nijae mwingi wazimu

katika zake hatamu

fursa hiyo adimu (Ubeti wa 2)

Shairi hili lina muundo wa mahususi katika uwasilishaji wake. Lina beti sita zenye

mishororo minne katika kila ubeti. Mizani yake ni kumi na miwili katika kila mshororo.

Hii ni tofauti na mtindo uliozowewa na ulio maarufu katika mashairi ya Kiswahili wa

ubeti kuwa na mishororo minne yenye vipande vinane na mizani kumi na sita katika kila

(45)

katika kila ubeti kuleta sura mpya kuonyesha kuwa umbo la shairi la Kiswahili

halikukomea katika huo muundo mmoja bali Iina nafasi kubwa sana ya kuweza

kuvyaziwa miundo kadha wa kadha (Abdalla, 1980:xiii). Huu ni mfano mzuri wa shairi

la kati; halifuati kaida zote za kiarudhi, haina mishororo minne katika kila ubeti au

mizani nane kwa nane (8,8), (jumla 16) katika kila mishororo iliyozowewa katika

mashairi ya kimapokeo ya Kiswahili, hivyo kuleta utata. Wakati huo huo hatuwezi

kuliita shairi huru kwa kuwa kuna baadhi ya kaida za kiarudhi anazozizingatia Mohamed katika diwani ya Jicha laNdani kama vile vina vya kati na vya mwisho vinavyofanana

katika kila mshororo, mtindo uliozoeleka katika mashairi ya kimapokeo. Mashairi haya

huhusisha utunzi wa mashairi bila kujifunga kwenye arudhi (Wamitila, 2010:269).

Kadhalika mashairi huru hufuata mbinu ya mpangilio wa sentensi, unyambuaji maneno, mpangilio wake na muundo wa beti kuzua hisia nzito ya utungo wa kishairi. Ushairi huru unahusishwa najuhudi za kutoa Ushairi wa Kiswahili kwenye 'ufunge' wa vina na mizani.

Mstari wa mwisho unaoitwa kituo unaruhusiwa uwe ama na kina kimoja cha ubeti (Abedi 1954:19), au kifuate mpango ule ule wa vina vya mistari mingine. Haya Yameafiki ufafanuzi wa kibwagizo kama istilahi mahususi katika ushairi kwa sababu

kibwagizo kina vina vinavyofanana na vya mishororo iliyokitangulia. Katika shairi

'Nikwambiye', vina vyake vya kati vinafanana na kutiririka katika kila ubeti. Vina vya

mwisho ni 'mu'. Vinafanana na kutiririka kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.

Kibwagizo katika kila ubeti ni tofauti.

Nifikiye Niraduwe Niigiwe

Nautuwa

Wasojuwa

Vile visa

daraja ya uwal imu (Ubeti wa 1) fursa hiyo adimu (Ubeti wa 2)

pigo mtimani humu (Ubeti wa 3) siutaki ukadimu (Ubeti wa 4)

Hebu wa'uze kaumu (Ubeti wa 5)

ni vya watu maalumu (Ubeti wa 6)

(46)

Katika kila ubeti kila kibwagizo kilicho tofauti kinakuwa hitimisho ya yanayosemwa katika huo ubeti. Hivyo, kina dhima ya kuusisitiza ujumbe wa mtunzi katika kila ubeti, hii ndio sababu kila ubeti una kibwagizo tofauti. Vina vya kati katika kila kibwagizo vinafanana na vina vya mishororo mitatu iliyotangulia katika kila ubeti. Vina vya mwisho katika kila ubeti ni 'mu' na vinafanana kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho. Vinatiririka na hivyo basi vinatimizajukumu ya kulipamba shairi nzima.

Kibwagizo cha aina hii pia kina dhima ya kumsaidia msomaji sio tu kusoma kwa kulifurahia shairi bali kutafakari na kuwaza kila anaposoma na kukariri kila ubeti wa shairi hili. Katika muktadha huu msomaji huchochewa afikirie anachokisema mtunzi katika mishororo mitatu ya kwanza katika kila ubeti na ujumbe anaotaka kupitisha katika mishororo hiyo na kuikolezea zaidi katika kibwagizo. Mtunzi katika kutumia mtindo wa kibwagizo tofauti katika kila ubeti anakusudia kujenga taharuki ili msomaji ashiriki kikamilifu katika ujumbe wa shairi.

Mtunzi katika shairi hili anaonyesha ubunifu katika mpangilio na idadi ya mishororo ya

kila ubeti. Mohamed ametumia mtindo na sifa za kiisimu na mnyambuliko wa maneno,

I' mpangilio wa mishororo na ruwaza ya mishororo ya ubeti. Kwa mfano maneno yaliyonyambuliwa ni kama; 'nikwambiye' (Ubeti wa 1), 'niigiwe' (Ubeti wa 2) 'mtambuwe' (Ubeti wa 3) na 'naigiwa' (Ubeti wa 5). Mishororo imegawa katika ukwapi

(47)

Katika uwasilishaji wa shairi hili Mohamed ameuchagua msamiati wa makusudi

kupitisha ujumbe wake. Hadhira kusudiwa hapa ina jukumu ya kuchunguza na

kutafakari zaidi uteuzi wa msamiati uliotumika. Pasipo kuuelewa msamiati uliotumika

katika shairi, hadhira haitauelewa ujumbe unaowasilishwa. Kibwagizo ambacho ni kilele

cha ujumbe wa mtunzi pia hutumia msamiati ambao msomaji lazima auelewe ili kuupata

kikamilifu ujumbe wa mtunzi. Mtunzi ana hiari ya kuteua kauli na miundo mahususi ya

lugha iliyopo katika mawasiliano ya jamii na kupuuza ile ambayo huihisi kuwa

haitaweza kusaidia katika ubainishaji na uelekezaji wa mawazo, maono na fikra katika

utungo kwa hadhira yake. Uteuzi huo huzingatia zaidi athari ambayo imekusudiwa

kuibuliwa katika akili kwa azma ya kuielekeza mielekeo ya hadhira pamoja na

kuiadilisha. Kilele cha uteuzi huu wa kauli na miundo hudhihirika zaidi na uwasilishwa

katika kibwagizo. Kibwagizo kama hiki basi huwa na dhima teule ya kuelekeza na

kuadilisha jamii.

Matumizi ya kituo tofauti katika kila ubeti ni mtindo wa makusudi alioutumia mtunzi

kwa dhima ya kutoichosha hadhira katika harakati ya usomaji. Aina hii ya kibwagizo pia imetumiwa na mtunzi kuundia muundo wa ubeti katika shairi zima. Hii ni kwa vile

kibwagizo kiwe kimetiririshwa au hakijatiririshwa huathiri muundo wa shairi. Haya

~

yanathibitishwa hapa na ukweli kwamba kibwagizo kinaafiki idadi maalumu ya mizani

na mishororo iliyokitangulia. Hivyo, mshairi amedhihirisha uhodari wake katika usarifu

wa kibwagizo.

References

Related documents

“Initial” model prediction for the work by Lee and Choi [2] of the change in (a) incident UV light intensity passing through the soot layer as a function of time, and (b)

The proportion of eyed beans is somewhat too large to result from two recessive factors and too small t o result from a single factor, but other- wise the theoretical

Results show that the Lyapunov-type inequality gives the worse and the Cauchy-Schwarz-type inequalitygives the best lower bound estimates for the smallest

Following the collection of the first harvests the F1 plants were again selfed and then all of the leaves and side branches were removed so that second harvests of seed were

ABSTRACT This paper is concerned with experimental and Analytical investigations of the mechanical properties of bidirectional Carbon fiber reinforced polymer (CFRP) sheet and

Rasmusson and Carpenter (1983) observed that El Niño years are associated with negative pressure anomalies in the southeast Pacific, positive anomalies over the Indian Ocean

In our examination, we have tried different inside and outside releases like void, surface and crown utilizing factual parameters, for example, skewness and

We therefore screened for gain-of-function enhancers of jing gain of function in the eye and identified the Drosophila homolog of the disease gene of human a